Jk aliingizwa uraisi kwa rusha hivi hivi na kwa mshikamano wa kambi yake ikiongozwa na Edward Lowasa na Rostam Aziz. Kiasi hata taarifa ya tume ya nidhamu haikusomwa ili mradi tu mlengwa aende magogoni. Leo kila mtu ni shahidi wa wapi taifa lilipo.
Rostam si Mtanzania, kinachomrudisha kuja kuanza kutuletea uharamia wake hapa ni nini kama si maslahi binafisi? Nchi isiyo na mwenyewe. Kama anauchungu na taifa, mbona anapoona mgombea wake anaelekea kukwama anaanza kutoa machozi. Machozi hayo ni ya kuwapenda sana watanzania au machozi ya mamba akikosa mawindo?
Na mfahamu hayo ndiyo yalikuwa makubaliano yao kwamba baada ya huyu wa sasa, eddo aingie ikulu.
Ninashangaa ccm hakuna hata mmoja aliyesalia mwenye maarifa na uzalendo akakakemea huu ugaidi?
Nguvu ya rushwa na udanganyifu unaotumika kwenye mafisadi kwenda ikulu = uzembe wa wana ccm maskini na hohehahe wasiojitambua wanaoimba nyimbo za kusifu maamuzi ya kifisadi ya chama bila kujua wanaua watoto wao na vizazi vyao.
Sasa lililopo ni kila mtanzania mwenye nia njema, kazi iwe moja. Peleka habari kwa mdomo kwa kila Mtanzania maskini, mgonjwa, aliyekoseshwa elimu kwa sababu ya ufisadi, aliyepoteza wazazi na ndugu kwa sababu ya ufisadi, aliyekosa mahala pa kuishi kwa sababu ya ufisadi na yeyote asiyejua kama atakula nini kesha kwa sababu ya ufisadi. Sote tuungane bila kujali vyama, dini wala kabila, tukajiandikishe kwa wingi ili siku ya kura tuikatae Ccm na ufisadi wao wajibebe!.
Ndugu zangu, kumbukeni wana ccm wakawaida hawafaidiki lolote kwenye ufisadi ila wanatumika tu. Misiba inayoletwa na ufisadi inatukumba wote, tunazika kwa wanaccm na kusiko na ccm. Ongezeko la majuha ni watoto wetu sote wana ccm na wasio. Maisha mabaya ni kwa wanaccm na wasio. Wanaofaidi ni mafisadi tu.
Tuungane sote, kwa nguvu zetu zote ccm ifutike kwa sababu ni mkono wa shetani ndani ya Tanzania.
Mwenye kufundisha afundishe.
Mwenye kutunga nyimbo atunge.
Mwenye sanaa za maigizo yatungwe na yaonyeshwe.
Mwenye kutayarisha prints kwenye mavazi afanye hivyo.
Mwenye kuandika vipeperushi atawanye kwa wingi.
Mwenye kuandika kwenye product zinazotumika majumbani kama viberiti, sabuni na mafuta, aweke label.
Mwenye kusimama jukwaana anene.
Mwenye ndugu na uwezo wa nyumba kwa nyumba asichoke.
Mwenye Kumch Mungu, aombe sana.
Mwenye chombo cha usafiri abandike mabandiko.
Ili kwa umoja wetu tukajiandikishe na 25 tukapig kura kinyume na ccm. Tanzania kwanza, vyama vitajengwa ndani ya Tanzania huru.