Asili ya Neno Inshaallah

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Wakazi wa makkah ambao ni maquraish walikuwa na mashaka juu ya Utume wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, hivyo walitaka kujiridhisha je huyu kweli ni Mtume wa Mungu au laa!

Basi kwakuwa wanajua kule Madina kuna wanazuoni wa Kiyahudi au watawa wa kiyahudi na wanaijua vizuri Taurati pamoja na manabii, basi wakawatuma watu ambao ni An nadr na Uqba, waende kule wawaeleze wasifu wa Muhammad na wawaeleze yale ambayo Muhammad anawahubiria,lengo ni kutaka kujua ukweli?

Basi wakaenda kwa hao mabwana wakubwa na kuwaeleza wajihi wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake na yale ambayo huwa anayahubiri.

Wanachuoni wa Kiyahudi wakasema muulizeni maswali matatu ambayo tutawaambia, kama akijibu basi huyo ni Mtume na mumfuate na kama akishindwa basi huyo sio mtume anasema uwongo na mtajua namna ya kudili naye.

Basi wakaenda kwa jamaa zao na kuwapa mrejesho kisha wote wakaenda kwa Muhammad kumuuliza hayo maswali.

Swali la kwanza, huko zamani kabisa kulikuwa na vijana ambao habari zao zilikuwa zenye kuajabisha na kushtua, je hao ni vijana gani?

Swali la pili, kuna mtu ambaye alikuwa mtembezi, alitembea mashariki ya dunia na magharibi, je ni mtu gani huyo?

Swali la tatu, tueleze kuhusu roho,je roho ni nini?

Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, kwakuwa anajua Malaika Jibril / Gabriel mara nyingi humjia na kuumpa ufunuo basi AKAWAAMBIA KUWA NITAWAJIBU KESHO.

kwa faida kidogo Malaika huyu ndio mkuu wa Malaika na ndiye ambaye tangu zama na zama kazi yake pamoja na mambo mengine ni kufikisha ufunuo kwa mitume wote tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Haya tuendelee, zikapita siku kumi na tano hajaletewa ufunuo kutoka mbinguni, huku nako watu wamelianzisha zengwe, huyu Muhammad alisema atatupa jibu kesho lkn sasa zimepita siku kumi na tano hana majibu, watu wakaanza kuwa na mashaka na Utume wake, na yeye huku anajisikia vibaya kwakuto wajibu na kusikia maneno yao ya Shombo.

Ndio baadae akaja Malaika Jibril na kushusha suratul Kahf ambayo pamoja na mambo mengine ikajibu yale maswali.

Kwanza Mtume aliambiwa katu usiseme jambo lolote lile kuwa ntalifanya kesho ila kuongeza na kusema INSHAALLAH /MUNGU AKIPENDA, hapa tunafundishwa kuwa hakika hakuna ajuaye kesho yake isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.

Swali kuhusu wale vijana, jibu walikuwa vijana wa pangoni ambao walikimbilia huko pangoni kuepuka jamii yao ambayo inamshirikisha Mungu, wao walikuwa wanamwamini Mungu mmoja tu, wakalazwa usingizini kwa miaka 309 kisha wakafufuliwa, habar yao ni ndefu ngoja niishie hapa.

Swali la pili, mmtembeaje aliyetembea mashariki na magharibi ya dunia ni Dhul Qarnain nae ana habar nzito, ngoja niishie hapa.

Swali la tatu, kuhusu roho ni nini, jibu ni kuwa roho elimu yake ipo kwa Mungu mwenyewe, wanadamu wamepewa sehemu ndogo sana ya elimu hiyo.

Ni hayo tu!
 
Wakazi wa makkah ambao ni maquraish walikuwa na mashaka juu ya Utume wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, hivyo walitaka kujiridhisha je huyu kweli ni Mtume wa Mungu au laa!

Basi kwakuwa wanajua kule Madina kuna wanazuoni wa Kiyahudi au watawa wa kiyahudi na wanaijua vizuri Taurati pamoja na manabii, basi wakawatuma watu ambao ni An nadr na Uqba, waende kule wawaeleze wasifu wa Muhammad na wawaeleze yale ambayo Muhammad anawahubiria,lengo ni kutaka kujua ukweli?

Basi wakaenda kwa hao mabwana wakubwa na kuwaeleza wajihi wa Muhammad rehma na amani ziwe juu yake na yale ambayo huwa anayahubiri.

Wanachuoni wa Kiyahudi wakasema muulizeni maswali matatu ambayo tutawaambia, kama akijibu basi huyo ni Mtume na mumfuate na kama akishindwa basi huyo sio mtume anasema uwongo na mtajua namna ya kudili naye.

Basi wakaenda kwa jamaa zao na kuwapa mrejesho kisha wote wakaenda kwa Muhammad kumuuliza hayo maswali.

Swali la kwanza, huko zamani kabisa kulikuwa na vijana ambao habari zao zilikuwa zenye kuajabisha na kushtua, je hao ni vijana gani?

Swali la pili, kuna mtu ambaye alikuwa mtembezi, alitembea mashariki ya dunia na magharibi, je ni mtu gani huyo?

Swali la tatu, tueleze kuhusu roho,je roho ni nini?

Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake, kwakuwa anajua Malaika Jibril / Gabriel mara nyingi humjia na kuumpa ufunuo basi AKAWAAMBIA KUWA NITAWAJIBU KESHO.

kwa faida kidogo Malaika huyu ndio mkuu wa Malaika na ndiye ambaye tangu zama na zama kazi yake pamoja na mambo mengine ni kufikisha ufunuo kwa mitume wote tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Haya tuendelee, zikapita siku kumi na tano hajaletewa ufunuo kutoka mbinguni, huku nako watu wamelianzisha zengwe, huyu Muhammad alisema atatupa jibu kesho lkn sasa zimepita siku kumi na tano hana majibu, watu wakaanza kuwa na mashaka na Utume wake, na yeye huku anajisikia vibaya kwakuto wajibu na kusikia maneno yao ya Shombo.

Ndio baadae akaja Malaika Jibril na kushusha suratul Kahf ambayo pamoja na mambo mengine ikajibu yale maswali.

Kwanza Mtume aliambiwa katu usiseme jambo lolote lile kuwa ntalifanya kesho ila kuongeza na kusema INSHAALLAH /MUNGU AKIPENDA, hapa tunafundishwa kuwa hakika hakuna ajuaye kesho yake isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.

Swali kuhusu wale vijana, jibu walikuwa vijana wa pangoni ambao walikimbia huko pangoni kuepuka jamii yao ambayo inamshirikisha Mungu, wao walikuwa wanamwamini Mungu mmoja tu, wakalazwa usingizini kwa miaka 309 kisha wakafufuliwa, habar yao ni ndefu ngoja niishie hapa.

Swali la pili, mmtembeaje aliyetembea mashariki na magharibi ya dunia ni Dhul Qurnain nae ana habar nzito, ngoja niishie hapa.

Swali la tatu, kuhusu roho ni nini, jibu ni kuwa roho elimu yake ipo kwa Mungu mwenyewe, wanadamu wamepewa sehemu ndogo sana ya elimu hiyo.

Ni hayo tu!
Shukran kwa Ilmu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom