Riwaya: Siri

Riwaya: Siri

#kwa yoyote alyechoxhwa na aroxto ya riwaya ya siri aje PM then me ntamtumia whtxp yote fo free km me nlvyotumiwa much thanks tu #shunie,#baba swalehe,#Mbududa
#kaz kwenu !!!
umefungamo pm fungua bas
 
Asante dear sema umefunga pm yako
pole kwa arosto mama,kama unaweza nichek pm nikutumie mana ww mara nying ukiwa nayo huwa unalusha mzigo fulu..so nahsi unaweza kuibadili huko kuleta hapa wadau wasome..
 
Brigedia kulubule wewe endelea na ratiba yako ya kushusha uhondo Kwa mana wengi walianzisha hii story wakaikatisha,, Kama walivyokatisha (kiapo cha jasusi) tuwekee episode zifuatazo
Tukachukue mzigo hapa ikiwezekana unaweza kuendelea kuutupia hapa Mkuu
 
Brigedia kulubule wewe endelea na ratiba yako ya kushusha uhondo Kwa mana wengi walianzisha hii story wakaikatisha,, Kama walivyokatisha (kiapo cha jasusi) tuwekee episode zifuatazo
Sawa nashusha mzigo mda so mrefu
 
SIRI

Episode
Mtunzi .Patrick CK

“Pamoja na kumueleza
kwamba ninafahamu mahala
alipo Olivia lakini Agrey bado
hajaonekana
kunikubali.Hakuniamini au
kuna tatizo lingine? Hainiingii
akilini kwa mtu ambaye
mwanae ametekwa na anatokea
mtu ambaye anajitolea maisha
yake kumsaidia kumtafutamwanae lakini bado inakuwa na
ukakasi kumkubali afanye
hivyo.Hata mke wake
amemshangaa sana kwa namna
alivyokuwa anasita.Agekuwa si
baba yake mzazi Olivia
ningehisi labda anahusika
katika suala hili kwa sababu
nilitegemea angefurahi sana
kupata taarifa za kufuruhisha
kuhusu mwanae.Namshukuru
mama yake Olivia kwa
kutokuwa na mashaka yoyote
nami na kunipa ruhusa
nikamtafute mwanae.Niache
kumuwaza yule mzee nijielekeze katika jukumu
kubwa lililoko mbele yangu”
akawaza Mathewbaada ya
kuondoka nyumbani kwa
wazazi wa Olivia
“Watu ninaokwenda
kukabiliana nao si watu wa
kufanyia mchezo.Wamejiandaa
kikamilifu na wana uwezo
mkubwa sana hivyo basi
natakiwa kujiandaa kwa silaha
na zana mbali mbali za
kunisaida kuikamilisha kazi
yangu.Kwa muda mrefu
sijashiriki purukushani zozote
na sikuwa nimejiwekea akiba ya silaha.Kuna ulazima wa kuwa
na silaha za kutosha ndani
kwani sijui ni muda gani
nitajikuta katika tukio” akawaza
Mathew
Kabla ya kwenda nyumbani
kwake akaelekea eneo la
Manziki katika nyumba ambayo
ukuta wa kuizunguka ulikuwa
unaendelea
kujengwa.Akachukua simu
akafungua sehemu ya kuhifadhi
namba za simu akatafuta jina
limeandikwa Tino akapiga
“Mathew” akasema jamaa
wa upande wa pili “Kaka vipi?akauliza
Mathew
“Mathewamani ipo mdogo
wangu? Simu yako imenistua
kidogo” akasema Yule jamaa
“Samahani kwa
kukustua.Niko hapa nje ya
nyumba yako.Upo ndani?
“Acha utani
Mathew.Umefikaje bila kunipa
taarifa?akauliza Tino
“Nimelazimika kuja
kimyakimya.Naomba tuonane
tafadhali nina shida
Tino”akasema Mathewna
mlango ukafunguliwa akatoka jamaa mmoja aliyevaa kaptura
na fulana iliyokatwa
mikono.Alikuwa ni kipande cha
mtu aliyejazia vyema.Mikono
yake ilichorwa michoro mbali
mbali.Mathewakawasha taa za
gari na yule jamaa akamfuata
wakasalimiana
“Sipendezwi na ujio kama
huu Mathew.Namba zangu
unazo kwa nini hukunijulisha
kama unakuja?akauliza Tino
“I’m sorry brother,it won’t
happen again” akasema
Mathew.Tino akamuangalia
kwa makini halafu akasema “Karibu ndani”
Wakaelekea sebuleni
“Tatizo gani limekuleta
usiku huu Mathew?akauliza
Tino
“Tino ninahitaji silaha.Kuna
kazi ya dharura imejitokeza”
akasema Mathew
“Hauweki akiba ya silaha
siku hizi?
“Hapana sina akiba zaidiya
bastora chache na vifaa vingine
vidogo vidogo”
“Mathewninataka kuachana
na biashara hii kwani hivi
majuzi imetaka kuniletea matatizo makubwa.Kuna watu
niliwapa silaha wakaenda
kufanya kazi na kwa bahati
mbaya mmoja wao akauawa na
silaha ile ikapatikana.Kama
nisingekuwa na mtandao
mkubwa hivi sasa ningekuwa
ndani.Ninafikiria kuachana na
biashara hii ya ukodishaji na
uuzaji wa silaha.Itaniletea
matatizo siku moja.Nitakuja
kwako nikuone tuzungumze
unielekeze biashara nyingine
ninayoweza kufanya ikanipatia
fedha badala ya hii” akasema
Tino “Usihofu Tino kama
unataka kubadili biashara mimi
niko tayari na nitakusaidia
kimawazo na hata kifedha kama
itahitajika.Tutazungumza hayo
siku nyingine lakini kwa usiku
wa leo nina haraka
kidogo”akasema Mathew
“Tatizo gani limetokea
Mathew? Akauliza Tino
“Umesikia kuhusu tukio
lililotokea leo la kutekwa kwa
yule daktari?akauliza Mathew
“Ndiyo nimesikia kuna
daktari ametekwa kwa namna
yake” akasema Tino “Anaitwa Dr Olivia ni mtu
wangu wa karibu sana.Nilipata
taarifa hizo nikiwa Arusha
ikanilazimu kuondoka
mkutanoni kuja Dar es salaam
kumtafuta.Tino najua wewe ni
mtu mwenye kupata taarifa
nyingi za mambo mengi
yanayoendelea hapa jijini.Una
tetesi zozote za watu
waliofanya kitendo
kile?akauliza Mathewna Tino
akatikisa kichwa
“Hapana sina taarifa zozote
za kuhusiana na tukio hili.Kwa
namna lilivyotokea lazima limefanywa na watu wataalamu
sana.Waliofanya tukio lile
lazima watakuwa ni watu
wenye taaluma kama
yako.Nilipigiwa simu na
kamanda wa polisi Dar es
salaam naye aliniuliza kama
nina tetesi zozote kuhusiana na
tukio lile.Hata polisi wenyewe
linawaumiza vichwa sana
namna tukio lile
lilivyoratibiwa.Kuna taarifa gani
mpaka sasa?
Ameshapatikana?akauliza Tino
“Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote na bado Olivia hajapatikana” akasema
Mathewna Tino akamtaka
amfuate wakaenda katika
chumba kimoja kilichojificha
ambacho ili kuingia ililazimu
kupita katika mtambo maalum
ambao ulimtambua Tino ndipo
milango ilipofunguka.
“Sijawahi kumuingiza mtu
katika chumba hiki kwani
nimehifadhi mzigo mzito ambao
huuza nje kwa vikundi vya
waasi nk.Silaha ipi unadhani
inaweza kukufaa?akauliza Tino.
“Wow ! akasema
Mathewkwa mshangao baada ya kuingia katika chumba kile
kilichosheheni silaha mbali
mbali.
“Nitachukua hii Uzi sub
machine gun kwa sababu ya
wepesi wake.Ziko ngapi hizi?
Akauliza Mathew
“Hizi ziko nne”
“Basi nitachukua mbili”
akasema Mathewna kuikagua
bunduki ile na kuiweka
pembeni.
“Desert eagle Mark XIX
pistol.Hii bastora ni hatari
sana,hizi nitachukua tatu” akasema Mathewna kuziweka
pembeni.
“AS50 Snipe
rifle.Nitachukua na hii pia”
Mathewakakusanya silaha
na vifaa ambavyo aliona
vingemfaa kwa kazi yake
akaelewana na Tino kuhusu
malipo kisha wakapakia silaha
zile katika gari akaondoka
“Tino anawezaje kuingiza
nchini silaha nzito kama
hizi?Chumba kile kimejaa silaha
nzito nzito.Ninaungana naye
katika mpango wake wa
kuachana na biashara hii ya kuuza silaha.Si biashara nzuri
kwani silaha anazouza
zinakwenda kuua watu wasio
na hatia.Hata hivyo
ninamshukuru kwa kunipatia
silaha hizi nzito ambazo
zitanisaidia mno.Watu
ninaokwenda kukabiliana nao
wamejiandaa kwa silaha nzito
na mimi siwezi kwenda nikiwa
na silaha nyepesi lazima niende
nikiwa nimekamilika” akawaza
Mathewbaada ya kuondoka kwa
Tino
Aliwasili nyumbani kwake
akashusha mizigo yake ya silaha na kwenda kuzihifadhi katika
chumba chake maalum cha
kuhifadhia zana na silaha.
“Sehemu moja ya
maandalizi imekamilika
kinachofuata sasa ni sehemu ya
pili nayo ni kuifahamu vyema
sehemu yenyewe alipo
Olivia.Hatua hii lazima
niwasiliane na Ruby ambaye
atanisaidia kupafahamu mahala
hapo” akawaza Mathewna
kuchukua simu akampigia Ruby
aliyeko nchini Uingereza.Simu
ikapokelewa
“Mathew” akasema Ruby “Ruby habari yako? Siku ya
nne leo hatujawasiliana.Vipi
maendeleo yako?akauliza
Mathew
“Ninaendelea vyema lakini
nimetoka kidogo nje ya London
nimekuja kuwapa pole familia
ya mmoja wa marafiki zangu
aliyefariki kwa ajali ya gari.Vipi
wewe unaendeleaje?akauliza
Ruby
“Mimi ninaendelea
vizuri.Ruby japokuwa uko
mwenye majonzi ya
kuondokewa na rafiki yako
lakini nina tatizo ninahitaji msaada wako” akasema
Mathew
“Umeingia kwenye tatizo
gani safari hii Mathew?Ruby
akauliza
“Unakumbuka ile program
uliyonipa ya kupata taarifa
kama mmoja wa watu wangu
yuko katika hatari?
“Ndiyo ninaikumbuka
Mathew.Kuna mtu yuko kwenye
hatari?akauliza Ruby
“Ninaye mtu wangu wa
karibu sana ni daktari anaitwa
OIivia aliwahi kunidokeza
kwamba yuko katika hatari nikampa namba apige pindi
akiwa katika hatari.Leo nikiwa
Arusha nikapokea ujumbe
kutoka katika namba zile na
baada ya kufuatilia nikapata
taarifa kwamba ametekwa na
watu wasiojulikana ikanilazimu
kuondoka haraka kurejea Dar
es salaam.Program
inanionyesha kwamba ujumbe
ule ulitumwa kutokea eneo
Fulani Kigamboni.Ninajiandaa
kuelekea huko ninataka
unisaidie kulifahamu vyema
eneo hilo kabla sijaenda huko
usiku huu” akasema Mathew “Sijatembea na kompyuta
yangu leo ndiyo maana
sijaupata ujumbe huo kwani
kwa namna nilivyotengeneza
program ile ni kwamba namba
utakayompa mtu ikipigwa
wewe utapata ujumbe na mimi
pia nitapata ujumbe.Kwa ufupi
tu ni kwamba namba zile ni
kirusi ambacho kitafanya kazi
ya kuiba taarifa na kuzituma
kwangu.Ninaamini katika
kompyuta yangu kutakuwa na
taarifa za kutosha kuhusiana na
mahala hapo alipo huyo rafiki
yako Olivia.Kwa kuwa niko mbali na nyumbani ngoja
nijaribu kutafuta kompyuta
yoyote hapa karibu ili nione
namna ya kufanya” akasema
Ruby na baada ya dakika sita
akapiga
“Mathewtayari nimepata
kompyuta nitakuomba uwe
karibu na kompyuta yako kuna
vitu ninataka kuvifahamu
kutoka katika ujumbe
uliotumiwa” akasema Ruby na
kuendelea kuwasiliana na
Mathew.Baada ya kupata taarifa
alizozihitaji Ruby akaomba
apewe muda kidogo azifanyie kazi.Wakati Ruby akiendelea
kuzifanyia kazi taarifa zile
Mathewaliendelea
kujiandaa.Zilipita dakika kumi
na tatu Ruby akapiga simu
“Mathewnimeshindwa
kuona chochote mahala hapo
it’s too dark.Satelaiti niliyoipata
haina uwezo mkubwa sana.Kwa
nini usisubiri hadi kesho
niangalie namna ya kupata
satelaiti nzuri ninayoweza
kuitumia kupachunguza vyema
mahala hapo?akauliza Ruby
“Ruby ahsante sana kwa
kujaribu lakini siwezi kusubiri hadi kesh😵livia yuko katika
hatari kubwa natakiwa
kuhakikisha usiku huu wa leo
anapatikana” akasema Mathew
“Mathewsikushauri uende
mahala hapo usiku huu bila
kujua namna palivyo.Ingekuwa
vyema uende ukiwa tayari
umepata picha nzuri”
“Usiogope Ruby.Lazima
niende huko kumtafuta
Olivia.Nitawasiliana nawe
kesho au baadae nitakaporudi”
akasema Mathew
“Mathewsikushauri uende
lakini kwa kuwa umedhamiria kwenda siwezi kukuzuia ila
kuwa makini sana.Kama
kutakuwa na tatizo lolote
nijulishe tafadhali.Unakwenda
na nani? Akauliza Ruby
“Sintakuwa peke yangu
nitakuwa na mbwa wangu
Bravo” akasema Mathewna
Ruby akapatwa na mshangao
“A dog?akauliza
“Yes.He’s a highly trained
military dog.Ana mafunzo
makubwa sana na anaweza
kufanya mambo makubwa
ambayo hata mwanadamu hawezi” akasema Mathewna
Ruby akabaki kimya
“Ruby ahsante
sana,nitawasiliana nawe
baadae”
“Mathewkuna kitu kingine
nimekigundua”
“Nini Ruby?
“Namba hizi zilipigwa
katika simu iliyounganishwa na
mfumo Fulani wa
mawasiliano.Kwa sababu
namba zile ni kirusi ninaamini
taarifa zitakuwa zimetumwa
katika kompyuta
yangu.Ninaondoka sasa hivi kurejea nyumbani kwangu
nikafuatilie kilichotumwa
katika kompyuta yangu”
“Sawa Ruby tutawasiliana
baadae” akasema Mathewna
kukata simu
“Siwezi kulala ndani wakati
Olivia hajulikani mahala
alipo.Lazima nifanye kila
niwezalo kuhakikisha ninafika
mahala alipo” akawaza
Mathewna kutoka akaenda
katika nyumba iliyokuwa
pembeni kidogo akafungua
mlango na kuingia ndani
akamtoa mbwa wake mkubwa. “Bravo tutakuwa pamoja
usiku wa leo” akasema
Mathewhuku akimkuna kuna
Bravo shingoni.Akatoka naye na
kwenda naye hadi chumbani
kwake akamfunga mkanda
shingoni.Mkanda ule ulikuwa na
kifaa maalum kabisa
kumuwezesha
Mathewkumuona gizani.
“Olivia alifanya jambo zuri
kuweka baadhi ya nguo zake
huku kwa ajili ya kubadilisha
siku akiamua kulala huku
kwangu” akawaza Mathewna
kufungua kabati la nguo akatoa nguo chache za Olivia
akaziweka katika begi dogo
halafu akaingia katika chumba
cha silaha akazibeba na
kuzipeleka garini
“Bravo it’s time.Let’s go to
find Olivia” akasema Mathewna
kumpakia Bravo ndani ya gari
wakaondoka
****************
Magari matatu yaliwasili
katika nyumba alimokuwa
amehifadhiwa Olivia ambayo ni
moja ya nyumba ambayo hutumiwa na idara ya siri ya
usalama wa taifa(SNSA)Watu
wapatao kumi na nne
wakashuka kutoka ndani ya
magari yale wote wakiwa na
bunduki nzito na mavazi
meusi.Kaiza ambaye ni
mkurugenzi msaidizi wa idara
hii akawapokea na kwenda nao
sebuleni
“Ahsanteni sana P3 Unit
kwa kufika kwa
haraka.Tumepokea taarifa
usiku huu kwamba kuna hatari
ya usalama mahala hapa hivyo
tunataka kuhakikisha panakuwa salama ndiyo maana
mkaitwa haraka.Jukumu lenu ni
kuhakikisha kwamba mahala
hapa panakuwa salama na
yeyote atakayethubutu kutaka
kujaribu kuingia mahala hapa
hakikisheni mnamtia mikononi
haraka sana.Mtaendelea
kupokea maelekezo mengine
kadiri muda unavyokwenda
lakini kwa sasa maelekezo
yaliyopo ni hayo” akasema
Kaiza
“Narudia tena kusisitiza
kwamba hakikisheni hakuna
mtu au watu watakaoingia humu ndani na yeyote
atakayethubutu mtieni
mikononi haraka sana.Hakuna
kuua bali hakikisheni mnamtia
mikononi”akasema Kaiza na
kikundi kile cha walinzi
wakatoka kwenda kuanza
majukumu yao ya kulinda
nyumba ile.Taa za nje za
nyumba ile zote zikazimwa
kukawa giza ili waweze kupata
nafasi nzuri ya
kujiicha.Kutokana na mavazi
meuzi waliyoyavaa haikuwa
rahisi kuonekana katika
giza.Wakati nyumba ile ikiwa imezungukwa na P3 unit ndani
ya nyumba vifaa vyote
vilivyokuwamo viliendelea
kupakiwa katika gari.Kompyuta
zote na mitambo yote
iliyokuwamo viliondolewa
ndani ya muda mfupi na
kupakiwa garini.Kaiza ambaye
ndiye aliyesimamia zoezi lile
alihakikisha kila kitu
kimekwenda kama ilivyotakiwa
akawataka vijana wote waingie
katika magari na kuondoka
“Jamani sisi
tunaondoka.The house is all
yours now” Kaiza akamwambia mkuu wa kikosi kile wakati
wakitoka
“Nini kimetokea hadi
mambo yakabadilika ghafla
namna hii?Kuna mtu tayari
amekwisha gundua
kinachoendelea hapa? Mpaka
rais atoe taarifa ile ya haraka
lazima kuna tatizo
kubwa.Naamini Devotha
atanieleza kila kitu” akawaza
Kaiza baada ya kuondoka kitalu
7.

***************** Devotha Adolph aliwasili
ikulu kama alivyotakiwa na
rais.Alimkuta Dr Evans akiwa ni
mwenye mawazo mengi.
“Karibu sana Devotha.Kabla
ya yote nataka kwanza nipate
taarifa kila kitu kimekwenda
kama nilivyoelekeza? Akauliza
Dr Evans
“Ndiyo mheshimiwa rais
kila kitu kimekwenda kama
ulivyoelekeza.Olivia
tumemuhamisha kutoka kitalu
7 na kumpeleka kitalu 2.Muda
mfupi uliopita nimewasiliana na
Kaiza akaniambia kwamba kazi ya kuondoa vifaa kitalu 7
imekamilika na kila kitu
kimeondolewa.P3 Unit tayari
wamekwisha fika pale na ulinzi
umeimarishwa” akasema
Devotha na Dr Evans akashusha
pumzi na kusema.
“Ahsante sana kwa
kutekeleza maelekezo kwa
haraka” akasema Dr Evans
“Kuna kitu gani kimetokea
mheshimiwa rais? Kila mtu
amebaki katika mshangao kwa
maagizo yako ya ghafla”
akasema Devotha.Dr Evans
akamfungulia faili la MathewMulumbi katika
kompyuta yake na kumtaka
asome.
“MathewMulumbi..who is
he?akauliza Devotha
akionyesha wasiwasi kidogo
“Read” akasema Dr Evans.
Wakati Devotha akiendelea
kusoma faili lile la
Mathew,DrEvans akatoka nje ya
kile chumba na kumpigia simu
Dr Mbeula
“Mheshimiwa rais”
akasema Dr Mbeula “Dr Mbeula nataka kujua
zoezi linakwendaje?akauliza Dr
Evans
“Tunaendelea na zoezi la
vipimo.Tutakapokamilisha
nitakujulisha”
“Coletha yuko wapi kwa
sasa?
“Anapumzika katika
mojawapo ya chumba cha watu
maalum.Usihofu mheshimiwa
rais tunamuangalia vyema”
“Ahsante sana Dr
Mbeula.Naomba pindi
mtakapokamilisha uchunguzi wenu unijulishe tafadhali”
akasema Dr Evans
“Nitakujulisha mheshimiwa
rais”akasema Dr Mbeula
wakaagana.Dr Evans akampigia
simu mkuu wa jeshi la polisi
“IGP nataka kujua zoezi la
kumtafuta Olivia limefikia
wapi?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais zoezi
linaendelea.Vijana wangu wako
kazini hakuna kulala”akasema
mkuu wa jeshi la polisi
“Kuna hatua yoyote
imepigwa hadi sasa? Kuna
viashiria vyovyote vya matumaini ya kumpata Olivia?

“Mheshimiwa rais mpaka
sasa bado hakuna viashiria
vyovyote kutuonyesha mahala
alipo Olivia lakini kwa mwendo
tunaokwenda nao nina uhakika
si muda mrefu sana tutafika
mahala pazuri.Watu hawa
waliofanya mchezo ule nao pia
ni wataalamu wazuri na
walifahamu kwamba nguvu
kubwa itatumika kumtafuta
Olivia na wakajiandaa
kikamilifu lakini mheshimiwa
rais tutahakikisha hadi kufikia kesho tunakuwa tayari na
mwangaza mkubwa wa suala
hili”akasema mkuu wa jeshi la
polisi
“Nafahamu juhudi zenu
ninaomba muongeze nguvu
zaidi ili Olivia aweze
kupatikana.Nina imani kubwa
sana na jeshi la polisi hata
wananchi pia wana imani
kubwa mno na jeshi lao na sote
tunaamini kwamba
mtafanikiwa kumpata Olivia
akiwa salama.Endelea
kuwasiliana nami kunijulisha
kila hatua mtakayokuwa mnapiga” akasema Dr Evans na
kuagana na mkuu wa jeshi la
polisi akarejea ndani
alikomuacha Devotha akipitia
faili la MathewMulumbi
“Umemaliza?akamuuliza
“Nimemaliza kulisoma.Faili
linaonyesha amewahi kufanya
kazi katika idaraya ujasusi
Tanzania na ni mmoja wa
majasusi mahiri kabisa
aliyewahi kutokea nchini.Kwa
nini umenipa nisome taarifa
hizi?akauliza Devotha
“Mapema usiku huu
nimepokea simu kutoka kwa Agrey Themba baba yake Olivia
akinifahamisha kwamba
amepata mgeni usiku huu
nyumbani kwake ambaye
amejitambulisha kama
MathewMulumbi.Amedai
kwamba yeye ni rafiki wa
karibu wa Olivia na alikwenda
pale ili kuwaomba wamruhusu
aweze kusaidia katika zoezi la
kumtafuta Olivia kwani
anafahamu mahala alipo”
Sura ya Devotha
ikaonyesha mstuko
“Anajua mahala alipo
Olivia?Amejuaje?akauliza “Yeye ndiye aliyempa Olivia
zile namba ambazo
aliwadanganya kwamba ni za
Sayid Omar na ambazo zilifunga
mifumo yetu”
Devotha na Dr Evans
wakabaki wanatazamana
“is that true?akauliza
Devotha
“Yes it is true.Mathewndiye
aliyempa Olivia zile namba
maalum kwa lengo la
kumjulisha pale atakapokuwa
ameingia katika hatari hivyo
basi mara tu baada ya kupiga
namba zile Mathewalitambua mara moja kwamba Olivia yuko
katika hatari na akalazimika
kuondoka Arusha kurejea Dar
es salaam haraka sana
kumtafuta.Kibaya zaidi tayari
anayo ramani inayoonyesha
mahala alipo Olivia ambako ni
kitalu 7 Kigamboni” akasema Dr
Evans
“This man.Where is he
now?akauliza Devotha
“Kwa sasa sifahamu yuko
wapi lakini alipotoka nyumbani
kwa Agrey alikuwa anajipanga
kwenda kitalu 7 Kigamboni
kumkomboa Olivia” “Nimestuka sana
mheshimiwa rais.Unadhani
huyu jamaa tayari anafahamu
kuhusu sisi?
“Kwa maelezo aliyonipa
Agrey inaonekana bado
hafahamu chochote kuhusu
nani waliomteka Olivia na
anajiandaa kuanza kufanya
uchunguzi.Kama angekuwa
anafahamu kwamba ni sisi ndio
tuliomteka Olivia angekwisha
mueleza Agrey” akasema Dr
Evans na ukimya ukapita
“Mathewamedhamiria
kumtafuta Olivia na tayari anao mwongozo ukimuelekeza
mahala alipo Olivia na ndiyo
maana nikachukua hatua ile ya
kumuhamisha kwanza Olivia
kutoka mahala pale na
kumpeleka sehemu nyingine
pili kuweka kikosi maalum kwa
ajili ya kumsubiri
Mathewambaye naamini lazima
atakwenda hapo kumfuata
Olivia.Hajui kama tayari
tumekwishapata taarifa zake
hivyo atakwenda akijiamini
kwamba hakuna
anayemfahamu na hiyo ni nzuri
kwetu kwani tutamchukua kwa kumstukiza.Sitaki auawe bali
nataka achukuliwe akiwa
mzima ahojiwe na kufahamu
watu wengine wanaoshirikiana
nao.Kumbuka Olivia ana
mawasiliano na watu wa IS
hivyo ninahisi hata huyu
Mathewanaweza akawa ni
mmoja wao.Taratibu ninaanza
kupata picha kwamba IS tayari
wameanza kujenga mtandao
wao hapa nchini na watu hawa
wawili Olivia na
MathewMulumbi wote ni
washirika wao.Juhudi za
kuufungua mfumo wetu zimefikia wapi? Akauliza Dr
Evans
“Mpaka sasa wataalamu
wanaendelea lakini bado
hawajafanikiwa.Nilimuuliza
Olivia akasema kwamba
amekupa wewe namba za
kufungulia mfumo ule.Nilitaka
kukuuliza kama kweli amekupa
lakini kwa hali uliyotoka nayo
niliogopa kukuuliza” akasema
Devotha
“Alikwambia hivyo?
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Nilimtaka atupe namba za
kufungua kompyuta zetu akadai kwamba amekwisha kueleza
kila kitu tukuulize wewe”
akasema Devotha
“Yule binti ana matatizo ya
akili”akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais najua
ukaribu ulio nao na familia ya
Olivia lakini kwa namna
nilivyomchunguza anaonekana
tayari amejiunga na IS.Kitendo
cha kwenda Congo kukutana na
Seif Almuhsin na kukuta
mawasiliano kati yake na Sayid
Omar vinatuonyesha wazi
kwamba kuna kitu kikubwa
kinaendelea kati yao.Tunachohitaji kujua ni
mipango yao kama kuna kitu
wanapanga kukifanya hapa
nchini na vile vile kuwafahamu
watu wengine ambao wako
katika mtandao wa IS hapa
nchini”akasema Devotha
“Devotha nitakueleza jambo
lakini naomba libaki kati yetu
asifahamu mtu mwingine
yeyote”
“Sawa mheshimiwa rais”
“Nilipozungumza na Olivia
alikiri kwa kinywa chake
kwamba alikwenda Kinshasa
kukutana na Seif almuhsin” “Alikueleza ni kwa nini
alikwenda kuonana na Seif?
Akauliza Devotha
“Alisema atanieleza sababu
ya kwenda kukutana na Seif
lakini kabla ya kunieleza kuna
kitu alitaka nikifanye”
“Alitaka ufanye nini
mheshimiwa rais?
“Nadhani unamkumbuka
Edger Kaka”
“Ndiyo ninamkumbuka si
yule mbunge aliyefariki katika
ajali ya gari”
“Ndiy😵livia anadai
kwamba Edger hajafariki dunia” “Hajafariki dunia?! Devotha
akashangaa
“Anadai hivyo.Hata mimi
amenishangaza sana kwani ni
yeye ambaye aliutambua mwili
wake hospitali.Olivia anadai
kwamba Edger hakufariki dunia
katika ile ajali na kwamba
serikali tulifanya mchezo ili
ionekane kwamba amekufa
katika ajali ya gari.Amekwenda
mbali zaidi na kunitaka
nimrejeshe Edger.Ili
kunishinikiza nimrejeshe Edger,
Olivia adai kwamba
ametengeneza virusi ambavyo vinaua na mwanangu Coletha
amechomwa sindano yenye
virusi hivyo na kama
sintamejesha Edger Kaka ndani
ya siku kumi basi mwanangu
atakufa lakini nikimrejesha
atamtibu mwanangu”
“Are you serious mr
President?akauliza Devotha
“Hicho ndicho alichonieleza
Olivia na ndiyo sababu ya
kutoka pale kama kichaa kwani
kichwa changu kilivurugika
kabisa”
“Yule mwanamke ana
matatizo ya akili mheshimiwa rais si bure.Hakupaswa
kutamka maneno kama
hayo.Wewe utamrejesha vipi
Edger? Akauliza Devotha
“Mwanzoni hata mimi
niliamini hivyo kwamba ana
matatizo ya akili lakini baada ya
kutafakari kwa kina nikaona
nisimpuuze Olivia.Aliponieleza
mambo haya alionekana
kumaanisha kile anachokisema”
“Do you believe
her?akauliza Devotha
“Nimempeleka Coletha
hospitali usiku huu na
madaktari wanaendelea kumfanyia vipimo ili kujua
kama kweli ana virusi hivyo
kama Olivia
alivyosema.Nimewasiliana na
daktari muda mfupi uliopita
bado wanaendelea na
uchunguzi na
watakapokamilisha
atanijulisha”
“Mheshimiwa rais hebu
tujiulize ni miaka mitatu sasa
toka alipofariki Edger,Kwanza
kwa nini Olivia aibuke sasa na
kudai kwamba Edger hajafa na
kwamba ni serikali ndio
waliofanya mchezo ule ili ionekane Edger
amefariki?Mheshimiwa rais
tukubali Olivia ana matatizo ya
akili”
“No she is not sick.Olivia ni
mzima kabisa.Baada ya
kutafakari sana nimegundua
kwamba kuna mchezo mbaya
unataka kuchezwa hapa na
ninaamini mpango huu
utakuwa na ufadhili kutoka nje
ya nchi kutaka kuvuruga amani
yetu.Wanataka kuzusha kashfa
kwamba Edger hajafa na
kwamba serikali ilighushi kifo
chake na tunamshikilia Edger sehemu Fulani na hapa
wananilenga moja kwa moja
mimi.Devotha hii ni kashfa
kubwa sana wanataka
kuianzisha ambayo
wakiipandikiza kwa wananchi
watawaamini haraka sana na
vurugu kubwa itazuka
nchini.Edger alikuwa na watu
wengi sana waliokuwa
wanamuunga mkono na kama
wakiaminishwa yuko hai
machafuko yataibuka.Olivia
anatumika tu kama chambo
lakini kuna watu wakubwa wako nyuma yake” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais unadhani
IS watakuwa wanahusika katika
mpango huu? Devotha akauliza
“Ni wazi lazima IS
wanahusika sana katika
mpango huu.Kwa miaka ya
karibuni IS wamekuwa
wakitafuta kujitanua hasa katia
nchi za afrika.Tumewasikia
tayari wana kambio zao katika
nchi majirani zetu lakini hapa
Tanzania hawajafanikiwa
kuweka mizizi yao na sasa
wanatafuta namna ya kuingia nchini ndiyo maana wanataka
kuleta machafuko ili wapate
nafasi ya kupenda na
kuingia.Olivia kwa nini
amekubali kutumika kiasi hiki
kuibomoa nchi
yake?Ameshindwa kupima
athari za kinachoweza kutokea
endapo uongo huu utafika kwa
wananchi? Olivia amekulia
katika mikono yetu
sikutegemea kama siku moja
angeweza kugeuka na kuwa
msaliti kwa taifa lake” akasema
Dr Evans “IS wana fedha nyingi na
wanazitumia katika
kutengeneza mtandao wao hapa
nchini.Wanawapa utajiri
mkubwa wale watu ambao
wanataka kuwatumia.Tazama
Olivia ni tajiri sana amejenga
kituo kile cha utafiti ambacho
kimegharimu mabilioni ya
fedha ambacho naamini
atakuwa amepewa fedha nyingi
na IS. Tazama pia Mathewni
bilionea.Ninaamini wote hawa
wawili utajiri wao umetoka kwa
IS ili kuwasaidia katika mipango yao hapa Tanzania” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais maelezo
yako yananipa picha kwamba
mapambano haya yaliyoanza ni
kati yetu na IS.Hayatakuwa
mapambano rahisi kwani IS ni
kikundi chenye nguvu kubwa
kwa sasa na kinaendelea
kujitanua sehemumbali mbali
duniani.”akasema Devotha
“Exactly,hii ni vita kati yetu
na IS.Olivia na Mathewni watu
wadogo naamini kuna watu
wakubwa nyuma yao.Huu ni
mtandao mkubwa wapo waliomo ndani ya nchi na wapo
waliopo nje ya nchi.Kazi yetu
kwa sasa ni kujipanga ili
kuufahamu mtandao huo
unawahusisha akina nani
tukianza na hawa waliomo hapa
nchini.Kwa kuwa tayari tunaye
Olivia na tunatarajia kumpata
Mathewusiku huu hawa wawili
watatusaidia sana katika
kuufahamu kwa kina mtandao
huu mkubwa” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais
tumeyafahamu haya yote baada
ya kumteka Olivia kama tusingefanya hivyo haya yote
yasingejulikana.Najiuliza nini
hasa ilikuwa mipango
yao?Walipanga wafanye nini
kuanzisha suala ili la
Edger?akauliza Devotha
“Nadhani walipanga
wamtumie Coletha kwani tayari
walikwisha mchoma sindano
yenye virusi kabla hata Olivia
hajatekwa.Nina uhakika
mkubwa kabisa kwamba Olivia
ndiye aliyeratibu mipango yote
hii.Hata kama tusingemteka
Olivia lazima wangetafuta
namna ya kunifikishia ujumbe kwamba mwanangu atakufa
hivyo nitekeleze kile
wanachokihitaji.Inaniumiza
sana kwa Olivia kufanya jambo
kama hili.Yeye na Coletha ni
kama ndugu wamekuwa
wakiishi kwa upendo mkubwa
sana iweje leo amfanyie hivi
mwenzake?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais usiwe na
hofu yawezekana hakuna virusi
hivyo anavyodai Olivia
yawezekana ikawa ni moja ya
njia zao za kutaka
kukuogopesha tu.Tusubiri
majibu ya daktari kama yataonyesha ni kweli
amechomwa virusi hivyo”
“Devotha suala hili hakuna
anayelifahamu zaidi
yako.Ninataka idara yako
ilishughulikie kikamilifu na
kuhakikisha wahusika wote
wanatiwa nguvuni.Ni suala
nyeti sana kwa usalama wa
nchi.Kuna kila dalili kwamba IS
wanataka kuvuruga amani yetu
na katu siwezi kuruhusu hilo
likatokea ndiyo maana idara hii
ya siri ikaundwa ambayo
majukumu yake ni kuhakikisha
taifa linakuwa salama.Nataka mjipange wewe na watu wako
muhakikishe kwamba
mnawatafuta na kuwapata watu
wote ambao hawalitakii mema
taifa letu.Nataka mtandao wote
wa IS hapa nchini ujulikane.”
“Mheshimiwa rais idara
yetu ina watu wenye ujuzi na
uwezo mkubwa
ninakuhakikishia kwamba
tutafanikiwa kuwapata watu
hao.Kitu kizuri ni kwamba
tayari tunaye Olivia na
Mathewtutampata si muda
mrefu sana.watu hawa wawili
watatusaidia kuufahamu mtandao wao wote ulio hapa
nchini na nje ya nchi”akasema
Devotha.Ukapita ukimya wa
dakika mbili Dr Evans akasema
“Sifa moja ya magaidi ni
kutokutoa siri kuhusiana na
mitandao yao na mipango yao
mbalimbali ya kigaidi.Sina
hakika kama Olivia atakuwa
tayari kutoa siri za watu
anaoshirikiana nao au kutaja
mipango yao yote hivyo basi
kuna kitu ninakifikiria
kukifanya ambacho
kitamlazimisha aweze kusema
kila kitu”
 
SIRI

Mwendelezo..


“Unafikiria tufanye nini
mheshimiwa rais?akauliza
Devotha
“Tunatakiwa kumpata
Agrey Themba baba yake
Olivia”
“Mheshimiwa rais !
Devotha akashangaa
“Tumchukue tena na Agrey
Themba?Tayari tunaye mwanae
tukimchukua na yeye huoni
kama tutazidi kukoroga
mambo?
“Hiyo ndiyo njia pekee ya
kumfanya Olivia
azungumze.Bila kutishia kumuua baba yake basi Olivia
hataweza kusema chochote.Hii
ni vita na ili tupate ushindi
lazima tutumie kila mbinu
kupigana.Olivia anampenda
mno baba yake hivyo kama
tukifanikiwa kumpata na
kutishia kumuua basi atatueleza
kila kitu”
“Ni vipi kama hata baada ya
kutishia kumuua baba yake
Olivia hatakuwa tayari kusema
chochote?akauliza Devotha
“Agrey ni rafiki yangu wa
siku nyingi sana lakini hapa
tunaweka mbele maslahi ya taifa hivyo kama ikilazimika
kumkata pumzi tutafanya hivyo
kwani tayari urafiki wetu
umekwisha ingia dosari kwa
suala hili la Olivia.Katu siwezi
kuwa na huruma kwa Olivia
kwani yeye amekubali
kutumika na magaidi na sasa
familia yangu yote iko
mashakani.” akasema Dr Evans
na ukimya mfupi ukapita
“Agrey alikuwa na wasiwasi
sana na Mathewndiyo maana
akanipigia kunipa taarifa zake
na kunitaka nimsaidie kufanya
uchunguzi kama kweli Mathewamewahi kufanya kazi
katika idara ya ujasusi
Tanzania.Nitampigia simu na
kumfahamisha kwamba
Mathewni kweli amewahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi na nitamshauri tumpe
nafasi Mathewya kuchunguza
suala hili la Olivia.Baada ya saa
moja kutoka sasa mtu mmoja
kutoka idara yako atampigia
simu Agrey akijifanya ni
Mathew.Atazungumza kama
vile yuko katika sehemu ya
kujificha na atamjulisha
kwamba amefanikiwa kumpata Olivia ingawa hali yake si nzuri
sana hivyo atamuelekeza
sehemu ya kwenda.Mtu huyo
amuonye Agrey asiwasiliane na
mtu yeyote yule kumueleza
kuhusu suala lile.Ninaamini
Agrey atafuata maelekezo hayo
na atakapofika mahala
alipoelekzwa na
Mathewatachukuliwa na vijana
wetu na huo utakuwa ni
mwisho wake” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais wazo
lako ni zuri lakini ..” “Agrey Themba lazima
apatikane Devotha. Hakuna
mjadala katika suala hilo.Bila
kumpata Agrey hatutapata
chochote kutoka kwa Olivia
ambaye anashirikiana na
magaidi hivyo kama
hatutatumia nguvu kubwa
hatutaweza kupata chochote
kutoka kwake.Nataka
operesheni ya kumchukua
Agrey Themba ifanyike usiku
wa leo.Kabla ya mapambazuko
ya kesho tuwe tayari tumeanza
kupata taarifa muhimu.Umenielewa Devotha?”
akauliza Dr Evans
“Niumekuelewa
mheshimiwa rais”
“Good.Wekeni nguvu usiku
huu katika mambo haya mawili
kwanza kumpata Mathewna vile
vile kumpata Agrey
Themba.Hakikisha unanijulisha
kila kinachoendelea” akasema
Dr Evans akachukua simu na
kumpigia Agrey
“Dr Evans” akasema Agrey
Themba
“Agrey nimekupigia kukupa
mrejesho kuhusiana na kinachoendelea.Nimewasiliana
tena na mkuu wa jeshi la polisi
nchini na amenihakikishia
kwamba jeshi la polisi
wanaendelea na uchunguzi na
wamefikia hatua
nzuri.Yawezekana hadi asubuhi
ya kesho wakawa na taarifa
nzuri za kutupa.Tuendelee
kuwa wavumilivu na
kuwaamini” akasema Dr Evans
“Nashukuru sana Dr
Evans.Imani yangu kwa jeshi la
polisi ni kubwa na ninaamini
watafanikiwa kumpata mwanangu” akasema Agrey
Themba
“Agrey suala la pili
uliniomba nikusaidie kufanya
uchunguzi kuhusiana na
MathewMulumbi.Nimewasilian
a na mkurugenzi wa idara ya
ujasusi Tanzania na amenitumia
faili la
MathewMulimbi.Nimelipitia
kwa umakini ni kweli
alichokisema aliwahi kufanya
kazi katika idara ya ujasusi na
faili lake linaonyesha kwamba
ni mmoja wa majasusi wa
kiwango cha juu kabisa.Baada ya kupitia faili lake
nimejiridhisha kwamba ni mtu
anayeweza kuwa na msaada
mkubwa.Ninashauri tumuache
aendelee na uchunguzi wake
lakini ahakikishe kwamba
uchunguzi wake hauleti
mkanganyiko kati yake na jeshi
la polisi.Mpe muda na nafasi ya
kufanya uchunguzi wake kwa
uhuru ninaamini anaweza
akasaidia sana”akasema Dr
Evans
“Dr Evans ahsante sana
kwa taarifa hizo nzuri.Nitampa
nafasi kama ulivyoshauri yawezekana akawa na msaada
mkubwa”akasema Agrey
“Sawa Agrey nitaendelea
kukupa taarifa kila pale
nitakapokuwa ninazipata.”
Akasema Dr Evans na kukata
simu akamgeukia Devotha
“Tayari nimetengeneza
njia.Pale atakapopokea simu
kutoka kwa mtu atakayejifanya
ni MathewMulumbi hatakuwa
na wasiwasi wowote lazima
atafuata maelekezo
atakayopewa” Akasema Dr
Evans akaagana na Devotha. RIYADH - SAUDI ARABIA
Saa nne za usiku magari
manne yaliwasili katika makazi
ya Habiba Jawad.Kabla magari
yale hayajasimama wakaruka
watu na kulizingira gari moja na
baada ya dakika chache mlango
wa lile gari ukafunguliwa
akashuka jamaa mmoja
mwenye ndevu nyingi
aliyejifunga kilemba kichwani
.Moja kwa moja akaingia ndani
ya jumba lile kubwa akaelekea
ndani katika chumba
kilichokuwa na meza ya duara na viti zaidi ya kumi.Ndani ya
chumba kile kulikuwa na watu
wapatao saba
“Sayid karibu sana.”
akasema Habiba Jawad
“Samahani sana kwa
kuchelewa.Nilipata dharura
iliyonichelewesha.Tayari kikao
kimeanza? Akauliza Sayid
“Bado hatujaanza tulikuwa
tunakusubiri wewe.Tunaweza
kuanza sasa.Abu wakaribishe
akina Khalid” Akasema
Habiba.Mbele ya chumba kile
kulikuwa na luninga mbili
kubwa Abu dahir akabonyeza kitufe katika kifaa cha kuwashia
na luninga zile zikawaka
wakaonekana watu
wawili.Yalikuwa ni
mazungumzo ya moja kwa
moja.Habiba akarekebisa koo
na kusema
“Karibuni sana Khalid
Radwan na
Rashid.Mtatusamehe kwa
kuchelewa kuanza kwa kikao
hiki muhimu ni kutokana na
Sayid kuchelewa kufika lakini
tayari yuko hapa tunaweza
kuendelea.” “Hakuna tatizo tuendelee”
akasema Khalid Radwan mmoja
kati ya viongozi wa juu wa
kundi la IS akiwa nchini Iraq
“Ndugu zangu kikubwa
katika kikao hiki ni kujadili kwa
kina kile kilichotokea Tanzania
siku ya leo na hatima ya
mipango yetu ya kumpata
Seif.Taarifa tulizozipata ni
kwamba,Olivia Themba
ambaye amekuwa akitusaidia
katika mambo mengi hasa
katika operesheni ya kumtafuta
Seif ametekwa nyara na watu
wasiojulikana.Huyu ndiye tulimtanguliza mbele hivyo
kama ametekwa mipango yetu
itatetereka sana ndiyo maana
nimeitisha kikao hiki ili tujadili
ni namna gani mipango yetu
itakavyoendelea.Karibuni sana
kwa michango ya mawazo”
akasema Habiba Jawad
“Kwa maelezo ambayo
Habiba amenipa ni kwamba
Olivia ametekwa wakati
akitokea Kinshasa alikoenda
kuonana na Seif al
muhsin.Nataka kujua mpaka
sasa kuna taarifa zozote
mmekwisha zipata kutoka kwa watu wetu walioko Tanzania
kuhusiana na tukio hilo?
Akauliza Khalid
“Tumekuwa na
mawasiliano na watu wetu
Tanzania na kwa taarifa za
mpaka jioni hii bado Olivia
hajapatikana na hajulikani
alipo” akajibu Sayid Omar
“Mnahisi nani anahusika
katika tukio hili la kumteka
Olivia? Akauliza Khalid
“Mpaka sasa hatujui ni nani
anahusika na tukio lile lakini
kwa namna lilivyotokea ni tukio
lililofanywa kitaalamu sana” akasema Sayid Omar na
kuelekea upande mwingine
kulikokuwa na luninga nyingine
kubwa.
“Tumejaribu kukusanya
picha kadhaa kutoka eneo la
tukio.Zinazoonekana hapa ni
gari mbili moja ikiwa ya Olivia
na nyingine ikiwa ni ya walinzi
wake.Kwa mujibu wa maelezo
yaliyotolewa na mashuhuda ni
kwamba magari haya
yalipokaribia kufika nyumbani
kwa Olivia ilitokea helkopta
angani na kuanza kufanya
mashambulizi.Walinzi wote wa Olivia waliuawa na mara
yakatokea magari mawili
yaliyofika kwa kasi kubwa na
kumchukua Olivia wakaondoka
naye na mpaka sasa hajulikani
mahala alipo.Tunajaribu
kulihusisha tukio hili na yale
ambayo yamewahi kutokea
sehemu nyingine Afrika
ambapo watu matajiri au
wanafamilia wao hutekwa na
kisha watekaji hudai fedha
nyingi.Tunahisi kwamba lengo
la watekaji hao ni kujipatia
fedha”akasema Sayid
Omar.Ukimya ulitawala mle ndani ya chumba kila mmoja
akiwa ameyaelekeza macho
yake mbele katika luninga na
baada ya muda Khalid akasema
“Kwa mtazamo
wangu,waliomteka Olivia
walifahamu alikuwa nchini
Congo na walikuwa
wanamfuatilia kwa karibu kila
anachokifanya.Ninafahamu
mbinu mbali mbali za utekaji
na kwa namna tukio hili
lilivyotokea ninaamini watekaji
hawajafanya hivi kwa ajili ya
kujipatia fedha.Hili tukio ni la
kitaalamu sana na limefanywa na watu wenye taaluma kubwa”
Khalid akanyamaza kwa muda
kisha akasema
“Naomba mkubaliane nami
kuwa tukio hili limefanywa na
watu wa serikali”
Watu wote mle ndani
wakatazamana
“Ninawahakikishia ndugu
zangu,kwamba huu mchezo
umechezwa na serikali.Nina
uzoefu mkubwa na mambo
kama haya ya utekaji na
ninafahamu aina mbali mbali za
utekaji na kwa utekaji huu wa
Olivia ninashawishika kuamini kwa asilimia mia moja kwamba
serikali ya Tanzania
wanahusika” akasema Khalid
“Serikali ya Tanzania wana
sababu yoyote ya kumteka
Olivia?akauliza Habiba
“Olivia ni mtu mwenye jina
kubwa Tanzania,baba yake ni
bilionea ni rafiki mkubwa wa
rais wa Tanzania.Inasemwa
kwamba urafiki wao umeanza
toka wakiwa vijana hadi
leo.Iweje serikali wamteke mtu
kama huyu mwenye ukaribu
mkubwa na rais?akauliza Abu
dahir “Jibu la swali hilo ni
rahisi,tayari kuna kitu
wamekigundua kwa Olivia
ndiyo maana wamemteka.Olivia
hana sababu yoyote ya kutekwa
na serikali isipokuwa kwa
sababu moja tu kubwa ambayo
ni kugundulika kushirikiana
nasi.Ninawaambia ukweli
ndugu zangu kwamba hiyo
ndiyo sababu pekee
iliyompelekea Olivia
akatekwa.Nina uhakika
mkubwa wamekuwa
wakifuatilia nyendo zake kwa
muda mrefu na wakagundua kila kitu kuhusu Olivia na
mtandao wetu.Mmekuwa
makini kwa muda mrefu na kila
kitu kikaenda vyema lakini
kuna mahala mlijisahau na
kuachia mwanya mkasababisha
Olivia akajulikana” akanyamaza
na wote walikuwa kimya
wakimsikiliza
“Jambo la pili” akaendelea
“Yawezekana Olivia
alikuwa anatumiwa na serikali
kuchota siri zetu na baada ya
kupata siri za kutosha kabisa
wakaamua kucheza mchezo
ionekane kwamba Olivia ametekwa na watu
wasiojulikana lengo ni
kumuhifadhi sehemu kwa muda
ili kushughulikia kwanza taarifa
zile walizozipata” akasema
Khalid.Bado chumba kiliendelea
kuwa kimya wote wakimsikiliza
yeye
“Katika hayo mawili
niliyoyaelezea moja wapo
linaweza kuwa ni sababu ya
kupotea kwa Olivia hata hivyo
kupotea kwa Olivia si sababu ya
kuturudisha nyuma na
kuvuruga mipango
yetu.Tunawapoteza watu wetu kila uchao na wengine ni
makamanda muhimu na bado
mapambano yanaendelea hivyo
mipango yetu yote itaendelea
kama kawaida hadi tuhakikishe
Seif anapatikana lakini
kutakuwa na mabadiliko
kidogo.Nataka kujua je kile
kirusi alichotengeneza Olivia
kimekwisha tumika kama
tulivyokusudia?akauliza Khalid
“Ndiyo.Tayari Coletha
mtoto wa rais amechomwa
sindano yenye virusi”akajibu
Sayid “Baada ya kuchomwa
mmefuatilia kujua maendeleo
yake? akauliza Khalid
“Toka alipochomwa
sindano ile yenye virusi Coletha
hajaweza kuingia darasani
tayari ameanza kuumwa na
amepewa mapumziko hadi pale
hali yake itakapokuwa nzuri”
akasema Sayid Omar
“Vizuri sana kama tayari
amekwisha chomwa sindano
yenye virusi .Mpango wetu wa
awali ulikuwa ni kumpigia simu
rais kumjulisha kwamba
mwanae amechomwa sindano yenye virusi na atakufa endapo
hatatupa taarifa za Edger lakini
baada ya hili lililotokea leo
itatulazimu kubadili
mpango.Tunatakiwa kumteka
huyo mtoto wa rais na kisha
tutawasiliana na rais moja kwa
moja na tutamuonyesha
maendeleo ya mtoto wake
anavyopata taabu na hii
itamfanya atekeleze kila
tunachokitaka.Wasiliana na
watu wetu Dar es salaam
waandae mpango huo haraka
sana ikiwezekana usiku huu
huu mtoto huyo wa rais apatikane.Wapigie simu
nizungumze nao sasa hivi
niwape maelekezo” akasema
Khalid.
Kwa kutumia simu
iliyokuwa mezani Sayid Omar
akampigia Fahad mmoja wa
watu wao aliyepo Tanzania.
“Hallo Sayid” akasema
Fahad
“Fahad nini kinaendelea
hapo Dar es salaam?akauliza
Sayid
“Huku bado mambo ni vile
vile.Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote za kupatikana Olivia” “Sawa Fahad nataka
uzungumze na Khalid Radwan”
akasema Sayid
“Fahad unazungumza na
Khalid Radwan naomba
nisikilize vizuri.Kufuatia tukio
la kutekwa kwa Olivia mipango
yetu imebadilika.Nataka
mjipange usiku huu wa leo
muweze kumpata mtoto wa rais
wa Tanzania.Najua
nimewastukiza lakini
nawaombeni mfanye kila
linalowezekana usiku wa leo
aweze kuchukuliwa kutoka
hapo chuoni hata kama ni kwa kufanya shambulio lakini lazima
huyo mtoto wa rais
apatikane”akasema Khalid
“Khalid kuna tatizo kidogo
katika mpango huo” akasema
Fahad
“Kuna tatizo gani?sura ya
Khalid ikabadilika
“Nimepewa taarifa na
Karim mtu wangu ambaye
anasoma katika chuo
anachosoma Coletha,rais
amefika usiku huu pale chuoni
na kumchukua mwanae
inasemekana amempeleka
hospitali”akasema Fahad “Amempeleka
hospitali?Khalid akauliza
“Ndiyo amempeleka
hospitali kuchunguzwa afya
yake”
“Una uhakika na taarifa
hizo Fahad?
“Ndiyo.Karim ana ukaribu
mkubwa na marafiki zake
Coletha ambao wamempa
taarifa hizo.Wanadai kwamba
Coletha amepelekwa hospitali
kufanyiwa uchunguzi wa afya
yake”
“Kwa nini rais amchukue
Coletha usiku huu na kumpeleka hospitali
kumchunguza afya yake?
Akauliza Sayid
“Msiumize vichwa
vyenu,tayari rais amefahamu
mwanae amechomwa sindano
yenye virusi.Niliwaambia
kwamba Olivia yuko upande wa
serikali na ndiye aliyempa rais
siri hii na nyingine nyingi
kuhusu sisi.Baada ya rais
kupewa taarifa kwamba
mwanae amechomwa sindano
yenye virusi amemchukua
haraka na kumpeleka hospitali
na huko lazima atapona kwani Olivia ndiye aliyetengeneza
virusi hivyo na anafahamu tiba
yake”akasema Khalid chumba
kikawa kimya.Baada ya muda
Sayid akasema
“Kuna swali
ninajiuliza,Olivia ndiye
aliyetengeneza kirusi kile na
angeweza kumtibu mtoto wa
rais kimya kimya kwa nini basi
rais amempeleka mwanae
hospitali kumchunguza afya
yake? akauliza Sayid Omar
“Swali zuri Sayid lakini
hatuwezi kupata majibu yake
kwa sasa.Ukweli ni kwamba tumerudi kwenye sifuri ndugu
zangu.Mipango yetu yote ya
muda mrefu imeshindikana kwa
sababu ya kumuamini
Olivia.Tunachotakiwa kufanya
kwa sasa ni kutumia nguvu
kumshinikiza rais ili atupe
taarifa tunazozihitaji.Bila
kutumia nguvu hatutafahamu
mahala alipo Seif kwani Olivia
tayari amekwisha tusaliti”
akasema Khalid
“Khalid unashauri nini
kifanyike? akauliza sema
Habiba. “Sikilizeni ndugu zangu
mpango wetu bado unaendelea
kama kawaida na hakuna
kitakachosimama.Rashid
Mombasa unanisikia?
“Ninakusikiliza mkuu”
akasema Rashid mmoja wa
viongozi wa IS aliyeko
Mombasa Kenya ambaye toka
kikao kilipoanza amekuwa
kimya
“Kwako kuna kikosi
kikubwa kuliko
Tanzania.Nataka uandae watu
kumi usiku huu kwa ajli ya
safari ya kuelekea Tanzania ambako watakutana na timu ya
Fahad wataungana katika
kumteka mtoto wa rais wa
Tanzania.Nataka kesho kwa
namna yoyote ile mtoto wa rais
akachukuliwe hospitali na
tukishafanikisha hilo ndipo
tutakuwa na uhakika wa
mipango yetu kuendelea kama
tunavyotaka. Katika mambo
tutakayomtaka rais wa
Tanzania ayafanye ni
kutukabidhi Seif pamoja na
Olivia ambaye tutamkata
kichwa kama adhabu ya usaliti
mkubwa aliotufanyia.Rashid na Fahad mmenielewa?akauliza
Khalid
“Nimekuelewa
Khalid.Maelekezo yako
yatafanyiwa kazi haraka sana”
akasema Rashid
“Nimekuelewa Khalid na
maandalizi yanaanza usiku huu
huu” akasema Fahad kutokea
Dar es salaam
“Safi sana.Kumbukeni
hatupaswi kushindwa vita hii
na yeyote ambaye atasababisha
tushindwe hii vita adhabu yake
ni kukatwa kichwa.Tanzania ni
muhimu sana tuipate kwani tukiipata tutakuwa tumeipata
Afrika nzima hivyo kila juhudi
zifanyike kuhakikisha kwamba
mipango yetu yote nchini
Tanzania inakwenda
vizuri.Nawatakia utekelezaji
mzuri wa mipango yetu”
akasema Khalid na kuzima
kamera.Wote mle ndani
wakatazamana kwa muda kisha
Habiba akasema
“Nadhani nyote mmesikia
maelekezo
yaliyotolewa.Mikakati ianze
mara moja kuitekeleza.Lazima tuhakikishe Seif anapatikana”
akasema Habiba
“Mimi bado nina mashaka
kidogo kuhusiana na kauli ya
Khalid kwamba Olivia
anatumiwa na serikali.Wote
humu tulionana naye alipokuja
na sote ni mashahidi namna
alivyokuwa tayari kusaidia
katika kupatikana kwa Edger.Ni
kwa sababu yake Seif yuko hai
mpaka leo,alipambana dhid yal
wale walijaribu kumuua kwa
kumuwekea sumu na kuokoa
maisha yake.Tuna uhakika
kwamba Edger yuko hai leo kwa sababu yake.Bila yeye
kusingejengwa kituo kile cha
utafiti nchjini Tanzania
ambacho kitakuwa na manufaa
makubwa kwetu.Iweje leo
itolewe amri ya kumkata
kichwa na wote humu tunakaa
kimya?akauliza Sayid kwa ukali
“Sayid yuko sahihi.Sina
hakika Olivia anatumiwa na
serikali.Tumekwisha shirikiana
naye mambo mengi hadi sasa
kama angekuwa anashirikiana
na serikali tusingefika hatua hii
tuliyofika.Ninaweza
kukubaliana na ile sababu yake ya kwanza kwamba huenda
serikali ya Tanzania
wamemgundua kwamba
anashirikiana nasi na ndiyo
maana wakamteka nyara lakini
Olivia kushirikiana na serikali
ya Tanzania hilo
ninalikataa”akasema Habiba
“Jambo lingine kama Olivia
angekuwa anashirikiana na
serikali asingekubali mtoto wa
rais achomwe sindano yenye
virusi.Angemjulisha rais
mapema na angemuondoa
mtoto wake lakini inaonekana
rais amefahamu leo hii kwamba mwanae amechomwa sindano
yenye virusi na atakuwa
ameambiwa na Olivia” akasema
Abu dahir
“Kama Olivia amemweleza
rais kwamba mwanae
amechomwa sindano yenye
virusi tujiulize ni kwa nini
alimwambia?Aliamua kutumia
njia hiyo kumshinikiza rais
amueleze kuhusu
Edger?akauliza Habiba
“Hata mimi ninaanza kuhisi
hivyo lakini hatuwezi kuwa na
jibu la uhakika hadi pale Olivia
atakapopatikana hivyo basi tujitahidi kumtafuta Olivia na
kumpata ili tufahamu sababu za
kutekwa kwake.Binafsi siko
tayari kumuona Olivia
anakatwa kichwa labda hadi
nitakapothibitisha kweli
anashirikiana na serikali hivyo
basi nitahakikisha ninasimama
upande wake na kunusuru
maisha yake” akasema Sayid
Omar
“Sayid sote hapa hakuna
anayetaka au kutamani
kumuona Olivia akikatwa
kichwa.Lazima tufanye kila
linalowezekana kumuokoa na tutamuokoa pale
tutakapothibitisha kwamba
hashirikiani na serikali ya
Tanzania ” akasema Habiba
wakaendelea na mjadala wa
kina kuhusiana na suala lile
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Mathewaliendesha gari
taratibu akiifuata ramani
iliyokuwa katika kompyuta
yake aliyoiweka pembeni na
kwa mujibu wa ramani yake
alikaribia sana kufika eneo
alilokuwa anakwenda “Nimekaribia kufika eneo la
tukio ninatakiwa kuhakikisha
eneo lote linakuwa giza ili
kuniwezesha kuingia mahala
aliko Olivia bila tatizo”akawaza
Mathewakiendelea kutazama
nje
“Eneo liko kimya watu wote
wamejifungia majumbani
mwao”
Mathewakasimamisha gari
akafungua begi lake na kutoa
kitu Fulani kilichofungwa nyaya
kadhaa akashuka garini
akatazama pande zote kama
kuna mtu lakini barabara ilikuwa tupu,kwa haraka
akaenda katika nguzo ya
umeme iliyokuwa pembeni ya
barabara akakipachika kifaa
kile katika nguzo ya umeme
akakifunga na gundi halafu
akarejea haraka garini na
kuondoka eneo lile.Baada ya
umbali mfupi akachukua kifaa
mithili ya simu ya mkononi
akabonyeza namba Fulani na
mlipuko ukatokea katika ile
nguzo aliyoweka kile kifaa na
eneo lote likawa giza umeme
ulikatika. “Kazi inaanzia hapa”
akasema Mathewbaada ya
umeme kukatika
Mathewaliendelea na safari
yake akiifuata ramani ile
akafika katika barabara ambayo
ilikuwa inaelekea mahala
ambako ramani ilionyesha
ndiko aliko Olivia.Aliipita
barabara ile akaendelea mbele
zaidi akazima gari akageuka na
kumtazama mbwa wake
“Bravo it’s time” akasema
huku akimkuna mbwa wake
shingoni.Akachukua bunduki
aina ya AS50 Snipe rifle na bastora mbili akaweka kichwani
miwani ya kumuwezesha kuona
vyema kwenye giza halafu
akaweka begi lake lenye vifaa
vingine mgongoni akashuka
garini akiwa na Bravo
wakaanza kutembea hadi
walipoikuta ile barabara
inayoelekea katika nyumba
aliko Olivia.Kulikuwa na maua
kandoni mwa barabara
ile.Mathewakiwa na bunduki
yake yenye uwezo mkubwa
aliambaa ambaa kandoni mwa
barabara ile akiwa na mbwa
wake wakijinga na miti ya maua.Alikuwa katika tahadhari
kubwa.Alikaribia sana kufika
katika jumba lile akamkuna
kuna mbwa wake shingoni
akampa maelekezo
“Bravo now go !
Mathewakamuelekeza mbwa
wake ambaye alitoka mbio
kuelekea katika ile
nyumba.Mathewaliyevaa
miwani ile maalum ya kuonea
kizani akaendelea kunyata huku
akimfuatilia Bravo aliyekuwa
amemuwekea kitu Fulani katika
mkanda wake ambacho kilimuwezesha kumuona
kupitia ile miwani aliyovaa.
Bravo alikwenda kimya
kimya hadi katika geti la
nyumba ile na taratibu bila
kutoa ukelele akanusa harufu
ya mtu eneo lile akamsogelea
jamaa mmoja aliyekuwa
amejibanza kandoni mwa geti
akiwa amevaa mavazi
meusi.Kwa macho ya kawaida
haikuwa rahisi
kumtambua.Yule jamaa alistuka
baada ya kumuona mbwa
karibu yake.Akawasha tochi ili
aweze kumtazama vyema yule mbwa.MathewMulumbi kupitia
miwani yake aliweza kumuona
yule jamaa vizuri na kwa
kutumia bunduki yake
aliyoifunga kiwambo cha kuzuia
sauti akampiga risasi kati kati
ya paji la uso akaanguka
chini.Baada ya yule jamaa
kuanguka Bravo akaambaa na
ukuta akakutana na mtu wa pili
aliyekuwa amejibanza nyuma
ya mti.Mathewakamuona na
kumdondosha kwa risasi moja
ya kichwa.Kazi kubwa ya Bravo
ilikuwa ni kuwatafuta walinzi
waliojificha gizani na Mathewaliweza kuwaona
kirahisi na kuwamaliza kwa
kutumia bunduki yake kubwa
iliyofungwa kiwambo cha sauti
“Hawa walinzi mbona
hawaishi?akajiuliza baada ya
kumuona Bravo akiendelea
kuzunguka ile nyumba
akimfuata mwingine baada ya
kuhisi harufu ya mtu.Tayari
alikwisha wakata pumzi watu
nane lakini bado ilionekana
wapo zaidi.Akiendelea
kumfuatilia Bravo akawaona
watu watano wakiwa wamekaa katika matofali wakizungumza
wote wakiwa na bunduki
“Kuna ulinzi mkubwa
kuzunguka hii nyumba.Nadhani
ulinzi huu wote ni kwa ajili ya
kumlinda Olivia.Naamini OIivia
yuko ndani ya nyumba hii kama
ramani
inavyonionyesha?akawaza
Mathewna kuielekeza bunduki
yake kwa wale jamaa ambao
mmoja wao alistuka na kuruka
baada ya kuguswa na
kitu.Wenzake walianza
kumcheka mwenzao baada ya
kumulika tochi na kugundua kilichomstua mwenzao ni
mbwa.Yule jamaa tayari
alikwisha iweka sawa bunduki
yake tayari kwa shambulio.
“Hey hey hey..ni mbwa
usiogope! Yule jamaa ambaye
aliruka alipoguswa na kitu
akaambiwa na mwenzake ndipo
alipotulia na kumuona mbwa
mkubwa akiwa karibu yao
akiwaangalia
“Katokea wapi huyu
mbwa?akauliza mmoja
wao.Wakati wakiendelea
kujiuliza mmoja wao
akaanguka.Wakapatwa na mstuko na kila mmoja akashika
silaha yake vyema mara
akaanguka wa pili na
watatu.Haikujulikana sababu
yakuanguka kwao mmoja kati
ya wawili waliobaki akainama
ili kuwatazama wenzake
walioanguka ajue sababu ya
kuanguka kwao akajikuta
akipigwa risasi ya bega
akaanguka na kutoa mguno wa
maumivu.Yule mwenzake
aliyebaki akaiweka sawa
bunduki yake akaanza kuangaza
pande zote kumtafuta mtu
aliyewapiga wenzake risasi lakini hakuona mtu yeyote
akamfuata yule mwenzake
aliyepigwa risasi ya
bega.Alikuwa anavuja damu
nyingi.Haraka haraka
akachukua redio ya
mawasiliano na kutaka
kuwajulisha wenzake lakini
alipobonyeza tu
Mathewakampa tiketi ya
kuzimu kwa risasi moja iliyotua
katikati ya paji la uso.Alibaki
yule jamaa mmoja aliyepigwa
risasi ya bega ambaye alikuwa
anagugumia kwa
maumivu.Mathewakanyata kumsogelea lakini kabla
hajamfikia akatokea mtu mmoja
ambaye naye alikuwa na
bunduki mkononi.Akamulika
tochi na kuwaona wenzake
wakiwa wamelala chini
wakivuja damu hawakuwa na
uhai.Kwa kasi ya umeme
akaitupa bunduki yake na
kutoka mbio.Mathewakaachia
risasi mbili lakini alichelewa
kwani jamaa alikwisha
potea.Akanyata kumuendea
yule jamaa aliyekuwa
amepigwa risasi ya bega.Yule
jamaa aliweza kusikia hatua za mtu akimsogelea haraka haraka
akachomoa bastora iliyofungwa
kiwambo cha sauti na kujipiga
risasi ya kichwa akafa pale pale.
“Oh no !! Huyu alikuwa
muhimu sana kwani angeweza
kunipa taarifa zote kuhusiana
na watu hawa” akawaza
Mathewmara Bravo akatokea.
“Thank you Bravo !
akasema Mathewkwa sauti
ndogo.
“Bravo amerejea nadhani
hakuna huku nje
wamekwisha.Nimewaondoa
watu kumi na tatu.Ni wengi sana.Walikuwa wamejizatiti
mno kiulinzi kama ningekuja
kichwa kichwa nisingetoka
salama eneo hili.Ulinzi huu
unanipa uhakika kuwa lazima
Olivia yuko ndani ya nyumba
hii.Lakini watu hawa ni wenye
bunduki nzito kama hizi ni
akina nani? Akajiuliza na
kutazama pande zote lakini
hakuona mtu akaanza
kutembea kwa tahadhari
kurejea getini.Mlango wa
pembeni ya geti haukuwa
umefungwa akausukuma
ukafunguka. “Sasa ni zamu ya
ndani.Kama nje kulikuwa na
watu wengi kiasi hiki huku
ndani wanaweza kuwa zaidi ya
wale.Lakini hata wakiwa
wangapi nitapambana nao.Ni
heri nife wakati nikipambana
kumuokoa Olivia kuliko kukata
tamaa.Sijawahi kukata tamaa
katika maisha yangu” akawaza
Mathewna kujibanda katik
aukuta wa geti akaangaza kila
upande lakini hakumuona mtu
yeyote.
“Ndani kuko kimya kabisa
kunaonekana hakuna mtu yeyote” akawaza halafu akampa
Bravo maelekezo afanya kama
alivyofanya kule nje.Bravo
akatoka mbio huku
Mathewakiendelea kumfuatilia
nyuma kwa
tahadhari.Waliizunguka
nyumba ile na hakukuwa na
mtu yeyote.Mathewakarejea
katika mlango mkubwa wa
kuingilia ndani ya
nyumba,akakiminya kitasa
ulikuwa umefungwa.Akatoa
vitu Fulani katika begi lake na
kuchokonoa kitasa mlango
ukafunguka.Mathewakatoa nguo za Olivia katika begi lake
na kumuwekea Bravo puani
“Go find Olivia ! akasema
Mathewna kumruhusu Bravo
aingie ndani ya nyumba ile
Mathewakimfuata kwa
kunyata.Ndani Kulikuwa giza na
hakukuwa na dalili zozote za
mtu.Mathewaliendelea
kumfuata Bravo aliyemuongoza
kuelekea katika chumba Fulani
ambacho mlango wake ulikuwa
wazi.Bravo akaanza kunusa
chini kisha akakwaruza sakafu
“Olivia was here” akawaza
Mathew “She was here.Where is she
now?akajiuliza kisha
akakikagua kile chumba kwa
makini sana hakupata chochote
cha kumsaidia akatoka na
kuanza kuzunguka katika
vyumba vingine.Nyumba
ilikuwa tupu hakukuwa na kitu
chochote ndani
“Hakuna kitu chochote wala
dalili zozote za kuishi mtu ndani
ya nyumba hii lakini
inaonekana kuna shughuli
maalum inayofanyika humu
ndani.Inaonekana kulikuwa na
mitambo au kompyuta humu ila zimeondolewa tena inaonekna
zimeondolewa haraka haraka
kwani kwani kuna baadhi ya
vitu vidogo vidogo
wamevisahau.Who are these
people? Olivia alikuwemo ndani
ya nyumba hii wamempeleka
wapi?akajiuliza akiendelea
kuchunguza kile chumba
kilichokuwa na nyaya nyingi
zilizokatwa katwa.
“Mmoja wa wale jamaa
alifanikiwa kukimbia naamini
tayari amewapa taarifa
wenzake kwamba
wamevamiwa na yawezekana wako njiani wanakuja
kupambana nami.Ngoja
niondoke haraka kwani hakuna
kitu chochote humu ndani cha
kunisaidia” akawaza Mathewna
kumchukua Bravo wakatoka
haraka sana ndani ya ile
nyumba wakatembea kwa
haraka kuelekea mahala
walikoacha gari na kuondoka
“Bado swali kubwa
ninalojiuliza ni kuhusu watu
hawa ni akina nani? Kwa nini
wamemteka Olivia? Naamini
kabisa Olivia alikuwemo ndani
ya nyumba ile lakini ameondolewa,amepelekwa
wapi? Hali niliyoikuta ndani ya
ile nyumba inaonyesha kuna
shughuli Fulani ilikuwa
inafanyika mle ndani lakini
wahusika wake waliondoka
kwa haraka haraka. Kuna kila
dalili za kunithibitishia watu
wale waliondoka kwa haraka
sana na kuna baadhi ya vitu
wameviacha na vingine
walishindwa kuvifungua
ikawalazimu kuving’oa.Nini
kiliwakimbiza? akajiuliza
“Nje ya jumba lile nimeua
walinzi kumi na tatu na wote wakiwa na silaha, namshukuru
sana Bravo kwani ndiye
aliyenisaidia kuweza
kuwatambua na kuwaondoa
wale jamaa.Swali ninalojiuliza
ni kwamba ndani ya nyumba ile
hakukuwa na mtu au kitu
chochote cha maana kwa nini
watu kumi na nne wenye silaha
wazunguke kuilinda nyumba
isiyokuwa na kitu chochote
ndani yake? Mathewakaendelea
kujiuliza maswali
Alipita mahala alipoilipua
nguo ya umeme na kuyakuta
magari zaidi ya matano ya Tanesco na mawili ya polisi
wakiwa wamelizunguka eneo
lile wakifanya
uchunguzi,hakusimama
akaendelea na safari yake.
“Zoezi la kumtafuta Olivia
linazidi kuwa gumu lakini sikati
tamaa nitahakikisha ninafanya
kila linalowezekana hadi nipate
mahala
alikohamishiwa.Natakiwa pia
kumjulisha mama yake ambaye
naamini hivi sasa atakuwa
hajalala anasubiri simu
yangu.Mama yule aliniamini
sana hivyo lazima nimpe mrejesho na kumpa moyo
kwamba Olivia lazima
apatikana ingawa zoezi la
kumtafuta halitakuwa rahisi
kwani watu waliomteka nyara
ni watu wanaonekana
wamejiandaa vya kutosha na
baada ya wenzao kumi na tatu
kuuawa itafanya mapambano
ya kumpata Olivia yawe
magumu zaidi” akawaza
Mathewna kusimamisha gari
pembeni ya barabara akawasha
simu yake akazitafuta namba za
Lucy Themba mama yake Olivia akampigia na simu ikapokelewa
haraka haraka
“Mathewnashukuru sana
umepiga baba.Nimekutafuta
sana katika namba uliyonipa
lakini haikuwa
ikipatikana.Nilitaka
nikushukuru kwa kazi kubwa
uliyoifanya mwanangu”
akasema Lucy na
Mathewakapatwa na mshangao
“Nlikuwa nimezima simu
mama nimeiwasha sasa hivi
kwa ajili ya kukupa mrejesho
wa ile kazi niliyokuja
kuifanya”akasema Mathew “Pole sana baba.Mzee tayari
amefika hapo? Akauliza Lucy na
Mathewakastuka akaitoa simu
sikioni akatazama jina la
aliyempigia liliandikwa Lucy
Themba.Alihisi amekosea
namba
“Mathew”akaita Lucy
“Mama samahani,mzee yupi
unamzungumzia?
“Namzungumzia Agrey
baba yake Olivia.Amekwisha
fika mahala hapo
ulipomuelekeza
akufuate?akauliza Lucy “Mama
sielewi.Nimemuelekeza Agrey
anifuate wapi?akauliza Mathew
“Mathewsi umempigia simu
Agrey muda si mrefu na
kumueleza kwamba
umefanikiwa kumpata Olivia
lakini hali yake si nzuri na
wewe umejeruhiwa kwa risasi
ukamuelekeza mahala ulipo ili
akufuate?Nataka kujua kama
tayari amekwisha fika mahala
ulipomuelekeza akufuate”
akasema Lucy.
“Mama sielewi
unazungumza jambo gani.Simu yangu niliizima na baada ya
kuiwasha mtu wa kwanza
kukupigia ni wewe.Nimekupigia
kukujulisha kwamba nimetoka
mahala ambako niliamini
alikuwepo Olivia nimefanikiwa
kuingia ndani ya nyumba hiyo
lakini Olivia sijamkuta ila kuna
kila dalili kwamba Olivia
alikuwemo ndani ya ile nyumba
na akahamishwa.Mama kwa
ufupi ni kwamba sijafanikiwa
kumpata Olivia lakini si mwisho
wa uchunguzi bado ninaendelea
na operesheni hii hadi nihakikishe Olivia amepatikana”
akasema Mathew
“Mathewunasema
hujampata Olivia?! Akauliza
Lucy Themba huku akihema
haraka haraka
“Ndiyo mama sijafanikiwa
kumpata lakini bado
ninaendelea na uchunguzi
wangu.Alikuwemo katika
nyumba ile ambayo programu
yangu ilinionyesha lakini
ameondolewa na sijui
amepelekwa wapi”
“Mungu wangu ! akasema
Lucy “Mama ulisema kuna mtu
aliwapigia simu akijifanya ni
mimi na kuwaeleza kwamba
Olivia
amepatikana?Mathewakauliza
“Mathewumenichanganya.
Ninahisi moyo wangu unataka
kupasuka kwa mstuko”
akasema Lucy
“Mama nieleze tafadhali
nini hasa kimetokea?akauliza
Mathew
“Kuna mtu amempigia simu
Agrey usiku huu kwa kutumia
namba nyingine tofauti na hii
akajitambulisha kwamba yeye ni Mathewna akadai kwamba
amefanikiwa kumpata Olivia
lakini amejeruhiwa kwa risasi
akamtaka Agrey amfuate mara
moja mahala alipomuelekeza ili
awapeleke hospitali.Hatukuwa
na shaka yoyote kuwa ni wewe
kwani mtu huyo alizungumza
akiwa katika hali ya maumivu
makali na tuliamini kwamba ni
wewe umejeruhiwa.Agrey
alitoka na
kukufuata.Nimeishiwa nguvu
kusikia kwamba si wewe
uliyepiga simu”
“My God ! akasema Mathew “Mimi sikupiga simu hiyo
mama na wala sina namba za
simu za mzee Agrey.Mama
naomba usihamaki
tunachotakiwa kufanya ni
kumzuia haraka sana mzee
asiende huko mahala
anakoelekea kwani anakwenda
katika hatari kubwa.Naomba
umpigie simu na umtake ageuze
haraka sana asiende huko
alikoelekezwa” akasema
Mathewna Lucy akaisubirisha
simu yake akampigia simu
Agrey lakini simu yake haikuwa
ikipatikana “Mathewsimu yake
haipatikani tena” akasema Lucy
akianza kulia.Mathewakahisi
miguu inamtetemeka
akaegemea kiti na kuvuta pumzi
ndefu.
“Mambo yanazidi kuwa
magumu” akawaza
“Mathewnitafanya nini
mimi?akauliza Lucy
“Mama huyo jamaa
alimuelekeza Agrey amkute
wapi?
“Alimuelekeza aende mtaa
wa Msanzi mbele kidogo ya
jengo la Zawama Saccos kuna jengo la ghorofa halijamaliziwa
kujengwa akamtaka wakutane
hapo”
“Mama ninakwenda hapo
sasa hivi.Ngoja nijaribu
kumuwahi kabla hajafika hapo”
akasema Mathewna kuwasha
gari akaingia barabarani
“Mathewtafadhali naomba
uhakikishe unampata
Agrey.Hakikisha haingii katika
tatizo lolote” akasema Lucy
huku akilia
“Mama nitafanya kila
niwezalo lakini nitakuomba
suala hili usimueleze mtu yeyote hadi nitakapompata
Agrey na kumfahamu mtu huyo
aliyewapigia simu.Hata hivyo
mama kuna kitu nataka
kukifahamu.Kuna mtu yeyote
ambaye mlimueleza kuhusu
mimi kwenda kumtafuta Olivia?
“Hakuna mtu tuliyemueleza
baba ndiyo maana ulipopiga ile
simu moja kwa moja tukaamini
ni wewe” akajibu Lucy
“Sawa mama nitawasiliana
nawe baadae” akasema
Mathewna kukata simu
“Ni nani aliyempigia simu
Agrey Themba akajifanya nini mimi? Lazima ni mtu
aliyefahamu kuwa nimekwenda
kumtafuta Olivia.Lucy anakataa
kwamba hawajamueleza mtu
yeyote kuhusu suala hili la mimi
kwenda kumtafuta Olivia sasa
mtu huyo amefahamu vipi kama
nimekwenda kumtafuta
Olivia?akajiuliza
“Mtu pekee ambaye
nilimueleza kuhusu mpango
wangu ni Tino ambaye
nilichukua silaha kwake.Tino
ninamfahamu sana hawezi
akafanya kitu kama
hiki.Mwingine aliyefahamu kuhusu operesheni hii ni
Ruby.Yule ni mwenzangu na
hawezi akatoa siri zangu.Huyu
mtu aliyepiga simu amefahamu
vipi kama nimekwenda
kumuokoa Olivia?Nini hasa
lengo la kumpigia Agrey
Themba na kumtaka amfuate
mahala hapo alipomuelekeza?
Mathewakajiuliza maswali
ambayo alishindwa kuyapatia
majibu
“Lucy hataki kuniambia
ukweli lakini lazima kuna mtu
wamemueleza kuhusu mpango
wangu wa kwenda kumuokoa Olivia.Ninaanza kupata picha
kwamba kuna mtu wa karibu
sana na familia ya Agrey
Themba ambaye anahusika na
tukio la kutekwa Olivia.Mtu
huyo lazima atakuwa
anawasiliana na watekaji na
kuwapa taarifa zote anazozipata
kutoka kwa akina
Agrey.Ninahisi kwamba hata
kitendo cha Olivia kuhamishwa
mtu huyo n diye aliyewapa
taarifa watekaji kwamba
ninafahamu mahala alipo Olivia
na ninakwenda kumuokoa
hivyo ndiyo maana wakamuondoa haraka sana
katika ile nyumba” akawaza na
kuongeza mwendo wa gari
“Sasa nimepata majibu kwa
nini nyumba ile tupu ilikuwa
inalindwa na watu kumi na nne
wenye silaha.Ulikuwa ni
mtego.Walijua lazima
nitakwenda pale hivyo
wakajipanga kunisubiri lakini
kwa bahati mbaya kwao mimi
ninazo mbinu nyingi zaidi
yao.Hii ni hatua kubwa sana
nimeipiga katika kufahamu
mahala alipo Olivia na
ninaamini nimekaribia sana kumpata.Nikimfahamu mtu
ambaye walimueleza kuhusu
mpango wangu wa kwenda
kumuokoa Olivia tutakuwa
tumempata Olivia.Ngoja
kwanza nifike mahala ambapo
wamemuelekeza Agrey
aende.Naomba nimuwahi kabla
hajafika mahala hapo kwani
naamini lengo lao kumtaka
aende hapo ni kumuua au
kuteka.Watu hawa ni
wataalamu sana wamejipanga
vizuri na wanahakikisha hakuna
kikwazo chochote kinajitokeza
katika kukamilisha mipango
 
Tenganisha maneno pindi unapoandika 'Mathew'
SIRI

Mwendelezo..


“Unafikiria tufanye nini
mheshimiwa rais?akauliza
Devotha
“Tunatakiwa kumpata
Agrey Themba baba yake
Olivia”
“Mheshimiwa rais !
Devotha akashangaa
“Tumchukue tena na Agrey
Themba?Tayari tunaye mwanae
tukimchukua na yeye huoni
kama tutazidi kukoroga
mambo?
“Hiyo ndiyo njia pekee ya
kumfanya Olivia
azungumze.Bila kutishia kumuua baba yake basi Olivia
hataweza kusema chochote.Hii
ni vita na ili tupate ushindi
lazima tutumie kila mbinu
kupigana.Olivia anampenda
mno baba yake hivyo kama
tukifanikiwa kumpata na
kutishia kumuua basi atatueleza
kila kitu”
“Ni vipi kama hata baada ya
kutishia kumuua baba yake
Olivia hatakuwa tayari kusema
chochote?akauliza Devotha
“Agrey ni rafiki yangu wa
siku nyingi sana lakini hapa
tunaweka mbele maslahi ya taifa hivyo kama ikilazimika
kumkata pumzi tutafanya hivyo
kwani tayari urafiki wetu
umekwisha ingia dosari kwa
suala hili la Olivia.Katu siwezi
kuwa na huruma kwa Olivia
kwani yeye amekubali
kutumika na magaidi na sasa
familia yangu yote iko
mashakani.” akasema Dr Evans
na ukimya mfupi ukapita
“Agrey alikuwa na wasiwasi
sana na Mathewndiyo maana
akanipigia kunipa taarifa zake
na kunitaka nimsaidie kufanya
uchunguzi kama kweli Mathewamewahi kufanya kazi
katika idara ya ujasusi
Tanzania.Nitampigia simu na
kumfahamisha kwamba
Mathewni kweli amewahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi na nitamshauri tumpe
nafasi Mathewya kuchunguza
suala hili la Olivia.Baada ya saa
moja kutoka sasa mtu mmoja
kutoka idara yako atampigia
simu Agrey akijifanya ni
Mathew.Atazungumza kama
vile yuko katika sehemu ya
kujificha na atamjulisha
kwamba amefanikiwa kumpata Olivia ingawa hali yake si nzuri
sana hivyo atamuelekeza
sehemu ya kwenda.Mtu huyo
amuonye Agrey asiwasiliane na
mtu yeyote yule kumueleza
kuhusu suala lile.Ninaamini
Agrey atafuata maelekezo hayo
na atakapofika mahala
alipoelekzwa na
Mathewatachukuliwa na vijana
wetu na huo utakuwa ni
mwisho wake” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais wazo
lako ni zuri lakini ..” “Agrey Themba lazima
apatikane Devotha. Hakuna
mjadala katika suala hilo.Bila
kumpata Agrey hatutapata
chochote kutoka kwa Olivia
ambaye anashirikiana na
magaidi hivyo kama
hatutatumia nguvu kubwa
hatutaweza kupata chochote
kutoka kwake.Nataka
operesheni ya kumchukua
Agrey Themba ifanyike usiku
wa leo.Kabla ya mapambazuko
ya kesho tuwe tayari tumeanza
kupata taarifa muhimu.Umenielewa Devotha?”
akauliza Dr Evans
“Niumekuelewa
mheshimiwa rais”
“Good.Wekeni nguvu usiku
huu katika mambo haya mawili
kwanza kumpata Mathewna vile
vile kumpata Agrey
Themba.Hakikisha unanijulisha
kila kinachoendelea” akasema
Dr Evans akachukua simu na
kumpigia Agrey
“Dr Evans” akasema Agrey
Themba
“Agrey nimekupigia kukupa
mrejesho kuhusiana na kinachoendelea.Nimewasiliana
tena na mkuu wa jeshi la polisi
nchini na amenihakikishia
kwamba jeshi la polisi
wanaendelea na uchunguzi na
wamefikia hatua
nzuri.Yawezekana hadi asubuhi
ya kesho wakawa na taarifa
nzuri za kutupa.Tuendelee
kuwa wavumilivu na
kuwaamini” akasema Dr Evans
“Nashukuru sana Dr
Evans.Imani yangu kwa jeshi la
polisi ni kubwa na ninaamini
watafanikiwa kumpata mwanangu” akasema Agrey
Themba
“Agrey suala la pili
uliniomba nikusaidie kufanya
uchunguzi kuhusiana na
MathewMulumbi.Nimewasilian
a na mkurugenzi wa idara ya
ujasusi Tanzania na amenitumia
faili la
MathewMulimbi.Nimelipitia
kwa umakini ni kweli
alichokisema aliwahi kufanya
kazi katika idara ya ujasusi na
faili lake linaonyesha kwamba
ni mmoja wa majasusi wa
kiwango cha juu kabisa.Baada ya kupitia faili lake
nimejiridhisha kwamba ni mtu
anayeweza kuwa na msaada
mkubwa.Ninashauri tumuache
aendelee na uchunguzi wake
lakini ahakikishe kwamba
uchunguzi wake hauleti
mkanganyiko kati yake na jeshi
la polisi.Mpe muda na nafasi ya
kufanya uchunguzi wake kwa
uhuru ninaamini anaweza
akasaidia sana”akasema Dr
Evans
“Dr Evans ahsante sana
kwa taarifa hizo nzuri.Nitampa
nafasi kama ulivyoshauri yawezekana akawa na msaada
mkubwa”akasema Agrey
“Sawa Agrey nitaendelea
kukupa taarifa kila pale
nitakapokuwa ninazipata.”
Akasema Dr Evans na kukata
simu akamgeukia Devotha
“Tayari nimetengeneza
njia.Pale atakapopokea simu
kutoka kwa mtu atakayejifanya
ni MathewMulumbi hatakuwa
na wasiwasi wowote lazima
atafuata maelekezo
atakayopewa” Akasema Dr
Evans akaagana na Devotha. RIYADH - SAUDI ARABIA
Saa nne za usiku magari
manne yaliwasili katika makazi
ya Habiba Jawad.Kabla magari
yale hayajasimama wakaruka
watu na kulizingira gari moja na
baada ya dakika chache mlango
wa lile gari ukafunguliwa
akashuka jamaa mmoja
mwenye ndevu nyingi
aliyejifunga kilemba kichwani
.Moja kwa moja akaingia ndani
ya jumba lile kubwa akaelekea
ndani katika chumba
kilichokuwa na meza ya duara na viti zaidi ya kumi.Ndani ya
chumba kile kulikuwa na watu
wapatao saba
“Sayid karibu sana.”
akasema Habiba Jawad
“Samahani sana kwa
kuchelewa.Nilipata dharura
iliyonichelewesha.Tayari kikao
kimeanza? Akauliza Sayid
“Bado hatujaanza tulikuwa
tunakusubiri wewe.Tunaweza
kuanza sasa.Abu wakaribishe
akina Khalid” Akasema
Habiba.Mbele ya chumba kile
kulikuwa na luninga mbili
kubwa Abu dahir akabonyeza kitufe katika kifaa cha kuwashia
na luninga zile zikawaka
wakaonekana watu
wawili.Yalikuwa ni
mazungumzo ya moja kwa
moja.Habiba akarekebisa koo
na kusema
“Karibuni sana Khalid
Radwan na
Rashid.Mtatusamehe kwa
kuchelewa kuanza kwa kikao
hiki muhimu ni kutokana na
Sayid kuchelewa kufika lakini
tayari yuko hapa tunaweza
kuendelea.” “Hakuna tatizo tuendelee”
akasema Khalid Radwan mmoja
kati ya viongozi wa juu wa
kundi la IS akiwa nchini Iraq
“Ndugu zangu kikubwa
katika kikao hiki ni kujadili kwa
kina kile kilichotokea Tanzania
siku ya leo na hatima ya
mipango yetu ya kumpata
Seif.Taarifa tulizozipata ni
kwamba,Olivia Themba
ambaye amekuwa akitusaidia
katika mambo mengi hasa
katika operesheni ya kumtafuta
Seif ametekwa nyara na watu
wasiojulikana.Huyu ndiye tulimtanguliza mbele hivyo
kama ametekwa mipango yetu
itatetereka sana ndiyo maana
nimeitisha kikao hiki ili tujadili
ni namna gani mipango yetu
itakavyoendelea.Karibuni sana
kwa michango ya mawazo”
akasema Habiba Jawad
“Kwa maelezo ambayo
Habiba amenipa ni kwamba
Olivia ametekwa wakati
akitokea Kinshasa alikoenda
kuonana na Seif al
muhsin.Nataka kujua mpaka
sasa kuna taarifa zozote
mmekwisha zipata kutoka kwa watu wetu walioko Tanzania
kuhusiana na tukio hilo?
Akauliza Khalid
“Tumekuwa na
mawasiliano na watu wetu
Tanzania na kwa taarifa za
mpaka jioni hii bado Olivia
hajapatikana na hajulikani
alipo” akajibu Sayid Omar
“Mnahisi nani anahusika
katika tukio hili la kumteka
Olivia? Akauliza Khalid
“Mpaka sasa hatujui ni nani
anahusika na tukio lile lakini
kwa namna lilivyotokea ni tukio
lililofanywa kitaalamu sana” akasema Sayid Omar na
kuelekea upande mwingine
kulikokuwa na luninga nyingine
kubwa.
“Tumejaribu kukusanya
picha kadhaa kutoka eneo la
tukio.Zinazoonekana hapa ni
gari mbili moja ikiwa ya Olivia
na nyingine ikiwa ni ya walinzi
wake.Kwa mujibu wa maelezo
yaliyotolewa na mashuhuda ni
kwamba magari haya
yalipokaribia kufika nyumbani
kwa Olivia ilitokea helkopta
angani na kuanza kufanya
mashambulizi.Walinzi wote wa Olivia waliuawa na mara
yakatokea magari mawili
yaliyofika kwa kasi kubwa na
kumchukua Olivia wakaondoka
naye na mpaka sasa hajulikani
mahala alipo.Tunajaribu
kulihusisha tukio hili na yale
ambayo yamewahi kutokea
sehemu nyingine Afrika
ambapo watu matajiri au
wanafamilia wao hutekwa na
kisha watekaji hudai fedha
nyingi.Tunahisi kwamba lengo
la watekaji hao ni kujipatia
fedha”akasema Sayid
Omar.Ukimya ulitawala mle ndani ya chumba kila mmoja
akiwa ameyaelekeza macho
yake mbele katika luninga na
baada ya muda Khalid akasema
“Kwa mtazamo
wangu,waliomteka Olivia
walifahamu alikuwa nchini
Congo na walikuwa
wanamfuatilia kwa karibu kila
anachokifanya.Ninafahamu
mbinu mbali mbali za utekaji
na kwa namna tukio hili
lilivyotokea ninaamini watekaji
hawajafanya hivi kwa ajili ya
kujipatia fedha.Hili tukio ni la
kitaalamu sana na limefanywa na watu wenye taaluma kubwa”
Khalid akanyamaza kwa muda
kisha akasema
“Naomba mkubaliane nami
kuwa tukio hili limefanywa na
watu wa serikali”
Watu wote mle ndani
wakatazamana
“Ninawahakikishia ndugu
zangu,kwamba huu mchezo
umechezwa na serikali.Nina
uzoefu mkubwa na mambo
kama haya ya utekaji na
ninafahamu aina mbali mbali za
utekaji na kwa utekaji huu wa
Olivia ninashawishika kuamini kwa asilimia mia moja kwamba
serikali ya Tanzania
wanahusika” akasema Khalid
“Serikali ya Tanzania wana
sababu yoyote ya kumteka
Olivia?akauliza Habiba
“Olivia ni mtu mwenye jina
kubwa Tanzania,baba yake ni
bilionea ni rafiki mkubwa wa
rais wa Tanzania.Inasemwa
kwamba urafiki wao umeanza
toka wakiwa vijana hadi
leo.Iweje serikali wamteke mtu
kama huyu mwenye ukaribu
mkubwa na rais?akauliza Abu
dahir “Jibu la swali hilo ni
rahisi,tayari kuna kitu
wamekigundua kwa Olivia
ndiyo maana wamemteka.Olivia
hana sababu yoyote ya kutekwa
na serikali isipokuwa kwa
sababu moja tu kubwa ambayo
ni kugundulika kushirikiana
nasi.Ninawaambia ukweli
ndugu zangu kwamba hiyo
ndiyo sababu pekee
iliyompelekea Olivia
akatekwa.Nina uhakika
mkubwa wamekuwa
wakifuatilia nyendo zake kwa
muda mrefu na wakagundua kila kitu kuhusu Olivia na
mtandao wetu.Mmekuwa
makini kwa muda mrefu na kila
kitu kikaenda vyema lakini
kuna mahala mlijisahau na
kuachia mwanya mkasababisha
Olivia akajulikana” akanyamaza
na wote walikuwa kimya
wakimsikiliza
“Jambo la pili” akaendelea
“Yawezekana Olivia
alikuwa anatumiwa na serikali
kuchota siri zetu na baada ya
kupata siri za kutosha kabisa
wakaamua kucheza mchezo
ionekane kwamba Olivia ametekwa na watu
wasiojulikana lengo ni
kumuhifadhi sehemu kwa muda
ili kushughulikia kwanza taarifa
zile walizozipata” akasema
Khalid.Bado chumba kiliendelea
kuwa kimya wote wakimsikiliza
yeye
“Katika hayo mawili
niliyoyaelezea moja wapo
linaweza kuwa ni sababu ya
kupotea kwa Olivia hata hivyo
kupotea kwa Olivia si sababu ya
kuturudisha nyuma na
kuvuruga mipango
yetu.Tunawapoteza watu wetu kila uchao na wengine ni
makamanda muhimu na bado
mapambano yanaendelea hivyo
mipango yetu yote itaendelea
kama kawaida hadi tuhakikishe
Seif anapatikana lakini
kutakuwa na mabadiliko
kidogo.Nataka kujua je kile
kirusi alichotengeneza Olivia
kimekwisha tumika kama
tulivyokusudia?akauliza Khalid
“Ndiyo.Tayari Coletha
mtoto wa rais amechomwa
sindano yenye virusi”akajibu
Sayid “Baada ya kuchomwa
mmefuatilia kujua maendeleo
yake? akauliza Khalid
“Toka alipochomwa
sindano ile yenye virusi Coletha
hajaweza kuingia darasani
tayari ameanza kuumwa na
amepewa mapumziko hadi pale
hali yake itakapokuwa nzuri”
akasema Sayid Omar
“Vizuri sana kama tayari
amekwisha chomwa sindano
yenye virusi .Mpango wetu wa
awali ulikuwa ni kumpigia simu
rais kumjulisha kwamba
mwanae amechomwa sindano yenye virusi na atakufa endapo
hatatupa taarifa za Edger lakini
baada ya hili lililotokea leo
itatulazimu kubadili
mpango.Tunatakiwa kumteka
huyo mtoto wa rais na kisha
tutawasiliana na rais moja kwa
moja na tutamuonyesha
maendeleo ya mtoto wake
anavyopata taabu na hii
itamfanya atekeleze kila
tunachokitaka.Wasiliana na
watu wetu Dar es salaam
waandae mpango huo haraka
sana ikiwezekana usiku huu
huu mtoto huyo wa rais apatikane.Wapigie simu
nizungumze nao sasa hivi
niwape maelekezo” akasema
Khalid.
Kwa kutumia simu
iliyokuwa mezani Sayid Omar
akampigia Fahad mmoja wa
watu wao aliyepo Tanzania.
“Hallo Sayid” akasema
Fahad
“Fahad nini kinaendelea
hapo Dar es salaam?akauliza
Sayid
“Huku bado mambo ni vile
vile.Mpaka sasa hakuna taarifa
zozote za kupatikana Olivia” “Sawa Fahad nataka
uzungumze na Khalid Radwan”
akasema Sayid
“Fahad unazungumza na
Khalid Radwan naomba
nisikilize vizuri.Kufuatia tukio
la kutekwa kwa Olivia mipango
yetu imebadilika.Nataka
mjipange usiku huu wa leo
muweze kumpata mtoto wa rais
wa Tanzania.Najua
nimewastukiza lakini
nawaombeni mfanye kila
linalowezekana usiku wa leo
aweze kuchukuliwa kutoka
hapo chuoni hata kama ni kwa kufanya shambulio lakini lazima
huyo mtoto wa rais
apatikane”akasema Khalid
“Khalid kuna tatizo kidogo
katika mpango huo” akasema
Fahad
“Kuna tatizo gani?sura ya
Khalid ikabadilika
“Nimepewa taarifa na
Karim mtu wangu ambaye
anasoma katika chuo
anachosoma Coletha,rais
amefika usiku huu pale chuoni
na kumchukua mwanae
inasemekana amempeleka
hospitali”akasema Fahad “Amempeleka
hospitali?Khalid akauliza
“Ndiyo amempeleka
hospitali kuchunguzwa afya
yake”
“Una uhakika na taarifa
hizo Fahad?
“Ndiyo.Karim ana ukaribu
mkubwa na marafiki zake
Coletha ambao wamempa
taarifa hizo.Wanadai kwamba
Coletha amepelekwa hospitali
kufanyiwa uchunguzi wa afya
yake”
“Kwa nini rais amchukue
Coletha usiku huu na kumpeleka hospitali
kumchunguza afya yake?
Akauliza Sayid
“Msiumize vichwa
vyenu,tayari rais amefahamu
mwanae amechomwa sindano
yenye virusi.Niliwaambia
kwamba Olivia yuko upande wa
serikali na ndiye aliyempa rais
siri hii na nyingine nyingi
kuhusu sisi.Baada ya rais
kupewa taarifa kwamba
mwanae amechomwa sindano
yenye virusi amemchukua
haraka na kumpeleka hospitali
na huko lazima atapona kwani Olivia ndiye aliyetengeneza
virusi hivyo na anafahamu tiba
yake”akasema Khalid chumba
kikawa kimya.Baada ya muda
Sayid akasema
“Kuna swali
ninajiuliza,Olivia ndiye
aliyetengeneza kirusi kile na
angeweza kumtibu mtoto wa
rais kimya kimya kwa nini basi
rais amempeleka mwanae
hospitali kumchunguza afya
yake? akauliza Sayid Omar
“Swali zuri Sayid lakini
hatuwezi kupata majibu yake
kwa sasa.Ukweli ni kwamba tumerudi kwenye sifuri ndugu
zangu.Mipango yetu yote ya
muda mrefu imeshindikana kwa
sababu ya kumuamini
Olivia.Tunachotakiwa kufanya
kwa sasa ni kutumia nguvu
kumshinikiza rais ili atupe
taarifa tunazozihitaji.Bila
kutumia nguvu hatutafahamu
mahala alipo Seif kwani Olivia
tayari amekwisha tusaliti”
akasema Khalid
“Khalid unashauri nini
kifanyike? akauliza sema
Habiba. “Sikilizeni ndugu zangu
mpango wetu bado unaendelea
kama kawaida na hakuna
kitakachosimama.Rashid
Mombasa unanisikia?
“Ninakusikiliza mkuu”
akasema Rashid mmoja wa
viongozi wa IS aliyeko
Mombasa Kenya ambaye toka
kikao kilipoanza amekuwa
kimya
“Kwako kuna kikosi
kikubwa kuliko
Tanzania.Nataka uandae watu
kumi usiku huu kwa ajli ya
safari ya kuelekea Tanzania ambako watakutana na timu ya
Fahad wataungana katika
kumteka mtoto wa rais wa
Tanzania.Nataka kesho kwa
namna yoyote ile mtoto wa rais
akachukuliwe hospitali na
tukishafanikisha hilo ndipo
tutakuwa na uhakika wa
mipango yetu kuendelea kama
tunavyotaka. Katika mambo
tutakayomtaka rais wa
Tanzania ayafanye ni
kutukabidhi Seif pamoja na
Olivia ambaye tutamkata
kichwa kama adhabu ya usaliti
mkubwa aliotufanyia.Rashid na Fahad mmenielewa?akauliza
Khalid
“Nimekuelewa
Khalid.Maelekezo yako
yatafanyiwa kazi haraka sana”
akasema Rashid
“Nimekuelewa Khalid na
maandalizi yanaanza usiku huu
huu” akasema Fahad kutokea
Dar es salaam
“Safi sana.Kumbukeni
hatupaswi kushindwa vita hii
na yeyote ambaye atasababisha
tushindwe hii vita adhabu yake
ni kukatwa kichwa.Tanzania ni
muhimu sana tuipate kwani tukiipata tutakuwa tumeipata
Afrika nzima hivyo kila juhudi
zifanyike kuhakikisha kwamba
mipango yetu yote nchini
Tanzania inakwenda
vizuri.Nawatakia utekelezaji
mzuri wa mipango yetu”
akasema Khalid na kuzima
kamera.Wote mle ndani
wakatazamana kwa muda kisha
Habiba akasema
“Nadhani nyote mmesikia
maelekezo
yaliyotolewa.Mikakati ianze
mara moja kuitekeleza.Lazima tuhakikishe Seif anapatikana”
akasema Habiba
“Mimi bado nina mashaka
kidogo kuhusiana na kauli ya
Khalid kwamba Olivia
anatumiwa na serikali.Wote
humu tulionana naye alipokuja
na sote ni mashahidi namna
alivyokuwa tayari kusaidia
katika kupatikana kwa Edger.Ni
kwa sababu yake Seif yuko hai
mpaka leo,alipambana dhid yal
wale walijaribu kumuua kwa
kumuwekea sumu na kuokoa
maisha yake.Tuna uhakika
kwamba Edger yuko hai leo kwa sababu yake.Bila yeye
kusingejengwa kituo kile cha
utafiti nchjini Tanzania
ambacho kitakuwa na manufaa
makubwa kwetu.Iweje leo
itolewe amri ya kumkata
kichwa na wote humu tunakaa
kimya?akauliza Sayid kwa ukali
“Sayid yuko sahihi.Sina
hakika Olivia anatumiwa na
serikali.Tumekwisha shirikiana
naye mambo mengi hadi sasa
kama angekuwa anashirikiana
na serikali tusingefika hatua hii
tuliyofika.Ninaweza
kukubaliana na ile sababu yake ya kwanza kwamba huenda
serikali ya Tanzania
wamemgundua kwamba
anashirikiana nasi na ndiyo
maana wakamteka nyara lakini
Olivia kushirikiana na serikali
ya Tanzania hilo
ninalikataa”akasema Habiba
“Jambo lingine kama Olivia
angekuwa anashirikiana na
serikali asingekubali mtoto wa
rais achomwe sindano yenye
virusi.Angemjulisha rais
mapema na angemuondoa
mtoto wake lakini inaonekana
rais amefahamu leo hii kwamba mwanae amechomwa sindano
yenye virusi na atakuwa
ameambiwa na Olivia” akasema
Abu dahir
“Kama Olivia amemweleza
rais kwamba mwanae
amechomwa sindano yenye
virusi tujiulize ni kwa nini
alimwambia?Aliamua kutumia
njia hiyo kumshinikiza rais
amueleze kuhusu
Edger?akauliza Habiba
“Hata mimi ninaanza kuhisi
hivyo lakini hatuwezi kuwa na
jibu la uhakika hadi pale Olivia
atakapopatikana hivyo basi tujitahidi kumtafuta Olivia na
kumpata ili tufahamu sababu za
kutekwa kwake.Binafsi siko
tayari kumuona Olivia
anakatwa kichwa labda hadi
nitakapothibitisha kweli
anashirikiana na serikali hivyo
basi nitahakikisha ninasimama
upande wake na kunusuru
maisha yake” akasema Sayid
Omar
“Sayid sote hapa hakuna
anayetaka au kutamani
kumuona Olivia akikatwa
kichwa.Lazima tufanye kila
linalowezekana kumuokoa na tutamuokoa pale
tutakapothibitisha kwamba
hashirikiani na serikali ya
Tanzania ” akasema Habiba
wakaendelea na mjadala wa
kina kuhusiana na suala lile
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Mathewaliendesha gari
taratibu akiifuata ramani
iliyokuwa katika kompyuta
yake aliyoiweka pembeni na
kwa mujibu wa ramani yake
alikaribia sana kufika eneo
alilokuwa anakwenda “Nimekaribia kufika eneo la
tukio ninatakiwa kuhakikisha
eneo lote linakuwa giza ili
kuniwezesha kuingia mahala
aliko Olivia bila tatizo”akawaza
Mathewakiendelea kutazama
nje
“Eneo liko kimya watu wote
wamejifungia majumbani
mwao”
Mathewakasimamisha gari
akafungua begi lake na kutoa
kitu Fulani kilichofungwa nyaya
kadhaa akashuka garini
akatazama pande zote kama
kuna mtu lakini barabara ilikuwa tupu,kwa haraka
akaenda katika nguzo ya
umeme iliyokuwa pembeni ya
barabara akakipachika kifaa
kile katika nguzo ya umeme
akakifunga na gundi halafu
akarejea haraka garini na
kuondoka eneo lile.Baada ya
umbali mfupi akachukua kifaa
mithili ya simu ya mkononi
akabonyeza namba Fulani na
mlipuko ukatokea katika ile
nguzo aliyoweka kile kifaa na
eneo lote likawa giza umeme
ulikatika. “Kazi inaanzia hapa”
akasema Mathewbaada ya
umeme kukatika
Mathewaliendelea na safari
yake akiifuata ramani ile
akafika katika barabara ambayo
ilikuwa inaelekea mahala
ambako ramani ilionyesha
ndiko aliko Olivia.Aliipita
barabara ile akaendelea mbele
zaidi akazima gari akageuka na
kumtazama mbwa wake
“Bravo it’s time” akasema
huku akimkuna mbwa wake
shingoni.Akachukua bunduki
aina ya AS50 Snipe rifle na bastora mbili akaweka kichwani
miwani ya kumuwezesha kuona
vyema kwenye giza halafu
akaweka begi lake lenye vifaa
vingine mgongoni akashuka
garini akiwa na Bravo
wakaanza kutembea hadi
walipoikuta ile barabara
inayoelekea katika nyumba
aliko Olivia.Kulikuwa na maua
kandoni mwa barabara
ile.Mathewakiwa na bunduki
yake yenye uwezo mkubwa
aliambaa ambaa kandoni mwa
barabara ile akiwa na mbwa
wake wakijinga na miti ya maua.Alikuwa katika tahadhari
kubwa.Alikaribia sana kufika
katika jumba lile akamkuna
kuna mbwa wake shingoni
akampa maelekezo
“Bravo now go !
Mathewakamuelekeza mbwa
wake ambaye alitoka mbio
kuelekea katika ile
nyumba.Mathewaliyevaa
miwani ile maalum ya kuonea
kizani akaendelea kunyata huku
akimfuatilia Bravo aliyekuwa
amemuwekea kitu Fulani katika
mkanda wake ambacho kilimuwezesha kumuona
kupitia ile miwani aliyovaa.
Bravo alikwenda kimya
kimya hadi katika geti la
nyumba ile na taratibu bila
kutoa ukelele akanusa harufu
ya mtu eneo lile akamsogelea
jamaa mmoja aliyekuwa
amejibanza kandoni mwa geti
akiwa amevaa mavazi
meusi.Kwa macho ya kawaida
haikuwa rahisi
kumtambua.Yule jamaa alistuka
baada ya kumuona mbwa
karibu yake.Akawasha tochi ili
aweze kumtazama vyema yule mbwa.MathewMulumbi kupitia
miwani yake aliweza kumuona
yule jamaa vizuri na kwa
kutumia bunduki yake
aliyoifunga kiwambo cha kuzuia
sauti akampiga risasi kati kati
ya paji la uso akaanguka
chini.Baada ya yule jamaa
kuanguka Bravo akaambaa na
ukuta akakutana na mtu wa pili
aliyekuwa amejibanza nyuma
ya mti.Mathewakamuona na
kumdondosha kwa risasi moja
ya kichwa.Kazi kubwa ya Bravo
ilikuwa ni kuwatafuta walinzi
waliojificha gizani na Mathewaliweza kuwaona
kirahisi na kuwamaliza kwa
kutumia bunduki yake kubwa
iliyofungwa kiwambo cha sauti
“Hawa walinzi mbona
hawaishi?akajiuliza baada ya
kumuona Bravo akiendelea
kuzunguka ile nyumba
akimfuata mwingine baada ya
kuhisi harufu ya mtu.Tayari
alikwisha wakata pumzi watu
nane lakini bado ilionekana
wapo zaidi.Akiendelea
kumfuatilia Bravo akawaona
watu watano wakiwa wamekaa katika matofali wakizungumza
wote wakiwa na bunduki
“Kuna ulinzi mkubwa
kuzunguka hii nyumba.Nadhani
ulinzi huu wote ni kwa ajili ya
kumlinda Olivia.Naamini OIivia
yuko ndani ya nyumba hii kama
ramani
inavyonionyesha?akawaza
Mathewna kuielekeza bunduki
yake kwa wale jamaa ambao
mmoja wao alistuka na kuruka
baada ya kuguswa na
kitu.Wenzake walianza
kumcheka mwenzao baada ya
kumulika tochi na kugundua kilichomstua mwenzao ni
mbwa.Yule jamaa tayari
alikwisha iweka sawa bunduki
yake tayari kwa shambulio.
“Hey hey hey..ni mbwa
usiogope! Yule jamaa ambaye
aliruka alipoguswa na kitu
akaambiwa na mwenzake ndipo
alipotulia na kumuona mbwa
mkubwa akiwa karibu yao
akiwaangalia
“Katokea wapi huyu
mbwa?akauliza mmoja
wao.Wakati wakiendelea
kujiuliza mmoja wao
akaanguka.Wakapatwa na mstuko na kila mmoja akashika
silaha yake vyema mara
akaanguka wa pili na
watatu.Haikujulikana sababu
yakuanguka kwao mmoja kati
ya wawili waliobaki akainama
ili kuwatazama wenzake
walioanguka ajue sababu ya
kuanguka kwao akajikuta
akipigwa risasi ya bega
akaanguka na kutoa mguno wa
maumivu.Yule mwenzake
aliyebaki akaiweka sawa
bunduki yake akaanza kuangaza
pande zote kumtafuta mtu
aliyewapiga wenzake risasi lakini hakuona mtu yeyote
akamfuata yule mwenzake
aliyepigwa risasi ya
bega.Alikuwa anavuja damu
nyingi.Haraka haraka
akachukua redio ya
mawasiliano na kutaka
kuwajulisha wenzake lakini
alipobonyeza tu
Mathewakampa tiketi ya
kuzimu kwa risasi moja iliyotua
katikati ya paji la uso.Alibaki
yule jamaa mmoja aliyepigwa
risasi ya bega ambaye alikuwa
anagugumia kwa
maumivu.Mathewakanyata kumsogelea lakini kabla
hajamfikia akatokea mtu mmoja
ambaye naye alikuwa na
bunduki mkononi.Akamulika
tochi na kuwaona wenzake
wakiwa wamelala chini
wakivuja damu hawakuwa na
uhai.Kwa kasi ya umeme
akaitupa bunduki yake na
kutoka mbio.Mathewakaachia
risasi mbili lakini alichelewa
kwani jamaa alikwisha
potea.Akanyata kumuendea
yule jamaa aliyekuwa
amepigwa risasi ya bega.Yule
jamaa aliweza kusikia hatua za mtu akimsogelea haraka haraka
akachomoa bastora iliyofungwa
kiwambo cha sauti na kujipiga
risasi ya kichwa akafa pale pale.
“Oh no !! Huyu alikuwa
muhimu sana kwani angeweza
kunipa taarifa zote kuhusiana
na watu hawa” akawaza
Mathewmara Bravo akatokea.
“Thank you Bravo !
akasema Mathewkwa sauti
ndogo.
“Bravo amerejea nadhani
hakuna huku nje
wamekwisha.Nimewaondoa
watu kumi na tatu.Ni wengi sana.Walikuwa wamejizatiti
mno kiulinzi kama ningekuja
kichwa kichwa nisingetoka
salama eneo hili.Ulinzi huu
unanipa uhakika kuwa lazima
Olivia yuko ndani ya nyumba
hii.Lakini watu hawa ni wenye
bunduki nzito kama hizi ni
akina nani? Akajiuliza na
kutazama pande zote lakini
hakuona mtu akaanza
kutembea kwa tahadhari
kurejea getini.Mlango wa
pembeni ya geti haukuwa
umefungwa akausukuma
ukafunguka. “Sasa ni zamu ya
ndani.Kama nje kulikuwa na
watu wengi kiasi hiki huku
ndani wanaweza kuwa zaidi ya
wale.Lakini hata wakiwa
wangapi nitapambana nao.Ni
heri nife wakati nikipambana
kumuokoa Olivia kuliko kukata
tamaa.Sijawahi kukata tamaa
katika maisha yangu” akawaza
Mathewna kujibanda katik
aukuta wa geti akaangaza kila
upande lakini hakumuona mtu
yeyote.
“Ndani kuko kimya kabisa
kunaonekana hakuna mtu yeyote” akawaza halafu akampa
Bravo maelekezo afanya kama
alivyofanya kule nje.Bravo
akatoka mbio huku
Mathewakiendelea kumfuatilia
nyuma kwa
tahadhari.Waliizunguka
nyumba ile na hakukuwa na
mtu yeyote.Mathewakarejea
katika mlango mkubwa wa
kuingilia ndani ya
nyumba,akakiminya kitasa
ulikuwa umefungwa.Akatoa
vitu Fulani katika begi lake na
kuchokonoa kitasa mlango
ukafunguka.Mathewakatoa nguo za Olivia katika begi lake
na kumuwekea Bravo puani
“Go find Olivia ! akasema
Mathewna kumruhusu Bravo
aingie ndani ya nyumba ile
Mathewakimfuata kwa
kunyata.Ndani Kulikuwa giza na
hakukuwa na dalili zozote za
mtu.Mathewaliendelea
kumfuata Bravo aliyemuongoza
kuelekea katika chumba Fulani
ambacho mlango wake ulikuwa
wazi.Bravo akaanza kunusa
chini kisha akakwaruza sakafu
“Olivia was here” akawaza
Mathew “She was here.Where is she
now?akajiuliza kisha
akakikagua kile chumba kwa
makini sana hakupata chochote
cha kumsaidia akatoka na
kuanza kuzunguka katika
vyumba vingine.Nyumba
ilikuwa tupu hakukuwa na kitu
chochote ndani
“Hakuna kitu chochote wala
dalili zozote za kuishi mtu ndani
ya nyumba hii lakini
inaonekana kuna shughuli
maalum inayofanyika humu
ndani.Inaonekana kulikuwa na
mitambo au kompyuta humu ila zimeondolewa tena inaonekna
zimeondolewa haraka haraka
kwani kwani kuna baadhi ya
vitu vidogo vidogo
wamevisahau.Who are these
people? Olivia alikuwemo ndani
ya nyumba hii wamempeleka
wapi?akajiuliza akiendelea
kuchunguza kile chumba
kilichokuwa na nyaya nyingi
zilizokatwa katwa.
“Mmoja wa wale jamaa
alifanikiwa kukimbia naamini
tayari amewapa taarifa
wenzake kwamba
wamevamiwa na yawezekana wako njiani wanakuja
kupambana nami.Ngoja
niondoke haraka kwani hakuna
kitu chochote humu ndani cha
kunisaidia” akawaza Mathewna
kumchukua Bravo wakatoka
haraka sana ndani ya ile
nyumba wakatembea kwa
haraka kuelekea mahala
walikoacha gari na kuondoka
“Bado swali kubwa
ninalojiuliza ni kuhusu watu
hawa ni akina nani? Kwa nini
wamemteka Olivia? Naamini
kabisa Olivia alikuwemo ndani
ya nyumba ile lakini ameondolewa,amepelekwa
wapi? Hali niliyoikuta ndani ya
ile nyumba inaonyesha kuna
shughuli Fulani ilikuwa
inafanyika mle ndani lakini
wahusika wake waliondoka
kwa haraka haraka. Kuna kila
dalili za kunithibitishia watu
wale waliondoka kwa haraka
sana na kuna baadhi ya vitu
wameviacha na vingine
walishindwa kuvifungua
ikawalazimu kuving’oa.Nini
kiliwakimbiza? akajiuliza
“Nje ya jumba lile nimeua
walinzi kumi na tatu na wote wakiwa na silaha, namshukuru
sana Bravo kwani ndiye
aliyenisaidia kuweza
kuwatambua na kuwaondoa
wale jamaa.Swali ninalojiuliza
ni kwamba ndani ya nyumba ile
hakukuwa na mtu au kitu
chochote cha maana kwa nini
watu kumi na nne wenye silaha
wazunguke kuilinda nyumba
isiyokuwa na kitu chochote
ndani yake? Mathewakaendelea
kujiuliza maswali
Alipita mahala alipoilipua
nguo ya umeme na kuyakuta
magari zaidi ya matano ya Tanesco na mawili ya polisi
wakiwa wamelizunguka eneo
lile wakifanya
uchunguzi,hakusimama
akaendelea na safari yake.
“Zoezi la kumtafuta Olivia
linazidi kuwa gumu lakini sikati
tamaa nitahakikisha ninafanya
kila linalowezekana hadi nipate
mahala
alikohamishiwa.Natakiwa pia
kumjulisha mama yake ambaye
naamini hivi sasa atakuwa
hajalala anasubiri simu
yangu.Mama yule aliniamini
sana hivyo lazima nimpe mrejesho na kumpa moyo
kwamba Olivia lazima
apatikana ingawa zoezi la
kumtafuta halitakuwa rahisi
kwani watu waliomteka nyara
ni watu wanaonekana
wamejiandaa vya kutosha na
baada ya wenzao kumi na tatu
kuuawa itafanya mapambano
ya kumpata Olivia yawe
magumu zaidi” akawaza
Mathewna kusimamisha gari
pembeni ya barabara akawasha
simu yake akazitafuta namba za
Lucy Themba mama yake Olivia akampigia na simu ikapokelewa
haraka haraka
“Mathewnashukuru sana
umepiga baba.Nimekutafuta
sana katika namba uliyonipa
lakini haikuwa
ikipatikana.Nilitaka
nikushukuru kwa kazi kubwa
uliyoifanya mwanangu”
akasema Lucy na
Mathewakapatwa na mshangao
“Nlikuwa nimezima simu
mama nimeiwasha sasa hivi
kwa ajili ya kukupa mrejesho
wa ile kazi niliyokuja
kuifanya”akasema Mathew “Pole sana baba.Mzee tayari
amefika hapo? Akauliza Lucy na
Mathewakastuka akaitoa simu
sikioni akatazama jina la
aliyempigia liliandikwa Lucy
Themba.Alihisi amekosea
namba
“Mathew”akaita Lucy
“Mama samahani,mzee yupi
unamzungumzia?
“Namzungumzia Agrey
baba yake Olivia.Amekwisha
fika mahala hapo
ulipomuelekeza
akufuate?akauliza Lucy “Mama
sielewi.Nimemuelekeza Agrey
anifuate wapi?akauliza Mathew
“Mathewsi umempigia simu
Agrey muda si mrefu na
kumueleza kwamba
umefanikiwa kumpata Olivia
lakini hali yake si nzuri na
wewe umejeruhiwa kwa risasi
ukamuelekeza mahala ulipo ili
akufuate?Nataka kujua kama
tayari amekwisha fika mahala
ulipomuelekeza akufuate”
akasema Lucy.
“Mama sielewi
unazungumza jambo gani.Simu yangu niliizima na baada ya
kuiwasha mtu wa kwanza
kukupigia ni wewe.Nimekupigia
kukujulisha kwamba nimetoka
mahala ambako niliamini
alikuwepo Olivia nimefanikiwa
kuingia ndani ya nyumba hiyo
lakini Olivia sijamkuta ila kuna
kila dalili kwamba Olivia
alikuwemo ndani ya ile nyumba
na akahamishwa.Mama kwa
ufupi ni kwamba sijafanikiwa
kumpata Olivia lakini si mwisho
wa uchunguzi bado ninaendelea
na operesheni hii hadi nihakikishe Olivia amepatikana”
akasema Mathew
“Mathewunasema
hujampata Olivia?! Akauliza
Lucy Themba huku akihema
haraka haraka
“Ndiyo mama sijafanikiwa
kumpata lakini bado
ninaendelea na uchunguzi
wangu.Alikuwemo katika
nyumba ile ambayo programu
yangu ilinionyesha lakini
ameondolewa na sijui
amepelekwa wapi”
“Mungu wangu ! akasema
Lucy “Mama ulisema kuna mtu
aliwapigia simu akijifanya ni
mimi na kuwaeleza kwamba
Olivia
amepatikana?Mathewakauliza
“Mathewumenichanganya.
Ninahisi moyo wangu unataka
kupasuka kwa mstuko”
akasema Lucy
“Mama nieleze tafadhali
nini hasa kimetokea?akauliza
Mathew
“Kuna mtu amempigia simu
Agrey usiku huu kwa kutumia
namba nyingine tofauti na hii
akajitambulisha kwamba yeye ni Mathewna akadai kwamba
amefanikiwa kumpata Olivia
lakini amejeruhiwa kwa risasi
akamtaka Agrey amfuate mara
moja mahala alipomuelekeza ili
awapeleke hospitali.Hatukuwa
na shaka yoyote kuwa ni wewe
kwani mtu huyo alizungumza
akiwa katika hali ya maumivu
makali na tuliamini kwamba ni
wewe umejeruhiwa.Agrey
alitoka na
kukufuata.Nimeishiwa nguvu
kusikia kwamba si wewe
uliyepiga simu”
“My God ! akasema Mathew “Mimi sikupiga simu hiyo
mama na wala sina namba za
simu za mzee Agrey.Mama
naomba usihamaki
tunachotakiwa kufanya ni
kumzuia haraka sana mzee
asiende huko mahala
anakoelekea kwani anakwenda
katika hatari kubwa.Naomba
umpigie simu na umtake ageuze
haraka sana asiende huko
alikoelekezwa” akasema
Mathewna Lucy akaisubirisha
simu yake akampigia simu
Agrey lakini simu yake haikuwa
ikipatikana “Mathewsimu yake
haipatikani tena” akasema Lucy
akianza kulia.Mathewakahisi
miguu inamtetemeka
akaegemea kiti na kuvuta pumzi
ndefu.
“Mambo yanazidi kuwa
magumu” akawaza
“Mathewnitafanya nini
mimi?akauliza Lucy
“Mama huyo jamaa
alimuelekeza Agrey amkute
wapi?
“Alimuelekeza aende mtaa
wa Msanzi mbele kidogo ya
jengo la Zawama Saccos kuna jengo la ghorofa halijamaliziwa
kujengwa akamtaka wakutane
hapo”
“Mama ninakwenda hapo
sasa hivi.Ngoja nijaribu
kumuwahi kabla hajafika hapo”
akasema Mathewna kuwasha
gari akaingia barabarani
“Mathewtafadhali naomba
uhakikishe unampata
Agrey.Hakikisha haingii katika
tatizo lolote” akasema Lucy
huku akilia
“Mama nitafanya kila
niwezalo lakini nitakuomba
suala hili usimueleze mtu yeyote hadi nitakapompata
Agrey na kumfahamu mtu huyo
aliyewapigia simu.Hata hivyo
mama kuna kitu nataka
kukifahamu.Kuna mtu yeyote
ambaye mlimueleza kuhusu
mimi kwenda kumtafuta Olivia?
“Hakuna mtu tuliyemueleza
baba ndiyo maana ulipopiga ile
simu moja kwa moja tukaamini
ni wewe” akajibu Lucy
“Sawa mama nitawasiliana
nawe baadae” akasema
Mathewna kukata simu
“Ni nani aliyempigia simu
Agrey Themba akajifanya nini mimi? Lazima ni mtu
aliyefahamu kuwa nimekwenda
kumtafuta Olivia.Lucy anakataa
kwamba hawajamueleza mtu
yeyote kuhusu suala hili la mimi
kwenda kumtafuta Olivia sasa
mtu huyo amefahamu vipi kama
nimekwenda kumtafuta
Olivia?akajiuliza
“Mtu pekee ambaye
nilimueleza kuhusu mpango
wangu ni Tino ambaye
nilichukua silaha kwake.Tino
ninamfahamu sana hawezi
akafanya kitu kama
hiki.Mwingine aliyefahamu kuhusu operesheni hii ni
Ruby.Yule ni mwenzangu na
hawezi akatoa siri zangu.Huyu
mtu aliyepiga simu amefahamu
vipi kama nimekwenda
kumuokoa Olivia?Nini hasa
lengo la kumpigia Agrey
Themba na kumtaka amfuate
mahala hapo alipomuelekeza?
Mathewakajiuliza maswali
ambayo alishindwa kuyapatia
majibu
“Lucy hataki kuniambia
ukweli lakini lazima kuna mtu
wamemueleza kuhusu mpango
wangu wa kwenda kumuokoa Olivia.Ninaanza kupata picha
kwamba kuna mtu wa karibu
sana na familia ya Agrey
Themba ambaye anahusika na
tukio la kutekwa Olivia.Mtu
huyo lazima atakuwa
anawasiliana na watekaji na
kuwapa taarifa zote anazozipata
kutoka kwa akina
Agrey.Ninahisi kwamba hata
kitendo cha Olivia kuhamishwa
mtu huyo n diye aliyewapa
taarifa watekaji kwamba
ninafahamu mahala alipo Olivia
na ninakwenda kumuokoa
hivyo ndiyo maana wakamuondoa haraka sana
katika ile nyumba” akawaza na
kuongeza mwendo wa gari
“Sasa nimepata majibu kwa
nini nyumba ile tupu ilikuwa
inalindwa na watu kumi na nne
wenye silaha.Ulikuwa ni
mtego.Walijua lazima
nitakwenda pale hivyo
wakajipanga kunisubiri lakini
kwa bahati mbaya kwao mimi
ninazo mbinu nyingi zaidi
yao.Hii ni hatua kubwa sana
nimeipiga katika kufahamu
mahala alipo Olivia na
ninaamini nimekaribia sana kumpata.Nikimfahamu mtu
ambaye walimueleza kuhusu
mpango wangu wa kwenda
kumuokoa Olivia tutakuwa
tumempata Olivia.Ngoja
kwanza nifike mahala ambapo
wamemuelekeza Agrey
aende.Naomba nimuwahi kabla
hajafika mahala hapo kwani
naamini lengo lao kumtaka
aende hapo ni kumuua au
kuteka.Watu hawa ni
wataalamu sana wamejipanga
vizuri na wanahakikisha hakuna
kikwazo chochote kinajitokeza
katika kukamilisha mipango
 
SIRI
PART 1: SEASON 4
MTUNZI: PATRICK CK
Swali ambalo mpaka sasa
sijalipatia majibu nini sababu ya
kumteka Olivia? Ni pesa au
kuna sababu
nyingine?akajiuliza Mathew
“Majibu yatapatikana baada
ya kumpata Olivia.Usiku huu
lazima nikaonane na Lucy
nikazungumze naye anieleze
kama kuna mtu yeyote
waliyempa taarifa zangu”
akawaza Mathew
***************
Kaiza akiwa na wataalamu
wa kompyua wa idara yao
wakiwa katika zoezi la kufunga
mfumo mpya wa mawasiliano
baada ya kuuondoa mfumo wa
zamani ambao uliingiwa na
kirusi hatari
ukajifunga,alipigiwa
simu.Mpigaji alikua ni Zakaria
mmoja wa watu walio katika
kikosi kilichokwenda kulinda
kitalu 7 mahala ambako Olivia
alihifadhiwa awali
“Hallo Zakaria”akasema
Kaiza
“Kaiza..!! akasema yule
jamaa akihema kwa kasi
“Zakaria nini
kimetokea?Hebu tulia nieleze
nini kimetokea” akasema Kaiza
“Kaiza tumevamiwa na
watu wasiojulikana na
wenzangu wameuawa”
“Unasema?!! Akauliza Kaiza
kwa mstuko
“Tumevamiwa na watu
wasiojulikana wenzangu
wameuawa”
Ukimya ukapita
“Zakaria hebu nieleze
taratibu nini hasa
kimetokea?Nani
wamewavamia?
“Tulikuwa tumejipanga
tukiendelea na ulinzi lakini
ghafla nikasikia kama
mwenzangu mmoja
anagugumia maumivu nikatoka
eneo langu na kwenda kujua
kilichomsibu nikamulika tochi
na kumkuta akiwa amepigwa
risasi na wengine wanne wote
wakiwa wamekufa
tayari.Nikakimbia huku na mimi
nikikoswa na risasi”
“Zakaria wait…Nani..ah I
mean…” Kaiza akababika.Alihisi
mwili kumtetemeka
“Kwa sasa uko wapi
Zakaria?Kaiza akauliza
“Nimekimbia
nimejificha.Naomba msaada
tafadhali”akasema Zakaria
“Zakaria endelea kukaa
mahala hapo hapo ulipo
nitawasiliana nawe baada ya
muda mfupi” akasema Kaiza na
kukata simu akashusha pumzi
Kaiza aliingiwa na hofu
kubwa akampigia simu Devotha
“Kaiza zoezi linakwendaje
hapo?Muda gani mfumo mpya
utakamilika?akauliza Devotha
“Devotha kuna tatizo
kubwa”
“Tatizo gani Kaiza?
“P3 Unit wamevamiwa”
“Wamevamiwa?
“Ndiyo wamevamiwa na
watu wasiojulikana.Nimepigiwa
simu na Zakaria muda mfupi
uliopita akanipa taarifa
hizo.kwa macho yake
ameshuhudia watu watano
wakiwa wameuawa” akasema
Kaiza
“MathewMulumbi”
akasema Devotha
“MathewMulumbi ni nani?
Kaiza akauliza
“Tutazungumza baadae
Kaiza kwa sasa tujielekeze
katika kusaidia watu
wetu”akasema Devotha
“Inaonekana wavamizi
wamekwenda na nguvu kubwa
ndiyo maana wakafanikiwa
kuwavamia watu wetu na
kuwazidi nguvu hivyo basi
tunatakiwa kutuma nguvu
kubwa kwenda kutoa msaada
wa haraka sana” akasema Kaiza
“Kaiza hatuwezi kutuma
kikosi kingine kikubwa kwa
haraka bila kujua
kinachoendelea kitalu 7.Chukua
watu watatu muende kitalu 7
mfanye uchunguzi ili tupate
picha halisi ya nini kimetokea
na tujue hatua zipi
tuzichukue.Yawezekana huo
aliyepiga simu ameshikiliwa
mateka na wavamizi hivyo
tukipeleka watu wetu wengine
wanaweza wakavamiwa na
kuuawa.Nataka ripoti ya kutoka
kitalu 7 haraka hivyo achana na
kila kitu unachokifanya sasa
uende kitalu 7” akasema
Devotha.
Kaiza alihisi
kuchanganyikiwa.Aliingiwa na
woga mwingi.
“Kwenda kitalu 7 ni
kujipeleka katika hatari
kubwa.Nimemsikia Devotha
akitaja jina la MathewMulumbi
ni nani?Yawezekana akawa
ndiye mvamizi?akajiuliza Kaiza
akachukua watu watatu kama
alivyoelekezwa wakaondoka
kuelekea kitalu 7.
Devotha alipomaliza
kuzungumza na Kaiza simuni
akampigia Denis
“Denis nipe ripoti.Mambo
yanakwendaje huko?
“Madam kazi imekamilika
na hivi sasa tuko njiani
tunarejea”
“Hakukuwa na tatizo
lolote?akauliza Devotha
“Hakukuwa na tatizo lolote
madam.Agrey alikuja peke yake
kama tulivyomuelekeza”
akajibu Denis
“Good job Denis” akasema
Devotha na kukata simu
“Agrey Themba tayari
tunaye mikononi mwetu.Nina
hakika Olivia lazima atafunguka
kila kitu atakapojua kwamba
baba yake tunaye.Kwa sasa
nguvu kubwa inaelekezwa kwa
MathewMulumbi. Anaonekana
ni mtu hatari sana.Anapaswa
apatikane haraka vinginevyo
ataharibu kila kitu.Ilikuwa
vyema tuliwahi kumuondoa
Olivia pale kitalu 7 kwani
tusingefanya hivyo angeweza
kumuokoa” akawaza Devotha
ambaye naye macho yake
yalionyesha woga kufuatia
taarifa zile za watu wake
kuvamiwa na kuuawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom