Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

mkuu nimejaribu kupitia iyo blog inagoma kufunguka mkuu,ntamaholo
 
SURA YA TANO
II

"Bado siamini kama Joram amefanya hivyo", mtu mmoja alikuwa akifoka pia. Akiwa ameketi katika kundi la watu wenye hasira na mshangao kama yeye. Mabega yao yalikuwa yakimeremeta kwa nyota ambazo ziliyapamba magwanda yao kudhihirisha nyadhifa zao. "Amefanya, lakini siamini kama Joram ni mtu wa kutenda kitendo cha aibu kama hiki. Jambo la kusikitisha zaidi ni jinsi habari hizi zilivyovuja kiasi cha kuyafikia masikio ya adui zetu wa Afrika. Leo nimesikia habari hizo zikitangazwa na vyombo vya habari vya Afrika Kusini", Inspekta Kombora aliendelea kulalamika.
"Ujerumani pia imeshatangaza habari hizi Afande", aliongeza mtu mmoja aliyekuwa karibu.
"BBC vilevile imetangaza", aliongeza mwingine.
"Unaona sasa habari mbaya zinavyosafiri upesiupesi?".
"Pamoja na kwamba Joram ametuasi kimsimamo tulikuwa na haki ya kumstili kutokana na vitendo vyake vya nyuma. Sasa nadhani hatuna tunachoweza kufanya. Maji yamekwisha kumwagika. Hayazoleki. Lililopo sasa ni kutafuta uwezekano wa kumpata ili arudishe pesa zetu, hasa za kigeni".
"Hilo ndio tatizo mzee", alijibu msaidizi wake mmoja. "Taarifa za mwisho zinathibitisha kuwa hayupo kabisa hapa nchini. kuna dalili kuwa ametorokea nchi jirani kwa ndege ya kukodi".
"Lazima, lazima apatikane", Kombora alisema kwa msisitizo. "Pesa alizochukua ni nyingi sana na zinahitajika sana. Ana haki ya kuzifuja kwa starehe zake binafsi. Wasiliana na nchi jirani zote. Wasiliana na Interpol. Wataarifu kuwa tunamhitaji Joram kwa hali na mali. Madamu siri imekwisha fichuka hakuna haja ya siri tena".
Baada ya majadiliano ya muda mrefu jalada lilifunikwa na kuletwa jingine ambalo lilikuwa 'Zito zaidi' lililohusu mkasa au maafa yalikuwa yamelitokea taifa pamoja na lile tishio la maisha ya watu na majumba muhimu. Walipima juhudi zao zote wakilinganisha habari mbalimbali. Haikuwepo dalili yoyote ya kujenga matumaini.
Kisha wakavirudia vifo vya watu wawili katika chumba kimoja cha hoteli hapa Jijini. Dalili zilionyesha kuwa marehemu hao walikuwa watu tofauti ambao wasiofahamiana kabisa kwa mjibu wa watu waliomtambua Edward pamoja na wafanyakazi wa hoteli ambao hawakuwa na la kueleza juu ya Chonde.
Pekuapekua yao katika chumba hicho haikuwapatia kitu chochote zaidi ya mavazi ambayo yalionyesha kuwa yameshonewa nchi za nje. Nyalaka walizohitaji, ambazo zingeweza kuwasaidia, hawakuzipata. Ilielekea vifo hivyo vingeingia katika yale majarada ambayo kesi zake hazikuwahi kutatuliwa. Hivyo, baada ya kuzitazama tena picha za marehemu wote, zilirudishwa katika majarada na kufunguliwa upya.
Kikao kikaendelea.
ITAENDELEA
 
Dah kidi kudi story yako unaifupisha sana aisee jitahidi kuiongeza mkuu
 
upo kidikudi kitambo umepiga kimya leo kiduchu mkuu
 
Kikundi cha BOSS...umenikumbusha riwaya yake ya Dar es salaam usiku
 
Thursday, June 4, 2015

TUTARUDI NA ROHO ZETU?



SURA YA TANO


III


"Kwanini umefanya hivyo Joram?", Nuru aliendelea kufoka akimtazama Joram usoni. Lakini Joram hakuonekana kujali tuhuma hizo.


Joram, ambaye alionekana kimawazo akiwa maili kadha wakadha nje ya chumba hicho alimtazama Nuru kwa muda. Kisha ikawa kama amemkumbuka. Tabasamu dogo likamtoka, likifuatwa na sauti nzito;


"Ilikuwa lazima nifanye vile, iko siku utanielewa Nuru".


"Nitakuelewa!", Nuru alifoka, "Nitaelewa nini Joram mwanaume mwenye heshima zake na hadhi kubwa duniani anathubutu kuingia benki na kuiba pesa ambazo nchi na watu wake wanazitegemea? Siwezi kukuelewa kabisa Joram. Ambacho naweza kuelewa ni wewe kuondoka sasa hivi na kwenda zako ofisi ya Ubalozi wetu zilizoko hapa Kenya ukaombe radhi na kurudisha kila senti uliyochua, tafadhali fanya hivyo Joram".


Hilo lilisababisha kicheko kwa Joram. "Nina haki ya kula pesa za Tanzania kama wengi wao wanavyozila, Nuru. Huoni watu wenye mishahara ya shilingi elfu mbili wanavyojenga majumba ya mamilioni? Unadhani wanazipata wapi bila ya wizi? Tofauti yangu na wao ni kwamba mimi nimeiba kimachomacho, wao wameiba kisirisiri. Mwizi ni mwizi tu", akasita kidogo kabla ya kuendelea, "Acha tuzitumie Nuru. Acha tuzifaidi. Hii ni nafasi pekee katika maisha yetu ambayo hatuyasahau. Jisikie starehe...".


"Siamini kama maneno hayo yanatamkwa na Joram Kiango. Kwanini umebadilika kiasi hicho Jorma?".


Kabla Nuru hajapata jibu mlango uligongwa na kufunguka. James aliingia. Uso wake ulionyesha kuwa alikuwa na habari ambayo si nzuri sana kwao. Baada ya kubadilishana salamu za kawaida aliwataka radhi na kumchukua Joram chemba.


"Kaka, samahani. Unajua pamoja na kujiita kwako Charles Morris, ni watu wachache sana ambao walikuamini?, sura yako si ngeni kabisa hapa Kenya. Umetokea mara nyingi katika magazeti na Televishani. Wewe ni yule mpelelezi mashuhuri Joram Kiango. Sivyo kaka?".


Joram alipochelewa kumjibu, James aliendelea, "Ziko habari mbaya zilizotokea katika vyombo mbalimbali vya habari. Inasemekana umetoroka nchini kwenu ukiwa umechukua fedha nyingi za kigeni. Kwa jinsi ninavyokufahamu nashindwa kuamini kama ni kweli. Lakini hilo si muhimu sana kwa sasa. Nilichokufuata ni kukufahamisha kuwa sasa hivi wapelelezi wa hoteli hii wamekaa kikao wakijadili suala lako. Waweza kutiwa msukosuko mkubwa. Kwa hiyo nakushauri utafute mbinu yoyote ambayo itakufanya uyaokoe maisha yako. Nina ndugu anayeishi Nyeri. Anaweza kukuficha kwa muda".


Joram alicheka na kumshukuru James. "Usijali rafiki yangu. Nitajua la kufanya. Kwa sasa niache nijipumzishe kidogo huku nikifikiria la kufanya", baada ya hayo aliutia mkono wake mfukoni na kuutoa ukiwa umeshikilia noti kumi za mia mia ambazo zilidakwa na James kabla hazijamfikia. "Kajipatie bia mbili", Joram alimwambia James huku akigeuka kuingia chumbani.


"Unaona Joram? twende zetu ofisi ya Ubalozi", Nuru alimdaka juujuu kwa maneno hayo.


"Kufanya nini?", Joram aliuliza kwa upole kama kawaida yake. "Tutakwenda zetu tunakotaka. Sasa hivi uwe binti mtulivu na ufanye kama nitakavyokwambia tafadhali. Baada ya dakika chache tutakuwa zetu angani tukielekea katika mji mwingine wenye starehe kuliko huu".


"Haiwezekani Joram. Lazima ukaombe radhi na kurejesha pesa za watu", Nuru aliendelea kukanusha.


"Alikuwa ameishi na Joram kwa muda mrefu. Lakini alikuwa hajapata kumuona Joram anavyokasirika. Leo hii aliziona hasira za Joram. Aliona nuru kali na tena baridi, ikijitokeza katika sauti yake ndogo, nzito, aliposema taratibu, "Haya. Nenda zako ofisi za Ubalozi. Chukua na pesa zetu wapelekee".


Dakika mbili tatu baadae mzee mmoja wa kiume, mwenye mvi nyingi na ndevu za kutosha alionekana akitoka katika hoteli hiyo. Alikuwa kafautana na kijana wa kiume mwenye sura nzuri ambaye alikifunika kichwa chake kwa kofia pana na macho kwa miwani ya jua. Mikononi mwao walikuwa na mifuko yao.


Wafanyakazi waliwatazama wakiondoka lakini hawakukumbuka lini wageni hao waliingia na kupanga katika hoteli hii na walikuwa katika vyumba gani. Waliwasindikiza kwa macho hadi walipotoka nje na kuondoka kwa taksi.


Kati ya wafanyakazi walioshuhudia wakiondoka ni James Kamau. Hata ndoto haikumjia kuwa aliokuwa akiwasindikiza kwa macho ni Joram Kiango na Nuru waliokuwa wakiondoka zao.


ITAENDELEA
 
nusu nusu,kwenye glasi au sio wakuu,twende kazi kidikudi na ntamaholo zamu yenu baada ya doppa
 
sawa doper tumekusoma.

sio mbaya kwa wakati wenu mkipata nafasi kupitia blog hii

MPIGANAJI - http://nyakasagani.blogspot.in/?m=1
nyakasagani.blogspot.in/?m=1
 
sawa doper tumekusoma.

sio mbaya kwa wakati wenu mkipata nafasi kupitia blog hii

MPIGANAJI - http://nyakasagani.blogspot.in/?m=1
nyakasagani.blogspot.in/?m=1

nashukuru nimeipata mkuu ntamaholo ipo sura ya sita,nimeshindwa jinsi ya kushare hapa jamvini
 
TUTARUDI NA ROHO ZETU?

-SURA YA SITA

Saa chache baadae, Joram na Nuru walikuwa angani tena, katika Ndege ya Shirika la Ndege la Uingereza. Tiketi zao za kusafiria zilionyesha kuwa walikuwa wakienda zao Jijini London kupitia Cairo, nchini Misri.

Habari za "Wizi wa Joram" zikiwa sasa zimetapakaa duniani kote, zikienezwa na kila chombo cha habari, haikuwa kazi ndogo kwao kuipata fursa hii ya kuiacha nchi ya Kenya. Polisi mitaani na katika vituo vyote vya usafiri walikuwa macho wakimtazama kila mtu aliyeelekea kufanana na Joram Kiango. Passport na vitambulisho vyao vilitazamwa kwa umakini zaidi, huku maswali mengi yakiulizwa. Hata hivyo Joram na Nuru walifauru kupenya vizingiti vyote huku wakicheka kimoyoni, kwani askari hao hawakuwatazama kabisa kwa jinsi walivyojibadili kimavazi na kitabia kinyume kabisa cha matarajio ya askari hao.

Nuru alikuwa ameuficha uzuri wake kwa kuiondoa ile hali ya uvulana aliotoka nayo hotelini na kujivika nywele ambazo zilionekana nusu zingemezwa na mvi. Mavazi yake pia yalikuwa yale ambayo vijana wa kisasa wasingeweza kuyatupia macho zaidi ya mara mbili. Jambo ambalo liliwafanya wawe sawa na huyu mzee mkongwe aliyetembea kizaifu, mfuko mgongoni na mkwaju mkononi. Mzee ambaye hakuwa mwingine zaidi ya Joram Kiango. Hali zao pia zilikuwa za wakazi halisi wa Nairobi. Hati zao halali pamoja na picha zao zilifichwa vilivyo katika mifuko ya siri iliyokuwemo katika mfuko waliorithi kwa hayati Chonde.

Ndani ya ndege Joram alitulia taratibu akinywa bia aliyoletewa kwa utulivu, huku mara chache akimtupia Nuru maongezi mafupi mafupi. Baada ya muda ambao haukuwa mrefu alipitiwa na usingizi. Aliamka pindi ndege ilipokuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Cairo. Misukosuko ya abiria wanaoshuka na kuingia ilipopungua walizungumza na Nuru maongezi machache ambayo dhamila yake kubwa ilikuwa kuwafanya watazamike kama watu wa kawaida wasio na dosari machoni mwa wasafiri wengine.

Safari ilipoanza tena Joram alikiweka kiti chake katika hali ya kulala huku akimuacha Nuru akipekua kitabu chake kutafuta ukurasa alipokuwa ameishia. Ilikuwa safari ndefu, ya kuvuka bahari kubwa kama hii ya Atlantic, Joram alikusudia kuitumia vyema nafasi hii kufidia usingiza wake ambao hakuwa ameupata kiukamilifu alipokuwa Nairobi. Na ndivyo ilivyomtokea. Hakupata nafasi kuyafungua macho yake kuyatazama maji mengi yaliyotapakaa kote ardhini. Alipoamushwa na Nuru na kutazama sirishani alishangaa kuona wakizunguka juu ya Jiji la London wakisubiri kutua.-

"Imekuwa safari fupi kuliko nilivyotegemea", Joram alisema.

"Hata! ilikuwa safari ndefu sana kama ilivyo", lilikuwa jibu la Nuru.

Taratibu, ndege ikaanza kushuka na kutua bila msukosuko wowote katika uwanja mashuhuri wa Heathrow. Pilikapilika za kuchukua mizigo na kutaka kutoka mapema za abiria zikaanza. Joram na Nuru wakiwa miongoni mwa abiria walioshuka mwishoni, Walichukua mizigo yao na kupita katika ofisi za forodha na abiria wengine waliokuwa wakisubiri usafiri.

Dereva mmoja, msichana, wa shirika la usafiri la AVIS and HERTZ, aliwafuata na kuwashawishi kuingia katika gari lake. Akawapeleka mjini katika Hoteli maarufu duniani ya Willson Press ambapo walijipatia chumba maridadi. Mapokezi yalikuwa ya kistaarabu, huduma za kistaarabu, na wahudumu waliosomea ustaarabu yote yaliwafanya waone kama wako nyumbani badala ya ugenini. Jambo ambalo liliwafanya wasijali chochote juu ya malipo makubwa yanayodaiwa na hoteli hii.

Kuna mzungu mmoja, mshairi, au mpenzi tu wa taifa lake aliwahi kusema: "When a man is tired of London, he is tired of life for there is all that life can afford", kwamba binaadam anayekinaishwa na Jiji la London basi amekinaishwa na maisha kwa ujumla kwani London inacho kila kitu ambacho maisha ya binaadam yanahitaji. Joram na Nuru wasingemuona mtu huyo kuwa muongo sana. Pamoja na kwamba wote hawakuwa wageni sana kwenye jiji hilo, macho yao yaliendelea kuvutiwa na vitu mbalimbali siku yao ya pili walipoamua kuzunguka jijini.

Walikuwa wamekodi gari lililowatembeza kila mahali kutokana na matakwa yao. Kwanza walipenda kuona ule Mto maarufu unaougawa mji wa London, Thames. Waliyatazama maji yake yanayopita kwa utulivu pamoja na madaraja yake murua. Kisha walizunguka katika miji ya Kingstone, Bromley, Croyon na kwingineko wakiona mambo tofauti tofauti katika mitaa mashuhuri kama Oxford, Kingsway, Dean na Sheftebury. Usiku ulipoingia walikwenda katika jumba la Her Majesty kutazama michezo ya kuigiza.

"Kesho tutakwenda kutembea Epping Forest", Joram alimnong'oneza Nuru walipokuwa wakirudi hotelini kwao".

"Ningependa kuingia Richmond Park", Nuru alimjibu Joram.

"Nilipokuwa kozi hapa miaka minne iliyopita nilikuwa nimedhamilia kuingia lakini sijui ilikuwaje nikashindwa, safari hii nisingependa kushindwa tena".

"Huwezi kushindwa. tuna muda na pesa. Tutafanya kila kitu ambacho roho zitatutuma kufanya. Nafasi kama hii hutokea mara chache sana katika maisha yote ya binaadam".

Chumbani kwao walivua uzee na kuurudia ujana wao. Wakatazamana na kucheka kidogo. Kisha walikumbatiana na kuongozana kitandani. Muda mfupi baadaye Nuru alikuwa akikoroma taratibu, huku Joram akinyata kukiacha kitanda. Aliiendea mizigo yao na kuikagua kwa makini. Kila kitu kilikuwemo kama kilivyokuwa kimehifadhiwa. Akatoa kile kisanduku chenye vigololi na kuvitazama kwa umakini. Kisha alivirudisha na kuchukua vitabu vyake ambavyo alikuwa akivisoma au kufanya majaribio ya maandishi na mahesabu kwa umakini na utulivu. Mara kwa mara alichana karatasi hii na kujaribu ile, mara akiacha kuandika na kuanza kusoma kwa umakini, kisha akaanza tena kuandika.

"Siwezi kukusaidia mpenzi?", ilikuwa sauti ya Nuru.

Sauti hii ilimzindua Joram katika rindi- hilo la shughuli nzito iliyokuwa mbele yake. Aligeuka na kumtazama Nuru ambaye alitulia nyuma yake akiwa uchi kama alivyozaliwa. Macho yake yakiyatazama mahesabu katika karatasi za Joram.

"Samahani kwa kukuvuruga. Nimekuwa nyuma yako kwa zaidi ya saa nzima sasa. Nadhani hata hujui kuwa kumepambazuka".

Ndipo Joram alipotupa macho nje. Hakuamini. Nuru ya jua lililochomoza kitambo ilikuwa ikipenya dirishani kiukamilifu. "Samahani Nuru. Usingizi ulikata ndio nikaja mezani kupoteza muda", alisema Joram huku akianza kufunika karatasi zake.

"Kupoteza muda?", Nuru alimuuliza Joram. "Nimekutazama kwa muda mrefu sana. Hata kuna nyakati ambazo ulikuwa ukijisemea peke yako. Najua una jambo ambalo linakusumbua. Jambo ambalo umeamua kulifanya siri moyoni mwako. Hutaki kinishirikisha. Huniamini hata kidogo, sijui nifanye nini ili uniamni Joram".

"Ndio. Afanye nini ili amuamini?". Joram alijiuliza.

Msichana huyo ambaye ameacha kila kitu hata kazi na nchi yake ili awe pamoja naye.

Msichana ambaye kuwa nae imemsaidia sana Joram katika kujifariji na msiba wa Neema na aibu aliyoipata kwa kushindwa kumuua Propa. Msichana ambaye majuzi tu aliyaokoa maisha yake kwa kumuua mtu ambaye angemwangamiza bila huruma. Zaidi ni msichana mzuri wa sura na tabia. Msichana ambaye ni ndoto ya kila mwanaume.

"Sikia Nuru. Huwezi kukadilia kiasi gani nakuamini na kukutegemea. Ni vile tu sina lolote la haja ambalo naweza kukwambia kwa sasa...", Joram alimwambia akimwendea Nuru na kumkumbatia.

Nuru alijitoa mikononi mwake na kusimama kando. "Ndio huna la kuniambia. Sifai kuambiwa lolote. Kwako mimi ni mwanamke tu ninayefaa kwa mapenzi ya kimwili tu. Siwezi kuwa Neema ambaye alikuwa mwenzi wako kikazi ambaye kimwili hukuwahi kumgusa".

"Sivyo Nuru".

"Wala sifai lolote na hata katika kukusaidia katika hesabu za Fizikia unazopiga au kusoma maandishi hayo na kuyalinganisha na hayo ya kijasusi kama unavyofanya. Sifai hata kwenda maktaba kukusaidia kupekuwa walau kitabu unachohitaji".

"Nuru!", Joram alifoka kwa sauti ambayo masikioni mwa mtu asiyemfahamu ingekuwa ya kawaida tu. "Nilidhani wewe ni mtu pekee unayeweza kunielewa. Nilidhani unaifahamu tabia na msimamo wangu. Sina tabia ya kuchukua matatizo yangu na kuyabwaga mikononi mwa binaadam mwingine. Sijazowea kuchukua fumbo ambalo limenishinda kufumbua na kumuomba mtu mwingine anisaidie. Wala tabia hiyo sikuanza leo. Hivyo ninavyokwambia sina la kukwambia maana yake sina la kukwambia. Nadhani umenielewa".

"Nadhani nimekuelewa. Hata zile pesa ulizozipokonya City Drive, ambazo tunachezea sasa naamini ni fumbo lingine ambalo hukupenda kulifumbua. Sivyo mpenzi?".

Joram akatabasam, "Yaelekea mimi na wewe tutakuwa na safari ndefu kimaisha".

Wakashikana mikono na kurudi kitandani
 
Tumshukuru ntamaholo kwa sasa imekuwa nikuchungulia kwa nyakasagani ikikutwa inatupiwa huku hapa tutamfanya kidikudi naye aanze kutusubiri!
 
shumaa kazi nzuri. tumepata wawakilishi wengi kule mpiganaji Blog, kwa kuwa inatembelewa na wengi ni sababu tosha ya nyakasagani kuogeza speed ya kuandaa kitu hii.

naamini naye anafurahishwa na visit ya watu kwa blog
 
Back
Top Bottom