Roma aweka wazi kilicho mzimba mdomo, adai angesema yote leo asingekuwepo hai, ni zaidi ya mziki

Bado hajasemA.... hatosema..na asiseme...
Akae kimya maisha yaendelee....ana familia mwenzenu..hiphop kitu gani banaa...nyinyi mtaishia tu kusema R.I.P Roma..muziki wako utakumbukwa daima na pengo lako halitazibika..halafu mtaendelea na maisha yenu wakati familia yake haitoona hilo pengo likizibwa wala hiyo Hiphop ikiwapeleka watoto shule...huo ndo ukweli ..

Mwacheni Roma afanye maisha yake..hilo fuko la siri libaki kifuani mwake limwelemee mpk siku anakufa lakini asilitue..hakuna atakayemsaidia Roma humu JF zaidi ya maneno tu kwa kutype kwa dole gumba au keyboards za PC huko maofisini..
[HASHTAG]#VIVAROMAVIVAAAAAA[/HASHTAG]
 
Chezeya utawala dhalimu usiostahili kukosolewa.
Ila Nina uhakika 2021 Mungu atamuweka hai atasema tuu na hapo ndio tutajua ukweli. Angetengeneza clip ya video akahifadhi kwa mwanasheria kueleza jambo zima ili akipotea tena liwekwe hadharani jambo hilo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mateso na mikwara wanayopewa huko sidhani kama atasema yote!! Wanapigika kisawa sawa na wale watu wa torture! Tena wanapigwa saa ingine ikiwa bila nguo!! Wanakuvuruga akili kisaikolijia saa ingine wanakupiga na kukubaka huku wanachukua video!! Kutishia ukivujisha na Wao wanaweka video yako hewani!! Utapotea haraka
 
Naona kama bado ni siasa vile...
Swai ni Je bado ataimba zile nyimbo ngumu kumeza dhidi ya serikali au ndo mapambio dhidi ya serikali maana kwa maneno hayo imnaonekana kama roma yule Kwisha....
Huyuu jamaa kashaonesha uzaifuu kwahyo tusitegemee tna zle ngoma zake bali ni lain saiv tna zakusifu ujinga au taaarabuu
 
ACheni kumpotosha roma wa watu akisema alichanwa marinda mtamwesabu mwanamume tena? Au ndo mtamwita antroma
 
Roma Mkatoliki amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa zilizomfanya kutokusema nini kilichopelekea yeye kutekwa na nini kilikuwa kinaendelea wakati akiwa chimbo na kudai aliamua kutumia busara ya kutokusema ili mwisho siku aendelee na kazi ya muziki.




Roma%20Mkatoliki.jpg

Roma Mkatoliki alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza toka alipoonekana kutoka chimbo walipokuwa baada ya kutekwa.

Roma Mkatoliki amesema hayo kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) na kusema alitambua kuwa anaweza kuwakwaza baadhi ya watu kwa kutokusema na kuweka wazi lakini alifanya maamuzi hayo kwa lengo la kulinda sanaa yake na maisha yake kiujumla.

"Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka ni zaidi ya muziki japo chanzo ni muziki ndiyo maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani, wala nyumbani unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani, wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile tunamaliza pale halafu usiku mwema, lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea,labda ningesema ukweli pengine ungekuwa mwisho wa Roma kwenye muziki, mashabiki wangeshangilia lakini wadau mbalimbali mchongo ndiyo ungekuwa umekwisha" alisema Roma Mkatoliki

Roma aliendelea kusisitiza kuwa kama angeweka wazi jambo hilo siku ile ambayo ametoka huko chimbo ingepelekea yeye kuacha muziki na kurudi Tanga kufanya mambo mengine kwani hakuna mtu ambaye angetaka kuwa karibu naye tena.

"Hata wewe hapo Dullah usingenipigia simu kunialika kwenye show hapa leo, nakwambia ungeniogopa, na mwisho wa simu Roma angerudi zake Tanga kushika jembe akalime, Je, mashabiki wangependa? Kwanini Roma sasa asiendelee kubaki halafu mashabiki wakaendelea kusikiliza ngoma zake na akaendelea kushusha dude kwa dude, kwa hiyo utaona kuwa yalihitajika maamuzi ya busara katika hili ila nashukuru sana wananchi na wabunge kwa kupaza sauti zenu mpaka tukaweza kutoka na kurudi mtaani kama hivi" alisema Roma Mkatoliki.

Mbali na hilo Roma Mkatoliki anasema toka ametoka mpaka sasa hataki hata kutazama video mbalimbali ambazo zinaonyesha jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kuwatafuta ili waweze kupatikana anadai hataki kutazama sababu hataki kukumbuka kabisa, hali ambayo alikuwa nayo kipindi hicho huku akisema hapendi kuona mtu mwingine yoyote anakwenda huko chimbo ambako wao walikuwa wamewekwa wakipata mateso hayo.

Mwanzoni wa mwezi wa 4 mwaka huu msanii Roma Mkatoliki, Moni Cetrozone, Binladen na Emmanuel walitekwa na watu wasiojulikana katika studio za Tongwe Records na kukaa kusikojulikana kwa siku tatu na baadaye kuja kuonekana wakiwa na majeraha mbalimbali.

Source: EATV
Bado hapa roma ana endelea kubwabwaja uongo.

Ukweli wote ulishadhihirika pale waziri wa utamaduni alipotoa Amri kwamba" wasanii msiimbe siasa."

Hivyo
Ni wazi Roma alikua anaongea chini ya shinikizo(intimidation). Hakua huru hata leo, bado hayupo huru.
.
Ni jambo baya analiamsha lililoanza kusahaulika tena kwa kuendelea na udanganyifu uleule ili kuwafikirisha watu.


Na Kwa maelezo yake ya sasa anataka kujionyesha kua ana mambo maovu anafanya/alikua akifanya ambayo ikiwa yataanikwa hadharani, watanzania watamchukia. Kwa ubashite(zero brain)wake Anajipaka uchafu ili kujikomba kwenye dola bila kuangalia athari za maneno yake.

Kwanini asionyeshe ujasiri uleule wa kuendelea kukaa kimya.?
 
Waandishi wetu bana. Huyu bado hajasema chochote zaidi ya kuthibitisha watu wanachojua tayari - kwamba siku ile hakusema ukweli wowote
 
Bado hajasemA.... hatosema..na asiseme...
Akae kimya maisha yaendelee....ana familia mwenzenu..hiphop kitu gani banaa...nyinyi mtaishia tu kusema R.I.P Roma..muziki wako utakumbukwa daima na pengo lako halitazibika..halafu mtaendelea na maisha yenu wakati familia yake haitoona hilo pengo likizibwa wala hiyo Hiphop ikiwapeleka watoto shule...huo ndo ukweli ..

Mwacheni Roma afanye maisha yake..hilo fuko la siri libaki kifuani mwake limwelemee mpk siku anakufa lakini asilitue..hakuna atakayemsaidia Roma humu JF zaidi ya maneno tu kwa kutype kwa dole gumba au keyboards za PC huko maofisini..
[HASHTAG]#VIVAROMAVIVAAAAAA[/HASHTAG]
Msaada wa mbongo ni kukuingiza kwenye matatizo tu baada ya hapo anarudi zake kwenye keyboard

Bidada wa kawe alivokuwa akiongoe alikishangiliwa sana lakini hadi sasa hivi ulizia kama kuna jitihada zozote kutoka kwa wale mashabiki zaidi ya kurejea kwenye keyboard tena
 
hiyo kusema hakuna mtu angenisogelea ninge rudi kijijini, imenifanya nifikirie kwamba huenda watesi wake walimsodomize pia.
 
Msaada wa mbongo ni kukuingiza kwenye matatizo tu baada ya hapo anarudi zake kwenye keyboard

Bidada wa kawe alivokuwa akiongoe alikishangiliwa sana lakini hadi sasa hivi ulizia kama kuna jitihada zozote kutoka kwa wale mashabiki zaidi ya kurejea kwenye keyboard tena
Na ndo iko hivyo mkuu...watu wanajua kuchochea tu..kikinuka huwaoni.
 
Back
Top Bottom