Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Nayaita Mungu wapi? Kivipi? Unajuamtu akiuliza hajasemawala kuita?

Hujayaita nini hivyo?

Nimeshakwambia sijui,utasemajenikikwambia sijui nakwepa swali?

Unataka nikudanganye najua kitu ambacho sijui?

Wewe maumbile chanzo chake ni nini na una uthibitisho gani kwamba ni hicho na ni hicho tu si kingine chochote asilani.
Maumbile chanzo au asili yake ni Mungu. Uthibitisho ni kwamba Yeye ndie amekiri kuwa chanzo kupitia nabii wake na hakuna mwingine.

Kama wewe una asili nyingine kuipinga hii ya Mungu ilete hapa.
 
Rafiki yangu umepewa maandiko ambayo Yesu anasema yeye sio Mungu sasa wewe unampinga Yesu?
Sheikh wangu, hayo yote ulioandika sio kwamba siyajui au kuyaelewa ila ndio sababu nilianza kukupa hadhari kwamba wewe kuna mtazamo unauona ni sahihi juu ya Yesu lakini na mimi nina mtazamo wangu dhidi ya Yesu tena ninaouona sahihi mno, na usioweza kubadilika kama sheria ya mmedi na muajemi, hata sekunde moja.

Wewe umekuwa na imani kwamba Yesu ni nabii Isa jambo ambalo halijawahi, halitawahi wala halitakaaliwahi kuniingia akilini asilan. Equation ya kumuequate Yesu na Issa haiwezekani hata katika Irreversible reaction Kamwe.
 
Sheikh wangu,,,hayo yote ulioandika sio kwamba siyajui au kuyaelewa ila ndio sababu nilianza kukupa hadhari kwamba wewe kuna mtazamo unauona ni sahihi juu ya Yesu lakini na mimi nina mtazamo wangu dhidi ya Yesu tena ninaouona sahihi mno,,na usioweza kubadilika kama sheria ya mmedi na muajemi,,hata sekunde moja...Wewe umekuwa na imani kwamba Yesu ni nabii Isa jambo ambalo halijawahi,,halitawahi wala halitakaaliwahi kuniingia akilini asilan...Equation ya kumuequate Yesu na Issa haiwezekani hata katika Irreversible reaction.Kamwe....
Mimi katika iman yangu ipo clear kwamba Yesu ni mtume na wamepita mitume wengi kabla yake, ila nataka kukusaidia wewe ambaye kitabu unachokiamin kimemrikodi maneno yake mwenyewe lakin wewe huyatakia, unataka maneno ambayo kaandikwa na wengine au kasingiziwa yeye ndio Mungu mkuu (tito 2) wakati yeye mweyewe anasema baba ni mkuu kuliko mimi!!! funguka rafiki yangu hakuna wakati ila ni huu, mwamini Yesu kisawasaw uione haki.
 
unashangaa Allah kuifanya dunia kama Mtihani? yeye ni mjuzi wa kila kitu na anafanya anachokusudia..siwezi kuhoji uadilifu wake lakini logically mtihan ni kwa sababu kila mtu apate anavyostahili baada ya maisha ya dunia, yule aliyefaulu afuzu kuingia pepon na aliyefel aadhibiwe na kuingia mtoni.
wewe mwenyewe sasa hivi umeanza ku fail exam ..maana unashindwa hata kitambua uwepo wake.
Jifikirie kama hii Dunia isingekuwa kama mtihan, watu wangefanya kufuru sana kwa sababu mwisho wa siku hakuna wa kusahihisha na kujua nani anastahili sawa na alivyoishi, huwezi kwa mfano kuua watu bila sababu za kisheria hapa dunian halafu uwe sawa na mtu aliyeishi kiungwana!!!.
umepewa hiyar, ukifanya mabaya unafeli mtihani ukifanya mazur unafaulu!
Lengo ni kutoa haki ambayo inaweza isipatikan hapa dunian kwenye mahakama zetu kutokana na limitation za kibinaadam.
Hujaelewa swali.

Unasema xxunia ingekuwa haina mtihani watu wangefanya kufuru.

Wakati mimi nishauliza awali kwamba kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Wewe unaishia kufikiri katika ulimwengu uliopo. Huwezi kufikiri ulimwengu unaowezekana ambao haupo.

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya, hauna mtihani, hauna kufuru? Ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Maumbile chanzo au asili yake ni Mungu. Uthibitisho ni kwamba Yeye ndie amekiri kuwa chanzo kupitia nabii wake na hakuna mwingine.
Kama wewe una asili nyingine kuipinga hii ya Mungu ilete hapa.

That is a circular argument.

Unasema chanzo cha asili ni Mungu. Toa uthibitisho ulio nje ya hadithi zinazosemwa zimesemwa na Mungu huyo.

Ukisema chanzo ni maneno ya Mungu huyo, unahakikishaje hayo maneno ni ya Mungu na si ya watu tu?

Amesema wapi? Kwa kutumia nabii gani?
 
Umeelewa hata nilichoandika ni nini?

Unafahamu contradiction ni nini?

Ukisema, Mungu ana uwezo wote, ana ujuzi wote ana upendo wote.

Halafu kaumba ulimwengu ambao njaa, matetemeko ya ardhi, mioto, mafuriko vinaweza kuua mamilioni ya watoto wasio na hatia, kila mwaka, wakati alikuwa na uwezo wakuumba ulimwengu ambayo mabaya hayo yote hayawezekani kufanyika na wala hayajulikani kabisa, habari yako ya kuwepo kwa huyo Mungu inajipinga yenyewe kabla mimi sijaipinga.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya haya kuwepo ni kujipinga yeye mwenyewe.

Mungu huyo hayupo.

Hawezikuwepo.

Kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Ni kama bachelor wa ndoa aliyeoa, au pembetatu duara katika Euclidean geometry.

By definition, pembetatu si duara na bachelor hajaoa, huwezikuwa na bachelor aliyeoa, huwezi kuwa na pembetatu duara.

Ni vitu vinavyojipinga kabla ya kupingwa.
Umekariri tu hii suala la contradiction ila unashindwa kuonesha uhusiano wa hayo majanga na hizo sifa za mungu.

Umeweka sifa tatu za mungu kwa maana ya upendo,uwezo na ujuzi. Kisha ukaanza kutaja majanga tu na kuhitimisha kuwa kuna contradiction.

Hebu eleza uwepo wa hayo majanga na hizo sifa za mungu inakuaje ni contradiction na kufanya ionekane kuwa huu ulimwengu haujaumbwa na mungu?
 
Sheikh wangu,,,hayo yote ulioandika sio kwamba siyajui au kuyaelewa ila ndio sababu nilianza kukupa hadhari kwamba wewe kuna mtazamo unauona ni sahihi juu ya Yesu lakini na mimi nina mtazamo wangu dhidi ya Yesu tena ninaouona sahihi mno,,na usioweza kubadilika kama sheria ya mmedi na muajemi,,hata sekunde moja...Wewe umekuwa na imani kwamba Yesu ni nabii Isa jambo ambalo halijawahi,,halitawahi wala halitakaaliwahi kuniingia akilini asilan...Equation ya kumuequate Yesu na Issa haiwezekani hata katika Irreversible reaction.Kamwe....
Unaweza kuwa unayajua lakin hujatafakari, ukitafakari baada ya kusoma utaelewa na haitakuwa ngumu kufuata njia ya ukweli na haki, Yesu mwenyewe anakwambia utafute ukweli sio uegemee tu mafundisho ya sunday school had sasa umekuwa na unaweza kutafakari mwenyewe!!!!!

angalia hapa chini Mwandishi mmoja amechambua hoja yako ya Muujiza wa kuzaliwa Yesu na ambavyo unakufanya umuelewe yesu kama Mungu wako!!!!! katika Biblia na Quran.

KUZALIWA BILA YA BABA

Labda katika miujiza yote ya kumthibitishia Yesu ungu ni kule kuzaliwa kwake na bikra bila ya baba. Wengi wanaona hayo ndiyo yanayoonyesha kwa nguvu zaidi kuwa yeye ni Mungu au Mwana wa Mungu. Mtaalamu mkubwa wa Kikristo, Maurice Wiles, Professor of Divinity and Canon of Christ Church Oxford, na Mwenyekiti wa Tume ya Imani ya Kanisa la Kiingereza, ameeleza vipi ilivyokuwa ni muhimu kabisa kuamini kuzaliwa na bikra kwa mwenye kutaka kuamini kwamba Yesu ni Mungu. Professor Wiles akiandika katika kitabu The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) amesema:
"Mwanzoni mwa karne hii (ya ishirini) zilipokuwa shaka shaka zinatamkwa kuwa ati ni kweli hakika Yesu alichukuliwa mimba na bikra, maneno hayo ya kuonyesha shaka yalionekana mara nyingi kuwa ni mashambulio khasa juu ya imani ya kuwa Mungu kawa mtu. Ilionekana kwamba imani ya kuzaliwa na bikra na kwamba Mungu amekuwa mtu ni kama pacha wasiobandukana, ama zitasimama pamoja au zianguke pamoja."

Biblia yasemaje juu ya jambo hili? Kwa hakika si kitu cha kawaida mtu kuzaliwa na mwanamke bikra asiyeingiliwa. Ni kweli huo ni muujiza. Lakini ndio ndivyo kuamini kuwa chenye kuzaliwa kwa muujiza ni Mungu? Au hata ndio ndivyo kuona tukio kama hilo ni dalili mojawapo ya kuzidisha ushahidi ya kuwa huyo mtoto ni Mungu au Mwana wa Mungu, kwa maana wanavyotaka wakuu wa makanisa wafwasi wao waamini?

Biblia inayotwambia kuwa Yesu kazaliwa bila ya mama yake kuingiliwa na mwanaadamu (Injili ya Mathayo 1.18) vile vile inatuambia ya kuwa Adamu hakuwa na baba wala mama. (Mwanzo 1.26- 27).

Kama wa Yesu ni muujiza wa Adam ni muujiza mardufu. Hali kadhaalika Paulo amewaandikia Waebrania:

Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Waebrania 7.1-3

Tunaona basi Biblia inatuhakikishia kuwa Yesu hakuwa pekee mwenye kuzaliwa bila ya baba. Wapo waliomtangulia katika muujiza huu. Kama huo ndio ungu, basi wangelikuwa Adam na Melkizedeki wa mbele, ambaye anasimuliwa na Biblia kuwa alikuwa

"hana baba, hana mama, hana mwanzo wala mwisho".

Hoja nyingi zimetolewa kukanya fikra ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aligeuka binaadamu akaishi duniani kwa sura ya Yesu wa Nazareti. Hoja hizo ziko za misahafuni mpaka za kisayansi. Katika Qur'ani ameshabihishwa Yesu na Adam.

Hali kadhaalika muujiza ulitokea kabla kidogo tu ya kuzaliwa Yesu, alipochukua mimba Elizabeti, mke wa Zakaria na ilhali huyo mama ni tasa tangu ujana wake na hapo kesha zeeka na kapindukia miaka ya kuzaa. Mumewe, naye, Zakaria alikuwa ni mkongwe.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur'ani, Sura ya Al Imran:

Akasema Zakaria: Mola wangu! Vipi nitapata mtoto, na hali ukongwe umesha nifika, na mke wangu ni tasa? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.

(Qur'ani) Al Imran 3.40

Ilipofika zamu ya Maryam kuchukua mimba Qur'ani inasema:

(Maryam) akasema: Mola Mlezi wangu! Vipi nitampata mtoto na hali hajanigusa mwanaadamu ye yote? (Mwenyezi Mungu) akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho; anapohukumu jambo, huliambia: Kuwa! Basi likawa.

(Qur'ani) Al Imran 3.47

Hizi ni hoja za misahafu, ni hoja za watu wenye imani. Wapo wengineo ambao wamepuuzilia mbali hadithi yote hiyo ya kuwa Maryam kachukua mimba bila ya kuingiliwa na mtu. Hao ni kama Mayahudi ambao wanamtukana Yesu na mama yake kwa kusema kuwa hiyo ni mimba ya haramu. Miongoni ya wataalamu wa Kizungu wenye asli ya Ukristo wapo wanaoamini hayo. Wanasema kuwa imani ya kuzaliwa na mama bikra ilikuwako tangu zamani katika dini za kipagani (kishirikina) kabla ya kuja Yesu. Bikra Rea Silvia alimzaa Romulus wa Roma. Horus wa Misri alizaliwa na Isis, malkia bikra wa mbinguni.

Hoja inayotolewa kama ilivyokuwa hizi na nyenginezo ni hadithi za kubuni tu zilioenea pande za Bahari ya Kati, basi ndio hivyo hivyo hadithi ya kuwa Maryam alikuwa bikra alipochukua mimba na kumzaa Yesu ni hadithi ya kubuni kuiga zile zilizotangulia.

Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri anawashutumu wakuu wa Kanisa kwa kutafuta kila kipengee katika Biblia kutoa ushahidi kuwa kuzaliwa kwa Yesu na bikra kuliaguliwa mbele.

Kipande kinachonukuliwa mno ni kile kiliomo katika Isaya ambacho kinasema:

Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.

Isaya 7.14

Mtaalamu huyu anasema maneno haya hayakukhusu kuzaliwa kwa Yesu hata chembe. Kwanza neno la asli halikutaja "bikira" lakini ni "mwanamke kijana". Tafsiri nyingine kama Revised Standard Version zimefuata hivyo ilivyo asli. Neno la Kiebrania liliotumiwa ni almah ambalo maana yake ni mwanamke kijana au msichana. Neno bikra kwa Kiebrania ni bethulah, kama ilivyo katika Kiarabu batuul. Na haya mambo ambayo yametokea zaidi ya miaka 700 kabla ya Yesu yalikhusiana na mke wake Isaya ambaye alikuwa umri wake ni miaka 20 wakati ule na kweli akaja kumzaa mtoto mwanamume. Ama hilo neno Imanueli, maana yake ni Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi, na wala sio maana yake kuwa huyo mtoto kuwa ndiye Mungu. Lugha ya Kiebrania imekaribiana na Kiarabu, na kwa Kiarabu ni Ma'anallah, nalo ni jina la kawaida, na kama kwamba kumwombea kheri huyo mwenye kuitwa. Mtaalamu Isaac Asimov ameeleza wazi juu ya utabiri huu wa Isaya katika kitabu chake, Asimov's Guide to the Bible.

Mtaalamu mwengine mwenye kupima mambo kiakili aitwaye G. Vermes amesema katika kitabu chake Jesus the Jew(Yesu Myahudi) akidai kuwa hili neno "bikira" hata lilivyotumiwa kwa Mariamu yawezekana sana kuwa maana yake ni kuwa mdogo mno kwa uzazi, kama walivyokuwa Sara, Hanna na Elizabeti kuwa ni wakongwe mno, au tasa.

Mwishoe kuna maoni ya mwana-sayansi na daktari juu ya hili suala la kushika mimba mwanamke hali naye ni bikra. Dr. T.H. Van de Velde M.D. akiandika katika kitabu chake cha kitaalamu, Ideal Marriage (Ndoa Bora) anasema:

"Mara nyingi imewahi kutokea, ijapokuwa ni nadra, kushika mimba kwa kupenya mbegu ya uzazi katika utupu wa mwanamke bila ya kuingiza kabisa dhakari, au utupu wa mwanamume. Mifano kama hiyo ni muhimu kabisa kimaisha. Ni dhaahiri kuwa inathibitisha vitu viwili. Kwanza, kuwa katika hali maalumu yawezekana mimba kutiwa ijapokuwa kizinda hakikupasuliwa. Na pili ya kwamba mbegu ya uzazi yaweza kufika ndani ya utupu wa mwanamke kwa njia isiyokuwa moja kwa moja, kwa mfano kwa mguso wa kidole..."

Hapana shaka pana utaalamu mkubwa katika mawazo na fikra hizi, za kidaktari, za kisayansi au za kiakili; lakini ni Qur'ani ndiyo inauweleza ukweli kwa maneno mepesi kabisa hata watoto wachanga wakaweza kuelewa na ikawa ya kuwatukuza Yesu na mama yake:

Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa mchanga kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa. Hii ni kweli inayotoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanaofanya shaka.

(Qur'ani) Al Imran 3.59-60
 
unashangaa Allah kuifanya dunia kama Mtihani? yeye ni mjuzi wa kila kitu na anafanya anachokusudia..siwezi kuhoji uadilifu wake lakini logically mtihan ni kwa sababu kila mtu apate anavyostahili baada ya maisha ya dunia, yule aliyefaulu afuzu kuingia pepon na aliyefel aadhibiwe na kuingia mtoni.

wewe mwenyewe sasa hivi umeanza ku fail exam ..maana unashindwa hata kitambua uwepo wake.
Jifikirie kama hii Dunia isingekuwa kama mtihan, watu wangefanya kufuru sana kwa sababu mwisho wa siku hakuna wa kusahihisha na kujua nani anastahili sawa na alivyoishi, huwezi kwa mfano kuua watu bila sababu za kisheria hapa dunian halafu uwe sawa na mtu aliyeishi kiungwana!!!.
umepewa hiyar, ukifanya mabaya unafeli mtihani ukifanya mazur unafaulu!
Lengo ni kutoa haki ambayo inaweza isipatikan hapa dunian kwenye mahakama zetu kutokana na limitation za kibinaadam.

1. Kama Mungu ni mjuzi, anashindwaje kuwapeleka watu motoni au peponi moja kwa moja bila kuwapa mtihani? Maana anapaswa kuwa na ujuzi wa kujua mwanzo, sasa na baadae. Hivyo Kumpa mtu mtihani maana yake huna ujuzi kama fulani atafaulu au atafeli.

2. Ili watu wasifanye kufuru kwanini Mungu asingeumba watu walio wakamilifu? Maana yeye si ndiye muweza
 
Umekariri tu hii suala la contradiction ila unashindwa kuonesha uhusiano wa hayo majanga na hizo sifa za mungu.

Umeweka sifa tatu za mungu kwa maana ya upendo,uwezo na ujuzi. Kisha ukaanza kutaja majanga tu na kuhitimisha kuwa kuna contradiction.

Hebu eleza uwepo wa hayo majanga na hizo sifa za mungu inakuaje ni contradiction na kufanya ionekane kuwa huu ulimwengu haujaumbwa na mungu?
Ni contradiction kwa sababu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Ana kila sababu, uwezo na upendo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Ni aghalabu sana kiongoz wa kiimani kuruhusu waumini na wasio waumini kuuliza maswali baada ya mada. Pengine utamaduni wa kuuliza maswali magumu ungekuwa ni Lazima, tusingeshuhudia utitiri wa madhehebu duniani, mengi yakiwa kwa maslahi ya viongozi wao.

Ni kiongoz mmoja tu (anayefahamika kwa sasa duniani) ambae ameenda mbali zaidi na kuruhusu maswali hata nje ya mada alizozungumzia na amekuwa akijibu kwa ufasaha na kutoa hata marejeo. Huyo Si mwingine bali ni Dr. Zakir Naik. katika video hii amejibu kuhusu kifo, kukata roho, roho ni nini na inaenda wapi baada ya kifo?

Usiishi kwa wasiwasi, maana hujui hata hiyo roho na moyo vina uhusiano gani...
 
1. Kama Mungu ni mjuzi, anashindwaje kuwapeleka watu motoni au peponi moja kwa moja bila kuwapa mtihani? Maana anapaswa kuwa na ujuzi wa kujua mwanzo, sasa na baadae. Hivyo Kumpa mtu mtihani maana yake huna ujuzi kama fulani atafaulu au atafeli.

2. Ili watu wasifanye kufuru kwanini Mungu asingeumba watu walio wakamilifu? Maana yeye si ndiye muweza
.
Mtihani wa mwanafunzi sii mtihani kwa mwalimu ila kwa mtahiniwa.
Lengo ni nini? Ni ili mtahiniwa ajiridhishe kuwa amepewa hukumu ya haki na ya kweli. Maana kama asipo ona na kuthibitisha mwenyewe kushindwa mtihani angeiita hukumu kumhusu yeye kuwa sii ya haki.

Ingeliwezekana mwalimu kutoa hukumu kwamba fulani na fulani hawana akili, lakini isingekuwa hukumu ya haki kama mhusika asingepewa mtihani ili athibitishe mwenyewe kwamba ni mshindwa.
 
Ni contradiction kwa sababu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hana sababu ya kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Ana kila sababu, uwezo na upendo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Mkuu bado hujaonesha uhusiano wa hivyo unavyovitaja na hiyo contradiction, kumbuka umepinga kuwa mungu hajaumba huu ulimwengu kwa sababu kuna contradiction,sasa naona unaishia kusema tu hana sababu za kuumba ulimwengu wa aina hii bila kuonesha contradiction inapatikana vp kwa hizo sifa tatu za mungu na haya majanga.

Tatizo wewe unaona kuna contradiction ila mie sioni hivyo,sasa unachotakiwa ni kunionesha hiyo contradiction na si kutaka tu mie nikubali kuwa kuna contradiction.
 
Mkuu ntabhaligwa katika andiko nililomtaja Meleckzedec mfalme wa Salem nilikutaka ujue kwamba huyu mfalme ni Yesu kamili asie na shaka.

Pili nilikuuliza kama uliwahi kumuona binadamu yeyote aliezaliwa bila sex ya mke na mume,,,Huwezi sema Adam....Adam hakuzaliwa na mwanamke hilo unalijua...Adam hakukaa tumboni kabisa...kwa hio ni jambo la kushangaza kufananisha kutokea kwao...

MWISHO nimeona ukiingiza habari za horus na isis na ukajaribu kutumia maelezo ya wasomi wajinga wa kiliberali kuhanikiza uwongo......kwamba ni nani labda alimwaga mbegu zake kwenye chupi ya bikira hata ziogelee zenyewe hadi kwenye uterus!!!! ,,,,,,hujaelewa nia ya maliberali???

Wameanza kuuchafua hata na uislam sasa,,,,,hujasikia ujerumani sasa wana msikiti wanaume na wanawake na mashoga wanaswali chumba kimoja cha waliouita msikiti????

Mimi nilijiuliza shoga akisujudu si atawajambia wenzie???(jokes))

Huwa naumwa nikiona maelezo yanayohusisha watu wachafu na wahalifu mfano wa waliberali...
 
Rafiki yangu ni vizur ukitoa maelezo ..weka rejea za maandiko ila kuweka uzito wa maelezo yako, kwa mfano ni wapi wamesema kuwa Merkzedec ndio Yesu ? nilikuwekea maandishi ya mliberal nikijua itakuwa rahisi wewe kumuelewa kwa sababu kimsingi ndio walioleta ukristo Afrika.

Baada ya kuuleta wamesoma vizur wale wenye free mind wakagundua wamedanganywa na wazazi wao mafundisho hayo ambayo yana utata mkubwa!! kwa sasa ni kama ulaya wameacha kusali makanisan isipokuwa wachache.

na maelfu wanasilim kila kukicha ikiwaacha wengine wameamua kuwa wapagani.
 
Waebrania7:1-28, Nimekutafutia madesa yote yanayomhusu YESU KRISTO. Naweza ita mjumuisho wa yote. Biblia haikuletwa na waliberali(ni kizazi kichafu kisicho na mda mrefu sana) Wapo wazungu wakristo wa kweli(wenye ROHO MTAKATIFU ndani yao) Bado wapo.

Nikupe mfano mdogo, kama Saudi Arabia itasubutu kuruhusu Ukristo kuhubiriwa na wakaingia hawa wakristo wenye huyu ROHO MTAKATIFU kwa kitambo cha miaka saba msikiti wenu wa AL KAABA Utawekwa msalaba(take it from me)

Pitia hio mistari pole pole, na si lazima uimalize yote kwa siku moja. Hio ndo hunipa mtazamo sahihi kuhusu YESU.
 
Yesu Si Mungu. Na hawezi kuwa Mungu.

Mungu haonekani hivyo hana mfano.
Hizo nyingine ni simulizi.

Hakuna sababu inayofanya Yesu Awe Mungu Mkuu
Mbaya zaidi hawa wana dini, hudhania Mungu anafanana na binadam kwa sura na maumbile akiwa na uwezo na nguvu zaidi ya binadam,

Hii sio haki na ni uongo mkubwa wafaa kupingwa kwa nguvu zote, kwani Mungu ni uwezo na nguvu isyokuwa na umbile,

Watu waamke vita kuu ya 3 ya dunia imekaribia,
 
Ile
Utata hapa ni pale tunajua roho zote baada ya kifo zinakwenda kwa Mungu. Sasa utata wa ile roho ya Mungu baada ya kufa ilienda wapi?
Roho kwa kuwa ilikuwa ya Mungu na ukikosa sehemu ya kwenda ndio maana ilimrudia na akafufuka. Au hujui kama Yesu alifufuka mkuu???
 
Ile

Roho kwa kuwa ilikuwa ya Mungu na ukikosa sehemu ya kwenda ndio maana ilimrudia na akafufuka. Au hujui kama Yesu alifufuka mkuu???
Hapo ndipo mlipodanganywa aisee. Ujinga kama huo Myahudi hataki kuusikia kabisa!
 
Yesu Si Mungu. Na hawezi kuwa Mungu.

Mungu haonekani hivyo hana mfano.
Hizo nyingine ni simulizi.

Hakuna sababu inayofanya Yesu Awe Mungu Mkuu
Ndio sio mungu mkuu ni mungu mwana
IMG-20171020-WA0006.jpg
 
Back
Top Bottom