Rostam Aziz amekuja kumharibia Lowasa badala ya kumjenga

Rostam Aziz amekuja kumharibia Lowasa badala ya kumjenga

Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa sasa kuna mgogoro mkubwa ambao umeibuka ndani ya Team Lowasa baina ya wale wanaomuunga mkono Apson Mwang'onda na kambi ya Rostam Aziz. Chanzo changu ndani ya Team Lowasa kimebainisha kuwa mara baada ya ujio wa Rostam, hali ndani ya kambi hiyo imeanza kwenda kombo kutokana na kutofautiana kifalsafa na mbinu za kumpeleka Lowasa Magogoni.

Taarifa zinasema kuwa kambi ya Apson inaundwa na watu weledi na wenye uzoefu kwenye mikakati mbalimbali hasa kutokana na wengi wao kuwa wamewahi kulitumikia taifa hili katika maeneo tofauti. Hata hivyo, weledi wao unaonekana kuwa si lolote wala chochote kutokana na kushindwa kufanikisha kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri kuu ambao wamekuwa wakimkemea waziwazi Lowasa pale anaposhindwa kwenda sambamba na kanuni na maadili ya chama. Pia kambi hii ni masikini na walala hoi kwa vile wamekuwa wakinyonya kambi ya Rostam kifedha kupitia kwa Lowasa mwenyewe. Kwa maana nyingine, kambi hii ni ya wanyonyaji na kwamba wapo kwa Lowasa kimaslahi zaidi na si kufanikisha lengo la Lowasa kwenda Ikulu. Hii ni kambi ya 'KUPE'.

Kambi Rostam, nguli wa kashfa mbalimbali za ufisadi nchini inaundwa na watu wenye jeuri ya pesa ambao wamekuwa wakiitwa au kujiita kwa majina yenye kuonesha jeuri ya pesa kama Mzee wa Vijisenti, Nyoka Mwenye Makengeza nk. Kambi hii inaamini kuwa fedha inaweza kufanya kila kitu ikiwa ni pamoja na kununua haki za wana CCM.

Kwamba wapende wasipende ni lazima Lowasa aende Ikulu kwa vile pesa zipo. Kwa maana nyingine Kambi Rostam ndio wafadhili wakuu wa Team Lowasa kifedha.

Kutokana na jeuri ya pesa waliyonayo, wamefanikisha kumshawishi Lowasa kuwatema baadhi ya washauri wake walio chini ya Apson na kwa sasa Rostam ndiye anayeratibu harakati zote za Lowasa huku akiwatumia vijana wake kama Peter Serukamba na Hussein Bashe.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona kuwa mwelekeo wa Team Lowasa kwa sasa ni mbaya na kwamba lengo lao la kumpeleka Magogoni halitafanikiwa. Kwamba, watu ambao wameteka kambi hiyo hawana taswira nzuri ndani ya chama na kwenye jamii kutokana na kuhusika kwao na kashfa mbalimbali zinazoibuka nchini ikiwa ni pamoja na EPA, RICHMOND, ESCROW, VODACOM nk.

Kwamba, ujio wa Rostam si kwamba amekuja kuimarisha kambi hilo bali amekuja kuliangamiza na kwamba amekuja kuzidisha uchafu kwenye uchafu. Ni sawa na kutupa kinyesi kwenye jalala.

Rostam hana pesa bali anatumia pesa alizokwapua kwa njia ya kifisadi kumweka fisadi mwenzake madarakani huku akiamini kuwa pindi Lowasa akiwa Rais, fedha zote zitarudi kwa njia ile ile ya kifisadi.

Hahahah sikuzote nasema wewe boya uliyetimuliwa Wama mnambinu za kisengese sana hivi ndo mmekaa eti kwa uharo huu muochanganishe timu ya Lowassa nakuhakikishia unapoteza muda tunajua tunachokifanya na kikubwa waambie wasengei wenzako kuwa mbinu ya kilofa subirini tuwanyoe Lowasa anaingia Ikulu matajiharia
 
Tutakuwa watu wa ajabu sana kama tutachagua viongozi wanaotafuta uongozi kwa kununua watu.

Simiyu yetu wewe ulikua mtu mwema sana na najua mwanzo ulikua na matumaini katika Lowassa wamekuloga watu wa Wama sasa nakuomba kaka yangu jirudi umemsikia Jakaya jana CC alichomwambia mangula na makaratasi yake ya mashtaka ya kipuuzi nakuambia Lowassa mmemtaabisha hajayumba amini amini nakuambia utayakumbuka maneno yangu huyu ndio Rais wa hii Jamhuri
 
Kwani nani alikuambia aliwahi kuondoka Tanzania? Mwanamme kama binti?
 
Matusi ya nini tena wewe punguani?
mnaonaje mkienda kupiga propaganda zenu majukwaani mkatuacha tunajadili mambo ya msingi?kuna repoti ya CAG,kuna hawa wanaitwa UKAWA tunawatathmin ili tuwape nchi.sasa mnakuja kutupigia makelele humu wapuuzi nyie
 
Lowasa angejua asitumie fedha alizonazo kwa kampeni kwani afya take tu ni mzigo kwa Taiga kwani Taifa kitatumia fedha nyingi kwa ajili ya kugharimia matibabu yake.
 
Matusi ya nini tena wewe punguani?
kummaliza Lowasa eleza mazuri ya Membe,punguzeni kutujambia humu kila dakika Lowasa,Lowasa.tambua CCM ni demaged beyond repair na ufisadi wa Lowasa ndio udhaifu wa CCM?!Sasa kama CCM ni imara Lowasa angewezaje kuiba,tena bila kuchukuliwa hatua mpaka dakika hii
 
tungekuwa tunaungana bila kujali itikadi za vyama vyetu kwenye kukemea ufisadi na wizi tungefika mbali sana kama kweli uliyoandika hapa una uchungu na hao mafisadi basi ni muda muafaka kuipumuzishe serikali ya ccm ambayo imeshindwa kuwachukulia hatua wahusika wote .VOTE FOR UKAWA .
 
Mkuu Lizaboni kinacho fanyika sasahvi kwenye siasa ni biashara kubwa ,urais imekua sio kutumikia tena wananchi bali ni biashara tena biashara isiyo na hasara na yenye uhakika wa faida kubwa. Iwe Rostam, iwe apson, iwe Chenge joka kubwa lenye makengeza ,yoyote atakayejiunga na kambi ya Lowasa itakua kwa ajili ya kuchuma pesa tu.

Hao wote uliowataja wanaongoza magenge makubwa ya wafanya biashaara wa ndani na nje ya nchi wanchotaka wao ni kimoja tu Lowasa ashinde kwa namna yoyote ile hata kwa kumtoa Kikwete kesho wanacho taka wao ni kupora rasilimali za Watanzania. Watanzania na tuombe Mungu kikombe hiki kituepuke.
hawa si ndio waliompeleka jk magogoni?iweje Leo muwaone hawafai.ndo maana watu wenye akili zao hawaoni president Wala kiongozi yeyote ccm,hicho kimebaki kichaka cha wezi na wanyanganyi wa haki na Mali za nchi hii na Raia wake
 
Historia itatucheka Watanzania kwa kushabikia wezi waingie ikulu,ni mwaka wa fedheha kwa WaTZ kuchagua kiongozi mwizi
Mkuu kwani tutakuwa tumeanz Leo?JK hakuwa kwenye list of shame?nadhani matokeo ya kuchagua wezi mpaka sasa tunayaona
 
Simiyu yetu wewe ulikua mtu mwema sana na najua mwanzo ulikua na matumaini katika Lowassa wamekuloga watu wa Wama sasa nakuomba kaka yangu jirudi umemsikia Jakaya jana CC alichomwambia mangula na makaratasi yake ya mashtaka ya kipuuzi nakuambia Lowassa mmemtaabisha hajayumba amini amini nakuambia utayakumbuka maneno yangu huyu ndio Rais wa hii Jamhuri

We ndio utapiga kura kwa niaba ya watanzania wote?Mbona mnakua ma stupid hivyo kwa kuendekeza njaa,akikuomba kiduara bila shaka utampa,tena bila hata ya kuombwa
 
Kweli kabla ya October mafisi yameanza kukimbia zizi kama hili jamaa limefunguka.


swissme
hili jamaa ni fisi sana
lilikuwa likidai ccm hamna ufisadi ila leo anawaita wana ccm mafisadi

hili jamaalipo kambi ya Membe na Magufuli wazee wa pesa za LIBYA na bil 262 za wizara ya ujenzi.
 
hawa si ndio waliompeleka jk magogoni?iweje Leo muwaone hawafai.ndo maana watu wenye akili zao hawaoni president Wala kiongozi yeyote ccm,hicho kimebaki kichaka cha wezi na wanyanganyi wa haki na Mali za nchi hii na Raia wake
NJAA inamsumbua kwa kizikosa pesa za ROSTAM
.........jk aliingizwa ikulu na akina nani kama sio ROSTAM
 
Tatizo la ccm nyie ni unafki uliopitiliza...hamna maamuzi,kama lowasa mchafu si mlikuwa mnaweza mpiga chini kwa nini mnashindwa,kazi kujitekenya nakujichekesha
 
Back
Top Bottom