Riwaya za Zamani, Hadithi ya Allan Quatermain | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Riwaya za Zamani, Hadithi ya Allan Quatermain

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by X-PASTER, Jun 18, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mambo ya Ajabu Yaliyompata Allan Quatermain na Wenzake.

  Leo nitadonoa kidogo Hadithi ya Allan Quatermain, Simulizi za Sir H. Rider Haggard kwenye moja ya simulizi zake zinazo elezea visa vya mwindaji Tembo hodari Bwana Allan Quatermain.

  allan Quatermain (Makumazan or Macumazahn)... Na msaidizi wake Msolopagazi (Umslopogaas) na shoka lake Inkosi kazi (Inkosi-kaas)... Bwana Henry Curtis, na rafikie Siri Good, (Bwana Mzuri).

  Kwenye riwaya hii ndipo pia lilipo patikana jina Gagula... Kibibi kilichokuwa kichawi (Kigagula).

  Vitabu hivi ni miongoni mwa vitabu ambavyo vinaonyesha au kusimulia ujasiri na ushujaa wa hali ya juu sana... Soma pia riwaya ya Machimbo ya Mfalme Suleiman na nchi ya Wakukuana... Na vitabu vyake vingine ambavyo havikuwahi kutafsiriwa kwa kiswahili kama vile SHE, Ayesha, The Virgin of the Sun na Vingine vingi. Gonga HAPA kupata orodha ya vitabu vyake.

  Wale waliowai kusoma Hadithi ya Allan Quatermain watamkumbuka sana Bwana Mslopagazi (Umslopogaas), na majigambo yake a.k.a Mikwara mizito aliyokuwa akiwatishia maadui zake...!

  Basi tega sikio, nikumegee japo kidogo.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  "Baba yangu, ninazo habari nitakazokuambia, lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyonge hawa, maneno yangu ni baina ya mimi na wewe tu. Baba yangu, nitasema haya tu:

  Mwanamke alinihaini mautini, akalifunika jina langu kwa aibu, ndiyo, mke wangu mwenyewe, mwanamwali mwenye uso kama mwezi, alinihaini, lakini niliokoka na mauti; ndipo nilipoponyoka katika mikono ya wale waliokuja kuniua. Nilipiga mapigo matatu tu kwa shoka langu hili Inkosikazi - hakika baba yangu atalikumbuka, moja upande wa kuume, moja upande wa kushoto, na moja mbele yangu, na hata hivyo niliwaacha watu watatu wamekufa. Kisha, nilikimbia, na kama baba yangu ajuavyo, ingawa mimi ni mzee, lakini miguu yangu ni myepesi kwenda mbio kama ile ya paa, wala hapana mtu anayeweza kunigusa tena niishapo kutoka mbavuni pake.

  Mbele nilikimbia, na matarishi wa mauti walinia ndama nyuma, na sauti zao zilikuwa kama sauti za mbwa wanaowinda. Kutoka nyumbani kwangu nilikimbia; nikampita yule aliyenihaini alikuwa akiteka maji kisimani. Nilimpita upesi kama kivuli cha mauti, na nilipokuwa nikipita nilimpiga dharuba moja kwa shoka langu, tahamaki! kichwa chake kilimtoka, kikaangukia kisimani. Kisha, nilikimbilia kaskazini. Siku baada ya siku nilisafiri; kwa miezi mitatu nilisafiri, nisipumzike, nisisimame, ila nilizidi kukimbilia kwenye usahaulifu, mpaka nilipoonana na safari ya yule mwindaji mweupe aIiyekwisha kufa, nami nimekuja hapa pamoja na watumishi wake.

  Wala sikuleta kitu pamoja nami. Mimi niliye mtoto wa watu, ndiyo, wa damu ya mfalme mkuu Chaka, mimi niliye mkuu mwenyewe, jemadari katika kikosi cha Nkomabakosi, sasa mimi ni mgaagaa, mtu asiye na nyumba. Wala sikuleta kitu pamoja nami ila shoka hili langu, kwa nguvu zake ambazo kwazo niliwatawala watu wangu. Wamewagawanya ng'ombe zangu; wamewatwaa wake zangu; na watoto wangu hawautambui uso wangu tena.

  Hata hivyo, kwa shoka lili hili nitakata njia nyingine nifike mpaka kwenye usitawi. Nimesema!"

  Basi, akalizungusha shoka lake kichwani likalialia lilipokuwa likiikata hewa.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nadhiri ya Umslopagaas

  Msikilize Mjivuni, akimwaga mkwara:

  "...kwa heri, na ninyi watu weupe wengine kwa herini, ambao makope yenu nitayafumba daima karibuni hivi.
  Kutakapo pambazuka utaleta jibu lako. Kama sivyo, basi, mambo yatakuwa kama nilivyosema." Kisha, akageuka akamtazama Umslopogaas aliyekuwa amesimama nyuma yake kama anamlinda, akasema, "Eh, fungua mlango upesi sana, haya upesi!"

  Amri hii ilimchukiza sana yule mzee Mzulu. Kwa muda wa dakika kumi alikuwa amesimama kama kwamba anatamani kumpiga yule Mjivuni, hapo basi hakuweza kustahimili zaidi, akauweka mkono wake mrefu juu ya bega la yule Mjivuni, akamvuta kwa nguvu hata kumgeuza kabisa na kumfanya amtazame usoni. Kisha, aliupeleka uso wake mkali katika uso wenye duara ya manyoya wa yule Mjivuni, akasema kwa sauti iliyonguruma:

  "Waniona?"
  Yule Mjivuni akajibu, "Ndiyo, nakuona kitwana."

  Umslopogaas akasema, "Waliona hili?" akaweka Inkosikazi mbele ya macho yake, Yule Mjivuni akasema, "Ndiyo, kitwana, nauona 'mchezo' wako; ya nini?"

  Umslopogaas akasema, "Wewe Mjivuni mbwa, wewe mpayapaya, wewe mjivunaji, wewe mkamata watoto wanawake; kwa 'mchezo' huu nitavikongoa viungo vyako. Ni vyema ya kuwa u tarishi, ama sivyo, ningevitawanya tawanya viungo vyako chini katika majani."

  Yule Mjivuni akautikisa mkuki wake mrefu, akacheka sana kwa muda mrefu, akajibu, "Laiti tungeweza kushindana mimi na wewe peke yetu, ningekuonyesha mambo."

  Akageuka aende zake huku anacheka. Umslopogaas akajibu, na sauti yake ingali ikinguruma, "Usiwe na shaka, tutashindana peke yetu mimi na
  wewe. Utashindana uso kwa uso na Umslopogaas, wa damu ya Chaka, wa kabila la Wazulu, mkuu wa jeshi la Nkomabakosi, kama wengi wengine walivyofanya; nawe utajiinamisha mbele ya Inkosikazi kama walivyofanya wengi wengine. Ndiyo, cheka, cheka! Usiku wa kesho
  fisi watakuwa wanacheka na huku wanavunja na kuzitafuna mbavu zako
  ."
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Basi yule mjivuni alipoona ya kuwa ingawa anakimbia kadiri awezavyo, lakini yule anayemfuata anazidi kumkaribia tu, akasimama akageuka ili apigane naye. Umslopagaas naye akasimama vile vile, akasema kwa dhihaka.

  "Ah, ah, ni wewe niliyesema nawe usiku. Mkubwa wa Wajivuni! tarishi! Mkamata watoto wa kike, aliyekuwa tayari kumwua mtoto wa kike! Ndiwe uliyetumaini kusimama uso kwa uso kuwahiana na Umslopogaas, mkubwa wa ukoo wa Makwilisini, wa kabila la Wazulu? Tazama, maombo yako yametimizwa! Nami, niliapa kuwa nitavikongoa viungo vyako, mbwa mfidhuli wewe. Tazama, nitaitimiza nadhiri yangu sasa!"

  Yule Mjivuni aliyasaga meno yake kwa hasira, akamrukia Umslopogaas na mkuki wake mkubwa. Alipomjia, Umslopogaas aliepa vizuri, akalipunga shoka lake juu kichwani kwa mikono yote miwili, akalishusha tena kwa nguvu, likampiga yule Mjivuni nyuma ya mabega shingo inapoungana na kiwiliwili, na makali yake yalikata mfupa na nyama na mishipa, yakawa karibu kutenga kichwa na mkono rnmoja na kiwiliwili. Umslopogaas aliitazama maiti ya adui yake, akasema, "Basi! Nimetimiza nadhiri yangu. Ama lilikuwa pigo zuri."
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Baada ya ile vita ya katika kipito, Masimulizi yanaendelea kama hivi.

  "...Basi, vivi hivi saa baada ya saa. Halafu niliona ya kuwa farasi mzuri niliyempanda anaanza kupotewa na nguvu. Nikaitazama saa yangu; ilikuwa karibu saa sita za usiku, na tulikuwa tumemaliza zaidi ya nusu ya safari yetu. Juu ya mwinuko palikuwa chemchemi niliyo ikumbuka nikamwashiria Umslopogaas asimame hapo, maana nilikusudia kuwapumzisha farasi zetu na sisi wenyewe muda wa dakika kumi. Basi; alisimama, tukashuka katika farasi zetu; na farasi walisimama wanatweta wakisimama kwanza kwa mguu huu halafu huu, na huku jasho linawatoka na mvuke wao unaonekana kama ukungu katika hewa kimya ya usiku.

  "...Basi, kisha Umslopogaas alinisaidia nipande juu ya farasi na yeye - mtu mwenye nguvu - akaruka juu yake bila kuvigusa vikuku vya matandiko yake, tukaanza tena safari yetu, kwanza taratibu mpaka farasl waka zoea, kisha mbio. Basi, hivyo tulienda mwendo wa maili kumi tena, ndipo tulipofika kwenye mwinuko wa mwendo wa maili sita au saba. Mara tatu farasi wangu alitaka kuanguka, lakini alipofika juu ya mwinuko alijipa moyo tena akaenda mbio kutelemka kwa hatua zilizokatikakatika na huku anatweta sana.

  Tulikwenda mwendo wa maili tatu nne zile mbio kuliko kwanza, lakini niliona ya kuwa ni juhudi ya mwisho ya farasi wangu. Basi, ghafula alishika sana lijamu katikati ya meno yake akaenda mbio sana kadiri ya yadi mia tatu nne, ndipo aliposita hatua mbili tatu akaanguka kikichwa kichwa, na mimi nilijitupa mbele yake kadiri nilivyoweza.

  Nilifanya haraka kusimama nikamtazama farasi wangu, akanitazama kwa macho ya kusikitisha, kisha kichwa chake kikaanguka akaguna, akakata roho. Moyo wake ulikuwa umepasuka.

  Umslopogaas alisimama, nikamtazama kwa fadhaa, maana hata sasa bado mwendo wa maili ishirini, tutafika namna gani kabla ya mapambazuko hali tuna farasi mmoja tu?

  IIikuwa kama haiwezekani, lakini nilikuwa nimesahau nguvu za kupiga mbio za Mzee Mzulu. Bila kusema neno akashuka katika farasi akanipandisha mimi. Nikamwuliza, "Wewe utafanya nini?"

  Akashika kikuku cha matandiko ya farasi, akajibu, "Nitapiga mbio."

  Ndipo tulipoanza tena kupata mbio karibu na zile za kwanza.

  Yule farasi Nuru alienda mbio na kila hatua alimsaidia yule Mzulu. Ilikuwa ajabu kumuona Umslopagaas akipiga mbio maili baada ya maili, na midomo yake i wazi na mianzi ya pua imepanuka kama ya farasi. Kila maili ya tano tulisimama ili kupumzika kidogo, kisha tukazidi kuendelea.

  Baada ya kupumzika mara tatu, nikamwuliza, "Je, unaweza kuendelea au nikuache unifuate nyuma?"

  Alilishika shoka lake akalielekeza kivuli cheusi mbele yetu, nikaona kumbe ni Hekalu la Jua, nalo halikuwa mbali zaidi ya maili tano. Akasema na huku anatweta "Nitalifikia ama nitakufa."
   
 6. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ni tamu. baadae utupa na za akina bunuasi na wengine
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Nakumbua mwisho wa riwaya Umsolopaganzi alipomaliza kazi ya kulinda ngazi kuu... Alikuwa amepata majeraha mengi mwilini... akajua kuwa mwisho wa uhai wake umekaribia ndipo alipoamua kufa na shoka lake (Bibi msemi).... alilizungusha shoka lake kiasi ya kuonekana kama mwali wa moto... kisha kwa pigo moja... pigo lililo takatifu... Pigo lililo nyooka... akalishusha shoka lake kwa kasi ya ajabu na kulipasuwa jiwe lile na huku shoka lake likitawanyika vipande vipande na kubakia akiwa ameshikilia mpini wa shoka ukiwa mzima.... Mzee wa kizulu akaanguka chini akakata roho...

  Pata uondo kidogo:

  Yule Mzulu mzee akacheka, akasema; "Je na wewe umekuja pia! Karibu-karibu shujaal Aha! Namsifu yule mtu anayeweza kufa kiume! Aha! Na nguvu za kuua na kishindo cha silaha! Aha!

  Tu tayari! Tunainoa midomo yetu kama tai, mikuki yetu inang'aa katika miali ya Jua; twaitikisa mikuki yetu tuna njaa ya kupigana. Nani anayekuja kumwamkia Inkosikazi? Nani anataka kumbusu yeye ambaye matunda ya kubusu kwake ni kufa? Mimi Gotagota, mimi mwuaji, mimi mwenye mbio, mimi Umslopagaas mwenye shoka, wa kabila la Kizulu, mkuu wa kikosi cha Nkomabakosi: mimi Umslopogaas, mwana wa ulimi wa Mfalme, mwana wa Makedama, mtoto wa Mosilikaatze, mimi, wa damu ya Mfalme Chaka, mimi, mshindi wa wasio shindika, mimi nawaita kama kulungu aitwavyo, nawakaribisha, nawangojea. Aha! Ni wewe, ni wewe!

  Ah ah ah ah, yaani jinsi masimulizi ya hii riwaya yalivyo mazuri, kiasi ya kwamba kama unaona sinema vile, na mwisho kabisa baada ya kuwamaliza maadui zake, mambo yalikuwa hivi...!


  Baada ya kuwamaliza maadui wote, Umslopagaas, alipita moja kwa moja katika sebule na huku anaacha alama za damu nyuma yake mpaka alipoufikia ule mwamba mtakatifu ulioko katikati, na hapo ikawa kwamba nguvu zake zinamwishia, akasimama akaliegemea shoka lake. Kisha, akapasa sauti yake akasema kwa sauti kuu,

  "Nakufa, nakufa lakini vilikuwa vita vya Kifalme. Wako wapi wale walioipanda ngazi kuu? Siwaoni. Wewe upo Makumazahn, au umekwisha nitangulia katika mahali pa giza ninakokwenda mimi? Damu inanipofusha - mahali panazungukazunguka - nasikia ngurumo ya maji: ninaitwa!"

  Ndipo alipoonekana kama kwamba amefikiwa na wazo jingine, akainua shoka lake jekundu akalibusu bamba lake. Akalia, "Kwa heri Inkosikazi. Hapana, hapana, tutakwenda pamoja; hatuwezi kuagana mimi na wewe. Tumeishi pamoja siku nyingi, wewe na mimi. Hapana mwingine hatakaye kushika. Pigo jingine moja tu! Pigo lililonyoka! Pigo lenye nguvu!"

  Akajinyosha urefu wake wote; akapiga ukelele uliotikisa hata moyo, akaliinua shoka lake juu ya kichwa chake kwa mikono yake miwili, akalizungusha kichwani mpaka likaonekana kama duara ya nuru. Ndipo alipolipiga kwa nguvu za kutisha sana juu ya mwamba mtakatifu na cheche za moto zikaruka juu, na nguvu zilikuwa za ajabu hata mwamba ule wa marmar ulipasuka kwa kishindo ukavunjika vipande vipande, na Inkosikazi nalo likavunjika pia vikasalia vipande vya chuma na kipini chake tu.

  Vile vipande vya mwamba mtakatifu vikaanguka chini kwa kishindo kikubwa, ndipo yule mzee Mzulu shujaa alipoanguka chini, amekufa; lakini angali anaishika sehemu ya kipini cha Inkosikazi mkononi mwake.

  Basi ndivyo alivyokufa yule shujaa.

  Nasi Waswahili tukapata methali mpya, "Palipovunjika shoka mpini ukabaki"
   
 8. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukuru umenikumbusha mbali, nilisoma kitabu Kama Mara kumi.
   
 9. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kibibi Gagula yupo kwenye King Solomon mines (machimbo ya mfalme Suleiman).

  Thanks kwa kunikumbusha stori hizi. Nakumbuka kwenye hii ya umsolopagaas, alipomwona Makumazha, aliongea risala fulani "mkuu, mkuu, mkuu, Makumazhan.... unakumbuka ...ilivyoua tembo..." Hapa ilikuwa kabla hawajaanza safari ya kuingia bara ambako ndiko walikutana na wajivuni, baadaye kupotea kwa kuchukuliwa na mto hadi kuingia nchi ya wazuvendi.
  Zilikuwa stori nzuri kuliko hizi za kwenye globalpublishers.
   
 10. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkuu hadithi hizi ndizo zilinifanya niwe ninapenda kusoma, zinasisimua na kujenga ujasiri wa hali ya juu-asante kwa kumbukumbu mkuu
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa kutukumbusha hadithi hizi. Zina mvuto na ushawishi wa kutaka kuendelea kusoma tena na tena. Hadithi za siku hizi zinaboa tu. Pokea 5 Mkuu!
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu nalijua ilo la bibi Kigagula kuwemo kwenye simulizi ya Machimbo ya Mfalme suleiman, hapo nilitaka kuandika kwa ujumla yaani "riwaya hizi" na ndipo vidole vikasahau kuchapa vema, ah ah ah ah.

  Enzi hizo wale jamaa waliokuwa wanajifanya wao bab'kubwa tukiwaita kwa majina mbali mbali, mojawapo ni ili kutoka simulizi ya Allan Quertamain... "Mpaya paya"
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Poa mkuu.
  Tupo pamoja.
  Hivi umegundua vijana siku hizi hawasomi vitabu?
  Tunatakiwa kufanya juhudi za makusudi ili kuwahamasisha wasome hadithi kama hizi na zingine. Vitabu vinafundisha ujanja, na vinaboresha lugha.

  Anyway, thanks again for the thread.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana, umenikumbusha zamani.
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ah ah ah ah, mkuu, unanichekesha, wasome vitabu na muda wa kucheza video game wamuachie nani, yaani wasome vitabu wapitwe na tamthilia za Eastender, Rebeka, shades of Sin, don't Mess with an Angel na Isidingo!?
  Wataalam wanasema kuwa wale wenye tabia za kujisomea wanakuwa na kumbukumbu nzuri sana kuliko wenye kutumia mitandao kutafuta refference.
   
 16. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280
  tulikuwa tukitembea na vishoka
   
 17. Kijuso

  Kijuso Senior Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 161
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  DU mzee leo umenikumbusha mbali sana! nakumbuka nilikuwa ninasoma hicho kitabu kila baada ya siku tatu,halafu unakwenda kutoa hayo maneno shuleni basi wenzeko wanakuona mjanja sana, tete tete haha haah!!
  Ahsante mkuu!
   
 18. Pipiro

  Pipiro JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 307
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  " Ndio kwanza natoka kumzika mwanangu, mwanangu pekee wa kiume.... Moyo umejaa simanzi...." Hivi ndivyo kinavyoanza....

  Jamani jamani hizi simulizi zilikuwa zimetafsiriwa kwa kiswahili fasaha.... Nilikuwa nasoma mpaka unapata picha halisi kama unaona kwenye sinema.... Mwandishi alikuwa mahiri sana.... Jamani naweza wapi kuvipata hizi vitabu ? Nilikuwa navyo nimeviweka mahali nilipoamini salama kabisa, nikasafiri kwenda nje ya nchi kwa masomo bila kujua kuwa kuviacha nyuma ni makosa.... Niliporudi la haula sijui vimepotelea wapi.....

  Nilikuwa naweza kukaa ndani siku nzima nasoma..... Anayejua vinapatikanaje aniambie tafadhali, nashukuru sana.....
   
 19. m

  mshangama Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  jamani nakala ya kitabu hiki inapatikana?
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Kwenye mtandao niliwahi kuipata ya kiingereza, jaribu ku google.
   
Loading...