Rombo wapandisha bendera ya Kenya?

Kwa hiyo Wachagga wa Rombo wameamua kuamia Kenya? Vizuri tunaheshimu maamuzi yao
 
Tarime Na Rorya ndo usiseme watu wameichoka bongo. huko radio RAMOGI FM ndo wanafungulia.
panatawaliwa kijeshi ila wananchi wana hasira sana na huo utawala wa kipolisi.
Polisi,TRA pamoja na Uhamiaji wamejazana daraja la kirumi utadhani ndiyo mpaka.
Viongozi kukosa busara na uchumi mbaya ndo unazidi unazidisha hasira kwa wananchi.
Poleni wana Rombo yote yana mwisho.
 

Mkuu haya unayoyasema nikweli? Sukari 4500? Nini hasa kimesababisha iwe hivyo? Hakika kama ni kweli, ifike wakati hata mbunge wao apige kelele sasa.
 
Ooh poleni sana wananchi wa rombo, ila kwa ushauri wangu, sioni kama ni busara kuhamia nchi jirani. Nchi ya kenya na yenyewe ina maswaibu yake, tena ni nchi yenye vurugu na vitukoza vya hapa na pale kila kukicha. Kwa hilo naona mmepotea njia.
 
Rombo ipi unayoizungumzia? Maana wakaazi wa Rombo (ya Oloitoktok) ya Kenya huduma zote huzipata Rombo ya Tanzania na Wa-Rombo wa Kenya wanajisikia Watanzania zaidi sasa hii ya Wa-Rombo wa Tanzania kujifanya wa- Kenya inawezekana? Ngoja tujifunze masuala ya hawa wakaazi wa mpakani mwa Tanzania na Kenya:

 
Last edited by a moderator:

Naomba uchunge mdomo wako
 
Kwa hiyo Wachagga wa Rombo wameamua kuamia Kenya? Vizuri tunaheshimu maamuzi yao

siyo kuheshimu maamuzi yao, inatakiwa ujiulize kwanini wamehamia kenya!
 
Serikali imekuwa ikiwatenga sana wananchi wa Rombo katika huduma.Mradi wa maji katika vijiji vya katangara na Mrere umeingiliwa kisiasa.Watu wanapata maji kisiasa,watu wa Useri na Tarakea ukanda wa chini ni kama vile hawaoni faida ya kuwapo serikali,halikdhalika watu wa Mkuu na Mengwe hasa maeneo ya Ibukoni

Mradi wa Umeme umekuwa na urasimu mkubwa,mazingiura ya kufanya biashara halali yameingiliwa na kugubikwa na Rushwa.Watendaji wa serikali si waaminifu na mara nyingi hutumia vitisho dhidi ya Raia katika kufanya majukumu yao.

Kwa kweli kuna ukiukwaji mkubwa haki.Sijui sertikali ya CCM inawachukulia vipi wananchi wa Rombo.Ni miezi michache tu imepita tangu mradi wa shule ya jumuiya ya wazazi ya CCM,shule ya sekondari Shauritanga umeleta mgogoro na wananchi baada ya kulazimisha kuziba barabara na kufanya eneo la barabara kuwa mali ya shule hiyo inayoomilikiwa na chama cha Mapinduzi.Ilizua mtafaruku nusura damu imwagike.Hili suala pamoja na mengine yanahitaji Mbunge asimame kidete na wananchi kuhakikisha haki inatendeka kwa wananchi wa Rombo.They deserve better than this.
 
wengi humu hawaijui Rombo, infact hao watu ni very realistic hata kisiasa. Km utakumbuka zamani sana walishampiga chini mramba then waka mrudisha na the fact kwamba alileta lami bado hakuwa ame-meet objectives alizopewa wakampiga chini. Niambie ni majimbo mangapi yenye upeo huo??
 
siyo kuheshimu maamuzi yao, inatakiwa ujiulize kwanini wamehamia kenya!

Serikali ya sisiemu imewazuilia wasipate bidhaa muhimu kama chakula, sijui inataka wafe?? Sukari inaishia hapo Himo, vipi kuhusu tarakea, mwika, keni...(au hawapendi chai na gah'wa??)
 

mzeee unaunga mkono warombo kupandisha bendera ya kenya?nassari naye alidai jamhuri ya kaskazini
 
Siamini kama kuna Mtanzania Mzalendo anaweza Kufanya ujinga Kama Huu.
Kama ni kweli, basi Hao ni wahaini....serikali ipeleke JWTZ wazunguke na magari yao mitaani
 

Kwa hiyo unataka kutuambia hizo ndo mbinu za chadema kudai haki? watu wa aina yako ndo mnaabisha chadema!
 
He!Kwa maana hiyo CDM wameshapoteza jimbo hivyo au?
 
Siamini kama kuna Mtanzania Mzalendo anaweza Kufanya ujinga Kama Huu.
Kama ni kweli, basi Hao ni wahaini....serikali ipeleke JWTZ wazunguke na magari yao mitaani

Tusitafute njia za mkato.Mbona ilikua rahisi kushulikia madai ya wananchi wa Rombo kuliko kutumia nguvu zote hizo?

Wananchi wa Rombo hawatishwi tena na matumizi ya ngivu kama serikali ilivyokua ikifanya kuwatisha watu kwa kuwapiga na kuwapeleka vijana kwa nguvu maituni kuzima moto katika mlima kilimanjaro

Badala ya serikali kuelimisha wananchi kutunza mazingira na kuwapa wananchi wake haki ili kujenga uzalendo mioyoni mwake wanaona ni afadhali watumie nguvu
 

Rombo wana mahusiano mazuri sana na jamii za kenya kuliko za Tanzania.Warombo wamekuwa na unafuu sana kuanza maisha Nairobi kuliko Hata moshi mjini,Mrombo anaweza ona mji wa kwanza kenya kuliko Tanzania,na Bidhaa nyingi watumiazo ni za kutoka Kenya.Warombo wanakodisha mashamba Kenya na kulima huko.

Nadhani ni Kipindi sasa serikali ya majimbo kuanza kufanya kazi, Hizi commands kutoka dar hazina tija kila eneo la Kaskazini.Hazina tija ktk aina ya utalii wetu, rasilimali zetu kama Tanzanite, mila zetu na mengine, Ni vipi ****** atajua haya?Ndio maana anataka Arusha isiwe na mimea.

Watu wa kaskazini kuanzia wameru,waarusha, wachaga huwa hawakai nyumba bila kuwa na miti ya kivuli,amri za dara zinatolewa na watu ambao hawajui jinsi tamaduni za watu wetu nyingi ni tofauti na tajiri sana za ustaarabu.

Im a great fan of greater kilimanjaro , kilimanjaro inajitawala ktk mipango yake ila ibaki kuwa Tanzania, warombo wana wazo zuri ila wamelifanya vibaya.Anyaway kama uamsho wanataka Zenj yao kwanini na wengine wasitake vipande vyao?Ya nini kutawaliwa na watu wasiojua nini mnahitaji na wapi mmefikia?Amri za dar zipo nyuma ya fikra za watu wa sehemu nyingi sana Tanzania,na mwishowe zinarudisha wengine nyuma.Ningependa kama wangebuni bendera yao kwani wangeonyesha kujitawala kuliko kubadili mtawala.
 

Mkuu mimi nakubaliana na wewe....Kwanza tukubaliane kwamba Kama kweli hili tukio limefanyika basi ni Uhaini...
Pili Kuna njia nyingi amabazo ni halali kikatiba amabazo Mtanzania anaweza kuzipitia kufikisha Malalamiko(Maoni).....

Anaweza Kuandamana...anaweza Kufungua Kesi....na mengineyo.....

Lakini Huwezi kufikisha ujumbe kwa Kupandisha bendera ya nchi JIRANI....Huku ni kujidharau na kudharau Wa-Tanzania wengine ....

Nimewahi kuishi na Wakenya ...Ki ukweli Wakenya wana dharau ya Hali ya juu kwa wa-Tanzania,Lakini walikuwa wanakoma Na mimi....

Wa-Tanzania ambao Hawapati huduma za kijamii ni wengi sana.....Kila pande za nchi hii kuna watu wanataabika kuhusu Hospitali,Wajawazito wanakufa Barabarani ,watu hawapati maji ya kunywa ...watu hawana hela ya kununua dawa...shule hakuna...chakula cha Tabu.....

Je hawa wote wapandishe Bendera za Kenya ?
Mimi nimesikia Kuwa Huko kilimanjaro(Rombo) Kuna Maendeleo Kuliko Sehemu nyingi za Tanzania....
Je Wana-Rombo wana Haki zaidi ya Kupandisha Bendera ya Kenya Kuliko Wa-Tanzania wengine ?

Mimi Naunga Mkono harakati zote za Kujiletea Maendeleo...Lakini Siungi Mkono kupandisha Bendera ya nchi Nyengine
Especially Kenya ... angalu wangepandisha ya Rwanda ningeweza Kuvumilia..lakini Kenya...Hapana..Hapana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…