Bilioni 2.9 fedha zilizopelekwa jimbo la Igunga kwenye miradi mbalimbali ya Maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
JIMBO LA IGUNGA

TAARIFA KWA UMMA

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetupatia Fedha za Maendeleo kwa Mwezi Novemba 2023 kwenye Halmashauri yetu ya Wilaya ya Igunga Shilingi Bilioni Mbili na Milioni Mia Tisa (Tshs. 2,900,000,000=/).

Kwenye Jimbo la Igunga, Tutatumia Fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa pamoja na;

1. Ujenzi wa Majengo mapya na Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya.
2. Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati Mbili za Vijiji (Mwabaratulu - Itunduru na Mwandihimiji - Kinungu)
3. Uzio wa Shule Maalum (Shule ya Msingi Igunga)
4. Ununuzi wa Vifaa Tiba
5. Ujenzi wa madarasa
6. Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
7. Ujenzi wa Vyoo kwenye Shule za Msingi na Shule za Sekondari.
8. Mfuko wa Jimbo

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Igunga, Ninatoa shukrani zetu kwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendelea kugusa maisha yetu kwa kuboresha huduma za kijamii.

" KAZI NA MAENDELEO"

NICHOLAUS GEORGE NGASSA
MBUNGE WA JIMBO LA IGUNGA
1 NOVEMBA, 2023

WhatsApp Image 2023-11-01 at 11.42.47.jpeg
 
Back
Top Bottom