Mambo ya kiroho ni magumu sana
DHAMBI zote zasameheka isipokua tu ile ya kumdharau ROHO MTAKITIFU
Rostam Ni Muislam Huu Ni Unafiki Analake Jambo Anatoa Rushwa Kumba Spika Kwa Mlango Wa Nyumba.wana Kkkt Chukueni Hela Hiyo Mungu Kampa Uwezo Wakuja Kuleta Hela
Anajipendekeza Kwa Spika
Kama Baba mwenyewe na Mwana mtakatifu ni sawa ama Wakuu kuliko Roho Mtakatifu, kwa nini hiyo iwe ndio dhambi isiyosameheka?
Na kwa nini kuwe kuna dhambi isiyosameheka?
Kwani Rostam kaenda kuomba msamaha ama ametoa pesa na kusema AMANI IOMBEWE KWA TAIFA?
Sasa mtuhumiwa top aje kutoa milioni saba kanisani na huku akisema amani iombewe,je alishawaambia waumini hao kuwa ni kwanini kutuhumiwa kwake ni upotevu wa AMANI?
Na ndio maana msimamo wangu ni kwamba...WAZIRUDISHE PESA HIZO HADI RIPOTI ZITAKAPOSOMWA NA UAMUZI KUTOLEWA NA BUNGE!
Tusichanganye mambo ya SIASA na KIROHO
Hukumu zote ziwe za kisiasa (yaliyo yake kaizar) Na hukumu za kiroho (Mungu) tumuachie yeye.
Kukataa zaka tayari ni hukumu ya kiroho inamaana hapo huyo Pasta kasimama nafasi ya MUNGU kumhukumu RA.
Enyi watu wa mataifa kuweni waelevu kama NYOKA
Tena nawaembieni muombapo jifungieni ktk vyumba vyenu kwani Baba aliye juu awaona na hakika mkifanya hivyo sara zenu zitapokelewa.
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).
Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...
Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.
Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!
Msingi wa haki uko kwenye sheria na si kanisani!
Huko kanisani ni politics tu!
Sheria ni mahakamani na bungeni....Huko chachi ni mwendo ule ule wa kujisafisha!
Walianza na ukabila na udini ukagoma...Sasa ni ziara za makanisani na misikitini...Subirini muone..Mambo ni tight kwani JK mwenyewe yuko huko G8 summit na akishatoka huko na majibu ama maamuzi ya ripoti zote!
Kama ni wote wameguswa basi watajiuzulu..Kwani tumeshawapa ushauri na wamegoma!
Kanisa halifuati sheria za dunia hii ,kanisa sheria zake kofi la kushoto mpe la kulia pia,akikunyanganya shati mwachie na joho pia.
MIsingi ya haki ni UPENDO wapendeni adui zenu ,maana mkipendana ninyi kwa ninyi nao wapendana wao kwa wao na tofauti yenu na wao itakua ipi??
Kwa mantiki hiyo unawataka waumini wamchaguwe tena ili aendeleze ufisadi kwa kutumia huo mfano wa sheria ya dini ya kuachiana na joho?
Yani sasa washaachiwa mali zote za nchi...Na hivyo milioni saba ni kibao na sasa upande wa pili wa shavu ni upi huo?
Na shati ndio kiwira na Richmond...Joho itakuwa nini tena?
Ama kibao ndio ufisadi? Hakuna upande mwingine wa shavu wa kupiga na hakuna joho la kumwachia mnyang'anyi!
Wametuacha uchi na yatima...Hawawezi kutupora kingine chochote na hatuna kingine cha kuwapa zaidi ya uhai wetu ambao hata hivyo inavyoelekea wanataka tuamini kuwa uko mikononi mwao na si mikononi mwa Mungu.
Milioni saba zitatupa amani? Ama utazilinganisha na mabilioni ya dola walizokwapua? Milioni saba si ela ya kula tu kwa watu kama yeye?
Jibu ni BIG NO!
Je Migodi yetu na mali nyingine ikiwa ni pamoja na mabilioni ya dola vitatupa amani...
Jibu hapa ni BIG YES...ONLY KAMA TUKIZIKA TOFAUTI ZETU ZA KIDINI NA KIKABILA NA ADUI YETU KUWA MMOJA....MFISADI!
ni saa ya UHURU!
Yaliyo ya Kaizar mpeni kaizar na yake Mungu mpeni Mungu.
RA mhukumuni kwa sheria zenu za kikaizar Na msimulazimishe Pasta amuhukumu kwa sheria ya Mungu
Sheria za Mungu ndizo makanisa wanazozifuata kama hawawezi kuzitekeleza basi wanakuwa ni wanafiki maana mahubiri yao na matendo yako yametofautiana kama usiku na mchana.
Sheria za Mungu ni kuwa HAKIMU mtoa hukumu ni yeye tu yani Mungu na sheria yake nyingine ni Usihukumu maana kipimo chahukumu ukitoacho ndicho hichohicho utachopimiwa.Na akohoji wakiona je kijiti kilicho ndani ya jicho la rafiki yako yumkini ktk jicho lako kuna boriti??
Mama kanisani zinaenda hela zote,chafu na nzuri na ndio maana kuna dhana ya kutakasa vipaji.Au wee unasemaje?kanisani nao wakapokea za ufisadi, Yesu na Maria na Yosef!