Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

Riwaya: Tutarudi na roho zetu?

dah! hii kitu inatutesa sana, alhamisi hii inakatika.
 
Mkuu tuletee mambo wenzio, nilivyoona ntamaholo nilijua umeshusha mambo kumbe bado bila bila

Bado kimya mkuu, wote tunamtegemea Nyakasagani na mpiganaji blog. Naona bado anaandaa. Uwe unatembelea link hii kumpa moyo na hamasa ya kutuandalia. soma habari za blog yake ili awe active kwa upabde wetu mkuu Jimena

MPIGANAJI
 
Sawa mkuu ntafanya hivyo
 
Jamani naomba sikukuu hii isitupite bure, hata aya moja tu.
 
SURA YA KUMI NA MOJA

Kioo nilionyesha majumba mbalimbali ambayo yalitokea na kupita. Kila chumba katika jumba hilo kilikuwa na vitu mbalimbali vya thamani ambavyo viliyavuta macho ya Nuru. Lakini ilionekana kuwa havikuwa vyumba ambavyo Von alivihitaji. Von aliuendesha mtambo huo harakaharaka kwa kubonyeza kidude hiki na kile kama karani anayepiga chapa. Mara kikatokea chumba ambacho ilielekea kuwa Von alikuwa akikitafuta. Kisha chumba hicho kilichoonekana kuwa kidogo, ndani yake walionekana watu wawili waliokuwa wakipigana. Mmoja hakuwa binadamu wa kawaida bali jitu. Jitu hilo lilikuwa pande la mwanaume, refu nene, jeusi lenye magumi maneno na macho ya kutisha. Lilionekana likipigana kwa maguvu zote katika hali ambayo ilionyesha kuwa lilikusudia kuua kwa mikono. Jitu hilo halikuwa na dalili yoyote ya uchovu wala maumivu. Tofauti kabisa na mtu wa pili lililokuwa likipambana nae.

Huyo alikuwa kijana wa Kizungu, mwenye dalili zote za ushujaa na ufundi wa kupigana ngumi na karate. Lakini ufundi wake ulionekana hauna dalili ya kulishinda jitu hilo kwani tayari kijana huyo alikuwa akivuja damu sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kupata majereaha makubwa ya kutisha huku akielekea kukata tamaa.

"Unaona?", Von alimwambia Nuru huku akicheka. "Mpenzi wako yuko msalabani, nilisema hapa ndio mwisho wake. Wakati wowote atakufa na kuiaga dunia. Hajawahi kutokea binadamu mwenye uwezo wa kushindana na Toto na akaweza kutoka ndani ya chumba kile akiwa hai".

Kwanza Nuru alikuwa hajaelewa. Baada ya kutuliza akili akaelewa kuwa huyo kijana wa Kizungu hakuwa mwingine zaidi ya Joram Kiango, akiwa bado katika hali ya Uzungu bandia. Moyo wa Nuru ulidunda haraka kwa hasira, akajiuliza moyoni kwanini ameketi kwenye kiti cha starehe wakati mpenzi wake Joram anateseka peke yake. Akamgeukia Von na kuangalia uwezekano wa kumuua ili atumie nafasi hiyo kwenda kumwokoa Joram. Macho ya Nuru yalikutana na macho makali ya Von yaliyokuwa katika hali ya kuyasoma mawazo wa Nuru. Bastola yake ilikuwa imetulia mkononi ikimwangalia Nuru kifuani. Nuru hakuwa na ujanja zaidi ya kuyerejesha macho yake kwenye screen na kuangalia jinsi pambano hilo lilivyokuwa likiendelea kati ya Jitu hilo na Joram Kiango. Dakika zilizokuwa zimesalia kwa ajili ya kuiteketeza miji ya Afrika hazikuhesabika tena, zilikaribia kwisha.

Kichwani Nuru alijiuliza jambo hili na lile kwa mshangao mkubwa, alijaribu kutafakari hilo ni jitu la aina gani, kubwa na jeusi kupindukia, lenye maguvu kupindukia likiwa katika hali ya kulinda mtambo huo kwa uwezo mkubwa tofauti na matarajio ya Joram, kwani jitu hilo pamoja na kuwa jeusi bado lilikuwa likipambana kwa nguvu zake zote kuutetea utawala dhalimu wa makaburu ili waiangamize Afrika.

Nuru alilazimisha kutulia akabaki akiangalia pambano hilo la kutisha, Joram aliendelea kukabiliana na jitu hilo, akibadili mbinu hizi na hizi akiyakwepa kwa ufundi baadhi ya makonde mazito yaliyorushwa na jitu hilo, lakini bado lilionekana kuwa imara katika kufanya kazi yake. Hata hivyo Joram hakukubali kushindwa kama kuku, alilazimika kurusha makonde mazito. Lakini hilo halikumsaidia Joram kuvuka kikwazo na kukifikia chumba kilichokuwa mbele yake. Chumba ambacho ndimo hasa mtambo huo ulikuwa umefungwa kwa ajili ya kuiangamiza Afrika. Kwa muda kadhaa Nuru alimwona Joram kama mtu aliyeanza kukata tamaa. Lakini Joram alifikiria kuitumia bastola yake kungewastua wahandisi waliokuwa katika chumba cha mtambo, ambao ndio hasa alikuwa akiwanyatia.

Baada ya Joram kukabiliana na jitu hilo kwa dakika kadhaa, huku Von na Nuru wakimwangalia. Joram alijaribu kutuliza akili, akawaza huku akilitazama jitu hilo kwa umakini wa hali ya juu. Wakati huo jitu hilo lilikuwa limesimama kando likimwangalia Joram kwa hasira baada ya kuwa amepigana nae kwa dakika kadhaa. Baada ya Joram kulitazama jitu hilo kwa muda, alifuta jasho na damu iliyojaa usoni, akatamka maneno fulani ambayo hayakuwafikia Von na Nuru waliokuwa wakifuatilia pambano hilo kwa makini. Von akihofu, Nuru pia akitetemeka.

Jitu hilo la kutisha lilitulia kama halikusikia kilichosemwa na Joram au alijui lugha yoyote inayosemwa katika dunia. Joram aliposogea hatua moja jitu hilo likakaa tayari kwa mapambano. Joram aliposogea hatua nyingine jitu hilo lilirusha ngumi nyingi mfululizo. Joram akarudi nyuma hatua moja na kuangua kicheko.

Kicheko cha Joram kilipokelewa na Von Iron kwa hofu, alikuwa akifuatilia mpambano huo moja kwa moja kupitia kwenye screen ya mawasiliano. Kicheko cha Joram kilimuongezea hofu akaanza kukata tamaa. "Naanza kumheshimu mpenzi wako. Tayari wamebaini kuwa hapigani na binadamu wa kawaida", Von alimwambia Nuru.

Nuru alijikuta akijiuma mdomo kwa hasira. Akajiuliza kwanini Joram muda wote huo alikuwa bado hajalibaini hilo? Kumbe Joram alikuwa hapigani na binadamu. Alikuwa akipambana na jitu lililotengenezwa kwa mikono ya binadamu katika umbo la kibinaadamu, yaani roboti. Aliwahi kusikia kuwa matajiri wengi wameshaanza tabia ya kuyaweka madude haya kama walinzi wao badala ya binadamu wa kawaida ambaye wanaamini kuwa hubadilika ama kukusalti.

"Sasa tuone atafanya nini?", Von alikuwa akisema.

Nuru aliyafuata macho ya Von kumtazama Joram ambae wakati huo alionekana akiacha kujisumbua kupambana na jitu hilo, akachungulia kwa makini, akafunua hapa na pale, huku Nuru akimwangalia kwa shauku kubwa kana kwamba hakuwa chini ya ulinzi wa Von mwenye silaha mkononi. Pilikapilika zake zilimwezesha kufunua mahali ambapo kulikuwa na waya nyingi za umeme. Joram alianza kuchomoa waya hizo moja baada ya nyingine hatimaye akaliona jitu hilo likijiweka sawa kama askari katika gwaride. Kisha likaanguka kifudifudi.

Nuru alifurahi na kushangilia moyoni. Kwa mshangao alishangaa kumwona Von nae akishangilia vilevile. "Ana akili za ziada huyu. Ameweza kubaini kuwa jitu hilo linaendeshwa kwa nguvu ya sumaku ya umeme, mahali ambapo mitambo yote inaendeshwa kupitia pale alipofungua, hakika ana uwezo mkubwa wa kufiri", Von alijisemea mwenyewe huku Nuru akiwa mwenye furaha lakini akiyahofia zaidi maisha yake mikononi mwa Von.

Nuru alishangazwa na jinsi Von alivyanza kucheka mwenyewe huku akiyarudia maneno yake. "Kijana huyu ana akili za ziada, lakini zitasaidia nini, labda nikudokeze jambo moja, jitu lile lina huruma sana, ndio maana lilikuwa likimrudisha kwa makonde ili asiende kujiua mwenyewe. Sasa mtazame. Muone mpenzi wako atakavyojiua mwenyewe... Ona anavyoangamia".

Wakati huo mapigo ya moyo wa Nuru yalibadilika, hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutazama. Alimwona Joram akiitazama saa yake na kuanza mwendo wa haraka kuelekea ndani ya chumba alichokuwa akihitaji. Mwendo wake ulikuwa wa hadhari na uhakika, macho yake yakiwa wazi, mikono yake ikiwa tayari kwa lolote ambalo lingetokea mbele yake. Mara akaufikia mlango wa mwisho, uliojitenga na lango lake. Alinyoosha mkono ili aguse kitasa. Papo hapo ardhi ilifunguka miguu yake ilibanwa na Joram akadidimia ardhini. Juhudi zake za kushika sehemu ili ajiokoe hazikuzaa matunda. Ardhi ilijifunika kama ilivyokuwa na Joram kupotea kama ndoto iliyofikia ukingoni.

"Kama nilivyosema, tayari amepotea", Von alichekelea.

Nuru alijikuta wima mbele ya Von akinyoosha mikono ili kumpiga huku akifoka, "Yuko wapi Joram? Sema yuko wapi?". Pigo la kitako cha bastola lilitua barabara kichwani mwa Nuru na kumpoteza fahamu. Fahamu zilipomrudia alijikuta kalazwa chali juu ya kochi alilokuwa amekalia awali. Alikuwa uchi kama alivyozaliwa. Mavazi yake yaliyochakaa yalikuwa yametupwa kando. Von akiwa na sigara yake mdomoni alionekana ameketi palepale alipokuwa. Macho yao yalipokutana, Von alimwangalia Nuru kwa namna ya mtu aliyekata kiu yake, Nuru liamtazama Von kisha akajitazama na kuona jinsi alivyochafuka. Nuru hakustahamili, haraka alisimama na kumwendea Von akiwa amejipanga kwa pambano jingine. Lakini hakumfikia Von. Hatua mbili alizopiga zilimfanya ashindwe kuendelea na badala yake Nuru akaanguka sakafuni. Hata hivyo mikono yake haikuwa na udhaifu kiasi hicho.

"Wewe ni mshenzi zaidi kuliko washeni wote niliopata kuwaona duniani", Nuru alifoka. "Mwanamume hayawani... Haya unasubiri nini? Niue kama ulivyomwua Joram. Niue..."

Von alitabasamu kifedhuli. Kitendo cha mapenzi ambacho kilimchukua dakika moja. Wakati Nuru akiwa hana fahamu, kilikuwa kimeupa moyo wake faraja kubwa. Hakutegemea. Mara akawa ameelewa sababu ya baba yake mzazi kupoteza maisha kwa ajili ya msichana mweusi. Hata hivyo baada ya kuonja ladha aliyohitaji sana alianza kuona athari za kumwacha kiumbe huyo aendelee kuwa hai. Mpambano aliouona kati ya Joram na roboti ilitosha kabisa kumwonyesha Von kuwa watu hawa ni wapiganaji wasiokata tamaa. Joram amekwisha, lakini huyo pamoja na kuwa mwanamke yungali hai, na anaweza kufanya lolote. Kifo cha haraka anachodai ilikuwa halali yake kabisa.

Hata hivyo Von alihitaji kumwona Nuru akifa kwa mateso zaidi. Alipenda pia kuona jinsi Nuru anavyotaabika kuona mji wao mashuhuri wa Dar es Salaam unavyoteketea kwa moto. Angependa kuona uso wa Nuru ukijaa hofu na majonzi kama alivyofanya wakati Joram alipokuwa akiadhibiwa na roboto Toto, na hasa wakati akididimia ardhini.

"Utapenda kufa sasa hivi au baadae kidogo?" Von alimwuliza Nuru bila kufanya mzaha wowote katika sauti yake. "Saa moja na dakika chache baadae kioo kilichokuwa kikionyesha mchezo wa ngumi kati ya Joram na roboti Toto kitaonyesha mchezo wa kupendeza zaidi. Jiji lenu Dar es Salaam, Tanzania na miji mbalimbali ya nchi zingine za Afrika itapata sura mpya ya kupendeza. Natamani ubaki hai kwanza ili ujionee maafa yatakavyofanyika, Je, utapenda kuona hali hiyo kabla hujafa? ili upate habari utakayomsimulia Joram mtakapokutana huko kuzimu alikotangulia".

Wakati huo nguvu na fahamu za Nuru zikaanza kumrudia, kiasi fulani aliufurahia uamzi wa Von. Akayakumbuka maneno na maelekezo fulani ya Joram kati ya mengi aliyoelekezwa, aliposema; katika mambo haya kila dakika ambayo inaweza kukuweka hai zaidi jitahidi kuinunua kwa gharama yoyote. Nuru aliafikia na Von. Wazo hilo lilimjia baada ya kubaini kuwa zilikuwa zimesalia dakika chache sana kutoka wakati huo kama walichosema ni kitu chenye uhakika na jiji la Johannesburg litakuwa mashakani, Von atakuwa akisema mengine. Nafasi kama hiyo itakapowadia Nuru asingeshindwa kuitumia.

Ili aweze kununua muda zaidi kabla ya muda wa kuibomoa Afrika haujawadia, Nuru alijifanya mnyonge zaidi. Akajiweka kiti hapo katika hali ambayo inaweza kumsumbua mwanaume yeyote aliyekamilika. Japokuwa Von alikuwa amefanya yote katika mwili wa Nuru, bado Nuru na elimu yake juu ya wanaume, alijua kuwa dakika chache baadaye roho ya mwanaume hurudiwa na hali ya tamaa ile ile tena kwa kiwango kikubwa zaidi.

"Wewe ni mshenzi..."Nuru akamchokoza tena ili atazamwe. Wakati huo akiyalegeza macho yake na kuzidi kujiweka juu ya kochi kwa mtindo fulani, hali hii ilimfanya Von apate wazimu
 
Asante sana mkuu shumaa usikawie tena basi
 
Last edited by a moderator:
SURA YA KUMI NA MOJA

II

Kitu hiki ambacho asili itabaki kuwa siri, kilichowekwa baina ya mwanaume na mwanamke, kitu ambacho hakika hakielezeki kikamilifu kwa maneno, kilitimiza wajibu wake. Nuru aliweza kuona jinsi Von na ukatili wake, pamoja na kuamini kwake kuwa ametosheka na kukinai, lakini alianza upya kutaabika. Macho yake hayakuweza tena kutulia, Mikono yake ilikuwa haikai pamoja. Alihangaika akienda hapa na pale akishika hiki na kile. Tahamaki akajikuta akiwa ameketi kochi moja na Nuru. Mkono wake mmoja ukapita na kushika paja moja nono la Nuru.

"Wewe ni mtu mbaya sana", Nuru alimwambia Von kwa sauti laini, huku akijisogeza kando kidogo.

"Sikiliza..." Von alijaribu kusema akashindwa.

Hata hivyo Nuru akajitia kumsiliza Von. Alichofanya hasa ilikuwa kuupima uwezekano wa kumzidi maarifa ili ikiwezekana aipokonye bastola yake iliyokuwa imara kwenye mkononi wake wa pili mfano wa hilizi.

Von hakuwa mgeni kwa silaha hii ya wanawake, iliyokuwa ikitumiwa na Nuru. Aliamini kuwa msichana huyu alitaka kujaribu mbinu hii ili ayaokoe maisha yake. Lakini pamoja na kubaini hali hii haikumfanya Von akate tamaa na shauku ya kutamani tena. Alihitaji tena, kwa mara ya mwisho. Nuru angefanya nini? Kama kuna kisu basi Nuru alikuwa ameshika makali na Von akiwa ameshikilia mpini. Hata hivyo Nuru alijua kuwa alikuwa akicheza mchezo wa hatari sana, tena akicheza na nyoka mwenye sumu kali. Haikuwa busara kuchezea roho kando ya shimo la mauti lililo wazi kiasi hicho. Ni hilo lililomfanya Von aendelee kushikilia bastola kama roho yake.

Wakati huo Von alikuwa tayari ameibonyeza mitambo yake ambayo alisema ingemwezesha kuiona setilaiti ikishuka taratibu kutoka angani na kuliendea anga la Tanzania ambapo ingesubiri muda uliopangwa kabla ya kuanza kuachia dhoruba za hewa ambayo ingezusha mioto ya kutosha. Katika kioo hicho waliweza kuyaona mawingu mazito mazito yakipita katika kioo. Kisha dude la ajabu lilijitokeza. Lilikuwa kubwa, jeusi lenye muundo wa ndege aina ya kunguru. Lilikuwa likisafiri kwa mwendo wa kasi sana kama vile linaifuata televisheni hiyo.

Von aliinuka ghafla huku akiwa ameshikwa na mshangao. Aliiendelea meza iliyokuwa na chombo chenye vidude vingi alivyokuwa akivimonyeza na kuvikagua kwa makini. Alivibonyeza kwa sekunde kadhaa kisha akatazama tena kwenye televisheni. Alikuwa kama ambaye hakuweza kuyaamini macho yake alipoona dude hilo likizidi kusogea. Mara jiji la Johannesburg likajitokeza katika kioo hicho. Majumba makubwa yakaanza kutoa nuru nyekundu mfano wa gari linalotoa ushara ya kuingia upande wa kulia ama kushoto. Nuru hiyo ilipokelewa na kujibiwa na dalili hiyo ya moto kutoka katika domo la chombo hicho ambacho sasa kilielekea juu ya jiji hilo kwa kasi.

Nuru aliweza kuyaelewa majumba yote hayo ambayo yalionyesha alama za moto. Ni yale ambayo yeye na Joram walikuwa wamefanikisha kutega vile vigololi ambavyo walivichukuwa kwenye mifuko ya marehemu Chonde. Nuru aliitazama saa yake. Ilikuwa ikikaribia muda uleule ambao Joram alikuwa ameviandaa vidude vile kufanya kazi. Nuru alitamani kupiga ukelele wa furaha. Tangu walipoanza kazi hiyo hakuamini kuwa walikuwa wakifanya kila kitu kwa uhakika. Wala hakumwona Joram kuwa na uhakika huo, pamoja na kufungua majitabu mengi ambayo nusura yamsababishie wazimu. Kumbe Joram alijua nini anafanya! Ndoto yake imetokea kuwa kweli.-

Wakati Nuru akifanya sherehe hiyo moyoni, Von alikuwa akitaabika kichwani. Hakuelewa kinachotokea. Dalili zilizojitokeza zilikuwa za kutisha sana, zisizokubalika. Ilionyesha kuwa wakati wowote jiji la Johannesburg lingewaka moto, badala ya Dar es Salaam, Tanzania Von aliwaza kwa hasira. Hakukuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuamru setilaiti hiyo iharibiwe na kuanguka. Si vibaya kama itaanguka na kuua watu kadhaa. Heri nusu shari kuliko kamili. Ni hilo Von alikusudia kufanya. Kuinua simu na kutoa amri kwa wahandisi.

Hilo pia hakuweza kulifanya. Alijikuta akitazamwa na bastola yake mwenyewe, aliyokuwa ameisahau kando baada ya kupagawa wakati akihangaika na mitambo. Bastola ilikuwa imara mikononi mwa Nuru, huku macho yake yasiyo na mzaha yakiitazama shari.

"Pokea haki yako, kaburu muuaji mkubwa", Nuru alinong'ona na kufyatua risasi.

Kwanza Von hakusikia maumivu. Alihisi kitu kikimtekenya kifuani na kupapasa moyo wake. Kisha alisikia moyo ukiwaka moto. Akahisi kifo. Akapiga kelele ya nguvu huku akichupa kumwendea Nuru mikono yake ikiwa wazi, tayari kumkaba koo. Lakini Nuru alimwepuka kwa urahisi sana na kumuongezea risasi nyingine ambayo ilifumua fuvu la kichwa chake. Von alidondoka chini na kulala kwa utulivu mfano wa nguruwe aliyechunwa kwa maji ya moto.

Nuru aliyatazama matokeo ya kazi yake haraka. Akaibusu bastola hiyo. Kisha akafanya haraka kujivika mavazi yake. Baada ya kujiweka sawa alikimbilia kabati la Von na kuanza kupekua haraka haraka. Haikupita dakika alipata anachotafuta. Ilikuwa ramani ya jengo hilo, ikiwa tofauti kabisa na ile waliyokuwa wakitumia awali. Aliisoma himahima, tena kwa umakini wa hali ya juu, kisha akaiweka mfukono na kuanza kuuendea ukuta ambao ulikuwa na funguo nyingi. Akazichukua na kuzihifadhi kwenye mfuko wake. Kisha bastola ikamtangulia akatoka ndani ya chumba hicho mbio kama miguu yake ilivyomruhusu akimbie
 
asante Mkuu Shumaa mmh! mambo mazito murua kabisa.
 
da!kweli kama movie la kivita vile!!!linavyonoga afu umeme ukatike du!..poa sana kiongozi shumaa!kwa uhondo mtamu!endelea kutupatia simulizi hii,,,.....✌✌✌✌
 
SURA YA KUMI NA MOJA
II
Kitu hiki ambacho asili itabaki kuwa siri, kilichowekwa baina ya mwanaume na mwanamke, kitu ambacho hakika hakielezeki kikamilifu kwa maneno, kilitimiza wajibu wake. Nuru aliweza kuona jinsi Von na ukatili wake, pamoja na kuamini kwake kuwa ametosheka na kukinai, lakini alianza upya kutaabika. Macho yake hayakuweza tena kutulia, Mikono yake ilikuwa haikai pamoja. Alihangaika akienda hapa na pale akishika hiki na kile. Tahamaki akajikuta akiwa ameketi kochi moja na Nuru. Mkono wake mmoja ukapita na kushika paja moja nono la Nuru.
"Wewe ni mtu mbaya sana", Nuru alimwambia Von kwa sauti laini, huku akijisogeza kando kidogo.
"Sikiliza..." Von alijaribu kusema akashindwa.
Hata hivyo Nuru akajitia kumsiliza Von. Alichofanya hasa ilikuwa kuupima uwezekano wa kumzidi maarifa ili ikiwezekana aipokonye bastola yake iliyokuwa imara kwenye mkononi wake wa pili mfano wa hilizi.
Von hakuwa mgeni kwa silaha hii ya wanawake, iliyokuwa ikitumiwa na Nuru. Aliamini kuwa msichana huyu alitaka kujaribu mbinu hii ili ayaokoe maisha yake. Lakini pamoja na kubaini hali hii haikumfanya Von akate tamaa na shauku ya kutamani tena. Alihitaji tena, kwa mara ya mwisho. Nuru angefanya nini? Kama kuna kisu basi Nuru alikuwa ameshika makali na Von akiwa ameshikilia mpini. Hata hivyo Nuru alijua kuwa alikuwa akicheza mchezo wa hatari sana, tena akicheza na nyoka mwenye sumu kali. Haikuwa busara kuchezea roho kando ya shimo la mauti lililo wazi kiasi hicho. Ni hilo lililomfanya Von aendelee kushikilia bastola kama roho yake.
Wakati huo Von alikuwa tayari ameibonyeza mitambo yake ambayo alisema ingemwezesha kuiona setilaiti ikishuka taratibu kutoka angani na kuliendea anga la Tanzania ambapo ingesubiri muda uliopangwa kabla ya kuanza kuachia dhoruba za hewa ambayo ingezusha mioto ya kutosha. Katika kioo hicho waliweza kuyaona mawingu mazito mazito yakipita katika kioo. Kisha dude la ajabu lilijitokeza. Lilikuwa kubwa, jeusi lenye muundo wa ndege aina ya kunguru. Lilikuwa likisafiri kwa mwendo wa kasi sana kama vile linaifuata televisheni hiyo.
Von aliinuka ghafla huku akiwa ameshikwa na mshangao. Aliiendelea meza iliyokuwa na chombo chenye vidude vingi alivyokuwa akivimonyeza na kuvikagua kwa makini. Alivibonyeza kwa sekunde kadhaa kisha akatazama tena kwenye televisheni. Alikuwa kama ambaye hakuweza kuyaamini macho yake alipoona dude hilo likizidi kusogea. Mara jiji la Johannesburg likajitokeza katika kioo hicho. Majumba makubwa yakaanza kutoa nuru nyekundu mfano wa gari linalotoa ushara ya kuingia upande wa kulia ama kushoto. Nuru hiyo ilipokelewa na kujibiwa na dalili hiyo ya moto kutoka katika domo la chombo hicho ambacho sasa kilielekea juu ya jiji hilo kwa kasi.
Nuru aliweza kuyaelewa majumba yote hayo ambayo yalionyesha alama za moto. Ni yale ambayo yeye na Joram walikuwa wamefanikisha kutega vile vigololi ambavyo walivichukuwa kwenye mifuko ya marehemu Chonde. Nuru aliitazama saa yake. Ilikuwa ikikaribia muda uleule ambao Joram alikuwa ameviandaa vidude vile kufanya kazi. Nuru alitamani kupiga ukelele wa furaha. Tangu walipoanza kazi hiyo hakuamini kuwa walikuwa wakifanya kila kitu kwa uhakika. Wala hakumwona Joram kuwa na uhakika huo, pamoja na kufungua majitabu mengi ambayo nusura yamsababishie wazimu. Kumbe Joram alijua nini anafanya! Ndoto yake imetokea kuwa kweli.
Wakati Nuru akifanya sherehe hiyo moyoni, Von alikuwa akitaabika kichwani. Hakuelewa kinachotokea. Dalili zilizojitokeza zilikuwa za kutisha sana, zisizokubalika. Ilionyesha kuwa wakati wowote jiji la Johannesburg lingewaka moto, badala ya Dar es Salaam, Tanzania Von aliwaza kwa hasira. Hakukuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuamru setilaiti hiyo iharibiwe na kuanguka. Si vibaya kama itaanguka na kuua watu kadhaa. Heri nusu shari kuliko kamili. Ni hilo Von alikusudia kufanya. Kuinua simu na kutoa amri kwa wahandisi.
Hilo pia hakuweza kulifanya. Alijikuta akitazamwa na bastola yake mwenyewe, aliyokuwa ameisahau kando baada ya kupagawa wakati akihangaika na mitambo. Bastola ilikuwa imara mikononi mwa Nuru, huku macho yake yasiyo na mzaha yakiitazama shari.
"Pokea haki yako, kaburu muuaji mkubwa", Nuru alinong'ona na kufyatua risasi.
Kwanza Von hakusikia maumivu. Alihisi kitu kikimtekenya kifuani na kupapasa moyo wake. Kisha alisikia moyo ukiwaka moto. Akahisi kifo. Akapiga kelele ya nguvu huku akichupa kumwendea Nuru mikono yake ikiwa wazi, tayari kumkaba koo. Lakini Nuru alimwepuka kwa urahisi sana na kumuongezea risasi nyingine ambayo ilifumua fuvu la kichwa chake. Von alidondoka chini na kulala kwa utulivu mfano wa nguruwe aliyechunwa kwa maji ya moto.
Nuru aliyatazama matokeo ya kazi yake haraka. Akaibusu bastola hiyo. Kisha akafanya haraka kujivika mavazi yake. Baada ya kujiweka sawa alikimbilia kabati la Von na kuanza kupekua haraka haraka. Haikupita dakika alipata anachotafuta. Ilikuwa ramani ya jengo hilo, ikiwa tofauti kabisa na ile waliyokuwa wakitumia awali. Aliisoma himahima, tena kwa umakini wa hali ya juu, kisha akaiweka mfukono na kuanza kuuendea ukuta ambao ulikuwa na funguo nyingi. Akazichukua na kuzihifadhi kwenye mfuko wake. Kisha bastola ikamtangulia akatoka ndani ya chumba hicho mbio kama miguu yake ilivyomruhusu akimbie.
 
Back
Top Bottom