Hapo umenena. Na mimi natambua hilo kosa lake!
Lazima upayuke ndio uonekane mbunge safi. Kuna watu humu wamezidi uzushi, ukiwauliza niambie kosa kimya; wanaingia mitini, kazi yetu humu inakuwa kama kazi ya magazeti ya udaku!
Kwanza mbunge haombi misaada serikalini! ni wajibu wa serikali kuwafanyia wananchi kila linalowezekana kuwaletea maendeleo! mbunge anakuwepo kuikumbusha serikali wajibu wake na kuainisha vipaumbele vya maendeleo jimboni kwake!
Watu hawachagui mbunge ili eti yeye ndiye ajenge barabara, ajenge mashule, aajiri walimu na kuwalipa, ajenge zahanati na mengine ya jinsi hiyo.Fikiria kama nchi yote iwe na wabunge wanaotoa fedha zao kwa kazi zote za maendeleo, kuna haja ya kuwa na serikali hapo???wala mfumo wa uwakilishi haulekezi wabunge kutoa fedha zao kugharimia maendeleo!!ni kazi ya serikali ya Tanzania.
Takwimu zimetolewa hapa, kwamba wilaya ya igunga ni ya mwisho kwa ubora wa elimu nchini, hili si tatizo? inasaidia nini hata kama unajenga barabara nzr ya lami, lakini watu hawana elimu!!kila mwaka wilaya ya igunga ina upungufu wa chakula licha ya kuwa na eneo kubwa lenye ardhi nzr kwa kilimo!! matatizo ni mengi.
RA amefanya nini kutatua matatizo haya ya msingi?? kwa mfano ingekuwa jambo jema na la kujivunia sana kama hizo fedha zinazosemwa RA anatoa zingetumika kusomesha watoto wa igunga!!! kama wanavyofanya wabunge wegine majimboni kwao, hata mwalimu Nyerere alisema, ukitaka kumkomboa maskini msomeshee watoto wake tu!!!! tuache kufanya utetezi usiokuwa na maana hapa, watu wa igunga ndio wanaojua kama RA anafaa au hafai!!
Hapa JF si mahali pa kufanya utetezi kwa kuuliza maswali ambayo majibu yake yapo tyr, tena kwa takwimu.
Mahitaji ya watu wa igunga si fedha za rostam!!!Igunga itajengwa na wanaigunga wenyewe.