Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

ntabhaligwa

Senior Member
Jan 2, 2017
141
102
Ni aghalabu sana kiongoz wa kiimani kuruhusu waumini na wasio waumini kuuliza maswali baada ya mada. Pengine utamaduni wa kuuliza maswali magumu ungekuwa ni Lazima, tusingeshuhudia utitiri wa madhehebu duniani, mengi yakiwa kwa maslahi ya viongozi wao.

Ni kiongoz mmoja tu (anayefahamika kwa sasa duniani) ambae ameenda mbali zaidi na kuruhusu maswali hata nje ya mada alizozungumzia na amekuwa akijibu kwa ufasaha na kutoa hata marejeo. Huyo Si mwingine bali ni Dr. Zakir Naik. katika video hii amejibu kuhusu kifo, kukata roho, roho ni nini na inaenda wapi baada ya kifo?

 
Ni aghalabu sana kiongoz wa kiimani kuruhusu waumini na wasio waumini kuuliza maswali baada ya mada. Pengine utamaduni wa kuuliza maswali magumu ungekuwa ni Lazima, tusingeshuhudia utitiri wa madhehebu duniani, mengi yakiwa kwa maslahi ya viongozi wao. Ni kiongoz mmoja tu(anayefahamika kwa sasa duniani) ambae ameenda mbali zaidi na kuruhusu maswali hata nje ya mada alizozungumzia na amekuwa akijibu kwa ufasaha na kutoa hata marejeo. Huyo Si mwingine bali ni Dr. Zakir Naik. katika video hii amejibu kuhusu kifo, kukata roho, roho ni nini na inaenda wapi baada ya kifo?


Imani, nafsi, Mungu.... Hivi vitu havina ithibati atakae jaribu kuvithibitisha kwa namna yeyote atakuwa anajiongopea .The brain and human mind are much smaller than God and faith.
 
Kutokans na upotoshaji huo wa Shetani ndio maana hata Mfalme Sauli alimuendea yule mama mchawi wa Endor akimuomba amuinulie Nathan Nabii. Ni kweli yule mama mchawi wa Endor alimuinua 'Nathan' na aliweza kumtabiria Sauli kuwa yeye na watoto wake wangekufa kesho yake. Jambo hilo ni kweli lilitokea kwani Sauli aliuawa yeye na Watoto wake kama vile 'Nathan'alivyomtabiria.

Hata hivyo ambacho Mfalme Sauli hakufahamu ni kuwa yule aliyemuona hakuwa Nathan bali ni roho wa Shetani aliyevaa umbo la Nathan. Nabii Nathan alishakufa kitambo na pia roho wa Bwana alishamuacha Sauli.
 
Hakuna utata wowote wapi roho inaenda baada ya kifo. Biblia takatifu imetoa ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo. Wanaosema kuna utata au wanaoleta hoja tofauti na Biblia hivyo yote ni kazi ya Shetani kuupotosha ukweli. Someni Biblia mkiongozwa na roho wa Bwana mtaelewa vema.
Wewe umeisoma biblia kwa kuongozwa na roho mtakatifu? Hata lete mistari sasa siyo kuongea kwa ujumla wake. Kwa taarifa tu biblia haijaelezea ni wapi roho zinapohifadhiwa baada ya mauti. Kama unajua toa andiko!
 
Hakuna utata wowote wapi roho inaenda baada ya kifo. Biblia takatifu imetoa ufafanuzi wa kina juu ya suala hilo. Wanaosema kuna utata au wanaoleta hoja tofauti na Biblia hivyo yote ni kazi ya Shetani kuupotosha ukweli. Someni Biblia mkiongozwa na roho wa Bwana mtaelewa vema.
Utata hapa ni pale tunajua roho zote baada ya kifo zinakwenda kwa Mungu. Sasa utata wa ile roho ya Mungu baada ya kufa ilienda wapi?
 
Hivi wakati yai la mwanamke linapoungana na mbegu ya mwanaume ni wakati huo roho inashuka kutoka kwa Mungu na kuanzisha maisha au maisha yanajianzisha yenyewe? Na kama inashuka kutoka kwa Mungu, zipo aina moja au kuna ya kike na kiume?

Ya kizungu, kiafrika, kichina nk. Anatuma nyingine inaazisha maisha ya akili finyu na akili ya kutisha, mtoa hoja mimi sina jibu, ila kinachokufanya uishi ndio roho ilipotaka kwangu ni utata
 
Back
Top Bottom