Roho ni nini? inaenda wapi baada ya kufa?

Pia unapoongelea uungu katika wakristo wa kweli Utatu Mtakatifu ni jambo la kuzingatia na linalofanya uungu wa Yesu kutokuwa wa kutilia shaka wala wa kuquestion.

Hii ni moja ya jambo la msingi sana katika Ukristo. Mwisho kama mwana wa binadamu ni binadamu kamili na mwana wa Mungu ni Mungu kamili.
 
Swali ulilolijibu ni lipi?

Kwanini ni muhimusana kwa Mungu huyu kuwa na mwanadamu anayemtii na kumuabudu?

Manasema Mungu mkubwa sana kwa uwezo, ujuzi etc, kwa nini ni muhimu sana mwanadamu amuabudu Mungu huyu?

Huyu Mungu hana mambo muhimu zaidi ya kufanya kuliko kutakakuabudiwa na mwanadamu kama rais dikteta anayependa kupigiwa makofi na wananchi masikini?

Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, mwanadamu ana uwezo wa kuchagua mazuri tu, angepungukiwa na nini?

Mungu anapenda kuabudiwa kiasi kwamba ameona ni sawa ulimwengu uweze kuwa na mabaya yote haya ili yeye aabudiwe tu?

Huyo ni Mungu mwenye upendo kweli?

Baba anampa mtoto mdogo asiye na akili pevu uamuzi wa kunywa maziwa au sumu, ili kusudi apate fahari tu kwamba mtoto anamsikiliza baba, wakati angeweza kuondoa sumu, mtoto anywe maziwa tu wala asipata nafasi ya kunywa sumu.

Huyu Baba utamsifia useme ana upendo?

Tushaona mwanadamu hana free will, hawezi hata kurudi nyuma katika muda aende kupiga story na mama yake aliyefariki 1982.

Kwa hiyo habari za fee will ni uongo. Pia,vitabu vya dini vinasema tunamjua Mungu kwa neema zake tu, si kwa jitihada zetu. Hapo hamna free will. Wanaomjua Mungu hawamjuikwa sababu wamejitahidi kumjua, bali kwa sababu yeye amewachagua wamjue,sasa kwa msingi huo, free will iko wapi?

Vitabu vya Mungu vinasema tunaokokakwa neema (Biblia). Quran inasema kuna watu Mungu atafanya mioyo yaoiwe migumu wasimjue Allah, hawa hata wakijitahidi vipi hawatamjua Allah, kwa sababu Allah mwenyewe atakuwa kaifanya mioyo yaoiwemigumu kumjua.

Sasa hawa wana free will gani?

Kwa nini baba mwenye uwezo wakumpa mwanawe maziwa tu, anywe ashibe, anampa uamuzi wa kuchagua maziwa anywe ashibe au sumu anywe afe?

Baba akitoa uchaguzi huo kwa mtoto ambaye hana akilipevu, utasema baba huyo ana upendo kweli?

Obviously huyo Adam hakuwa na akilipevu ndiyo maana akashawishika.

Kwa nini Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote alimpa uchaguzi wa mema na mabaya Adam wakati alikuwa na uwezo wa kumpauchaguzi wa mema tu katika dunia ambayo mabaya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.

Ukisema alitaka wanadamu wawe watii, utii unamuongezea nini Mungu? Kwa nini anapenda utii ambao unakuja na mabaya mengi sana?

Unaweza kumpa mwanao sumu apate chance ya kufa ili upate ufahari tu kwamba asipokunywa sumu ni mtii?

Mbona ukiwa baba kama huyo mwanadamu utaitwa katili? Mungu wenu katili?
Mkuu nahisi kuwa una shupaza shingo tu wakati ukweli uko wazi mbele yako jiulize kwanini Baba na Mama wakipata mtoto wanataka huyu mtoto husika awatii na kuwaheshimu na isitoshe mtoto anapoleta ukaidi kuna msemo tumezoea kuusikia kuwa nimekuzaa mimi na mimi ndo niliyekulea na pia kuwa tumbo miezi tisa nimekubeba hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo wazazi wanastahili kupewa heshima kwa sababu bila wao watoto wasingekuwepo yaani wao ndio waliowaleta ulimwenguni hivyo heshima yao lazima iwepo.

Sasa kama mzazi anapewa heshima hivi na anapewa hii heshima kwa sababu ndiye aliyemleta huyu mtoto ulimwenguni na pili ndiye aliyemtunza huyo mtoto yaani kamlea sasa je vipi Mungu aliyetuumba je hapaswi kuheshimiwa na je hapaswi kupewa utii kwa sababu Yeye ndiye aliyetuumba bila Yeye sisi tusingekuwepo na ni kwa uwezo wake mimi na wewe tupo hai hadi sasa je huyu Mungu hapaswi kuabudiwa na kupewa sifa na kutukuzwa kwa hiyo Yeye ndiye aliyetuumba na tunapaswa kumuabudu kwa sababu bila Yeye tusingelikuwepo
 
16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.Mungu alidhihirishwa katika mwili,Akajulika kuwa na haki katika roho,Akaonekana na malaika,Akahubiriwa katika mataifa,Akaaminiwa katika ulimwengu,Akachukuliwa juu katika utukufu.

1Timotheo3:16

Uungu wa Yesu unaweza ukauelewa taratibu kama ukitafakari na kutafiti...Hivi wamjua mfalme Melkizedecki ambae Ibrahim alimtolea fungu la kumi baada ya kutoka vitani

MWANZO14:18-19 umejaribu kumfuatilia kwa undani??
 
Kwanza kabisa, kamanilivyoeleza hapo juu, kisichopo,hakina proof nje ya logical construct,kwa sababu hakipo.

Huwezi kufanyia proof kitu ambacho hakipo kwamba hakipo. Kwa sababu, ilikufanya proof (iliyo nje ya logical constructs tu) inabidi kiwepo.

Nakikiwepo, huwezi kukifanyia proof kwamba hakipo, kwa sababu kipo.

Ukitakaku prove kwamba mwizi kaingia kwako,unaweza kufanya forensic fingerprint ukapata fingerprints za huyo mwizi.

Unaweza kuangalia security camera ukamuona mwizi kaingia.

Kama hakuna mwizi aliyeingia, uta prove vipi kwamba hakuna mwizi aliyeingia? Utatoa fingerprints za mwizi useme "hizi hapa fingerprints za mwizi ambaye hajaingia kwangu,hivyo hakuingia. Nime prove. Fingerprint hizi hapa" ?

Au utatoa mkanda wa security camera uoneshe kwamba "hii hapa video inaonyesha mwizi kaingia kwangu,hivyo huu ni ushahidi mwizi hajaingia"?

Hivyo, ambacho hakipo hakina sehemukubwa ya kuwa proved kwamba hakipo.

Kilichopo ndicho kina proof.

Zaidi, kisichopokinaweza kuwa proved hakipo kwakutumia logical construct. Proof by contradiction.Ukiweza ku contradict kitu unanonesha hakipo, hakiwezikuwepo, kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Ninaposemakwamba Mungu hayupo kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe,hiyo ni proof by contradiction kwamba Mungu hayupo.

Ni vipi dhana ya kuwepo Mungu ina contradiction?

1.Mnasema Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
2.Mungu mweye ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani ni contradiction.
3.Ulimwengu huu mabaya yanawezekana.
4. Ulimwengu huu ina m contradict Mungu huyo.
5. Mungu huyo hayupo.Kwa sababu ana contradiction.

Nime prove Mungu huyo hayupo kwa "proof by contradiction".

Ondoa contradiction hiyo u prove Mungu yupo.
Uwepo wa Mungu hauondolewi na contradiction za viumbe wake.
Namna watu wanavyomtafsiri Mungu ni katika kiwango cha ufahamu wao ulipofikia.
Ni sawa na mtu aliyeliona sikio la tembo na asiuone mwili wote, kama akili yake haitamtuma kwamba kuna makuzi ya kielimu kuhusu kile anachokifahamu na kwamba upeo wake sii absolute basi atang'ag'ana kwa nguvu zote kwamba tembo ni lile sikio.

Kwamba mungu ana upendo wote? Maana ya upendo ni nini na umeipata wapi. Upendo wa Mungu ni kwenda chini ndio kwenda juu. Na utii ndio ithibaki. Wewe una namna yako ya kutafsiri upendo. Baba anaweza akawa anamchapa mtoto wake viboko kwa masahihisho na hili linasukumwa na upendo na mwingine akawa hamchapi pia kwa sababu ya upendo.
Contradiction itainuka pale mmoja kwa mwingine atakapotaka kuwa ile hatua yake ndio upendo na sii ile ya mwingine.

Mungu ameumba kila kitu kiwe kama kilivyo na anaufahamu mwisho wake tokea mwanzo. Ni sawa na mcheza sinema hachezi isipokua kwanza amelichora wazo la kile anachotaka kiwe na kwamba kuna hatua ipi itacchuka nafasi gani hadi hitimisho.

Mcheza sinema anaujua mwisho wa sinema yake tokea mwanzo wa kuanza kwake. Vivyo hivyo Mungu.
 
Mkuu nahisi kuwa una shupaza shingo tu wakati ukweli uko wazi mbele yako jiulize kwanini Baba na Mama wakipata mtoto wanataka huyu mtoto husika awatii na kuwaheshimu na isitoshe mtoto anapoleta ukaidi kuna msemo tumezoea kuusikia kuwa nimekuzaa mimi na mimi ndo niliyekulea na pia kuwa tumbo miezi tisa nimekubeba hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo wazazi wanastahili kupewa heshima kwa sababu bila wao watoto wasingekuwepo yaani wao ndio waliowaleta ulimwenguni hivyo heshima yao lazima iwepo.
Sasa kama mzazi anapewa heshima hivi na anapewa hii heshima kwa sababu ndiye aliyemleta huyu mtoto ulimwenguni na pili ndiye aliyemtunza huyo mtoto yaani kamlea sasa je vipi Mungu aliyetuumba je hapaswi kuheshimiwa na je hapaswi kupewa utii kwa sababu Yeye ndiye aliyetuumba bila Yeye sisi tusingekuwepo na ni kwa uwezo wake mimi na wewe tupo hai hadi sasa je huyu Mungu hapaswi kuabudiwa na kupewa sifa na kutukuzwa kwa hiyo Yeye ndiye aliyetuumba na tunapaswa kumuabudu kwa sababu bila Yeye tusingelikuwepo
Baba na mama wanataka mtoto awatii kwa sababu hawana uwezo wakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Wanamwambia mtotowao "mwanetu, tusikilize, tutii. Usiibe, usiue.Utaishia pabaya. Tutii."

Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao kuiba na kuua hakuwezekani hata kufikirika maana hakupo, kwa nini aone haja ya kutaka utii ambao unakuja na kuwepo kwa mabaya mengi?

Angeumba dunia ambayo haina mabaya, ambayo haihitaji utii kwani haina uasi, angepungukiwa nini?
 
Uwepo wa Mungu hauondolewi na contradiction za viumbe wake.
Namna watu wanavyomtafsiri Mungu ni katika kiwango cha ufahamu wao ulipofikia.
Ni sawa na mtu aliyeliona sikio la tembo na asiuone mwili wote, kama akili yake haitamtuma kwamba kuna makuzi ya kielimu kuhusu kile anachokifahamu na kwamba upeo wake sii absolute basi atang'ag'ana kwa nguvu zote kwamba tembo ni lile sikio.
Kwamba mungu ana upendo wote? Maana ya upendo ni nini na umeipata wapi.
Upendo wa Mungu ni kwenda chini ndio kwenda juu. Na utii ndio ithibaki . Wewe una namna yako ya kutafsiri upendo. Baba anaweza akawa anamchapa mtoto wake viboko kwa masahihisho na hili linasukumwa na upendo na mwingine akawa hamchapi pia kwa sababu ya upendo.
Contradiction itainuka pale mmoja kwa mwingine atakapotaka kuwa ile hatua yake ndio upendo na sii ile ya mwingine.
Mungu ameumba kila kitu kiwe kama kilivyo na anaufahamu mwisho wake tokea mwanzo. Ni sawa na mcheza sinema hachezi isipokua kwanza amelichora wazo la kile anachotaka kiwe na kwamba kuna hatua ipi itacchuka nafasi gani hadi hitimisho.
Mcheza sinema anaujua mwisho wa sinema yake tokea mwanzo wa kuanza kwake. Vivyo hivyo Mungu.
Unawezaje kuthibitisha kwamba Mungu yupo na si hadithi tu?

Sijaona ulipothibitisha Mungu yupo.

Unaanza kwa ksuema tu yupo. Thibitisha kwanza kabla ya kusema yupo.
 
Unawezaje kuthibitisha kwamba Mungu yupo na si hadithi tu?

Sijaona ulipothibitisha Mungu yupo.

Unaanza kwa ksuema tu yupo. Thibitisha kwanza kabla ya kusema yupo.
.
Kisayansi ni kwamba hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu.
Maumbile yanashika asili yake kwa mtizamo wako ni nini?
 
Ulimwengu unakufanyaje uamini Mungu?

Mbona unasema mambo unayaacha yanaelea elea hewani tu bila ufafanuzi kama mtu ambaye ana matatizo ya kujieleza vizuri?
Huu ulimwengu unanifanya nifikiri kuwepo kwa aliyeuumba na hapo ndipo imani ya uwepo wa mungu inapokuja.
 
.
Kisayansi ni kwamba hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu.
Maumbile yanashika asili yake kwa mtizamo wako ni nini?
Kama hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu, hilo linathibitishaje kwamba Mungu yupo?

Nauliza, unaweza kuthibitisha hii hela imewekwa mezani na Baba?

Unanijibu, kisayansi hakuna hela inayoweza kujiweka mezani yenyewe.

Jibu lako si la swali langu.
 
Huu ulimwengu unanifanya nifikiri kuwepo kwa aliyeuumba na hapo ndipo imani ya uwepo wa mungu inapokuja.
Kwa nini huu ulimwengu unakufanya ufikiri kuwepo kwa aliyeuumba?

Kwa nini ukufanye ufikiri "aliyeuumba" na si "kilichouumba" ?

Na kwa nini aliyeuumba ni lazima awe Mungu tu, na si kingine chochote?
 
Kwa nini huu ulimwengu unakufanya ufikiri kuwepo kwa aliyeuumba?

Kwa nini ukufanye ufikiri "aliyeuumba" na si "kilichouumba" ?

Na kwa nini aliyeuumba ni lazima awe Mungu tu, na si kingine chochote?
Hivyo ndivyo navyoamini na ndiyo imani yangu,hivyo kama unaona ni imani potofu unaweza kuonesha au kueleza upotofu wa hivyo navyoamini.
 
Hivyo ndivyo navyoamini na ndiyo imani yangu,hivyo kama unaona ni imani potofu unaweza kuonesha au kueleza upotofu wa hivyo navyoamini.
Hujajibu maswali.

Upotofu waimani yako ni kwamba unaamini bila sababu, nakuuliza, sababu zinazokufanya uamini hivyoni zipi, unajibu hivyo ndivyo unavyoamini.

Huna tofauti na anayesema yeye ndiye mzazi wa baba yake.

Ukimuuliza sababu gani inakufanya uamini hivyo, labda ana mantiki.

Anajibu hivyo ndivyo anavyoamini.

Mungu wako hayupo kwa sababu hana logical consistency.

Ana contradiction.
 
Kama hakuna kitu cha kushikika kinachotokana na utupu, hilo linathibitishaje kwamba Mungu yupo?

Nauliza, unaweza kuthibitisha hii hela imewekwa mezani na Baba?

Unanijibu, kisayansi hakuna hela inayoweza kujiweka mezani yenyewe.

Jibu lako si la swali langu.
.
Wewe umekalia ubishi na sikulaumu kwa hilo maana ndiyo sehemu yako ya kufanya maisha yasonge.

Unaambiwa hakuna cha kushikika kutoka katika utupu unakuja na mfano usioendana kabisa.
Pesa kuwekwa au kutokuwekwa mezani kana uhusiano gani na material yaliyoitengeneza pesa? Nakuuliza tena, maombile ni ya kushikika mfano wa jua, sayari, wanyama nk. Asili yake ni nini?
 
.
Wewe umekalia ubishi na sikulaumu kwa hilo maana ndiyo sehemu yako ya kufanya maisha yasonge.
Unaambiwa hakuna cha kushikika kutoka katika utupu unakuja na mfano usioendana kabisa.
Pesa kuwekwa au kutokuwekwa mezani kana uhusiano gani na material yaliyoitengeneza pesa?
Nakuuliza tena, maombile ni ya kushikika mfano wa jua, sayari, wanyama nk. Asili yake ni nini?
Kama hujaelewa mfano, uliza.

Umesema hakuna kisichoshikika kilichotoka katika utupu.

Hilo halithibitishi kuwepokwa Mungu.

Kwa sababu, vinavyoshikika vilivyopo vinaweza kuwa havijatoka katika utupu, lakini pia havijatoka kwa Mungu.

Mfano wa hela iliyo mezaniunakujaje?

Kusema kwamba hakuna kinachoshikika ambacho hakijatoka kwenye utupu,ni sawa na kusema hakuna hela iliyo mezani iliyojiweka yenyewe mezani, lazima kutakuwa na namna iliyofanyika kuifanya hela iwe mezani.

Kufikiri kwamba ukisema hakuna kinachoshikika kinachotoka katika utupu ni uthibitisho wa kwamba kinachoshikika kimetoka kwa Mungu ni sawasawa na kusema ukiona hela imekaa mezani, lazima imewekwa na baba.

Inawezekana nyumba haina Baba, hela imewekwa mezani na mama.

Au nyumba haina baba, hela imewekwa mezani na mtoto.

Kwa nini unasemakwakuwa kuna hela mezani tu, basi hela imewekwa na baba?

Kwa nini unafikirikwa kuwa hakuna kinachoshikika kinachotoka katika utupu tu, na kinachoshikika kipo, basilazima kimetoka kwa Mungu?

Ndiyo maana nikakwambia, ukisema hakuna kinachoshikika kinachotoka katikautupu, hilo halithibitishi uwepo wa Mungu.
 
Hujajibu maswali.

Upotofu waimani yako ni kwamba unaamini bila sababu, nakuuliza, sababu zinazokufanya uamini hivyoni zipi, unajibu hivyo ndivyounavyoamini.

Huna tofauti na anayesema yeye ndiye mzazi wa baba yake.

Ukimuuliza sababu gani inakufanya uamini hivyo, labda ana mantiki.

Anajibu hivyo ndivyo anavyoamini.
Naepusha kujadili mambo ambayo yameshajadiliwa sana,mimi nauelekeza mjadala tujadili vitu vipya ila naona ushazoea kurudia mambo yaleyale ili mwisho unaze kusema hakuna aliyeweza kuthibitisha kama kuna mungu.

Sababu zinazowafanya watu waamini zinajulikana hivyo sioni ulazima kuanza kulieleza kwa sana.

Na ndiyo maana nikakwambia kama unaona hii ni imani potofu basi onesha huo upotofu,maana imani ya mungu inajulikana.
 
Imani ya kuwepo kwa Mungu ni potofu kwa sababu inajipinga yenyewe. Ina contradictions.

Nimezitaja contradictions hapo juu,kamaunaweza kuziondoa, ziondoe.

The problem of evil is a big contradiction for an all knowing, all loving and allcapable Godhead.

This contradiction is not yet solved.

Because, such a God does not exist. he is fictitious.
 
Baba na mama wanataka mtoto awatii kwa sababu hawana uwezo wakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Wanamwambia mtotowao "mwanetu, tusikilize, tutii. Usiibe, usiue.Utaishia pabaya. Tutii."

Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao kuiba na kuua hakuwezekani hata kufikirika maana hakupo, kwa nini aone haja ya kutaka utii ambao unakuja na kuwepo kwa mabaya mengi?

Angeumba dunia ambayo haina mabaya, ambayo haihitaji utii kwani haina uasi, angepungukiwa nini?
Kwani Mungu alivyouumba ulimwenguni kulikuwa Kuna baya lolote si mpaka Adamu na Hawa walipokula tunda ndio mabaya yakajitokeza na kama wasingekula yaani wakatii mpango WA Mungu hayo mabaya si yasingekuwepo na unauliza kwanini aliweka vitu vingi at stake na hili linajibiwa kiurahisi Tu Kwa kuonyesha kuwa kumtii Mungu si jambo au swala Tu la maarifa ila kumtii kunampa mwanadamu uhai na kutokumtii Mungu muweza wa yote basi lazima kuwe na matokeo na matokeo yake Ni kifo.

Kwa hiyo swala la kumtii Mungu msingi wake upo kwenye uhai wa kiumbe husika kilichouumbwa yaani mwanadamu kwa kuwa kilichoumbwa hakiwezi kumuuliza Muumba mbona wafanya hivi na raha Ni kwamba mwanadamu alipewa uhuru na cha pili alipewa onyo kuwa akila atakufa kwa hiyo hili linaonyesha upendo wa ajabu na hata mabaya yalipoingia basi Yeye akaja kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi hivi vyote vinaonyesha Upendo mkuu wa ajabu na Mungu sio dikteta mkuu bali Ni Upendo
 
Kwani Mungu alivyouumba ulimwenguni kulikuwa Kuna baya lolote si mpaka Adamu na Hawa walipokula tunda ndio mabaya yakajitokeza na kama wasingekula yaani wakatii mpango WA Mungu hayo mabaya si yasingekuwepo na unauliza kwanini aliweka vitu vingi at stake na hili linajibiwa kiurahisi Tu Kwa kuonyesha kuwa kumtii Mungu si jambo au swala Tu la maarifa ila kumtii kunampa mwanadamu uhai na kutokumtii Mungu muweza wa yote basi lazima kuwe na matokeo na matokeo yake Ni kifo. Kwa hiyo swala la kumtii Mungu msingi wake upo kwenye uhai wa kiumbe husika kilichouumbwa yaani mwanadamu kwa kuwa kilichoumbwa hakiwezi kumuuliza Muumba mbona wafanya hivi na raha Ni kwamba mwanadamu alipewa uhuru na cha pili alipewa onyo kuwa akila atakufa kwa hiyo hili linaonyesha upendo wa ajabu na hata mabaya yalipoingia basi Yeye akaja kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi hivi vyote vinaonyesha Upendo mkuu wa ajabu na Mungu sio dikteta mkuu bali Ni Upendo
Hiujaelewa swali langu si kwa nini ulimwengu una mabaya.

Hili si swali langu.

Swali langu ni, kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa ana uwezo wakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea.

Hjaelewa swali mpaka sasa.

Sishangai hujaweza kulijibu.

Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, kutotii kusingewezekana kwa hivyo suala la utii lingekuwa moot.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kabisa?
 
Hiyo akili yako ingewezaje kujua kuwa haya ni mazuri? Utajuaje mwanga bila Giza?
 
Back
Top Bottom