Roho ya kukataliwa: Chanzo/asili na madhila yake

Mkuu mshana jr hapa tusidanganyane kabisa. Leviticus 2:13(WALAWI) inasema hivi; "Tena kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la MUNGU w
Asante ila naona unataka tuitafsiri Biblia kama novel na si kitabu kitakatifu chenye tafsiri za kiroho.. Nimekuwekea vifungu hivyo kama njia ya kupanua ufahamu... Vipo vingi kama chumvi ilitumika kutengeneza vingine kwanini isitumike kwenye maji?
Bado naomba niseme kuwa inawezekana kabisa hujaelewa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi... Kuogea maji ya chumvi sio uchawi ndugu yangu
 
Mkuu mi mwenyew naijua biblia vizur, ilaa nakushauri ukaisome vizuri.
Acha kupanik bro..

Ni hv Yesu mwenyew alimtibu yule kipofu kwa kutumia matope Refer. The book of Luke
Pia Paulo alimwambia Timotheo atumie kilevi kwa ajil ya uponyaji wa tumbo lake. Likewise Mfalme Naaman aliambiwa na Elisha akajichovye mtoni mara 7 na ukoma wake ukaisha.
Ipo mifano mingi tu, ukitaka nitaendelea kukutajia, ila cha muhmu faham kuwa Mungu kuna wakat anaponya kwa kutumia vtu mbalimbali ikiwemo chumvi hata tope, na kingine ukijuacho.

Mungu n mpana kulko tumzaniavyo mkuu
Mimi nataka uniambie ni wapi YESU aliagiza mtu akipatwa na matatizo achukue maji aweke chumvi na aoge kisha hayo matatizo yake yatakwisha au mikosi itakwisha. Au unioneshe ni wapi MITUME waliwaagiza watu hayo mambo ya kuoga na CHUMVI.

Ukiniambia sijui YESU alitumia tope, YESU hakutumia tope peke yake, alichanganya tope na mate yake. Je! leo hii wewe waweza changanya tope na mate yako na mtu akapona?? Tena YESU hakuwaagiza wanafunzi wake nao watumie tope na mate yao kuwaponya watu. Bali aliwaagiza watumie JINA LAKE (YESU KRISTO) kuponya. Soma Biblia yako vizuri, siyo PETRO, wala PAULO, wala mtume yeyote yule aliponya kwa kutumia tope na mate, hakuna! Waliwaponya watu kwa JINA LA YESU WA NAZARETI.

Kuhusu wine (mvinyo) hii inajulikana ni dawa ya tumbo. Waisraeli walikuwa wanaitumia kujitibu tumbo miaka yote kabla hata Paulo hajazaliwa duniani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumeza dawa kwa ajili ya ugonjwa na kuoga maji ya CHUMVI kwa ajili ya kuondoa eti "mikosi".

Mikosi ni matatizo yanayomwandama mtu. Matatizo mengi yanayotuandama sisi binadamu yanasababishwa na DHAMBI zetu. Mikosi ipo ndiyo, lakini sababu mikosi inasababishwa na dhambi, haiwezekani kuiondoa kwa kuoga maji ya CHUMVI. Mikosi inaondolewa kwa mtu kutubu dhambi zake, kumwamini YESU KRISTO, na kubatizwa kwenye maji kwa JINA LA YESU. Hiyo ndiyo njia pekee ya kusafisha dhambi, na dhambi ndiyo inayobeba mikosi ya kila aina na mabalaa ya kila namna.

Shetani ni mjanja sana, anawadanganya mtumie chumvi kuogea na ninyi bila ufahamu wa NENO la MUNGU mnapotea kwenye madanganyo ya ULIMWENGU huu. Njia pekee ya kukuondolea mikosi, na laana na mabalaa ni JINA LA YESU peke yake. Tena mikosi mingine haitoki hivi hivi tu pasipo KUVUNGA NA KUOMBA KWA DHATI.

Endeleeni kudanganyika na chumvi zenu.
 
Asante ila naona unataka tuitafsiri Biblia kama novel na si kitabu kitakatifu chenye tafsiri za kiroho.. Nimekuwekea vifungu hivyo kama njia ya kupanua ufahamu... Vipo vingi kama chumvi ilitumika kutengeneza vingine kwanini isitumike kwenye maji?
Bado naomba niseme kuwa inawezekana kabisa hujaelewa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi... Kuogea maji ya chumvi sio uchawi ndugu yangu
Acha kabisa kuwadanganya watu ndugu yangu. Hizo ni imani za kishirikina kabisa. Mimi kamwe sikubaliani nazo. Lakini kila mtu yuko huru kuifuata njia aitakayo. Lakini pia njia ya "KWELI" ipo na anayetaka kuifuata na awe huru kuifuata.

Njia ya KWELI ni JINA LA YESU KRISTO na mafundisho yake basi. YESU alisema hivi; "Mimi ndiyo NJIA, KWELI na UZIMA."

Tafakari ndugu yangu.
 
Mimi nataka uniambie ni wapi YESU aliagiza mtu akipatwa na matatizo achukue maji aweke chumvi na aoge kisha hayo matatizo yake yatakwisha au mikosi itakwisha. Au unioneshe ni wapi MITUME waliwaagiza watu hayo mambo ya kuoga na CHUMVI.

Ukiniambia sijui YESU alitumia tope, YESU hakutumia tope peke yake, alichanganya tope na mate yake. Je! leo hii wewe waweza changanya tope na mate yako na mtu akapona?? Tena YESU hakuwaagiza wanafunzi wake nao watumie tope na mate yao kuwaponya watu. Bali aliwaagiza watumie JINA LAKE (YESU KRISTO) kuponya. Soma Biblia yako vizuri, siyo PETRO, wala PAULO, wala mtume yeyote yule aliponya kwa kutumia tope na mate, hakuna! Waliwaponya watu kwa JINA LA YESU WA NAZARETI.

Kuhusu wine (mvinyo) hii inajulikana ni dawa ya tumbo. Waisraeli walikuwa wanaitumia kujitibu tumbo miaka yote kabla hata Paulo hajazaliwa duniani. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kumeza dawa kwa ajili ya ugonjwa na kuoga maji ya CHUMVI kwa ajili ya kuondoa eti "mikosi".

Mikosi ni matatizo yanayomwandama mtu. Matatizo mengi yanayotuandama sisi binadamu yanasababishwa na DHAMBI zetu. Mikosi ipo ndiyo, lakini sababu mikosi inasababishwa na dhambi, haiwezekani kuiondoa kwa kuoga maji ya CHUMVI. Mikosi inaondolewa kwa mtu kutubu dhambi zake, kumwamini YESU KRISTO, na kubatizwa kwenye maji kwa JINA LA YESU. Hiyo ndiyo njia pekee ya kusafisha dhambi, na dhambi ndiyo inayobeba mikosi ya kila aina na mabalaa ya kila namna.

Shetani ni mjanja sana, anawadanganya mtumie chumvi kuogea na ninyi bila ufahamu wa NENO la MUNGU mnapotea kwenye madanganyo ya ULIMWENGU huu. Njia pekee ya kukuondolea mikosi, na laana na mabalaa ni JINA LA YESU peke yake. Tena mikosi mingine haitoki hivi hivi tu pasipo KUVUNGA NA KUOMBA KWA DHATI.

Endeleeni kudanganyika na chumvi zenu.
Mtumishi naona upeo wako wa kuyafahamu na kuyatizama mambo n mdogo sana..
Na sabab ni kuwa umekariri biblia kama ulivyofundishwa. Biblia ni pana Sana kuliko umavyoifaham.
Si kwel kwamba kila anayepitia mateso/balaa/magonjwa fulan bas ni kwa sabab ya dhambi... No si kwel
Nakujibu kwa andiko toka kitabu cha Marko pale yesu alivoletewa yule kipofu na yule kilema kuwaponya, ndiposa wanafunz wake wakamwuliza Je? Ni kwasabab ya nn had wale wamepata upofu na kilema? Yesu akajibu si yeye (kipofu/kilema) wala wazaz wake wala ndugu zake aliyesababsha madhila hayo kwake, bali wamefanywa hvyo ili utukufu wa Mungu udhihirike.
****//÷**TAFAKARI HILI SANA **////****

Aidha, tambua kuwa bwaba yesu alimsamehe dhambi yule kahaba aliyemlilia kwa kutoa machoz miguun mwake na pia yesu alitumia ishara ya kupaka mafita kama alama ya kusamehewa na kupokea baraka. Nnachotaka kusema ni kuwa si kila kitu kinatoka kwa jina la Yesu, bali yapo mambo mengne ywtaondoka kwa njiq mbalimbal kama zilivyoelwzwa hapo awali.
 
Hakuna hoja yoyote ya msingi uliyoandika hapa. Ukweli utabakia pale pale kuwa dhambi ndiyo iliyoleta matatizo yote duniani na siyo vinginevyo. Kama dhambi isingekuwepo hata hiyo mikosi pia isingekuwepo. Huo ndiyo ukweli dhahiri. Biblia yenyewe imeandika wazi kabisa kuwa wanadamu wote wamefanya dhambi chini ya jua. Hakuna hata mmoja aliyemsafi. Wewe ukatae au ukubali lakini mikosi na mabalaa husababishwa na dhambi.

Na isitoshe hiyo chumvi mnayosema haiwezi kumfanya kipofu aone tena HAIWEZI kumfanya kilema atembee. Kutumia chumvi kwa imani ya kuondoa sijui mikosi au sijui kusafisha nyota, ni aina ya ushirikina, and its not Biblical. Hizo ni imani potofu za kishirikina na siyo maagizo ya Mitume. Hii mambo ya chumvi, ni tiba za waganga wa kienyeji, tiba za vigagula. Akili zenu zimejaa imani za kishirikina kuliko imani ya MUNGU. Mnaupenda uwongo kuliko KWELI ya MUNGU. Mmekulia katika familia zinazojishughulisha na uchawi na ushirikina ndiyo maana inawawia vigumu sana kuifahamu KWELI ya MUNGU. Matokeo yake mnaichanganya KWELI ya MUNGU na imani za KICHAWI.

Nimesema, na narudia tena kusema; nataka unioneshe ni wapi Mitume walifundisha kuwa, mtu akipata matatizo, achukue chumvi aweke kwenye maji na aoge kisha matatizo yake yatakwisha. Kama kweli hii ni tiba inayokubalika na MUNGU, basi hata Mitume wa MUNGU wangeifahamu na wangeifundisha kwa wanadamu kama tiba halali.

Narudia tena kusema, suluhisho la matatizo ya mwanadamu ni JINA LA YESU pekee. Hakuna suluhisho lingine lolote zaidi ya JINA LA YESU KRISTO.
 
.
IMG_20180325_090833_305.jpg
 
Kama wewe si mmojawapo basi kwa vyovyote kuna mtu unamfahamu mwenye hili tatizo.. Anaweza kuwa ndugu jamaa ama rafiki... Ni jambo baya na lenye kutatiza mno... Watoto wa mtaani wanasema KIMAVI

Mind you sizungumzii ile kuchukiwa na mtu mmoja mmoja kwa sababu zisizoeleweka... Huwezi kupendwa na kila mtu.. Ni lazima haters wawepo... Ni watu wasiokupenda tu... Na huweza hata kujenga uadui mkubwa na wewe
Pia sizungumzii ishu za kisiasa, umaarufu, mali, mafanikio na uongozi... Kwakuwa hapa kuna watu automatically hawapendi kuwaona wengine wana maisha mengine positive tofauti na wao.. Kushindwa kwako ndio furaha yao.... Kadiri unavyofanikiwa kimaisha ndio maadui huongezeka.. Kwahiyo singumzii kwa muktadha huu pia

Nazungumzia kuhusu wale ambao kiasili bila kujali kama wanacho ama hawana.. Ni watu wenye nyota iliyofifia ama kufa kabisa... Hawapendwi at the first place... Hata kama hawajaongea chochote, hata kama hawajafanya chochote... Kwa mfano unafika mahali penye mkusanyiko wa watu... Mara zinapigwa kelele za mwizi bila hata hujajua nini kimetokea unakuwa mtuhumiwa wa kwanza... Anakuja chizi mahali mko wengi lakini anakunasa kibao wewe... Mnapita mahali kuna mbwa anawaacha wengine wote na kukuandama wewe.. Yaani ni karaha mwanzo mwisho

Hakuna kitu kinachokosa chanzo... Ama asili.... Mimba zinapotungwa huwa kuna vita ya kumgombea kiumbe atakayezaliwa.. Hapa kuna nguvu hasi na nguvu chanya.. Hii hutokea pia wakati wa kujifungua... Hii vita hutokea sehemu hizo mbili... Kumbuka mada ya manii zilizokosea njia, je kuna mimba za bahati mbaya?
Nguvu chanya ndio yenye nguvu zaidi, ni uumbaji uliokusudiwa na Maulana, ndio uumbaji wa nyota inayowaka lakini shetani na mawakala wake( wanga, wachawi na mabaradhuli) hupenda kufanya shindano na Maulana.. Kumbuka alishafanya hivyo pale Eden basi tambua hata leo hii anaendelea hajaacha
Hapo sasa kuna mambo mawili nyota yako inaweza kuwaka kwa njia chanya.. Utapendwa na karibia kila mtu kwa upole ucheshi, huruma, kujitoa kwako nk nk... Nyota yako ikiwaka kwa njia hasi utaogopeka na kila mmoja kwa matendo yako mabaya ya kikatili ya kutisha na ya kibaradhuli kabisa... Sasa nyota yako ikisimama kwenye 0 yaani sio hasi wala sio chanya ndio roho ya kukataliwa inapozaliwa... Yaani shetani alijaribu kukupoka kwenye chanya lakini akaishia kukuangusha njiani... Hapo ni tabu tupu

Sasa basi kama nilivyoeleza hapo juu shetani na mawakala wake daima ni watu wa mashindano... Hivyo akikukosa wakati wa kutungwa mimba, akikukosa wakati wa kuzaliwa, akikukosa wakati wa makuzi atakutafuta tu popote mpaka akupate! KIAJE!?

1. Kipindi cha balehe... Unapoingia hatua ya ukubwani.. Hatua ya kujitambua... Unaanza kutafakari maisha yako ya nyuma , wazazi ama walezi au ndugu waliokukuza.. Unaingalia jamii na kuhisi kutengwa... Hapa ukikosea tu na kumpa shetani nafasi umekwenda na maji.. Ataanza kukuonyesha vitu vidogo vidogo mno.. Atakuonyesha kuwa nyumbani hupendwi kama fulani, shuleni mwalimu fulani hakupendi... Marafiki nao unahisi hivyo hivyo... Taratibu unaanza kujichukia na kujiona hufai.. Unajenga inferiority complex, unajitenga na jamii na tayari roho ya kukataliwa inazaliwa...
Wazazi na walezi... Tuwe makini sana na hatua hii kwa vijana wetu.. Tuwasaidie waweze kuivuka salama...

2. Baada ya balehe ni kipindi cha ndoto nyingi... Kuota mafanikio, kuota umaarufu, kuota utajiri, kupendwa nknk... Hapa napo shetani hachezi mbali.. Ataanza kukuonyesha agemate wako walivyo na maisha mazuri na mafanikio... Na sometimes sio kwamba uko vibaya bali ni ile roho ya kutaka zaidi... Hapa sasa ndio unaingizwa rasmi kwenye ulimwengu wa maagano ya kuboost nyota bila kujua
Hiki ndio kipindi cha kutafuta ndele ya mvuto kwenye mapenzi, Pete za bahati, hirizi za mafanikio.. Wataalam wa kusafisha nyota nknk... Ukikubali kuuingia huu mkenge UMEKWISHA... utaenda kwa mganga kutafuta ndele.. Hakwambii madhara anakupa tuu.. Utaanza kuwa na mvuto utapendwa na kila mwanamke kuanzia chizi mbaya mzuri mlemavu mrefu kwenda chini, kipipa nknk wote watakuwa wako mpaka unakereka.. Ila mganga kakuficha kitu kimoja... Ndele ina life span.. Ikiisha utachukiwa mpaka na siafu.. Mapete ya bahati, hirizi za mafanikio, kusafisha nyota vyote hivi vina kikomo cha matumizi

3. Maisha ya ukubwani sasa... Hapa umepambana na changamoto za maisha umefeli na kufaulu... Umepita kwingi na kufanya mengi.. Umeshawahi kujaribu hata option no 2 ya mapete na mahirizi na kusafisha nyota.. Ukapata mafanikio ya muda.. Lakini baadae ukaanguka vibaya kabisa... Kwa Neema tu ukaweza kusimama tena sasa unataka kurudi hewani... Hapa hutaki tena njia ya giza...unataka njia ya nuru lakini kumbuka shetani bado yuko nawe hakuachi
Badala ya kukuacha uende njia sahihi.. Anakuelekeza kwa mitume na manabii wanakohubiri mafanikio na utajiri wa vitu viharibikavyo... Unarudi kule kule kwa wapiga ramli na waganga wasafisha nyota.. Unauziwa maji ya baraka vitambaa nk.. Unaanza kuhangaika kwenye masinagogi ya hawa watu na mwisho unakufa bila kupata ulichotarajia

Rafiki mpendwa pambana na hali yako, usimwache muumba wako hata nukta moja.. Hakuna binadamu aliyezaliwa na mwanamke anaweza kusafisha nyota yako ikasafishika milele.. HAKUNA.. hakuna mganga atakayeweza kukupa mafanikio yasiyo na maagano HAKUNA... hakuna Pete ya bahati isiyokosa mawaa HAKUNA... jaribu kuivua siku moja uone shughuli yake...
Usifuate mkumbo ila kama ukiona mambo hayaendi na kweli kabisa unajiona wewe mwenyewe una roho ya kukataliwa.. Basi simama na Mungu wako kwa imani yako huku ukijitakasa na chumvi... Ile asilia.. Chumvi haina gharama. Chumvi haina maagano.. Chumvi haina madhara... Itumie kawaida kwa kuogea ni chaja bora isiyochuja

Nakuombea....!!!

Jr future pastor
Duuu....kama kuna ukweli fulani hivi mana kiwango kikubwa kwangu yana ukweli kabisa roho hiyoo ipo yani hata nikivaa smart kabisa bado na one kana nipo ovyo yani nipo nipo tuu hali ya kiuchumi sio haba sana a ila daa story ndefu mkuu ...

Mshana Jr. ..
 
Pole sana kama hutojali unaweza kufunguka hapa ama la njoo PM tuongee machache
 
Back
Top Bottom