Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

haya kipande kidogo hiki hapa......

TUTARUDI NA ROHO ZETU?

SURA YA TANO

Jiji la Nairobi lilimraki Joram Kiango na
Nuru kwa hewa yake yenye ubaridi ambao
ulikuwa kinyume kabisa na joto aliloliacha
Dar es Salaam. Waliuacha Uwanja wa
Kimataifa wa Kenyatta kwa teksi ambayo
iliwafikisha Hilton Hoteli.
"Mr and mrs Charles Moris", Joram
alijitambulisha katika kitabu cha wageni.
Mhudumu wa mapokezi aliwatazama kwa
muda akivutiwa na sura na maumbile yao.
Kisha aliwapatia chumba kimoja Self
Contenal kama walivyotaka. Alimwamru
kijana mmoja ambaye aliwaongoza hadi
katika chumba chao kilichokuwa ghorofa
ya nane. Baada ya kuwafikisha aliwapa
ratiba ya chakula, vinywaji na maelekezo
mengine ambayo masikioni mwa
wasikilizaji wake yalikuwa kama wimbo
baada ya kuyasikia mara kwa mara.
Walimkubalia yote na kumtupia maswali
huku mara kwa mara wakimuonyesha
meno kulijibu tabasamu lake ambalo
halikuwa na mpaka. Kisha Joram
alimfukuza kwa kumpa noti ya shilingi mia
moja ambayo ilidakwa kwa heshima zote
na kupotelea mfukoni.
"Wakati wowote, mkihitaji chochote usisite
kuniita mzee. Naitwa James", alieleza
kijana huyo wakati akitoka ndani.
"Bila shaka, James".

Mara tu walipobaki peke yao Nuru
alimtupia Joram jicho lililojaa maswali.
Alipoona Joram hatamki lolote aliamua
kuzungumza.
"Nadhani una mengi ya kunieleza Joram.
Kila nilipojaribu kukuuliza kisa cha safari
yetu tulipokuwa angani hukupenda
kunijibu".
"Sidhani kama kweli. Ulikuwa hupendi
kuzungumza mbele ya yule rubani".
"Kwanini? kwani kuna siri yoyote?".
"Bila shaka. Ulipokuwa uwanja wa ndege
Dar es Salaam ulikuwa umejivika mavazi ya
kizee tofauti na ulivyokuwa asubuhi.
Ulipofika hapa jambo la kwanza ulilofanya
ilikuwa kubadili mavazi na kuwa kama
ulivyo. Tulipofika hapa umelipa kwa fedha
za kigeni bila shaka. Umezipata wapi? na
...".
"Ala, hivi sikwambia? kati ya pesa nyingi
tulizopata katika mfuko wa marehemu
Chonde nyingi zilikuwa za kigeni", Joram
alidakia. "Nadhani nilikuonyesha Nuru".
"Ulinionyesha. Na kwanini umeamua
kupanga kwa majina ya bandia?". Nuru
aliendelea kusaili. "Na hapo utakapoombwa
kuiona hati ya usafiri utaonyesha nini?".
"Hilo lisikusumbue. Uongo sikuanza jana.
Lakini sababu kubwa iliyonishawishi
kuandika jina la bandia ni hofu ya
kusumbuliwa na waandishi wa hanari.
Unawajua walivyo Nuru. Mara nyingi
wanakuwa hawana kitu cha kuandika.
Hivyo wanapopata kijambo wanakikuza ili
kijae ukurasa. Umaarufu wangu nchini
Tanzania ni jambo ambalo waandishi wa
Nairobi wanaweza kuliondolea uvivu kwa
haki kabisa". Joram akasita na kucheka
kidogo.
"Hapana Nuru", aliendelea. "Tumekuja
kustarehe. Tunahitaji kustarehe. Nairobi ni
mwanzo tu wa starehe zetu. Toka hapa,
tutakwenda zetu London, Paris, Hong
Kong, New York na kokote ambako roho
itatuita. Lazima tufurahie maisha.
Binadamu huishi mara moja tu. Hatuna
budi kuitumia nafasi hiyo ili tukifa tuwe
tumefaidi maisha".
Joram alikuwa akiongea kwa sauti imara,
ingawa Nuru alihisi na kuamini kuwa
hakuwa mkweli. Hata hivyo kwa kadili
alivyomfahamu Joram alihisi kuwa alikuwa
na jambo. Jambo ambalo lilikuwa
halijakamilika kichwani mwake na kuona
haja la kuliongelea. La sivyo,
ingewezekanaje Joram ashambuliwe na
mtu, Nuru amuokoe kwa kumuua mtu huyo,
Waache maiti chumbani na kukodi ndege
hadi huko, wapange kwenda zao bila
sababu maalumu?, hiyo si itakuwa hadithi?
Bila shaka kuna jambo.
Nuru alilingoja kwa hamu jambo hilo.
Baada ya kuwa na Joram kwa muda mrefu,
baada ya kukinaishwa na starehe, na
baada ya risasi aliyofyatua kuondoa roho
ya mtu, roho ya Nuru ilikuwa juujuu
ikitegemea jambo. Jambo jipya. Jambo
ambalo litampa haki na wadhifa halisi kwa
kuwa na Joram Kiango kama alivyokuwa
hayati Neema Iddy. Alikuwa ameamua
kuichukua nafasi ya Neema, katika mwili na
akili ya Joram. Si kuichukua kwa kunywa
pombe na kucheza muziki. Ni kuichukua
kikazi. Na ni kazi hiyo ambayo aliisubiri
kwa hamu.
Nuru alipomtazama Joram tena alimuona
kazama katika mawazo mengi. Akamwacha
na kuingia bafuni ambako alioga kwa
utulivu. Alipotoka bafuni hakumuona
Joram. Badala yake alipata kipande cha
karatasi ambacho kilikuwa walaka, Joram
akimtaka radhi kuwa amelazimika kwenda
maktaba mara moja na kwamba angerudi
baada ya muda fulani.

Upweke ulimfanya aamue kwenda chumba
cha maongezi ambako alijipatia bia mbili
huku akitazama televisheni. Aliangalia
vipindi kadhaa vya burudani na taarifa za
habari.
Hakukuwa na mapya zaidi ya yale ambayo
yameondokea kuwa ya kawaida masikioni
na machoni mwa binaadam. Macho
yalipokinai televisheni, aligeukia chupa
iliyokuwa mbele yake. Mara akatanabai
ameketi na mtu ambaye alikuwa
akizungumza.
"Nasema, samahani naweza kuketi nawe?".
"Bila samahani?".
Mtu huyo aliketi na kuanza kumwaga
vinywaji na maongezi. Maongezi yake
yaligeuka kumtaka Nuru. Alisema mengi
akidai kwa viapo kuwa hakupata kumuona
msichana aliyeumbika kama Nuru. Kwamba
alikuwa tayari kufa ili ampate. Mara mikono
yake ikakoswa utii. Ikaanza kutambaa juu
ya mapaja ya Nuru. Ni hilo lililomuondoa
hapo na kumrudisha chumbani kwao.
Joram alikuwa hajarudi. Masaa kadhaa
tayari yalikuwa yamepita. Akitahamaki,
usiku ulikuwa umeingia alikula peke yake
chumbani humo akiogopa kwenda chumba
cha maakuli ambako kuna wanaume
ambao hawakuzoea kukubali kuwa
mwanamke angeweza kuwa pale peke
yake. Uchovu ulimfanya ajilaze kitandani.
Hakujua usingizi ulivyomchukua.
Alipoamka alijikuta mikononi mwa Joram.
"Samahani mpenzi", Joram alimnongoneza.
"Hakujishughulisha kumjibu kwa maneno.
Badala yake alilijibu busu la Joram kwa
vitendo. Kisha usingizi ulimchukua tena
alipoamka aliupeleka mkono kumkumbatia
Joram na kujikuta akigusa godoro tu.
Joram hakuwa kitandani. Alipofumbua
macho alimuona akiinama mezani akisoma
kwa makini. Akanyoosha mkono na
kuichukua saa yake ndogo ya mkononi na
kuitazama. Ilikuwa saa kumi na nusu za
alfajiri. Hakuna sababu za kumsumbua
Joram. Akajifunika na kujaribu kulala
usingizi haukuafikiana nae. Asubuhi hiyo
baada ya kuoga na kufungua kinywa Joram
alimuomba Nuru kuwa angerudi tena
maktaba.
"Leo nitamaliza shughuri zangu. Baada ya
hapo tutakuwa pamoja katika kila la heri na
shari", Joram alimweleza Nuru. Kisha
akampatia kitita cha noti akimwambia.
"Unajua tutakuwa na msafara mrefu?
natata uende huko ukiwa katika hali halisi
ya kumvutia kila mwanaume. Kwa hiyo
tafadhali leo pitapita madukani ununue kila
vazi ambalo litakustahili. Usijali bei.
Kumbuka pesa tunazo".
Nuru alizipokea na kumuuliza, "Na wewe
huhitaji nguo mpya?".
"Nahitaji. Hata hivyo mimi sina haraka
wanaume hawatazamwitazamwi kama
wanawake".
"Najua unahitaji muda wa kuwa peke yako",
Nuru alimwambia Joram. "Endelea baba,
siwezi kukuzuia".

Mara tu Nuru alipoondoka zake Joram
aliingia kazini. Alifungua begi lake na kutoa
myaraka za Chonde ambazo alikuwa
akitumia kila njia, kuzielewa akatoa kitabu
ambacho amekipata kwa taabu sana
kinachoelezea mbinu mbalimbali za
kusoma maandishi ya mafumbo.
Akaketi na kuanza kukitumia kitabu hicho
kuyasoma tena maandishi ya Chonde.
Haikuwa kazi ndogo. Ilihitaji muda mrefu
na utulivu mkubwa. Alichofanikiwa ni
kupata manu ambayo ilieleza namna ya
kukifungua kile kisanduku. Akakifungua
bila tatizo lolote.
Ndani kulikuwa na vijigorori kumi na mbili.
Joram aliinua kimoja na kukutazama kwa
makini. Katikati ya kigorori aliweza kuona
vidude ambavyo vilikuwa vikichezacheza
mfano wa saa za elekronic. Alikitazama
kigorori kwa makini akijaribu kutafuta
umuhimu wake hakuupata. Chini ya
vigorori hivyo Joram alipata ramani
ambayo alipoifungua alikuta ni ya Jiji la
Dar es Salaam. Ramani hiyo ilionyesha
majengo maarufu kama Ikulu, vituo vya
kijeshi, mabenki, na kadharika. Vitu vyote
hivyo vilikuwa vimewekewa namba za
kirumi kuanzia moja na kuendelea. Namba
ya jengo la benki kuu iliyoungua ilikuwa
imewekewa alama ya x kwa wino
mwekundu.

Mara baada ya kuona hayo Joram alipatwa
na wasiwasi mkubwa. Alihisi kuwa Chonde
kwa namna moja ama nyingine alihusika
na moto ulioteketeza benki kuu. Hofu yake
kubwa ilikuwa zile hisia kuwa alama
zilizofuata ambazo zilikuwa hazijawekwa x
kwa wino mwekundu zilikuwa katika
orodha zikisubiri. Jambo ambalo lingeleta
maafa na madhara makubwa kwa nchi na
wananchi. Zaidi, ingekuwa ushindi
mkubwa kwa maadui wa taifa. Kwa hiyo,
kwa mara nyingine, alifanya sherehe
moyoni kushangilia kifo cha Chonde.
Kisha alilifunga sanduku hilo kikamilifu
akairudia meza ambayo alikuwa ameinamia
na kuanza kujifunza tena mbinu ya
kuyasoma maandishi hayo kwa makini
zaidi.

Alikuwa hajatulia vizuri mlango
ulipofunguka ghafla na Nuru kuingia huku
macho yake yakiwa mekundu kwa
mchanganyiko wa hasira na mshangao.
Alisimama akitweta na kumtazama Joram
kwa namna ya mtu asiyejua la kusema.
"Usiniambie kuwa kuna mtu aliyekuvamia
kwa nia ya kukunajisi mchana wote huu",
Joram alimwambia Nuru kwa dhamila ya
kumfariji.
"Acha mzaha Joram. Sikutegemea kama
ungekuwa mtu wa kufanya kitendo kama
kile", alijikongoja kutamka. "Kwanini
umefanya?".
"Kufanya nini?".
"Kuiba".
"Kuiba?".
Nuru akamkazia jicho la hasira Joram.
"Usijifanye kuwa hufahamu. Dunia nzima
sasa inafahamu. Kwa kweli sikutegemea
kabisa. Imenishangaza kukuona katika
televisheni ukitangazwa kama mtu hatari
sana ambaye ameweza kuiba fedha za
kigeni ambazo nchi yake inazitegemea
kama dawa", Nuru alisita akamtazama tena
Joram kwa chuki ambayo iliendana na
mshangao. "Kwanini ufanye hivyo Joram?".
ITAENDELEA
 
Kulikua hakuna namna nyingine ya kupata pesa. Alishakataa kufanya kazi angepata wapi pesa ya starehe? Ila kwa upande mwingine wakubwa zake hawajui kama yuko mzigoni kama kawaida.

Joram anafikiria mbali mno na hayupp kianasa, matokeo ya maandishi ya Chonde serikali na watanzania watamwita shujaaa. ngoja tusubiri
 
mijicho yantoka daily hapa jukwaani kidikudi dhambi hii ya nan?
 
SURA YA TANO
Jiji la Nairobi lilimraki Joram Kiango na Nuru kwa hewa yake yenye ubaridi ambao ulikuwa kinyume kabisa na joto aliloliacha Dar es Salaam. Waliuacha Uwanja wa Kimataifa wa Kenyatta kwa teksi ambayo iliwafikisha Hilton Hoteli.
"Mr and mrs Charles Moris", Joram alijitambulisha katika kitabu cha wageni.
Mhudumu wa mapokezi aliwatazama kwa muda akivutiwa na sura na maumbile yao. Kisha aliwapatia chumba kimoja Self Contenal kama walivyotaka. Alimwamru kijana mmoja ambaye aliwaongoza hadi katika chumba chao kilichokuwa ghorofa ya nane. Baada ya kuwafikisha aliwapa ratiba ya chakula, vinywaji na maelekezo mengine ambayo masikioni mwa wasikilizaji wake yalikuwa kama wimbo baada ya kuyasikia mara kwa mara. Walimkubalia yote na kumtupia maswali huku mara kwa mara wakimuonyesha meno kulijibu tabasamu lake ambalo halikuwa na mpaka. Kisha Joram alimfukuza kwa kumpa noti ya shilingi mia moja ambayo ilidakwa kwa heshima zote na kupotelea mfukoni.
"Wakati wowote, mkihitaji chochote usisite kuniita mzee. Naitwa James", alieleza kijana huyo wakati akitoka ndani.
"Bila shaka, James".
Mara tu walipobaki peke yao Nuru alimtupia Joram jicho lililojaa maswali. Alipoona Joram hatamki lolote aliamua kuzungumza.
"Nadhani una mengi ya kunieleza Joram. Kila nilipojaribu kukuuliza kisa cha safari yetu tulipokuwa angani hukupenda kunijibu".
"Sidhani kama kweli. Ulikuwa hupendi kuzungumza mbele ya yule rubani".
"Kwanini? kwani kuna siri yoyote?".
"Bila shaka. Ulipokuwa uwanja wa ndege Dar es Salaam ulikuwa umejivika mavazi ya kizee tofauti na ulivyokuwa asubuhi. Ulipofika hapa jambo la kwanza ulilofanya ilikuwa kubadili mavazi na kuwa kama ulivyo. Tulipofika hapa umelipa kwa fedha za kigeni bila shaka. Umezipata wapi? na ...".
"Ala, hivi sikwambia? kati ya pesa nyingi tulizopata katika mfuko wa marehemu Chonde nyingi zilikuwa za kigeni", Joram alidakia. "Nadhani nilikuonyesha Nuru".
"Ulinionyesha. Na kwanini umeamua kupanga kwa majina ya bandia?". Nuru aliendelea kusaili. "Na hapo utakapoombwa kuiona hati ya usafiri utaonyesha nini?".
"Hilo lisikusumbue. Uongo sikuanza jana. Lakini sababu kubwa iliyonishawishi kuandika jina la bandia ni hofu ya kusumbuliwa na waandishi wa hanari. Unawajua walivyo Nuru. Mara nyingi wanakuwa hawana kitu cha kuandika. Hivyo wanapopata kijambo wanakikuza ili kijae ukurasa. Umaarufu wangu nchini Tanzania ni jambo ambalo waandishi wa Nairobi wanaweza kuliondolea uvivu kwa haki kabisa". Joram akasita na kucheka kidogo.
"Hapana Nuru", aliendelea. "Tumekuja kustarehe. Tunahitaji kustarehe. Nairobi ni mwanzo tu wa starehe zetu. Toka hapa, tutakwenda zetu London, Paris, Hong Kong, New York na kokote ambako roho itatuita. Lazima tufurahie maisha. Binadamu huishi mara moja tu. Hatuna budi kuitumia nafasi hiyo ili tukifa tuwe tumefaidi maisha".
Joram alikuwa akiongea kwa sauti imara, ingawa Nuru alihisi na kuamini kuwa hakuwa mkweli. Hata hivyo kwa kadili alivyomfahamu Joram alihisi kuwa alikuwa na jambo. Jambo ambalo lilikuwa halijakamilika kichwani mwake na kuona haja la kuliongelea. La sivyo, ingewezekanaje Joram ashambuliwe na mtu, Nuru amuokoe kwa kumuua mtu huyo, Waache maiti chumbani na kukodi ndege hadi huko, wapange kwenda zao bila sababu maalumu?, hiyo si itakuwa hadithi? Bila shaka kuna jambo.
Nuru alilingoja kwa hamu jambo hilo. Baada ya kuwa na Joram kwa muda mrefu, baada ya kukinaishwa na starehe, na baada ya risasi aliyofyatua kuondoa roho ya mtu, roho ya Nuru ilikuwa juujuu ikitegemea jambo. Jambo jipya. Jambo ambalo litampa haki na wadhifa halisi kwa kuwa na Joram Kiango kama alivyokuwa hayati Neema Iddy. Alikuwa ameamua kuichukua nafasi ya Neema, katika mwili na akili ya Joram. Si kuichukua kwa kunywa pombe na kucheza muziki. Ni kuichukua kikazi. Na ni kazi hiyo ambayo aliisubiri kwa hamu.
Nuru alipomtazama Joram tena alimuona kazama katika mawazo mengi. Akamwacha na kuingia bafuni ambako alioga kwa utulivu. Alipotoka bafuni hakumuona Joram. Badala yake alipata kipande cha karatasi ambacho kilikuwa walaka, Joram akimtaka radhi kuwa amelazimika kwenda maktaba mara moja na kwamba angerudi baada ya muda fulani.
Upweke ulimfanya aamue kwenda chumba cha maongezi ambako alijipatia bia mbili huku akitazama televisheni. Aliangalia vipindi kadhaa vya burudani na taarifa za habari.
Hakukuwa na mapya zaidi ya yale ambayo yameondokea kuwa ya kawaida masikioni na machoni mwa binaadam. Macho yalipokinai televisheni, aligeukia chupa iliyokuwa mbele yake. Mara akatanabai ameketi na mtu ambaye alikuwa akizungumza.
"Nasema, samahani naweza kuketi nawe?".
"Bila samahani?".
Mtu huyo aliketi na kuanza kumwaga vinywaji na maongezi. Maongezi yake yaligeuka kumtaka Nuru. Alisema mengi akidai kwa viapo kuwa hakupata kumuona msichana aliyeumbika kama Nuru. Kwamba alikuwa tayari kufa ili ampate. Mara mikono yake ikakoswa utii. Ikaanza kutambaa juu ya mapaja ya Nuru. Ni hilo lililomuondoa hapo na kumrudisha chumbani kwao.
Joram alikuwa hajarudi. Masaa kadhaa tayari yalikuwa yamepita. Akitahamaki, usiku ulikuwa umeingia alikula peke yake chumbani humo akiogopa kwenda chumba cha maakuli ambako kuna wanaume ambao hawakuzoea kukubali kuwa mwanamke angeweza kuwa pale peke yake. Uchovu ulimfanya ajilaze kitandani. Hakujua usingizi ulivyomchukua. Alipoamka alijikuta mikononi mwa Joram.
"Samahani mpenzi", Joram alimnongoneza.
"Hakujishughulisha kumjibu kwa maneno. Badala yake alilijibu busu la Joram kwa vitendo. Kisha usingizi ulimchukua tena alipoamka aliupeleka mkono kumkumbatia Joram na kujikuta akigusa godoro tu. Joram hakuwa kitandani. Alipofumbua macho alimuona akiinama mezani akisoma kwa makini. Akanyoosha mkono na kuichukua saa yake ndogo ya mkononi na kuitazama. Ilikuwa saa kumi na nusu za alfajiri. Hakuna sababu za kumsumbua Joram. Akajifunika na kujaribu kulala usingizi haukuafikiana nae. Asubuhi hiyo baada ya kuoga na kufungua kinywa Joram alimuomba Nuru kuwa angerudi tena maktaba.
"Leo nitamaliza shughuri zangu. Baada ya hapo tutakuwa pamoja katika kila la heri na shari", Joram alimweleza Nuru. Kisha akampatia kitita cha noti akimwambia. "Unajua tutakuwa na msafara mrefu? natata uende huko ukiwa katika hali halisi ya kumvutia kila mwanaume. Kwa hiyo tafadhali leo pitapita madukani ununue kila vazi ambalo litakustahili. Usijali bei. Kumbuka pesa tunazo".
Nuru alizipokea na kumuuliza, "Na wewe huhitaji nguo mpya?".
"Nahitaji. Hata hivyo mimi sina haraka wanaume hawatazamwitazamwi kama wanawake".
"Najua unahitaji muda wa kuwa peke yako", Nuru alimwambia Joram. "Endelea baba, siwezi kukuzuia".
Mara tu Nuru alipoondoka zake Joram aliingia kazini. Alifungua begi lake na kutoa myaraka za Chonde ambazo alikuwa akitumia kila njia, kuzielewa akatoa kitabu ambacho amekipata kwa taabu sana kinachoelezea mbinu mbalimbali za kusoma maandishi ya mafumbo.
Akaketi na kuanza kukitumia kitabu hicho kuyasoma tena maandishi ya Chonde. Haikuwa kazi ndogo. Ilihitaji muda mrefu na utulivu mkubwa. Alichofanikiwa ni kupata manu ambayo ilieleza namna ya kukifungua kile kisanduku. Akakifungua bila tatizo lolote.
Ndani kulikuwa na vijigorori kumi na mbili. Joram aliinua kimoja na kukutazama kwa makini. Katikati ya kigorori aliweza kuona vidude ambavyo vilikuwa vikichezacheza mfano wa saa za elekronic. Alikitazama kigorori kwa makini akijaribu kutafuta umuhimu wake hakuupata. Chini ya vigorori hivyo Joram alipata ramani ambayo alipoifungua alikuta ni ya Jiji la Dar es Salaam. Ramani hiyo ilionyesha majengo maarufu kama Ikulu, vituo vya kijeshi, mabenki, na kadharika. Vitu vyote hivyo vilikuwa vimewekewa namba za kirumi kuanzia moja na kuendelea. Namba ya jengo la benki kuu iliyoungua ilikuwa imewekewa alama ya x kwa wino mwekundu.
Mara baada ya kuona hayo Joram alipatwa na wasiwasi mkubwa. Alihisi kuwa Chonde kwa namna moja ama nyingine alihusika na moto ulioteketeza benki kuu. Hofu yake kubwa ilikuwa zile hisia kuwa alama zilizofuata ambazo zilikuwa hazijawekwa x kwa wino mwekundu zilikuwa katika orodha zikisubiri. Jambo ambalo lingeleta maafa na madhara makubwa kwa nchi na wananchi. Zaidi, ingekuwa ushindi mkubwa kwa maadui wa taifa. Kwa hiyo, kwa mara nyingine, alifanya sherehe moyoni kushangilia kifo cha Chonde.
Kisha alilifunga sanduku hilo kikamilifu akairudia meza ambayo alikuwa ameinamia na kuanza kujifunza tena mbinu ya kuyasoma maandishi hayo kwa makini zaidi.
Alikuwa hajatulia vizuri mlango ulipofunguka ghafla na Nuru kuingia huku macho yake yakiwa mekundu kwa mchanganyiko wa hasira na mshangao. Alisimama akitweta na kumtazama Joram kwa namna ya mtu asiyejua la kusema.
"Usiniambie kuwa kuna mtu aliyekuvamia kwa nia ya kukunajisi mchana wote huu", Joram alimwambia Nuru kwa dhamila ya kumfariji.
"Acha mzaha Joram. Sikutegemea kama ungekuwa mtu wa kufanya kitendo kama kile", alijikongoja kutamka. "Kwanini umefanya?".
"Kufanya nini?".
"Kuiba".
"Kuiba?".
Nuru akamkazia jicho la hasira Joram. "Usijifanye kuwa hufahamu. Dunia nzima sasa inafahamu. Kwa kweli sikutegemea kabisa. Imenishangaza kukuona katika televisheni ukitangazwa kama mtu hatari sana ambaye ameweza kuiba fedha za kigeni ambazo nchi yake inazitegemea kama dawa", Nuru alisita akamtazama tena Joram kwa chuki ambayo iliendana na mshangao. "Kwanini ufanye hivyo Joram?".
ITAENDELEA
 
ahsante mkuu kwa jipande nono ikiwezekana jingind tena kwani kidikudi mtesaji
 
ahsante mkuu kwa jipande nono ikiwezekana jingind tena kwani kidikudi mtesaji

yeye anatuletea tu toka kwa source nyingine nje ya JF. nilipogundua hilo, siku hizi simlaum kabisa.
 
yeye anatuletea tu toka kwa source nyingine nje ya JF. nilipogundua hilo, siku hizi simlaum kabisa.

Wapi huko?
Mimi nimeitafuta sana kuna sehemu nimeikuta ila kuna baadhi ya kurasa zimekataa kufunguka.
 
Mbona umeirudia kipande hiki sehemu ya tano?
 
Nuru anamng'ang'aniza joram waende wote joram anamwambia"tatizo sio kwenda Nuru tatizo je tutarudi na roho zetu?
 
ntamaholo vp mkuu source gan mnapata japo kwa pm
 
hao ni watu wawili tofauti kuna moja ya ntamaholo na nyingine ya kidikudi

aisee, inapatikana kwa blogger mmoja anajiita Nyakasagani. Blog inaitwa Mpiganaji Blog. search hayo maneno utaikuta. Na nimefuatilia nimegundua riwaya nyingi tunaletewa toka huko.

Da Pretty
 
aisee, inapatikana kwa blogger mmoja anajiita Nyakasagani. Blog inaitwa Mpiganaji Blog. search hayo maneno utaikuta. Na nimefuatilia nimegundua riwaya nyingi tunaletewa toka huko.

Da Pretty

Basi mkuu sio mbaya ukiwa unatupia kidogokidogo anapochelewa kidikudi.
 
Back
Top Bottom