Mbeya: Dkt. Slaa akataa kuchukuliwa Sample ya Sauti yake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,733
218,322
Screenshot_2023-08-16-21-04-00-1.jpg


Taarifa iliyotolewa na Wakili wa Dr Slaa inasema kwamba , kabla ya kufikishwa Mahakamani leo Polisi walitaka kuchukua Sample ya Sauti ya Dkt Slaa (Haifahamiki walitaka kuifanyia nini) , ambapo Dkt Slaa amekataa jambo hilo kufanyika , kwa vile tayari polisi walishasema wanayo sauti yake ambayo wanadai waliinasa akipanga Uhaini wake , basi ni vema wakiitumia hiyo waliyo nayo ili kufanyia mambo yao .

Vinginevyo Wakili wake amedai kwamba wakitaka sauti ya Dkt Slaa basi wafungue kesi mahakamani kuiomba sauti hiyo , inatajwa kwamba jambo hili ndilo limekwamisha Watuhumiwa hao kufikishwa Mahakamani siku ya leo kutokana na mabishano makali kuhusu Sauti hiyo .

========

Bali wadau wengi wanaona Polisi hawakujipanga na kesi hii wameburuzwa tu na Watawala ili kuwalinda Waarabu wa DP WORLD , na ndio maana wanaokoteza
na kuunga unga sauti ya Dkt Slaa ili kutengeneza ushahidi wa magumashi .

Lakini ni vema tukafahamu kwamba , Hakuna popote pale kwenye dunia hii ambako Shetani aliwahi kumshinda Mungu.
---

DKT. SLAA AKATAA KUCHUKIWA SAMPLE YA SAUTI YAKE MBEYA, WAKWAMA KUPELEKWA MAHAKAMANI.

Wakili wa Balozi Dkt. Wilbroad Slaa, Dickson Matata, amesema mchakato wa kumpeleka mahakamani mteja wake Balozi Dkt Slaa na wenzake umekwama baada ya kutokea mabishano ya kisheria katika kituo cha Polisi cha kati Mkoani Mbeya, baada ya kukataa kutoa sampuli ya sauti yake akiwa kituoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari Wakili Matata amesema mteja wake Balozi Dkt Slaa alisafirishwa usiku wa kuakia Jana hivyo ameonananae mapema hii leo Ili kuanza taratibu za kwenda mahakamani, ambazo zimeshindikana kwa sababu za kiupelelezi ikiwemo kutakiwa sampuli ya sauti iliyokataliwa na mtuhumiwa.

Balozi Dkt Wilbroad Slaa na wenzake, Wakili Boniface Mwabukusi pamoja na Mdude Nyagali walikamatwa na jeshi la Polisi katika maeneo tofauti mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Wanataka waitumie sauti kutengenezea voice note ya uhaini

Mtu anajirekodi voice note "Mimi Slaa nmeapa ntaipindua nchi " halafu hio sample ya sauti inawekwa juu ili isikike sauti ya Slaa.

wanachotaka ni ile sample ya sauti safi kutoka kwenye chumba kama kile cha kwenye studio .

1692211196154.png
 
Back
Top Bottom