Riwaya za Zamani, Hadithi ya Allan Quatermain

MAKUMAZAHN maana yake AKESHAE: Kamwe hawezi kupata usingizi penye hatari
 
Loh.. Wakati umekwenda wapi...(?)...jamani! Taim iz kwending!! Kwi kwi kwi. Mkuu XP senkyu bai ze wei.
 
Kwakweli nimefurahi sana maana nilisoma zamani sana copy iliyochakaa na nikiwa bado primary na maneno mengi sikuyaelewa vizuri, sadly I've never come across it baada ya enzi hizooo
 
Baada ya ile vita ya katika kipito, Masimulizi yanaendelea kama hivi.

"...Basi, vivi hivi saa baada ya saa. Halafu niliona ya kuwa farasi mzuri niliyempanda anaanza kupotewa na nguvu. Nikaitazama saa yangu; ilikuwa karibu saa sita za usiku, na tulikuwa tumemaliza zaidi ya nusu ya safari yetu. Juu ya mwinuko palikuwa chemchemi niliyo ikumbuka nikamwashiria Umslopogaas asimame hapo, maana nilikusudia kuwapumzisha farasi zetu na sisi wenyewe muda wa dakika kumi. Basi; alisimama, tukashuka katika farasi zetu; na farasi walisimama wanatweta wakisimama kwanza kwa mguu huu halafu huu, na huku jasho linawatoka na mvuke wao unaonekana kama ukungu katika hewa kimya ya usiku.

"...Basi, kisha Umslopogaas alinisaidia nipande juu ya farasi na yeye - mtu mwenye nguvu - akaruka juu yake bila kuvigusa vikuku vya matandiko yake, tukaanza tena safari yetu, kwanza taratibu mpaka farasl waka zoea, kisha mbio. Basi, hivyo tulienda mwendo wa maili kumi tena, ndipo tulipofika kwenye mwinuko wa mwendo wa maili sita au saba. Mara tatu farasi wangu alitaka kuanguka, lakini alipofika juu ya mwinuko alijipa moyo tena akaenda mbio kutelemka kwa hatua zilizokatikakatika na huku anatweta sana.

Tulikwenda mwendo wa maili tatu nne zile mbio kuliko kwanza, lakini niliona ya kuwa ni juhudi ya mwisho ya farasi wangu. Basi, ghafula alishika sana lijamu katikati ya meno yake akaenda mbio sana kadiri ya yadi mia tatu nne, ndipo aliposita hatua mbili tatu akaanguka kikichwa kichwa, na mimi nilijitupa mbele yake kadiri nilivyoweza.

Nilifanya haraka kusimama nikamtazama farasi wangu, akanitazama kwa macho ya kusikitisha, kisha kichwa chake kikaanguka akaguna, akakata roho. Moyo wake ulikuwa umepasuka.

Umslopogaas alisimama, nikamtazama kwa fadhaa, maana hata sasa bado mwendo wa maili ishirini, tutafika namna gani kabla ya mapambazuko hali tuna farasi mmoja tu?

IIikuwa kama haiwezekani, lakini nilikuwa nimesahau nguvu za kupiga mbio za Mzee Mzulu. Bila kusema neno akashuka katika farasi akanipandisha mimi. Nikamwuliza, "Wewe utafanya nini?"

Akashika kikuku cha matandiko ya farasi, akajibu, "Nitapiga mbio."

Ndipo tulipoanza tena kupata mbio karibu na zile za kwanza.

Yule farasi Nuru alienda mbio na kila hatua alimsaidia yule Mzulu. Ilikuwa ajabu kumuona Umslopagaas akipiga mbio maili baada ya maili, na midomo yake i wazi na mianzi ya pua imepanuka kama ya farasi. Kila maili ya tano tulisimama ili kupumzika kidogo, kisha tukazidi kuendelea.

Baada ya kupumzika mara tatu, nikamwuliza, "Je, unaweza kuendelea au nikuache unifuate nyuma?"

Alilishika shoka lake akalielekeza kivuli cheusi mbele yetu, nikaona kumbe ni Hekalu la Jua, nalo halikuwa mbali zaidi ya maili tano. Akasema na huku anatweta "Nitalifikia ama nitakufa."

Ubarikiwe mkuu! Umenikumbusha mbali mkuu. Huyu Mhandisi wa Kiingereza, Sir Allan Stephen Quartemaine alikuwa moto wa kuotea mbali (apumzike kwa amani)

 
Namie pia umenigusa!
Nimewakumbuka Bw Good
Sir Henry Bogwan
Malkia Nelephta na Sorais.
Na mwanae Hary aliyemzika kwenye kimvuli cha kanisa la kale.
 
Ubarikiwe mkuu! Umenikumbusha mbali mkuu. Huyu Mhandisi wa Kiingereza, Sir Allan Stephen Quartemaine alikuwa moto wa kuotea mbali (apumzike kwa amani)


Namie pia umenigusa!
Nimewakumbuka Bw Good
Sir Henry Bogwan
Malkia Nelephta na Sorais.
Na mwanae Hary aliyemzika kwenye kimvuli cha kanisa la kale.
Pamoja sana wakuu, ila hasara kwa vizazi vya dot com...!
 
"Baba yangu, ninazo habari nitakazokuambia, lakini siwezi kusema mbele ya watu wanyonge hawa, maneno yangu ni baina ya mimi na wewe tu. Baba yangu, nitasema haya tu:

Mwanamke alinihaini mautini, akalifunika jina langu kwa aibu, ndiyo, mke wangu mwenyewe, mwanamwali mwenye uso kama mwezi, alinihaini, lakini niliokoka na mauti; ndipo nilipoponyoka katika mikono ya wale waliokuja kuniua. Nilipiga mapigo matatu tu kwa shoka langu hili Inkosikazi - hakika baba yangu atalikumbuka, moja upande wa kuume, moja upande wa kushoto, na moja mbele yangu, na hata hivyo niliwaacha watu watatu wamekufa. Kisha, nilikimbia, na kama baba yangu ajuavyo, ingawa mimi ni mzee, lakini miguu yangu ni myepesi kwenda mbio kama ile ya paa, wala hapana mtu anayeweza kunigusa tena niishapo kutoka mbavuni pake.

Mbele nilikimbia, na matarishi wa mauti walinia ndama nyuma, na sauti zao zilikuwa kama sauti za mbwa wanaowinda. Kutoka nyumbani kwangu nilikimbia; nikampita yule aliyenihaini alikuwa akiteka maji kisimani. Nilimpita upesi kama kivuli cha mauti, na nilipokuwa nikipita nilimpiga dharuba moja kwa shoka langu, tahamaki! kichwa chake kilimtoka, kikaangukia kisimani. Kisha, nilikimbilia kaskazini. Siku baada ya siku nilisafiri; kwa miezi mitatu nilisafiri, nisipumzike, nisisimame, ila nilizidi kukimbilia kwenye usahaulifu, mpaka nilipoonana na safari ya yule mwindaji mweupe aIiyekwisha kufa, nami nimekuja hapa pamoja na watumishi wake.

Wala sikuleta kitu pamoja nami. Mimi niliye mtoto wa watu, ndiyo, wa damu ya mfalme mkuu Chaka, mimi niliye mkuu mwenyewe, jemadari katika kikosi cha Nkomabakosi, sasa mimi ni mgaagaa, mtu asiye na nyumba. Wala sikuleta kitu pamoja nami ila shoka hili langu, kwa nguvu zake ambazo kwazo niliwatawala watu wangu. Wamewagawanya ng'ombe zangu; wamewatwaa wake zangu; na watoto wangu hawautambui uso wangu tena.

Hata hivyo, kwa shoka lili hili nitakata njia nyingine nifike mpaka kwenye usitawi. Nimesema!"

Basi, akalizungusha shoka lake kichwani likalialia lilipokuwa likiikata hewa.
X-PASTER ​Niambie kwa sasa hivi vitabu vinapatikana wapi?
 
X-PASTER ​Niambie kwa sasa hivi vitabu vinapatikana wapi?
KARIA, kuvipata hivi vitabu kwa sasa ni tabu sana, labda jaribu ku google online Amazon. Mimi niliviagiza Mombasa Kenya, mwaka 2001. Pamoja na vitabu vya Bwana Msa.
 
Last edited by a moderator:
Nilisoma hizi riwaya mbili Mara nyingi sana kwa kuzirudia rudia hasa hii ya HADITHI YA ALLAN QUATERMAIN NA WENZAKE hadi kitabu kikachakaa NA kurasa kunyofoka nyofoka.
 
KARIA, kuvipata hivi vitabu kwa sasa ni tabu sana, labda jaribu ku google online Amazon. Mimi niliviagiza Mombasa Kenya, mwaka 2001. Pamoja na vitabu vya Bwana Msa.
Unaweza kuniagizia na mimi? Maana natamani sana kuwa navyo hivi vitabu.
 
Unaweza kuniagizia na mimi? Maana natamani sana kuwa navyo hivi vitabu.
@KARIA, Tafuta online au wasiliana na watu wanaoishi Kenya, au unaweza kwenda pale kwenye maduka ya vitabu TPH kama bado lipo, kwa mimi hivi sasa sina nimjuae uko Mombasa.
 
Pamoja sana wakuu, ila hasara kwa vizazi vya dot com...!

Sema X-Paster, ni vema ya kua umekumbusha kwa maana ni juu yao kutwaa. Ama kwa mimi, nadhani umenifanya nifungue mitungi yangu ya kumbukumbu. Nakumbuka yule Mzulu Shupavu alisema kumwambia Rafiki yake " Sikiliza Makumazani, watu waovu hao wakija, mimi nitalinda ngazi kuu mpaka iishe kujengwa. Kweli kitakua kifo cha kiuume maana mwisho huu ulitabiriwa na mtu aliekufa zamani sana". Hii ni moja ya mistari ilionifanya nimuheshimu sana huyu mwafrika. kumbuka huyu anaesema silaha yake ni kashoka tena kamekwisha kwisha. Lakini kijishoka hicho ndicho kilichomua Agon Mkuu, Msolopa alisema kabla ya kumpasua kichwa "Na hiki chako mfanya mvua"


Mkuu kizazi cha dot com, tunaweza kumuintroduce Msolopa kwao kwa namna ambayo wanaweza kufuatilia, na wakachukuliwa kifikra hadi miaka ya 1800 Afrika Mashariki. Nadhani Hadithi ya Alan Quaterman, ilitoke Afrika Mashariki.
 
Sema X-Paster, ni vema ya kua umekumbusha kwa maana ni juu yao kutwaa. Ama kwa mimi, nadhani umenifanya nifungue mitungi yangu ya kumbukumbu. Nakumbuka yule Mzulu Shupavu alisema kumwambia Rafiki yake " Sikiliza Makumazani, watu waovu hao wakija, mimi nitalinda ngazi kuu mpaka iishe kujengwa. Kweli kitakua kifo cha kiuume maana mwisho huu ulitabiriwa na mtu aliekufa zamani sana". Hii ni moja ya mistari ilionifanya nimuheshimu sana huyu mwafrika. kumbuka huyu anaesema silaha yake ni kashoka tena kamekwisha kwisha. Lakini kijishoka hicho ndicho kilichomua Agon Mkuu, Msolopa alisema kabla ya kumpasua kichwa "Na hiki chako mfanya mvua"


Mkuu kizazi cha dot com, tunaweza kumuintroduce Msolopa kwao kwa namna ambayo wanaweza kufuatilia, na wakachukuliwa kifikra hadi miaka ya 1800 Afrika Mashariki. Nadhani Hadithi ya Alan Quaterman, ilitoke Afrika Mashariki.
Ni kweli huyasemayo, masimulizi na riwaya za zamani nyingi zilikuwa na mafunzo ya kiujasiri na aina fulani ya uzalendo... Leo hii ile tabia na mazoea ya kujisomea imekwisha kabisa... Utakuta mtu anaandika makala yake alafu vijana wanalalamika eti ni ndefu mno, na urefu wenyewe ni just 3 pages tu.

Hizi simulizi nyingi zimewekwa kwenye filamu na matokeo yake zimekuwa kama zimechakachuliwa na hazileti ule mvuto wenyewe... Ukikisoma kitu kukisahau ni vigumu sana, kwa sababu unajenga taswira zako mwenyewe na si za kutengenezewa
.
 
makumazahn watakapokuja waovu nitailinda ngazi kuu usinikataze kwani kifo hiki kimetabiriwa na watu wa zamani,ah saa yetu na tumeishi si haba lakini ningependa kuona vita vingine kama vilr vya jana.
 
Assalaam alaykum......ni kumbukumbu tu zilizonifamya mpaka nifike huku kutokea hukooo gugo,nimesoma hiyo kitabu nikiwa darasa la tatu ama la nne,leo mimejikuta napekuapekua inkosikazi,mpaka kufika huku......cjui ntakipata wapi tena nikisome..! maana naskia kilipigwa marufuku eti kinadhalilisha utu wa muafrika, cjui kama ni kweli lakini...!
 
Bougwan nitakupa hadithi nawe unisikilize alikuwapo mtu na ndugu yake na yule mtu alimpenda sana ndugu yake,yule ndugu alikuwa na mwanamke,lakini pia alikuwa na mwanamke mwingine mpaka yule mwanamke wake akajua na kwa kuwa alikuwa mwerevu na moyo wa kisasi
Akamwambia yule mtu fanya vita na ndugu yako nami nitakusaidia yule mtu akajua kuwa yule mwanamke ni muongo ila kwa kuwa alimpenda sana akakubali kufanya vita na ndugu yake.Hata ndugu yake akamtumia ujumbe"mbona wataka kuniua wakati tulipokuwa vijana tulienda kupigana vita pamoja tukagawana ng'ombe kwa ng'ombe na mwanamke kwa mwanamke?yule mtu moyo wake ukawa mzito akavikomesha vita na kuja kuishi na ndugu yake.Muda ukapita akaja tena yule mwanamke na kumwambia yule mtu kuwa tusahau yaliyopita nitakuwa mke wako mwema yule mtu akajua yule mwanamke anasema uongo lakini kwa kuwa alimpenda sana akakubali.Basi ulipofika usiku yule mwanamke akatoka na kwenda kumuua yule ndugu kisha akarudi kimya kama simba aliekwisha kula shibe yake na kumuwekea shoka lenye damu yule mtu.Asubuhi kulivyo pambazuka watu wakaja kuwakia wafalme wakakuta yule ndugu kauwawa wakaenda kumpa khabari yule mtu wakakuta anaamka huku akiwa na shoka lenye damu
.Wakavikumbuka vile vita wakasema tizama amemuua ndugu yake nae wakataka kumuua akakimbia na kumuua yule mwanamke.Lakini mauti ya yule mwanamke hayakuweza kufuta dhambi alioifanya yule mwanamke kwani mzigo wa dhambi ametwishwa yule mwanaume peke yake nae hana ndugu anakaa peke yake nae atakufa kama mnyama alie pigwa na jina lake ni tezo katikati ya watu wake kwani watu husema alimuua ndugu yake lousta kwa hila nyakati za usiku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom