Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

Mkuu Kulubule shusha vitu acje muhusika akaja kama kipnd kile cha Kiapo......
 
SIRI
Episode 6
Mtunzi. Patrick CK

MIAKA MITATU ILIYOPITA
Kipindi cha asubuhi cha
maswali na majibu kilimalizika
katika bunge la jamhuri ya
muungano wa Tanzania.Maswali
yote yaliyopangwa kuulizwa siku
hii yalipata nafasi ya kuulizwa na
kutolewa majibu toka kwa
mawaziri husika.Kumalizika kwa
kipindi cha maswali kukampa spika
wa bunge Bi Bernadetha makawala
nafasi ya kusimama na kusema
machache ikiwa ni pamoja na
kutambulisha wageni muhimuwaliofika bungeni na kusoma
matangazo mbali mbali ya kazi .
Dakika takribani tano
alizitumia katika kusoma
matangazo ya kazi na
kuwatambulisha baadhi tu ya
wageni waliohudhuria kikao
hiki,halafu akamwita katibu wa
shughuli za bunge siku hiyo ndugu
Wilson ndendeki aweze kuliongoza
bunge kwa shughuli
inayofuata.Akasimama na kutamka
shughuli inayofuata
“Hoja binafsi za wabunge”
Baada ya kauli hiyo spika wa
bunge akasimama na kutoa
maelekezo mafupi.
“Waheshimiwa wabunge,leo
tutakuwa na hoja binafsi mbili.Ya
kwanza inatoka kwa mheshimiwa
mbunge Edger kaka inayohusu
kuliomba bunge kuunda kamati
teule kuchunguza ufisadi mkubwa
uliofanywa katika benki ya taifa ya
vijana na kupelekea benki hiyo
kufilisika.Hoja ya pili inatoka kwa
mheshimiwa mbunge Marewa
shawe inahusu uvunaji wa mazao
ya misitu katika msitu wa
Isambe.Kila mtoa hoja amepewa
muda usiozidi dakika sitini za
kuwasilisha hoja yake.Kwa kuwa
hatutakuwa na muda wa kutosha
wa kuanza kuzichangia hoja hii
katika kipindi hiki cha asubuhi basi tutakaporudi mchana tutaanza
moja kwa moja kuchangia katika
hoja zote mbili kwa pamoja.Kwa
maana hiyo mnatakiwa muanze
kujiorodhesha kuchangia hoja hizi
kuanzia sasa hivi ili tuone tutakuwa
na wachangiaji wangapi mpaka
mchana.Naomba sasa nimwite
mtoa hoja wa kwanza mheshimiwa
Edger kaka.Karibu sana
mheshimiwa” Spika akakaa katika
kiti chake tayari kwa kuanza
kuisikiliza hoja ya mheshimiwa
mbunge Edger,mmoja kati ya
wabunge vijana machachari mno
Bunge lote lilikuwa kimya
kabisa wakimsubiri mhesimiwa
mbunge ainuke.Edger alikuwa ameinamia meza yake bila kustuka
hali inayomlazimu spika kusimama
tena.
“Mheshimiwa
mbunge,tafadhali karibu uwasilishe
hoja yako”
Pamoja na mwito ule wa spika
bado Edger alikuwa ameinamia
meza yake.Wabunge wote
wakageuza vichwa vyao
kumuangalia mheshimiwa mbunge
yule kijana huku wengine
wakidhani labda amepitiwa na
usingizi.Minong’ono na vicheko vya
chini chini vikaanza kusikika..Spika
akasema “Waheshimiwa wabunge mlio
karibu naye hebu tusaidieni
kumstua hapo “
Mheshimiwa Salama awadh
mbunge wa viti maalum akainuka
na kwenda kumstua.Akamshika
bega na kumtikisa kidogo,lakini
bado mheshimiwa mbunge
hakuamka,akampiga piga
mgongoni lakini bado hakuonyesha
dalili zozote za kustuka ndipo
alipoamua kumuinua
kichwa.Nusura aanguke kwa
mstuko alioupata.Mheshimiwa
mbunge Edger hakuwa na
fahamu,alikuwa anakoroma,jasho
linamtiririka usoni na povu lilijaa
mdomoni.Taharuki ikatanda bungeni.Haraka haraka wabunge
waliokuwa karibu wakamuinua na
kumtoa nje kumkimbiza katika
zahanati ya bunge.Shughuli za
bunge zikasimama kwa muda.Kila
mtu alishangaa kwani asubuhi
alipoingia bungeni mheshimiwa
mbunge Edger alikuwa mzima wa
afya na alipata nafasi ya kuuliza
swali la nyongeza katika kipindi
cha maswali na
majibu,hakuonyesha dalili zozote
za ugonjwa.Hali iliyomtokea ilimpa
wasi wasi kila mtu mle bungeni.
“Waheshimiwa wabunge
naomba tukae…..” Ilikuwa ni sauti
ya mheshimiwa spika akiwataka
wabunge watulie na shughuli za bunge ziweze kuendelea.Bado
mazungumzo yaliendelea licha ya
mwito ule wa spika.
“Naomba utulivu ndani ya
bunge tafadhali….waheshimiwa
wabunge naomba tukae katika
sehemu zetu ili shughuli za bunge
ziendelee.”
Taratibu wabunge wakaanza
kurejea katika sehemu zao na
mazungumzo yakapungua.
“Waheshimiwa
wabunge,mwenzetu amepatwa na
matatizo ya ghafla na amepelekwa
katika zahanati yetu ya bunge kwa
huduma ya kwanza.Naomba tuwe
watulivu wakati mwenzetu
anapatiwa matibabu.Mtajulishwa kila kitu juu ya maendeleleo yake
baada ya uchunguzi wa kidaktari
kufanyika.Kwa sasa naomba
shughuli za bunge ziendelee.Kwa
kuwa mheshimiwa Edger ndiye
aliyekuwa awe wa kwanza
kuwasilisha hoja yake asubuhi hii
napenda sasa nimwite mheshimiwa
Marewa aweze kuwasilisha hoja
yake.Hoja ya mheshimiwa Edger
tutaipangia siku
nyingine.Mheshimiwa Marewa
karibu uwasilishe hoja yako”
akasema Spika **************
Zahanati ya bunge ghafla
iligeuka sehemu ya heka heka
.Madaktari wa bunge walikuwa
wakijitahidi kwa kila walivyoweza
kumpa huduma ya kwanza
mheshimiwa Edger wakisaidiana
na wabunge ambao ni
madaktari.Vipimo vya awali
vilionyesha kuwa shinikizo la damu
lilikuwa juu isivyo kawaida na hata
sukari ilikuwa imepanda
mno.Pamoja na jitihada zote za
madaktari wa bunge bado hali ya
mheshimiwa mbunge iliendelea
kuwa mbaya,ikamlazimu daktari mkuu wa bunge aamuru
mheshimiwa spika aitwe.
Akiwa mezani kwake huku
mheshimiwa mbunge Marewa
akiendelea kuwasilisha hoja
yake,mhudumu wa bunge
akampelekea ujumbe wa kumtaka
afike mara moja katika zahanati ya
bunge.Bila kupoteza hata sekunde
spika akawasiliana na mmoja wa
wenyeviti wa bunge akamtaka
ajiandae kuongoza kikao kile na
alipokuwa tayari Spika akasimama
na mheshimiwa aliyekuwa
akiendelea kuwasilisha hoja yake
akanyamaza na kwenda kukaa
akampisha spika wa bunge. “Waheshimiwa
wabunge,nimepata taarifa toka kwa
daktari wetu mkuu wa bunge
akinitaka nifike mara moja katika
zahanati yetu.Naomba nimuachie
mwenyekiti aweze kuendelea na
shughuli zilizobaki za
bunge”akasema Spika na kutoka
Kitu cha kwanza alichotaka
kufahamu mheshimiwa spika baada
ya kufika katika zahanati ya bunge
ni hali ya mheshimiwa
Edger.Daktari akamuomba
waongozane hadi katika ofisi yake.
“Daktari hebu nieleze hali ya
mbunge inaendeleaje?
Anasumbuliwa na kitu gani?
Akauliza mheshimiwa spika . “Mheshimiwa spika nimeona
nikuite nikueleze ukweli kwamba
hali ya mbunge si nzuri hata
kidogo.Vipimo vyetu vinaonyesha
kuwa shinikizo la damu liko juu
mno na hata sukari yake imepanda
sana.Mpaka sasa hivi bado
hatujaweza kufanikiwa kushusha
sukari wala shinikizo la damu.Hali
ya mbunge inaendelea kwa mbaya
hivyo nashauri haraka sana
tumuwahishe katika hospitali kuu
ya St Francis ili akachekiwe zaidi”
Huku uso wake ukionyesha
wasi wasi mheshimiwa spika
akaamuru haraka sana
mheshimiwa Edger ahamishiwe
katika hospitali ya St Francis.Ni kitendo ambacho hakikuchukua
hata dakika kumi tayari mbunge
alikwisha pakiwa katika gari la
wagonjwa na kukimbizwa St
Francis hospital.
Madaktari na wauguzi
walikuwa wamekwisha jiandaa
kumpokea mheshimiwa
mbunge.Walipigiwa simu na ofisi
ya bunge.Baada tu ya gari
kusimama Edger akashushwa
garini na kukimbizwa katika
chumba cha wagonjwa
mahututi.Mara moja akaanza
kupatiwa matibabu.Kwa zaidi ya
nusu saa juhudi zikaendelea za
kuhakikisha hali ya mheshimiwa
huyu kijana kipenzi cha wengi hatainaimarika lakini bado hali yake
ikaendelea kuwa mbaya na
kuwashangaza hata
madaktari.Mwishowe madaktari
wakafikia uamuzi wa
kumuhamishia mheshimiwa Edger
katika hospitali kuu ya magonjwa
ya moyo Tanzania Heart hospital
iliyoko jijini Dar es salaam.
****************
Kupitia matangazo ya moja
kwa moja yaliyokuwa yakirushwa
na vituo mbali mbali vya
televisheni na hata redio Taifa zima
liliweza kushuhudia na kusikia
moja kwa moja kilichotokea bungeni.Ulikuwa ni mstuko
mkubwa sana.Kutokana na ukuaji
wa teknolojia,kwa kipindi kifupi
sana idadi kubwa ya watu waliweza
kupata taarifa ya kilichojiri
bungeni. Kupitia mitandao ya
kijamii,simu za mikononi,blogu na
vyombo vingine vya upashanaji
habari taarifa ziliweza kuwafikia
watu kwa haraka mno.Taarifa
kubwa iliyokuwa ikizunguka katika
mitandano na jumbe za simu za
mikononi ni kwamba Mheshimiwa
Edger amefariki dunia
ghafla.Taarifa hii ilizua taharuki
kubwa katika jamii,taifa
likazizima.Watu wengi walikuwa na
mapenzi makubwa kwa mbunge huyu kijana.Mheshimiwa Edger
alipendwa na watu wa rika zote
bila kujali itikadi ya dini au
vyama.Wengi walikuwa na imani
kuwa muda utakapofika huyu ndiye
angeweza kuwa raisi wa Tanzania
na kuwakomboa watanzania katika
maisha duni waliyokuwa nayo.Hii
ilitokana na uzalendo wa kweli
aliouonyesha kijana huyu katika
kipindi kifupi.
Taarifa zikaanza kusambaa
tena kuwa mwili wa mheshimiwa
Edger ulikuwa njiani kusafirishwa
kwa ndege kuja Dar es
salaam.Makundi ya vijana
washabiki wake yakaanza
kukusanyika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ili
kuthibitisha kama taarifa zile za
kufariki Edger Kaka ni za kweli.

**************
Ndege iliyombeba
mheshimiwa Edger ilitua katika
uwanja wa kimataifa wa Julius
Nyerere.Kwa haraka mgonjwa
akashushwa na kupakiwa katika
gari la wagonjwa na kukimbizwa
katika hospitali kuu ya magonjwa
ya moyo Tanzania heart
hospital.Waandishi wengi wa
habari na wapiga picha walikuwa
wamejazana hapo uwanjani ili
kujaribu kupata walau habari na picha za tukio hili ambalo liliteka
hisia za watu wengi na
kuuhabarisha umma wa
watanzania uliokuwa ukisubiri
taarifa zenye uhakika kwa hamu
kubwa.
Gari la wagonjwa likiwa
limetanguliwa na piki piki ya polisi
liliondoka kwa kasi hapo uwanjani
na kuwaacha watu wakiwa kimya
na wengine wakiangua vilio
wakijua ni kweli mpendwa wao
mheshimiwa Edger amefariki
dunia.
Tanzania heart
hospital,ilikwisha taarifiwa juu ya
kuletwa kwa mheshimiwa mbunge
hivyo madaktari na wauguzi waliwekwa tayari ili pindi tu
mgonjwa atakapofika basi aanze
kushughulikiwa haraka
iwezekanavyo.Hopsitali hii ni moja
kati ya hospitali kubwa ya
magonjwa ya moyo katika ukanda
wa afrika mashariki,iliyosheheni
madaktari bingwa wa moyo.
Geti la kuingilia hospitali
lilikuwa wazi na gari lililombeba
Edger likapita kwa kasi
kubwa.Baada tu ya kusimama
,haraka haraka akashushwa na
kukimbizwa katika katika chumba
maalum cha wagonjwa
mahututi.Kazi ya kumuhudumia
ikaanza. Umati wa watu ulizidi
kuongezeka katika hospitali hii
kubwa wengi wakitaka kupata
uhakika wa afya ya mbunge wao na
kulazimu geti la hospitali kufungwa
na kikosi maalum cha askari polisi
kikafika ili kukabiliana na aina
yoyote vurugu inayoweza
kujitokeza.
Mpaka saa kumi na moja za
jioni bado hakukuwa na taarifa
zozote toka kwa madaktari juu ya
maendeleo ya mgonjwa.Saa kumi
na mbili za jioni mheshimiwa spika
wa bunge akawasili ,akafunguliwa
geti na kuingia ndani.Akiwa
ameongozana na baadhi ya
wabunge na maofisa wengine wa bunge waliweza kuingia hospitalini
hapo lakini taarifa aliyopewa ni
kwamba bado hali ya mheshimiwa
mbunge haikuwa nzuri.Spika na
ujumbe wake wakatoka humo
hospitali na kuondoka kwa sababu
hakukuwa na ulazima wa wao
kuendelea kuwepo hapo hospitali
wakati bado mgonjwa alikuwa
akipatiwa matibabu.
*****************
Saa mbili za usiku ,katika
hospitali kuu ya magonjwa ya moyo
katibu wa bunge akajitokeza mbele
ya waandishi wa habari waliokuwa
wamekusanywa katika chumba cha mikutano cha hospitali hiyo.Akakaa
kitini na chumba chote kikawa
kimya kabisa.
“Ndugu wandishi wa habari
nimewaiteni hapa ili kuwapa
taarifa fupi juu ya maendeleo ya
afya ya mbunge Edger Kaka
ambaye alipatwa na maradhi ya
ghafla katika kikao cha bunge
asubuhi ya leo.Alikimbizwa katika
zahanati ya bunge akapatiwa
huduma ya kwanza halafu
akakimbizwa katika hospitali ya
mkoa wa Dodoma na kutoka pale
akakimbizwa katika hospitali kuu
ya moyo.
“Mheshimiwa Edger
amepokelewa hapa katika hospitali kuu ya moyo na toka wakati huo
madaktari wamekuwa
wanamuhudumia.Napenda
kuchukua nafasi hii kukanusha
uvumi ulioenea na unaoendelea
kuenea kuwa mheshimiwa Edger
amefariki dunia.Taarifa ya ukweli
ni kwamba mheshimiwa mbunge
ni mzima japo anaumwa lakini
napenda niwatoe hofu watanzania
kuwa mbunge wetu atapona kwa
sababu anashughulikiwa na timu
kubwa ya madaktari bingwa wa
moyo.Kikubwa ninachowaomba
watanzania tuendelee kumuombea
ili Mwenyezi Mungu amjalie aweze
kupona haraka na arejee katika
majukumu yake ya kuwatumikia wananchi.Tutaendelea kuwajulisha
kila mara maendeleo ya hali
yake.Ahsanteni sana”
Akamaliza katibu wa
bunge,akainuka na kutoka humo
ukumbini huku waandishi wa
habari wakisimama kutaka kuuliza
maswali.
Katika chumba cha wagonjwa
mahututi alikokuwa anahudumiwa
Edger bado hali ya mheshimiwa
Edger haikuwa nzuri.Hili
lilimuumiza mno Dr Olivia Themba
mkuu wa hospitali ile.Akatoka na
kwenda ofisini kwake akakaa kitini
huku akitafakari nini cha
kufanya.Ugonjwa huu wa Edger
ulimshangaza mno.Baada ya kama dakika tano za tafakari akachukua
simu na kumpigia msaidizi wake.
“Susan,naomba mtaarifu Spika
wa bunge kuwa namuhitaji haraka
hapa hospitali”
Muda wa dakika ishirini toka
apate mwito ule wa haraka spika
wa bunge akawasili hospitali na
moja kwa moja akaelekea katika
ofisi ya Dr Olivia
“Mheshimiwa Spika,naomba
kwanza nikuombe samahani kwa
mwito huu wa haraka” akaanza
maongezi Dr Olivia
“Usijali Dr Olivia.Hii ni moja ya
majukumu yangu ya kazi
kuhakikisha wabunge wote
wanapopatwa na hali kama hii kupata matibabu na
kupona.Nimeacha vikao vya bunge
vikiendelea Dodoma ili kuja
kufuatilia maendeleo ya
mheshimiwa Edger.Kuna taarifa
yoyote mpya? Akauliza Spika
“Mheshimiwa Spika napenda
niwe muwazi kuwa bado hali ya
mheshimiwa Edger si
nzuri.Tumejitahidi sana toka
tulipompokea hapa mchana lakini
bado hali yake imekuwa inabadilika
badilika mara kwa mara.Bado
tunaendelea na uchunguzi wa nini
kinachosababisha hali yake
kubadilika kila wakati.Mheshimiwa
spika hospitali yetu ni kubwa na ya
kuaminika katika ukanda huu wa afrika mashariki na kati na
imesheheni madaktari bingwa wa
magonjwa ya moyo lakini pamoja
na ukubwa na sifa hizo zote
tulizonazo napenda nitoe
pendekezo kuwa mheshimiwa
mbunge anahitaji kupelekwa nje ya
nchi haraka iwezekanavyo kwa
matibabu zaidi.Mimi ni daktari
bingwa wa moyo lakini kwa
ugonjwa huu ninavyouona hatuna
njia nyingine zaidi ya kumpeleka
mgonjwa katika hospitali kubwa
zaidi kwa uchunguzi mpana.Kuna
hospitali moja iko nchini Israel
katika mji wa Haifa inaitwa
Rambam medical center.Pale
wamesheheni mabingwa wa moyo na kuna vifaa vikubwa zaidi vya
uchunguzi kuliko tuliyo navyo
sisi.Hospitali hii ni rafiki zetu na
tumekuwa tukisaidiana mara kwa
mara na hata kubadilishana
wataalamu.Nimekwisha ongea nao
na wako tayari kumpokea
mheshimiwa Edger”
Dr Olivia akamtazama
Mheshimiwa Spika aliyekuwa
amenyamaza akimsikiliza kwa
makini sana.
“Dr Olivia nakushukuru sana
kwa jitihada zote unazozichukua
wewe na timu yako kuhakikisha
kuwa mbunge wetu anapona.Edger
ninamlea kama mwanangu licha ya
kwamba mimi ndiye kiongozi wake bungeni lakini kama mzazi na kama
mtanzania mwenye moyo wa
uzalendo niko tayari kwa lolote lile
linaloweza kufanyika
litakalomsaidia kijana huyu
apone.Wazo lako la kumpeleka nje
ya nchi ni zuri sana lakini kuna
taratibu ambazo lazima
zifuatwe.Ingekuwa ni kwa ridhaa
yangu basi ningekuruhusu sasa hivi
umuandae mgonjwa kwa
safari.Kwa kuwa umeshauri hivyo
ngoja na nianze taratibu za
kumpeleka Edger nje ya nchi”
Dr Olivia akamtazama Spika
kwa makini sana kisha akasema
kwa sauti ya taratibu. “Mheshimiwa Spika najua
kuna taratibu za kufuata lakini kwa
leo sidhani kama utaratibu huo una
nafasi.Kinachotakiwa hapa si
utaratibu bali maamuzi ya
haraka.Nafahamu taratibu za
serikali zinachukua muda mrefu na
hatuna muda mrefu wa
kusubiri,tukifanya mzaha tunaweza
kumpoteza mgonjwa”
“Dr Olivia mambo ya kiserikali
ni magumu.Siwezi kutoa uamuzi
mimi mwenyewe bila kufuata
taratibu husika.Ninachoomba nipe
kama saa moja hivi ili niweze
kufuata taratibu za kiserikali
kumuondoa mbunge hapa nchini ” akasema spika wa bunge na
kuagana na Dr Olivia akatoka

******************
 
SIRI
episode 7
Mtunzi. Patrick CK

Waziri wa afya Dr maneno
kilugwa alikuwa amejipumzisha
katika baa tulivu katika ufukwe wa
bahari.Ni siku ya mwisho ya
mkutano wa wadau wa afya
afrika,mkutano uliochukua
takribani siku nne na uliomfanya
asiwepo Dodoma katika vikao vya
bunge.Baada ya kazi ngumu
iliyofanyika ya kuhakikisha kuwa kujipumzisha sehemu
tulivu.Mezani chupa kadhaa za bia
zilikuwa imesimama.Dr maneno
alikuwa peke yake akijaribu
kuwazua hili na lile,hakutaka
bughudha ya aina yoyote ile.Wakati
akiendelea kukata maji,simu yake
ikaita.Akaitoa mfukoni na
kuangalia.Alikuwa ni spika wa
bunge.
“Madam spika”akasema Dr
Maneno
“Mheshimiwa waziri uko
wapi?
“Madam spika tumemaliza
mkutano wetu na sasa niko sehemu
Fulani ninajipumzisha.Haikuwa
kazi nyepesi kufanikisha mkutano
mkutano ule
unafanikiwa,Mheshimiwa waziri
aliamua kutoka na kwenda
mkubwa kama ule.Vipi maendeleo
ya mheshimiwa Edger?
“Mheshimiwa waziri
nimelazimika kukutafuta.Hali ya
Edger bado si nzuri na madaktari
wameshauri haraka sana apelekwe
nje ya nchi.Kwa maana hiyo
naomba ndani ya dakika kumi na
tano toka sasa tukutane hapo
katika ofisi yangu ndogo.Fanya
hima”
Kauli ile ya mheshimiwa Spika
ikamfanya mheshimiwa waziri wa
afya nywele zimsisimke.
“Bastard!!!!!!!………..akasema
kwa hasira “He’s still breathing….”
Akanong’ona kwa ghadhabu Dr
maneno.
“This cant be..” Akafoka tena
kwa hasira.Akachukua simu yake
na kupiga ikapokelewa
“Mr Nkebo habari za saa hizi?
Akasema Dr maneno huku amefura
kwa hasira
“Habari nzuri Dr Maneno.Niko
hapa na Karim,mheshimiwa
Ngimarwa na wengine wote
tunajipongeza kwa ushindi wetu”
Akasema Mr Nkebo huku akicheka
kicheko cha chini chini.
“Mnafurahia ushindi gani
wakati mpaka sasa hivi Edgerbado
mzima? Bado anapumua na hivi sasa Spika kanipigia simu
tuonane.Edger anatakiwa apelekwe
nje ya nchi haraka iwezekanavyo”
Kikapita kimya cha sekunde kadhaa
halafu Mr Nkebo akasema kwa
sauti kavu.
“Maneno don’t let it
happen.Edger must die
tonight.Ukiacha Edger apelekwe nje
ya nchi basi tumeumia.Kama
atapona itakuwa mbaya kwa
upande wetu.Fanya kila
uwezalo,tumia madaraka yako yote
kuhakikisha kuwa Edger hapelekwi
nje ya nchi.Ukifanikiwa kwa hilo
Edger hatafika
asubuhi.Umenielewa ? Dr maneno akavuta pumzi
ndefu kisha akajibu.
“I understand that.I wont let it
happen”Akasema na kukata simu
halafu kwa haraka akaelekea lilipo
gari lake akapanda na kumuelekeza
dereva wake ampeleke katika ofisi
ndogo ya bunge
Ilimchukua dakika ishirini
kuwasili katika ofisi ndogo ya
bunge.Tayari spika alikuwemo
ofisini mwake akimsubiri.
“karibu sana mheshimiwa
waziri.”
“Ahsante mheshimiwa
Spika.Nimeitika mwito.Vipi hali ya
bunge inaendeleaje? Akasema Dr
maneno huku akivuta kiti na kuketi “Hali ya mbunge si nzuri
imekuwa inabadilika badilika kila
wakati.Nimezungumza na daktari
mkuu Dr Olivia Themba ameshauri
kuwa ili kuokoa maisha ya
mheshimiwa Edger inabidi
tumpeleke katika hospitali kubwa
nchini Israel.Nimemuoma anipe
muda ili niweze kushughulikia
taratibu za kumpeleka Edger nje ya
nchi.Nimekuita hapa ili tujadiliane
kwa haraka nini cha kufanya ili
mheshimiwa Edger apelekwe nje ya
nchi usiku huu.Kwa kuwa hivi sasa
ni usiku na hatuwezi kukamilisha
taratibu zote nataka kitolewe kibali
cha dharura ili Edger aweze
kusafirishwa kwenda nje ya nchi na mambo mengine yaliyobaki
yatamaliziwa kesho wakati
matibabu yanaendelea”akasema
Spika wa bunge na kumtazama Dr
maneno aliyekuwa akimsikiliza
kwa makini .
“Mheshimiwa spika,suala la
ugonjwa huu wa ghafla wa Edger
limetugusa wote na ninatamani
sana kufanya kila linalowezekana
ili aweze kupona kwa haraka.Suala
la kumpeleka Edger nje ya nchi lina
taratibu zake ambazo lazima
zifuatwe hatuwezi kukurupuka tu
na kumsafirisha mgonjwa hata
kamakuna kibali cha dharura.Kuna
taratibu za kiuhamiaji lazima
zifuatwe,lazima tuwasiliane nan chi tunakotaka kumpeleka mgonjwa na
wao wakikubali mgonjwa wetu
aende ndipo tumpeleke na lazima
vibali vipatikane,kwa ujumla kuna
mlolongo mrefu kidogo wa mambo
na hatuwezi kuukamilisha kwa
usiku huu.Ushauri wangu mimi ni
kwamba kwa usiku wa leo Edger
aendelee kupata matibabu na kuwa
chini ya uangalizi wa madaktari
wetu na kesho tuanze taratibu za
kumsafirisha.Lazma taratibu zote
zifuatwe na hatuwezi kupindisha
mambo hata kama mgonjwa ni
mbunge.Tayari nimewasiliana na
madaktari wa kitengo cha moyo
katika hospitali ya Muhimbili na
wamesema kuwa ugonjwa huo wa
Mheshimiwa Edger unaweza
kutibika humu humu
nchini.Hakuna sababu ya
kumpeleke mgonjwa wa shinikizo
la damu nje ya nchi wakati tunao
wataalamu wetu wengi wa serikali
ambao ni mabingwa wa maradhi
haya ya moyo.Hivi tunavyoongea
maandalizi yanafanyika ili
mheshimiwa Edger ahamishiwe
katika hospitali ya taifa ya
muhimbili ambayo ina wataalamu
wa hali ya juu kabisa”akasema Dr
Maneno bila wasi wasi .Spika
akasimama na kumtazama Dr
maneno kwa hasira.Hakutegemea
katu kusikia jibu kama lile. “Waziri sijakuelewa
vizuri,unasemaje?? Akauliza spika
“Nimesema kwamba
nimeagiza kuwa mheshimiwa
mbunge ahamishiwe katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili.Pale
kuna wataalamu wa hali ya juu
watakaoutibu ugonjwa wake na
tayari maandalizi yameanza
kufanyika.Muda mfupi ujao nataka
mheshimiwa mbunge ahamishwe
toka katika hospitali ya moyo na
kuhamishiwa katika hospitali ya
Muhimbili.Mbunge Edger atatibiwa
hapa hapa nchini hadi pale
tutakapojiridhisha kwamba kuna
ulazima wa kumpeleka nje ya nchi” Akasema Dr maneno kwa sauti
iliyokuwa na aina Fulani ya ukali
Spika wa bunge akamtazama
na macho yake yakalengwa na
machozi
“Siamini hayo unayoniambia
Dr maneno.Nashindwa kuelewa
umetumia vigezo gani kutaka
kumuhamisha mheshimiwa Edger
kutoka katika hospitali ambayo
inategemewa afrika mashariki na
kati kwa matibabu ya moyo na
umpeleke katika hospitali ya
Muhimbili”
“Mheshimiwa Spika pale
Muhimbili kuna kitengo cha moyo
chenye mabingwa na hata
wataalamu wa kichina wako pale.Sioni tatizo lolote kwa
mheshimiwa mbunge kuhamishiwa
pale akaendelea na matibabu.Zote
ni hospitali za serikali na Muhimbili
ni hospitali kubwa kuzidi hata hiyo
alikopelekwa Edger.Mimi kama
waziri wa Afya nina Imani sana na
hospitali ya Muhimbili na Edger
atashughulikiwa na madaktari
wazalendo na atapona tu”akasema
Dr Maneno.Spika wa bunge
akamtazama kwa hasira na kusema
“We’re done in here.Unaweza
kwenda.” akasema Spika
Waziri wa afya Dr maneno
akatoka katika ofisi ya spika baada
ya kuona tayari mheshimiwa spika
amekasirika.Spika wa bunge akafanya mawasiliano na mawaziri
kadhaa lakini hakukuwa na hata
mmoja aliyeweza kumpa jibu lenye
uhakika.Wote walisema wasubiri
asubuhi ili waone ni jinsi gani ya
kulishughulikia suala hilo.Akatoka
ofisini kwake na kumuamuru
dereva wake kumpeleka hospitali
haraka iwezekanavyo.
Alipofika hospitali akafululiza
kwa kasi hadi katika ofisi ya Dr
Olivia.
“Dr Olivia mgonjwa
anaendeleaje?”akauliza spika
“Mgonjwa bado hali yake
inazidi kuwa mbaya.Vipi umefikia
wapi kuhusu suala la kumsafirisha
nje ya nchi? “Mambo magumu Dr
Olivia.Nimetoka kuongea na waziri
wa afya lakini tumeshindwa
kuelewana.Ameamuru Edger
ahamishiwe katika hospitali ya taifa
ya muhimbili”
“Whaaaat!!!!????? …..akauliza
Dr Olivia kwa mshangao.
“Hawa watu wanatania”
akasema Dr Olivia
“Its not a joke Dr Olivia.Hivi
tunavyoongea maandalizi
yanafanyika na muda si mrefu
mtataarifiwa juu ya uhamisho huo
wa Dr Edger”
Dr Olivia akamuangalia spika
kwa macho makali. “Mheshimiwa spika mnajua
athari za mnachotaka kukifanya??
Akauliza Dr Olivia,Spika hakujibu
kitu.
“You are going to kill
him…He’s going to die” Akasema Dr
Olivia na kumtazama Spika
“Mheshimiwa spika
umekubaliana na uamuzi huo wa
kumtoa hapa Edger na kumpeleka
katika hospitali ya Muhimbili?
“Hapana sijakubaliana nao
hata kidogo”akajibu spika
Dr Olivia akamtazama spika
kwa makini sana halafu akasema.
“Mheshimwa Spika naomba
unisikilize.Toka mheshimiwa Edger
ameletwa hapa wewe ndiye kiongozi pekee wa juu wa serikali
uliyefika hapa kujua maendeleo
yake na unayehangaika
kuhakikisha Edger anapona.Wewe
ni kiongozi jasiri.Umenihakikishia
kwamba ukiwa kama mzazi
hutapenda kuona mbunge huyu
kijana anafariki dunia.Mimi binafsi
sikubali mbunge huyu afariki dunia
na ndiyo maana ninajitahidi
kufanya kila linalowezekana
kuhakikisha Rdger anapona.Mama
tukikubali suala hili la
kumuhamisha Edger kumpeleka
katika hospitali ya Muhimbili
tutakuwa tumefanya kosa kubwa
mno kwani tutampoteza hivyo basi
ninaomba kama kweli una nia ya dhati tushirikiane mimi na wewe
kuhakikisha kuwa Edger
ahamishiwi Muhimbili na usiku huu
huu anasafirishwa nje ya nchi.Are
you ready for this madam?
Bila kusita spika wa bunge
akajibu.
“Dr Olivia kwa kuyaokoa
maisha ya kijana huyu niko tayari
kwa lolote lile.Kama una mipango
yoyote mizuri nieleze nitakuunga
mkono
“Nimeumia sana moyoni kwa
kitu anachotaka kufanyiwa
Edger.Kitendo cha kutaka
kumuhamisha hapa na kumpeleka
hospitali ya taifa ya Muhimbili bila
sababu ya msingi kinanipa picha ya wazi kuwa kuna kitu kinaendelea
hapa”
“Dr Olivia hata mimi nimeanza
kuhisi kitu kama hicho kwa sababu
hii si kawaida”akasema spika
“Usijali spika kwa vile
umekubali kushirikiana na mimi
basi napenda kukuhakikishia kuwa
ndani ya nusu saa ijayo
tutamsafirisha mheshimwa
mbunge.Ni bora kujaribu kuliko
kukaa na kusubiri kuhani
msiba.Naomba sasa unisubiri hapo
nje kama dakika tatu hivi” akasema
Dr Olivia
Spika akatoka na kwenda
kukaa katika masofa yaliyokuwa
nje ya ofisi ya Dr Olivia. Dr Olivia akachukua simu na
kuzitafuta namba za baba yake
Agrey Themba bilionea mkubwa
nchini
“Olivia my sweetie.How are
you” akasema Agrey
“I’m fine dady how are you? Dr
Olivia akauliza
“I’m fine too.Mbona sauti yako
iko tofauti? Is there anything wrong
my love? akauliza Agrey
“Dady I have a problem”
“My love,nimekwisha kwambia
kuwa ,wakati niko hai duniani
sintataka hata siku moja tabasamu
likauke usoni mwako.Wewe ndiye
binti wangu wa pekee na niko tayari kufanya lolote lile kwa ajili
yako”
Tabasamu likaanza kujengeka
usoni mwa Dr Olivia baada ya kauli
ile
“Niambie nini tatizo? Akauliza
Agrey
“Daddy tatizo ni kubwa lakini
kwako wewe si kubwa na unaweza
ukanisaidia” Dr Olivia akasema
“Mbona unashindwa kulisema
tatizo gani linakusumbua my
love.Sema tu mimi ndiye baba yako
na nitafanya lolote lililo katika
uwezo wangu kukusaidia” akasema
Agrey “Daddy nafikiri una taarifa juu
ya mbunge aliyepatwa na matatizo
leo bungeni anaitwa Edger Kaka”
“Ndiyo nimepata taarifa zake”
akasema Agrey
“Edger ameletwa hospitali
kwetu.Tumempokea mchana na
tumeendelea
kumuhudumia.Pamoja na jitihada
zetu zote lakini bado hali yake si
nzuri,tumeamua apelekwe nje ya
nchi kwa uchunguzi
zaidi.Nimeongea na mheshimiwa
spika nikamueleza jambo hili
akakubali lakini kumetokea
tatizo.Waziri wa afya amekataa
Edger apelekwe nje ya nchi na
badala yake ameagiza mgonjwa ahamishiwe katika kitengo cha
magonjwa ya moyo cha hospitali ya
Muhimbili.Dady hali ya Edger si
nzuri na sisi tumeamua aende nje
ya nchi katika hospitali kubwa
zaidi.Tusipofanya hivyo Edger will
die.I won’t let him die just like that.I
need to fight for him.Dady wewe
unanifahamu ni mwiko kwangu
mgonjwa kufa kwa uzembe hivyo
niko tayari kufanya lolote
linalowezekana kwa ajili ya kuokoa
uhai wa Edger.Nimekwisha ongea
na rafiki zangu wa hospitali ya
Rambam iliyoko Haifa Israel na
wamekubali kumpokea
mgonjwa.Ninataka kumpeleka Edger nchini Israel ndani ya muda
mfupi ujao”
“Unataka kumpeleka Israel?
Akauliza Agrey
“Ndiyo day.Nataka nimpeleke
nje ya nchi lakini nimekwama,sina
uwezo wa kufanya hivyo.I need
your help” akasema Dr Olivia
Kimya kikatanda.Ombi la
mtoto wake lilimstua mno Agrey.
“Dady are you there? Dr Olivia
akauliza baada ya kuona baba yake
yuko kimya.
“I’m here love” Akajibu Agrey
kwa upole
“Natafakari uzito wa ombi
lako.Kwa nini lakini us………………..” Dr Olivia akakamkatisha baba yake
aliyekuwa akitaka kuongea
“Dady No..this is not
politics.This is life of someone.I
need your help.Nataka kumpeleka
Edger nchini Israel.Rais Dr Evans ni
rafiki yako mkubwa zungumza
naye ili aniwezeshe niweze
kumpeleka Edger nchini Israel.Ni
yeye pekee ambaye anaweza
akatumia uwezo wake kuruhusu
Edger apelekwe nje ya
nchi.Unaweza kunisaidia kwa hilo
baba?akauliza Dr Olivia
Agrey alimpenda mno binti
yake Olivia na alikuwa tayari
kufanya lolote lile kwa ajili yake. “Okay my love,nipe dakika
chache nizungumze na rais”
akasema Agrey.
Baada ya dakika kumi Agrey
akampigia Dr Olivia
“Olivia my love nimezungumza
na rais,anashukuru sana kwa
namna ulivyojitoa kumuhudumia
Edger Themba.Rais anasema
kwamba hakuwa na taarifa kamili
kuhusu maendeleo ya
Edger.Amekubali Edger akimbizwe
nje ya nchi haraka sana kuokoa
maisha yake.Tayari amekwisha
zungumza na balozi wa Israel hapa
nchini na kumweleza dharura hii
iliyotokea,na vile vile ameongea na
waziri mkuu wa Israel na kumfahamisha juu ya suala hili na
mgonjwa wake ameruhusiwa
kwenda nchini Israel kwa
matibabu.Rais ametoa ndege yake
kwa ajili ya kumpeleka Edger
nchini Israel.Maandalizi yafanyike
haraka sana kwani ndege iko tayari
inawasubiri”
“Thank you so much
daddy.You did great.I love
you”akasema Dr Olivia na kukata
simu akatoka mle ofisini kwake
kwa kasi na kumkuta spika wa
bunge akimsubiri .
“Mheshimiwa Spika kila kitu
tayari.Rais ametoa ruhusa Edger
asafirishwe nje ya nchi”akasema Dr
Olivia “Kweli?akauliza spika ambaye
hakuamini
“Kweli mama spika.Ndani ya
muda mfupi ujao Edger
atasafirishwa.Naomba unipe muda
wa kumuandaa” akasema Dr Olivia
Dakika kumi na tano tu
zilitosha kabisa kumuandaa
mgonjwa tayari kwa safari ya
kuelekea nchini Israel.Gari la
wagonjwa lilikuwa
tayari,mheshimiwa Edger
akapakiwa garini na safari ya
kuelekea uwanja wa ndege ikaanza.
Uwanjani ndege ya Rais
ilikwisha wekwa tayari kwa ajili ya
kumsafirisha mbunge Edger Kaka
na bila kupoteza muda akaingizwa ndegeni tayari kwa safari.Dr Olivia
akamkumbatia spika kwa furaha
wakaagana na ndege ikapaa
kuelekea nchini Israel

***************
Timu ya madaktari toka
kitengo cha magonjwa ya moyo
hospitali ya taifa ya Muhimbili
kikawasili katika hospitali ya
magonjwa ya moyo ya Tanzania
heart hospital ili kumuhamisha
mheshimiwa mbunge Edger kama
walivyoamriwa na waziri wa
afya.Taarifa waliyoipata toka kwa
msemaji wa hospitali
zikawachanganya na kumlazimisha mkuu wa msafara ule ampigie simu
waziri wa afya.
“Mheshimiwa waziri,kuna
mambo yamejichanganya
hapa.Taarifa tuliyoikuta hapa
hospitali inasema kuwa mgonjwa
tuliyekuja kumchukua tayari
amesafirishwa nje ya nchi”
“Unasemaje? Akahamaki
waziri wa afya
“Taarifa tuliyoikuta hapa
hospitali ni kwamba mgonjwa
tuliyemfuata hapa Mheshimiwa
Mbunge Edger kaka,amepelekwa
nje ya nchi akiongozana na daktari
mkuu wa hospitali hii Dr Olivia
Themba na muuguzi mmoja..” “Nani katoa ruhusa ya
kumsafirisha mgonjwa
huyo?Nilikwisha toa maelekezo
kwamba mgonjwa huyo
ahamishiwe katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili.Nani anapingana
nami?Nisubirini nakuja hapo sasa
hivi”Akasema waziri Maneno.Jasho
lilikuwa likimtoka.
“Lazima kuna kitu kimefanyika
hapa.Watakuwa wamemficha
mgonjwa.Si rahisi kumsafirisha
mgonjwa nje ya nchi bila mimi
kujua.Mgonjwa ni lazima yuko
humo humo
hospitalini.Nitakwenda na kikosi
cha askari na kufanya upekuzi
hospitali yote.Lazima atakuwa amefichwa katika moja ya vyumba
vya hospitali hiyo”akawaza Dr
Maneno
Haraka haraka akapanda
katika gari lake na kuondoka
kuelekea hospitalini ambako
aliwakuta madaktari toka hospitali
ya muhimbili wakimsubiri.
Daktari mkuu wa zamu ya
usiku ule akamhakikishia kuwa
mbunge Edger amesafirishwa nje
ya nchi.Bado waziri wa afya
hakuamini akaamua kumpigia simu
Spika.
“Mheshimiwa spika una taarifa
zozote juu ya kusafirishwa kwa
mbunge Edger nje ya nchi?” “Ndiyo ninazo taarifa hizo.Ni
kweli amesafirishwa na mimi
mwenyewe nimemsindikiza hadi
uwanja wa ndege na kuhakikisha
ndege imepaa”
Sura ya mheshimiwa waziri wa
afya ikazidi kujikunja kwa hasira
“Sikutegemea mheshimiwa
spika kama na wewe unaweza
ukashiriki katika uvunjifu huu wa
taratibu za nchi.Unafahamu wazi
kuwa zipo taratibu za kufuatwa
lakini kwa makusudi kabisa
umeshiriki katika kukiuka taratibu
hizo na kumsafirisha
mgonjwa.Mheshimiwa wewe
nikiongozi wangu lakini umeonyesha dharau kwangu mimi
kama waziri mwenye dhamana ya
afya” Akasema waziri Maneno kwa
hasira
“Mheshimiwa waziri,aliyetoa
maamuzi ya kumsafirisha Edger nje
ya nchi ni rais hivyo kama ni
lawama mtupie yeye na si mimi”
akasema spika
“Rais?!! Dr Maneno
akashangaa
“Ndiyo.Mheshimiwa rais ndiye
aliyetoa maelekezo Edger apelekwe
nje ya nchi na kama haitoshi
ametoa pia ndege yake impeleke
Edger nchini Israel” akasema spika
na Dr Maneno akabaki kimya. “It's now more complicated
than I thought” Akawaza
mheshimiwa waziri wa afya huku
amejishika kiuno na jasho
likimtiririka.
*******************
“Wamefanikiwa kumsafirisha”
Ilikuwa ni sauti ya kinyonge ya
waziri wa afya akimfahamisha
Donald Nkebo katika simu kuhusu
kusafirishwa kwa mbunge Edger
Kaka.
“How could you let it happen
Dr Maneno? Nkebo akauliza kwa
ukali “Its complicated
Donald.Wamepata msaada kutoka
kwa rais”
“Rais? Donald Nkebo
alionekana kustushwa na kauli ile
“Rais ndiye aliyesaidia Edger
apelekwe nje ya nchi? Akauliza
Donald Nkebo
“Hata ndege yake ndiyo
imetumika kumsafirisha Edger”
akasema Dr Maneno.Kimya
kikapita halafu Nkebo akasema
“Upepo umebadilika.Hata
hivyo bado hakijaharibika
kitu,kinachotakiwa kufanyika hapa
ni kucheza na rais”akasema Donald
Nkebo “Mheshimiw Rais? Akauliza
waziri Maneno
“Ndiyo.Hapa ilipofika mtu
pekee wa kucheza naye ni
mheshimiwa rais.Kuna uwezekano
huko alikopelekwa Edger anaweza
akapona na Mungu akimnusuru
katika hili,naamini atakuja na
nguvu mpya na mashambulizi yake
yatakuwa makali sana,atatuandama
kila kona.Ili tuweze kummaliza
Edger lazima tuongeze
nguvu,lazima tumshirikishe rais
ambaye atakuwa ni ngao
yetu”akasema Donald Nkebo
“Mr Nkebo una mawazo
mazuri sana,lakini bado sijakupata
vizuri.How are we going to convince Mr president to join
us?Hudhani kuwa tunajiweka
katika hatari kubwa? Akauliza
waziri maneno
“Leave everything to me.Mimi
ndiye nitakayekwenda kuonana na
rais.Kesho mheshimiwa rais
atakuja Dodoma kwa vikao vya
chama vitakavyoanza kesho
kutwa.Rais ananifahamu vizuri na
akisikia niko Dodoma na ninahitaji
kumuona basi atakubali haraka
sana”
“Nimekuelewa Mr
Nkebo.Kama mtahitaji ushirikiano
wowote toka kwangu msisite
kunitaarifu kwa sababu sitegemei
kuja Dodoma hivi karibuni” akasema Dr Maneno na kuagana na
Donald Nkebo
****************
Wakati sakata la ugonjwa wa
ghafla wa mbunge Edger kaka
likiendelea kutikisa nchi huku hali
yake ikiwa haijawekwa
bayana,katika ukumbi mdogo wa
hoteli ya Dodoma palace hotel
kikao kilikuwa kikiendelea.Mbunge
Damiani mwamba alikuwa ndiye
mwenyekiti wa kikao hicho
kilichowakutanisha baadhi ya
wabunge wenye nguvu bungeni na
katika chama,walikuwepo pia
baadhi ya viongozi na watendaji wa chama waliokuwepo jijini Dodoma
kwa ajili ya vikao vya chama.
Damiani Mwamba anatajwa
kuwa mbunge tajiri zaidi.Amewahi
kushika nyadhifa mbali mbali
serikalini na katika
chama.Amekuwa mbunge kwa
miaka karibu ishirini sasa na bado
wananchi wake wameendelea
kuwa na imani naye na kumtaka
aendelee kuwasemea bungeni.Ni
mmoja wa wabunge aliyefanikisha
maendeleo mengi kupatikana
katika jimbo lake.
Damiani Mwamba ni mmoja
wa watu wa karibu sana na rais Dr
Evans,walikutana chuo kikuu na
huko ndiko walikoanzia shughuli za siasa.Kwa muda wa miaka kumi na
sita alikuwa waziri katika wizara
mbali mbali hadi pale rais Dr Evans
alipolivunja baraza lake la
mawaziri na yeye kuushangaza
umma kutokurudi tena katika
baraza la mawaziri.Hakuna ajuaye
ni kwa nini Mheshimiwa Damian
hakupewa uwaziri tena.Pamoja na
kutopewa uwaziri katika serikali
,bado mheshimiwa Damian
aliendelea kuwa na nguvu kubwa
katika chama na bunge.Idadi kubwa
ya viongozi wa chama na serikali
walikuwa upande wake.
“Ndugu wajumbe ,karibuni
sana katika kikao hiki cha leo.Hiki
ni moja ya vikao vyetu vya kawaida ambavyo tutaendelea kukaa na
kujadili mwenendo wa siasa hapa
nchini.Kikao cha leo ni kwa ajili ya
kukumbushana baadhi ya mambo
bila kusahau mkakati wetu wa
kuchukua urais katika uchaguzi
mkuu ujao ambao umekaribia
sana.Nawashukuru ndugu wajumbe
kwa kazi kubwa na nzuri
mliyoifanya na mnayoendelea
kuifanya kila siku.Nguvu yetu
katika chama imeongezeka,idadi ya
wajumbe wanaotuunga mkono
imeongezeka na hivyo kuzifanya
mbio za kinyang’anyiro cha
kuteuliwa kuwania urais ndani ya
chama kuwa nyepesi sana kwa
upande wetu.Nina imani tutashinda.Imani kwa wananchi na
kwa wanachama imeongezeka na
inaendelea kuongezeka licha ya
kuwa kuna upinzani mkubwa kati
yangu na rais Dr Evans ambaye
naye anataka kuwania tena muhula
mwingine.Kuna watu wengine vile
vile ambao wanawezekana wakawa
tshio katika mbio hizi ingawa
hawajaweka bayana dhamira zao
za kugombea nafasi hiyo.Mmoja
wao ni huyu kijana Edger
Kaka.Kijana huyu nyota yake
inang’aa kwa sasa na ina nguvu
kubwa.anakubalika mno katika
jamii na anakubalika mnop hasa
kwa vijana ambao ndio kundi
kubwa.Ikiwa ataweka nia ya kugombea urais kijana huyu ni
tishio mno ndani na nje ya
chama.Amepatwa na ugonjwa wa
ghafla asubuhi ya leo na hali yake
bado si nzuri.Hatumuombei
mabaya lakini kama atapona na
akaamua kuwania urais anaweza
kuwa tishio kwetu.Hata hivyo
ninawatoa wasi wasi kwani nguvu
yetu ndani ya chama ni kubwa sana
na hatuwezi kubabaishwa na yule
bwana mdogo.Kitu cha msingi kwa
sasa ni kuanza kuchunguza kambi
za wenzetu hasa ya rais
wanajiandaa vipi na nguvu yao
ikoje.Mchakato huu ni lazima
tuanze mapema sana.Sina wasi
wasi na utendaji wenu kwa sababu kazi yenu tayari
inaonekana.Tunakotakiwa
kuongeza nguvu kwa sasa ni kwa
wajumbe wa mikoani.Inatakiwa
tujiimarishe kule zaidi ii kusiwe na
taizo la uungwaji mkono”akasema
Damiani Mwamba akiwa na baadhi
ya watu wa timu yake wakiwa
katika mbio za kuwania kuteuliwa
kupeperusha bendera ya chama
katika uchaguzi mkuu wa
urais.Kikao kilikuwa kirefu na
kiliendelea hadi usiku wa manane .
 
Mkuu acha tabia za ajabu utatumaje Riwaya hii bila ruhusa ya mwandishi huuuu ni upuzi unamkosesha mwenzio mapato acha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom