RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

M
sasa kilichobaki nikukubaliana na ukweli tu ajiachie kwa kudo
Moneytalk ohoo acha hizo mambo bana huoni kama unaniharibia labda nilikuwa natka kukufuata pm huoni kma wanivunja moyo?

Au labda nilitaka kumtokea shunie dah acha hizo asee
 
sehemu ya tano

Nikaanza kukifuata kijia walichonielekeza huku nusu nikikimbia na nusu nikitembea,sikutaka kugeuka nyuma maana niliamini zaidi hisia zangu za mlango wa nane kuliko macho yangu.

Nilizidi kukimbia huku kwa nyuma nikizisikia kelele za wale askari wa wanyama pori wakija kwa kasi na hapo nikatambua walikuwa wapo juu ya gari yao na wengine walikuwa wanakimbia kwa miguu.

“usiende ule mwelekeo wa adui alie nyuma yako” nikayakumbuka maaelekezo ya mkufunzi wangu jeshini.Unashangaa Albino kuwa jeshi nitakwambia huko mbele kwanini niliingia jeshi.

Nikasimama na kuweka sikio moja ardhini na hapo nikapata kuusikia muungurumo wa gari ukija usawa wa njia niliopita lakini miguu ya watu niliisikia ikihama kuelekea kulia mwa njia ile niliopita.Nikasimama na kutazma huko kulia nikaona hakuna pori nene kama huku kushoto na hapo nikajua kwanini walielekea kule.

Nikabidi kucheza na hisia za watu wale walioaamini nitapita kulia ili niwahi kufika barabara kuu,nikakata shauri kuelekea kushoto kuliko na pori nene na bila kusita nikaanza kufuata vijia vyembamba na ambavyo bila shaka vilikuwa vinapitwa na wanyama wa msitu ule.

Ni wakati nilipohisi nipo salama upande huo lakini kumbe kuna macho ya watu yalikuwa yakinitizama na sikufika mabli sana risasi ikalia karibu na kichwa change nahapo nikajua nimekoswa na mtu anaeniona na atakuwa kwenye miti ile mirefu kajificha ikabidi nianze kukimbia huku nikiitumia miti kama nago yangu huku nikijaribu kuwaza uapande atakaokuwa yule mtu na kama kaniona ina maana atakuwa kawapa taarifa wenzie na mara moja wataanza kunifuata.

Paah!! Risasi nyingine ikasikika nakuja kuchimba kwenye mti nilikuwa nimejikinga,lakini mlio huu ulitanipa taarifa ya kuwa mtutu uliotumika hapa si wa kudungulia ni mtu alie na sub machine gun mkononi na ilivolia nikajua kabisa mpigaji alikuwa anakimbia na hivyo muda huo baada ya kunikosa atakuwa anatembea kwa tahadhari kubwa kuja nilipo.

Nikatazama juu ya mti ule niliojificha nikaona itanichukua dakika si zaidi ya moja kufika juu kabisa na hapo mtu yule atakuwa kaniona na kunifanyia shambulizi,nikautazama tena mti ule na hapo nikajiridhisha na unenen wake.

Nikaliacha begi langu chini kisha nikatumia njia ya nyani kukwea mti hii nilifundishwa na mlezi wangu aliekuwa ni komando wa daraja la juu ncini Tanzania,isha nikawa kama kima anavyoning’inia awapo kwenye shina la mti hivyo sikuwa nimempa nafasi adui yule ya kuniona nilipo.

Haukupita muda nikaona askari yule akiwa chini analitazama begi langu katika namna ya kushangaa na mimi sikutaka kumchelewesha nikaruka kutoka juu katika namna ya kupenedeza japo wewe ukijaribu uaneza ishia vunja kiuno,na nilipofika chini tayari mikono yangu ilikuwa imeidaka shingo yake huku miguu ikikita chini na muda mfupi uliofuata hakuwa katika idadi ya waliohai askari yule.

Nikaikota silaha yake aina ya micro sub machine gun ya kichina na nilipoibeba mikoni mwangu nikaikadiria risasi zake bila kutoa magazine yake na niliona kabisa uzito wake utakuwa 3.68 na hii ilimanisha tayari ilikuwa imeshatema risasi kama kumi natano hivi na zilisalia kumi na mbili.

Nikampekuwa tena hakuwa nacha zaidi tena na nilipotazama angani nagalau tayari jua lilikuwa limeanza kutoa mwangaza wa mionzi ya kuleta joto.

Wakati nikirudisha macho yangu chini ili nichukue begi langu nikaona mi mfupi mbele yangu ukicheza katika namna ya kuficha kitu,nilitaka kusema labda ni wale nyoka tena lakini haikuwa hivyo yule alikuwa ni mtu tena alieenda pale ndani ya dakika chache zilizopita naalikuwa anajaribu kuniweka katika windo.

Nikaokota begi langu kwa mkono wa kushoto na kuhama pale katika kasi ya kukwepa mshale na bunduki niliochukua kutoka kwa mtu yule ikiwa mikononi mwangu.

Ilikuwa ni kutoka mti mmoja hadi mwingine huku nikijaribu kwenda kinyume na akili za mtu yule nilie amaini yupo kwenye kile kichaka,nikaufikia mti mmoja mnene na kujibanza pale na kisha nikaanza kuchungulia upande ule kwa chati ya akudoakudo yaani natoa kichwa kwa kutanguliza zaidi jicho moja kuliko kichwa kizima na sikukawia kumwona mtu yule nae akihama upande ule ili aelekee kwenye kichaka kingine kilichokuwa karibu.

Sikutaka kumkawiza maana tayari akili yangu ilikuwa inahesabu kifo tu kutoka kwa watu wanaonidharau kabisa kila kukicha kisa mimi ni Albino.

Nikaachia risasi yangu katika shabaha ya ajabu kabisa na kabla hata hajisitiri kwenye kile kichaka tayari risasi ilishamfikia na kumtupa juu na alipodondoka chini hakuwa na uhai tena.

Nikataka kuanza kugeuka ili nianze kukimbia kusonga mbele lakini akili yangu ikanasa tukio kutoka kwa mtu yule niliempiga risasi,hakuwa amevaa sare zile za kijani kama sakri wale wa wanyama pori na hapo ikabidi nicheze na roho yangu ikabidi nirudi kwa kasi eneo lile alipodondokea na nilipofika kweli mtu yule hakuwa maevaa sare zile ila laivaa sare kama za watu wale waliokuwa wananikimbiza jana yake wakati nilipokuwa nikiuvuka mto Iyumbi.

Mtu huyu alikuwa amefunika uso wake kwa vitambaa vipana au skafu katika lugha ya wengi.ikanilizamu nimfunue na hapo nikapigwa na butwaa mtu yule alikuwa na asili ya kisomali,nikataka kumpekuwa zaidi lakini tayari nilikuwa nimelisikia lile gari likizidi kusogea nilipokuwa ikabidi niachane nae kisha nikaiokota bunguki yake iliokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti na kuanza tena kukimbia kwenda mbele zaidi huku nikiamini kabisa wale askari watamuona mtu yule na hapo nilitaka kuhakikisha kama watu wale ni wamoja nikapanga kuukwewa mti mmoja mrefu utakaoniwezesha kuwaona watu wale,pindi wakimfikia mtu yule pale chini wataonesha jambo gani kati ya kushangaa na kuomboleza.

*******


asalaamu kudo
Ylikua unafata nini burundi au ulitaka ukacheze soka na Nkurunzinza
 
M

Moneytalk ohoo acha hizo mambo bana huoni kama unaniharibia labda nilikuwa natka kukufuata pm huoni kma wanivunja moyo?

Au labda nilitaka kumtokea shunie dah acha hizo asee
Mm tena uliyenifukuza nitoke na mgazeti wako ulioniandikia
 
Mm tena uliyenifukuza nitoke na mgazeti wako ulioniandikia
Eeeh ww ndie ulizingua bana na yule mwenzio

Lakini all in all ni maisha tu yanaendelea sometimes jokes,sometymes angry life go on na usawa huu wa mr kipara
 
M

Moneytalk ohoo acha hizo mambo bana huoni kama unaniharibia labda nilikuwa natka kukufuata pm huoni kma wanivunja moyo?

Au labda nilitaka kumtokea shunie dah acha hizo asee
[emoji47][emoji47][emoji47]kiruu yamekuwa hayo tena??daah nimeishiwa pozi acha nimuachie shunie
 
Kwani nikikufuata pm utakataa eti mmh
Eeeh ww ndie ulizingua bana na yule mwenzio

Lakini all in all ni maisha tu yanaendelea sometimes jokes,sometymes angry life go on na usawa huu wa mr kipara
Kuzingua kukwambia ukweli ndio mana sijataka kukujibu kwenye mgazeti wako nilijua tu utakuja ule sio utani ulimaanisha ulichoongea byeee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom