Rostam Aziz amekuja kumharibia Lowasa badala ya kumjenga

Rostam Aziz amekuja kumharibia Lowasa badala ya kumjenga

Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa sasa kuna mgogoro mkubwa ambao umeibuka ndani ya Team Lowasa baina ya wale wanaomuunga mkono Apson Mwang'onda na kambi ya Rostam Aziz. Chanzo changu ndani ya Team Lowasa kimebainisha kuwa mara baada ya ujio wa Rostam, hali ndani ya kambi hiyo imeanza kwenda kombo kutokana na kutofautiana kifalsafa na mbinu za kumpeleka Lowasa Magogoni.

Taarifa zinasema kuwa kambi ya Apson inaundwa na watu weledi na wenye uzoefu kwenye mikakati mbalimbali hasa kutokana na wengi wao kuwa wamewahi kulitumikia taifa hili katika maeneo tofauti. Hata hivyo, weledi wao unaonekana kuwa si lolote wala chochote kutokana na kushindwa kufanikisha kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa sekretarieti, Kamati Kuu na Halmashauri kuu ambao wamekuwa wakimkemea waziwazi Lowasa pale anaposhindwa kwenda sambamba na kanuni na maadili ya chama. Pia kambi hii ni masikini na walala hoi kwa vile wamekuwa wakinyonya kambi ya Rostam kifedha kupitia kwa Lowasa mwenyewe. Kwa maana nyingine, kambi hii ni ya wanyonyaji na kwamba wapo kwa Lowasa kimaslahi zaidi na si kufanikisha lengo la Lowasa kwenda Ikulu. Hii ni kambi ya 'KUPE'.

Kambi Rostam, nguli wa kashfa mbalimbali za ufisadi nchini inaundwa na watu wenye jeuri ya pesa ambao wamekuwa wakiitwa au kujiita kwa majina yenye kuonesha jeuri ya pesa kama Mzee wa Vijisenti, Nyoka Mwenye Makengeza nk. Kambi hii inaamini kuwa fedha inaweza kufanya kila kitu ikiwa ni pamoja na kununua haki za wana CCM.

Kwamba wapende wasipende ni lazima Lowasa aende Ikulu kwa vile pesa zipo. Kwa maana nyingine Kambi Rostam ndio wafadhili wakuu wa Team Lowasa kifedha.

Kutokana na jeuri ya pesa waliyonayo, wamefanikisha kumshawishi Lowasa kuwatema baadhi ya washauri wake walio chini ya Apson na kwa sasa Rostam ndiye anayeratibu harakati zote za Lowasa huku akiwatumia vijana wake kama Peter Serukamba na Hussein Bashe.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona kuwa mwelekeo wa Team Lowasa kwa sasa ni mbaya na kwamba lengo lao la kumpeleka Magogoni halitafanikiwa. Kwamba, watu ambao wameteka kambi hiyo hawana taswira nzuri ndani ya chama na kwenye jamii kutokana na kuhusika kwao na kashfa mbalimbali zinazoibuka nchini ikiwa ni pamoja na EPA, RICHMOND, ESCROW, VODACOM nk.

Kwamba, ujio wa Rostam si kwamba amekuja kuimarisha kambi hilo bali amekuja kuliangamiza na kwamba amekuja kuzidisha uchafu kwenye uchafu. Ni sawa na kutupa kinyesi kwenye jalala.

Rostam hana pesa bali anatumia pesa alizokwapua kwa njia ya kifisadi kumweka fisadi mwenzake madarakani huku akiamini kuwa pindi Lowasa akiwa Rais, fedha zote zitarudi kwa njia ile ile ya kifisadi.
[/QUOTE

]Lizaboni,msemakweli ni mpenzi wa Mungu. Hivi inauhakika mfalme yeye hausiki kabisa na hizi deal za epa,escrow na zinginezo unazozitaja?Au mnasubiri atoke madarakani ndio muanze kusema?Pia wewe upo team gani?
 
ukisikia kukengeuka ndio hivo...... c wakati kambi kutofautiana ww...na km wamegundua wana tofauti muda huu basi ni dalili za kushinda...hawajachelewa....!!
 
Lizaboni acha kujitoa ufahamu,CCM hakuna msafi.Cha msingi mjiandae kisaikolojia,octoba UKAWA wanakabidhiwa nchi na Watanzania
 
Last edited by a moderator:
Sasa ni dhahiri kuwa joto la mchuano wa urais nchini umefika nyuzi 90 huku wagombea wakiwatumia watu mbalimbali kuwaunga mkono na kuwapigia chapuo.

Yule fisadi namba moja nchini Rostamu Aziz amebeba mikoba ya kumpigania fisadi mwenzake waliyeshirikiana naye kuiua nchi kwa miaka mingi ili aingie ikulu...yeye ameahidiwa uwaziri wa fedha na kusimamia mikataba ya madini na mafuta katika serikali ya fisadi huyo endapo ataukwaa huo urais (GOD forbid).

Watanzania tuwe macho na hawa walaghai
 
Sasa ni dhahiri kuwa joto la mchuano wa urais nchini umefika nyuzi 90 huku wagombea wakiwatumia watu mbalimbali kuwaunga mkono na kuwapigia chapuo. Yule fisadi namba moja nchini rostamu aziz amebeba mikoba ya kumpigania fisadi mwenzake waliyeshirikiana naye kuiua nchi kwa miaka mingi ili aingie ikulu...yeye ameahidiwa uwaziri wa fedha na kusimamia mikataba ya madini na mafuta katika serikali ya fisadi huyo endapo ataukwaa huo urais (GOD forbid).
Watanzania tuwe macho na hawa walaghai

Mbona kwa jk yeye ndie aliyekua mweka hazina na amkusema haya?
 
Mbona aliweza kumuingiza huyu fisadi mwingine anayemaliza muda?
 
Adaiwa kuwa nyuma ya mipango yote ya mgombea mmoja wa Urais mwenye sifa ya kugawa fedha
Aratibu vikao mbalimbali vya Urais nyumbani kwake Adaiwa kuapa: ‘ije mvua, lije jua ni lazima tuinunue nchi' Wachambuzi wahofia kuanguka kwa Taifa iwapo akifanikisha azma yake hiyo. Wakumbushia hoja ya uraia na ufisadi papa, zilizowahi kutolewa na Mtikila na Mengi dhidi yake. Wadadisi wahoji kama alisema kuwa anaachana na siasa uchwara sasa anarudi kufuata

Na Mwandishi Wetu.

Mfanyabishara Rostam Aziz aliyelazimika kujiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011 kwa shinikizo ili kukiokoa CCM na sura za kashfa ya ufisadi zilizokuwa zimekiandama, amerudi kwenye siasa kwa nguvu kubwa huku akiapa kuwa ni lazima ahakikishe anamuingiza Rais wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2015 kwa kutumia fedha alizonazo.

Katika kuitimiza azma yake hiyo ya kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma, tayari amekuwa akiratibu vikao mbalimbali vya kimikakati nyumbani kwake Oysterbay, ili kuhakikisha kuwa mgombea wake ambaye amejijengea sifa ya kuwa mgawaji fedha maarufu kwenye harambee na tafrija mbalimbali, anapitishwa na CCM na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania. Pamoja na kuwa jina lake na la mgombea amtakaye tayari yameshachafuka sana mbele ya macho ya Watanzania, kutokana na kashfa zao za ufisadi zilizowahi kuwakumba huko nyuma; wawili hao wamepanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kununua vyombo vya habari ambavyo watavitumia kuendesha kampeni ya kujisafisha na hatimaye waonekane ni watu safi kabisa mbele ya wananchi. Tayari mgombea huyo wa Rostam amesikika akiwaambia watu wake wa karibu kuwa kambi yake imeshavishika vyombo vya habari karibu vyote hapa nchini.

"Karibu vyombo vya habari vyote vya Tanzania tumeviweka mkononi. Simuoni mtu wa kuzuia harakati zangu, mimi ni kama mafuriko sizuiliki," mgombea huyo alisikika akitamba. Katika kufanikisha harakati zao, wawili hao, wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza ushawishi kwa makundi mbalimbali ya kijamii. Tayari mgombea huyo wa Rostam ameonekana akishiriki harambee mbalimbali na kutoa fedha nyingi na pia amekuwa akitoa kauli zenye kuashiria kujipigia debe ili apitishwe kugombea Urais na CCM. Pia, mgombea huyo ameendesha harakati za chini kwa chini za kuwagawa wabunge na wanachama wa CCM katika makundi ili afanikishe azma yake ya kuupata Urais. Wawili hao ambao wamekuwa pamoja katika harakati za muda mrefu wanadaiwa kujivunia nguvu kubwa ya fedha waliyonayo kufanikisha mambo yao.

Mdau mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedokeza: "Hawa jamaa wanaamini kuwa kwa fedha walizonazo wanastahili kabisa kuinunua nchi. Wanadhani kuwa sifa ya kuwa na fedha nyingi ndiyo sifa ya kipekee kabisa ya wao kupata Urais, masuala ya uadilifu na uaminifu kwao siyo muhimu kabisa." Mtazamo wa wachambuzi wa mambo. Hata hivyo, pamoja na nia yake hiyo, wachambuzi wa mambo, wameyatathmini maisha ya Rostam na kubaini kuwa ni mtu hatari sana ambaye amefanikiwa kupata utajiri mkubwa kutokana na kujihusisha na ‘dili' za kifisadi ambazo zimeliacha taifa katika umaskini mkubwa.

"Huyu mtu ameshiriki katika ufisadi mkubwa ambao umechangia kudhoofisha uchumi wa nchi hii halafu anarudi kwa kutumia fedha alizozipata kifisadi kutaka kuwarubuni Watanzania na kuchukua uongozi tena, hii haikubaliki," mmoja wa wachambuzi ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini alisema. Rostam ametajwa kwenye orodha za matajiri wakubwa Afrika na Jarida la Forbes. Pia inadaiwa kuwa miongoni mwa makampuni anayoyamiliki yeye na familia yake kuwa ni pamoja na: Africa Tanneries Ltd- Mwanza, Tanzania Leather Industry Ltd- MOROGOR, African Trade Development Group (Tz), Tanzania Packages Manufacturing, Caspian construction, New Habari corporation na Wembere Hunting Safari company. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa mara nyingi Rostam hutumia staili ya kuanzisha makampuni kwa kutumia mawakala kufanikisha dili zake.

Inadaiwa kwa hufanya hivi ili yakitokea matatizo aweze kuruka kwamba hahusiki. Tabia ya kukwepa kujibu tuhuma za ufisadi Pia, wachambuzi wamesema kuwa Rostam Aziz amekuwa na tabia ya kukimbia kujibu hoja mbalimbali za ufisadi zinazoibuliwa dhidi yake kwa kutoa matusi kwa watoa hoja hizo. "Kuna kipindi Rostam alibanwa kila kona kuhusu ushiriki wake katika ‘dili' kadhaa za kifisadi. Baada ya kuzidiwa alitumia staili ya kuwaita majina mabaya wale wote ambao walikuwa wakiongelea kuhusu dili zake chafu za kudidimiza uchumi wa nchi huku akizunguka nyuma na kujifanya kuwa yeye ni mtu mwema," anaendelea kueleza mchambuzi huyo.

Imeelezwa kuwa bado taifa halijasahau namna ambavyo Mchungaji Mtikila alipoambiwa arudishe hela alizokopa pale alipoibuka na kuuzungumzia ufisadi wa Rostam. "Kilichomponza Mtikila ni kitendo chake cha kuandika kijarida kilichobeba kichwa cha "Hatima ya Mwajemi Sakarir" alichokitoa mwezi juni mwaka 2008, ambacho kilizungumzia namna ambavyo nchi inatafunwa na pia kikagusa kuhusu maisha na uraia wa Rostam Aziz," mchambuzi mwingine anaeleza. Katika kijarida hicho Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni kiini cha uporaji mkubwa wa rasilimali za nchi unaoendelea kufanyika.

Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliofanyika katika Benki Kuu na Hazina. Sehemu ya kijarida hiyo inaeleza: "Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja na utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya 'mataahira' kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la 'Rostam'. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ng'ombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu." Mtikila alitahadharisha kuwa Watanzania wawe makini kwasababu Rostam anazo hati za kusafiria (passport) mbili ambazo anazitumia kusafiria maeneo mbalimbali na kwamba mambo yakiharibika nchini anahamia nchi nyingine.

"Nilipoanza kuzungumzia uraia wa 'Rostam' Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo…'Rostam' amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli. Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu," Mtikila alieleza katika kijarida hicho.

Mtikila alimalizia kwa kuitaka Serikali imkamate na kumweka ndani Rostam. Siku chache baada ya kutoa tuhuma hizi, Rostam aliibuka na kuitisha mkutano na vyombo vya habari ambako alisema kuwa Mtikila anamwita yeye fisadi wakati alikuwa amemkopesha shilingi milioni tatu na akasema kuwa anabaguliwa kwa kuzingatia misingi ya rangi yake.

Hoja hizi zilipingwa na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa kuwa ni nyepesi ambapo wadau mbalimbali walisema kuwa nchi hii ina maelfu ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia; Kizungu, Kiarabu ambao wana mafanikio makubwa sana kibiashara lakini hawakuwahi kuhusishwa na ufisadi wa kutisha kama alionao Rostam, sasa kwanini yeye aonewe? Ugomvi na Mengi Mbali na Mtikila, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, pia alikumbwa na mkono mkali wa Rostam pale alipomtaja kuwa ni miongoni mwa mafisadi papa wanaoididimiza Tanzania.

Badala ya kuongelea kuhusu tuhuma zake, Rostam aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuanza kumshambulia Mengi kwa kusema kuwa Mengi ni fisadi nyangumi ambaye amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari ‘kuwachafua wenzake' Katika hali ya kushangaza, Rostam alienda mbali zaidi na kuyatumia magazeti na vyombo vya habari anavyovimiliki kuandika habari, makala na tahariri zilizoonyesha kuwa Mengi ni mtu asiyefaa katika Jamii na kwamba wananchi wamchukie. Rostam alisema kuwa Mengi aliifilisi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kukopa deni lililofikia 28 Bilioni. Wakati akimtuhumu Mengi alisahau kuwa na yeye aliinunua kampuni ya ngozi iliyokuwa chini ya umiliki wa Serikali.

Hata pale Rostam aliposhauriwa na watu kuwa kama anaona anazushiwa aende mahakamani kushtaki, alisema kuwa hawezi kwenda mahakamani kwa kuwa tuhuma dhidi yake ni za kutungiwa. Uamuzi wake huu ulitafsiriwa na wengi kuwa ilikuwa ni kama amezikubali tuhuma alizotupiwa za wizi wa mabilioni ya kodi za Watanzania kupitia EPA, Richmond na Dowans. Pia, baada ya kuona ufisadi wake umeanikwa aliamua kuwaandama Dk. Harrison Mwakyembe kama kulipiza kisasi kwa sababu Kamati Teule ya Bunge aliyoiongoza kuanika wizi katika mkataba wa Richmond, ambao Rostam alikuwa na maslahi nayo. Vyombo vyake vikawa vikiwaandama Spika wa Bunge, Samwel Sitta, na viongozi wengine kutokana na sababu hiyo hiyo.

Kutokana na hali hiyo wadau wengi wametahadharisha harakati hizo za wawili hawa kurudi tena kwenye nafasi za uongozi wa nchi kuwa sawa na nchi kuruhusu awamu mpya ya uchotwaji mkubwa wa fedha za wananchi. "Huyu Rostam alipokuwa akijiengua kwenye Ubunge alisema kuwa ameamua kuachana na siasa za Tanzania kwakuwa ni siasa uchwara, sasa anapoamua kumuandaa mgombea Urais maana yake ni kushiriki katika siasa hizo hizo ambazo yeye aliziita kuwa ni uchwara. Inaonekana kuwa wakifanikiwa sasa hivi wataifilisi nchi kabisa," mchambuzi mwingine wa kisiasa alisema.
 
Sitakuja kusahau mradi wa mapacha watatu (lowasa, kiwete na rostam) wa kujichongea kampuni feki ya richmond ambayo haikuwa na fedha, ofisi, mitambo wala uzoefu. Kila siku walikuwa wanaikamua tanzania milioni 152. IMAGINE. Nasikia wasingeshitukiwa kwenye dili hii walikuwa wameesha undakampuni km 20 feki ili kurudisha pesa walizokuwa wametumia wkt wa uchaguzi. Style ileile waliyotumia kumuingiza kikwete wanataka kuitumia tena. ZILE KAMPUNI FEKI 20 AMBAZO ZILIFELI KUINGIZWA KWENYE SYSTEM SASA ZITATUMIKA KUPORA UTAJIRI WA NCHI KM KWELI IKATOKEA lowasa jambazi sugu na fisadi papa akawa rais wa tz
 
rostam amerudi kwa kasi kuja kumuunga mkono rafiki yake. inasadikika wamefanikiwa kuiteka ccm kwa 79% na wanaendelea kupambana. watanzania tuamke toka usingizini mafisadi wanapambana kuhakikisha mtu wao anaingia magogoni
 
Adaiwa kuwa nyuma ya mipango yote ya mgombea mmoja wa Urais mwenye sifa ya kugawa fedha
Aratibu vikao mbalimbali vya Urais nyumbani kwake Adaiwa kuapa: ‘ije mvua, lije jua ni lazima tuinunue nchi’ Wachambuzi wahofia kuanguka kwa Taifa iwapo akifanikisha azma yake hiyo. Wakumbushia hoja ya uraia na ufisadi papa, zilizowahi kutolewa na Mtikila na Mengi dhidi yake. Wadadisi wahoji kama alisema kuwa anaachana na siasa uchwara sasa anarudi kufuata

Na Mwandishi Wetu.

Mfanyabishara Rostam Aziz aliyelazimika kujiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011 kwa shinikizo ili kukiokoa CCM na sura za kashfa ya ufisadi zilizokuwa zimekiandama, amerudi kwenye siasa kwa nguvu kubwa huku akiapa kuwa ni lazima ahakikishe anamuingiza Rais wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka 2015 kwa kutumia fedha alizonazo.

Katika kuitimiza azma yake hiyo ya kuingia Ikulu kwa mlango wa nyuma, tayari amekuwa akiratibu vikao mbalimbali vya kimikakati nyumbani kwake Oysterbay, ili kuhakikisha kuwa mgombea wake ambaye amejijengea sifa ya kuwa mgawaji fedha maarufu kwenye harambee na tafrija mbalimbali, anapitishwa na CCM na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania. Pamoja na kuwa jina lake na la mgombea amtakaye tayari yameshachafuka sana mbele ya macho ya Watanzania, kutokana na kashfa zao za ufisadi zilizowahi kuwakumba huko nyuma; wawili hao wamepanga kutumia kiasi kikubwa cha fedha kununua vyombo vya habari ambavyo watavitumia kuendesha kampeni ya kujisafisha na hatimaye waonekane ni watu safi kabisa mbele ya wananchi. Tayari mgombea huyo wa Rostam amesikika akiwaambia watu wake wa karibu kuwa kambi yake imeshavishika vyombo vya habari karibu vyote hapa nchini.

“Karibu vyombo vya habari vyote vya Tanzania tumeviweka mkononi. Simuoni mtu wa kuzuia harakati zangu, mimi ni kama mafuriko sizuiliki,” mgombea huyo alisikika akitamba. Katika kufanikisha harakati zao, wawili hao, wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza ushawishi kwa makundi mbalimbali ya kijamii. Tayari mgombea huyo wa Rostam ameonekana akishiriki harambee mbalimbali na kutoa fedha nyingi na pia amekuwa akitoa kauli zenye kuashiria kujipigia debe ili apitishwe kugombea Urais na CCM. Pia, mgombea huyo ameendesha harakati za chini kwa chini za kuwagawa wabunge na wanachama wa CCM katika makundi ili afanikishe azma yake ya kuupata Urais. Wawili hao ambao wamekuwa pamoja katika harakati za muda mrefu wanadaiwa kujivunia nguvu kubwa ya fedha waliyonayo kufanikisha mambo yao.

Mdau mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake amedokeza: “Hawa jamaa wanaamini kuwa kwa fedha walizonazo wanastahili kabisa kuinunua nchi. Wanadhani kuwa sifa ya kuwa na fedha nyingi ndiyo sifa ya kipekee kabisa ya wao kupata Urais, masuala ya uadilifu na uaminifu kwao siyo muhimu kabisa.” Mtazamo wa wachambuzi wa mambo. Hata hivyo, pamoja na nia yake hiyo, wachambuzi wa mambo, wameyatathmini maisha ya Rostam na kubaini kuwa ni mtu hatari sana ambaye amefanikiwa kupata utajiri mkubwa kutokana na kujihusisha na ‘dili’ za kifisadi ambazo zimeliacha taifa katika umaskini mkubwa.

“Huyu mtu ameshiriki katika ufisadi mkubwa ambao umechangia kudhoofisha uchumi wa nchi hii halafu anarudi kwa kutumia fedha alizozipata kifisadi kutaka kuwarubuni Watanzania na kuchukua uongozi tena, hii haikubaliki,” mmoja wa wachambuzi ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini alisema. Rostam ametajwa kwenye orodha za matajiri wakubwa Afrika na Jarida la Forbes. Pia inadaiwa kuwa miongoni mwa makampuni anayoyamiliki yeye na familia yake kuwa ni pamoja na: Africa Tanneries Ltd- Mwanza, Tanzania Leather Industry Ltd- MOROGOR, African Trade Development Group (Tz), Tanzania Packages Manufacturing, Caspian construction, New Habari corporation na Wembere Hunting Safari company. Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa mara nyingi Rostam hutumia staili ya kuanzisha makampuni kwa kutumia mawakala kufanikisha dili zake.

Inadaiwa kwa hufanya hivi ili yakitokea matatizo aweze kuruka kwamba hahusiki. Tabia ya kukwepa kujibu tuhuma za ufisadi Pia, wachambuzi wamesema kuwa Rostam Aziz amekuwa na tabia ya kukimbia kujibu hoja mbalimbali za ufisadi zinazoibuliwa dhidi yake kwa kutoa matusi kwa watoa hoja hizo. “Kuna kipindi Rostam alibanwa kila kona kuhusu ushiriki wake katika ‘dili’ kadhaa za kifisadi. Baada ya kuzidiwa alitumia staili ya kuwaita majina mabaya wale wote ambao walikuwa wakiongelea kuhusu dili zake chafu za kudidimiza uchumi wa nchi huku akizunguka nyuma na kujifanya kuwa yeye ni mtu mwema,” anaendelea kueleza mchambuzi huyo.

Imeelezwa kuwa bado taifa halijasahau namna ambavyo Mchungaji Mtikila alipoambiwa arudishe hela alizokopa pale alipoibuka na kuuzungumzia ufisadi wa Rostam. “Kilichomponza Mtikila ni kitendo chake cha kuandika kijarida kilichobeba kichwa cha "Hatima ya Mwajemi Sakarir" alichokitoa mwezi juni mwaka 2008, ambacho kilizungumzia namna ambavyo nchi inatafunwa na pia kikagusa kuhusu maisha na uraia wa Rostam Aziz,” mchambuzi mwingine anaeleza. Katika kijarida hicho Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni kiini cha uporaji mkubwa wa rasilimali za nchi unaoendelea kufanyika.

Mtikila alimtaja Rostam kuwa ni mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati iliyo mingi ya wizi wote uliofanyika katika Benki Kuu na Hazina. Sehemu ya kijarida hiyo inaeleza: “Mwajemi huyu jina lake halisi alilopewa pamoja na utambulisho wake alipozaliwa kule kwao Iran ni SAKARIR mwana wa AZIZ. Sakarir alipokuja Tanzania kuipora Nchi ya 'mataahira' kama anavyopenda kutudharau yeye mara nyingi, alijipa jina la 'Rostam'. Wazazi wa Sakarir hawajawahi kuishi hapa, wapo kwao Iran, wakiwa na biashara kubwa ya nyama na kufuga ng’ombe. Sakarir alipozaliwa alipata elimu yake ya msingi kwao Iran, na baadaye akapata elimu ya juu Uingereza ambako pia anao ndugu.” Mtikila alitahadharisha kuwa Watanzania wawe makini kwasababu Rostam anazo hati za kusafiria (passport) mbili ambazo anazitumia kusafiria maeneo mbalimbali na kwamba mambo yakiharibika nchini anahamia nchi nyingine.

“Nilipoanza kuzungumzia uraia wa 'Rostam' Aziz alibabaisha kuwa alizaliwa Ndala Mission, lakini ni mwongo…'Rostam' amepata kudanganya kwamba alisoma shule ya msingi Mwisi, alipoona atagundulika upesi akasema alisoma Mwamala, Nzega, lakini siyo kweli. Rostam Aziz anazo Passport mbili za kusafiria, yaani ya nchi yetu ambayo aliipata kwa udanganyifu, anayoitumia kusafiria hadi Nairobi, na ya kwao Uajemi yaani Iran ambayo husafiria kutoka Nairobi kwenda kwao, Dubai na kwingine alikolimbikiza mapesa aliyaipora Nchi yetu,” Mtikila alieleza katika kijarida hicho.

Mtikila alimalizia kwa kuitaka Serikali imkamate na kumweka ndani Rostam. Siku chache baada ya kutoa tuhuma hizi, Rostam aliibuka na kuitisha mkutano na vyombo vya habari ambako alisema kuwa Mtikila anamwita yeye fisadi wakati alikuwa amemkopesha shilingi milioni tatu na akasema kuwa anabaguliwa kwa kuzingatia misingi ya rangi yake.

Hoja hizi zilipingwa na wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa kuwa ni nyepesi ambapo wadau mbalimbali walisema kuwa nchi hii ina maelfu ya wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia; Kizungu, Kiarabu ambao wana mafanikio makubwa sana kibiashara lakini hawakuwahi kuhusishwa na ufisadi wa kutisha kama alionao Rostam, sasa kwanini yeye aonewe? Ugomvi na Mengi Mbali na Mtikila, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, pia alikumbwa na mkono mkali wa Rostam pale alipomtaja kuwa ni miongoni mwa mafisadi papa wanaoididimiza Tanzania.

Badala ya kuongelea kuhusu tuhuma zake, Rostam aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuanza kumshambulia Mengi kwa kusema kuwa Mengi ni fisadi nyangumi ambaye amekuwa akitumia vyombo vyake vya habari ‘kuwachafua wenzake’ Katika hali ya kushangaza, Rostam alienda mbali zaidi na kuyatumia magazeti na vyombo vya habari anavyovimiliki kuandika habari, makala na tahariri zilizoonyesha kuwa Mengi ni mtu asiyefaa katika Jamii na kwamba wananchi wamchukie. Rostam alisema kuwa Mengi aliifilisi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kukopa deni lililofikia 28 Bilioni. Wakati akimtuhumu Mengi alisahau kuwa na yeye aliinunua kampuni ya ngozi iliyokuwa chini ya umiliki wa Serikali.

Hata pale Rostam aliposhauriwa na watu kuwa kama anaona anazushiwa aende mahakamani kushtaki, alisema kuwa hawezi kwenda mahakamani kwa kuwa tuhuma dhidi yake ni za kutungiwa. Uamuzi wake huu ulitafsiriwa na wengi kuwa ilikuwa ni kama amezikubali tuhuma alizotupiwa za wizi wa mabilioni ya kodi za Watanzania kupitia EPA, Richmond na Dowans. Pia, baada ya kuona ufisadi wake umeanikwa aliamua kuwaandama Dk. Harrison Mwakyembe kama kulipiza kisasi kwa sababu Kamati Teule ya Bunge aliyoiongoza kuanika wizi katika mkataba wa Richmond, ambao Rostam alikuwa na maslahi nayo. Vyombo vyake vikawa vikiwaandama Spika wa Bunge, Samwel Sitta, na viongozi wengine kutokana na sababu hiyo hiyo.

Kutokana na hali hiyo wadau wengi wametahadharisha harakati hizo za wawili hawa kurudi tena kwenye nafasi za uongozi wa nchi kuwa sawa na nchi kuruhusu awamu mpya ya uchotwaji mkubwa wa fedha za wananchi. “Huyu Rostam alipokuwa akijiengua kwenye Ubunge alisema kuwa ameamua kuachana na siasa za Tanzania kwakuwa ni siasa uchwara, sasa anapoamua kumuandaa mgombea Urais maana yake ni kushiriki katika siasa hizo hizo ambazo yeye aliziita kuwa ni uchwara. Inaonekana kuwa wakifanikiwa sasa hivi wataifilisi nchi kabisa,” mchambuzi mwingine wa kisiasa alisema.
Ina maana kanunua hadi vyombo vya mzee Mengi? Kweli pesa haina adabu. Si Rostam huyu rafiki wa Lowassa alimtukana Mengi kwenye vyombo vya habari leo vyombo vya IPP vinamsaidia rafiki yake Lowassa awe rais? Mengi upo?
 
Back
Top Bottom