Riwaya: Siri

jamani nimeshindwa kuweka mzigo kwa kupitia free basic nikosehem ambako siwezi kutoka nje kununua vocha ya bando kambini sehem ya kuweka by free basic haipo
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
SIRI

Episode 17
Mtunzi.Patrick CK

Saa tatu na robo za usiku mzee
Damian Mwamba aliwasili
nyumbani kwake akiwa
ameongozana na mke,watoto wake
pamoja na watu kadhaa baada ya
kuruhusiwa kutoka hospitali.Hali
yake ilikuwa nzuri.Alipofika
nyumbani kwake alikuta watu
wengi waliokuja kuwapa pole
familia yake wakiwa ni ndugu
marafiki na majirani ambao
hawakuweza kufika hospitali
kumjulia hali.Walikuwepo pia
baadhi ya viongozi wa chama na
serikali .Aliwashukuru wote
waliofika kumpa pole
akawasilimulia kilichotokea pale
hotelini .Wakati akiendelea
kusimulia tukio lile lilivyotokea
simu yake ikaita.Akaitoa mfukoni
na kuangalia mpigaji,akaguna na
kuikata akaendelea na
maongezi.Alitumia zaidi ya saa
moja kuzungumza na watu wale
waliokuja kumfariji halafu
akawaomba wamuache apumzike
kwani alihisi kichwa
kinamuuma.Baada ya ugeni ule
kuondoka Damian Mwamba
akamuita mkewe na kumtaarifu
kwamba anataka kutoka kidogo
kuna sehemu muhimu anakwenda
na angerejea baada ya muda
mfupi.Mkewe alionyesha wasi wasi
lakini Damian akamuhakikishia
kwamba yuko salama na anaweza
kuendelea na shughuli zake kama
kawaida.
“Usihofu kitu mke wangu.Mimi
niko salama kabisa na
ndiyopmaana hata madaktari
wameamua kunipa ruhusa ya
kutoka hospitali.Kumbuka bado
nina kazi ngumu inanikabili kwa
hiyo kuna wajumbe ambao nahitaji
kuonana nao usiku huu.Hakuna
kulala hadi pale nitakapopewa
ufunguo wa kuingia ikulu” Akasema
Mr Mwamba huku akimbusu
mkewe na kutoka nje akamwita
dereva wake wakaingia garini na
kuondoka
“Huyu Sintah nilikwisha
muonya kuhusu kunipigia simu
usiku na hasa nikiwa
nyumbani,mbona anataka kuniletea
matatizo huyu mtoto? Mzee
mwamba akawazaakiwa garini
akaichukua simu yake na kupiga
“Sintah,hujambo? Akasema
Mwamba huku sura yake ikiwa
imekunja ndita
“Mimi sijambo mpenzi
shikamoo.” Ikasema sauti nyororo
ya msichana toka upande wa pili
wa simu.
“Marahaba hujambo?
Unaendeleaje? Akasema Mr
mwamba
“Nimepoa baada ya kuisikia
sauti yako darling.Nilisikia tukio
lililokutokea nikashindwa hata kula
siku nzima ya leo,niliogopa
sana.Unaendeleaje baby
wangu?akauliza Sintah.Sauti ile
laini ilimfanya Damiani Mwamba
kutabasamu .
“Ni kweli Sintah nilipata
matatizo kama ulivyosikia lakini
usiwe na wasi wasi niko
salama.Nilikuwa hospitali kwa siku
nzima na kwa sasa nimekwisha
ruhusiwa”
“Nashukuru darling kama
unaendelea vizuri.Nilikuwa na wasi
wasi mwingi ndiyo maana
nikaamua nikupigie simu japokuwa
umekwisha nikataza kufanya
hivyo.Lengo lilikuwa ni kujua hali
yako ilinafsi yangu itulie” Sintah
akasema kwa sauti laini ya
kubembeleza
“Uliniudhi sana Sintah kwa
kwenda kinyume na makubaliano
yetu.Nimekwisha kuambia kwamba
hata itokee nini don’t call me when
I’m home” Akasema Mr Mwamba
kwa sauti ya juu kidogo.
“Naomba unisamehe mpenzi
wangu,sintarudia tena.Nilifanya
vile kwa sababu ya mstuko
nilioupata.Nisingeweza kulala bila
kuisikia sauti yako ikinihakikishia
kwamba uko salama.Kwa sasa uko
wapi darling?
“Niko garini kuna mahala
ninaelekea.Kesho nitakuwa na
safari ya kuelekea Dodoma na
nitapita hapo hapo Morogoro ila
sintapata nafasi ya kuonana nawe
labda wakati wa kurudi” Akasema
Mr mwamba.
“Jamani Darling usifanye
hivyo.Nakuomba ulale hapa
Morogoro kwa kesho tu halafu
kesho kutwa uendelee na safari
yako.Ninakuhitaji sana
baby.Nakuhitaji sana siku ya kesho
darling nashindwa hata kusoma
nikikuwaza wewe.Halafu darling
nina jambo nataka nikueleze,sitaki
uniulize ni jambo gani nitakwambia
iwapo utakubali kulala Morogoro
kesho” Akasema Sintah.Damian
mwamba akatafakari kidogo halafu
akasema
“Haya mama unajua kucheza
na akili yangu,nitalala kesho
Morogoro kwa sababu
uking’ang’ania jambo hutaki
kuambiwa hapana.” Akasema
Damian huku akicheka.
“Thank you darling,thank you
so much.You are the best !!
akasema Sintah huku akimwagia
Damian mabusu katika simu
“Nitafikia hoteli mpya ya City 5
star.Mimi ni mtu mkubwa sana
katika nchi hii kwa hiyo sitaki
ijulikane kama nina uhusiano wa
kimapenzi na wasichana wadogo
kama wewe halafu tena ni
mwanafunzi ndio maana siku zote
nimekuwa nikijitahidi sana
kujificha ili uhusiano wetu
usijulikane hasa kwa familia
yangu.Nitakutaarifu kesho ni
chumba namba ngapi nitakuwepo
ili uje uniliwaze mtoto mzuri.Kila
nikiwa nawe najihisi ni kijana tena”
Akasema Damian Mwamba huku
akicheka kwa nguvu na kumfanya
dereva wake acheke pia kicheko
cha chini chini.
“Kwa jinsi unavyonipa raha
siamini kama wewe ni mzee
mwenye umri kama wako.Mimi
nahisi ni hizo mvi ndizo
zinakufanya uonekane mzee lakinio
kiuhalisia wewe bado kijana
mbichi” Akasema Sintah na
kumfanya Damian kucheka kicheko
kikubwa sana.
“Umeanza vituko vyako we
mtoto.Shuleni kwako hakutakuwa
na tatizo lolote? Sitaki mtu yeyote
afahamu kama umetoka shuleni
wanaweza wakaanza kukufuatilia”
“Shuleni kwangu hakuna tatizo
lolote darling.Walimu wote
nimekwisha waweka
mikononi.Hapa ninaishi kama
mtoto wa rais.Lolote nitakaloamua
kufanya ninafanya tu bila tatizo
lolote” Akasema Sintah na kuifanya
sura ya Damian ijenge tabasamu
pana sana.
“Sawa mtoto mzuri lala salama
tutakuwa wote hiyo kesho”
“Ahsante darling I love you!
Akasema Sintah na kumfanya
Damian mwamba atabasamu
akamtazama dereva wake na
kumwambia
“Sam,unapokuwa na watoto
kama hawa basi inakuwa ni
burudani kama nini ,kuna mambo
wanakufanyia ambayo yanakufanya
unahisi ni kama umerudia ujana
wako.Vijana mnafaidi sana
hahahahaaa” akasema Mr Mwamba
na kuangua kicheko kikubwa,Sam
dereva wake naye akaangua
kicheko.
*******************
Inakaribia saa tatu za usiku
bado Donald Nkebo alikuwa
amejifungia katika ofisi yake ndogo
iliyo nyumbani kwake.Siku hii
alikuwa na kazi nyingi na sura yake
ilionyesha uchovu.Akiwa bado
ameinamia mafaili yake mara simu
yake ya mkononi ikaita ,haraka
haraka akaichukua na kuangalia
mpigaji alikuwa ni Paul akaipokea
“Paul nipe habari” Akasema
Donald
“Habari nzuri Mr Donald.Nina
taarifa mbili.Ya kwanza ambayo
nitakutumia ni kutoka kwa Edger
ambaye anafikiria kujiunga na
chama cha Democratic.Halafu ya
pili ambayo nina imani utaifurahia
ni kwamba tayari Mr Mwamba
tumemtia mtegoni”
“Mbona unanifanya
nitabasamu kabla hata sijajua
umepata kitu gani? Akauliza Mr
nkebo
“Tulia nisikilize
Donald,mambo yanazidi kukolea”
akasema Paul
“Nieleze tafadhali” akasema
Donald
“Jambo la
kwanza,unakumbuka tulifanikiwa
kuweka kitu katika simu ya Damian
mwamba na tumeweza kufuatilia
mazungumzo yake ya simu.Muda
mfupi uliopita Damian alikuwa
anazungumza na binti anayeitwa
Sintah.Binti huyu kwa mujibu wa
maongezi yao ni mwanafunzi wa
sekondari na ana mahusiano ya
kimapenzi na Mr mwamba.Kesho
Mwamba ana safari ya kuelekea
Dodoma lakini kwa ombi maalum la
binti huyo Damian atalala
Morogoro ili aweze kuutumia usiku
akiwa na huyo msichana.Donald
huoni kwamba mpaka hapo tayari
Mr Mwamba tumekwisha mmaliza
kisiasa? Akasema Paul huku
Damian Nkebo akiachia tabasamu
pana na kucheka kicheko kidogo
kama kawaida yake.
“Kazi nzuri sana Paul.Nipe
mipango yako unataka kufanya
nini? Akauliza Damian
“Nimechunguza na kugundua
kwamba Sintah Leonard ni mkaazi
wa Morogoro na hata wazazi wake
Bwana na Bi Apolo Leonard
wanaishi maeneo ya Forest
Morogoro.Kwa muda huu mfupi
nimegundua kwamba Sintah
anasoma shule ya wasichana ya
Forest girls high school na ni
mwanafunzi wa kidato cha sita
shuleni hapo.Kesho Damian na
Sintah watakutana hotelini City
5.Baada ya kupata uhakika kwamba
Mr mwamba na Sintah wako ndani
ya hoteli hiyo,tutawachukua wazazi
wake ambao ni wachungaji wa
kanisa ,tutaambatana pia na
wandishi wa habari pamoja na
askari polisi halafu tutafanya
fumanizi kubwa.Magazeti yote siku
itakayofuata yataandika habari hii
kubwa ya Mwamba kufumaniwa na
mwanafunzi wa sekondari na
wakati huo huo atashtakiwa kwa
kufanya mapenzi na
mwanafunzi.Donald mpaka hapo
Damian atakuwa amefikia mwisho
wa kufanya siasa”akasema Paul.
Donald Nkebo akacheka
kicheko kikubwa sana.halafu
akasema
“Good Job Paul.Finaly Damian
is going down.Huyu ndiye hasa
ambaye amekuwa akimsumbua rais
Dr Evans.Kumuangusha huyu ni
sawa na kuuangusha mbuyu
mkubwa.Rais atafurahi sana na
hatajuta kwa kuwalipa fedha nyingi
kwa kazi hii kubwa
mnayoifanya.Hii ni salamu kwa
Damian na wenzake kwamba nchi
hii ina wenyewe na wenyewe ndio
sisi.Go on with your plan Paul.Vipi
kuhusu huyu Edger,ulisema
anataka kuhamia chama gani?
“Nitakutumia mazungumzo
yake na Stanley utayasikiliza na
utamjulisha rais” akasema Paul
HAIFA – ISRAEL

Mlio kutoka katika kompyuta
ulimstua Dick ambaye alikuwa
amepitiwa na usingizi akaamka
haraka na kuitazama kompyuta
yake.Mlio ule ulikuwa ni wa kumpa
taarifa kwamba kamera alizofunga
katika chumba cha Edger zilinasa
sura ya mtu.Ndani ya chumba cha
Edger kulikuwa na watu
watatu,mwanamke mmoja
mwafrika aliyejifunika ushungi
kichwani na wanaume mwanaume
walioonekana wenye asili ya
kiarabu walikuwa wamesimama
mlangoni.Yule mwanamke
aliyeonekana mtu wa makamo
alikwenda katika kitanda alicholala
Edger na kuuweka mkonoi wake
wa kulia katika paji la uso wa Edger
ambaye alikuwa amelalausingizi
mzito kufuatia dawa ile ya usingizi
aliyoipulizia Dick alipokwenda
kufunga kamera ndani ya chumba
kile.
“Yule mwanamke ni
nani?akajiuliza Dick akiendelea
kumfuatilia y ule mwanamke mle
ndani ya chumba cha
Edger.Hakuchukua muda mrefu
mwanamke yule akaondoka lakini
aliacha kitu kama bahasha ndogo
pembeni ya mto wa
Edger.Wanaume wale wawili
ambao walionekana kama walinzi
wake wakamfungulia mlango na
kutoka wakaondoka huku
mwanamke yule akiwa anafuta
machozi
“Who is that woman?Kwa nini
aje muda huu usiku? Akaendelea
kujiuliza Dick
“Mwanamke yule ni mpenzi
wake?akaendelea kujiuliza Dick
“Kama ni mpenzi wake mbona
anaonekana ni mtu mzima kuliko
Edger?Na kama ni mpenzi wake
kwa nini aje usiku?Kuna kitu nahisi
cha tofauti hapa” akawaza Dick
“Ninatakiwa niipate ile
bahasha aliyoiacha pembeni ya
Edger nijue kuna nini ndani
yake,yawezekana ikawa imepakwa
sumu” akawaza Dick na kufungua
mlango wake akachungulia nje
kulikuwa kimya kabisa akanyata
hadi katika chumba cha Edger
akafungua mlango taratibu na
kuingia ndani akanyata hadi
katikakitanda cha Edger
akaichukua bahasha ile aliyoiacha
yule mwanamke akaifungua na
ndani akakuta kunba kadi ndogo
iliyoandikwa
“Please call” halafu
zikaandikwa namba ambazo
alitakiwa apige.Dick akatoka mle
chumbani mwa Edger akiwa na ile
bahasha akaenda chumbani kwake
na kujilaza kitandani.Sekunde
chache alipotoka chumbani kwa
Edger akasikia vishindo vya mtu
akipita alikuwa ni muuguzi
aliyeingia katika chumba cha Edger
kuangalia maendeleo yake.Dick
akajifunika vizuri kwani alijua
muuguzi yule baada kutoka kwa
Edger angeingia chumbani
kwake.Kama alivyokuwa
ametegemea baada ya kutoka
chumbani kwa Edger muuguzi yule
akaingia chumbani kwa Dick
akamuamsha na kutaka kujua
maendeleo yake.Dick akamjulisha
kuwa anaendelea vyema na
muuguzi yule akaondoka.Baada ya
muuguzi kuondoka Dick
akaziandika zile namba katika
kitabu chake halafu akafungua
mlango akachungulia nje na
kwenda chumbani kwa Edger
ambayo bado aliendelea
kulala,akairejesha ile bahasha
pembeni ya mto akatoka akarejea
chumbani kwake na kurejea
kutazama kumbu kumbu za
kamera.Alimtazama kwa makini
sana yule mwanamke
“Kuna kitu kinanipa mashaka
sana kuhusu yule
mwanamke.Kwanza amekuja usiku
na baada ya kumuona Edger
alijawa na simanzi usoni
akanyoosha mkono na kumshika
paji la uso.Kama angekuwa
amekuja kwa nia mbaya kwa nini
akatokw ana machozi alipomuona
Edger?Ni nani huyu mwanamke?
Sitakiwi kupoteza muda napaswa
haraka sana kufahamu mwanamke
huyu ni nani na nini lengo la kuja
hapa” akawaza Dick na kuanza
kucheza na kompyuta yake
akaipata picha nzuri ya yule mama
na kumtumia Yair akamtaka
amsaidie kupata taarifa za yule
mwanamke.
Baada ya dakika tano Yair
ambaye ni jasusi wa shirika la
ujasusi la Israel Mosad akamtumia
ujumbe Edger
“Dick mwanamke huyu pichani
umemuona wapi?
Dick akatafakari akaamua
kumueleza ukweli
“Amekuja hapa hospitali usiku
huu kumtazama Edger.Umekwisha
mfahamu ni nani?akauliza Dick
“Una hakika kweli amefika
hapo hospitali?akauliza Yair
“Ndiyo amekuja hapa hospitali
si muda mrefu sana”
“bado yuko hapo hospitali?Yair
akauliza
“Hapana amekwisha ondoka”
akajibu Dick
“Ninakuja hapo hospitali sasa
hivi” akasema Yair na kumshangaza
Dick
“Mbona Yair amestuka baada
ya kuiona picha ya huyu
mwanamke?Anamfahamu?akajiuliz
a Dick
“Lazima kuna kitu kuhusiana
na huyu mwanamke kwani Yair
asingeweza kupata mstuko baada
ya kuiona picha ya yule mama
kama hakuna jambo.Ngoja
nimsubiri atakapokuja atanijulisha”
akawaza Dick
Zilipita dakika kumi Yair
akawasili pale hospitali na moja
kwa moja akaelekea chumbani kwa
Dick
“Dick! Akasema Yair
“Yair karibu sana.Nimefurahi
kukuona tena”
“Vipi maendeleo yako
hapa?akaulkiza Yair
“Ninaendelea vyema kila kitu
kinakwenda vyema”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Nimerejea kutoka safari
yangu na nikiwa na nilipanga nije
nikutembelee kesho lakini picha ile
uliyonitumia imenistua na
kunilazimu nije kukuona haraka
sana.Nieleze kuhusu huyu
mwanamke namna ulivyoweza
kumnasa” akasema Yair.Dick
akamueleza kila kitu alichokifanya
akamuonyesha kila kitu kuhusiana
na yule mama aliyekuja chumbani
mwa Edger
“Yair mwanamke huyu ni
nani?Mbona umeonyesha kustuka
sana baada ya kupata taarifa
zake?Tafadhali nieleze ukweli
unaoufahamu kuhusu huyu
mwanamke” akasema Dick.Yair
akafikiri kwa muda na kusema
“Huyu mwanamke anaitwa
Habiba Jawad.Ni raia wa Kenya
lakini taarifa zinasema kwamba
anatokea chini Somalia.Habiba
aliwahi kuolewa na mtu anaitwa
Nasser Jawad aliyekuwa
mfanyabiashara mkubwa nchini
Kenya ambaye alikuwa anatajwa
kufadhili makundi mbali mbali ya
kigaidi hasa wanamgambo wa
kikundi cha Alshabaab.Nasser
alifariki dunia kwa ugonjwa wa
saratani na baada ya kufariki mke
wake Habiba ndiye aliyemamia
biashara za mumewe na alipata
mwanaume mwingine anaitwa
Abdul ambaye naye ni mfanya
biashara mkubwa anamiliki visima
vya mafuta katika nchi mbali mbali
za kiarabu.Huyu Abdul kwa muda
mrefu alikuwa anatafutwa na
serikali ya Israel kwa kufadhili
makundi ambayo yamekuwa
yakiingia,kufanya vurugu na kuua
wayahudi.Baba yake Abdul ambaye
ni mpalestina aliuawa na vikosi vya
Israel na toka hapo Abdul alikuwa
na visasi na wayahudi na amekuwa
akifadhili vikundi vinavyoendesha
mapambano dhidi ya serikali ya
Israel na kuua wayahudi.Abdul
alipatikana na kuuawa na vikosi
vya Israel na baada ya kuuawa mke
wake Habiba ndiye aliyemiliki
utajiri wote wa mumewe.Baada ya
Abdul kufariki matukio ya
wayahudi kuuawa yalipungua
kwani Abdul ndiye aliyekuwa
mfadhili mkuu wa vikundi
vile.Tuliendelea kumchunguza
Habiba lakini hatukupata ushahidi
wa kumuhusisha na kufadhili
vikundi vya ugaidi.Baadae aliibuka
mtu mmoja wa karibu sana na
Abdul anaitwa Sayid Omar huyu
ndiye anayetajwa kufadhili kikundi
cha IS kifedha na kuwawezesha
kufanikisha kupanua mtandao wao
sehemu mbali mbali duniani.Baada
ya kumchunguza Sayid Omar
tumegundua utajiri alionao
umetokana na Habiba.Tunahisi
kwamba yawezekana Habiba
anamtumia Sayid katika kufadhili
kikundi cha IS.Habiba ni mtu
muhimu sana na sijui amewezaje
kuingia hapa Israel bila ya vyombo
vyetu kujua ndiyo maana
uliponiambia kwamba amekuja
hapa hospitali nilistuka sana”
akanyamaza akamtazama Dick
aliyekuwa makini akisikiliza
“Swali tunalopaswa kujiuliza
hapa ni Habiba na Edger Kaka wana
mahusiano gani hadi aje
kumtembelea?Je
wanafahamiana?akauliza Dick
“Hilo ndilo swali kubwa
tunalopaswa kujiuliza,Habiba
amekuja kufanya nini hapa?Ana
mahusiano gani na Edger?
“Yair nina wazo.Kwa nini
nisijifanye mimi ndiye Edger na
tupige zile namba alizoziacha
Habiba?
“Ni vipi kama anaifahamu sauti
ya Edger?akauliza Yair
“Kwa sasa Edger anaumwa
hivyo lazima sauti yake
ibadilike.Tujaribu tuone tunaweza
kugundua jambo” akasema Dick.
“Hilo naona ni wazo zuri.Nipe
dakika kumi nitarejea” akasema
Yair na kutoka haraka.
“Edger ana mahusiano gani na
hawa watu wenye mahusiano na
vikundi vya kigaidi?Amefahamiana
vipi na Habiba?akawaza Dick na
kurudia tena kuitazama ile video ya
Habiba akiwa chumbani kwa
Edger.Akaitazama kwa makini sana
“Hisia alizozionyesha Habiba
mara tu alipomuona Edger zinanipa
maswali mengi sana.Je
wanafahamiana?Kama
wanafahamiana Edger anafahamu
kama Habiba anahusishwa na
kufadhili kikundi cha IS? Dick
alijiuliza maswali mengi kuhusiana
na Habiba
Baada ya dakika kumi na mbili
Yair akarejea.Akatoa simu mfukoni
“Hii simu imeunganishwa na
ofisi yetu hivyo utakapozungumza
naye itasaidia kujua mahala alipo”
akasema Yair.Dick akaandika zile
namba katika simu ile aliyopewa na
Dick na kupiga simu ikaita
“hallo” ikasema sauti ya
mwanamke upande wa pili.Edger
akakaa kimya
“Hallo” ikaita tena sauti ile
upande wa pili.Yair akamfanyia
ishara azungumze
“hallo” akasema Dick na
mwanamke yule upande wa pili
akashusha pumzi
“Wewe ni nani?akauliza kwa
kiingereza
“Ed..Edger kaka” akajibu Dick
“Edger?akauliza yule
mwanamke akionekana kustuka
“Wewe ni nani?Nimekuta
ujumbe hapa pembeni ukinielekeza
nikupigie? akajibu Dick kwa
wasiwasi
“Edger mwanangu” akasema
yule mwanamama na Dick akastuka
sana
“Edger..!! akaita yule
mwanamke
“Mama?! Akauliza Edger kwa
mshangao na simu ikakatwa.
“Amekata simu.Yair siamini
nilichokisikia masikioni
mwangu.Habiba amemuita Edger
mwanae!
“Piga tena! Akasema Yair.Dick
akapiga tena lakini simu
haikupatikana ilikwisha zimwa.
“Hapatikani amekwisha zima
simu” akasema Dick
“Yair hiki kilichotokea
kimenistua sana.Habiba amemuita
Edger
mwanae.Wanafahamiana?akauliza
Dick.
“Hilo ndilo swali ambalo
tunapaswa kujiuliza kuhusu wawili
hawa kama wanafahamiana na
iweje Habiba amuite Edger
mwanae?Kabla ya hayo yote ngoja
tujue kama wamefanikiwa kujua
mahala aliko Habiba” akasema Yair
na kupiga simu ofisini kwao
akazungumza nao kwa muda halafu
akakata simu na kumtazama Dick
“Wameshindwa kupata mahala
alipo Habiba.Muda ulikuwa mdogo
sana uliozungumza naye.Ulipaswa
kumuweka kwenye simu kwa muda
mrefu ili waweze kufuatilia kujua
mahala alipo”
“Kuna uwezekano Habiba
aligundua mimi si Edger akauliza
“Sina hakika lakini kitendo cha
kukata simu na kuizima kabisa
kinatia shaka kidogo.Hata hivyo
tumepata kitu kikubwa
sana.Kitendo cha kumuita Edger
mwanae ni jambo kubwa sana
kwetu.Inaonyesha wazi kuna
mahusiano kati yao kwani Habiba
asingeweza kuja kumtazama Edger
kama hawafahamiani.Kitendo cha
Edger kuwa na mahusiano na watu
wenye kushukiwa kufadhili ugaidi
kinamfanya awe ni mtu wetu wa
muhimu sana.Kuna mambo mengi
ya siri kuhusu huyu jamaa na ni
jukumu letu kumchunguza kwa
undani” akasema Yair
“Nakubaliana nawe Yair kuna
siri anayo huyu jamaa.Nitaendelea
kumchunguza na kukupa jibu
nitakachokipata” akasema Dick
HAIFA – ISRAEL
Kitu cha kwanza alichokiona
Edger Kaka baada ya kufumbua
macho ni bahasha ndogo nyeupe
ambayo hakukumbuka nani
aliyeileta.Akaifungua na kukuta
kadi ndogo ndani ikimuelekeza
apige namba
zilizoandikwa.Alishangaa sana na
kujiuliza mtu aliyeileta kadi ile
katika kitanda chake.
“Jana nililala usingizi mzito
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom