Rostam Aziz amekuja kumharibia Lowasa badala ya kumjenga

Rostam Aziz amekuja kumharibia Lowasa badala ya kumjenga

Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa sasa kuna mgogoro mkubwa ambao umeibuka ndani ya Team Lowasa baina ya wale wanaomuunga mkono Apson Mwang'onda na kambi ya Rostam Aziz. Chanzo changu ndani ya Team Lowasa kimebainisha kuwa mara baada ya ujio wa Rostam, hali ndani ya kambi hiyo imeanza kwenda kombo kutokana na kutofautiana kifalsafa na mbinu za kumpeleka Lowasa Magogoni.

Taarifa zinasema kuwa kambi ya Apson inaundwa na watu weledi na wenye uzoefu kwenye mikakati mbalimbali hasa kutokana na wengi wao kuwa wamewahi kulitumikia taifa hili katika maeneo tofauti. Hata hivyo, weledi wao unaonekana kuwa si lolote wala chochote kutokana na kushindwa kufanikisha kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri kuu ambao wamekuwa wakimkemea waziwazi Lowasa pale anaposhindwa kwenda sambamba na kanuni na maadili ya chama. Pia kambi hii ni masikini na walala hoi kwa vile wamekuwa wakinyonya kambi ya Rostam kifedha kupitia kwa Lowasa mwenyewe. Kwa maana nyingine, kambi hii ni ya wanyonyaji na kwamba wapo kwa Lowasa kimaslahi zaidi na si kufanikisha lengo la Lowasa kwenda Ikulu. Hii ni kambi ya 'KUPE'.

Kambi Rostam, nguli wa kashfa mbalimbali za ufisadi nchini inaundwa na watu wenye jeuri ya pesa ambao wamekuwa wakiitwa au kujiita kwa majina yenye kuonesha jeuri ya pesa kama Mzee wa Vijisenti, Nyoka Mwenye Makengeza nk. Kambi hii inaamini kuwa fedha inaweza kufanya kila kitu ikiwa ni pamoja na kununua haki za wana CCM.

Kwamba wapende wasipende ni lazima Lowasa aende Ikulu kwa vile pesa zipo. Kwa maana nyingine Kambi Rostam ndio wafadhili wakuu wa Team Lowasa kifedha.

Kutokana na jeuri ya pesa waliyonayo, wamefanikisha kumshawishi Lowasa kuwatema baadhi ya washauri wake walio chini ya Apson na kwa sasa Rostam ndiye anayeratibu harakati zote za Lowasa huku akiwatumia vijana wake kama Peter Serukamba na Hussein Bashe.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona kuwa mwelekeo wa Team Lowasa kwa sasa ni mbaya na kwamba lengo lao la kumpeleka Magogoni halitafanikiwa. Kwamba, watu ambao wameteka kambi hiyo hawana taswira nzuri ndani ya chama na kwenye jamii kutokana na kuhusika kwao na kashfa mbalimbali zinazoibuka nchini ikiwa ni pamoja na EPA, RICHMOND, ESCROW, VODACOM nk.

Kwamba, ujio wa Rostam si kwamba amekuja kuimarisha kambi hilo bali amekuja kuliangamiza na kwamba amekuja kuzidisha uchafu kwenye uchafu. Ni sawa na kutupa kinyesi kwenye jalala.

Rostam hana pesa bali anatumia pesa alizokwapua kwa njia ya kifisadi kumweka fisadi mwenzake madarakani huku akiamini kuwa pindi Lowasa akiwa Rais, fedha zote zitarudi kwa njia ile ile ya kifisadi.

Hivi wewe kichwa cha panzi unalipwa sh. ngapi kwa kuchafua watu??
 
Nimeshalieleza hili tangu kitambo. Sipo Team Membe na wala sina kundi. Nipo huru naongozwa na utashi wangu

Rostam Ajawi kushndwa mkakati wowote ni master minder wa hali ya juu tungekua na watanzania kumi kama yeye tungenyooka na kushka adabu
 
Maneno ya jikoni haya. Manamke akiandika huku amelalia kifua cha mwanaume ndo anaandika kama haya aliyoandika Suzan

Hivyo ndivyo akili yako Mkurugenzi mzima wa idara ya Habari na maelezo ilipogotea. Ndio maana idara unayoiongoza imepoteza dira na mwelekeo kutokana na kuongozwa na Mburula kama ww. Hiyo ndio tatizo la vyeo vya kitandani unatoka "kugongwa" na Member hata haujanawa unapewa cheo.
 
Weledi unaozungumzwa hapa ni wa kupanga mikakati. Si vinginevyo. Kumbuka Apson anampigania Lowasa kwa vile ameahidiwa kupewa kazi maalum ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa. Rostam anamsaidia Lowasa kwa lengo la kutunyonya Watanzania. Hizi ni kambi mbili zenye malengo tofauti kwa Lowasa

Sasa tatizo liko wapi hapo?
 
Hivi wewe kichwa cha panzi unalipwa sh. ngapi kwa kuchafua watu??
Kichafu huwa hakichafuliwi. Ni sawa na kinyesi ama mkojo. Lowasa ni mchafu hivyo inashangaza kusikia kuwa anachafuliwa
 
Hivyo ndivyo akili yako Mkurugenzi mzima wa idara ya Habari na maelezo ilipogotea. Ndio maana idara unayoiongoza imepoteza dira na mwelekeo kutokana na kuongozwa na Mburula kama ww. Hiyo ndio tatizo la vyeo vya kitandani unatoka "kugongwa" na Member hata haujanawa unapewa cheo.
Pole sana ndugu. Kama mmezoea kupeana vyeo kwa kugongwa nakuhurumia sana. Sijui wamekugonga wangapi
 
Acheni mambo yaende hivyo hivyo, kifo cha Lowassa kimetimia, kitendo cha kujisahaulisha kuwa Rostam ni miongoni mwa waasisi wa rushwa nchini ni dhahiri Lowassa anajimaliza.
 
Kichafu huwa hakichafuliwi. Ni sawa na kinyesi ama mkojo. Lowasa ni mchafu hivyo inashangaza kusikia kuwa anachafuliwa

Yap ni kweli huko kwenu magamba ugambani wote ni wachafu hakuna msafi hata mmoja ,UKAWA ndiyo mpango mzima chagua CHADEMA ,chagua UKAWA
 
Acheni mambo yaende hivyo hivyo, kifo cha Lowassa kimetimia, kitendo cha kujisahaulisha kuwa Rostam ni miongoni mwa waasisi wa rushwa nchini ni dhahiri Lowassa anajimaliza.
Tena anajimaliza vibaya mno.
 
Yap ni kweli huko kwenu magamba ugambani wote ni wachafu hakuna msafi hata mmoja ,UKAWA ndiyo mpango mzima chagua CHADEMA ,chagua UKAWA
Hahahahahahaaaaa! Mtasota sana mwaka huu. CCM daima ni nambari one. Wengine mtasubiri sana
 
Mkuu Lizaboni kinacho fanyika sasahvi kwenye siasa ni biashara kubwa ,urais imekua sio kutumikia tena wananchi bali ni biashara tena biashara isiyo na hasara na yenye uhakika wa faida kubwa. Iwe Rostam, iwe apson, iwe Chenge joka kubwa lenye makengeza ,yoyote atakayejiunga na kambi ya Lowasa itakua kwa ajili ya kuchuma pesa tu.

Hao wote uliowataja wanaongoza magenge makubwa ya wafanya biashaara wa ndani na nje ya nchi wanchotaka wao ni kimoja tu Lowasa ashinde kwa namna yoyote ile hata kwa kumtoa Kikwete kesho wanacho taka wao ni kupora rasilimali za Watanzania. Watanzania na tuombe Mungu kikombe hiki kituepuke.

Mungu ametupa uwezo na akili timamu ya kujua yapi mazuri na yapi mabaya. Pia ametupa uwezo wa kufanya maamuzi yetu wenyewe bila kushurutishwa.

Naamini kama maombi watu tunafanya sana na kama jib la aina gani ya Kiongozi tunamhitaji naamini tena Mungu ameshatupa, kinachokosekana ni sisi kuamua na hii hatakuja Mungu kukushika mkono ukapige kura abadan.

Kwa hiyo tuache kusema tuombe Mungu atuepushe na kikombe hiki ni sisi wenyewe ndio wakujiepushisha.
 
Last edited by a moderator:
Harakati za Lowassa kuutaka urais kukumbatiwa na watu wachafu kama Rostam ni kielelezo tosha kuwa Lowassa ni mchafu. Hatma ya Tanzania isiyo na watu wachafu Iko mikononi mwa wana CCM.
 
Back
Top Bottom