Habari za leo wana jf
napenda kuongelea suala la ubunge igunga. Wilaya ya igunga imerudi nyuma kimaendeleo kielimu,kiuchumi na hata kifikira tangu alipofariki kabeho. Baada ya rostam kuachia ngazi sasa wanaigunga wanapumua vizuri. Imefika wakati sasa wa wananchi wa igunga kuchagua mtu makini sana ambaye atasimama kidete kwa maendeleo ya igunga. Igunga kwa taarifa ina wasomi kadhaa ambao wakao ndani na nje ya nchi. Kuna watu kama dr. Kafumu kamishna wa madini,inishati na madini, mboje ambaye anataaluma ya masuala ya uvuvi, wizara ya mifugo na uvuvi nasikia yuko marekani kimasomo,malembela shile ambaye yuko kigoma mkuu wa shule,jafary omary sukari kilimanjaro ,hamis mapinda mkonge tanga na wengine wengi wenye uhusiano mzuri na mataifa ya nje wanaweza wakawa viongozi wazuri sana katika jimbo la igunga na likawa mfano wa kuigwa. Watu wa igunga msiletewe watu ambao hawatakuwa na maana katika maendeleo ya jimbo lenu.chagueni mtu ambaye atasikiliza na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yenu, asiyepokea wa kutoa rushwa, mtu ambaye atatatua matatizo ya maji, madaraja, kilimo, elimu afya na mengine mengi. Anatakiwa mtu makini ambaye ataona mbali na kufanya vitu vya ukweli.
Hao watu niliowataja chama chochote kiangalie namna yakuwatumia kwa manufaa ya wanaigunga na nchi kwa ujumla.
Hawa ni wasomi wakubwa na viongozi wenye dira. Wajaribuni kwenye tanuru ya moto muone kama wanafaa kwa uongozi thabiti.
Ituganhila mashi
igunga