Rose Mhando achumbiwa, atambulishwa ukweni Kahama

Jemima Mrembo

JF-Expert Member
Jul 19, 2021
2,791
8,005
ROSE MUHANDO ACHUMBIWA NA KUTAMBULISHWA UKWENI KAHAMA.

IMG-20231006-WA0161.jpg

Wiki hii imekuwa wiki ya baraka kwa Malkia wa nyimbo za Injili Tanzania, Rose Muhando baada ya kwenda kutambulishwa ukweni Kahama kwa ndugu wa mchumba wake. Kama wanavyoonekana pichani Rose Muhando akiwa na mawifi zake na mwanaume wa pembeni yake aliyevaa t-shirt rangi nyekundu ndiye mume wake mtarajiwa.

Kama atafanikiwa kuolewa na ndoa ikapita salama basi hii itakuwa ndoa yake ya kwanza kwa mwanamama huyo mwenye watoto watatu ambao amezaa na wanaume tofauti.

Mungu awaongoze na ikawe ndoa ya kheri🙏
 
Nimejaribu kupiga hesabu ya Ndoa nilizoziona Mwaka Huu hadi kufikia sasa ni Wanawake zaidi ya 25 wameolewa.

Kati yao mabinti wenye miaka 21 hadi 28 (Slay queen) ni 7

Na Wanawake wa miaka 29 hadi 34 ni 9

Wanawake wenye umri wa miaka 35 na zaidi (Mashangazi) kama wanavyofahamika na Vijana wengi ni 9

Huenda Waoaji wengi wanaangalia Akili za Mwanamke(Maturity) katika kufanya maamuzi ya Kuoa, maana Slay queen wengi huwa ni mapepe na hawajui kutulia.

Kwa trend hii ya Ndoa za Mashangazi inaonesha Umri ni namba tu.

Kila la Kheri Rose Mhando, kwenye hatua inayofuata.
 
Back
Top Bottom