Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

SIRI
episode 8
Mtunzi. Patrick CK

************
Kumepambazuka Tanzania na
habari kuu iliyotawala vinywani
mwa watu na katika vyombo vyote
vya habari ni hali tete ya
mheshimiwa Edger Kaka.Hali yake
bado iliendelea kuwa siri na
kilichowachanganya zaidi watu ni
taarifa za kusafirishwa kwake
kupelekwa nje ya nchi kwa
siri.Gazeti moja la kila siku
linaloandika habari za kiuchunguzi
lilizipata taarifa za Edger
kusafirishwa kwenda nje ya nchi na
kuandika kichwa kikubwa cha
habari chenye maandishi mekundu. EDGER ASAFIRISHWA NJE YA
NCHI KWA SIRI.Ndivyo
kilivyoandikwa kichwa cha habari
cha gazeti hili pendwa lenye kutoa
habari za kina na
uhakika.Waandishi wa habari wa
gazeti hili walikuwa wamepiga
kambi katika hospitali aliyolazwa
mheshimiwa Edger mpaka usiku
wa manane na kuhakiksha kuwa ni
kweli Edger alisafirishwa nje ya
nchi.Kwa nini asafirishwe kwa siri
namna ile lilibaki ni swali gumu
ambalo hakuna aliyekuwa na jibu
lake.
Spika wa bunge alirejea
Dodoma alfajiri na mapema tayari
kwa kuendelea kuongoza vikao vya bunge.Saa tatu kamili kama
kawaida kikao cha bunge kikaanza
kikiongozwa na Spika ambaye
alianza kwa kusoma dua halafu
akawaruhusu wabunge
waketi.Walipoketi wote Spika
akasimama na kutoa taarifa fupi.
“Waheshimiwa wabunge,jana
katika kikao cha asubuhi mbunge
mwenzetu Edger kaka alipatwa na
ugonjwa wa ghafla.Alikimbizwa
katika zahanati yetu ya bunge lakini
hali yake haikuwa nzuri
,akahamishiwa katika hospitali ya
St Francis hapa Dodoma ambako
madaktari wakashauri kuwa
ahamishiwe katika hospitali kuu ya
moyo iliyoko Dar es salaam.Mheshimiwa Edger
akakimbizwa Dar es salaam jana
mchana na kupokelewa katika
hospitali kuu ya moyo.Madkatari
walijitahidi sana kumuhudumia
mheshimiwa mbunge lakini bado
tatizo lilionekana kukomaa hivyo
wakashauri mbunge ahamishiwe
nje ya nchi.Taratibu za kusafirisha
mgonjwa nje ya nchi nafikiri wote
mnazifahamu isingewezekana kwa
usiku ule kuweza kukamilisha
taratibu zote.Namshukuru
mheshimiwa rais kwa sababu yeye
alitoa maelekezo kuwa Edger
apelekwe nje ya nchi na alitoa
ndege yake itumike kumsafirisha
mheshimiwa Edger kuelekea nchini Israel pamoja naye alikuwepo Dr
Olivia Themba.Bado tunajitahidi
kuwasiliana nao kwa kutumia
ubalozi wetu nchini Israel.Taarifa
zote tutakazopata tutakuwa
tukiwataarifu.Nawashukuru sana
madaktari wote kuanzia madaktari
wetu wa bunge na katika hospitali
zote alikopelekwa mheshimiwa
Edger.Tuzidi kumuombea ili Mungu
amjalie uponaji wa
haraka”akasema spika. Kupitia
taarifa hii fupi ya mheshimiwa
spika,bunge na taifa liliweza kujua
kinachoendelea kuhusu Edger
kaka.Nyoyo za watanzania na hasa
mashabiki wa Edger zilitulia wakati wakisubiri kupata taarifa zaidi za
maendeleo yake nchini Israel.
HAIFA - ISRAEL
Rambam medical center moja
kati ya hospitali kubwa za rufaa
nchini Israel,ilianzishwa mwaka
1938.Ikiwa na vitanda vya
wagonjwa zaidi ya 2000,na
madaktari zaidi ya 700 ,idara za
kila ugonjwa na wafanyakazi
wenye taaluma na
uzoefu,inahudumia watu zaidi ya
milioni mbili.
Toka katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Haifa moja kati ya
uwanja mkongwe kabisa na wa kwanza kujengwa nchini
Israel,Edger akiwa katika gari la
wagonjwa akawahishwa
hospitalini.Kwa kuwa walikwisha
taariwa juu ya mgonjwa huyu mara
tu gari la wagonjwa lilipofika
hakukuwa na muda wa
kupoteza.Kwa haraka akaingizwa
katika chumba cha wagonjwa
mahututi akaanza kuhudumiwa.
Dr Olivia alikuwa amechoka
kwa kazi kubwa aliyoifanya toka
alipompokea Edger.Akachukuliwa
na daktari mkuu hadi ofisini kwake
na kutoa maelezo ya kina ya
ugonjwa wake.Baada ya maelezo
yale Dr Olivia akachukuliwa na
kupelekwa katika hoteli moja kubwa mjini Haifa iitwayo
Leaonardo Hotel.Hoteli hii iko
katikati ya Mlima Carmel na bahari
ya Mediteranea.Chumba chake
kilikwisha andaliwa tayari na kwa
uchovu aliokuwa nao akajitupa
kitandani na kuanza kutafakari kwa
kina juu ya mshike mshike
alioupata.
“Naomba Mungu amsaidie
mgonjwa wangu aweze
kupona.Kwa hapa tulipofika nina
imani atapona.Mungu yuko upande
wetu” Akawaza Olivia na kupitiwa
na usingizi
Saa kumi na moja za asubuhi
akastushwa na mlio wa simu ya mezani iliyo chumbani.Akainuka na
kuipokea
“Hallo” akaita Dr Olivia
“Dr Jacob ninaongea toka
hospitali ya Rambam.”
“Dr Jacob.Mgonjwa
anaendeleaje?
“Hali ya mgonjwa ndiyo
iliyonifanya nikupigie simu mida
hii.Nakuomba tuonane saa mbili leo
asubuhi” Akasema Dr Jacob.
“Sawa Dr Jacob Nitafika mida
hiyo”akasema Dr Olivia na kukata
simu
Dr Olivia akaanza kuingiwa na
wasi wasi mwingi kutokana na
mwito ule wa Dr Jacob. “Inawezekana hali ya mgonjwa
ni tete sana.Nina wasi wasi na
maisha ya mgonjwa.Kama hawa
wakishindwa sijui kama kuna
sehemu nyingine tena ambayo
wanaweza kuutibu ugonjwa ule
usioeleweka” Akawaza Dr
Olivia.Hakuweza kulala tena.Toka
alipopigiwa simu ile akawa katika
mawazo mengi.
Kulipambazuka na kijua
kuanza kuchomoza.Dr Olivia
akasimama dirishani na
kuishuhudia mandhari ya kuvutia
ya mji huu wa Haifa asubuhi
hii.Pamoja na mandhari yote nzuri
na ya kuvutia lakini mawazo ya
Olivia yalikuwa sehemu moja tu,hospitalini kwa mheshimiwa
Edger .Akaingia bafuni kuoga na
ndipo alipogundua kuwa hakuwa
amekuja na nguo zozote za
kubadilisha.Alisafiri na pochi ndogo
iliyokuwa na vitu vyake muhimu
ambavyo huwa anavihifadhi ofisini
kwake kama kadi ya benki ,hati ya
kusafiria n.k.
“Itanibidi leo nizunguke
madukani kununua vitu vichache
vitakavyonisaidia kwa muda wote
nitakaokuwa hapa.”akawaza
Gari maalum la kukodi lilikuwa
tayari likimsubiri.Akapanda na
kuelekea hospitalini ambako Dr
Jacob alikuwepo ofisini kwake
akimsubiri “Karibu sana Dr Olivia.”
“ahsante sana Dr Jacob”
Akajibu Olivia akiwa na shauku ya
kutaka kufahamu alichoitiwa.
“Dr Olivia nimekuita ili nikupe
picha halisi ya hali ya
mgonjwa.Mgonjwa anaendelea
vizuri kwa sasa.Timu ya madaktari
wetu wamemuhudumia toka
alipofika hapa na hali yake kwa
sasa naweza kusema ni tofauti na
ile aliyokuwa nayo wakati anafika
hapa.Hata hivyo kuna kitu
tumekigundua kuhusiana na huyu
mgonjwa.Tumegundua kwamba
mgonjwa huyu alipewa sumu.”
Dr Olivia akapatwa na mstuko
wa ghafla. “Sumu aliyopewa inaitwa
Spaxloxy ambayo ikiingia mwilini
inaweza kuua kwa muda wa masaa
kuanzia saba.Katika uchunguzi
wetu tumegundua kwamba sumu
hii imeingiwa mwilini kwa kupitia
katika ngozi.Tuna wasiwasi
yawezekana amepuliziwa au
ameogea sabuni yenye sumu au
ameshika kitu kilichopakwa sumu
hiyo. Sumu hiyo ikiingia mwilini
huanza kufanya kazi taratibu na
mgonjwa hawezi kuhisi chochote
hadi baada ya masaa manne au
matano ndipo huanza kufanya kazi
kwa kasi na hapo ndipo mgonjwa
asipowahiwa anaweza
akafariki.Imekuwa bahati kwamba dawa alizowahi kupewa mgonjwa
zimemsaidia sana kwani baadhi ya
dawa alizopewa zilikuwa sahihi
kabisa katika kupambana na sumu
ile.Kitakachofuata tutamfanyia
operesheni ili kuondoa baadhi ya
sehemu ambazo zimeharibiwa na
sumu katika mwili wake.Ni
operesheni kubwa lakini nina imani
baada ya operesheni hiyo hali yake
itakuwa nzuri zaidi.Kwa sasa ondoa
shaka kwani hayuko tena katika
hatari kwa sababu tumefanikiwa
kuiondoa sumu yote
mwilini.”akasema Dr Jacob
Dr Olivia akahisi kijasho
kikimtoka baada ya taarifa ile ya Dr
Jacob.Akakohoa kidogo kurekebisha koo lake halafu
akasema
“Dr Jacob nashukuru kwa kazi
kubwa mliyoifanya na kuokoa
maisha ya Edger.Tulifanya jambo la
msingi sana kufanya maamuzi ya
kumleta mgonjwa hapa kwani
tusingeweza kugundua kama
ameathiriwa na sumu.Kwa ufupi tu
ni kwamba huyu mgonjwa ni
mwanasiasa.Ni mbunge ambaye
anapendwa na watu
wengi.Kupendwa huko
kumemfanya awe na maadui wengi
vile vile.Nina imani hata sumu hiyo
iliwekwa makusudi na maadui zake
kisiasa.Dr Jacob naomba
asiruhusiwe mtu yeyote asiye muhusika wa hospitali hii kumuona
mgonjwa zaidi yangu mimi au
nitakayemruhusu kwa sababu watu
hawa waliofanya hivi hawatasita
kumfuata Edger hadi huku .”
“Usihofu kitu Dr Olivia.Hopitali
yetu ina usalama mkubwa na
hakuna mtu yeyote anayeweza kuja
kufanya kitendo chochote kibaya
hapa.Hata hivyo tutafanya kama
ulivyoomba na tutaweka ulinzi
mkali katika chumba cha mgonjwa
na hatutamruhusu mtu yeyote
kwenda kuonana na mgonjwa.Kwa
sasa operesheni inaandaliwa na
baada ya masaa mawili tutakuwa
tumeanza na tutakutaarifu kila kitu
kitakavyokuwa kikiendelea.Naahidi kumshughulikia mgonjwa huyu
kwa kila namna tunayoweza na
atapona.Tumekuwa na mahusiano
mazuri na hospitali yako na
tunakuheshimu sana”akasema Dr
Jacob
Dr Olivia
akatabasamu,akaagana na Dr Jacob
akatoka kuelekea madukani kwa
ajili ya kujinunulia vitu vichache
vya kutumia kwa muda
atakaokuwa hapo Haifa.

TANZANIA
Ni saa mbili za usiku ikulu jijini
Dodoma rais wa Tanzania Dr Evans
mwaluba alikuwa na mfanyabiashara mkubwa Donald
Nkebo wakipata chakula cha usiku
huku wakibadilishana mawili
matatu.Ni Donald Nkebo aliyeomba
kuonana na rais Dr Evans Mwaluba
usiku huu.Dr Evans hakuweza
kukataa ombi la Mr Nkebo kwa
kuwa ni mmoja kati ya watu
muhimu na wanaoheshimika
sana,ni mmoja kati ya wafadhili
wakubwa wa chama.Ni kwa sababu
ya kutambua umuhimu wake ndiyo
maana usiku huu rais alitenga
muda ili aweze kuonana na tajiri
huyu mkubwa
“Mheshimiwa rais ni muda
sasa hatujaonana,siwezi
kukulaumu kwani nafahamu majukumu uliyonayo,na hii ndiyo
sababu nimeomba nionane nawe
walau tuzungumze kidogo”
Akasema Donald Nkebo huku
ajimiminia mvinyo katika glasi yake
“Mr Donald ni kweli muda
umepita hatujaonana nimekuwa
natafuta sana nafasi niweze
kukutana na watu wangu lakini
ninakosa,nimetingwa mno na
mambo mengi.Nimekuwa na ziara
nyingi za kitaifa na kimataifa na
ndiyo maana nimekuwa sipatikani
kwa urahisi.Leo nilipopata taarifa
kwamba uko Dodoma na unataka
kuonana nami nilifurahi
sana.Karibu sana Donald.Vipi
biashara zinaendaje? “Mr President hata mimi
ninafurahi sana kuonana
nawe.Kuhusu biashara zinakwenda
vizuri licha ya kushuka kwa
thamani ya shilingi na kuongezeka
kwa bei ya mafuta katika soko la
dunia lakini bado biashara
zinakwenda vizuri” Akasema
Donald Nkebo
“Hilo la kushuka kwa thamani
ya shilingi yetu linatuumiza vichwa
mimi na viongozi wenzangu
serikalini.Tumekwisha anza juhudi
mbali mbali za kuhakikisha shilingi
yetu inapanda thamani.Nina imani
tutafanikiwa”
“Ninakuamini mheshimiwa
rais.Naamini utafanikiwa katika hilo.Watu uliowapa dhamana ya
kulishughulikia suala hilo ni
wachapa kazi hodari.”
Dr Evans akacheka kidogo
akainua glasi yake ya mvinyo na
kupiga funda dogo.
“Mheshimiwa rais upepo wa
kisiasa unakwendaje?Naona
vuguvugu la urais ndani ya chama
limeanza kupamba moto”akasema
Donald
“Upepo wa kisiasa si
mbaya,bado unavuma vizuri
japokuwa kuna changamoto na
vikwazo lakini sina wasi wasi
nimekwisha jiweka vizuri ndani ya
chama”akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais hata mimi
sina wasi wasi wowote na nguvu
yako ndani ya chama lakini nina
ushauri mdogo kwako.Usijipe
uhakika sana kwamba hauna
upinzani ndani ya chama”
“Kwa nini unasema hivyo
Donald?
“Kwa hali tuliyoanza kuiona
kwa sasa inaonekana hamasa ya
kuwania uteuzi imeongezeka sana
ndani ya chama.Japo hatujui bado
nani na nani wana nia ya kuwania
uteuzi huo lakini tayari dalili
zimekwisha anza kujionyesha na ni
dhahiri unaweza ukakumbana na
upinzani mkali sana” “Nakubaliana nawe
Donald,upinzani utakuwepo lakini
kwa upande wangu sina wasiwasi
wowote naamini watajitokeza
wengi kuwania uteuzi lakini
nitakayepita ni mimi.Kwa nini
unakuwa na wasi wasi Donald?
Sura ya Donald Nkebo
ikapambwa na tabasamu.Akainua
glasi yake akapiga funda kubwa
halafu akasema.
“Mheshimiwa rais hilo ndilo
hasa ambalo limenifanya nitake
kuonana nawe ili nikupe taarifa
ambazo naamini bado hujazipata”
“Karibu Donald nakusikiliza”
akasema Dr Evans “Mheshimiwa rais tayari ndani
ya chama kuna watu wamekwisha
anza kutengeneza makundi ya
kuhakikisha kuwa wanashinda
katika uteuzi” Kauli ile ikamfanya
Dr Evans kujiweka sawa
“Jana usiku nilipata taarifa
toka katika moja ya vyombo vyangu
vya taarifa kwamba kuna kikao cha
siri kilifanyika katika hoteli ya
Dodoma palace na mwenyekiti
wake alikuwa Damian Mwamba”
akanyamaza kwa sekunde kadhaa
na kuendelea
“Damian Mwamba tayari
amekwisha anza harakati za
kuwania uteuzi ndani ya
chama.Ninazo taarifa zenye uhakika kuwa tayari amekuwa na
uungwaji mkono wa kuridhisha
toka kwa wajumbe.Timu aliyoiteua
ifanye kazi ya kutengeneza
mtandao inafanya kazi yake kwa
umakini na usiri mkubwa na
kusema ukweli hawalali wanafanya
kazi usiku na mchana kuhakikisha
wanatengeneza mtandao
mkubwa.Harakati hizi Damian
amezianza kitambo sana kwa
kujenga jina katika jamii ndiyo
maana hadi sasa jina la Damiani
Mwamba linatajwa sana katika
orodha ya watu wenye sifa na
uwezo wa kuiongoza nchi
hii.Amekuwa akitoa misaada mbali
mbali kwa vikundi vya akina mama na vijana,amejenga
mashule,hospitali na kila
linapotokea suala lolote la kitaifa
amekuwa mstari wa mbele sana.Si
kwamba namuhofia Damiani lakini
kasi anayokwenda nayo ndiyo
iliyonisukuma kutaka kuonana
nawe tujadili kwa kina kuhusu
suala hili”akasema Donald
Rais akavuta pumzi ndefu na
kumuangalia Donald Nkebo
usoni.Alionyesha uoga wa dhairi
kwa maneno yale aliyoambiwa.
Nkebo akaichukua chupa na
kumimina tena mvinyo katika glasi
yake.
“Mheshimiwa rais ,wewe ni
rafiki yangu na mimi ni mmoja wa watu wanaokuunga mkono
sana,mimi na timu yangu
tulikuunga mkono katika awamu ya
kwanza na ukafanikiwa kushinda
na bado tutaendelea kukuunga
mkono.Nadhani unafahamu kuwa
pamoja na makundi yote yaliyomo
ndani ya chama lakini timu yetu
ndiyo yenye nguvu kubwa ndani na
nje ya chama,sisi ndiyo wenye
kuamua nani awe rais wa nchi hii
na nani asiwe.Tunaangalia nani
ambaye atakuwa na manufaa
kwetu na wewe bado unaonekana
kuwa na umuhimu mkubwa kwetu
ndiyo maana nimekuja
kukuhakikishia kwamba bado
tunakuunga mkono na utapita kwa awamu nyingine.Pamoja na yote
mazuri ambayo umetufanyia
mheshimiwa rais lakini kuna jambo
dogo sana umelikosea labda ni kwa
kutokujua”akasema Donald na
kunyamaza
“Jambo gani Donald?akauliza
Dr Evans
“Ni kuhusu yule mbunge Edger
kaka.Mheshimiwa rais kama
umegundua yule kijana ni tishio
kubwa kwako kisiasa.Ugonjwa
wake alioupata ghafla
umetuonyesha ni jinsi gani
anavyopendwa na watu.Sikufichi
mheshimiwa rais yule kijana ana
nguvu kubwa.Nchi yote ilizizima
baada ya taarifa kusambaa kuwa amefariki dunia.Kasi anayokuja
nayo inaleta wasi wasi
mwingi.Naamini bado hajaweka nia
ya kugombea lakini kama akiamua
kutangaza kuwania urais tutakuwa
na kazi kubwa.Naelewa hana
mtandao mkubwa ndani ya chama
lakini anaweza kushawishiwa
kujiunga na chama pinzani ili
agombee urais na kama akifanya
hivyo mheshimiwa rais basi
shughuli itakuwa ngumu.Kuna
uwezekano mkubwa kijana yule
akatwaa nchi” Donald akatulia
akanywa funda kubwa la mvinyo
akaendelea
“Kilichomtokea Edger ni
mkakati mzito wa kumuondoa katika ulingo wa siasa kwani
uwepo wake bungeni na katika
siasa ni hatari kwa watu
wengi.Edger alitakiwa afariki dunia
jana.Mheshimiwa rais kosa
ulilolifanya ni kutoa ndege yako
kumsafirisha Edger kumpeleka
kutibiwa nje ya nchi.”
Rais akatoa kitambaa na
kujifuta jasho lililoanza kumtoka.
“Donald sikujua kama tukio lile
ni makakati maalum na wala
sikuwa nikiifahamu hatari ya huyu
kijana.Kama ningeambiwa kwamba
ule ni mkakati maalum wa
kumuondoa ningeweka nguvu
yangu kubwa na kummaliza haraka
sana lakini sikujua lolote ndiyo maana nikaamua kumsaidia kuokoa
maisha yake.Donald nashukuru
umenifumbua macho kuhusu
mambo yanayoendelea chini kwa
chini ndani ya chama,nakiri hakuna
katika watu wangu wa karibu
aliyekuja kunieleza mambo haya
uliyonieleza.Nashangaa hata
washauri wangu wamekaa kimya
wakati kuna hatari kubwa
inatukabili.Ninaanza kuhisi
yawezekana hata washauri wangu
watakuwa tayari
wamesharubuniwa na ndio maana
wamekaa kimya na kusubiri
kuanguka kwangu.Haiwezekani
wakashindwa kuwa na taarifa za
kinachoendelea ndani ya chama.Ahsante sana Donald kwa
taarifa hii uliyonipa.Imenifumbua
macho” Akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais,usipate
shida yoyote mimi na timu yangu
tupo na tunakuhakikishia nafasi ya
urais ni yako ila nitakuelekeza nini
cha kufanya kama utakuwa tayari
kufuata ushauri wangu”
“Kwa nini nisifuate ushauri
wako Donald wakati wewe ndiye
uliyekuja kunifumbua macho?
Nielekeze nifanye nini.”
“Kama nilivyokwisha kueleza
mheshimiwa rais mimi na timu
yangu tutahakikisha unashinda
katika awamu ijayo lakini kuna
mambo ambayo lazima tuyafanye.Kitu cha kwanza
tunachotakiwa kukifanya ni kuunda
timu ndogo ya watu ambayo
itafanya kazi ya kuchunguza
mwenendo wa siasa na kuangalia
nini tufanye ili tuweze kupata
ushindi ambayo itakubidi
mheshimiwa rais uiwezeshe ili
iweze kufanya kazi zake kikamilifu
bila kugundulika.Timu hii itakuwa
ya watu sita ambao nitakupa
majina yao.Ni watu ambao
inakupasa uwaamini kwa sababu ni
wataalamu katika michezo hii ya
kisiasa.Kitu cha pili ambacho
tutakifanya baada ya kuunda timu
hii ni kuwanyamazisha wale wote
wanaoonekana kuwa na nguvu kisiasa na kuhatarisha urais wako
kwa kipindi kingine.”
Dr Evans akamtazama Donald
Nkebo halafu akauliza.
“Kuwanyamazisha kivipi?
“Mr resident politics is a dirty
game and to win this game you
need to play dirty too” Akasema
Nkebo.
“Bado sijakuelewa Nkebo hebu
nifafanulie vizuri”
“Mheshimiwa rais ninaposema
kumnyamazisha mtu yeyote
mwenye kuwa na nguvu kisiasa
nina maana ya kumpunguzia nguvu
aliyonayo na wakati mwingine
ikibidi hata kumuondoa katika uso
wa dunia hii iwapo kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.Kazi hii
si rahisi,inahitaji umakini na
wataalamu wa hali ya juu mno
ndiyo maana nikasema inabidi
tuwezeshwe ili kufanikisha
shughuli kama hizi.Kwa
kuanzia,tutaanza na wale ambao
tayari wamekwisha onyesha wazi
dhamira zao za kuwania urais kama
Mr Damian na huyu kijana
Edger.Sisi tutawashughulikia bila
hata ya mtu yeyote kuhisi kuwa
unahusika kwa namna yoyote na
wao.Ninakuhakikishia Mheshimiwa
rais kuwa hakuna mtu atakayejua
nini tunakifanya”
Sura ya rais ikajenga tabasamu
pana baada ya Donald kumchambulia kwa kina jinsi
mambo yatakavyoendeshwa ili
kuwamaliza wabaya wake
kisiasa.Mpaka wanamaliza
maongezi Dr Evans akamkabidhi
rasmi Donald Nkebo jukumu la
kuhakisha kuwa wale wote
wanasiasa wanaoonekana kuwa na
nguvu ndani na nje ya chama na
ambao wanaonyesha dhamira ya
wazi ya kugombea urais
wanamalizwa kimya kimya.Rais
alimuahidi Nkebo kumuwezesha
yeye na kamati yake kwa kila kitu
watakachohitaji,kama vile ulinzi na
fedha.Saa saba za usiku walimaliza
maongezi yao na Donald akaagana
na rais akaondoka .
 
We endelea na episode zetu **** hujaingiwa na utamu wa riwaya hii tuachie sisi tuendeleee
 
SIRI
Episode 9
Mtunzi. Patrick CK

BAADA YA SIKU 5
HAIFA - ISRAEL
Siku ya tano zimepita toka
mheshimiwa Edger kaka apelekwe
Rambam medical center mjini Haifa
Israel.Operesheni aliyofanyiwa ili
kuondoa sehemu za mwili wake
zilizoharibiwa na sumu,ilifanikiwa
na madaktari walifanikiwa
kuyaokoa maisha ya mbunge
Edger.Dr Olivia Themba hakuweza
kuizuia furaha aliyonayo baada ya
kupambana na kuokoa maisha ya
Edger.Kwake lilikuwa ni jambo la
furaha kubwa.Moyoni alijipongeza
kwa ujasiri alioupata wa
kumsafirisha Edger nje ya nchi.

Hali ya Edger ilikuwa
imeimarika sana.Licha ya hali yake
kuonyesha maendeleo mazuri,bado
alikuwa katika uangalizi maalum
wa madaktari na kwa muda huo
wote hakuna aliyeruhusiwa
kuonana naye zaidi ya Dr Olivia na
ulinzi uliimarishwa sana katika
chumba alimokuwemo.
Siku ya tano Edger aliamka
vizuri akiwa mchangamfu na
anayeweza kuongea
vizuri.Madaktari wakachukua tena
vipimo na majibu yalionyesha
hakukuwa tena na hatari yoyote
inayomkabili Edger.Hizi zilikuwa ni
taarifa nzuri sana kwa Dr Olivia Daktari aliyekuwa
akimuhudumia Edger akamuacha
Edger na Dr Olivia.
“Edger nimefurahishwa sana
na maendeleo yako” akasema Dr
Olivia
Edger alijitahidi
kutabasamu.Alitamani ainuke na
kwenda kumkumbatia Dr Olivia
lakini hakuwa bado na nguvu za
kufanya hivyo.
Dr Olivia aliiona furaha
aliyokuwa nayo Edger na kwa kuwa
hakuwa na nguvu za kuinuka
akamfuata pale kitandani
akamkumbatia huku naye machozi
ya furaha yakimtoka akiwa haamini
kama ni kweli kijana yule kipenzi cha wengi aliyekuwa anachugulia
kaburi amenusurika kifo.
“Dr Olivia sijui nikushukuruje
kwa namna ulivyoyaokoa maisha
yangu.Wewe ni daktari wa kweli”
Edger alisema huku naye machozi
yakimlenga lenga.
“Usijali Edger haya yote ni
maongozi ya Mungu.Yeye ndiye
anayepanga kila kitu kiwe.Sifa zote
na utukufu tumrudishie yeye”
Dr Olivia akaenda kukaa katika
kiti kilichokuwa pembeni ya
kitanda.Dr Olivia alikuwa akiipitia
ripoti ya madaktari kuhusu
maendeleo ya mgonjwa lakini
Edger bado aliendelea kumtazama
Dr Olivia kwa makini. “Dr Olivia nani anakulipia
gharama za hoteli na kila kitu?
Edger akauliza
“Gharama zote ninalipa
mwenyewe” Olivia akajibu huku
akitabasamu.Edger akashangaa.
“Unalipa mwenyewe?
Akauliza.
“Ndiyo mheshimiwa ninalipa
mwenyewe.Kuna ubaya wowote?
“Hakuna ubaya Dr Olivia,ila
kwa kawaida gharama hizi
zilipaswa kulipwa na serikali”
Dr Olivia akacheka kidogo
halafu akasema
“Usijali mheshimiwa
Edger.Mimi nitalipa tu si gharama
kubwa za kunishinda.” “Serikali hawajui kama
nimefuatana na wewe huku? Edger
akauliza
“Mheshimiwa Edger kuna
mambo mengi ya kuongea lakini
kwa sasa naomba tujielekeze
kuhakikisha unapata nguvu za
kutosha na hayo masuala mengine
tutaongea baadae”
Huku akitabasamu kwa mbali
Edger akasema
“Dr Olivia huku tuko ugenini
hivyo naomba mambo ya
uheshimiwa tuyaweke
pembeni.Niite Edger inatosha”
Dr Olivia akatabamu.
“Unaitwa Dr Olivia
Themba,right? “Ndiy😵livia Themba” Akajibu
Olivia huku akitabasamu
“Are you related in anyway
with Agrey Themba?Mmefanana
sana” akasema Edger
Kicheko kidogo cha chini chini
kikamtoka Dr Olivia
“He’s my father”Akajibu kwa
ufupi
“Nilikuwa nahisi hivyo kwani
unafanana naye sana.Ninamfahamu
Agrey japo hatuna ukaribu
mkubwa”akasema Edger
Edger akakaa kimya kidogo
akiwaza
“Kumbe Olivia ni mtoto wa
Agrey Themba.Sura yake si ngeni
machoni mwangu.Hata hivyo ninachoshukuru mrembo huyu
ameyaokoa maisha yangu.Lakini
kuna kitu bado kinanisumbua akili
yangu kwa nini hawataki kuniweka
wazi ugonjwa ninaoumwa
uliosababisha nikaletwa hapa
Israel? Nimefanyiwa upasuaji na
sielewi ni upasuaji wa nini.Serikali
kugharamia matibabu yangu nje ya
nchi lazima tatizo langu liwe
kubwa.Nimekuwa makini sana
katika kupima afya mara kwa mara
na kila ninapopima nakutwa na
afya nzuri,nashangaa ni ugonjwa
gani huu ulionitokea ghafla?
Akajiuliza Edger na kurejesha
kumbu kumbu bungeni. “Nakumbuka nikiwa najiandaa
kuwasilisha hoja yangu
bungeni,nilianza kuhisi
usingizi,nikajikuta macho yakiwa
mazito.Sikujua kilichoendelea hadi
nilipofumbua macho na kujikuta
nchini Israel nikiwa hospitali tena
nimefanyiwa upasuaji ambao sijui
ni wa nini.Si kawaida yangu mimi
kusinzia bungeni,nashangaa siku ile
nini kilinitokea hadi nikalala.Lakini
toka asubuhi kabla ya kuanza
kujisikia kulala nilikuwa na nguvu
za kutosha na nikauliza swali la
nyongeza? Najaribu kuunganisha
picha lakini sijapata picha kamili.I
think something is wrong
here.They must tell me everything” Edger akazama katika lindi la
mawazo
“Edger unawaza nini?
Akauliza Dr Olivia baada ya
kumuona Edger amenyamaza
akionekana kuwa katika mawazo
mengi.
“Dr Olivia kuna mambo bado
yananiumiza kichwa kuhusiana na
ugonjwa wangu.Bado nahitaji
ufafanuzi wa kina ninaumwa nini
,ilitokeaje nikaletwa huku
Israel,nimefanyiwa upasuaji lakini
sijui nimefanyiwa upasuaji wa
nini.Hakuna aliyenieleza
chochote,naamini wewe utakuwa
unafahamu kuhusu ugonjwa
wangu.Kama unafahamu chochote naomba unieleze
tafadhali”akasema Dr Olivia
Dr Olivia akamtazama Edger
usoni kwa sekunde chache halafu
akamsogelea na kusema
“Edger ni kweli una haki ya
kujua kila kitu kuhusu ugonjwa
wako,kilichotokea mpaka wewe
ukaletwa hapa.Kwa hivi sasa bado
unahitaji kupata nguvu za kutosha
na wala si wakati wa kuuchosha
ubongo wako kwa kuwaza mambo
mengi.Ninakuahdi utakapokuwa na
nguvu za kutosha utaelezwa kila
kitu”akasema Dr Olivia
Kauli ile ilimfariji Edger.
“Edger nahitaji kuwasiliana na
mheshimiwa spika nimjulishe juu ya maendeleo yako.Waheshimiwa
wabunge pamoja na wananchi wote
hususan wafuasi wako wanafuatilia
kwa karibu sana kuhusu maendeleo
yako.”
Dr Olivia akatoka mle
chumbani na kuelekea ofisini kwa
daktari kwa ajili ya kumpigia simu
spika wa bunge kumjulisha kuhusu
maendeleo ya Edger kaka
“Madam Spika shikamoo” Dr
Olivia akamsalimu spika wa bunge
baada ya kumpata simuni.
“Marahaba Dr Olivia,habari za
huko? Mgonjwa anaendeleaje?
“Mama Spika,hali ya Edger
inaendelea vizuri.Nimetoka
kuongea naye muda si mrefu.Maendeleo yake yanatia
moyo sana.Mama spika kuna suala
sikuwa nimekueleza lakini Edger
alikuwa na tatizo kubwa mno na
kama tusingechukua hatua za
haraka basi tungempoteza”
“Alikuwa akisumbuliwa na nini
Dr Olivia?
“Mama spika naomba
usimwambie mtu yeyote kwa
sababu hata Edger mwenyewe
bado hajui chochote.Edger
aliwekewa sumu.Kwa mujibu wa
madaktari ni kwamba sumu hiyo
maarufu kwa kuua taratibu iliingia
mwilini kwa kupitia ngozi na
inawezekana sumu hiyo alipuliziwa au alitumia sabuni ya kuogea yenye
sumu”
Spika wa bunge alistushwa
mno na taarifa ile.Alipomaliza
kuongea na Dr Olivia mheshimiwa
spika akavuta pumzi
ndefu.Akasimama na kuzunguka
zunguka humo ofisini kwake.
“Nilihisi lazima kuna kitu
hakiko sawa.Suala la ugonjwa wa
Mheshimiwa Edger lilikuwa na
sarakasi nyingi hivyo na nilihisi
kuna mchezo unafanyika.Lengo la
kumuwekea sumu ni kumuua na
ninadhani sababu kubwa ni huu
mswaada binafsi aliotaka
kuuwakilisha ili kuliomba bunge
liunde kamati teule kuchunguza kufilisika kwa benki ya taifa ya
vijana.Katika muswaada ule Edger
ametamka wazi kuwa na ushahidi
wa kutosha wa kuwatia hatiani
vigogo waliohusika na ubadhirifu
na kusababisha kufilisika kwa
benki ya taifa ya vijana. Nina hakika
hii itakuwa ni sababu tosha.Nina
uhakika lengo la watu hawa
lilikuwa ni kuzuia kusomwa kwa
muswaada ule bungeni.Tuna kila
sababu ya kumlinda kijana huyu ili
asije akadhurika.I need to do
something.I need to find someone I
can trust ….”akawaza spika
Mwenendo wa siasa ulianza
kumtisha spika wa bunge.Akakaa
kitini akatafakari na kuchukua kikaratasi akaandika ujumbe mfupi
akamuita mtumishi wa ofisi yake
na kumpatia kile kijikaratasi.
“Maria nenda kampe waziri
mkuu ujumbe huu”
Kwa sasa waziri mkuu
mheshimiwa Adamson mwakaleli
ndiye aliyekuwa mtu pekee
aliyeweza kumwamini.
Shughuli za bunge zilikuwa
zikiendelea kama
kawaida,mtumishi wa ofisi ya spika
akaingia bungeni na moja kwa moja
akaelekea alipokuwa amekaa
waziri mkuu na kumpatia ile
karatasi iliyotoka kwa mheshimiwa
spika.Waziri mkuu akaifungua ile
karatasi na kuisoma. “Mheshimiwa waziri mkuu
naomba tuonane nyumbani kwako
leo jioni.Muhimu sana” ndivyo
ulivyosomeka ujumbe ule
Haikuwa kawaida ya
mheshimiwa Spika kuomba
kuonana na mheshimiwa waziri
mkuu hasa mida ya jioni tena
nyumbani kwa waziri mkuu.Moja
kwa moja akahisi kuna suala nyeti
la kuongea.Mheshimiwa Waziri
mkuu akaandika ujumbe mfupi
katika kikaratasi na kumpatia
mtumishi wa bunge aupeleke kwa
spika kuwa waonane jioni hiyo
nyumbani kwake..
Kikao cha jioni
kilipomalizika,mheshimiwa spika akamaliza shughuli zake za siku
haraka kisha akapanda gari na
kuelekea moja kwa moja nyumbani
kwa waziri mkuu.
“Pole sana kwa kazi za leo
mheshimiwa waziri mkuu”
akasema spika baada ya kufika na
kupokelewa na waziri mkuu
nyumbani kwake.
“Ahsante spika nimeshapoa.
Mijadala ya leo ilikuwa moto moto
kweli” akasema waziri mkuu.
“Nilipata ujumbe
wako,nikaogopa.Nikasema moyoni
mpaka mheshimiwa spika aamue
kuonana na mimi nyumbani
kwangu usiku huu lazima kuna
jambo nyeti sana” Spika wa bunge akamtazama
waziri mkuu kisha akasema
“Ndiyo waziri mkuu.Kuna
taarifa niliipata mchana wa leo
ikanichanganya na kunifanya
niombe kuonana nawe..”
Waziri mkuu akatoa miwani
yake akiweka mezani na kumkazia
macho Spika.
“Taarifa gani hiyo mheshimiwa
spika?
“Mheshimiwa waziri
mkuu,jambo ninalotaka kukueleza
ni siri kubwa.Linamuhusu mbunge
Edger”
“Mheshimiwa Edger?
“Leo mchana nimepigiwa simu
na Dr Olivia Themba ambaye ndiye aliyempeleka Mheshimiwa Edger
nchini Israel.Dr Olivia amenieleza
kwamba ripoti ya uchunguzi ya
madaktari katika hospitali
anakotibiwa Edger inaonyesha
kuwa alipewa sumu”
“Sumu ?? Mheshimiwa waziri
mkuu akauliza kwa mshangao.
“Ndiyo mheshimiwa waziri
mkuu.Kilichotaka kumuua ni sumu
kali ambayo kwa mujibu wa
madaktari sumu hiyo iliingia
mwilini kupitia katika ngozi na
inahisiwa aidha alipuliziwa au
ilipakwa katika sabuni ya
kuogea.Mheshimiwa waziri mkuu
kama utakumbuka alitaka
kuwasilisha muswada binafsi bungeni lakini alishindwa kufanya
hivyo baada ya kuumwa
ghafla.Ninahisi sababu ya kutaka
kuuawa ni muswada ule kwani
katika muswada ule kuna mahala
anaeleza wazi kwamba anao
ushahidi wa kutosha wa
kuwahusisha baadhi ya vigogo wa
serikalini na wafanya biashara
wakubwa kushiriki katika ufisadi
mkubwa uliopelekea benki ya taifa
ya vijana kufilisika”akasema Spika
ukapita ukimya mfupi
“Nilikwenda Dar es salaam
kuhakikisha Edger anapatiwa
matibabu stahili.Sijamueleza mtu
yeyote mambo yaliyotokea
huko.Mheshimiwa waziri mkuu,kulikuwa na sarakasi nyingi
kuhusiana na matibabu ya Edger”
akasema Spika na kumsimulia
waziri mkuu kila kitu kilivyokuwa
hadi Edger akasafirishwa kwenda
Israel.
Waziri mkuu alisikiliza kwa
makini huku huku akiutikisa mguu
wake wa kulia.
“Mheshimiwa spika hili suala
ulilonieleza limenistua na hata
kuniogopesha sana,sikuwa
nikifahamu kama kijana yule yuko
katika hatari kubwa namna hii.
Nimekuwa katika siasa kwa muda
mrefu lakini sijawahi kuona wala
kutegemea kama siasa yetu
inaweza ikatupeleka mahala hapa.Taarifa hii imenipa picha ya
wazi kuwa mbunge huyu yuko
katika wakati mgumu
sana,anapambana vita kubwa na
kundi la watu wachache weye
nguvu.Sijausoma muswada wa
mheshimiwa Edger lakini kama
kuna mahala ameonyesha kuwa
anao ushahidi wa wazi wa
kuwahusisha baadhi ya vigogo
serikalini na kufilisika kwa benki ile
ya vijana,basi hiyo ni sababu tosha
ya kumsababishia matatizo haya
makubwa hata kutaka kuuawa”
Ukimya mfupi ukapita kila
mmoja akitafakari “Nionavyo mimi ngoja
niwasiliane na Mheshimiwa rais ili
tuangalie nini cha kufanya”
“Hapana waziri mkuu” Spika
akadakia
“Sidhani kama hilo ni wazo
zuri.Hatujui mtandao huu
unawahushisha akina nani.Huu
unaonekana ni mtandao wenye
nguvu kubwa.Ninachokifikiria
inabidi tushirikiane kwanza
mimi,wewe na Dr Olivia
kuhakikisha Edger anapona na
kurudi nyumbani
salama.Atakaporudi tutapata wasaa
mzuri wa kujua tufanye nini
kumsaidia kupambana na genge hili
la mafisadi ambao wametaka kumuua.Nina hofu hata huko aliko
anaweza akafuatwa na kuawa hivyo
nguvu kubwa kwa sasa ni
kuwekeza katika kuhakikisha
Edger anapona.Dr Olivia
amenihakikishia kuwa ameomba
ulinzi wa kutosha hapo hospitalini
na hakuna mtu yeyote
anayeruhusiwa kuonana na Edger
labda kwa ruhusa maalum toka
kwake yeye Dr Olivia”akasema
spika
Waziri mkuu akakuna
kichwa,akarekebisha miwani yake
akasema.
“Nakubaliana na mawazo yako
mheshimiwa Spika kuwa kwa sasa
usalama wa Edger ni muhimu zaidi.Kama ulivyoshauri naomba
suala hili liwe siri kati yangu
mimi,wewe na Dr Olivia hadi hapo
tutakapopata nafasi ya kukaa na
Edger akatueleza kila kitu ili tujue
tutafanya nini kukabiliana na hili
genge la mafisadi.Ninashauri pia
kama kuna mambo Edger
aliyagundua kuhusiana na mtandao
huu wa mafisadi na anao ushahidi
kuna kila ulazima wa kuulinda
ushahidi huo kwa gharama zozote
ili tuutumie kuwafikisha mbele ya
sheria wale wote waliohusika
katika sakata zima la kuifilisi benki
ya vijana.Nimefikiria kumpatia
Edger mlinzi wa siri wa kumlinda
na hatari zozote zile.Huyu ni mlinzi wangu wa siri aitwaye Dickson
Kipuma.Huyu ni kijana hatari
mno.Alikuwa anafanya kazi katika
idara ya usalama wa taifa na kwa
kuwa naufahamu vema utendaji
wake wa kazi niliamua kumchukua
na kumuweka kuwa mlinzi wangu
wa siri.Nakuhakikishia
mheshimiwa spika kuwa kijana
huyu ana uwezo mkubwa sana.Nina
uhakika Edger atakuwa katika
mikono salama.Yeye hatajionyesha
kwake wazi wazi,bali atakuwa
akimlinda kwa siri kama
anavyonilinda mimi.Tukifanya
hivyo tutakuwa na uhakika wa
kuyalinda maisha ya Edger na kuulinda ushahidi alionao juu ya
hili genge la mafisadi”
Waziri mkuu alionyesha wazi
hasira aliyokuwa nayo juu ya genge
la mafisadi lenye nguvu.Spika na
waziri mkuu wakakubaliana
kumpatia Edger mlinzi wa siri kwa
ajili ya kuhakikisha anakuwa
salama
HAIFA - ISRAEL

Dr Olivia akiwa katika hoteli
alikofikia alimpigia simu baba yake
Agrey Themba
“Baba shikamoo” Akasema Dr
Olivia “Marahaba Olivia hujambo?
Nimekuwa na wasi wasi mwingi
kuhusiana na ukimya wako kwa
sababu umenipigia simu mara moja
tu.Unaendeleaje huko?Vipi hali ya
mgonjwa wako?
“Samahani baba kwa ukimya
huu lakini ni kutokana na
kukabiliwa na mambo mengi
.Kuhusu mgonjwa nashukuru
Mungu kwa sasa anaendelea
vizuri.Alifanyiwa upasuaji na hali
yake inatia matumaini.Kwa sasa
anaweza kuongea na ameanza
mazoezi mepesi.Nina imani muda si
mrefu atakuwa katika afya njema
kabisa” “Nafurahi kusikia
hivyo.Nimefarijika mno kwa
maendeleo mazuri ya mbunge
wetu.Unastahili pongezi kubwa
kwa kazi nzito
uliyoifanya”akasema Agrey
“Usijali baba,hii ni kazi yangu
na siku zote siko tayari kuona
mgonjwa akipoteza maisha wakati
kuna uwezekano wa kuyaokoa
maisha yake.Nilichokifanya
kingeweza kufanywa na daktari
yeyote yule ambaye anaijua vyema
kazi yake.”Dr Olivia akasema
“Nimekuelewa Olivia.Lini
unatarajia kurudi nyumbani?
“Kwa sasa siwezi kuwa na jibu
lini nitarudi hadi nitakapohakikisha kuwa mgonjwa amepona
kabisa.Mimi ndiye niliyemleta huku
Israel na ndiye nitakaye mrudisha
nyumbani.Usihofu kitu baba ,nina
uwezo wa kujihudumia mwenyewe
na hakuna tatizo lolote”
Agrey akafikiri kidogo halafu
akasema.
“Olivia mwanangu,kama
mgonjwa anaendelea vizuri,kwa
nini basi usimuache wewe ukarudi
kuendelea na shughuli zako?Kwa
hapo ulipofika unaweza ukaiachia
serikali iendelee
kumuhudum………..”Dr Olivia
akadakia kabla baba yake
hajamaliza alichotaka kukisema “Baba kamwe siwezi kufanya
kitu kama hicho kumuacha Edger
katika mikono ya serikali.Baba
kuna mambo mengi yanayofanyika
ndani ya serikali wewe huwezi
kuyajua.Hili sakata la ugonjwa wa
Edger limenifundisha mambo
mengi.Kama nisingefanya maamuzi
magumu ya kumleta Edger huku
Israel hivi sasa
tungekwishamzika.Daddy kwa
taarifa yako tu ni kwamba Edger
alitaka kuuliwa kwa
sumu.Madaktari hapa Israel
wamelithibitisha hilo”akasema Dr
Olivia
Agrey Themba akavuta pumzi
ndefu “Hii taarifa imenistua
kidogo.Nani hawa walitaka kumuua
yule kijana? Akauliza Agrey
“Edger aliwekewa sumu kali ya
kuua taratibu na ndiyo maana
kulikuwa na dana dana nyingi
katika kulishughulikia suala la
kumsafirisha Edger nje ya nchi kwa
sababu lengo lilikuwa kupoteza
muda ili Edger afe”
“Olivia hili suala tayari
limeniogopesha.Kuwa karibu na
Edger ni hatari kubwa
kwako.Kama maadui zake
walikuwa na lengo la kumuua ni
wazi wanaweza wakamfuata hata
huko huko aliko na kumuua.Achana
na mgonjwa huyo mwanangu rudi nyumani haraka kwa ajili ya
usalama wako” Agrey akasema kwa
sauti yenye wasiw asi.
“Baba nimesema siwezi kurudi
kwa sasa na kumuacha mgonjwa
peke yake,nitarudi nyumbani pale
Edger atakapokuwa amepona
kabisa.Usijali baba nitakuwa
salama,tumepatiwa ulinzi wa
kutosha”akasema Dr Olivia
“C’mon Olivia”
“Please dady” akasema Dr
Olivia
“Nani mwingine anajua kuhusu
suala hili la Edger kuwekewa
sumu? Agrey akauliza “Nimemueleza spika wa bunge
pekee,hata Edger mwenyewe hajui
chochote bado”
“Sawa Olivia naomba hii ibaki
siri yako.Usimwambie tena mtu
yeyote suala hili itakuweka katika
hatari kubwa”
“Dady,siwezi kuwaeleza watu
suala hili lakini kwa Edger siwezi
kuendelea kumficha kwa muda
mrefu.Pindi hali yake itakapokuwa
nzuri ni lazima nimweleze ukweli
ili achukue hatua stahili”
“Olivia nashukuru kwa
kunipigia simu.Tafadhali kuwa
mwangalifu siku zote.Muda
wowote ukiona au kuhisi jambo lolote baya nipigie simu haraka
sana”akasema Agrey
“Nitafanya hivyo dady
.Ahsante.Bye”
Dr Olivia alimaliza
kuzungumza na baba yake Agrey
Themba na kukata simu.
“I hate politics” akanong’ona
DAR ES SALAAM
Baada ya kumaliza kuongea na
mwanae,Agrey Themba akampigia
simu rais Dr Evans.
“Agrey” akasema Dr Evans
“Evans nimetoka kuzungumza
na Olivia muda si mrefu”
 
SIRI
Episode 10
Mtunzi. Patrick CK

“Nilikuwa na mpango wa
kukupigia nizungumze nawe
kuhusu Dr Olivia.Amefanya kazi
kubwa sana ya kuokoa maisha ya
Edger Kaka.Anastahili heshima
kubwa sana.Kwa sasa baada ya hali
ya Edger kuendelea vyema Dr
Olivia anaweza akarejea nyumbani
kuendelea na majukumu
yake,serikali tutapeleka muangalizi
maalum wa kumuhudumia Edger
hadi hapo atakapopona
kabisa”akasema rais Dr Evans
“Nimezungumza naye kuhusu
suala hilo la kurejea nyumbani kuja
kupumzika lakini amegoma kabisa
amedai kwamba atarejea nyumbani
pale Edger Kaka atakapopona
kabisa”akasema Agrey Themba
“Basi hakuna tatizo kama
anapenda kuendelea kukaa kule
kumuhudumia Edger hakuna tatizo
anaweza kuendelea lakini yeye ni
mtu mkubwa ni daktari tegemeo
kabisa katika hospitali kuu ya moyo
alipaswa awepo huku akihudumia
watu kuliko kupoteza muda kule
kumuhudumia mgonjwa mmoja”
akasema Dr Evans
“Evans kuna jambo amenieleza
limenistua kidogo ndiyo
limenifanya nikupigie simu”
“Jambo gani Agrey? “Ameniambia kwamba
madaktari wamegundua kwamba
Edger aliwekewa sumu”
“Sumu?akauliza DrEvans kwa
mshangao
“Ndiyo wanadai aliwekewa
sumu.Nina hofu sana na maisha ya
Olivia.Watu hawa waliotaka
kumuua Edger wanaweza
wakamfuata hata huko aliko.Kwa
kuwa Olivia amekataa kurudi hadi
Edger apone ninaomba umsaidie
ulinzi.Wewe ni rais unaweza
ukaomba ulinzi hata kwa uongozi
wa Israel wawalinde Edger na
Olivia kwa muda wote
watakaokuwa nchini Israel”
akasema Agrey “Agrey hizi taarifa za Edger
kuwekewa sumu ninazisikia kwa
mara ya kwanza kwako”
“Ni taarifa ya siri ambayo hata
Edger mwenyewe bado
hajaambiwa.Evans nina hofu sana
na mwanangu Olivia”
“Usihofu Agrey nitafanya
utaratibu wa haraka kuwatafutia
ulinzi Olivia na Edger na watakuwa
salama”
“Nitashukuru sana kwa hilo
Evans.Tafadhali hakikisha Olivia
anakuwa salama” akasema Agrey
Baada ya kuzungumza na
Agrey,rais Dr Evans akampigia
simu Donald Nkebo “Mheshimiwa Rais” Akasema
Donald Nkebo.
“Donald ,uko wapi mida hii?
“Bado niko Dodoma
mheshimiwa rais” akajibu Donald
“Donald naomba unisikilze
kwa makini” akasema Dr Evans
“Nakusikiliza mheshimiwa
Rais”
“Nimepata taarifa kutoka
Israel anakotibiwa Edger
kaka.madaktari kule wamegundua
kuwa Edger aliwekewa sumu”
“Mheshimiwa rais kama
tulivyozungumza jana kwamba huu
ulikuwa ni mpango mahsusi wa
kumuondoa Edger.This is politics
Mr president.It’s a dirty game and to win this game you have to play
dirty too.Edger aliingia mahala
kusikomuhusu na lengo lake likawa
ni kutafuta sifa na umaarufu kwa
wananchi kwa kuanika baadhi ya
mambo yasiyo muhusu.Kwa ufupi
mheshimiwa rais mimi na
wenzangu kuna vijisenti tulivichota
pale katika benki ya taifa ya vijana
na benki ikatetereka na kufa
kabisa.Edger katika ufukunyunyu
wake akaligundua hilo na akaona ni
suala ambalo litaweza kumuweka
juu kisiasa.Kama nilivyokueleza
tulipokutana Dodoma endapo
Edger angefanikiwa kulianika suala
hili hadharani angejiimarisha sana
kisiasa.Watanzania kwa sasa wamechoshwa na mambo haya ya
ufisadi usiokwisha.Mheshimwa
Rais kwa ajili ya kujilinda sisi
wenyewe,na kwa ajili ya kukulinda
wewe mwenyewe tukaamua
kuutekeleza mpango ule ambao
japo haukufanikiwa,lakini kwa kiasi
kikubwa umempa onyo yule kijana
na sisi tumepata nafasi ya
kujipanga vyema kukabiliana naye”
akasema Donald.
Dr Evans akakaa kimya
akitafakari halafu akasema.
“Nimekuelewa Donald,nataka
kujua namna mlivyojipanga.Ni
hatua gani inafuata kukabiliana na
haya mambo? Huku akitabasamu Donald
Nkebo akasema
“Mheshimiwa rais,tayari
nimeteua watu sita ambao wote ni
wataalamu wa michezo hii ya
siasa.Kwanza niko mimi halafu
yuko waziri wa afya Dr Maneno
,halafu yuko Mr Faidh al
badir,Mheshimiwa mbunge
Ngimarwa,mheshimiwa mbunge
Alfred sakalani,na mheshimiwa
mbunge Maria Cheseko.Hii ndiyo
timu itakayokurudisha madarakani
Mheshimiwa Rais.Wote hawa ni
wazoefu wa miaka mingi wa
mambo haya ya siasa.Baada ya
kuiunda timu hii kitu cha kwanza ni
kuanza kutafiti kwa kina hali ya upepo wa kisiasa inavyovuma hapa
nchini kwa sasa halafu tutaanza
kuwashughulikia wale wote wenye
kuonyesha nia ya kugombea urais
na ambao wanaonekana kuwa na
nguvu kubwa kisiasa ndani na nje
ya chama.Kwa kuanzia tutaanza na
hawa waheshimiwa wawili ambao
ni Mheshimiwa Damiani mwamba
na mheshimiwa Edger.
Mheshimiwa rais kwa kuwa
umeshatukabidhi jukumu hili kaa
pembeni tuachie sisi tuucheze
mchezo huu na wewe usubiri
matokeo mazuri.Edger tunataka
kumuondoa kabisa lakini Damiani
yeye tunataka kumuua kisiasa
lakini pale itakapoonekana kuna ulazima wa kumuondoa tutafanya
hivyo” Akasema Donald Nkebo.
“Nimekuelewa Donald lakini
nina ombi moja.Naomba kwa sasa
msifanye lolote kuhusiana na Edger
hadi hapo atakapokuwa amerejea
nyumbani.Binti wa rafiki yangu
mkubwa yuko naye huko Isarel
anamuuguza na sitaki adhurike
kwa namna yoyote ile”
“Mheshimiwa rais sisi ni watu
makini mno na tunafanya kazi zetu
kwa umakini mkubwa.Hatutaweza
kufanya kitu chochote cha
kumdhuru Edger akiwa nje ya nchi
isipokuwa akiwa kule tutamtuma
mtu wetu ambaye atakuwa
akimchunguza na kutupa taarifa zake zote.Tunataka utusaidie kwa
hilo mheshimiwa rais.Kuna binti
atakayefanya kazi hiyo ambaye
atapelekwa nchini Israel kwa ajili
ya kumsaidia Dr Olivia kumuuguza
Edger.Dr Olivia akijua wewe ndiye
uliyemtuma binti yule aende
akamsaidie hatakuwa na shaka
yoyote” akasema Donald Nkebo
“Donald nimekuelewa vizuri
sana,ila tafadhali naomba binti
yangu aihusishwe na kwa namna
yoyote ile na lolote litakalokuwa
likendelea kwa Edger.Msichana
huyo tutakayemtuma ni mpelelezi
mzoefu na anajua nini cha
kufanya.Yeye kazi yake ni
kukusanya taarifa ili tujue Edger anafanya nini,anawasiliana na nani
na wanaongea nini”
“Sawa nimekuelewa Donald
tutawasiliana zaidi” akasema Dr
Evans akaagana na Donald
****************

“Judy kama nilivyokueleza kazi
unayotakiwa kuifanya huko Israel
ni kuhakikisha unapata mwenendo
mzima wa maisha ya Edger.Fuatilia
mawasiliano yake yote ya
simu,rekodi maongezi yote
anayoongea,na chochote
anachofanya,hadi watu wanaokuja
kumtembelea.Tafadhali usifanye
kosa ambalo litamfanya agundue kuwa unamchunguza nyendo
zake.Tumeelewana? Akauliza
Donald Nkebo
“Nimekuelewa Bosi
wangu.Nakuomba usiwe na shaka
yoyote na mimi.Unafahamu
utendaji kazi wangu ulivyo.Kamwe
sijawahi kukuangusha.” Akasema
Judy msichana ambaye anatumwa
kwenda Israel kumchunguza Edger
kwa kivuli cha kumsaidia Dr Olivia .
“Nafurahi kusikia hivyo
Judy.Nakutakia safari njema hiyo
kesho” Donald Nkebo akaagana na
Judy ambaye aliondoka na kwenda
kujiandaa na safari ya Israel. Baada ya Judy kutoka
wakaingia vijana wanne katika ofisi
ya Donald Nkebo
“Vijana wangu,kama
nilivyowadokeza awali ni kwamba
kazi ya sasa hivi ni ngumu na
inahitaji umakini mkubwa,lakini ni
kazi yenye maslahi mazuri
mno.Kwa taarifa yenu ni kwamba
hii ni kazi ya mheshimiwa
Rais.Nadhani yote mnafahamu
kuwa siku si nyingi sana ule
mchaka mchaka wa kuwania nafasi
ya kugombea urais wa Tanzania
katika ngazi ya vyama vya siasa
utaanza.Lakini kabla mchakato
rasmi haujaanza tayari kuna watu
wamekwisha anza kutengeneza njia za chini kwa chini kutafuta
kuteuliwa.Kuna watu tayari wana
nia ya kugombea urais na tayari
wameshaanza kutafuta uungwaji
mkono katika vyama.Mheshimiwa
rais ameliona hilo na
limemuogopesha sana hasa
ukichukulia,siku za karibuni
umaarufu wake kisiasa umekuwa
ukiporomoka siku hadi siku.Kwa
kuwa bado anahitaji kupewa tena
nafasi ya kugombea kwa mara ya
pili, akanikabidhi kazi hii mimi na
wenzangu kuhakikisha anarejea
tena ikulu.Nimeamua kuwaita ninyi
ili tusaidiane katika kazi hii
ngumu,nafahamu utendaji wenu wa
kazi,na ninawaamini kwa asilimia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom