Wema ni chanzo cha matatizo, roho mbaya ni kinga dhidi ya majanga

Son Of Almighty

Senior Member
Jun 28, 2017
123
428
Habarini za usiku wana JamiiForums,

Aisee, katika vitu nimejifunza tena kwa ushuhuda katili kweli kweli, kamwe usimuamini kiumbe anayeitwa BINADAMU maana kubadilika/ kukubadilikia ni sekunde.

Katika maisha yangu nimesaidia watu wengi sana ikijumuisha ndugu, marafiki na watu baki ambao kwa huruma ya changamoto ambazo wanapitia nilishawishika kufanya hivo, sijawahi hata siku moja na sikuwasaidia kwa kutaka malipo yeyote bali nina roho ambayo nikiona mtu anapitia changamoto na nina uwezo wa kumsaidia basi nitafanya.

Imagine unampatia mtu permanent contract, ulipomtoa alikuwa na hatihati ya kufukuzwa, hivi sasa amekuwa adui mkubwa sana kwangu. Anakosoa kila unachofanya tena waziwazi, msimamo wangu tayari awali ulikuwa mwiba kwa wengine na wamefanikiwa kumwin sasa wameunda genge na wanapambana kweli kweli dhidi yako.

Now, imani kwa mabosi wako imepungua kwa sehemu kubwa sana, mengi yalokuwa ndani ya majukumu yako hivi sasa unaona wameingilia na wanafanya pasipo wewe kuwa na taarifa yeyote, mengi unakuja kutambua kwenye management meetings.

Binafsi si mtu wa kujikomba, kuabudu, kujipendekeza, au kuwa chawa ofisini as means ya kusurvive ofisini. To some extent naona as days go by wamewin trust from the management ambayo mostly hawako Tanzania.

Nina amini zaidi katika taaluma, ujuzi, uzoefu, na ndo njia pekoe ambayo imekuza career yangu kwa zaidi ya miaka 8 kufikia level niliyopo ambayo siwezi kudisclose.

Njaa ni kitu kibaya sana, na shibe hupumbaza watu. Watu wasiokuwa na shukrani kama hawa, hupelekea vijana wengine kukosa watu wa kuwashika mkono kwa kuogopa/ kuhofia mbeleni yataibuka kama haya.

Nimetafakari sana, mwisho nimeamua kukaa kimya, natambua itaniumiza ila muda sahihi utafika na ukweli wote utakuwa wazi.

Kwa ninayopitia, sidhani kama nitakuja kusaidia tena binadamu suala la kazi hasa ofisi moja. Nimejifunza pakubwa sana, na Mungu anipe hekima ya kudeal na yanayoendelea kwa sasa.
 
Pole sana ndugu yangu.Mara nyingi patokeapo chuki,ujue wema ulitangulia.Story yako inataka kufanana na ya kwangu.

Japo mimi imetokea kwa marafiki na wengine ndugu zangu kabisa.

Binadamu hawana wema.Lakini pia Mungu anaweza kukuacha ukapigwa storms hadi ukashangaa kwamba inakuwaje sisi ambao tupo kwa Mungu wala hatuendi kwa waganga tunaaibishwa hivi wakati kuna wajinga flani tu kila siku kwa waganga na wanazidi kufanikiwa?

Kwa nini Mungu kuna kipindi anachelewa kuwajibu wenye haki?

MUNGU uliye hai kwa nini usijifunue haraka kwa watu wema ili wabaya wakuone wewe na kupata ushuhuda kuwa upo wakurudie wewe?
 
kama unawezo wa kusaidia saidia, wema wako hauozi kama hutakuja kulipwa wewe bas kizazi chakob kitanufaika na matunda ya wema wako

stori yangu iko tofauti na ww,**** jamaa alitaftiwa kazi na mtu wa ambaye walisoma wote huko nyuma, sasa anajutia msaada na ameamua kumfungia viooalimtoa tangu hajajipata, anampigia sim anamwambia mbona mwezi huu hujanitumia hela ya asante mimi mambo yangu yamevurugika, so imagine wewe unamsaidia mtu humdai mwengine huko ni denina usumbufu,Mungu kajumba hivo dunia kwa uwiano tofauti,tungekua wote tuna roho kama yako nzuri dunia ingeboa sana
 
Yuko mmoja tulimdhamini kwenye kampuni ya usafirishaji.....
Ghafla akawa chawa wa bosi....anamtumia picha watu wanavyoiba diesel...wanavyopakia vimizigo vya kujikimu njiani n.k.
Siku ya siku bosi kamtoa nishai hadharani....wewe fulani...kuanzia leo sitaki uniletee umbeya ofisini kwangu unanigombanisha na madereva ......watu aaah......jamaa aliona haya ......hakurudi tena ofisini.....Mara ya mwisho nilimkuta kwenye geti la dangote anasotea kazi.
 
Habarini za usiku wana JamiiForums,

Aisee, katika vitu nimejifunza tena kwa ushuhuda katili kweli kweli, kamwe usimuamini kiumbe anayeitwa BINADAMU maana kubadilika/ kukubadilikia ni sekunde.

Katika maisha yangu nimesaidia watu wengi sana ikijumuisha ndugu, marafiki na watu baki ambao kwa huruma ya changamoto ambazo wanapitia nilishawishika kufanya hivo, sijawahi hata siku moja na sikuwasaidia kwa kutaka malipo yeyote bali nina roho ambayo nikiona mtu anapitia changamoto na nina uwezo wa kumsaidia basi nitafanya.

Imagine unampatia mtu permanent contract, ulipomtoa alikuwa na hatihati ya kufukuzwa, hivi sasa amekuwa adui mkubwa sana kwangu. Anakosoa kila unachofanya tena waziwazi, msimamo wangu tayari awali ulikuwa mwiba kwa wengine na wamefanikiwa kumwin sasa wameunda genge na wanapambana kweli kweli dhidi yako.

Now, imani kwa mabosi wako imepungua kwa sehemu kubwa sana, mengi yalokuwa ndani ya majukumu yako hivi sasa unaona wameingilia na wanafanya pasipo wewe kuwa na taarifa yeyote, mengi unakuja kutambua kwenye management meetings.

Binafsi si mtu wa kujikomba, kuabudu, kujipendekeza, au kuwa chawa ofisini as means ya kusurvive ofisini. To some extent naona as days go by wamewin trust from the management ambayo mostly hawako Tanzania.

Nina amini zaidi katika taaluma, ujuzi, uzoefu, na ndo njia pekoe ambayo imekuza career yangu kwa zaidi ya miaka 8 kufikia level niliyopo ambayo siwezi kudisclose.

Njaa ni kitu kibaya sana, na shibe hupumbaza watu. Watu wasiokuwa na shukrani kama hawa, hupelekea vijana wengine kukosa watu wa kuwashika mkono kwa kuogopa/ kuhofia mbeleni yataibuka kama haya.

Nimetafakari sana, mwisho nimeamua kukaa kimya, natambua itaniumiza ila muda sahihi utafika na ukweli wote utakuwa wazi.

Kwa ninayopitia, sidhani kama nitakuja kusaidia tena binadamu suala la kazi hasa ofisi moja. Nimejifunza pakubwa sana, na Mungu anipe hekima ya kudeal na yanayoendelea kwa sasa.
Popote pale penye ubaya jua kuna Wema ulitangulia.
 
Yuko mmoja tulimdhamini kwenye kampuni ya usafirishaji.....
Ghafla akawa chawa wa bosi....anamtumia picha watu wanavyoiba diesel...wanavyopakia vimizigo vya kujikimu njiani n.k.
Siku ya siku bosi kamtoa nishai hadharani....wewe fulani...kuanzia leo sitaki uniletee umbeya ofisini kwangu unanigombanisha na madereva ......watu aaah......jamaa aliona haya ......hakurudi tena ofisini.....Mara ya mwisho nilimkuta kwenye geti la dangote anasotea kazi.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mswahili: bro naomba uniazime elfu kumi japo watoto wangu wale leo.

Mtendawema: sawa hii hapa kaka Chukua.

Kesho yake mswahili anaenda kilingeni kwa mganga: Mganga nimekuja nataka huyu jamaa tumroge kwa sababu anajifanya ana hela sana...

Usipo mpa sasa : " mganga huyu jamaa nataka tumroge anajifanya ana dharau sana yani Mimi ndo wa kushindwa kunipa elfu kumi kweli
 
Back
Top Bottom