Rostam Aziz, Watanzania tukueleweje? Unawauzia Wakenya Gesi yako Bei Chee na kwa Watanzania unatuuzia Bei Juu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,551
108,888
"Kuanzia Mwezi wa Tano nategemea Kutangaza Kuuzwa kwa Gesi zote nchini Kenya kwa Tsh 500/ ya Kenya ( kama Tsh 9,500/ hadi Tsh 10,000/ tu za Tanzania ) kwani tayari Rafiki yetu kutoka Tanzania Rostam ameshakuja Kuwekeza hapa Kwetu hivyo nataka Wakenya wafurahie Maisha na wapate Gesi kwa gharama ndogo" amesema Rais William Ruto wa Kenya Juzi.

Chanzo Taarifa: Nipashe Radio One

Tunajitahidi mno Kumsahau Jemedari na Mtetezi wa Watanzania Hayati Rais Dkt. Magufuli ila tunashindwa kutokana na Kutuumiza hivi Watanzania wakati huko nje mnawafanyie Wema na Kuwaonea Huruma.

Laleni salama huko mliko Viongozi wangu Wapendwa na mlioifanyia Mema Tanzania yetu hii Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

GENTAMYCINE huwa siishii tu Kuwakumbukeni huku nikiionea Huruma Tanzania yangu na inakokwenda bali huwa Nalia mno nikiona Watanzania tunafanywa Wapumbavu ( Mapopoma ) na Watanzania wachache waliojipa Hatimiliki yote ya Mama Tanzania na Familia zao.

Endeleeni tu ila haya yote yana mwisho.
 
Acha undezi, kwani Rostam anatoa Msaada?

Kwanza gas yake anaagiza Uarabuni Wala sio Tanzania. Pili Kenya Wana kodi ndogo kwenye gas kuliko Tanzania ndio inaamua bei.

Na mwisho ndio kwanza Ruto amesema mtungi mdogo kuanzia Juni utauzwa elfu 5 Serikali yake itaweka Ruzuku.

Laumu serikali Ya CCM wenzio sio Rostam.
 
Gesi ya Rostam alikuwa ananunua kwao IRAN, kwa sasa anaingiza shehena kubwa kutoka Urusi ambapo gesi ya Urusi iko deepsea inauzwa kama karanga tu, lakini pia kodi ya bidhaa gesi kwa Genya iko chini kuliko Tanzania na malengo ya Rostam ni kutaka kusambaza gesi kuanzia Eritria, Ethiopia, Kenya, Uganda, Msumbiji, Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi, Botswana, Zimbabwe, Afrika kusini na hapo analenga kwanza mataifa yenye bandari kama Mombasa kwa Kenya itakua center kubwa kwake, kumbuka Rostam kwenye mchongo wa gesi habahatishi, anamaanisha.
 
"Kuanzia Mwezi wa Tano nategemea Kutangaza Kuuzwa kwa Gesi zote nchini Kenya kwa Tsh 500/ ya Kenya ( kama Tsh 9,500/ hadi Tsh 10,000/ tu za Tanzania ) kwani tayari Rafiki yetu kutoka Tanzania Rostam ameshakuja Kuwekeza hapa Kwetu hivyo nataka Wakenya wafurahie Maisha na wapate Gesi kwa gharama ndogo" amesema Rais William Ruto wa Kenya Juzi.

Chanzo Taarifa: Nipashe Radio One

Tunajitahidi mno Kumsahau Jemedari na Mtetezi wa Watanzania Hayati Rais Dkt. Magufuli ila tunashindwa kutokana na Kutuumiza hivi Watanzania wakati huko nje mnawafanyie Wema na Kuwaonea Huruma.

Laleni salama huko mliko Viongozi wangu Wapendwa na mlioifanyia Mema Tanzania yetu hii Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

GENTAMYCINE huwa siishii tu Kuwakumbukeni huku nikiionea Huruma Tanzania yangu na inakokwenda bali huwa Nalia mno nikiona Watanzania tunafanywa Wapumbavu ( Mapopoma ) na Watanzania wachache waliojipa Hatimiliki yote ya Mama Tanzania na Familia zao.

Endeleeni tu ila haya yote yana mwisho.
Wewe si wamana ccm na hayo yanafanywa na wanaccm? Tutolee kelele hapa. Kama unaweza na wewe kaichimbe hiyo gesi uuze bei unayotaka.
 
Negotiation power of the investor to a host country of investment, new entrant competitive strategy, enabling carpet for investment by Kenyan government. Rostam has gone with huge production/supply at na affordable price, with maximum distribution across Kenya,(leveraging on fair taxation and levies gives stability and predictability, on sales, cash flows, also cost effective, geographically he is gonna feed south Sudan and somalia.
This shit country Tanzania is a captive state meant for exploitation as a plot for extractions.

FDI ni Akili sio Utopolo
 
Back
Top Bottom