RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
SAUTI YA MTUTU
(MTAZIKA KILA IKISIKIKA)

Na BAHATI MWAMBA
0758573660,0624155629


Bunduki yangu ilikuwa imeisha risasi na kitu pekee nilichokuwa nakitegemea ni hatua za miguu yangu japo maungio ya magoti yalianza kugoma kunipa ushirikiano.

Mvua kubwa ilikuwa bado inazidi kunyesha,sikuwa mnaona mbele wala sikuwa naona nyuma na mara chache sana nilijikuta nikitamani sana radi ipige tena ili niweze kuona mbele na wale waliokua wakinikimbiza nyuma niweze kuwakwepa.

Kracha,kacha..mlio huu ulizidi kunidhirishia ya kuwa sikuwa japo nimefanikiwa kubakiza risasi hata moja kwenye bunduki yangu niliopenda tangu nifahamu aina za bunduki hii ilikuwa bora kwangu,niliweza kuimudu vyema ilkuwa ni AK 12 bunduki ya kirusi na sio zao la nchi za kisoviet hii ilikuwa imetengenezwa Urusi kwa ubora ulio zaidi yah ii ya AK 47 iliozoeleka kwa wengi.

Nikatazama nyuma tena ila sikufanikiwa kuwaon wale watu walioanza kunikimbiza tangu nilipouvuka mto Iyumbi,mto ulioko karibu kabisa na mpaka wa Kigoma na Burundi na sasa ilikuwa yapata masaa matatu tangu nianze serekasereka ya kukimbizana na watu hawa ambao sikujua dhamira yao kwangu ni nini na kwanini waliamua kupambana na mimi na kila dakika walikuwa wanazidi kunisogelea na hata nilipo jaribu kutengeneza mazingira ya kuwakwepa bado walionesha umahiri wao katika misitu ile yam to Iyumbi.

“wanaujua msitu huu vyema” ndivyo nilivojiambia katika akili yangu na hapo nikapanga kufanya jambo ambalo naamini lingewachanganya na kuwaacha wakiwa hawajui nimeelekea wapi.

Nikasimama na kutumia hisia za mlango wa nane kuhisi umbali wa watu wale hadi kunifikia na hapo nikatuliza kabisa akili yangu,sikutaka kuisikia ile sauti ya matone ya mvua na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi ya ajabu usiku ule.

Kwa mbali nikaisikia sauti ya miguu ya watu zaidi ya ishirini ikikimbia kwa pamoja lakini haikuwa sauti ya miguu ya watu tu kulikuwa naziada ya miguu ya mnyama,ndio ilikuwa ni mnyama na hapo nikatambua watakuwa ni mbwa waliofunzwa na hapo nikapata jibu kwanini walidumu wakati wananikimbiza watu hawa.

Nikainama na kuvua kiatu kimoja na kubaki na soksi iliokuwa imelowa maji chapachapa nikaitupa juu ya mti ulikuwa mbele yangu hatua kadhaa na kweli ikakubali kukaa juu ya tawi moja,nilipokwisha kuhakikisha imekaa kule juu nikavaa kiatu kile kasha nikaanza kulekea kulia kwangu huku mguu mmoja ukiwa upo chini na mmoja nimeuning’iniza juu, na mikono yangu ikifanya kazi ya kuyapangua majani yaliokuwa yamefungamana na kulala chini,bunduki yangu ilikuwa ipo mgongoni ikibembea huku na huko.

Nilipotembea usawa wa mita kadhaa nikaushusha mguu ule kisha nikavua tena mguu mwingine na kutoa soksi nyingine kisha nikavaa na hpo nikaanza tena kutembea kwa kutumia mguu mmoja na kwenda kuitupa ile soksi chini ya majani kisha nikaanza tena kurudi kule nilikovulia soksi ya kwanza.

Sauti ya mbwa kubweka ilikuwa inazidi kunikaribia na hapo nikaliokota begi langu na kuliweka mgongoni huku bunduki yangu nikiihamishia kifuani mwangu kisha nikaanza tena kukimbia kwenda mbele huku nikijaribu kuona kama chenga yangu itakuwa imefanya kazi.

nilienda umbali mrefu huku nikiamini kabisa wale watu waliokuwa wakinikimbiza huku wakinirushia risasi watakuwa wamekosa mwelekeo wangu,lakini mvua ilikuwa bado inazidi kunyesha huku nikijaribu kubashiri muda huo utakuwa saa ngapi nilipojaribu kukadiria nikahisi itakuwa inaelekea saa tano za usiku na mimi sikutaka kutulia sehemu moja ili nipumzike nilihitaji kwenda mbali ili kujihakikishia usalama wangu.

*******

Yalikuwa yamepita masaa kama matatu hivi tangu nipande juu ya mti huu huku nikipumua kwa pumzi za kawaida baada ya kujitahidi kuzua zile pumzi za mchoko ziniathiri katika mwili wangu,usiku nao ulikuwa unazidi kuwa mkubwa na nilikadiria itakuwa inaelekea saaa tisa kasoro hivi na nilikuwa sijapata kitu tumboni na nilisikia tumbo likiunguruma kwa kukosa haki yake.

Nikajitikisa kidogo na nikapata egemeo zuri kisha nikalitoa begi langu mgongoni na nikaliweka karibu ya uso wangu na nikalifungua na hapo mkono wangu ukatoka na vipande vitatu vya mkate,nikalifunga lile begin a kuanza kuvifakamia viapnde vile ndani ya dakika moja tu nikawa nimemaliza kuvitia tumboni,kisha nikajipapasa kiunoni mwangu nahapo nikagusa kibuyu cha maji nilichokuwa nimekifunga kiunoni mwangu,nikanywa maji funda kadhaa lengo likiw ni kuacha mwili wangu huru bila kuupa uzito na hii ni kanuni ya mwanajeshi anapokuwa katika ulingo wa vita.

Nikiwa najaribu kutafakari mwenendo wa maisha yangu nikasikia ule mti ukitikisika,mwanzo nilijua ni ule upepo wa kufukuza mvua ulikuwa ukiyumbisha miti,laini kadri muda ulivyokuwa ukienda nilihisi ule mtikisiko sio wa upepo kuna kitu cha zaidi ya kile nilichokiwaza.

Mwanga mkali wa radi ukamulika na hapo nikapata kuona kile nilichokuwa nakihisi,nilipata kushuhudia macho kama ya paka yaking’aa kwa kunitizama mimi,kisha kukafuatiwa na muungurumo mkali wa kiumbe Yule aliekuwa akinitizama.

Damu yangu ilichemka kutokana na hatari ile na hapo nikaupa mwili wangu utayari wa kukabiliana na mnyama Yule amabae sikumuona ila niliamini ni chui au mnyama wa aina hiyo.


asalaam Kudo
 
sehemu ya pili
na BAHATI MWAMBA
0758573660

Nilikaza macho yangu ili niweze angalau kuona hata mjongeo wa mnyama yule huku mkono wangu ukijaribu kusogea kilipo kisu change nilichokuwa nakitegemea kama silaha ya mwisho kwangu maana bunduki iliisha risasi.

Mnyama yule alizidi kuunguruma huku mimi nikiwa nimetulia palepale bila hata kujitikisa maana mkufunzi wangu alinambia wakati kama huu adui yako hata kama ni paka usijaribu kumpa mafanikio kwa kutikisa hata ukope wako maana kwa kufanya hivyo unampa hesabu nzuri za kukushambulia.

Mkono wangu wa kushoto ulifanikiwa kutoka na kisu huku akili yangu ikipiga hesabu za kumtoka mnyama yule maana nilijua shambulio lake kuu anategemea kunirukia.

Nikatazama chini nikaona umbali nilipo hadi chini usingeweza kunipa madhara makubwa, lakini sikutaka kuruka kwenda chini ila nilitaka kupiga hesabu ambazo ni hatari kwangu lakini nikifanikiwa kuzitimiza basi yule mnyama angeambulia maumivu yeye.

Nikapanga kumhadaa,nikatikisa mgongo na begi likacheza,yule mnyama alipoona natikisika akajua nataka kukimbia hivyo nikaona akijongea kwa kasi kunifuata,aliponikaribia kama mita tatu kutoka nilipo, nikautumia mkono wa kulia kuushika mtawi ule niliokuwa nimekalia huku mwili wangu ukiwa kama unataka kujirusha chini lakini sikufanya hivyo nikaupinda mgongo wangu kuja juu mana hapo tumbo likarudi ndani huku miguu ikipanda kuelekea juu,nilipofanya vile nikasikia kwa mbali upepo mkali ukinipita karibu na makalio yangu na hapo nikapata kushudia yule mnyama akienda chini huku akilia kwa manunguniko ya kukosa windo lake.

Nikarudisha mkono wa kushoto usaidiane na mkono wa kulia kunisaidia kurudi juu ya mti ule.

Wakati nikikaa tu ya tawi la mti ule nikashuhudia tena kiumbe yule akipanda kwa kasi kunifuata juu ya mti ule,roho yangu ikajaa woga sasa na hapo nikaona nikizembea nitakufa ikiwa sijatimiza lengo langu la kwenda nchini Burundi.

Nikatumia nguvu zangu kujirusha chini kiufundi kabisa huku nikitanguliza visigino vya miguu yangu chini kisha sikutaka kuzembea macho yangu yakaelekea upande ule nlipokiona kiumbe kile kikijaribu kupanda tena juu ya mti na hapo nikakishuhudia kikijitupa kunielekea na hapo nikaupinda mgongo kuelekea nyuma huku miguu yangu ikiwa bado ipo chini na kiliponipita kwa juu nikageuka haraka na kisu changu mkononi lakini wakati nikijiandaaa kwa lolote nikakishudia kiumbe kile kikiwa kimezungukwa na joka kubwa mithili ya chatu lakini hakuwa chatu maana joka hili lilikuwa jembamba.

Nikajua yule nyoka alikuwa katika mawindo yake,nikapiga hatua kadhaa na kuanza tena kukimbia huku nikiacha yule mnyama akipambana kujiokoa kivyake na nilijua hataweza kufanikiwa maana alikuwa kakamatwa vibaya.

*******

Nilitembea kufuata kingo za kijito kidogo nilichokikuta msituni mle.

Nikazidi kuambaa na kingo zile huku nikijaribu kufuata usawa ule nilikoona kijito kile kinakotokea.

Kulikuwa kunaenda kupambazuka nab ado nguo zangu zilikuwa zimelowa maji japo ziliznza kukauka na mvua ilkuwa imekatika na anga lilikuwa linaonesha kushamiri wingu zito huku ngurumo za hapa na pale zikisikika na mara kadhaa mwanga wa radi ulinisaidia kuona mbele nialekeako.

Nilikuwa nimetembea kilomita kadhaa nab ado niliamini nina mwendo mrefu kufika karibu na makazi ya watu.

Wakati kunazidi kupambazuka nikawa nimefika kwenye kilima kilichokuwa kinatiririsha maji yale ayaliotengeneza mto ule niliokuwa naufuta.Nikajaribu kutazama kilima kile na kwa mbali nikaona kijia kiielekea ,kule kilimani, sikutaka kujichelesha katika kuwaza kijia kile nikaamua kukifuata.

Nikatembea katika kijia kile na kwa umakini wa hali ya juu huku nikijaribu kuisikia kila hatua yangu ili kusiwepo kuingilia harakati zangu.

Nilizidi kupita katiakati ya miti minene na mirefu ilikuwa juu ya kilima kile,nikazidi kusogea mbele huku na wakati nikijaribu kuanza kukishuka kilima kile ili niwe upande wa pili wa kule nilikotokea nikaona kwa mbali nyumba kadhaa zikiwa zimekaa katika mkao wa kambi.

Nikasimama ili nipate kutathimini eneo lile na hapo nikaikumbuka ramani ya nchi ya Burundi ilikuwa katika begi langu.Nikaitoa na kutazama nikaona hapo nilipo bado nipo kwenye pori la mto Iyumbi lakini ile kambi niliokuwa naiona na askari wa hifadhi ya wanyama ilio katika pori hilo la Iyombi lakini ilikuwa umbali wa kilomita kama kumi kutoka mto Iyombi ulipo,na kutoka hapo nilipo kulikuwa na njia ambayo kama ningeifuata basi ingenipeleka hadi nje kidogo ya pori lile na huko ningekutana barabara kuu ya kuingia bunjumbura.

Nikairudisha ramani ile kisha nikaendelea na safari huku nikiwa najaribu kujua jinsi gani nitaachana na njia ile itakayonipitisha kule kwenye ile kambi ya askari wa hifadhi ya wanyama.

Wakati natembea niakihisi harufu kali ikitoka katika mwili wangu na hapo nikajua ni mimi ninaenuka lakini hii harufu ni yakitu kilicho katika mwili wangu na si ya mwilini kwangu.

Nikajitazama usawa bega langu sikuona kitu lakini nikajaribu kujishika mgongoni na huko mkono wangu ukarudi na uteute uliokuwa ukitoa harufu kali ya kitu kuoza.

Nikageuka mwili mzima ili nitazame nyuma maana nilijua lazima hayo ni mate ya kiumbe kilicho nyuma yangu,nilitambua hili kwa sababu wakati tupo kuruti tulifundishwa hila za viumbe hatari wa msituni,na kama kanitemea mate maana ake anataka anifuate nyuma bila mimi kumpotea.

Wakati naangaza macho yangu kule nilikotokea nikasikia mti mmoja ukitikisika kwa nguvu na hapo sikuchelea kuona nyoka mrefu na mwembamba akiruka mti mmoja na kwenda mwingine na hapo nikajua nipo katika hatari nyingine zaidi ya huyu nyoka hatari ambae ni mara ya pili namuona na yawezekana hata katika viyabu hakuna nyoka wa aina hii amewahi kuandikwa.

ASALAAM KUDO
 
Nitamaliza hakuna sehemu itakayo baki

Afu KIKOSI CHA PILI

hujawahi kupita bila Shaka jaribu kupita na huko pia utaamini ninachokwambia mizigo yote itaisha
Hiyo story inanipa uvivu ilipofikia naona imefika mbali naona uvivu kuanza ndio mana hunioni
 
Mkuu kudo900 utatumaliza na AROSTO. Ungemaliza moja moja mkuu. Wapenzi wa RIWAYA zako tunapata shida....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom