Goodluck Haule, Maria Sarungi, wampaisha Roma Mkatoliki na Wimbo mpya “Naitwa Roma”

Jul 2, 2019
32
43
Roma Mkatoliki azua taharuki
Jumapili , 17 Nov , 2019
Mwandishi: Ismail Sarumbi

Rapa Roma Mkatoliki amewaacha njia panda mashabiki wake kwa kile alichokiimba katika wimbo wake mpya wa 'Naitwa Roma' ambapo watu wengi wameshindwa kutafsiri mashairi yalitumiwa humo huku wengine wakijiulza kwa nini ameamua kumkosoa Rais John Pombe Magufuli na kuikosoa serikali ya awamu ya tano katika wimbo huo ambao unaongoza kuangliwa zaidi katika mtandao wa YouTube.

Naitwa Roma: Umewakera sana viongozi wa Serikali kutokana na ujumbe mzito ambao unailenga serikali kama utekaji wa watu,watu kuuliwa, wakulima wa korosho kutokulipwa pesa zao,pia Roma ametaja kuwa viongozi wa awamu ya tano wanapenda sifa na hawapendi kukosolewa. Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe ni kiongozi wa kwanza kuongelea hadharani wimbo huo na kusema kama Roma darasa la saba atamwambia nini yeye ana shahada nne na pia ni mwalimu mbobezi wa falsafa katika vyuo vingi. Akaendelea kusema kwamba kama Roma ataendelea kuikosoa Serikali hivo bora basi ananzishe chama chake cha siasa ili ijulikane ni mwanasiasa. Pia tuliona katika mtandao wa Twitter Msemaji wa Ikulu Msigwa aliposti akisema “Anaitwa JPM” muda mchache baada ya Roma kuwa ana-trend katika mitandao.

Katika wimbo huo Roma Mkatoliki amejaribu kuhusisha matukio mbalimbali ya kisiasa pamoja na lile la kwake kubwa la kutekwa ambapo hii ndiyo kazi yake ya kwanza kufunguka wazi tokea ule mkasa wake wa kutekwa kuisha na kusababisha maumivu mengine makali kutoka kwa mashabiki zake baada ya kuona 'video' yake mpya iliyojaa hisia kali za maumivu.


Hata hivyo, kuna tetesi kwamba wimbo huo mashairi pamoja na gharama za kuutengeneza na kuupeleka studio kuna kikundi cha wanaharakati Nchini ambao wamekuwa wakipigania haki pamoja na mabadiliko ya uwongozi wakina Maria Sarungi, Fatma Karume, ambao inaaminika kwamba wana vikundi vya vijana waliopo nje na ndani ya nchi kama vile Tito Magoti ambaye ni mfamyakazi katika kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kigogo14 ambaye pia inaaminika anasapotiwa na viongozi wa upinzani Mh Zitto Kabwe ametajwa sana. Pia kuna watu wengine kama Mwanaharakati wa Haki za LGBT anayeitwa Goodluck Haule, pia View attachment 1264856kuna mtu anatumia jina la Mcomoro kwenye mtandao wa Twitter. Hawa wamekuwa mstari wa mbele kuusambaza na kuupigia kampeni wimbo huo ambao ndani ya masaa 24 ulifika namba moja ukizipita nyimbo kama “Baba Lao” ya Diamond na “Mshumaa” ya Ali Kiba.

Bashite ya wadau wa mziki nchini wametoa maoni yao jinsi walivyoupokea ujio mpya wa Roma na hizi ni baadhi tu ya zile zilizoandikwa na mashabiki wa Roma.

Pharergy Ramson: “#AnaitwaRoma ni harakati atazifanya nani zaidi ya Roma 'but' ngoma iko poa hujawahi kuniangusha ila umebadirika kidogo mzee. Nadhan kwenye hii ngoma umejibu maswali ya watu wengi sana kipindi unafanya 'show' pale 'Dar live' nilitamani urudie hii nyimbo 'but' sikuwa na uwezo ila umefanya vizur."


Blandina Bilau: "Simjui sana Roma wala kufuatilia nyimbo zake lakini huu wimbo umeniliza, 'message' imefika jipe moyo. Mtetezi wako Mungu aendelee kukutetea"

Arthur Oyaro: "Duuh 'so sad' na utu uzima huu machozi nimeshindwa kuyazuia,'thank' pia kwa kunifikirisha. Viva Roma viva''

Mdachi Classic: "Nimefatilia 'comment' nyingi sana ila sijaona hato komenti inayozungumzia vibaya hii ngoma zaidi ni za upendo na za kuumizwa tu. 'In short' hii imetugusa sana pole sana kaka yupo mungu hakimu wa yote".


Ibrahim Utenga: ''This song reflects the real prevailing situation, it's very sensitive song, congratulations to you brother, God save you "

Ndongo Nyambalya: "Nina wasiwasi wewe Mkatoliki hicho siyo kichwa ni semi-computer, kwenye Mungu wa John na Daud hapo nimefikiria hadi najikuta nurudiarudia kusikiza, U deserve bro! Gat u! 100".

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki amemwagiwa sifa kedekede na mashabiki zake ambao walikuwa wamemisi kusikia na kuona kazi zake na kuweza kurudi katika uhalisia wake bila ya kuhofia jambo lolote litakaloweza mtokea tena mbele yake kwa ukali wa tungo zilizojaa za kufikirika.
 
Baada ya huyu Jamaa ROMA kutekwa kipindi kile nikajisemea moyoni ndio basi tena sijui kama tutasikia nyimbo za harakati na kukosoa zaidi tutasikia tu za kusifia za kina Babalao na nyinginezo,ila nashukuru ROMA kwa huu ujio,best Song....Kama serikali kuna nyimbo zinazowasifia basi kubalini na zinazowakosoa,that's life mitizamo haifanani.Big up Roma
 
Roma tangu nimjue taranta yake ya nyimn
Bo si kuimba mapenzi ama kitu kingine kama kina Diamomd, Harmonize Chameleone bali ni kuimba siasa!

Na hili analijua yeye bila kuimba siasa muziki hatauweza, Roma hajaanza leo kuimba siasa na kukosoa serikali , nashangaa wanaohangaika na Roma alimradi wanajua historia ya muziki wake ,

Hakuna cha nini Roma ndo taranta yake na alipojaribu kuimba mapenzi alishindwa ku win hii inajulikana ya nini Kuhangaika? Hata hao mnaowataja hata hawapo mtawasingizia bure tu , nawashangaa viongozi wa kiserikali kujibizana nae

Ukimya nalo huwa jawabu murua kabisa kufanya hivyo ni kumpa KIki ndio maana yeye sasahv ni shavu tu kwake
 
Roma yuko poa sana,ila kumuhusisha na hao kina Sarungi unataka kumchonganisha na watu mkuu. Ana familia na inamtegemea hatutaki vichwa kama hivi vipotee kirahisi. Kwasababu yeye hajataja yupo upande gani sisi wasikilizaji tusimchagulie upande. Muhimu kama msanii kafikisha ujumbe kwetu. Ukizingatia wengi wetu ni waoga kila sehemu ID fake.
 
Huu uzi ni wa kichochezi. Moderator naomba uufunge. Mwakyembe ajasema Roma ni MTU wa darasa la saba. Hii ni complex inferiority ya mfungua uzi kama sio chuki binafsi na wivu.
Kwanza nikurekebishe!!
Roma sio darasa la saba kama ulivoandika bali Roma alisoma old moshi PCM na sikumbuki aliendachuo gani lakini kusema ni darasa la saba huo sio ukweli
 
Huyu ndiye Roma Mkatoliki ninayemfahamu! Wa tangu enzi za Tanzania, 2030, nk. Kama una akili timamu, utagundua Roma ana sifa zote za kuwa na digrii 4 na huku yule mhishimiwa akistahili kabisa kuwa na hiyo elimu ya darasa la 7 B!
 
Back
Top Bottom