Je, wajua nini hutokea katika Ulimwengu wa Roho wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,102
22,539
Salaam / Shalom!!

INTRODUCTON.

(Mwanzo 2:18,21-24) na (Mathayo 19:3-9).

NDOA ni muunganiko wa KIMWILI kati ya mume mmoja na mke mmoja KIMWILI na kiroho.

Asili ya NDOA ni Mbinguni, NDOA ni usafi, NDOA ni utakatifu.

Kila mtu aliyezaliwa Huwa anae mtu mmoja ambaye Huwa ndiye ubavu wake. Na hao kukutana, ni Hadi wamwombe Mungu, Kuzini kabla ya Kuoa kunamweka mtu katika position ya Kuoa au Kuolewa na mtu mume au mke asiye ubavu wako sahihi.

Matatizo mengi ya NDOA na magomvi ni sababu ya Kuoa au Kuolewa na mtu asiye chaguo Kutoka Kwa MUNGU.

Mwanaume anapofikia uamuzi wa Kuoa, shetani huleta wanawake wengi karibu Yako, na Mungu Huwa tayari amemleta mtu sahihi, ukiitumia macho ya MWILI kuchagua mke, utaangukia Kuoa uliyeletewa na shetani, ndomana Kila aliyeoa Huwa na simulizi, hujikuta katika wakati ambapo huhitaji achague, wakati kiuhalisia, atokaye Kwa Mungu, ubavu wako Huwa ni MMOJA tu!!!

Utaniuliza, kwanini wanawake ni wengi kuliko wanaume, kwamba tukioana mke mmoja, mume mmoja, wanawake watabaki bila waume, Hilo Lina sababu na majibu yake, Si Leo.

Utaniuliza pia ikiwa aliumbwa Adam mmoja na Hawa mmoja, kwanini idadi ya wanawake iwe kubwa kuliko wanaume? Hilo nalo majibu yake Si Leo!!

Ulimwengu wa Giza NDOA Yao ni kinyume na NDOA aliyoasisi Mungu, Ulimwengu wa Giza hakuna NDOA, wachawi, mama na mwanae wanajamiiana, USHOGA ,USAGAJI,kujamiiana na wanyama na Kila UOVU,umeanzia katika Ulimwengu wa Giza,Kisha kuletwa duniani, huko hawana mipaka, ni tafrani tupu.

Ili kuivuruga Dunia, Ulimwengu wa Giza hufanya jitihada juu chini Ili kwenda kinyume na maagizo ya Mungu Ili watu wasioane na kufikia baraka za wawili wanapoungana katika NDOA Takatifu.

Ibilisi na shetani ajua akivuruga NDOA Takatifu atavuruga uzao wa mwanadamu, sababu watoto wakipatikana na kutunzwa vizuri katika taasisi aliyoasisi Mungu, watazaliwa watoto watakaomcha Mungu.

MADA: NINI HUTOKEA WAWILI, MUME NA MKE WANAPOUNGANA NA KUWA MWILI MMOJA KIMWILI NA KIROHO?

Katika mwili, anaposimama Mchungaji kufungisha NDOA Takatifu kati ya mke na mume KIMWILI,

Pia, Katika Ulimwengu wa Roho pia wawili Hawa huunganika, Mungu akiwa shahidi.

Muunganiko huo hutokea Kwa Mfano wa nyota mbili zenye uelekeo tofauti angani, zinapokutana na kupata crash, nyota na Nuru kubwa huzaliwa sababu ya muunganiko huo. Na mng'ao huongezeka sana, sababu nyota mbili kuungana na kuwa moja kubwa inayong'aa zaidi.

Mamajusi, alipozaliwa Yesu, wao waliona Nyota yake, na ilionyesha nini Yesu amebeba, lakini Kwa watakatifu, hatuchunguzi Nyota, sisi huomba Mungu atuzidishie mafanikio Kutoka KIBALI tulichozaliwa nacho.

Kila mtu ana KIBALI, KIBALI Kutoka Kwa MUNGU ndiyo Bahati na mafanikio ya mtu huzaliwa nazo Toka tumboni, Mtu mume na mke sahihi wanapoungana katika NDOA Takatifu huunganisha KIBALI Cha mke na KIBALI Cha mme na kuwa kitu kimoja. Nguvu na uwezo wa mafanikio ya mke na mume sahihi Huwa hayazuiliki, baraka Huwa ni mara mbili, na hatua zao Huwa za haraka sana.

Narudia, hakuna mchawi au Pepo awezaye kuzuia mafanikio ya mtu mume na mke waliofunga NDOA sahihi Walio mwili mmoja, kuwatenganisha hao ni Hadi uvunje NDOA kwanza ndipo uweze kuwatenganisha.

Mafanikio Yako kijana yapo katika NDOA, watoto na uzao sahihi umo katika NDOA sahihi, jambo muhimu la kuzingatia, ni upate Mume au mke sahihi aliye Ubavu wako.


HITIMISHO
NDOA na iheshimiwe na watu wote, vijana wajitunze na kutunza bikira zao kabla ya Kuoa na Kuolewa Ili kupata baraka za NDOA.

Usipojitunza, usipotunza Bikra Yako, utapata wa kufanana nae, Pipa na mfuniko.

Kwa Leo niishie hapa.

Mungu na Awabariki.

NOTE: Ikiwa hujampokea Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha ya, fuatisha Sala ifuatayo:

EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO,NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE NA NIMEDHAMIRIA KUZIACHA, NIPE UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI,FUTA JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, NA ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA. AMEN

Karibuni.

Amen
 
Dunia hii imepitia uongo/utapeli/propaganda kubwa sana na zikapita lakini uongo pekee ulio dumu kwa muda mrefu ni huu

Hebu fikiri unaambiwa kuna MUNGU muweza wa yote yupo sahihi na hajawahi kukosea.

Ameumba dunia kwaajili yetu na ataiangamiza dunia kwaajili yetu.

Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba lakini aliiumba hivyo hivyo ili aje kuiangamiza,
Ameumba moto wa jehanamu kwakuwa ametuumba tukosee ili atuchome moto japo alikua na UWEZO wakutuumba tusiwe wakosefu ili atuumbie Pepo tu tukale bata

Anajua tunacho hitaji lakini lazima tumuombe ili atupe, lakini hata tukimuomba hatupi tunavyo taka sisi maana tayari amekwisha tupangia kila mtu atampa nini, ataishije na atakufaje

Ndio muumba wa kila kitu(magonjwa, bangi, majini, ulabu nk) na anaweza kudhibiti chochote lakini anamlaumu msaidizi wake muasi(Shetani) kuleta mambo hayo mabaya duniani(magonjwa nk) kwa watu wake aliyewaumba wakati yeye ndiye aliye mtupa msaidizi wake huyo huku duniani.

Yaani yeye kashindwana naye huko mbinguni kaja kumtupa kwetu sisi viumbe dhaifu tupambane naye na tukishindwa tutachomwa moto milele, lakini anasisitiza anatupenda sana kama mtu anavyopenda na kujali mboni ya jicho lake

Hebu tafakari hili, kawaumba Adam na Hawa na wakati bado wageni duniani akawatupia Nyoka(Shetani) ili awarubuni, na kwa ugeni wao wakarubunika matokeo yake katupa adhabu ya shuruba watu wote hata ambao tulikua hatupo na hata ambao hawajazaliwa chamoto watakiona...... Not fair

Mungu muweza wa yote hayupo WAZI PASI NA SHAKA kwa watu wote kujua huyu ndio MUNGU badala yake Mungu ndio amekua sehemu kubwa ya mgawanyiko wa watu na kusababisha kuwa na imani za MIUNGU zaidi ya milioni dunia nzima.

Na kibaya zaidi unatakiwa to blindly believe him, usihoji wala kuwa na shaka juu ya uwepo wake(ni laana na kufuru) vinginevyo moto wa milele unakuhusu

Yaani kuna Fundi Kapenta mmoja huko Galilaya eti kafa kwaajili ya dhambi za watu wote duniani.... seriously ?
Akaitwa Mungu lakini Mungu huyu akajaribiwa na shetani.

Fundi kampenta huyu hakuandika kitabu chochote ila wahuni walio kuwa wanampinga ndio wakaja kuandika vitabu kuhusu fundi huyu na vinaitwa “Bibilia Neno la Mungu takatifu”.

Mabilioni ya watu dunia kote wanakesha makanisani wakimlilia na kumuomba awape uponyaji, mali, waume/wake nk

Hebu fikiria huko Arabia kuna Maamuma mmoja hajui kusoma wala kuandika alidai anashushiwa maagizo na Mungu kukata vichwa watu wote watakao pinga na kutokutii maagizo yake, “akashushiwa” aya za vitisho na neema kwa watakao tii, yaani ukifa unampigania Mungu unakwenda kupewa mbikra 72 kazi yako ni kuzagamua tu.

Mabilioni ya watu duniani wanasujudu mara 5 kwa siku na kushinda njaa mwezi kila mwaka ili wakale naye bata Peponi

Kwamba maisha yako hapa duniani ni ya mpito tu maisha yako yapo baada ya kufa
Unachotakiwa kufanya ni kumuamini na kufanya aliyoa agiza ili ukale bata sana baada ya kufa

Asante. Jibu la utapeli wako hilo hapo
 
Utamtambuaje huyo wa ubavu wako aliye sahihi ?... Mke/mume sahihi ?
Hilo nalo ni somo jingine, tuombe Mungu asaidie pia niletee humu.

Bt in short, ukijazwa Roho MTAKATIFU, utasikia maelekezo kabisa Kutoka ndani,

Ni muhimu pia kushirikisha waliookoka wakusaidie kuomba.

Ndipo linapotimia neno lisemalo,

MKE MWEMA HUTOKA KWA BWANA. AMEN
 
Yakobo alikuwa na mke zaidi ya mmoja,Ibrahim alikuwa na wake wawili,suleiman nae hivyo hivyo kifupi manabii wengi walikuwa na wake zaidi ya mmoja...nyinyi wakristo kwanini hamtaki tuwe na wake zaidi ya mmoja?

Ukiachana na hilo dini kabla hazijafika africa mababu zetu walikuwa na wanawake zaidi ya mmoja,kwanini nyinyi wachungaji hamtaki tuoe mke zaidi ya mmoja?
 
Back
Top Bottom