SIRI PART2: MTUNZI PATRICK CK
MAISHA NA KIFO CHA MELANIE CHUMA
SEASON 2: EPISODE 7
Austin aliwasili katika
makazi ya Gosu Gosu saa
tatu kasoro dakika nane za
asubuhi na kukaribishwa
ndani na mwenyeji
wake.Hakuwa peke yake
alikuwa ameambatana na
watu wawili
“Papaa kutana na
Stanley na Nasibu.Hawa ni
vijana wangu,wataalamu
sana wa masuala ya
elektroniki.Watatusaidia
katika masuala ya Kamera”
akasema Austin na Gosu
Gosu akasalimiana na wale
vijana alioambatana nao
Austin
“Kama nilivyokueleza
simuni kwamba tayari
nimetuma vijana wawili
kuanzia asubuhi kumfuatilia
balozi Benjamin na taarifa
niliyopewa muda mfupi
uliopita kabla sijafika hapa
ni kwamba mke wa balozi
ndiye aliyetangulia kuondoka
nyumbani balozi alifuata
muda mfupi baadae.Hivi
sasa vijana wanaendelea
kumfuatilia na watatupa
taarifa baadae.Kuondoka
kwa balozi Benjamin
kunatuwashia taa ya kijani
kuwa sasa tunaweza kwenda
nyumbani kwake” akasema
Austin
“Tukifika pale
tutajitambulisha kama watu
wa Tanesco tunaopita
nyumba kwa nyumba
kukagua mita za
umeme.Tayari nimekwisha
tengeneza vitambulisho
vyetu vikituonyesha kama
wafanyakazi wa
Tanesco.Nimetaarifiwa kuna
mlinzi mmoja getini hivyo
tutamuonyesha vitambulisho
na kuingia ndani.Nina
uhakika mita hiyo ya umeme
itakuwa nje hivyo basi vijana
wangu wawili wataingia
ndani kujifanya wanakagua
mfumo mzima wa umeme
huku wakifunga kamera za
siri.Ni zoezi ambalo
halitachukua muda mrefu
litakuwa limekamilika”
akasema Austin kila mmoja
akachukua kitambulisho
chake wakaingia garini na
kuondoka.Wakiwa njiani
bado Austin aliendelea
kuwasiliana na vijana
aliowatuma kumfuatilia
Benjamin na wakamjulisha
kwamba balozi tayari
amewasili ofisini kwake na
wako nje wakimsubiri.
Walifika katika makazi
ya balozi Benjamin.Kulikuwa
na askari mmoja mwenye
silaha akilinda.Austin
akashuka garini na
kumsalimia vizuri Yule
askari halafu akamueleza
kwamba wao ni watu wa
kutoka tanesco ambao
wanapita nyumba baada ya
nyumba kukagua mita za
umeme.Walimuonyesha
vitambulisho na askari Yule
akaridhika akapiga simu
ndani akatoa taarifa kwamba
kuna wageni.Mtumishi wa
ndani akatoka na kwenda
kuwapokea.Austin
alijitabulisha kwamba wao ni
maafisa wa kutoka shirika la
umeme tanesco na
wanatembelea nyumba mbali
mbali kukagua
mita.Mfanyakazi Yule wa
ndani wa balozi hakuonyesha
wasi wasi wowote wala
hakutaka kutazama
vitambulisho akawapeleka
moja kwa moja ilipo mita ya
umeme.Austin akiwa na
kifaa cha kupimia umeme
akapima halafu akamgeukia
Yule mfanyakazi akamtaka
akawaonyeshe vijana wake
vifaa vyote vikubwa
vinavyotumia umeme
ndani.Bila kusita mfanyakazi
Yule aliyekuwa amevaa
suruali ya jeans ya bluu na
fulana neykundu
akawazungusha mle ndani
akiwaonyesha vifaa mbali
mbali vinavyotumia umeme
halafu wakatoka nje.Austin
akampa Yule msichana mita
aishike halafu akawataka
Stanley na Nasibu waingie
ndani waanze kuzima kifaa
kimoja kimoja cha umeme.
“Zima friji ! akasema kwa
sauti Austin na Stanley
akaenda kuzima friji.Wakati
zoezi hilo likiendelea Nasibu
alikuwa na kazi moja ya
kufunga kamera za siri
katika vyumba bali
mbali.Kwanza alifunga
sebuleni halafu akafunga
jikoni kisha akafunga
chumba cha mapumziko na
chumba cha mwisho
alichotakiwa kufunga ni
chumba cha kulala balozi
ambacho kilikuwa
kimefungwa kwa
funguo.Mlango wa chumba
kile ulikuwa na kifaa
maalum cha kupiga kelele
kama utafunguliwa endapo
balozi au mke wake
hayupo.Nasibu akachomoa
kifaa Fulani katika begi lake
akakiweka karibu na kifaa
kile cha kutoa ukelele halafu
akachukua vyuma Fulani
vidogo akaufungua ule
mlango akaingia
ndani.Akafunga kamera
mahala ambako si rahisi
kuonekana .Wakati akishuka
akaona kitu Fulani
mezani.Ilikuwa ni kadi ya
mwaliko.Akaisoma
akairudisha mahala pake na
kutoka akaufunga mlango
akachukua kile kifaa chake
chenye usumaku ambacho
kilizuia kelele kutoka katika
kile kifaa kilichowekwa
mlangoni halafu akatoka
nje.Austin alipomuona
akajua kila kitu tayari
akamaliza zoezi la kupima
na kumjulisha Yule
mfanyakazi kwamba hakuna
tatizo lolote wakaaga na
kuondoka.
“Kila kitu tayari
mkuu.Nimefunga kamera
sebuleni,jikoni,chumba cha
mapumziko na chumba cha
kulala balozi” akasema
Nasibu
“Good job guys” akasema
Austin
“Katika chumba cha
kulala balozi kuna kitu
nimekiona”akasema Nasibu
“Umeona nini?
“Nimekuta kuna kadi ya
mwaliko.Balozi amealikwa
katika hafla ya uchangishaji
fedha itakayofanyika kwa
ajili ya mabweni ya kulala
watoto wanaoishimazingira
magumu.Hafla hiyo
itafanyika Zimba hotel siku
ya ijumaa”
“Hizo ni habari njema.Ni
kesho kutwa hivyo
tujipange.Tutamfuata balozi
kila mahala
atakapokwenda.Tutamfuata
kama kivuli anapoamka hadi
anapokwenda kulala”
akasema Austin
Baada ya kutoka
nyumbani kwa balozi
walielekea moja kwa moja
nyumbani kwa Gosu Gosu
ambako ndiko kila kitu
kitafanyika kutokea
hapo.Vijana wale mahiri
Stanley na Nasib walifanya
mambo haraka haraka na
wakaanza kupata picha
kutoka katika kamera
walizozifunga nyumbani kwa
balozi Benjamin.
“Okay guys,ninyi makazi
yenu yatahamia hapa kwa
muda.Kazi yenu kubwa
itakuwa ni kufuatilia kila
kinachofanyika mle
ndani.Hakikisheni
mnafuatilia simu zote
zinazopigwa,watu wote
wanaoingia mle ndani na kila
anachokifanya balozi.
“Tunafanya zoezi hili
kwa muda gani
mkuu?akauliza Nasibu
“Hakuna muda maalum
hadi pale tutakapopata kile
tunachokitafuta” akasema
Austin
“Msijali kila kitu
mtakipata hapa ndani.Kitu
cha msingi ni macho yenu
yasibanduke katika
kompyuta kufuatilia kila
kinachoendelea ndani ya
nyumba ile”
“Yule mfanyakazi
ulikuwa naye nje wakati sisi
tunafanya mambo yetu ndani
una hakika hajahisi
chochote? Akauliza Stanley
“Hapana hajahisi
chochote.Ameamini asilimia
mia moja kwamba sisi ni
watu kutoka tanesco.Hata
Yule askari aliamini hivyo”
akajibu Austin kisha
akamuaga Gosu Gosu
kwamba anakwenda
kufuatilia masuala yake ya
likizo ya dharura.
TEL AVIV – ISRAEL
Inakaribia saa moja za
jioni katika chumba cha
gereza walimo Mathew
Mulumbi na Ammar
Nazari.Ni siku ya tatu toka
Mathew alipoanza
kuzungumza na Ammar na
wa muda huo tayari
walikuwa marafiki
wakubwa.Walizungumza
mambo mengi sana
kuhusiana na harakati zao
na Ammar alikubali kujiunga
na Mathew katika mpango
wake wa kutoroka pale
gerezani na alimtaka
watakapofanikiwa kutoroka
basi akajiunge na kundi lale
la Ammar Nazari Brigades
ombi ambalo Mathew
alilikubali.
Siku hii ndiyo ambayo
ilipangwa Mathew akapewe
maelekezo yote kuhusu
namna watakavyotoroka pale
gerezani.Ammar aliamini
alivyoambiwa na Mathew
kwamba kuna mwanamke
anayeitwa Abeba raia wa
Ethiopia ndiye anayemsaidia
kutoroka kwa kumpa ramani
ya gereza.Jioni ya siku hiyo
waliandaa mpango ambao
ungemfanya Mathew aweze
kutolewa mle chumbani na
kupelekwa hospitalini
“Muda unakaribia
Ammar.Tafadhali tufanye
kama vile
tulivyokubaliana.Kwa namna
yoyote ile leo hii lazima
nitoke humu nikaonane na
Abeba kwani aliniahidi leo
hii tayari atakuwa amepata
ramani ya gereza
itakayoniwezesha kutoroka”
akasema Mathew
“Usijali Abu kila kitu
kitakwenda kama
tulivyokubaliana” akajibu
Ammar
Saa moja na nusu za jioni
wapishi wakiwa na torori
kubwa la chakula walikuwa
wakipita chumba hadi
chumba kugawa chakula
wakiwa wameongozana na
askari wa gereza.Mlango wa
akina Mathew ukafunguliwa
akaingia mpishi kuwapa
chakula.Mathew akaishika
sahani ile ya chakula
akakitazama na kuirusha ile
sahani
“Nimechoka kula aina
moja ya chakula kila
siku.Sisi pia ni binadamu
kama ninyi !! akasema kwa
ukali
“Tafadhali kuwa na
adabu kwa chakula
unachopewa.Unadhani
imewachukua muda gani
kwa wapishi kuandaa
chakula hiki?Siku nyingine
ukirudia kitendo kama hicho
nitakuadhibu vikali”
akasema kwa ukali Ammar
“Unasemaje ?! akauliza
Mathew na kumsogelea
Ammar akamvuta kilemba
chake Ammar akakasirika na
kumtandika ngumi nzito
Mathew akaanguka chini
lakini akawahi kuinuka
akamfuata Ammar na
kumuangusha chini Ammar
akachukua uma ya kulia
chakula akamchoma nayo
mkononi damu zikaanza
kumtoka askari wakaingia
na kuwaamua
“Samahani ndugu zangu
nilikuwa namfunza adabu
huyu mwenzangu kwa kosa
la kudharau
chakula.Mpelekeni akatibiwe
jeraha lake” akasema Ammar
na Mathew akatolewa mle
ndani na kupelekwa hospitali
akatibiwa jeraha lile kisha
akatolewa na kupelekwa
katika ofisi ya mkuu wa
gereza alikomkuta Efraim
Dagan na maafisa wengine
wa gereza na wa Mossad
wakimsubiri.
“Mathew Mulumbi
karibu tena.Kwanza pole
kwa maumivu lakini vile vile
hongera kwa kazi
nzuri.Tumekuwa
tunakufuatilia kila
unachokifanya mle ndani na
tunafurahi kwa kuwa
umefanikiwa kumshawishi
Ammar hadi akakuamini”
akasema Efraim Dagan
“Haikuwa kazi nyepesi
lakini nashukuru
ameniamini na yuko upande
wangu” akasema Mathew
“Baada ya hatua ile
kukamilika sasa
kinachofuata ni mpango wa
kutoroka gerezani.Tayari
tumekwisha andaa mpango
huo” akasema Efraim Dagan
na kumpa nafasi mmoja wa
maafisa wa gereza
kuendelea.Wote wakaelekeza
macho yao katika runinga
kubwa iliyokuwa mbele
ikawashwa na ramani
ikaonekana
“Hii ni ramani ya gereza
lote.Hapa kwenye mduara
mwekundu ndipo chumba
mlimo wewe na
Ammar.Mpango
tulioutengeneza utakuwa
hivi.Siku ya kutoroka
utajifanya umepoteza
fahamu ghafla na Ammar
atabonyeza kengele ya
dharura na watafika askari
wawili haraka kujua
kumetokea nini.Atawaeleza
kwamba umeanguka na
kupoteza fahamu kisha
mmoja wa askari hao
atakusogelea kujua nini
kimekutokea na hapo ndipo
utakapokurupuka kama
Mamba na kumrukia na
wakati huo huo Ammar
atamdhibiti askari
mwingine.Hakikisha askari
hao hamuwaui bali
wapotezeni fahamu
tu.Mtachukua mavazi yao
pamoja na redio ya
mawasiliano kisha
mtaondoka kwa kufuata
ramani tutakayokupa.Baada
ya dakika tano kitalia
king’ora cha hatari kuashiria
kwamba kuna wafungwa
wanatoroka na ninyi
mtakuwa na redio ya
mawasiliano kutoka kwa
wale askari na mtakuwa
mkisikiliza kila
kinachoendelea.Mkifika hapa
geti kumi na moja tutaweka
askari mdunguaji ambaye
atamdungua Ammar kwa
risasi ya mguu na wewe
utaachia risasi kadhaa kama
vile unamlenga askari huyo
kisha utambeba
Ammar.Mtapita katika
mfereji huu wa maji machafu
utakaowatoa nje ya gereza
ambako tutakuwa
tumewaondoa askari
wanaolinda upande huo na
kuwataka waingie ndani ili
kusaidia kuwatafuta
wafungwa
waliotoroka.Mfereji huu ni
mrefu na unakwenda
kuungana na mfumo
mwingine wa maji taka toka
sehemu nyingine za jiji lakini
kabla ya kufika sehemu
ambapo mfereji huu
unaungana na mifereji
mingine mtakuta kuna ngazi
ya kupanda na juu kuna
mfuniko mtatoka nje na hapo
tayari mtakuwa mko nje ya
gereza.Baada ya kutoka nje
mtafuata barabara kuelekea
Kaskazini na kwa dakika
kama saba hivi mtakuta
daraja mtajificha chini ya
daraja kisha atakuja Dr
Abeba atamulika tochi na
kuzima mara tatu
utamtambua kisha
atawapeleka sehemu ambako
Ammar atapatiwa matibabu
na kutoka hapo atawasaidia
kuondoka Israel” akasema
Yule afisa wa gereza
“Mathew unasemaje
kuhusu mpango huo?
Akauiza Efraim
“Ni mpango mzuri lakini
kuna maboresho nataka
yafanyike.Kwa namna
mpango ulivyo tutatoka bila
kutumia nguvu nyingi na
itaonekana ni rahisi
kutoroka.Gereza hili lina sifa
ya ulinzi mkali hivyo basi
lazima ionekane tumetoka
ndani ya gereza kwa bahati”
akasema Mathew na kutoa
maelekezo kadhaa ya
kuboresha mpango ule kisha
akapewa karatasi yenye
ramani ya gereza ikionyesha
njia watakazopita kisha
akarudishwa katika chumba
chake
“Mambo yamekwendaje?
Akauliza Ammar akiwa na
shauku kubwa ya kutaka
kujua namna mambo
yalivyokwenda
“Mambo yamekwenda
vizuri.Nimefanikiwa kuipata
ramani” akasema Mathew na
kutoa karatasi katika nguo
yake ya ndani akaikunjua
ilikuwa ni ramani ya
gereza.Ammar akashindwa
kulizuia tabasamu katika
uso wake baada ya kuiona
ramani ile.Hakuamini kama
kile alichokuwa anakiona ni
kitu cha kweli.
“Ninaona haya kama
maajabu.Sikuitegemea hata
siku moja kama ningeweza
kuikamata ramani ya gereza
hili.Hii itatusaidia sana
tutakapotoka hapa kuandaa
kuja kuvamia na
kuwawachukua watu wetu
waliofungwa hapa” akasema
Ammar na Mathew akaanza
kumuelekeza namna mpango
wote utakavyokuwa na njia
watakazopita.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ni siku ya ijumaa ikiwa
ni siku ya tatu toka akina
Austin walipoanza
kumfuatilia balozi Benjamin
Hudson.Kwa muda wa siku
zote tatu Stanley na Nasibu
hawakubandua macho katika
kompyuta wakifuatilia kila
kinachofanyika nyumbani
kwa balozi Benjamin lakini
kwa muda wote huo wa siku
tatu hawakuwa wamepata
kitu chochote cha
muhimu.Timu iliyokuwa
inamfuatilia balozi Benjamin
kila aendako nao walifanya
kazi yao kwa umakini
mkubwa na kupata picha ya
kila aliyezungumza na balozi
Benjamin.Ubao uliokuwemo
katika ofisi yao ulikuwa na
picha za watu mbali bali
ambao Benjamin alikutana
nao katika siku hizo tatu na
wote walifanyiwa uchunguzi
lakini bado hawakuwa
wamepata mtu ambaye
walimuhisi anaweza kuwa
anashirikiana na balozi
Benjamin na kumpa siri
mbali mbali.
Austin January akiwa
amevalia suti nyeusi jioni hii
alikuwa ameegemea meza
akitazama picha za watu
kadhaa waliofanya
mazungumzo na Benjamin
“This dude is very clever”
akasema Austin
“Anajua sana kuficha
mambo yake.Karibu watu
wote hawa aliokutana nao ni
watu wa kawaida
sana.Katika siku hizi zote
tatu hatujamuona na simu
yoyote ya
mkononi.Tumekuwa
tukifuatilia simu zote
zinazopigwa nyumbani
kwake lakini hakuna simu
yoyote tuliyoitilia
shaka.Anafanyaje
mawasiliano yake? akauliza
Austin
“Kuna kitu kimoja
ambacho mimi na wenzangu
tumekiona na
tukajiuliza.Kila ifikapo saa
tano usiku Benjamin hutoka
chumbani kwake”akasema
Stanley
“Huelekea wapi? Austin
akauliza
“Hatujajua huelekea
wapi kwani kamera
tumeweka chumbani
kwake,sebuleni,jikoni na
katika chumba cha
mapumziko”
“Tulipaswa kuweka
kamera kila sehemu ili tujue
kila kinachofanyika mle
ndani.kama anatoka kila saa
tano usiku lazima kuna
mahala huwa anakwenda”
akasema Austin
“Kwa hiyo tunafanya nini
kuhusu hilo?akauliza Gosu
Gosu
“Lazima tutafute namna
ya kurudi tena mle ndani
kufunga kamera nyingine
sehemu mbali mbali kujua
usiku huo akitoka Benjamin
huenda wapi.Kwa sasa
tujielekeze katika tukio la
usiku wa leo ambapo
Benjamin amealikwa katika
hafla ya uchangiaji fedha
kwa ajili ya mabweni ya
watoto waishio katika
mazingira
magumu.Mimi,GosuGosu,na
Nasibu wote tutakuwemo
ndani ya ukumbi huo.Macho
yetu wote tutayaelekeza kwa
mtu mmoja tu Benjamin
Hudson.Wote tutakuwa
tumevaa kamera ambazo
zitamuwezesha Stanley
atakayekuwa amebaki
nyumbani kupata picha za
kila kinachoendelea mle
ndani ya
ukumbi.Tuhakikishe
tunapata picha ya kila
anayezungumza na
Benj……” akanyamaza
Austin baada ya simu yake
kuita.Walikuwa ni vijana
wanaomfuatilia Benjamin
“Hallow” akasema
Mathew baada ya kuipokea
simu
“Mkuu,huyu jamaa
ametoka na ndani ya gari
yuko yeye na mke wake”
“Nadhani wanaelekea
katika hafla waliyoalikwa
jioni hii ya leo.Endeleeni
kumfuatilia na sisi
tunaelekea ukumbini”
akasema Austin na kukata
simu.
“Tayari balozi Benjamin
anaelekea
ukumbini.Tusipoteze muda
tuelekee huko” akasema
Austin.Ni Stanley pekee
aliyebaki pale nyumbani
wengine wote wakaingia
katika magari na
kuondoka.Austin alikuwa na
Nasib Gosu Gosu alikuwa
peke yake.
Zimba hoteli usiku huu
iling’aa kwa mataa ya rangi
mbali mbali yaliyozunguka
hoteli hii ya hadhi ya nyota
tano.Usiku huu mahala hapa
kulikuwa na hafla ya
kuchangisha fedha kwa ajili
ya kuwasaidia watoto
waishio katika mazingira
magumu wa kituo cha
kulelea watoto cha Mama wa
Afrika.Watu wengi
walialikwa kuhudhuria hafla
hiyo ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kujenga
mabweni ya watoto hao
waishio katika mazingra
magumu.Katika sehemu ya
kuegesha magari kulikuwa
na watu watatu wakiongoza
magari kwani usiku huu
kulikuwa na magari mengi
ya watu waliofika katika
hoteli hii kuhudhuria hafla
hiyo.Akina Austin waliwahi
kufika kabla ya balozi
hajafika.Hawakuwa na kadi
za mwaliko kwani kadi
zilitolewa kwa watu maalum
tu lakini kwa wengine ambao
waliguswa na kutaka
kuchangia walikaribishwa
pia hivyo akina Austin
walikuwa katika kundi hili
wakaingia ndani ya
ukumbi.Watu walikuwa
wengi na bado waliendelea
kuingia ukumbini.Nasib
alipanda sehemu ya juu,Gosu
Gosu na Austin kila mmoja
akachukua sehemu yake.
Wakiwa mle ukumbini
Austin akapigiwa simu na
vijana wake kwamba balozi
Benjamini tayari amefika
hapo ukumbini na ameshuka
garini yeye na mkewe
wanaelekea ukumbini.Austin
akawatumia ujumbe Gosu
Gosu na Nasibu kuwajulisha
kwamba muda wowote balozi
Benjamin ataingia ukumbini
hivyo wajiandae.
Balozi Benjamin akiwa
ameongoza na mkewe na
watu wawili walioonekana ni
walinzi wake,wakaingia
ndani ya ukumbi.Toka
alipoingia ukumbini macho
ya Nasibu yalimng’aza na
kuelekeza kamera
kumfuatilia.Alipokewa na
mtu maalum aliyewekwa
kwa ajili ya kupokea
wageni.Alielekezwa kukaa
katika meza ya tatu kutoka
meza ya mbele.Kulikuwa na
watu wengine watatu katika
meza hiyo
wakasalimiana.Wakati
wakiendelea na
mazungumzo,Austin
akainuka kama vile
anakwenda maliwato lakini
aliporejea hakwenda tena
kukaa katika meza ile
aliyokuwa amekaa badala
yake akaenda kukaa karibu
na meza ya balozi huku
macho yae akiyageuza kama
kinyonga kutazama kila
kinachoendelea katika meza
ile aliyokaa balozi.Wote
walikuwa wamevaa kamera
za siri ambazo zote
walizielekeza kwa balozi.
Muongoza shughuli
aliposhika kipaza sauti na
kutangaza kwamba muda si
mrefu shughuli
itaanza,Benjamin
akaitazama saa yake ya
mkononi halafu akainuka na
kutembea kama vile
anaelekea maliwato Gosu
Gosu naye akasimama
akaelekea huko.Nasibu naye
akashuka ghorofani na
kumfuata Gosu
Gosu.Benjamin aliingia
maliwato baada ya dakika
mbili akatoka lakini
hakurejea ukumbini
akachepuka na kufuata
korido akaelekea
baa.Akaenda kaunta na
kununua chupa ya bia.Gosu
Gosu akabaki nyuma
akamuacha Austin aingie
mle baa.Balozi Benjamin
akamimina bia ile katika
glasi akanywa huku
akiangaza huku na kule
halafu akalipa na kumuachia
muhudumu chenji akatoka
mle baa na kuelekea katika
lifti.Wakati akisubiri lifti
iliyokuwa juu Nasibu naye
akafika akaungana naye
kusubiri lifti.Baada ya muda
mfupi milango ya lifti
ikafunguka wakaingia
walikuwa jumla watu
sita.Balozi akaomba
abonyezewe namba sita
akimaanisha anakwenda
ghorofa ya sita.Nasibu
akawaandikia ujumbe akina
Gosu Gosu kwamba balozi
anaelekea ghorofa ya
sita.Haraka haraka Gosu
Gosu aliyefika katika eneo
lile la lifti akaingia katika
lifti ya pembeni ambayo
haikuwa na mtu na
kubonyeza ghorofa ya sita
lifti ikaondoka.
Milango ya lifti
ikafunguka ghorofa ya sita
lakini balozi hakushuka
badala yake akaingia
mwanamke Fulani aliyekuwa
amevaa suruali ya jeans ya
bluu na fulana nyeupe
iliyombana na viatu virefu
vya bluu.Mwanamke Yule
alimsogelea zaidi balozi
ambaye alikuwa karibu na
Nasib.Hakuna aliyemjali
akachomoa mfukoni bahasha
ya khaki na kumuwekea
balozi kwenye
koti.Mwanamke Yule
alishuka ghorofa ya nane
Nasibu naye
akashuka.Baada ya kushuka
mwanamke Yule akaanza
kushuka ngazi kwa
miguu.Nasibu akajibanza
mahala na kupiga simu kwa
Austin
“Kuna mwanamke
amepanda lifti ghorofa ya
sita na akamuwekea balozi
bahasha ya khaki kwa
uficho.Mwanamke huyo
ameshukia ghorofa ya nane
na anashuka kwa kutumia
ngazi za kawaida.Amevaa
suruali ya jeans ya
bluu,fulana nyeupe ya
kumbana na viatu vya bluu
ana mkoba mweupe”
“Kazi nzuri sana Nasib
shuka taratibu rejea chini
uendelee kumfuatilia balozi”
akasema Austin halafu
akampigia simu Gosu Gosu
aliyekuwa ghorofa ya sita
akamjulisha amfuatilie
mwanamke Yule anayeshuka
ngazi.
Milango ya lifti
ilifunguka na balozi
Benjamin akatoka na
kuelekea baa akasimama
kaunta akaangaza angaza
kama vile anamtafuta mtu
halafu akaondoka akaelekea
ukumbini.
“Anarejea ukumbini”
Nasibu akamjulisha Austin.
Balozi aliingia ukumbini
na kukuta tayari hafla
imeanza akaenda kuketi
katika meza yake.
Gosu Gosu aliendelea
kumfuatilia taratibu
mwanamke Yule akapita baa
halafu akatoka nje na moja
kwa moja akaelekea katika
maegesho.Gosu Gosu naye
akaelekea katika
maegesho.Mwanamke Yule
akaingia katika gari la
kifahari aina ya range rover
e vogue rangi nyekundu
akaliwasha na kuondoka
Gosu Gosu naye akawasha
gari lake na kuanza
kumfuatilia
“Ameondoka hapa
hotelini.Ninamfuatilia
kumfahamu ni nani” Gosu
Gosu akamwambia Austin
“Sawa Gosu Gosu
endelea kumfuatilia sisi
tunaendelea kumfuatilia
balozi tayari amerejea
ukumbini.Tunahitaji kujua
bahasha aliyopewa ina nini?
Naamini ina kitu kikubwa
hadi akaenda kumpa
kiuficho namna hiyo.Ruby
alikuwa sahihi huyu jamaa
ni mtu anayechukua
tahadhari kubwa sana katika
mambo yake.Tafadhali
hakikisha unapata majibu
mwanamke huyo ni nani na
amempa nini balozi.Kama
utahitaji msaada nijulishe
haraka sana” akasema
Austin
Baada ya kutoka Zimba
hoteli mwanamke Yule
akaenda hadi Dar es salaam
supermarket.Gosu Gosu naye
akaenda hapo akaegesha gari
na kumuachia mlinzi shilingi
elfu kumi amlindie lile gari
atakuja kulichukua baadae
akamfuata dereva wa boda
boda akamtaka waelekee
sehemu fulani lakini
akamtaka wasubiri kuna
gari wanalifuata.Dakika
kama kumi baadae gari la
Yule mwanamke likatoka na
Gosu Gosu akamuelekeza
Yule dereva wa boda boda
walifuate.
Mwanamke Yule aliingia
katika jumba moja kubwa la
ghorofa moja lililokuwa na
geti lenye nakshi za
kuvutia.Gosu Gosu na Yule
dereva wakalipita jumba lile
na kwenda mbele kidogo
kisha Gosu Gosu akamlipa
Yule dereva kiasi cha pesa
alichohitaji akaondoka
zake.Gosu Gosu akaanza
kurejea taratibu katika
jumba lile.Ni mtaa uliokuwa
na majumba mazuri na kwa
muda ule hakukuwa na watu
wengi barabarani.Kulikuwa
na taa kubwa getini iliyotoa
mwangaza mkubwa.Gosu
Gosu akaenda kuegemea
nguzo ya umeme akatazama
pande zote halafu akachomoa
bastora yake yenye kiwambo
cha sauti akailenga ile taa
ikapasuka.Eneo lile likawa
na mwanga hafifu sana
halafu akatulia pale kwa
muda akiangaza pande zote
kama kuna mtu.Zilipita piki
piki mbili na magari matatu
halafu akavuka barabara na
kwenda katika geti akajaribu
kuusukuma mlango mdogo
wa geti ulikuwa umefungwa
kwa ndani haraka haraka
akavua viatu na kurudi
nyuma hatua kadhaa halafu
akatoka mbio na kuruka
akashika kingo za juu za
geti akapanda na
kuchungulia ndani.Aliliona
gari la Yule dada likiwa
limeegeshwa mbele ya
nyuma akajirusha ndani na
kutua bila kelele.Akaangaza
angaza mara akasikia
muungurumo wa mbwa
mkubwa aliyemsogelea
kimya kimya kwa wepesi wa
aina yake Gosu Gosu
akaizinga bastora yake na
mbwa Yule akaanguka chini
kimya kimya.Akamvuta na
kumtupa pembeni kwenye
maua akatembea taratibu
hadi katika kibaraza
akachungulia ndani sebuleni
akamuona mwanamke
mmoja amekaa sebuleni
akitazama filamu.Yule
mwanamke aliyempa
bahasha balozi
hakuwepo.Akazunguka kwa
nyuma akajaribu
kuusukuma mlango ulikuwa
wazi akaingia ndani
akatokea jikoni hakukuwa
na mtu akatokea sehemu ya
kulia chakula akasikia hatua
za mtu akajibanza pembeni
katik anguzo kwa bahati
mbaya akagonga glasi
ikaanguka na kuvunjika.
“Dada ? akaita Yule
msichana aliyekuwa akipita
akitokea sebuleni lakini
alipoona kimya akaamua
kuingia katika chumba cha
chakula kuangalia kwa nini
glasi ile imevunjika.Mara tu
alipoingia akajikuta
akitazamana na mtu mwenye
bastora
“Mamaaaa ! akapiga
kelele
“Shhhh !! usipige kelele
nitakufumua kichwa kwa
risasi ! akasema Gosu
Gosu.Yule msichana alikuwa
anatetemeka mwili kwa
woga
“Dada yako yuko
wapi?akauliza Gosu Gosu
“Yuko chumbani
kwake”akajibu Yule
msichana akitetemeka
“Nipeleke chumbani
kwake haraka sana”
akasema Gosu Gosu na mara
ikasikika sauti ikiita
“Nancy !
“Nancy !
“Dada ananiita” akasema
Yule msichana
“Itika” akasema Gosu
Gosu na Yule msichana
akaitika
“Nimesikia unapiga
kelele kuna nini
huko?akauliza
“Hakuna kitu dada”
akasema Nancy
“Kamuangalie mtoto
kama amelala” akasema Yule
dada kule juu
“Nipeleke katika chumba
alimo mtoto” akasema Gosu
Gosu na Yule msichana
Nancy akampeleka katika
chumba alimo mtoto mdogo
wa kike mwenye umri wa
kama miaka mitano.
“Anaitwa nani huyu
mtoto?akauliza Gosu Gosu
‘Anaitwa Teddy” akajibu
Yule Nancy na Gosu Gosu
akampa pigo kichwani
akaanguka chini na kupoteza
fahamu akamuinua Yule
mtoto aliyekuwa usingizini
akambeba na kuelekea
ghorofani kilipo chumba cha
Yule dada.Akagonga mlango
“Nancy ! akaita yule dada
mle chumbani na Gosu Gosu
akagonga kwa mara ya pili
na mlango
ukafunguliwa.Yule dada
hakuamini alipojikuta
akitazama na Gosu Gosu
aliyekuwa na bastora huku
akiwa amembeba mwanae.
“Who are you? Akauliza
Yule dada ambaye mstuko
alioupata ulikuwa mkubwa
“Sit down ! akasema
Gosu Gosu na Yule dada
akatii na kukaa
kitandani.Gosu Gosu
akaichukua bastora
iliyokuwa mezani ya Yule
dada akaifutika kiunoni
akamtazama Yule dada
ambaye midomo ilikuwa
inamtetemeka
“Wewe ni nani?Unataka
nini?Tafadhali naom……”
akasem Yule dada lakini
Gosu Gosu akamnyamazisha
“Quiety !
“Nina muda mfupi sana
hapa nataka unijibu maswali
nitakayokuuliza kiufasaha
na kama utathubutu kuleta
jeuri au kujaribu kutaka
kufanya ujinga wowote
nitakuua wewe na
mwanao.Umenielewa?akauli
za
“Nimekuelewa.Tafadhali
naomba usimdhuru
mwanangu.Unataka nini?
Pesa? Akauliza Yule
mwanadada
“Jina lako nani?
“Naitwa Rahel”
“Rahel unafanya kazi
wapi?
“Mimi ni mfanya
biashara wa vipodozi”
“Are you sure?
“Ndiyo mimi ni mfanya
biashara”
“Usiku huu ulikutana na
balozi wa umoja wa ulaya
katika hoteli ya Zimba una
mahusiano naye yapi?
“Balozi wa
Ulaya?akauliza Rahel
“Ndiyo”
“Simfahamu wala sijafika
Zimba hoteli usiku
huu.Nilipotoka kwenye
biashara zangu nimekuja
moja kwa moja
nyumbani.Utakuwa
umenifananisha”
“Nilikwambia nina muda
mfupi sana hapa.Nakupa
nafasi ya mwisho unieleze
una mahusiano gani na
balozi wa Ulaya hapa nchini
bwana Benjamini
Hudson?akasema Gosu
Gosu.Huku machozi
yakimtoka Rahel akajibu
“Naomba uniamini kaka
yangu sina mahusiano yoyote
na huyo balozi wala simjui ni
nani”
“Nilikutaka uwe mkweli
kwangu,kwa kuwa umekuwa
muongo nitaanza kumpiga
risasi moja moja mwanao
hadi utakapokuwa tayari
kunieleza ukweli” akasema
Gosu Gosu na kumuelekezea
yule mtoto bastora mguuni
“Nitahesabu mpaka tatu
kama hautakuwa tayari
nitaufumua mguu wake kwa
risasi” akasema Gosu Gosu
“Tafadhali kaka yangu
nakuomba sana usimuumize
mwanangu.Unamuonea bure
mimi simfaham…….”
“Tatu ! akasema Gosu
Gosu kwa ukali
“Kaka nakuomba ..”
akasema Rahel huku akitaka
kuinuka
“Usiinuke hapo
nitakuchakaza kwa
risasi.Mbili ! akasema kwa
ukali
“M….”
Kabla Gosu Gosu
hajamaliza kutamka mlango
ukapigwa teke zito na bomu
dogo la kurusha kwa mkono
likatupiwa mle ndani
“Oh my God ! akasema
Gosu Gosu.Rahel macho
yakamtoka pima.Picha ya
Mathew Mulumbi akidaka
bomu na kulirusha nje
walipokuwa katika misheni
ya kuwakomboa watoto
waliotekwa na magaidi
ikapita haraka haraka
kichwani kwake
“Mathew Mulumbi
aliwahi kudaka bomu na
kulitupa nje” akawaza na
kufanya kitendo ambacho
Rahel hakuwa
amekitarajia.Gosu Gosu
alimrusha Teddy kitandani
huku akimrushia Rahel
bastora ambaye aliidaka
kiufundi sana akaanguka
chini na kumimina risasi
mlangoni .Gosu Gosu aliruka
akalishika lile bomu na
kulirusha katika dirisha
lililokuwa wazi bomu lile
likaenda kutua ndani ya
bwawa la kuogelea.Alikuwa
anatweta.Hakuamini kama
walikuwa
wamenurusika.Akainuka na
kuelekeza macho yake
mlangoni watu wawili
walikuwa wameanguka
wakivuja damu.Ilikuwa kazi
ya Rahel.Aliwachakaza watu
wale kwa risasi kutoka
katika bastora aliyopewa na
Gosu Gosu
Gosu.Akawasogelea watu
wale akawachunguza
walikuwa
wamekufa.Akamgeukia
Rahel aliyekuwa amejibanza
pembeni ya meza ya vipodozi
alikuwa anatetemeka
“Are you okay?akauliza.
“I’m..I’m … fine” akajibu
kwa kitetemeshi.
“Good job Rahel”
akasema Gosu Gosu
“Thank you.Umeokoa
maisha yangu na ya
mwanangu” akasema Rahel
na kwenda kumkumbatia
mwanae aliyekuwa kitandani
akilia.Gosu Gosu akamtaka
asitoke mle chumbani
akashuka chini kwenda
kuangalia kama kuna watu
wengine lakini hakukuwa na
mtu akarejea chumbani kwa
Rahel
“Unawafahamu watu
hawa?akauliza Gosu Gosu
“Hapana siwajui”akajibu
“Okay we need to get out
of here immediately.Hapa
tayari ni sehemu hatarishi
kwenu.Zima kompyuta na
simu zako zote”akasema
Gosu Gosu na Rahel
akafungua zimu zake mbili
akatoa laini zake
“Unatupeleka wapi?
“Sehemu salama”
akasema Gosu Gosu na
kumtaka Rahel akusanye
kila kitu chake cha muhimu
akaweka katika sanduku
dogo wakatoka mle chumbani
akaenda katika chumba cha
chakula akambeba Yule
msichana ambaye mpaka
sasa bado hakuwa na fahamu
akamuingiza garini.Akarudi
tena ndani na kuibeba miili
ya wale jamaa waliouawa
akaipakia garini na
kuifunika na turubai
“Hao unawapeleka
wapi?akauliza Rahel kwa
wasiwasi
“Miili hii haipaswi
kuendelea kukaa mle ndani
mwako ninakwenda
kuitupa.Polisi hawatakiwi
wajue kuhusiana na tukio
hili” akasema Gosu Gosu
akiwa katika usukani.Bado
Rahel alikuwa amemkubatia
mwanae aliyekuwa
anatetemeka.Alichokishuhud
ia usiku ule kilimstua
sana.Safari ilikuwa ya kimya
kimya wakielekea nje kidogo
ya jiji hadi walipokuta
vichaka Fulani Gosu Gposu
akazima gari na kushusha
miili ya wale jamaa akaitupa
vichakani kisha wakaanza
safari ya kurejea jijini.
“Who are you?akauliza
Rahel
“You’ll soon know who I
am” akajibu Gosu Gosu
“Tafuta sehemu salama
tuliache hili gari hatupaswi
kuendelea kulitumia”
akasema Rahel
“Kwa nini Rajel?
“Kwa sababu
wanatufuatilia.Wanajua hivi
sasa tuko wapi” akasema
Rahel na Gosu Gosu
akamtazama
“Akina nani
wanatufuatilia?
“Do as I say ugly man !
akasema Rahel kwa ukali
“Fine”
Gosu Gosu akaiingiza
gari ile katika baa moja
wakashuka wakashuka
halafu wakachukua taksi
hadi Dar es salaam
supermarket ambako Gosu
Gosu aliacha gari lake
wakaingia garini na
kuondoka
“Huyu mwanamke
anaonekana ana mambo
makubwa sana.Alisema
hawajui watu wale waliokuja
kumuua na sasa anasema
kwamba tunafuatiliwa.Kuna
jambo analifahamu nidyo
maana akataka kuuawa”
akawaza Gosu Gosu
Walipokaribia kufika
katika makazi ya Gosu Gosu
ndipo alipokumbuka kutaka
kuwasiliana na wenzake
akina Austin lakini kumbe
simu yake ilikuwa imepata
hitilafu katika ule mshike
mshike na
ikazimika.Alipofika katika
makazi yake akawakaribisha
ndani Rahel na mwanae
pamoja na Nancy yule
msichana aliyekuwa
amepoteza fahamu ambaye
tayari alikwisha rejewa na
fahamu.Bila kupoteza muda
akamuelekeza mtumishi wa
ndani awaandalie wageni
wale chumba cha wageni na
baada ya muda mfupi
chumba kikawa tayari Rahel
akaenda kumlaza mwanae
na Yule mdogo wake.Wakati
Rahel akimbembeleza
mwanae alale Gosu Gosu
akabadili simu na kumpigia
Austin akamjulisha kila
kilichoendelea.
“Pole sana
Papaa.Niliingiwa na
wasiwasi mkubwa baada ya
simu yako kutopatikana kila
nilipojaribu kupiga”akasema
Austin
“Hata mimi mwenyewe
sikuwa nakumbuka kabisa
kuhusu simu hadi nilipofika
nyumbani.Austin I saw death
today” akasema Gosu Gosu
“Pole sana
Papaa.Umefanya kazi kubwa
sana hadi ukafanikiwa
kumpata huyo mwanamke
ambaye naamini atakuwa na
msaada mkubwa kwetu.Kwa
sasa mpe muda apumzike ila
usimruhusu kufanya
mawasiliano na mtu yeyote
Yule na kila kitu chake
kizimwe kwani wanaweza
wakamfuatilia wakajua
mahala alipo.Mimi
nitawaachia vijana
waendelee kumfuatilia balozi
ninakuja hapo nyumbani
sasa hivi kuungana nawe
tumuhoji huyo
mwanamke.Kuna mambo
mengi ambayo tunahitaji
kuyafahamu kutoka kwake”
akasema Austin
Alipomaliza kuzungumza
na Austin Gosu Gosu
akachukua bia baridi katika
friji akaigugumia yote halafu
akasimama akiwa
ameegemea friji.
“Haikuwa siku yangu ya
kufa leo lakini tayari
nilikwisha chungulia
kaburi.Kama nisingepata
ujasiri wa kuliokota bomu
lile na kulirusha nje mimi na
wote mle ndani tungekwisha
kufa.Namshukuru Mathew
kwa kunipa ujasiri kwani
naye pia aliwahi kudaka
bomu akalirusha nje
akatuokoa wote na leo
nimefanya kama alivyofanya
yeye.” Akawaza na kuvuta
pumzi ndefu sana na
kuelekea katika chumba cha
wageni waliko akina Rahel
akagonga kidogo halafu
akaruhusiwa kuingia
akausukuma mlango
akaingia ndani.Rahel
alikuwa amekaa kitandani
mwanae Teddy na Yule
msichana Nancy walikuwa
wamelala
“Wanaendeleaje?akauliza
Gosu Gosu
“Nashukuru wamepata
usingizi lakini mstuko
walioupata ni
mkubwa”akasema Rahel
“You need something to
drink?Wine,beer or whisky?
Akauliza Gosu Gosu
“No thank you”akajibu
Rahel
“Rahel kama hutajali
naomba tuzungumze
tafadhali” akasema Gosu
Gosu na Rahel akainuka pale
kitandani wakaelekea
sebuleni.Gosu Gosu
akafungua friji akatoa chupa
ya maji ya kunywa
akamminia Rahel katika
glasi akampa yeye
akachukua chupa ya bia
“Rahel hapa ulipo ni
sehemu salama hakuna
anayeweza kukufuata hapa
hivyo jisikioe amani.Baada
ya yote yaliyotokea nadhani
sasa ni wakati muafaka wa
kuzungumza.Niliweka
hatarini maisha yangu
kukuokoa wewe na mwanao
hivyo ninahitaji kuufahamu
ukweli.Nataka unieleze
ukweli bila kunificha na
mimi nitakusaidia lakini
kama ukiamua
kunidanganya utakuwa
unajidanganya wewe
mwenyewe kwani watu wale
ambao walikufuata kukuua
hawatachoka wataendelea
kukutafuta usiku na mchana
hadi watakapohakikisha
wamekumaliza.Nataka
kufahamu wewe ni
nani?Unafanya kazi wapi na
nani unashirikiana naye na
kwa nini watu wale walikuja
kutaka kukuua?akauliza
Gosu Gosu.Rahel akainama
akafuta machozi halafu
akamtazama Gosu Gosu
“Nilikudanganya.Jina
langu si Rahel.Naitwa
Agatha”akanyamza kidogo
halafu akaendelea
“Kabla sijakueleza
chochote nataka
unihakikishie usalama
wangu na familia
yangu.Hawatachoka
kunitafuta hadi pale
watakapohakikisha
nimeuawa.I was so stupid to
believe them” akasema
Agatha
“Agatha nimekuokoa
kutoka kwa wale watu usiku
wa leo na nitaendelea
kukulinda.Nakuahidi wewe
na familia yako mtakuwa
salama”
“You don’t know what
you’re talking about Gosu
Gosu.The people I’m talking
about they’re dangerous than
you think.I know their
secrets so they must find and
kill me” akasema Agatha
“Agatha nakutoa hofu
kwamba utakuwa
salama.Mimi na wenzangu
tutakulinda na kuhakikisha
unakuwa salama.Niambie ni
akina nani hao watu?
“This place is not safe for
me why don’t you
understand?akauliza Agatha
kwa ukali
“Find me somewhere safe
and I’ll tell you everything I
know” akasema Agatha
“Agatha tafadhali
naomba unisikilize.This
place is very safe for you and
for your family.Hakuna
anayejua uko hapa na
hakuna atakayejua kama
uko hapa.Ninaibeba
dhamana ya usalama wako
wewe na familia
yako.Naomba uniamini
tafadhali.Mimi ndiye peekee
unayeweza ukaniamini kwa
maisha yako kwa wakati
hii.Me and my friends we’ll
keep you guys safe I give you
my word” akasema Gosu
Gosu.Rahel akamtazama
kwa muda halafu akasema
“I work for SNSA”
“SNSA? What’s
that?akauliza Gosu Gosu
“Secret Nation security
Agency.Idara ya siri ya
usalama wa nchi
inayojishughulisha na
usalama wa ndani wa nchi”
akasema Agatha na picha ya
Devotha ikapita kwa haraka
katika akili ya Gosu Gosu
“Idara ya siri? Akauliza
“Ndiyo.Hii ni idara
inayofanya kazi zake kwa siri
kubwa hapa nchini na ni
watu wachache sana ambao
wanafahamu uwepo
wake.Mimi nilikuwa katika
kitengo cha udukuzi.Kuna
mambo mengi ambayo
yanafanywa na kitengo hiki
ambayo watu
hawayafahamu.Kila siku
maelfu ya simu zinadukuliwa
tunasikiliza mawasiliano yao
bila wao kujua.Tumekwisha
ingia katika mitandao yote
ya simu iliyopo hapa nchini
na tunao uwezo wa kufuatilia
kila simu tunayoitaka bila ya
wao kujua.Tunaweza
kuwasha mikrofoni ya simu
bila mtu kujua hata kama
simu yake ikiwa imezimwa
na kumfuatilia.Mtu yeyote
tunayemtilia shaka tunao
uwezo wa kumfuatilia ”
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Nilipewa kazi ya
maalum ya kudukua
mawasiliano yote ya Rais
kujua anawasiliana na nani
na wanawasiliana kuhusu
nini.Hukusanya mawasiliano
ya Rais kwa siku nzima na
kuyaweka katika faili
maalum ambalo mwenye
uwezo wa kulifungua
ukiacha mimi ni Tamar.Kila
jioni ninapowasilisha taarifa
ya siku Tamar hunipatia
shilingi milioni moja na nusu
kama malipo ya kazi
niliyoifanya na hii ni nje ya
mshahara ndiyo maana
sikuacha kuifanya kazi hii
kwani ilikuwa na malipo
mazuri”
“Pesa hizo nyingi Tamar
alizipata wapi? Na kwa nini
akulipe kiasi hicho kikubwa
cha fedha kwa kazi ambayo
ungeweza kuifanya kama
sehemu ya kazi yako ya
siku?akauliza Gosu Gosu
“Alinilipa fedha nyingi ili
kunifanya kwanza nitunze
siri na pili nipate moyo wa
kuendelea kuifanya ile kazi
kwa kujua kwamba ina
malipo mazuri.Kuhusu
anakotoa fedha sikuhitaji
kujua lakini ninachofahamu
Tamar ni tajiri.Anamiliki
magari ya kifahari sana”
akajibu Agatha
“Ulifahamu rekodi zile
anazipeleka wapi
ukishazihifadhi? Gosu Gosu
akauliza
“Hapana sikujua
anazipeleka wapi na
nilitamani sana kufahamu
lakini kutokana na malipo
makubwa aliyokuwa
akinilipa sikutaka
kufuatilia”akajibu Agatha
“Usiku wa leo umempa
balozi Benjamin bahasha ya
khaki ilikuwa na kitu gani
ndani yake?akauliza Gosu
Gosu
“Kama nilivyokueleza
kwamba kazi yangu mimi
ilikuwa ni kukusanya rekodi
zote za mawasiliano ya Rais
na kuzihifadhi katika faili
maalum na baada ya hapo
kazi yangu huwa imekwisha
ninachukua fedha zangu na
kurudi nyumbani.Siku
chache zilizopita nilinasa
mawasiliano ya Rais Dr
Fabian na Rais wa Congo
Patrice Eyenga.Ilikuwa ni
muda mchache baada ya
Yule mwanamama tajiri
Lucy Muganza na mumewe
kuuawa jijini Dar es
salaam.Katika mazungumzo
yao Dr Fabian alimjulisha
Rais Patrice kwamba kazi
imekamilika na Lucy
Muganza tayari
ameuawa,Congo na Afrika
Mashariki watakuwa na
amani.Nilistuka sana baada
ya kunasa mazungumzo hayo
na sikuyaweka katika orodha
ya mawasiliano niliyompa
Tamar.Nilinasa tena
mazungumzo mengine Dr
Fabian akimjulisha Rais
Patrice Eyenga kwamba
kulifanyika makosa madogo
katika operesheni ya
kumuua Lucy Muganza na
umoja wa Ulaya umekwisha
anza kuwa na wasi wasi
kwamba ni serikali yake
ndiyo waliotekeleza mauaji
yale na wametaka
wachunguzi wa kimataifa
waingie nchini kuja
kuchunguza kuhusu mauaji
hayo.Rais Patrice alimpa
pole Dr Fabian kwa
kumsababishia yeye na nchi
yake matatizo yale makubwa
lakini Dr Fabian
alimuhakikishia kwamba
suala lile watalimaliza asiwe
na wasi wasi.Niliingiwa na
hofu ya kumuonyesha Tamar
maongezi hayo kati ya Rais
wetu na Patrice Eyenga na
hivyo nikayaficha.Kutokana
na kufanya kazi mfululizo
bila kupumzika,Tamar
alinipa mapumziko ya siku
tatu kuanzia jana lakini leo
aliniita na kunipa maelekezo
ya kwenda Zimba hotel
kukutana na balozi wa umoja
wa Ulaya hapa nchini bwana
Benjamin Hudson.Alinipa
maelekezo yote ya namna
nitakavyoweza kukutana
naye na kumpatia bahasha
ile”
‘Benjamin hakuwa na
simu ya mkononi uliwezaje
kufanya mawasiliano naye
hadi mkakutana katika lifti?
“Benjamin anatumia saa
yake ya mkononi katika
kuwasiliana.Ana saa
maalum inayotumika kama
simu hivyo ukimpigia katika
namba yake,huonyesha
katika saa na kisha
hubonyeza kidude katika saa
yake na sikioni huwa
ameweka kifaa maalum
kidogo sana cha kusikilizia
maongezi.Hivyo ndivyo
hufanya mawasiliano
yake.Niliyajua haya yote
kutoka kwa Tamar” akajibu
Agatha
“Endelea” akasema Gosu
Gosu
“Nikiwa njiani nilipata
hamu ya kujua kuna nini
ndani ya ile bahasha
nikasimamisha gari na
kuifungua nikakuta kuna
flashi ya kuhifadhia
kumbukumbu nikaichomeka
katika kompyuta yangu
nikakuta kuna rekodi za yale
mazungumzo ya Rais Dr
Fabian na Rais Patrice
Eyenga ambayo sikutaka
kumpa Tamar.Inaonekana
kuna kitu alikigundua ndiyo
maana akanipa siku tatu za
kupumzika na wakati nikiwa
mapumzikoni akapitia upya
rekodi zote za Rais na
kugundua kuna baadhi ya
rekodi nilizificha.Hapo ndipo
nilipogundua kuwa rekodi
zile huwa anampatia
Benjamin lakini sikujua nini
hasa lengo la kufanya vile”
akasema Agatha.
“Pole sana
Agatha.Ahsante kwa kuwa
mkweli lakini nataka
kufahamu kwa nini
hukutaka kumuonyesha
Tamar rekodi hizo za
mazungumzo ya Rais Dr
Fabian na Patrice
Eyenga?Gosu Gosu akauliza
“Niliponasa mazungumzo
yale nikajua Rais wetu
pamoja na Patrice wote
wawili wanahusika katika
mauaji yale ya Lucy
Muganza hivyo sikutaka
jambo hilo lijulikane ndiyo
maana nikayaficha.Kabla ya
kuingia SNSA nilikuwa
nafanya kazi ikulu na Rais
aliyepita Dr Evans ndiye
aliyenipeleka SNSA kwa ajili
ya kumpa taarifa zote
zinazoendelea pale.Baada ya
kuja Rais mpya Dr Fabian
bado nimeendelea kubaki
pale pale.Nikiwa nafanya
kazi ikulu nilikula kiapo cha
kulinda siri hivyo nilijihisi
hatia kubwa sana kufanya
kile nilichokuwa nakifanya
kudukua mawasiliano ya
Rais lakini sikuweza kukataa
kwani yalikuwa ni maagizo
ya wakubwa wangu”
“Good job
Agatha.Unadhani…oh my
God ! Gosu Gosu akashindwa
kuendelea na kushika
kichwa.
“Suala hili limekuwa
kubwa.Idara nyeti ya serikali
tayari imekwisha ingiliwa”
akawaza Gosu Gosu
“Nataka uniambie
kuhusu Tamar ?Who is she?
Akauliza Gosu Gosu
“Ndiye kiongozi wa SNSA
kwa sasa”
“Kuna mtu anaitwa
Kaiza.Do you know him?
“Kaiza?
“Ndiyo.Unamfahamu?
“Kaiza is dead.Alifariki
mwaka jana.Alikutwa
amefariki katika chumba cha
hoteli nchini Afrika
kusini”akasema Agatha
“Baada ya Kaiza kufariki
dunia ndipo alipoletwa
Tamar kuchukua nafasi
yake.Umemfahamuje Kaiza?
“He was a friend of mine”
“Unafahamu kuhusu
idara hii ya siri?akauliza
Agatha
“Ndiyo ninaifahamu
kidogo.Aliwahi kunieleza
Kaiza” akasema Gosu Gosu
“Who are you?akauliza
Agatha
“Naitwa Gosu Gosu.Mimi
na kikosi cha rafiki zangu
tulipata taarifa kwamba
Lucy Muganza anakuja
Tanzania.Mwanamke Yule
tajiri alikuwa anatumiwa na
mataifa makubwa ya nje
kwanza kwa ajili ya kutaka
kuisambaratisha jumuiya ya
Afrika mashariki na pili
kuleta machafuko nchini
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo ili mabeberu hao
wanaomtumia waweze
kupata nafasi ya kuendelea
kuchota rasilimali.Mimi na
wenzangu ndiyo tuliofanya
tukio lile.We killed her.”
Akasema Gosu Gosu na
Agatha akamtazama kwa
mshangao.
“Najua nimekustua
Agatha lakini ni kweli mimi
na wenzangu ndiyo
tuliomuua Lucy
Muganza.Mwanamke Yule
alikuwa hatari sana kwa
nchi yetu na jumuiya ya
afrika Mashariki.Kuna
mpango mkubwa
unaandaliwa na nchi kubwa
kwa ajili ya kusambaratisha
jumuiya ya Afrika
Mashariki.Mpango
unaandaliwa pia kwa ajili ya
kuiondoa madarakani
serikali ya jamhuri ya
kidemokrasi ya Congo na
Lucy Muganza ndiye
aliyekuwa ameandaliwa kwa
ajili ya kushika nafasi ya
Rais wa Congo.Baada ya
kugundua mpango huo
ikatulazimu kumuondoa na
kitendo hicho kimeleta
mtafaruku mkubwa
sana.Kuna vita kubwa ya
chini chini inaendelea hivi
sasa baada ya Lucy Muganza
kuuawa.Umoja wa Ulaya
wanataka wachunguzi wa
kimataifa waweze kuingia
nchini kufanya uchunguzi wa
kifo hicho.Kikubwa
wanachokitafuta hapa ni
ushahidi wa kumuhusisha
Rais wetu na mauaji
hayo.Ulifanya jambo la
kizalendo sana kutowapa
rekodi za mazungumzo kati
ya Rais wetu na Rais Patrice
Eyenga.Naamini walikuwa
wanazitafuta sana taarifa
hizo lakini tumechelewa
kwani tayari wamekwisha
zipata kupitia flashi ile
uliyompa balozi Benjamin
usiku huu”akasema Gosu
Gosu
“Hapana bado
hawajazipata.Nilipogundua
kilichomo ndani yake nilifuta
rekodi zile na kupandikiza
kirusi katika ile flashi
nadhani baada ya kugundua
nilichokifanya ndipo
walipoanza kunitafuta
waniue”akasema Agatha
“Ulifahamu fika kwamba
wangegundua ulichokifanya
lakini bado ukafanya.Kwa
nini?Ulijiamini nini?
Akauliza Gosu Gosu
“I have money.Lot’s of
money hivyo nilikuwa
nimejiandaa kesho niondoke
zangu nchini.Tayari nilikuwa
na tiketi za ndege kwa ajili
ya kuelekea nchini China”
“Agatha unadhani Tamar
kiongozi wako anashirikiana
na balozi Benjamin kwa ajili
ya fedha au kuna jambo
lingine?
“I think it’s more than
money.Baada ya kunielezea
kile kinachoendelea hivi sasa
hapa nchini nimeanza
kupata picha kamili kuhusu
Tamar.There’s must be
something bigger than
money.Ili kujua
kinachoendelea kati yao
lazima kwanza
mumchunguze
Tamar”akasema Agatha.
“One more thing”
akasema Agatha na kutulia
kidogo
“Sikumpa balozi
Benjamin ile flashi
niiyotumwa nimpelekee
lakini haina maana kwamba
hataweza kupata zile rekodi
kwa kuwa bado zipo katika
hifadhi za SNSA.Ili
kujihakikishia kwamba Rais
yuko salama katika hili
tunapaswa kuharibu mfumo
mzima wa kuhifadhi
kumbukumbu za SNSA na
vile vile……….” Akanyamaza
kidogo
“Endelea Agatha
“Kuipata kompyuta ya
Tamar.Kila jioni huhifadhi
rekodi zote nilizozipata kwa
siku katika faili maalum
ambalo tunaoweza
kulifungua ni mimi na
Tamar pekee na faili hilo
limeunganishwa na
compyuta ya Tamar na
anaweza akalifungua hata
akiwa mbali na ofisi yake”
akasema Agatha na
kunyamaza baada ya Austin
kuingia mle ndani.Agatha
akaonyesha woga kidogo
“Agatha huyu anaitwa
Austin January ni mkuu wa
kikosi cha jeshi cha
operesheni maalum na ndiye
kiongozi wangu.Mimi na yeye
tunashirikiana katika yale
niliyokueleza na huyu ndiye
kiongozi wangu” Gosu Gosu
akafanya utambulisho na
kisha akamueleza Austin
yale yote aliyoelezwa na
Agatha.
“Dah ! Pole sana Agatha
na hongera pia kwa ujasiri
mkubwa uliouonyesha.Hapa
ulipo uko sehemu salama
kabisa na mimi na wenzangu
tunakuahidi kukulinda kwa
kila namna
tunavyoweza.Ahsante sana
kwa kutupa taarifa hii
muhimu.Kwa sasa kitu
ambacho tunatakiwa
kukifanya kwa haraka ni
kuharibu hilo faili ambalo
umekuwa ukihifadhi rekodi
zote za mazungumzo ya simu
ya Rais”akasema Austin
“Ili kuharibu faili hilo
ninapaswa kuharibu mfumo
wote wa SNSA.Ninaweza
kupandikiza kirusi katika
mfumo huo na kuuharibu
lakini nina hofu yawezekana
hadi sasa tayari nitakuwa
nimekwisha ondolewa katika
mfumo na sintakuwa na
uwezo wa kuingia na
kufanya chochote.We need
someone from inside”
akasema Agatha
“Kuna mtu yeyote
unayemuamini anayeweza
kukusaidia bila kuhatarisha
maisha yako? Akauliza
Austin.Agatha akafikiri
kidogo na kusema
“Kuna kijana mmoja
anaitwa Samson.Huyu
nimekuwa nikimsaidia na
kumfundisha mambo
mengi.Anaweza akanisaidia”
“Good.You can call him”
akasema Austin na kumpatia
simu yake akapiga
“Hallow ! ikasema sauti
ya kiume upande wa pili
“Hallo Sam it’s me
Agatha.Where are
you?akauliza Agatha
“Niko barabarani
ninaelekea nyumbani.Agatha
nini kimetokea leo?Ujumbe
umesambazwa kwamba
kuanzia sasa wewe ni mtu
hatari sana kwa idara na
yeyopte atakayekuona au
kujua mahala ulipo atoe
taarifa haraka
sana.Umefanya nini?
“Samson sina muda wa
kueleza kwa sasa ila kuna
jambo kubwa linaloendelea
hapo katika idara
yetu.Nitakueleza siku
nyingine,kwa sasa
nimekupigia nahitaji msaada
wako” akasema Agatha
“What do you
need?akauliza Samson
“I need access to our
system”
“What?Are you Crazy
Agatha? How can you access
the system? Tayari
umekwisha ondolewa katika
mfumo nakushauri tafadhali
huko uliko endelea kujificha
kwani ukijaribu kufanya
chochote watajua mahala
ulipo”
“Sikiliza Samson.Nataka
unisaidie niingie katika
mfumo kwa kupitia akaunti
yako.Kuna mambo nataka
niyafanye ambayo kama
nisipoyafanya yataniletea
matatizo makubwa.Samson
ni wewe pekee
ninayekutegemea kwa sasa
unisaidie katika
hili.Nimekuwa msaada
kwako kwa muda mrefu sasa
ni wakati wako
kunisaidia.Please Samson I
need help” akasema
Agatha.Zilipita sekunde
kadhaa Samson akasema
“Agatha unaniweka
katika hatari kubwa.Hata
hivi nnavyozungumza nawe
ni hatari kubwa kwani
wanaweza wakajua”
“Samson please.Help me”
akasema Agatha
“What do you want me to
do?
“I need you to go back
there to the server room and
I’ll direct you what to do”
akasema Agatha
“Sawa Agatha naomba
unipe dakika kumi nirejee
ofisini nitakupigia
nikishafika”
“Ahsante sana Sam and
I’m so sorry for this.Sina mtu
mwingine wa kumkimbilia
zaidi yako” akasema Agatha
“Usijali Agatha”
“Sam jambo lingine
naomba usilitaje jina langu
utakapokuwa unazungumza
na mimi ili watu
wasijue.Sitaki kukuweka
katika matatizo”
“I’m already in touble
anyway” akasema Samson na
kukata simu kisha Agatha
akaelekea chumbani
kuchukua kompyuta yake
Baada ya muda mfupi
Agatha akarejea akiwa na
kompyuta yake akaiwasha
akajaribu kuingia katika
mfumo wa SNSA lakini
namba alizoingiza hazikuwa
sahihi
“Nilijua tu tayari
nimekwisha fungiwa”
akasema Agatha
“Agatha wakati
tunamsubiri Samson afike
ofisini nataka kumfahamu
vizuri huyu Tamar.Umekuwa
naye karibu hadi akakuamini
kufanya kazi ya hatari kama
hii ya kudukua mawasiliano
ya Rais.Nataka kumfahamu
ni mtu wa aina gani?Austin
akauliza
“Ni kweli nimekuwa na
ukaribu na Tamar na
hakuona mtu mwingine wa
kumpa kazi ile zaidi yangu
na nimeifanya kwa uaminifu
mkubwa kuhusu Tamar ni
mtu msiri sana.Ni mtu
mwenye kuchukua tahadhari
kubwa kila wakati.Hapendi
mambo yake binafsi
yajulikane.Anaishi peke yake
na mfanyakazi wake
hajawahi kuzungumzia
chochote kuhusu kuwa na
familia…” akanyamaza
Agatha baada ya simu ya
Austin kuita
“Samson” akasema
Austin na kumpatia simu
Agatha
“Hello Sam” akasema
Agatha
“Tayari nimefika.Nipe
maelekezo unayotaka”
akasema Samson kwa sauti
ndogo
“Good.Nataka unipe
namba za kufungulia akaunti
yako” akasema Agatha na
Samson akampa namba zake
Agatha akaifungua akaunti
ya Samson halafu akaenda
hadi katika faili lile
anakohifadhi rekodi zote za
Rais akajaribu kulifuta
lakini Samson hakuwa na
uwezo wa kulifuta faili lile
ambalo waliokuwa na uwezo
wa kuingia na kulifuta ni
Agatha na Tamar pekee
“Nimejaribu kuingia
katika mfumo kwa kutumia
akaunti ya Samson lakini
imeshindikana kulifuta
faili.Only one option left.To
destroy the whole system”
akasema Agatha
“Do it”akasema Austin
na Agatha akapandikiza
kirusi katika mfumo wao na
mara tu Samson
alipoufungua ujumbe wenye
kirusi kile kikaanza
kusambaa kwa haraka
katika mfumo na ndani ya
muda mfupi mfumo wote
ukasambaa kirusi na kuanza
kuleta mauza uza.
“Done” akasema Agatha
na kuifunga akaunti ya
Samson na
“Samson nakushukuru
sana kwa msaada
wao.Nitakutafuta nikueleze
nini kilichonitokea”
“What have you done?
akauliza Samson
“Get out of there now
Samson” akasema Agatha na
kukata simu
“Nimemaliza.Mfumo
wote umeharibika
kinachofuata ni kuitafuta
kompyuta ya Tamar ambayo
lazima itakuwa na hifadhi ya
zile rekodi” akasema Agatha
“This is another
mission.Hakuna kulala usiku
huu wa leo lazima
tuhakikishe kwa namna
yoyote ile tuanipata
kompyuta ya Tam……….”
akasema Austin na
kunyamaza baada ya Stanley
kutokea alikuwa anahema
kwa kasi
“Stanley kuna
nini?akauliza Gosu Gosu
“Limetokea shambulio
katika ukumbi walimo akina
Nasib.Nikiwa nafuatilia
kilichokuwa kinaendelea
ukumbini mle kupitai
kamera ya Nasb waliingia
watu wapatao sita wakiwa
wamefunika nyuso zao na
kuanza kumimina risasi
hovyo.Sijaweza tena kupata
pich a nyingie kwani
mawasiliano na Nasibu
yamekatika” akasema
Stanley na Austin
akachukua simu na kupiga
namba ya Nasib simu
ikaanza kuita lakini
haiupokelewa.Akapiga tena
lakini haikupokelewa.Wote
wakabaki wamesimama
wakitazamana.
“We need to go back
there” akasema Austin
“Austin mahala pale ni
hatari sana kwa sasa” `
“I have my men in there.I
need to g………..” Austin
akanyamaza baada ya simu
yake kuita alikuwa ni
Nasib.Austin akaipokea
haraka haraka
“Nasibu mambo
yanakwendaje huko?
“Mkuu …” akasema
Nasibu akihema kwa nguvu.
“Nasibu nini kimetokea
hapo?akauliza Austin
“Something happened
here”
“Nini kimetokea?Nieleze
tafadhali”
“balozi Benjamin
ameuawa”
“What?Austin akastuka
“Balozi Benjamin
ameuawa”
Austin akashusha pumzi
na kuuliza
“Nasib tafadhali naomba
unieleze kama taarifa hizo ni
za kweli”
“Kweli kabisa
mkuu.Balozi Benjamin
amefariki.Ameuawa muda
mfupi uliopita”
“Kauawa?Nani
kamuua?akauliza Austin
“Wakati sherehe
zikiendelea waliingia watu
sita wakiwa na silaha huku
wakiwa wamefunika nyuso
zao wasionekane.Walianza
kumiminia watu risasi hovyo
hovyo na kuwaua.Balozi
Benjamin alikuwa mmoja wa
watu waliopigwa risasi kwa
haraka sana baada ya watu
wale kuingia ukumbini na
akafariki pale pale.Mimi
nilikuwa sehemu ya juu
hivyo niliweza kuona
kilichokuwa kinaendelea
upande wa chini.Nilimuona
jamaa mmoja akimfuata
balozi na kuanza
kummiminia risasi ili
kuhakikisha amekufa kabisa
halafu akamvua saa ya
mkononi,akamsachi mfukoni
na kuchukua vitu
fulani.Inaonekana
waliyekuwa wamemlenga ni
balozi Benjamin kwani baada
tu ya kuhakikisha amekufa
wakaondoka zao”
“Wewe na vijana wengine
wote mko salama?
“Wote tuko salama
kabisa mkuu.Mimi nilikuwa
upande wa juu nikajificha
katika nguzo huku
nikishuhudia kilichokuwa
kinaendelea upande wa
chini.watu wengi wameuawa
hapa lilikuwa ni tukio la
kinyama sana.Wenzangu
waliokuwa upande wa nje
wanasema kwamba watu
wale waliondoka kwa
kutumia magari mawili
ambayo hayakuwa na namba
huu wakipiga risasi
hovyo.Tukio hilo limetokea
haraka sana na hatukuweza
kufanya chochote”
“Poleni sana
Nasib.Hakuna mnachoweza
kufanya hapo kwa
sasa.Rudini hapa nyumbani
tujipange”akasema Austin na
kukata simu
“Balozi Benjamin
ameuawa”akasema Austin
“Mungu wangu !
akasema Agatha
“Kwa mujibu wa Nasib
kuna watu sita waliokuwa na
silaha wameingia ukumbini
nak uanza kuwafyatulia
watu risasi hovyo na balozi
alikuwa mmoja wa watu wa
mwanzo kushambuliwa kwa
risasi.Kuonyesha kwamba
balozi ndiye aliyekuwa
amelengwa mmoja wa
washambuliaji alimfuata na
kummiminia risasi
kuhakikisha wanamuua
kabisa”akasema Austin
“Haya lazma ni mauaji
ya kupangwa na
ninakubaliana na Austin
kwamba aliyekuwa mlengwa
hapa ni balozi
Benjamin.Nani anaweza
kuwa amefanya mauaji
haya?akauliza Gosu Gosu
“Ni vigumu kwa sasa
kujua nani aliyepanga
mauaji haya lakini sababu
kuu ilikuwa ni kumuua
balozi Benjamin”
“Wameturudisha nyuma
sana.Tayari tulikwisha anza
kupata mwangaza lakini kifo
cha Benjamin kimeuzima
mwangaza ule”akasema
Gosu Gosu
“Natakiwa kumpigia
simu Rais kumjulisha
kuhusu jambo hili” akasema
Austin na kumpigia simu Dr
Fabian
“Austin habari za usiku
huu?
“Habari si nzuri sana
mheshimiwa Rais.Kuna
tukio limetokea usiku huu
muda mfupi uliopita.Balozi
Benjamin ameuawa akiwa
katika hafla ya uchangiaji
ujenzi wa mabweni ya watoto
waishio katika mazingira
magumu”
“Ameuawa? Dr Fabian
akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Balozi Benjamin
ameuawa.Ukumbi ulivamiwa
na watu wasiojulikana
waliofunika nyuso zao
wakaanza kumimina risasi
ukumbini na kuua watu
hovyo.Balozi Benjamin na
mke wake wameuawa na
inaonekana wao walikuwa
walengwa wakuu wa
shambulio kwani baada ya
kuhakikisha wamefariki
dunia wauaji hao
wakaondoka zao”akasema
Austin ukapita ukimya mfupi
“Mheshimiwa Rais”
akaita Austin
“Austin nimestushwa
sana na taarifa hizo.Wewe
ndiye wa kwanza
kunijulisha.Nitawasiliana na
vyombo vya ulinzi kupata
taarifa kamili ya nini
kimetokea hapo na watu
wangapi wameuawa.Kuna
chochote mlichokuwa
mmekipata kabla ya balozi
kuuawa?akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais,kuna
jambo tulikuwa tumelipata
na tunaendelea kulifuatilia
tutakapolikamilisha nitakuja
kukufahamisha” akasema
Austin
“Austin hakikisha
mnawajua nani waliomuua
balozi Benjamin kwani suala
hili linaonekana ni kubwa
zaidi ya tunavyodhani”
akasema Dr Fabian
“Sawa mheshimiwa
tutafanya hivyo” akajibu
Austin na Dr Fabian akakata
simu Austin akamgeukia
Gosu Gosu
“Rais anataka tuwapate
waliomuua balozi
Benjamin.Sehemu pekee ya
kuanzia uchunguzi wetu
kuwafahamu waliomuua
Benjamini ni kwa
Tamar.Nina uhakika kubwa
anaweza kuwa na mahusiano
na mauaji hayo”akasema
Austin
“Kwa nini Tamar ahusike
katika kumuua balozi
Benjamin ambaye ni
mshirika wake mkubwa?Kwa
maelezo ya Agatha picha
tunayoipata ni kwamba
rekodi zile alizokuwa
anazikusanya Tamar
alikuwa anazipeleka kwa
balozi Benjamin na nina
uhakika kwamba fedha
alizokuwa akilipwa Agatha
zilitoka kwa
Benjamin.Tamar naye lazima
alikuwa akipata fedha nyingi
sana kwa ajili ya kazi
hiyo.Kama alikuwa
akifaidika wa kudukua
mawasiliano ya Rais kwa
nini ashiriki kumuua mtu
aliyekuwa anamuuzia taarifa
hizo? Akauliza Gosu Gosu
“Hata mimi napata
shaka kama Tamar anaweza
kuhusika na mauji hayo
lakini tukirejea katika
taarifa ya Nasib ni kwamba
watu wale walipoingia tu
Benjamin alikuwa ni mtu wa
mwanzo kulengwa risasi na
kuonyesha kwamba
walimlenga yeye mmoja wa
wauaji alimfuata
akamuongeza risasi na kisha
akamvua saa ya mkononi
halafu akampekua na
kuchukua kila kitu
alichokuwa nacho na hii ina
maanisha kwamba ile flashi
aliyopewa na Agatha
wameichukua hawa
wauaji.Kwa picha hii
inaonyesha wazi kwamba
wauaji walifahamu fika
kwamba balozi Benjamin
anatumia saa ya mkononi
katika kuwasiliana pili
walifahamu kuhusu flashi
aliyopewa na
Agatha.Aliyepanga mauaji
haya ni mtu ambaye
anamfahamu vizuri sana
Benjamin Hudson na katika
watu ambao lazima
tuwachunguze Tamar ni
mmoja wao” akasema Austin
na kunyamaza baada ya
simu yake kuita alikuwa ni
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais”
akasema Austin
“Austin nimepata taarifa
sasa hivi kwamba nyumba ya
balozi Benjamin inawaka
moto hivi sasa.Unadhani
moto huo unaambatana na
tukio la kuuawa kwake?
“Nahisi hivyo
mheshimiwa rais kwani
muda wa kutokea kwa
matukio haya mawili
umekaribiana
sana.Nalazimika kuamini
kwamba waliomuua
Benjamin ni hao waliochoma
nyumba yake”
“Mpaka sasa kuna lolote
mmekwisha lipata kuhusu
mauaji hayo?akauliza Dr
Fabian
“Mpaka sasa bado
hatuna fununu zozote lakini
tunajipanga kuanza
uchunguzi wetu” akasema
Austin
“Taarifa niliyoipata
kutoka kwa mkuu wa jeshi la
polisi ambaye yuko eneo la
tukio ni kwamba mpaka sasa
watu hamsini na sita
wamefariki dunia na
wengine wamekimbizwa
hospitali na kuna uwezekano
idadi ya vifo
ikaongezeka.Tafadhali
fanyeni juu chini kuweza
kujua aliyemuua balozi
Benjamin” akasema Dr
Fabian akakata simu
“Nyumba ya balozi
Benjamin inawaka moto
ndiyo taarifa aliyonipa Rais”
akasema Austin
“Dah ! akasema Gosu
Gosu.Taarifa ile
ilimshangaza sana
“Hata mimi nalazimika
kuamini kwamba
walioichoma nyumba ya
Benjamin ni wale wale
waliomuua.Swali
ninalojiuliza kama kumuua
tu haikutosha kwa nini
wakaenda kuichoma nyumba
yake kuna nini hapa
wanakificha?akauliza Gosu
Gosu
“Swali hilo ndilo
tunatakiwa kulitafutia
majibu.Agatha tuelekeze
tafadhali nyumbani kwa
Tamar.Suala hili haliwezi
kusubiri.Tunaanza
kumfuatilia usiku huu huu”
akasema Austin
PARIS – UFARANSA
Milio ya wadudu ndiyo
iliyotawala usiku huu katika
sehemu tulivu kuzunguka
ziwa dogo ambako Peniela na
mpenzi wake Nahum
walikwenda
kupumzika.Angani kulikuwa
na mbalamwezi kali
ikimulika na wapenzi hawa
walikuwa wamekaa nje
katika kibaraza huku moto
wa kuni ukiwaka mbele
yao.Walinzi wa Peniela
walikuwa wamejipanga
mbali kidogo kuwapa
wapenzi hawa nafasi ya
kuwa peke yao.
“Peniela kwa muda huu
mfupi niliokutana nawe
ninakiri kwamba nimeishi
maisha yangu yote hata
nikifa leo sina wasi
wasi.Nimeipata ile furaha
yote ya maisha yangu
niliyoihitaji” akasema
Nahum
“Nahum mpenzi una nini
leo?Kutwa nzima ya leo
umekuwa ukizungumzia
masuala ya kufa”akasema
Peniela
Nahum akatabasamu na
kuuchukua mkono wa
Peniela akambusu kiganjani.
“Maisha haya ni mafupi
sana Peniela.Ukipata nafasi
ya kufurahi itumie
kikamilifu kwani huwezi
kujua nini kinafuata mbele
yako.Kifo kimetuzunguka
kila mahali” akasema
Nahum
“Nahum sitaki kusikia
ukizungumzia habari ya kifo
tena.Tumekuja hapa
kufurahi na si
kuhuzunika.Kifo kipo na sote
tutakufa hivyo tusiongelee
masuala hayo kwa sasa”
akasema Peniela
“Sawa malaika
wangu,lakini naomba
ufahamu wewe ni
mwanamke wa pekee kabisa
ambaye sijawahi kukutana
naye katika maisha
yangu.Naomba nikiri jambo
moja kwako”
“Nakusikiliza” akasema
Peniela huku akitabasamu
“Kwa muda mrefu
nimekuwa mchezeaji tu
wanawake na sikuwahi
kupenda.Nimekutana na
wanawake wengi na ……..”
Nahum akanyamaza baada
ya mmoja wa walinzi wao
kutokea akikimbia
“Ingieni ndani
harak……..” Hakumaliza
alichokuwa anawaeleza
akina Peniela
akapigwa risasi ya mgongo
akaanguka chini.Kwa kasi ya
aina yake Nahum akaruka
kutoka mahala alipokuwa
amekaa akamrukia Peniela
wakaanguka chini ya kiti.
“Peniela nisikilize.Watu
hawa wananitafuta mimi
wamekuja kuniua hivyo
kama nikifa nakuomba
umtafute Mathew
Mulumbi.Yuko hai”
“Nahum !! akasema
Peniela
“Nisikilize
Peniela.Mathew Mulumbi
yuko hai.Tafadhali mtafute”
akasema Nahum na
kusimama akitaka kukimbia
akapigwa risasi tatu na
kuanguka chini akafa pale
pale.
Peniela mwili
ulimtetemeka alikosa nguvu
akabaki amejificha chini ya
kiti.Baada ya dakika tano
kupita akasikia sauti
ikimuita
“Mama Peniela ! Mama
Peniela ! ilikuwa ni sauti ya
mmoja wa walinzi
wake.Peniela hakuweza
kufungua mdomo wake
kuitika.Walinzi wale
walikuwa na tochi
wakamulika eneo lile ambalo
liikuwa giza baada ya taa
kupasuliwa wakamuona
Peniela akiwa amejificha
chini ya kiti.Hatua chache
mbele yake alilala Nahum
akiwa hana uhai.Mmoja wa
walinzi wale akamfunika
Peniela koti kisha
wakamuinua na kumpeleka
katika gari wakaondoka kwa
kasi eneo lile wakipishana na
magari ya askari
waliojulishwa kuhusu
kutokea kwa mauaji yale.
“Nini kimetokea?Nani
kafanya mauaji yale?Peniela
akawauliza walinzi wake
“Mpaka sasa hatujui nani
kafanya mauaji yale lakini
nilichokishuhudia mimi ni
watu waliovaa makoti
marefu na kufunika nyuso
zao wakiwa na bunduki za
kulenga masafa marefu
wakitoweka katika
msitu.Usihofu mama
tutachunguza na tutajua ni
nani waliofanya tukio lile”
akasema mmoja wa walinzi
“Hivi ni kweli Nahum
amekufa au niko
ndotoni?akajiuliza Peniela na
kuendelea kumwaga machozi
,akakumbuka namna
alivyomuona Nahum
akipepesuka huku
akichakazwa risasi
“Huu ni mkosi gani
unanikuta mimi?Kila
mwanaume ambaye
ninakutana naye na moyo
wangu ukampenda
hadumu.Mathew alipotea na
sasa Nahum”akawaza na
kuendelea kulia
TEL AVIV – ISRAEL
Simu ya Efraim Dagan
aliyekuwa na maafisa
wengine wa Mossad pamoja
na maafisa wa gereza ambalo
Mathew Mulumbi
alifungwa,ikaita akatoika nje
na kuipokea
“Hallow” akasema
Efraim
“Mkuu tumeimaliza
kazi.Nahum tayari amekufa”
“Kazi nzuri sana.Mna
hakika hakutakuwa na tatizo
lolote?
“Tumemuondoa
kiumakini sana hakutakuwa
na tatizo lolote hata hivyo
tulilazimika kuwaua pia
walinzi wachache wa Peniela
ndipo tukaweza kumfikia
Nahum”
“Ahsanteni sana kwa
kazi hii nzuri” akasema
Efraim na kukata simu
“Nahum alikuwa ni
mmoja wa watu wetu wa
muhimu sana lakini
alichagua mapenzi akasahau
kazi na hivyo kuhatarisha
maisha yake mwenyewe na
ya shirika.Amekipata
alichokihitaji” akawaza
Efraim na kurejea ndani
walikuwa wanaendelea
kufuatilia kile
kinachoendelea chumbani
alimo Mathew Mulumbi na
Ammar Nazari
“Ammar muda
umewadia.Nataka kupata
tena uhakika kutoka kwako
kama uko tayari kuendelea
na mpango wetu wa
kutoroka” akasema
Mathew.Ammar akawaza
kidogo halafu akasema
“Tuendelee na mpango
wetu Abu.Ninataka
kuondoka humu ndani”
akasema Ammar
“Safi sana.Kila kitu
kitakwenda kama
tulivyopanga” akasema
Mathew na Ammar akatikisa
kichwa kukubaliana naye
halafu Mathew akalala
sakafuni kama mtu
aliyepoteza fahamu.Ammar
akasogea karibu na mlango
akanyoosha mkono na
kubonyeza kitufe cha kengele
ya dharura.
“Mambo yameanza”
akasema Efraim akiwa
katika ofisi ya mkuu wa
gereza.
Askari wawili wa gereza
walifika katika mlango wa
chumba cha akina Mathew
na kuuliza kuna nini,Ammar
akawajulisha kwamba
mwenzake Abu ambaye ni
Mathew ameanguka ghafla
na kupoteza fahamu.Mlango
ukafunguliwa na askari wale
wakaingia ndani,Ammar
akatakiwa kusogea kwenye
kona wakati askari mmoja
akienda kumtazama
Mathew.Akammulika tochi
machoni halafu akapiga
magoti ili aweze kumtazama
vizuri mara kwa kasi ya
ajabu akajikuta amedakwa
shingo yake akageuzwa na
kuangushwa chini akataka
kuinuka lakini akapigwa
ngumi nzito akalala
sakafuni.Lilikuwa ni tukio
lililotokea kwa kufumba na
kufumbua.Mara tu Mathew
alipomvamia askari Yule
aliyekuwa
anamuangalia,askari
aliyekuwa na Ammar
akageuka kutazama nini
kimetokea ndipo Ammar
akamrukia kama Simba
anayerukia windo akampiga
kichwa kizito akaanguka
chini halafu akaiokoa
bunduki akampiga na kitako
kichwani akamuinua na
akamkaba na kumvunja
shingo kisha akamtupa chini
“Nimeingia kwenye
ulimwengu wa makatili”
akawaza Mathew.Ammar
akachukua mto akaukunja
halafu akachukua bastora ya
Yule askari aliyekuwa
amedhibitiwa na Mathew
akamuwekea kichwani
akaachia risasi na
kumfumua kichwa.
“Tulipanga kutokuua
askari lakini huyu jamaa
ameamua kuua.Nikimzuia
anaweza akaingiwa na
mashaka” akawaza Mathew
na haraka haraka
wakawavua sare wale askari
wakavaa na kuchukua redio
ya mawasiliano pamoja na
kadi ya kufungulia
milango.Wakawaficha askari
wale chini ya kitanda
“Uko tayari?akauliza
Mathew
“Niko tayari” akajibu
Ammar.Mathew akachukua
ramani ile ya gereza
wakaipitia kisha wakatoka
kwa tahadhari wakafunga
mlango.
“Tulikubaliana kutokuua
askari.Mbona wameua askari
wangu?akafoka mkuu wa
gereza.
“Kama Mathew
angemzuia Ammar kutokuua
wale askari angeweza
kuingiwa na wasi wasi ndiyo
maana akaamua kumuacha
awaue”akajibu Efraim
Mathew na Ammar
wakifuata ramani ile
waliyopewa walipita korido
la kwanza halafu wakatokea
katika ngazi wakapanda na
kutokea katika korido la
pili.Kwa mbele wakawaona
askari wakajibanza
wakasubiri askari wale
wapite halafu wakatembea
haraka haraka wakakuta
kuna njia mbili wakafuata
njia ya kushoto wakaifuata
njia ile na mara tu
walipolifikia geti la kwanza
king’ora cha hatari
kikalia.Askari wakaanza
kukimbia kwenda kujua nini
kimetokea.Walipitisha kadi
katika geti lile la kwanza
likafunguka wakavuka na
kukimbia hadi katika ujia
ambao walikuta askari
watatu wakikikimbia
,Ammar akawamiminia
risasi.Mathew akaitazama
ramani akakuta lazima
waruke ukuta kuingia
upande wa pili haraka
haraka akamtaka Ammar
kuinama akapanda juu ya
mgongo na kushika kingo za
ukuta kisha akamvuta
Ammar naye akapanda
wakajirusha upande wa
pili.Walikwaruzwa na
seng’enge zilizokuwa juu ya
ukuta.Mathew akainuka na
kumtaka Ammar waendelee
baada ya kusikia katika
redio kwamba wafungwa
waliotoroka wamevaa sare za
askari.Mathew akiwa
ametangulia mbele mara
ghafla wakamulikwa na tochi
zenye mwanga mkali na
kutakiwa kusimama.Kwa
kasi ya aina yake Mathew
aliyekuwa ametangulia
mbele akajitupa chini na
Ammar akamimina risasi
askari watatu wakaanguka
chini kisha wakakimbia
kuelekea katika geti la
pili.Wakati Mathew
akijandaa kufungua geti lile
mara Ammar akatoa mguno
wa maumivu alikuwa
amepigwa risasi ya mguu
akaangua chini.
“Nimepigwa risasi ya
mguu !! akalalama
Ammar.Mathew akageuka
na kumimina risasi halafu
akamfuata Ammar
akamuinua na kumtaka
ajitahidi wamekaribia.
“Ammar jitahidi utembee
tunakaribia sana kufika
katika ule mfereji mkubw..”
akasema Mathew na risasi
zikaanza kuvuma akamkinga
Ammar na kuanza kumimina
risasi halafu akamuinua na
kuvuka geti mara Ammar
akapigwa tena risasi
nyingine ya mguu
ikamlazimu Mathew
kumuinua na kumuweka
begani
“Naona mambo yanaanza
kuwa magumu.Mpango
ulikuwa apigwe risasi moja
lakini amepigwa
mbili.Yawezekana kuna
askari ambao hawajui
kuhusu huu mpango wa
kutoroka.Kinachofuata kwa
sasa ni kuwafagia tu kila
atakayetukaribia kwani
tukifanya mchezo wanaweza
wakatumaliza hawa.”
Akawaza Mathew na mara
taa zikazima.Hii ilikuwa ni
ishara kwamba wanakaribia
kufika katika mfereji
mkubwa wa maji taka.Katika
mfuniko wa kuingilia katika
mfereji wa maji taka
kulikuwa kimya lakini
Mathew akageuka na
kumimina risasi kwa nyuma
kana kwamba kuna watu
walikuwa wanawafuatilia
halafu akamuweka chini
Ammar akalifungua geti
akambeba Ammar hadi
katika mfuniko.Akachana
shati lake na kumfunga
Ammar pajani halafu
akautafuta mfuniko
akauona.Ulikuwa ni mfuniko
mkubwa wa zege akajitahidi
kuusogeza pembeni
akashindwa
“Natakiwa kujitahidi
vinginevyo wakitukuta hapa
watatuua” akawaza Mathew
na kukusanya nguvu
akausukuma mfuniko ule
ukasogea akajitahidi tena
ukasogea zaidi akamulika
ndani na kuziona ngazi za
kushukia chini.Haraka
haraka akamfuata Ammar
akamsogeza pale kwenye
shimo na kuanza kumshusha
chini taratibu kisha
wakaanza kutembea katika
maji yaliyokuwa na
harufu.Baada ya dakika
kumi na moja wakazikuta
ngazi ambazo kwa mujibu wa
maelekezo aliyopewa
Mathew zinatokea
barabarani Mathew
akapanda na kuusukuma
mfuniko wa chuma
akachungulia nje ni kweli
walikuwa
barabarani.Akampandisha
Ammar na kuufunika
mfuniko ule wa chuma
akamtegemeza wakavuka
barabara wakaanza
kutembea hadi walipokuta
daraja wakaingia kwa chini
wakajificha
“Tuko nje ya gereza
sasa” akasema Mathew
“Ahsante sana Abu.Bado
naona kama ni ndoto”akajibu
Ammar akihisi maumivu
makubwa
“Si ndoto ni kweli kabisa
tuko nje ya
gereza.Kinachotakiwa sasa
ni kutafuta namna ili uweze
kupata matibabu kwanza
kuondoa risasi ambazo
umepigwa na pili
kuongezewa damu.Dr Abeba
atafika kutupeleka sehemu
salama”
“Unamuamini huyo
Abeba?akauliza Ammar
“Ndiye aliyetusaidia
tukafika hapa na ndiye
atakayetusaidia tuweze
kuondoka hapa Israel
salama” akasema Mathew na
magari kadhaa yakapita pale
juu ya daraja.
“Tutafute namna
nyingine ya kujiokoa huyo
mtu wako hawezi kuja
tena.Ninazidi kupoteza damu
nitakufa”akasema Ammar
akiwa katika maumivu
baada ya kusubiri kwa muda
bila Abeba kutokea
“Vuta subira
atakuja.Ninamtegemea yeye
kwa kila kitu” akasema
Mathew na kuendelea
kusubiri
Baada ya dakika kadhaa
likapita gari moja na kwenda
kusimama mbele kidogo ya
daraja halafu mlango
ukafunguliwa.Tochi
ikawashwa na kuzimwa
mara tatu kisha Mathew
akajitokeza.Alikuwa ni
Abeba.Wakasaidiana
kumbeba Amar
wakamungiza katika gari na
kuondoka
“Nashukuru sana Abeba
kwa msaada huu
mkubwa.Nadhani hii ni mara
ya kwanza watu
wanafanikiwa kutoroka
katika gereza lile” akasema
Ammar lakini Abeba
hakujibu kitu.Aliendesha
gari hadi nje kidogo ya mji
wakaingia katika shamba la
matunda kulikuwa na
nyumba wakaingia ndani na
bila kupoteza muda Abeba
akaanza kumshughulikia
Ammar.Wakafanikiwa kutoa
risasi mbili katika mguu
wake na kumuongezea damu
kwani Abeba alikuwa
amekwenda na akiba ya
damu.
Baada ya kumuhudumia
Ammar ikafuata zamu ya
Mathew akamganga
majeraha mbalimbali
aliyoyapata wakati akiwa
mle gerezani.
“Mnatakiwa kabla ya
mapambazuo muwe
mmeondoka hapa Israel
kwani picha zenu
zitasambazwa kila mahali
kwamba ni wahalifu na
mnatafutwa.Wapi mnaelekea
ili niwapeleke?akauliza
Abeba na Mathew
akamtazama Ammar
aliyekuwa amelala kitandani
“Naomba unisaidie simu
tafadhali” akasema Ammar
na Abeba akampa simu
Ammar akaandika namba na
kupiga.Simu ilipopokelewa
akazungumza na mtu na
kumpa maelekezo kadhaa
halafu akamuelekeza Abeba
sehemu ya kuwapeleka.
Chupa ya damu
ilipomalizika wakaingia
garini na safari ikaanza
kuelekea Ramallah huku
Ammar akimuelekeza Abeba
njia ya kupita kukwepa
vizuizi vya wanajeshi.Safari
ilikuwa ya kimya kimya na
baada ya mwendo wa saa
moja wakasimamishwa na
kundi la watu wenye
silaha.Mathew akaiweka
sawa bunduki yake lakini
Ammar akamzuia
“Hawa ni watu wangu
niliwaelekeza niwakute
hapa” akasema Ammar na
kumshukuru Abeba kwa
msaada mkubwa
aliowasaidia.Kundi lile la
watu wenye silaha
wakalisogelea gari lile na
Ammar akafungua mlango
akashuka.Watu wake
walipomuona wakambeba
huku wakishangilia na
kupiga risasi juu
“Be safe” Abeba
akamwambia Mathew
“Go now.This place is too
dangerous” akasema Mathew
na Abeba akageuza gari
akaondoka zake.Mathew
akabaki amesimama.Ammar
akapelekwa katika gari kisha
akaagiza Mathew aletwe
katika gari alimo na msafara
wa magari ukaondoka
eneolile huku watu
wakishangilia na kupiga
risasi juu
“Abu nashukuru sana
rafiki yangu.Bado sijaamini
kama niko nje ya gereza
lile.Siamini kama leo
ninakwenda nyumbani
kwangu.Sina namna nzuri ya
kukushukuru kwa msaada
huu mkubwa.Karibu sana
katika himaya
yangu.Eneolote hili ni la
kwangu” akasema Ammar
Abeba baada ya
kuwaacha akina Mathew
akasimamisha gari na
kusubiri huku akiwatazama
kupitia kiona mbali maalum
chenye uwezo wa kuona
kwenye giza akaona Mathew
akiingizwa katika gari alimo
Ammar na msafara wa
magari ukaondoka
akachukua simu na
kumpigia Efraim
“Mathew na Ammar
tayari wamekutana na
wanamgambo wa Ammar
Nazari Brigades
wamewachukua na
wameondoka”
“Kazi nzuri Abeba.Sasa
unaweza
ukarudi.Tumuombee Mungu
aweze kufanikisha mpango
wetu.Kwa namna
ulivyomuona Ammar
anawasi wasi wowote kuhusu
Mathew?
“Hana wasi wasi
wowote.Furaha yake
haielezeki”
“Safi sana.Hii ni bahati
nasibu tumecheza tuendelee
kusubiri” akasema Efraim