TUTARUDI NA ROHO ZETU?
SURA YA KUMI
II
Baada ya Nuru kupigwa chenga ya mwili na Joram, kiasi fulani alipagawa, na hali hili iliwafanya makachero wamtilie shaka na kutoa taarifa haraka. "Bado yuko mbele yetu mzee...", haraka taarifa zilimfikia Von Iron ambaye wakati huo alikuwa ametulia ofisini kwake, mara kwa mara alisimama kuangalia saa yake ya mkononi. "...Tufanyeje mzee? Tumuue"... sauti iliendelea kusikika masikioni mwa Von.
"Nimesema mwacheni. msimuue kwanza", Von aliunguruma kupitia walkie volkie iliyokuwa mbele yake. "Mtakapopata nafasi nzuri akamatwe. Tunamtaka akiwa hai", Von aliongeza.
"Huyu msichana inaelekea kuwa anaweza kuleta madhara, mzee. Anaweza kuwa na silaha za hatari...", sauti hiyo iliendelea kushawishi.
"Unataka kuniambia kuwa wanaume wanne mlioshiba mnashindwa kumkamata malaya mmoja tu wa Kiafrika?", Von alihoji kwa sauti nzito.
"Si hivyo mzee. Lakini".
"Lakini nini?, mnachotakiwa kufanya ni kumleta hapa mbele yangu akiwa hai, ili atueleze wapi alikotorokea Joram Kiango. Mkishindwa kufanya hivyo nadhani hamtashangaa kwa lolote litakalowapateni", Von alimaliza na kuzima radio hiyo.
Taarifa za kuonekana kwa Nuru zilikuwa zimemfikia Von nusu saa iliyopita. Fununu zilizosaidia kuonekana kwa msichana huyu zilitokana na mtu aliyefia hospitali baada ya kuruka kupitia dirishani kwa maumivu ya kuchomwa kisu. Kabla ya kukata roho mtu huyo alifanikiwa kutamka kuwa alichomwa kisu hicho na msichana wa Kizungu mwenye lafidhi ya Kiafrika. Wakagundua kuwa mafanikio yote ya Joram yalitokana na hila za kujifanya Mzungu. Ndipo walipoanza upelelezi kwa njia nyingine. Na haukupita muda kabla msichana huyu aliyekuwa akipta mitaani hajatiliwa mashaka kwani haikuwa kawaida kwa wasichana wa kizungu kupita mitaani alfajiri kama hii. Ili kumbaini mtu mmoja alimsogelea ili kumsabahi. Majibu aliyotoa aliutia kasoro uzungu wake kutokana na lafidhi. Mwingine alimkaribia. Ajitia kukosea na kuugonga mkoba wake, kisha akainama mbio mbio kumsaidia kuokota, lakini akashangazwa na wepesi wa msichana huyo katika kuuokoa mboba wake. Alimtazama vizuri zaidi akaona dalili ya Uzungu bandia katika uso na mwili wake. Ndipo akaandamwa, bila ya yeye kufahamu, dakika yoyote akiwa tayari kupigwa risasi, endapo Von angeafiki...
Von hakuwa tayari kuafikiana na makachero hao waliojaa hasira na uchu wa kumwua Nuru. Hakuafiki kwa kuwa yeye pia alikuwa na uchu moyoni. Uchu wa kumpata Nuru akiwa hai. Uchu wa kuonja kile ambacho alikuwa ameambulia kushuhudia kwa macho tu. Ndio, kufa Nuru alikuwa hana budi. Lakini angeweza kufa baadaye. Hakuona sababu yoyote ya kufanya haraka.
"Bosi tayari tumemnasa... yuko mikoni mwetu". taarifa zilimfikia Von.
"Safi sana, mleteni kwangu". Von aliagiza.
Mara zikasikika purukushani katika chombo hicho cha mawasiliano. Zilifuatiwa na milio ya risasi tatu. Moyo wa Von uliodunda kwa hofu. Asingevumilia endapo msafara wa risasi hizo ungeishia katika mwili wa Nuru, kabla.
"Bosi, mchana huyu kamjeruhi mmoja wetu, turuhusu tummalize", alisema kiongozi wa makachero waliomkamata Nuru.
"Nimesema mleteni kwangu akiwa hai", Von aligiza kwa sauti ya msisitizo.
Mara chombo cha mawasiliano kikazimwa. Dakika chache baadaye mlango wa ofisi ya Von ukafunguliwa na kuruhusu msichana aliyekuwa akisukumwa kwa mitutu ya bastola nne, akaingizwa ndani ya ofisi hiyo huku akipepesuka. Alikuwa hai. Lakini jeraha la kisu katika mkono wake wa kulia, michubuko katika sehemu ya shavu, na uvimbe usoni vilidhihilisha kuwa Nuru alipigania uhai wake kwa gharama kubwa lakini hakufanikiwa.
"Ni msichana hatari sana, amemua watu wetu wawili", kiongozi wa msafara huo alieleza.
"Atajuta kuzaliwa...", lilikuwa jibu pekee la Von.
"Ni msicha jeuri mwenye kiburi, amegoma katakata kueleza habari za mwenzake".
"Ataeleza", Von alisema kwa kujiamini.
Makachero wakashangazwa na tabia hiyo mpya ya kiongozi wao Von. Alionekana kama siyo Von Iron waliyemzoea au kumjua. Von Iron wanayemjua angekuwa wa kwanza kutamka kwa ukali "Ua huyo", Na endapo kifo kisingetokea mapema Von Iron waliyemfahamu angekuwa akishuhudia ukali wa hali ya juu ukiendelea katika mwili wa msichana huyo jeuri Nuru. Msichana ambaye zlitisha hasa kwa jinsi ngozi yake bandia ilipoanza kubanduka hapa na pale kutokana na purukushani na kufanya mabaka ya ngozi yake ya asili yajitokeze kwa namna ya kuchekesha na kutisha kiasi.
"Sikilizeni", Von aliamru. "Huyu niachieni mimi. Nitajua la kumfanya. Fanyeni hivi, endeleeni kumsaka Joram Kiango, naamini atapatikana. Mkimpata huyo mtu namtaka vilevile. Hai au maiti. Sawa. Namtaka kumuona mbele yangu akiwa hai.
"Sawa, bosi", makachero waliomkamata Nuru waliafiki na kutoka ofisini kwa Von mmoja mmoja baada ya kutazamana kwa mshangao.
Walipobaki peke yao Von Iron alikiacha kiti chake na kumsogelea Nuru. Akamkazia macho yake makali. Mara akalazimika kuyainamisha macho hayo mara moja baada ya kuona kitu ambacho hakupata kukiona katika macho ya msichana yeyote. Kitu kisichoelezeka kwa ukamilifu. Kitu kama nuru ya aina yake ambacho kilifunua mapazia fulani na kuacha barabara ndefu inayoelekea kusikojulikana. Kilichomfanya Von ayaepuke macho hayo ni zile hisia za kutatanisha ambazo zilimjia ghafla zilimfanya ajihisi kama anayefuata barabara hiyo akielekea huko ambako hakujulikani, katika dunia nyingine inayotatanisha.
"Unazo habari kuwa maisha yako yamo mikononi mwangu?", Von alimuuliza Nuru. Lakini hakupata jibu, jambo ambalo lilimfanya ainue tena macho yake kumtazama Nuru.
Ile nuru ya kutisha, nuru ya ajabu aliyokuwa ameiona awali katika macho hayo haikuwemo tena. Badala yake Von alikutana na macho yale yale aliyoyategemea. Macho ambayo alitamani kuyaona. Macho ya msichana, yenye dalili zote za usichana. Mara Von akawakumbuka marehemu wazazi wake. Akakumbuka kuwa ni kitu fulani katika mambo ya msichana mweusi kama huyu ambacho kiliwafanya waondoke duniani kwa aibu na uchungu. Kitu ambacho yeye Von Iron alikuwa akikitumaini, ili akione na kukionja. Leo ilikuwa fursa ya pekee kwa Von kumtumia msichana huyu. Akaona hii ndio njia pekee kwake kumtumia msichana huyu kujua siri hiyo, kisha angemuua baadaye.
"Unatambua kuwa maisha yako yamo mikononi mwangu?", Von alirusia kuuliza swali.
Bado Nuru hakumjibu. Akaendelea kusimama pale pale alipokuwa amesimama, uchovu ukimsumbua, maumivu yakimtesa. Moyoni hasira kali ilikuwa ikichemka dhidi ya watu hawa. Hakuwa na woga wala shaka kuwa maisha yake yalikuwa ukingoni. Lakini si hilo lililomtia hasira. Hasa alisikitika kuona kuwa amekamatwa kabla ya kazi ya mwisho kukamilika. Japokuwa alikuwa na uhakika kuwa Joram Kiango alikuwa hajakamatwa, lakini aliamini kuwa ingekuwa haki yake kushirikiana na Joram bega kwa bega katika awamu ya mwisho kama walivyofanya ile ya awali. Kiasi vile vile alikuwa akijiuliza kama hakuwa amefanya makosa kwenda kinyume na matakwa ya Joram na kumfuata kwa siri badala ya kumsubiri kama alivyoagizwa. Nuru alijua wazi kuwa ni kitendo hicho ambacho kilikuwa kimemtia mashakani.
Hata hivyo Nuru hakuwa na hofu kubwa sana juu ya maisha yake. Hakuamini kuwa kifo kilikuwa karibu kiasi hicho. Mipango waliyokuwa wameiandaa yeye na Joram ilimpa matumaini kuwa itatokea fursa nzuri ambayo angepata upenyo na kutoroka hadi nchi jirani zilizoko mstari wa mbele. Imani hiyo ilijengeka katika moyo wake, wakati akifikiria hayo, mara akajikuta amezungukwa na makachero wenye silaha lakini wakiwa hawana dalili ya kuzitumia silaha hizo dhidi yake. Hata baada ya yeye kutoa bastola yake na kuua wawili kati yao, wao walifyatua risasi zao kwa dhamula ya kumtisha tu, akajua kuwa wanamtaka akiwa hai, ili wamlazimishe kutoa siri fulani. Hivyo hata alipozidiwa nguvu, baada ya kuvamiwa na kupigwa sana hakuwa na shaka sana.
Na hasa huyu mtu mnene aliyeonekana kama kiongozi wao. Huyu ambaye tamaa ya kimwili ilikuwa wazi katika macho yake. Kosa analofanya huyu la kumtamani lingeweza kabisa kusaidia kuyaokoa maisha yake na Joram Kiango. Nuru alichohitaji ni muda kidogo.
Suala hili la kupendwa na kuhitajiwa kimapenzi halikumshangaza sana Nuru. Maana alilitegemea. Kwani Joram alikuwa amemfafanulia kuhusu umuhimu wa nafasi hiyo pia walipokuwa kwenye maandalizi ya kuingia Afrika Kusini. Joram alikuwa amemwambia kwa lugha ya kishairi akisema kuwa "Katika silaha zote za mwanamke uzuri ni silaha ya kwanza", Akamweleza kinagaubaga nini cha kufanya inapobidi silaha hii kutumika. Hata walipokuwa wakifanya mapenzi kitandani kabla ya kukiharibu kile chombo chao cha kutazamia, Joram alikuwa amemnong'oneza, "Tutafanya kila kitu. Najua wanatutazama usione haya nataka ufanye utundu wake ili wapate homa ili endapo watatukamata, watamani kuyashuhudia waliyoyaona kwa vitendo. Nafasi ambayo natumaini kuwa hutashindwa kuitumia", Haya sasa nafasi hiyo imetokea... Nuru alijiambia kimoyomoyo. Kuwa nafasi ni hiyo aliyofundishwa jinsi ya kutumia silaha ya mapenzi.
Akayainua macho yake, akayalegeza kidogo, akaruhusu tabasamu dogo. "Najua kuwa nitakufa..." Nuru alimjibu Von kwa sauti ndogo ambayo kwenye masikio ya mwanaume ilitosha kuanzisha kongamano fulani baina ya mwili na damu.
Kufa hana budi lazima atakufa! Von alisema moyoni... Utakufa kifo kibaya. Lakini itakuwa baada! Kwa mdomo alisema. "Nimesema maisha yako yamo mikononi mwangu. Vitendo vyenu vilikuwa vya kinyama mno. Pamoja na kupokelewa vizuri katika nchi hii na kuahidiwa kuishi kwa amani na starehe, bado mkadiliki kufanya mambo yasiyoeleweka. Mnapita kuua watu wasiokuwa na hatia tena bila sababu yoyote. Naamini ulikuwa ushauri wa huyu mwendawazimu uliyefuatana naye. Unafahamu alikokimbilia?".
Nuru aliendelea kunyamaza, lakini baada ya sekunde kadhaa aliinua uso na kusema. "Sifahamu".
"Amekutoroka", Von alidakia, "Amekutoroka. Bila shaka wakati huu anajaribu kuitoroka nchi yetu. Hawezi kufika mbali. Bado kidogo atakamatwa na kuletwa hapa akiwa hai au maiti", Von alimaliza huku akiwa ametoa macho yake makali kwa Nuru. Macho yake yalikumbuka alichohitaji. Akazisahau hasira zake dhidi ya Joram na kumnong'oneza Nuru kwa sauti ambayo yeye ilimpa upendo. "Suala lako ni tofauti kabisa bi mdogo. Una nafasi nzuri ya kusamehewa dhambi zako iwapo tu... iwapo...
Von hakujua lipi amwambie Nuru. Hakuwa hodari wa kupambanua mambo, yaani kutongoza. Ingawa alikuwa amesoma riwaya nyingi za hadithi za mapenzi na ilikuwa vigumu sana kwake kujiweka wazi na kila alipotamani kuyaweka wazi aliyoyasoma katika hadithi hizo vitendo vilimshinda. Sababu moja kati ya nyingi zilizomfanya awe hana mke ni kutojua kuwajibika katika suala zima la kuwakabili wasichana. Wote aliowahitaji ilikuwa kama anawadhihaki huku akisubiri watasema nini. Wale ambao hakuwataka ndio walioonekana kumuhitaji na kujileta kwake kwa urahisi. Lakini leo kichwani akiwa hana hata tone moja la pombe hakuona vipi atampata Nuru. Akaduwaa akimtazama.
Nuru akauhisi unyonge huu akaamua kusubiri.
Dakika zilipotea kabla ya Von kuelewa aseme nini. Kisha alikumbuka kuwa alikuwa na akiba nzuri ya vinywaji vikali. Akafungua kabati na kutoa chupa moja ya John Walker ambayo aliimimina katika glasi. Alimkaribisha Nuru ambaye aliikataa. Akaimimina tumboni mwake. Glasi ya pili ilimchangamsha. Akarudisha vifaa hivyo kabati na kumsogelea Nuru akamgusa bega huku akinong'ona kwa sauti ambayo kichwani mwake alihisi kuwa imejaa mahaba. "Wewe ni msichana mzuri sana wa Kiafrika. Sijapata kumwona mwingine wa aina yako". Mkono wake ukagusa mahali ambapo ngozi ya bandia ya Uzungu aliyovaa Nuru ilikuwa imebandukabanduka kwa purukushani. Von akaishika ngozi hiyo na kuanza kuibandua. Gundi nyepesi iliyokuwa imetumiwa kuambatanisha ngozi hiyo ya nailoni na mwili iliacha mabaka meupe. Lakini nyuma ya mabaka hayo ulijitokeza uso mzuri, uso wa asili wa Nuru. "Wewe ni mzuri kama ulivyo. Huhitaji kabisa ngozi hii", Von alisema huku akiendelea kubandua ngozi hiyo sehemu za mapaja ya Nuru.
Sasa aliyekuwa amesimama mbele yake hakuwa tena msichana wa Kizungu. Alikuwa msichana wa Kiafrika. Msichana mzuri ambaye kila muda uzuri wake ulimpumbaza kaburu Von Iron. Kisha tamaa ikaanza kumzidi nguvu mikono yake ikapoteza utulivu na kuanza kutambaa katika mwili wa Nuru, Ulimi wake ukaanza kudai njia katika kinywa cha Nuru. Wakati huo Von alikuwa akitweta kwa nguvu huku akinong'ona maneno ambayo Nuru hakuyaelewa. Von hakutofautiana na sokwe mweupe aliyeonjeshwa asali.
Kile kitendo cha Von kilizidisha hasira katika moyo wa Nuru. Alihisi kama aliyeguswa na kinyaa mikono hiyo ilipoyafikia matiti yake na kuyachezea. Aliona kichefuchefu ulimi ulipokuwa ukibishana na meno yake ukutafuta njia ya kuingia mdomoni mwake. Ambacho Nuru alitamani kufanya ni kuitumia fursa hiyo kuachia pigo ambalo lingeondoa uhai wa Von na kisha kutafuta fursa ya kutoroka. Hata hivyo hakuthubutu kufanya hivyo, kwa kuchelea kuharibu mambo. Hakuwa akikoma kutazama saa kubwa iliyokuwa ukutani. Kila dakika iliyopita alikuwa akiisherehekea kimoyomoyo. Sasa ilikuwa imesalia kama saa moja tu kabla ya mitego waliyotega kuanza kufyatuka. Wakati huo asingekosa mwanya wa kutoroka. Kabla ya hapo Nuru alihitahitaji kuubembeleza muda kwa gharama yoyote: Isingegharimu chochote kuendelea kuliruhusu jitu hili nene liendelee kujipumbaza katika mwili wake. Mara moja mbili Nuru aliguna na kutetemeka kwa namna ya kumfanya aonekane kama aliyeshikwa na ashiki.
Kitendo hicho kiliongeza wazimu kwa Von. Mara akaanza kupambua mavazi ya Nuru. Mikono yake iliyokuwa ikitetemeka iligombana na vifingo vya mavazi hayo huku akinong'ona hili na lile.
"Sikiliza...", Nuru alieleza huku akiushika mkono wa Von na kuutoa mapajani mwake huku akiufinyafinya kwa mahaba. "Hapa ni ofisini. Mtu yeyote anaweza kuingia na kukatisha penzi letu...".
"Hii ni ofisi yangu", Von alikoroma. "Hakuna mtu anayeweza kuingia hapa bila ruhusa yangu".
"Sawa, lakini siyo vizuri".
"Tafadhali", Von alisema kisha akajilaumu kwa kutamka neno hilo. Vipi amtafadhalishe mtu mweusi? Tena mtu ambaye roho yake iko katika mikono yake. Akaupeleka mkono wake wa pili katikati ya mapaja ya Nuru tena safari hii kwa nguvu kidogo. Nuru aliyabana mapaja yake. Ndipo Von alipokumbuka kuwa haitakuwa kazi ndogo kumuingia msichana huyu kwa hiari yake. Hakuwa amezisahau zile picha za sinema ambazo huonyesha jinsi jasho linavyowatoka watu wanaojaribu kunajisi. Wala hakusahau yaliyoandikwa katika kitabu cha mapenzi alichowahi kukisoma zamani, ..."Hicho ni kitu pekee ambacho mwanamke ana mamlaka nacho mwenyewe..., kitu pekee anachoweza kujivunia... ni rasilimali yake pekee...", Hivyo Von akajikuta akilazimika kutumia njia nyingine.
"Una habari kuwa maisha yako yamo mikononi mwangu? Dakika yoyote nikiamua ufe utakuwa marehemu. Najaribu kukuokoa kwa sababu sioni kama unastahili kufa mapema kiasi hiki", Von alimweleza Nuru.
"Nitakuamini vipi kuwa hunidanganyi? Nitajuaje kuwa baada ya kumaliza shida zake hutaniua", Nuru alimwambia Von huku akimlembulia macho yake mazuri.
"Nakuhakikishia kuwa nitakulinda kwa uwezo wangu wote na utakwenda zako kwa amani na furaha tena utasindikizwa kokote utakakotaka kwenda" von alipoona Nuru hajamwamini kikamilifu kwa maneno na ahadi zake alimwacha kwa muda akaiendea kabati baada ya kulifungua alitoa bahasha kubwa. Ndani ya bahasha hiyo kulikuwa na pesa nyingi za mataifa mbalimbali. "Hizi ni pesa zenu. Ni miongoni mwa vitu vyenu mlivyonyang'anywa baada ya kufika hapa Afrika Kusini. Sasa nakukabidhi pesa hizi uwe nazo ili utakapoondoka hapa uweze kuishi nchi yoyote utakayopenda", Von alikabidhi bahasha hiyo kwa Nuru ambaye wakati huo alikuwa akichekelea moyoni, lakini Nuru akaamini kuwa mara baada ya Von kumaliza haja yake angeuawa na pesa hizo kurudi kwenye himaya ya Von.
"Sasa tunaweza kuendelea", Von alisema huku akianza upya kuuchezea mwili ya Nuru. Safari hii Nuru hakumzuia, lakini alikuwa katika mahesabu makali akiwaza na kutafakari atumie hila gani ili aendelee kumchelewesha.
Safari hii kilichomwokoa Nuru ni king'ora kilichotoa mlio wa aina ya paka aliyekabwa koo katika moja ya mitambo ya Von. Sauti hiyo ilimfanya Von aruke hadi kwenye simu na kuichukua kwa ajili ya kusikiliza kwa makini. Sauti nyembamba ilisema kwa wasiwasi.
"Bosi. Inaelekea kuwa tatizo kubwa katika mtambo maalumu. King'ora cha tahadhali kimekuwa kikilia kwa muda mrefu. Simu zote za askari wa zamu hazipokelewi".
"Imposble", Von alifoka. Unataka kunieleza kuwa maafa yanayotokea mjini yanaweza kuhamia huko nje ya mji?", Von aliuliza kwa shauku.
"Inaelekea ndivyo mzee. Kwa sababu huyu mtu anayeitwa Joram haelezeki. Anaweza kuwa yuko huko wakati huu.
"Imposble", Von alifoka tena, "Na kama kweli kaenda huko basi kajipeleka mwenyewe kwenye kifo na kaburi lake litakuwa huko, Von alisita kidogo. Kisha akasema. "Sikia. Andaa helikopita yangu na dereva. Nataka kufika huko mara moja. Nataka kushuhudia kwa macho yangu mwenyewe jinsi mtu huyo anayejiita Joram Kiango anavyosulubishwa.
UTAENDELEA 0784296253