sehemu ya nane
Nikajaribu kufyatua tena lakini nilikuwa nimeishiwa tena risasi na hapo nikafanya hima kushuka juu ya mti ule nakuanza kukimbia lakini kumbe nilionekana na hapo zikafuata risasi nyingi nyuma yangu lakini zote zilinikosa na hivyo kuniacha nikiwa huru na nikazidi kuchanja mbuga katikati yam situ ule mnene wenye nyoka wa ajabu kabisa kupata kutokea duniani.
Nilizidi kusonga mbele huku nyuma nikiwasikia wale askari nao wakizidi kojongea kunifuata na mimisikutaka kujisalimisha kwao na kamaningefanya hivyo ina maana ningelikufa kabla sijafanya kile kilichonipeleka Burundi.
Mbio zangu na begi langu mgongoni zilinifikisha hadi karibu na mbuga ya majani marefu na mbele hakukuwa na miti wala vichaka na kwa mbali nikaanza kuona wanyama wakiwa kwenye ile mbuga na hapo nikajua sasa nipo kwenye mbuga ya wanyama Iyumbi.
Sikuwa na namna ilibidi tu nikimbie kuingia katikati ya majani yale marefu na humo nikaanza kutambaa kama nyoka huku kwa mbali nikiwasikia wale askari wa hifadhi ile wakija huku wakipiga makelele ya kushangilia harakati zao.
Nikiwa sasa nipo umbali wa kutosha nikasimama katikati ya majani yale huku nikijaribu kutazama kule nilikotokea na hapo nikawaona wale askari wakijaribu kujongea kunifuata kupitia yale malalio ya nyasi walioyaona,nikarudi pale ili niendelee na safari yangu lakini sikufanikiwa japo kutambaa hata hatua moja nikasikia sauti ya mnyama mbele yangu na sauti hii haikuwa ngeni masikioni kwangu.
“simba” nikajisemea
Nikaanza kuwaza nifanye nini ikiwa nyuma kuna adui nambele kuna kubwa la maadui,lakini hapo nikatafakari vile simba dume anavyolinda himaya yake kwa hiyo hapa nipo ndani ya ufalme wa simba na tayari ameshagundua nipo hapa karibu.
Nikiwa hapo hapo nimetulia tuli nikasikia kitu kikijongea kulia kwangu na nilipotazama uso kwa uso na mtoto wa simba na hapo nikajua kabisa familia nzima ya kiumbe yule ipo hapa mbugani na hapa wanafundishwa namna ya kuwinda na bahati mbaya nipo kwenye macho ya motto mmoja asietaka kudharauliwa mbele ya wenzie na yupo tayari kunijeruhi.
Nikapeleka mkono kiunoni kwangu na hapo nikaambulia patupu kisu hakikuwepo na nikakumbuka sikukiweka tangu kulipokucha na hata mkononi sikuwa na kitu chochote kile ikabidi nitumie zaidi akili na si nguvu.
Nikamtazama tena kisha nikawa kama namtisha hivi na kweli katishika lakini alip9iga ukunga na hapo nikatambua kabisa ya kuwa ametoa tahadhari kwa baba yake au mama na kweli nikaaznza kusikia kwa mbali vile alivyokuwa akikimbia kuja usawa wa pale tulipo huku akitoa muungurumo wa kutisha.
Nikaona isiwe tabu nikaamua kugeuka nirudi huko waliko hao askari wa hifadhi yani ni bora kufa kwa risasi kuliko kuraruriwa na simba wale wenye gadhabu.
Nikaanza kukimbia katikati ya majani yale marefu huku nyuma nikisikia kishindo cha simba dume kikifuata nyuma yangu.
“usitazame nyuma kama adui unaemhofia zaidi yupo karibu yako” nikakukmbuka kauli ya mkufunzi wangu wakati tukiwa katika mafunzo ya awali kabisa ya ukuruti pale Makutupora Dodoma.
Mbele yangu walikuwepo wale askari wakizidi kuijaribu shabaha yao kuelekea kwangunamimi nilijitahidi kuzikwepa zile risasi kadri nilivyoweza, nilikuwa nakimbia kama kangaraoo nakimbia nikiwa nimeinama kisha nasimama kuona umbali nilipo na askari wale.
Sijui kwanini hawakujua ninachokimbia huko nyuma wao wakazidi kunifuata huku wakijaribu kurusha risasi zao na kila pahali mbugani pale pakawa panasikika sauti za bunduki tu huku mimi nikizidi kukimbia kama kware kwenye yale majani marefu na hatua kama hamsini nyuma alikuwepo kubwa la maadui.
Askari wale walipokuja kugundua ninachokimbia na wao wakaanza kuhaha namna ya kumdhibiti mnyama yule kwanza hivyo wakaanza kurudi kule walipotokea huku sasa mimi nikiwa nyuma yao na simba akiwa nyuma yangu.
Nilikuwa namafunzo ya kukimbia maeneo kama yale hivyo sikupata tabu kuwapita askari wale na kisha kuwaachia msala ule askari wale wavivu walioniita mwanaharamu na hapo nikataka kuwaonesha kweli mwana haramu,nilpowapita nikawa usawa wa gari yao na pale nikamkuta yule askari alienipiga mtama akiwa anachukua bunduki maalumu ya kumshambulia simba yule na sikurtaka kumkawiza nikampitia kama upepo kisha nikasimama na kutazma askari waliokuwa wamezamia mle mbugani wanavyojaribu kupambana kukimbia ndani ya majani marefu,lakin kabla sijakaa sawa nikatandikwa ngumi shavuni kwangu nahapo nikajua yule askari mkorofi atakuwa kasimama baada yakuanguka wakati nimemshambulia.
Nikamtazama na hapo nikashudia alivyojipanga katika mtindo safi wa mapigo maarufu ya kule japani au maarufu huitwa karate,ila mimi nikaaamua kujipanga kwa mtindo wa moto kombati mtindo wa hapa Tanzania mtinndo unaojumuisha mapigano yote yawe kungfu au karate kisha nikapanga kutumia pigo lakombora yani anaepigwa harudi tena katika ulingo wa ngumi na hii tunafundishwa hasa pale unapokuwa unauhitaji wa kuwahi jambo na kuna mdudu anakuchelewesha.
Akaanza kushambulia yeye lakini ni ngumi mbili tu zilizotupwa nay eye na yatatu ikajaa mkononi mwangu na hapo nikamvuta upande wangu kwa kasi kisha nikaachia ngumi matata ikatua katikati ya paji la uso wake kisha nikamwachia na kumwacha kipepesuka huku nikijua kabisa ubongo wake umepata mtikisiko wa haja.
PASAKA NJEMA WAPENDWA
Asalaaam Kudo