Uvamizi JF una uhusiano na Press ya Rostam Aziz?

Uvamizi JF una uhusiano na Press ya Rostam Aziz?

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
581
Jana majira ya mchana ziliibuka habari za kuvamiwa kwa Ofisi za JF Mikocheni.

Inasemekana wavamizi walikuwa wanamtafuta Ndg Melo.

Usiku wa Jana hiyo hiyo Mfanyabiashara mashuhuri Rostam Aziz alionekana akitolea maelezo baadhi ya mambo anayotajwa kuhusika nayo kwenye biashara zake na pia kundi la Mtandao analodaiwa kuwa kinara wake ndani ya CCM.

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita tulitangaziwa kuwa Rostam angekuwa Live UTV. Haikuwa hivyo mpaka hapo jana ambapo alitoa press yake ikiwa imerekodiwa.

Bila shaka yoyote, makonzi ambayo amekuwa akipokea Rostam kutoka kwa wale wanaokosoa, yamemsababishia maumivu kwa namna Moja au nyingine ndio maana kajitokeza kujibu kama njia ya kujisafisha na kupunguza maumivu pia.

Kwa maelezo yake, unamuona Rostam mjanja, unamuona Rostam mzalendo, unamuona Rostam msafi na unamuona Rostam Mtanzania.

Kutokana na tuliyoambiwa mwanzo kuwa angeruka live UTV, lakini badala yake akatoa press akiwa ame rekodiwa, binafsi naona Kuna uoga fulani, Kuna kutojiamini kwa namna fulani.

Bila shaka, inawezekana Rostam alijua wazi kuwa baada ya hiyo Press yake, kutakuwa na outbreak kubwa ya watu kuhoji na kukosoa maelezo yake.

Podium kubwa ya wakosoaji na wapongezaji ni mitandao ya Kijamii ikiwa ni pamoja na JF.

Yaweza kuwa wavamizi wa JF wanalenga kumtisha boss wa mtandao huu wa Kijamii na wanachama wake, ili baada ya hiyo Press ya Rostam, kuwe na hofu katika kuhoji, kudadavua na hata kukosoa majibu aliyoyatoa kwenye Press hiyo kutokana na mengi yanayosemwa dhidi yake.
 
Back
Top Bottom