Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Hii riwaya noma, lete vitu kidi kudi hakika unachukua tuzo ya mtu bora 2015 kutoka kwangu.
 
Hii riwaya niliisikia kitambo kweli,nimefurahi kuikuta hapa! Big up kidi kudi
 
Kid apingwe ban kwa kuwatesa wana jf
Mtakuwa hamumtendei haki. Mnajua hii kazi ilikuwa katika hardcopy sasa huenda anaichapa hadi iwe katika muundo huu tunaoutaka. Au naye kuna website anachukua sasa hao ndio wamekwama labda.
 
Mtakuwa hamumtendei haki. Mnajua hii kazi ilikuwa katika hardcopy sasa huenda anaichapa hadi iwe katika muundo huu tunaoutaka. Au naye kuna website anachukua sasa hao ndio wamekwama labda.

Katavi angetupa hata taarifa kah.
 
Last edited by a moderator:
Hii inakuwa kama mwenye mpira wa gozi miaka ya 80 lazima aringe ndio atoke nao kwao
Kudikudi acha utoto
Usianzishe riwaya ambayo inatesa jamii
 
kidi kama ni hivi bora uwe unaiandaa, ikisha kuwa tayari unatuwekea hapa mfululizo. riwaya raha yake uisome bila kuruka kipindi
 
User Name: kidi kudi
User Title: JF Senior Expert Member
Last Activity: 16th April 2015 10:44
 
SURA YA TATU
III

Joram alifika chumbani kwake baada ya dakika
kadhaa. Akiwa mchovu, huku jicho lake moja
likiwa limevimba kutokana na pambano lake na
Chonde, alipita moja kwa moja hadi bafuni ili
ayaepuke maswali ya Nuru. Huko ndani alioga
vizuri, akaisafisha damu yote na kushevu
kikamilifu; kisha taratibu akarudi chumbani
ambako macho yake yalivutwa na hali ya vurugu
lililokuwa limetokea hapo.
Alitazama vitanda vyote na kutoiona dalili ya
kuwepo Nuru. Akaenda mezani ambako
hakushangaa kukuta ujumbe ule ukiwa juu ya
karatasi yenye damu damu. Aliusoma kwa makini,
akiuchunguza mwandiko huo ambao ulikorogwa
katika hali ya kupoteza uhalisi wake. Akatikisa
kichwa na kutokwa na tabasamu jembamba.
Usiku huo alilala huku akiwa amelisahau
tabasamu hilo katika uso wake.
ITAENDELEA
 
labda kidikudi wamemteka kama dk.ulimboka

nipo nipo mkuu. Nitumie fursa hii kuwaombeni radhi sana kwa usumbufu mnaoupata bila shaka baada ya riwaya hii kuisha ntajitahidi kuandaa riwaya nyingine mpaka mwisho ndipo niwaletee.
 
nipo nipo mkuu. Nitumie fursa hii kuwaombeni radhi sana kwa usumbufu mnaoupata bila shaka baada ya riwaya hii kuisha ntajitahidi kuandaa riwaya nyingine mpaka mwisho ndipo niwaletee.

kidi kudi hadi watu tunasahau tulipoishia. yaani raha ya riwaya kuunganisha matukio. sasa hapa wkt nafikiria Amata kumbe huku ni Joramu.

malizia bwana tuachane nayo
 
Back
Top Bottom