Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 2,696
- 5,324
Katika mmoja ya wasanii ambao Tanzania imebarikiwa kuwa nao na wana vipaji vya ajabu ni Rose Muhando hakika hakuna atakaepinga hilo na nyimbo zake kwa miaka mingi zimetubariki na kutusogeza karibu na muumba kwa namna ya pekee kabisa, Mungu aendelee kumbariki.
Wengi wasichokijua ni kuwa Rose Muhando alizaliwa katika familia ya kiislamu na akapewa jina la Shadya Muhando na akapata makuzi ya dini hiyo akiimba kaswida na kujifunza Quran ambapo alimudu kuhifadhi juzuu zote 30 na anasema alikuwa na bidii kubwa sana Madrasa.
Baba yake alikuwa ni Sheikh mkubwa tu huko Dumila Morogoro na ndio alimpa muongozo ya dini hiyo.
Alipokuwa mdogo aliugua na kukonda sana kitu kilichomsumbua kwa muda mrefu na afya yake ilikuwa dhoofu kisa hayo maradhi
Ilifikia kipindi anasema alikonda sana kiasi akilalia mkeka ngozi inashikana na kubaki kwenye mkeka
Familia ilijaribu kumpa matibabu mpaka kwa waganga mbalimbali lakini hakufanikiwa kupata tiba hivyo familia ikaacha tu liwalo na liwe kwani imeshindikana
Wakati akiwa bado mahututi kitandani anajiuguza na hajajiweza kwa muda wa mwaka mmoja siku moja usiku mwangaza mkubwa ulitokea nyumbani kwao ambapo yeye, Baba yake na Mama yake waliuona
Ndani ya ule mwangaza alimuona mtu mweupe ambaye alijitambulisha kama masihi akimwambia inuka nimekuponya ili uje unitumikie
Baada ya mwanga kupotea alipiga yowe akihisi ni ndoto kuwa amepona na kweli akaweza kusimama, Baba na Mama yake walipigwa na butwaa wasijue cha kusema kwani waliuona mwangaza japo yale maneno aliyoyasikia Rose hawakusikia
Kesho yake ilikuwa gumzo kubwa mtaani kwao iweje mtu aliye lala takribani mwaka mzima mahututi ndani kuweza kunyanyuka ndani ya usiku mmoja tu kufumba na kufumbua
Baada ya hapo alijiuliza sana yule mtu ni nani, asipate majibu wakati huo alikuwa na miaka 9 na sauti hiyo ilikuwa ikiendelea kujirudia mara kwa mara
Kuna jirani yao walimmegea shamba ili awe analima alikuwa ni mlokole na alikuwa anataja mara kwa mara jina la mtu huyo
Ndipo Rose alipomfata na kumwambia amwambie habari za mtu huyo ni nani na ikibidi ampeleke kwake maana alisikia sauti yake akijitambulisha kwa jina ila hamjui
Yule Mama Mlokole akamjulisha kuwa huyo unaemsema ni YESU na hayupo hapa duniani bali mbinguni, ila akamshauri akitaka kumjua zaidi hana budi kuokoka na kukubali kubatizwa
Alipofika miaka kumi na miwili akarudisha juzuu madrasa na akamwambia Baba yake anaenda kubatizwa, hii ilizua tafrani nyumbani na kwa nduguze
Siku ya kubatizwa wengi walijaa kanisani kuona kwani alikuwa anafahamika na wengi hapo Dumila
Akabatizwa katika kanisa la Anglikana hapo Dumila, na kupewa Jina Rose lakini uamuzi huo haukupokelewa vyema na nduguze hatimae akafukuzwa kwao na kuhangaika mitaani mpaka watu wa kanisani walipomchukua na kumuhifadhi
Akaanza kuimba kwaya, alipoiva zaidi akaanza kufundisha yeye kutokana na kutokea katika dini isiyo ya ukristo akashauriwa kujifunza masomo ya biblia ambapo aliisoma kwa muda wa miaka miwili huko Morogoro
Akaenda Arusha kufundisha kwaya, kisha akarejea Dodoma ambapo alifanya kazi ngumu ili aishi, mwaka 1997 akataka kurekodi nyimbo zake mwenyewe alipomshirikisha mmoja ya watu kanisani akamshauri wafunge na kuomba ili wapate jibu
Jibu lilikuja asubiri miaka saba ndipo arekodi, akakata tamaa juu ya muziki hasa kurekodi nyimbo zake mwenyewe akaendelea tu na maisha
Baadae sana, alimwomba mchungaji mmoja amsaidie kurekodi baada ya kuulizwa angependa afanye nini, akaenda Dar kwa Master Jay ambapo alitunga albamu nzima kwa siku tatu na kufanya mazoezi ndani ya siku tatu peke yake
Kisha alirekodi nyimbo zote ndani ya siku moja tena one take bila kukosea mpaka studio wakashangaa, hakujua afanye nini baada ya kurekodi kwani yeye kiu yake ilikuwa kurekodi tu basi
Prodyuza akamshauri apeleke albamu kwa wahindi kwani wengine wanapeleka huko, basi akaipeleka albamu na ikatokea kupendwa sana ndipo akakumbuka kuwa nyuma alipata ufunuo kuwa asubiri mpaka baada ya miaka 7 ili arekodi na mwaka huo wa saba ndio 2004 albamu ya mteule uwe macho inaingia sokoni
Ndipo alipostaajabu juu ya kufunuliwa kule na jinsi ilivyokuja kuwa kweli
Tokea hapo kilichofuatia ni historia wote mnakijua, na hiyo ndio historia fupi ya huyu Mama mwenye sauti ya kipekee
(nimeiandika kwa upendo tu kama kuna mahali nimekosea mniwie radhi)
SOURCE : ushuhuda alioutoa kanisani inapatikana pia Youtube pia na mahojiano na vituo mbalimbali vya habari ikiwemo Clouds Media.