Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,289
Hii ishu ya ndoa ukikurupuka kama mwendawazimu hutoweza kuelewa.
Hii ishu kuna kipindi ilishajadiliwa sana mpaka tukapata kuelewa kuwa kisheria mtu ukikaa na mpenzi within a 6 mnth basi huyo atahesabika kuwa mke wako kihalali na hata siku mkitengana basi utalazimika kugawana nae mali mlizochuma.
Tuchukulie hicho kipengele ni kweli (kuwa ni miezi sita na sio miaka miwili) basi kuna uwezekano wa kuwa Dr.Slaa ni mume wa Rose Kamili kama mwenyewe (Rose Kamili) anavyodai kuwa waliishi pamoja kama mke na mume na hivyo inabidi aachane na Rose Kamili kwanza ndio aoe mwanamke mwengine.
Tukichukulia kuwa hilo halipo, hakuishi na Rose Kamili, walikuwa wanapeana ngono tu hadi kuzaa watoto wawili basi kuna hili la Josephine. Ya kuwa, hata kama Dr.Slaa anaishi na Josephine sasa kwa zaidi ya miezi sita, haiondoi ukweli kuwa Josephine ni mke wa mtu mwengine kisheria na serikali haiwezi kuandika cheti cha ndoa kati ya Josephine na Slaa kwa sababu tayari ni mke wa mtu kisheria [Unless useme mwanamke mmoja anaweza kuwa na waume wawili KISHERIA kwa wakati mmoja]