RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

Haya bana mvumilivu~~~~~~~
Chief majukumu ya hapa kazi tu ndo yanaleta yote haya afu njoo whatsapp kama vipi maana SEASON TWO
 
sehemu ya saba

Nikajaribu kufyatua tena lakini nilikuwa nimeishiwa tena risasi na hapo nikafanya hima kushuka juu ya mti ule nakuanza kukimbia lakini kumbe nilionekana na hapo zikafuata risasi nyingi nyuma yangu lakini zote zilinikosa na hivyo kuniacha nikiwa huru na nikazidi kuchanja mbuga katikati yam situ ule mnene wenye nyoka wa ajabu kabisa kupata kutokea duniani.

Nilizidi kusonga mbele huku nyuma nikiwasikia wale askari nao wakizidi kojongea kunifuata na mimisikutaka kujisalimisha kwao na kamaningefanya hivyo ina maana ningelikufa kabla sijafanya kile kilichonipeleka Burundi.

Mbio zangu na begi langu mgongoni zilinifikisha hadi karibu na mbuga ya majani marefu na mbele hakukuwa na miti wala vichaka na kwa mbali nikaanza kuona wanyama wakiwa kwenye ile mbuga na hapo nikajua sasa nipo kwenye mbuga ya wanyama Iyumbi.

Sikuwa na namna ilibidi tu nikimbie kuingia katikati ya majani yale marefu na humo nikaanza kutambaa kama nyoka huku kwa mbali nikiwasikia wale askari wa hifadhi ile wakija huku wakipiga makelele ya kushangilia harakati zao.

Nikiwa sasa nipo umbali wa kutosha nikasimama katikati ya majani yale huku nikijaribu kutazama kule nilikotokea na hapo nikawaona wale askari wakijaribu kujongea kunifuata kupitia yale malalio ya nyasi walioyaona,nikarudi pale ili niendelee na safari yangu lakini sikufanikiwa japo kutambaa hata hatua moja nikasikia sauti ya mnyama mbele yangu na sauti hii haikuwa ngeni masikioni kwangu.

“simba” nikajisemea

Nikaanza kuwaza nifanye nini ikiwa nyuma kuna adui nambele kuna kubwa la maadui,lakini hapo nikatafakari vile simba dume anavyolinda himaya yake kwa hiyo hapa nipo ndani ya ufalme wa simba na tayari ameshagundua nipo hapa karibu.

Nikiwa hapo hapo nimetulia tuli nikasikia kitu kikijongea kulia kwangu na nilipotazama uso kwa uso na mtoto wa simba na hapo nikajua kabisa familia nzima ya kiumbe yule ipo hapa mbugani na hapa wanafundishwa namna ya kuwinda na bahati mbaya nipo kwenye macho ya motto mmoja asietaka kudharauliwa mbele ya wenzie na yupo tayari kunijeruhi.

Nikapeleka mkono kiunoni kwangu na hapo nikaambulia patupu kisu hakikuwepo na nikakumbuka sikukiweka tangu kulipokucha na hata mkononi sikuwa na kitu chochote kile ikabidi nitumie zaidi akili na si nguvu.

Nikamtazama tena kisha nikawa kama namtisha hivi na kweli katishika lakini alip9iga ukunga na hapo nikatambua kabisa ya kuwa ametoa tahadhari kwa baba yake au mama na kweli nikaaznza kusikia kwa mbali vile alivyokuwa akikimbia kuja usawa wa pale tulipo huku akitoa muungurumo wa kutisha.

Nikaona isiwe tabu nikaamua kugeuka nirudi huko waliko hao askari wa hifadhi yani ni bora kufa kwa risasi kuliko kuraruriwa na simba wale wenye gadhabu.

Nikaanza kukimbia katikati ya majani yale marefu huku nyuma nikisikia kishindo cha simba dume kikifuata nyuma yangu.

“usitazame nyuma kama adui unaemhofia zaidi yupo karibu yako” nikakukmbuka kauli ya mkufunzi wangu wakati tukiwa katika mafunzo ya awali kabisa ya ukuruti pale Makutupora Dodoma.

Mbele yangu walikuwepo wale askari wakizidi kuijaribu shabaha yao kuelekea kwangunamimi nilijitahidi kuzikwepa zile risasi kadri nilivyoweza, nilikuwa nakimbia kama kangaraoo nakimbia nikiwa nimeinama kisha nasimama kuona umbali nilipo na askari wale.

Sijui kwanini hawakujua ninachokimbia huko nyuma wao wakazidi kunifuata huku wakijaribu kurusha risasi zao na kila pahali mbugani pale pakawa panasikika sauti za bunduki tu huku mimi nikizidi kukimbia kama kware kwenye yale majani marefu na hatua kama hamsini nyuma alikuwepo kubwa la maadui.

Askari wale walipokuja kugundua ninachokimbia na wao wakaanza kuhaha namna ya kumdhibiti mnyama yule kwanza hivyo wakaanza kurudi kule walipotokea huku sasa mimi nikiwa nyuma yao na simba akiwa nyuma yangu.

Nilikuwa namafunzo ya kukimbia maeneo kama yale hivyo sikupata tabu kuwapita askari wale na kisha kuwaachia msala ule askari wale wavivu walioniita mwanaharamu na hapo nikataka kuwaonesha kweli mwana haramu,nilpowapita nikawa usawa wa gari yao na pale nikamkuta yule askari alienipiga mtama akiwa anachukua bunduki maalumu ya kumshambulia simba yule na sikurtaka kumkawiza nikampitia kama upepo kisha nikasimama na kutazma askari waliokuwa wamezamia mle mbugani wanavyojaribu kupambana kukimbia ndani ya majani marefu,lakin kabla sijakaa sawa nikatandikwa ngumi shavuni kwangu nahapo nikajua yule askari mkorofi atakuwa kasimama baada yakuanguka wakati nimemshambulia.

Nikamtazama na hapo nikashudia alivyojipanga katika mtindo safi wa mapigo maarufu ya kule japani au maarufu huitwa karate,ila mimi nikaaamua kujipanga kwa mtindo wa moto kombati mtindo wa hapa Tanzania mtinndo unaojumuisha mapigano yote yawe kungfu au karate kisha nikapanga kutumia pigo lakombora yani anaepigwa harudi tena katika ulingo wa ngumi na hii tunafundishwa hasa pale unapokuwa unauhitaji wa kuwahi jambo na kuna mdudu anakuchelewesha.

Akaanza kushambulia yeye lakini ni ngumi mbili tu zilizotupwa nay eye na yatatu ikajaa mkononi mwangu na hapo nikamvuta upande wangu kwa kasi kisha nikaachia ngumi matata ikatua katikati ya paji la uso wake kisha nikamwachia na kumwacha kipepesuka huku nikijua kabisa ubongo wake umepata mtikisiko wa haja.

asalaaam kudo
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] mzee baba hii story yako leo nimeisoma nikicheka sana wallahi.
 
sehemu ya 9

Nikamtazama anavyohangaika kuupata mhimili wake ili asimame lakini alishindwa na kujibwaga chini kisha mimi nikatazma kiunoni kwake alikuwa amekipachika kisu change mbweha yule nikampokonya kisha nikatazama kule waliko askari wake nikaona bado wanamshambulia simba aliekuwa kama kapagawa katikati ya vita na binadamu wale dhalimu.

Nikaianza safari yangu ndani ya pori lile huku roho yangu ikiwa na woga kiasi hasa nilipowakumbuka nyoka wale lakini nilijipa tumaini tu nitafika ninakoenda.

********

Nilikuwa nimefika katikati ya wilaya ya salimbe ndani ya mkoa wa bunjumbura na nilikuwa najaribu kukumbuka ramani ya kunifikisha kule nilikokutaka.

Niliipita mitaa kadhaa huku nikishudia watu baadhi wakinishangaa,hawakunishangaa kwa sababu ya michubuko mwilini kwangu au lile begi nililobeba,walikuwa wanashangaa ile rangi yangu na nywele zangu nilizokuwa nimezikata kwa mtindo wa Afro.

Nikazidi kuchukia tabia ya watu hawa wa afrika kwa nini wana tabia hii ya kubagua watu wenye ulemavu wa ngozi na huku wakishindwa kuwabagua wazungu,nikajitazama kwani nilikuwa ninatofauti gani na mzungu au huu mapauko nilionao au kitu gani labda,lakini nikaamua kuachana nao.

Niliingia katika duka moja wapo pale mtaani na kutaka kununua maji ya kunywa maana nilikuwa nimeishiwa akiba ya maji na kiu kilinisumbua.Ajabu wakati nimekaribia mlango wa duka lile nikapata kumshudia muuzaji akininyooshea kidole huku akianza kukoroma kwa lugha ya kitutsi ambacho sikukielewa lakini nilitambua anajaribu kunionya nisikaribie dukani kwake.

Pembeni kidogo ya duka lile kulikuwa na duka lingine basi nikajaribu kusogea hapo ili nipate kununua maji lakini kabla hata sijafika mlangoni kwake lango likafungwa na ndani alikuwepo mwanamke.

Nilipojaribu kuwatazama wakazi wa eneo lile nikaona kabisa wanavyojaribu kunikwepa ili nisiwasogelee nahapo nikaumia moyoni mwangu na hakuna kitu kilichokuwa kinaniumiza kama hicho kitu cha kunyanyapaliwa hadharani na nilishindwa cha kufanya zaidi machozi yalikuwa yakinitoka tu na hapo nikauona umuhimu wa kamanda Malebo,mtu pekee alieniokota na kuniliea kama mwanae na kunifunza ukakamavu ambao unanisaidia hadi sasa,hakunitenga wakati naumwa na hakunitenga wakati nilipokuwa nina shida zaidi alinipa ujasiri wa kupambana na walimwengu na maneno yao.

Na hapo nikawakumbuka wazazi wangu walionizaa kisha wakanitelekeza ili nisipate kuwepo kabisa na kwanini walinitelekeza kisa tu hii ngozi au waliamini nini kama wangenilea hadi hapa nilipofikia,dunia haina usawa kabisa na hata usawa unaotafutwa hapa sio usawa wa watuwote ni usawa wa pande moja tu yenye rangi thabiti,lakini kama mungu yupo kwanini ameniweka hivi nilivyo na wengine wapo tofauti na mimi?

Niliendelea kulia huku nikikufuru na kisha nikajifuta machozi machache yaliokuwa usoni pangu na kutazama pemebni watu walikuwa wanazidi kunishangaa na mwenye duka yule alinikoromea akiwa nanitazama huku dukani kwake wateja wakiwa hawaingii tangu niliposimama pale.

Mwenye duka alipoona bado nipo kibarazani kwao akatoka na kipanga butu huku akikoroma na mate yakimtoka mdomoni na watu pembeni wakaanza kupiga kelele za shwangwe na pembni kulikuwa na bodaboda nao wakaanza kupiga honi za vyombo vyao.

Bwana yule mwenye roho mbaya akanisogelea zaidi huku akiwa kanyanyua kipanga chake.Aliponifikia akataka kunipiga kwa ubapa,lakini nikawahi kumkwepa kisha nikampiga ngumi ya kisogo na kumwacha kaipepesuka kama anaetaka kuangukia mbele huku mimi nikiwa nipo nyuma yake.

Yule bwana hakutaka kushindwa mbele ya watu waliokuwa wameanza kujaa eneo lile.Akageuka kwa kasi na kutaka tena kunishambulia napo nikamuwahi kwa kumtandika teke aina ya mawashi yaani hili nit eke unalompiga adui kama kofi hivi.Akadondoka huku akipiga ukulele wa gadhabu na sikutaka kupambana nae nikamnyang’anya kile kipanga kisha nikakitupa mbali kidogo na nikageuka lilipo duka lake nikapiga hatua kukiendea kimlango kidogo kilichokuwa wazi nikazama ndani yake na nikafikia kuchukua maji chupa ya kama lita moja unusu hivi kisha nikaanza kutoka na hapo nikashuhudia kundi kubwa la watu wakiwa wanapiga makelele ambayo ni kama walikuwa wanajishinikiza kunivamia ama kunipigia kelele za mwizi.

Nikatoa kisu change kilichokuwa kiunoni pangu nikakishika sawia kabisa huku nikiwa tayari nimeanza kuyanywa maji yale.Watu wale walipoona nimeshika kisu wakaanza kurudi nyuma kwa woga na mimi sikutaka kuleta fujo zaidi nikaanza kupiga hatua kutoka sehemu ile.

Ikiwa nakaribia kutoka kwenye eneo lile ambalo sikujua jina lake nikasikia king’ora cha gari la polisi kikija usawa nilipo,sikutilia maanani sana mi nikazidi kutembea huku nikisoma maeneo yale na lengo nilikua natafuta jina la nyumba ya kulala wageni.

Gari ile ya polisi ilinifikia na haraka nikashangaa nikizungukwa na askari polisi kama sita hivi huku wakiwa wananinyooshea silaha zao,walikuwa ni makonstebo wote wale na waliongozwa na sajenti ambae alikuwa ana teremka ndani yalile gari.

Askari wale hawakunisemesha chochote na mimi sikutaka kusema nao maana nilijua hatutaelewana katika lugha yao lakini sikutaka kujihangaisha maana nilijua taarifa itakuwa imetoka kwa wale watu kule salimbe.

Mmoja wa askari polisi wale akanisogelea na pingu mikononi mwake nikajua wanataka kunifunga wajinga hawa.

Nikawatazama kila mmoja wao na nikaona hawana masihala askari wale na tayari silaha zao zote zilikuwa zimeondolewa usalama,na nilijionya kwa sababu nilijua kabisa sina thamani mbele ya watu hawa weusi wasio na ulemavu wa ngozi kama mimi na mra nyingi uniona kama vile mimi ni mkosi katika jamii yao ya watu walioumbwa kamili.

Nikanyoosha mikono yangu mbele ili askari yule asipate mashaka na kweli akaja akanitia pingu na baada tu ya kutiwa pingu wakaanza kunisukuma kwa nguvu ili nieliekee ndani ya gari lao.Nikazidi kushangaa hizi taratibu za Askari wetu wa Afrika kuwa na tabia moja kila nchi hata mtuhumiwa wao ukitii sheria bila shuruti ni lazima watakupa adha tu watu hawa.

Nikapandishwa ndani ya gari lile huku tayari askari mmoja akiwa amenipiga kofi kali la uso,sikujali sana nikapanda na kukaa kwenye karandinga lile ili nisiendelee kubugudhiwa zaidi na watu hawa na safari ikaendelea kupita kule Salimba nilikoavha kizazaa kwa mwenye duka.

Tulipofika mitaa ile gari lile likasimama na akashuka yule sajenti na akaelekea kule dukani na huko nikaona anachukua pesa kutoka kwa bwana yule na kisha wakazungumza kidogo na askari yule akarudi tena na sfari ikaendelea.

Hatukucukua muda mrefu tukawa tumefika kituoni kwao na hapo nikashushwa mzegamzega na kupelekwa ndani huku sasa askari wale wakiwa wananipiga mateke kwa nyuma na mwingine akawa ananipiga kwa kitako cha bunduki yani ili maradi tu ni kero walinipa.

Tulifika hadi ndani na huko nikasikia wakiiulizana kwa lugha ya Kiswahili kibovu

“kafanya nini?”

“Ameleta ukorofi huko mtaani”

“Anakuwaje mkorofi wakati ni mlemavu huyu”

“ ndo hivyo mkuu”

Yule alieitwa mkuu akanigeukia akanitazama kwa muda kisha kaniuliza katika lugha ambayo sikuilewa na mimi sikumjibu kabisa na hapo nikaona anapatwa gadhabu zaidi na kuninasa kofi kali lililopelekea nione nyotanyota usoni,lakini alikuwa ananionea tu maana sikuwa naelewa kile alichotaka kuniuliza.

Alipoona simjibu akamuru nipekuliwe na hapo ndo ukazuka utata na mateso ndani yakituo kile cha polisi.

Alienipekuwa alinikuta na kisu changu ambacho si cha kawaida lakini pia alikuta viatambulisho vyangu vya jeshi na kikubwa alikuta ramani ya mji mzima wa Bunjumbura na viunga vyake.

Hali ya tahadhari ikatanagazwa kituoni pale sikujua kwanini lakini nikajikuta umakini uanongezwa kuelekea kwangu huku yule mkuu akiwa anamalizia kuvisoma viyambulisho vyangu na kisha kanigeukia tena.

‘wewe ni mtanzani?” kaniuliza na mimi nikatikisa kichwa kukubali

“hapa Bunjumbura umefuata nini” aliuliza tena kwa Kiswahili cha lafudhi ya Kirundi na nilishindwa kujua ni lafudhi ya kabila gani hasa.

“nikuja kutembea tu’” nikamjibu na hapo nikaona anakunja ndita kisha kama aliekumbuka kitu hivi akachukua simu na kupiga pahali akasikiliza kidogo na kuzungumza tena kisha akakata simu ile na kunigeukia tena.

“umeua watu wangapi huko Iyumbi” akaniuliza kwa upole kabisa

Na hapo haofu yangu ikaongezeka zaidi inakwaje watu ahawa wamejua nimeua,lakini nikaona najiuliza swali la kipuuzi sana na nikaanza kujilaumu kwanini nilikubali kirahisi vile kuingia mikononi mwa askari wale na hapo nafsi yangu ikakubali ya kuwa sikio la kufa halisikii dawa.

Askari yule mkuu akaamuru niwekwe sero na hilo likatekelezwa mara moja na nikiwa nimevuliwa mkanda na viatu,lakini pia hawakunipeleka kwenye sero ya watu wote nilipelekwa kwenye ile sero ya mtu mmoja na huko nikafungiwa humo huku vitu vyangu vikihifadhiwa nisikokujua.

***********
 
sehemu ya 10

Kwa makadirio tu nilikuwa nimekaa mle ndani kama lisaa lizima hivi na kichwa change kilizidi kupata moto wa mawazo kutokana matukio yanayonitokea kila siku na nini hatima ya maisha yangu ya baadae,lakini niliamini kabisa ninachokitafuta kina manufaa kwangu na ni deni langu kama sitolifanikisha jambo hilo.

Lakini nikiwa hivyohivyo katika fikira mlango wa pale sero ukafunguliwa na wakaingia askari polisi saba wakiwa na smg vifuani kwao na nyuma yao walikuwepo askari jeshi wa jeshi la Burundi nao walikuwa wamebeba siliha za kivita za AK 47 na hawakuonekana kuwa na masihara nyusoni mwao.

Wakanifunga mnyororo miguuni na mikononi huku mnyororo mwingine nikafungwa shingoni na ndio uliotumika kushika minyororo ya miguuni na mikononi kisha wakaanza kunikokota kulekea nje na huko nikakuta kuna gari tatu za askari jeshi zikiwa na askari walioiva katika masuala ya field masho na mikoni walishika bunduki za kivita za AK 47 na M16 na MP44.

Nikashaangaa sana huu ulinzi niliopewa una maanisha nini kwa mtu kama mimi na sikujua kwa kweli kama tayari wale askari jeshi walikuwa na taarifa ya sereka langu kule msituni lakini kikubwa walikuwa na taarifa ya kufukuzwa huko Tanzania kwa makosa ya kuua wenzangu kambini.

Niliongozwa kupanda kwenye gari dogo amabalo lilikuwa limetengenezwa kiajabu kabisa,lilikuwa limetengenezwa kwa bomba nene ina maana hata lingedondoka waliondani tungetoka wazima kabisa na huko ndani nikapokelewa na askari wawili ambao sikuchelea kujua walikuwa ni makomando wa jeshi lile la Burundi.

Safari ilianza huku nikiwa katikati ya ulinzi mkali wa askari jeshi waliojizatiti kwa silaha kali kabisa za kivita na sio wale asksri ndani ya lile gari nililokuwamo kulikuwa na askari wengine kwenye gari mbili zilizokuwa mbele huku kukiwa na askari wengine kwenye gari mbili zilizokuwa nyuma na zile gari za mbele zilipiga ving’ora kuashiria kuomba njia kwa dharura walionayo.

*******

Nilifikishwa kwenye kambi ya jeshi ya Rwaruzambo iliokuwa ndani ya wilaya ile ya Salimbe,nilipokelewa katika namna ya pekee kabisa, wakati nashuka ndani ya gari lile nilikuta askari wengine wakiwa wapo tayari kwa lolote na bunduki zao mkononi.nikashindwa kuelewanini maana yake uimara huu wa ulinzi ndani ya kambi hii.

Nikaongozwa kuingia ndani zaidi ya kambi ile huku nikiharakishwa kutembea kwa haraka na minyororo yangu mwili mzima.

Walinipeleka hadi katika nyumba moja hivi iliokuwa katikati ya kambi ile na huko nikakuta ulinzi mkali wa askari wale wa jeshi la Burundi.

Walipokwisha kuniingiza ndani wakafunga na kuniacha mle ndani nikiwa sijui nini hatima yangu na kwanini wananiweka katika ulinzi mkali kiasi kile.

Nikiwa bado nawaza vile mlango ukafunguliwa na wakaingia askari zaidi ya watano na walikuwa wanongozwa na luteni usu mwenye nyota moja begani na alikuwa amepitisha skafu shingoni pake na alivaa mawani ya jua.

Nilimtazama katika namna ya kujiuliza zaidi maswali kuhusu ile skafu kama ilikuwa sahihi kwake kuivaa wakati yupo kazini,lakini kubwa ni namna ile skafu ilivyokuwa ilikuwa haitofautiani kabisa na ile skafu iliokuwa kwenye shingo ya yule askari niliomuua kule msituni na pia ilikuwa sawa kabisa na zile nilizoziona kwa wale watu walioanza kunikimbiza wakati nilipokuwa naingia Burundi.

Akili yangu ilijaa maswali zaidi ya uwezo wake wa kujibu na hapo nikagutul;iwa kutoka mawazoni na askari yule aliekuwa kavaa skafu shingoni pake ilihali yupo na gwanda za kazi.

“NIYONZIMA!!”askari yule aliniita jina langu ambalo niliitwa mara mojamoja sana na mlezi wangu kamanda Malebo,\.

Nilimtazama askari yule kisha nikajiuliza amelijuaje jina langu katika wakati kama ule ambao nilijua kabisa watakuwa na jina la kwenye vitambulisho ambalo niliitwa James Malebo! Amelijuaje huyu mtu mna hapo nikataka kumuuliza na kabla hata sijamuuliza aksimama akawapa ishara askari wake wakarudi nyuma na kutupa nafasi zaidi huku mimi nikiwa nimekalishwa kwenye kiti mle ndani.

“umelijuaje jina langu” nikamuuliza huku nikiwa nimemkodolea macho ya kiulizo haswa.

“labda nikuulize wewe lengo la kuja hapa Burundi mmh,na vipi kuhusu hazina yetu James umekuja nayo au…” nikamkatisha

“hazina ipi mzee unayoongelea asee hebu nijibu swali langu umenifahamu vipi?” ikabidi niwe mkali maana niliona ananiletea hadithi nyingi nisizozielewa.

Akanitazama huku akionekana kabisa hahitaji kunipa jibu la maswali yangu lakini ikabidi sasa nicheze pata potea kama mtu huyu ananijua jina basi atakuwa na majibu ya kilichonileta hapa bunjumbura.

“yuko wapi kamanda Malebo” nikamuuliza huku nikiwa nimetuliza jazba na nikitaka kumsoma mawazo yake kiumbe yule.na hata hakunijibu akaishia kunitolea tabasamu tu na kusimamana hapo nikafanikiwa kuona jina lake aliitwa E.MUSIZA nikaliweka akilini jina lile huku yeye akiendelea kucheka na kunitazama katika namna ya kudharau swali langu kisha akasema

“Malebo mtu mbaya sana ila kakutana na wabaya zaidi,na hata wewe usipoleta ushirikiano basi hakutakuwa na namna lakini pi…” hakumaliza kauli yake akasita kuendelea kusema na katazama pembeni walipo vijana wake na bila kuongeza neno zaidi akatoka huku akiacha nikiwa katikati ya ulinzi mkali.

Baada ya yeye kutoka hakukawia sana kurudi lakini aliporudi hakuwa peke yake alikuwa na mzee wa makamo tu huku akiwa na cheo cha afisa daraja la kwanza na mkononi mwake afisa yulealikuwa kabeba kimkoba kidogo.

Walipokwisha kuingia ikatolewa ishara tena na punde vijana wale wakaja na kuninyanyua msegamsega na kunipeleka chumba cha pili na huko nikatupwa kwenye meza moja iliokuwa mle ndani na hata kabla sijasema lolote nikajikuta nimefungwa juu ya ile meza huku sasa mikono yangu ikiwa hewani kama mtu anae ogelea na kutupa mikono huku na huko na miguu yangu nayo ilikuwa imetanuliwa na kitu pekee kilichopata nafuu ni mgongo uliokua juu ya meza.

Nikavuliwa nguo zote kisha yule mzee akazama kwenye kile kimkoba na kutoka na kichupa kidogo ambapo nilipokitazama nikaona ni zile chupa zinazohifadhi vilipuzuzi.

Akanisogelea hadi pale nilipolazwa kisha kama alieogopa kunigusa akaanza kumwaga ule unga mwilini pangu na alipohakikisha ule unga umeishia mwilini kwangu akakiweka kile kichupa kando na kuchukua birika la maji lililokuwa mule chumbani na kabla hajanimwagia kilichomo luteni E.Musaza akamzuia kisha kanisogelea pale nilipokuwa nakuniinamia hadi sikioni na akaanza kuongea kama vile hakutaka wengine wasikie tulichozungumza.

“Niyonzima naomba useme ukweli baba yako alikwambia nini kuhusu Hazina?” nilibaki kumtaazam tu maana sikuwa na cha kumjibu na sikuelewa alitaka kusema nini luteni yule mwenye nyota mbili,hili la hazina ni geni kwangu na sio lililonileta huku mimi nimekuja hapa kwa mabo mawili makubwa kwanza kumtafuta kamanda Malebo ambae ni sawa na baba yangu lakini pia nimekuja kumtafuta babu yangu mwenye jina kama langu au mzee Niyonzima ambae nina vinasaba nae na huku ndiko nilikotoka miaka ishirini na tano iliopita,na sasa nimekuja kutafuta hao wa kuitwa wazazi wangu hasa huyu mzee ambae aliniokota wakati mwanae aliponitupa na akanikabidhi mikononi mwa kamanda Malebo aliekuwa katika harakati zake huko bunjumbura.

Luteni E.Musaza alipoona nipo kimya akatoa ishara yule mzee aendelee kuniadhibu.

Yule afisa daraja la kwanza alinisogelea na lile birika kisha akamwaga kimiminika kilichokuwamo mule ndani na kukaa pembeni kama sie alienimwagia kimiminika kile ambacho kilikuwa na harufu ya kama gundi ya kubandikia mbao.

Wote walikaa kimya huku wakinitizama,na nilishindwa kutambua kwanini wametulia tu japo nilihisi ni jambo baya litakalo fuata.
 
sehemu ya 11

Ilikuwa inaelekea kuwa kama dakika ya tatu hivi tangu wanimwagie ule unga na kimiminika kile na hapo nikaanza kuyapata matokeo ya zoezi lao.

Mwili ulianza kutoa jasho huku kwa mbali ni kama ukiwa unapashwa kwenye moto uliowekwa mita kumi kutoka nilipokaa.Jasho lilizidi kuchuruzika na huku mwili nikisikia kama unaungua hivi,lakini mabo yakazidi kubadilika baada ya mwili mzima kuanza kuwasha kama nimemwagiwa upupu.

Nililia kama motto mdogo lakini muwasho ule haukunitoka wala lile joto halikuwa likiisha na sasa mikono na miguu ikaanza kuuma kwa kukosa egemeo maana ilining’inia juu juu tu.nikiwa nalia kwa maumivu yale Musaza alinisogelea tena na kuniuliza kifedhuli

“hazina ipo wapi Niyonzima uhurumie mwili wako kijana” nikamtemea mate kwa uchungu nae akyafuta kisha akampa tena ishara afisa yule wa daraja la kwanza nae nikaona anatoa kitu kutoka kwenye mkoba,vilikuwa ni kama vile vifaa vya kusafishia kucha na hapo akaja hadi kifuani kwangu akaanza kunichana kwenye kifua changu huku akikandamiza na kusigina kama anae taka kutoboa boksi la biscuit.

Damu ilianza kunitoka kwenye majeraha yale yalikuwa kifuani kwangu huku yule mzee akiwa tena amekirudia kimkoba kile na tena akatoka na kichupa kingine kilichokuwa na kimiminika cha kijani na kuja kunimwagia kwenye yale majeraha,uchungu nilioupata kutoka kwenye majeraha yale hausimuliki kwa kuandika,nikajaribu kupambana na hali ile lakini nilishindwa na kujkuta nikitoa kilio kama cha kahaba anaedhihakiwa na mabwana waliomtumia bila kumlipa.

Nikatumia nguvu ili anagalau nigalegale lakini minyororo ile ilikuwa imefungwa thabiti kabisa na haukunipa nafasi ya kufanya lolote lile.Maumivu yanizidi na joto pia lilizidi mwilini kwangu na hapo nikaona kama kiza kikinijia kwa kasi na kufunika fahamu zangu na kilichokuja endelea pale sikukifahamu tena.

**********

Nilikuja kuzinduka na kujikuta nipo mikononi kwa watu nikiwa nimebebwa huku mmoja akiwa kanishika mikono na mwingine alikuwa kanishika miguu,sikujua wananipeleka wapi wakati ule na nilipofumbua macho tayari ilikuwa ni kiza huku nikiwa mazingira yakionesha nipo nje ya nyumba ile ya pale kambini.

Watu wale walizidi kutembea na mimi na kisha nikasikia wakiteta jambo kwa kilugha na hapo wakasimama na kunitua chini na wakati natua chini nikapata kuyasikia yale maumivu kifuani kwa sababu walinitua kwa kunibwaga chini kama mzigo.

Wakateta tena na hapo nikasikia watu wengine wakiongezeka na kisha yakafuatia malumbano katika lugha ambayo niliisikia baadhi ya maneno na hata nilipoyaelewa hayakuleta maana katika ubongo wangu.

Watu wale wakanibeba na kunitupia kwenye gari ambayo kutokana na udogo wake basi nilijua itakuwa ni Toyota mandolini ya kizamani kabisa,kisha nikawsikia tena wakiteta kidogo na watu wengine wakapanda kwenye gari ile na likawashwa na kuondoka.

Tukiwa tupo ndani ya safari sikutaka kuleta fujo yoyote maana sikujua mazingira yapo vipi na kwanini nimetolewa kule kambini kulikokuwa na ulinzi mkali afu kizembe tu waniachie tena bila ulinzi kama vile hawanihitaji tena.

Nikiwa bado nawaza nikasikia mkono ukinipapasa kwenye uume wangu,kisha alienipapasa akasema katika lugha ileile nisioilewa na hapo nikasikia wakiteta tena jambo na mkono ule ulionishika mwanzo ukarudi tena kunipapasa na wakati huu ukaenda hadi kwenye pumbu zangu na kisha akaacha zoezi lake na muda wote huu nilikuwa bado nipo uchi wa mnyama na baaridi ilikuwa imeanza kuniathiri maana nilianza kutetemeka lakini sikutaka nionekane kama natetemeka.

Safari yetu ilikuwa bado inaendelea nab ado yule mtu alikuwa anazidi kuutomasa mwili wangu huku sasa akiwa kaleta mkono wake hadi usawa wa pua yangu na hapo bado nilikuwa sijapata japo kujua watu hawa wanataka nini kwangu hadi wakati huo na kwanini wanitomasa na kisha kujadili jambo.

**********

Gari ilisimama na kisha nikawasikia wakiteremka chini watu wale na kisha waliokuwa wamebaki mle garini wakajipanga kunibeba na walipokwisha kunibeba wakawapa walioko chini na walioko chini wakaanza kuondoka na mimi baada ya kunipokea.

Walinibeba kama walivyokuwa wamenibeba kule mwanzo lakini walioko nyuma nikasikia wameanza kuimba nyimbo za ajabu ajabu na safari ikiendelea na hapo hisia mbaya zikajijenga kichwani ya kuwa watu wale walikuwa wanapanga kunitoa kafara,lakini kafara ya nini na donge kubwa likajijenga kifuani kwangu,nikaona ni kama wanataka kucheza na roho yangu wanaharamu hawa kwanini eti.

Baada ya mwendo mdogo wakanitua chini lakini ilikuwa ni kama juu yakifusi hivi na hapo nikasikia sauti nyingine zikiongezeka kutoka eneo lile na kwa mbali macho yangu yakanasa mwanga na hapo nikajua ni lazima kutakuwa na taa maeneo yale na kwa mbali nikafumbua macho yangu lakini nikakutana mwanga mkali wa kurunzi ukinimulika usoni na nikashindwa kutambua kinachoiendelea eneo lile.

Nikafumbua tena macho yangu na kutazama tena na hapo mwanga ulke ulikuwa umehamia kwenye uume wangu,na nilipojari kupata idadi kamili ya watu wale kwa haraka haraka walikuwa ni kama watu saba hivi wakiwa wamenizunguka na akili yngu ikanambia sikupaswa kuendelea kuwaza ilihitajika nifanye jambo ili kujiokoa na hatari ya kutolewa kafara.

Nikamtazama tena yule alieshika kurunzi nikaona bado anashangaa vidole vya miguu yangu na hapo nikafanya kile amabacho hawakukitarajia wadhalimu wale.



RIWAYA HII IPO YOTE HADI MWISHO ANAEHITAJI NAOMBA TUWASILIANE KWA
0758573660

Asalaaam Kudo
 
SEHEMU YA 12

Nikaipiga teke kurunzi ile na ikadondoka mbali na kisha nikaweka mikono yangu chini na kubetua miguu yangu na kusimama wima,na wakati huohuo masikio yangu yakaunasa usauti mdogo wa kukokiwa silaha ya uzi micro na bila kujiuliza nikajinyonga na kurusha ngumi matata kwa mtu yule alieikoki silaha ile na ikampata sikioni na kudondoka chini huku akitoa mlio wa maumivu na hapo nikanasa tena sauti ya hatua za mtu akija kwa kasi nyuma yangu na hapo nikageuka kwa kasi na kuachia teke msawazo yaani teke linalopigwa kimo cha pembe za ng’ombe na kupata yule mtu kifuani na kumtupa nyuma huku mikono yangu ikiwa tayari imenasa shingo ya mtu na kuivunja.

Waliobaki kama wane hivi wakaanza kukimbia huku wakipiga makelele ya woga na mimi ikabidi nitulie kwanza na kutazama eneo nililopo na kuona pembeni yangu kuna shimo refu lililochimbwa kama yale mashimo ya migodini na hpo nikajua nipo migodini na nilipotazma upande mwingine nikaona kuna matuyrubai na taa zikiwaka huku kukiwa na makelele mengi upande huo na hapo nikatazama chini nikamwona mwanajeshi mmoja amelala chini na bunduki yake akigalagala nikamfuata na kumtandika teke la mbavu na nikamsikia akikohoa nakutema kitu nikajua ni damu hiyo.

Nikamtazma mwingine tena alikuwa katulia kimya chini kama mfu huyu ni yule niliekuwa nimempiga teke msawazo na nilipomkazia macho nikaona anakimo na mwili kama mimi sikuchelea kumvua mavazi yake na kuyatia mwilini kwangu pamoja na viatu vyake vya kutoka kampuni ya didasi,navyo nikaviyia mguuni na kuutikisa kidogo mguu wangu nikatambua havinitoshi viatu vile.

Pale nilipokuwa kulikuwa na kimlima kidogo na hivyo ikanilazimu kushuka bondeni kulikokuwa na makele ya watu huku nikikutana na mashimo mengi yaliochimbwa na kuachwa na hapo akili yangu ikatambua kabisa nilkitaka kutolewa kafara na watu wale wapuuzi.

Sikutaka maumivu yautawale mwili wangu hivyo nikajikaza na kuanza safari ya kuelekea kule kunakosikika kelele nyingi za watu na umeme ukiwaka vyema.

Nilianza kuyakaribia makazi yale na hapo nikapokelewa na sauti za muziki wa kilevilevi kutoka kwa wasanii wa pale Burundi,mitaa ile ya machimboni ilikuwa imechangamka kweli huku walevi wakiwa ni wengi kuliko waliosafi kiakili.

Kadri nilivyozidi kusogea ndivyo nilivyozidi kujionea mambo ya ajabu eneo lile kuna watu walikuwa wakijamiaana hadharani huku kitu pekee kilichowasitiri ni vijumba vya maturubai,miguno ilisikika huku na huko na baadhi ya watu wanavuta bangi hadharani kabisa yaani ilimradi kila mtu alifanya kile alichojisikia.

Macho yangu yakavutiwa na watu wawili waliokuwa wamegandiana kwenye kichochoro kimoja hivi,kilichonivutia ni yule mwanume aliekuwa amemwinamisha mwanamke mmoja wakingonoka,kilichonivutia kwake ni mavazi yake,alikuwa amevaa koti refu lililomfunika kichwani na nilihitaji lile koti.

Niliwafuata wale watu huku mwanamke akiwa wa kwanza kuniona na kujichomoa kwa mwanaume wake huku mwanaume akitoa tusi kubwa kulaani kitendo kile lakini mwanamke wake akamnyooshea kidole kuja nilipo yule bwana huku akiongozwa na pombe akanifuata kwa gadhabu za kukatishiwa uroda wake na mimi sikutaka kumkawiza nilikuwa nimejiandaa kumpa ngumi nzito.

Aliponifikia kweli sikutaka kumkawiza nikampiga ngumi katikati ya kifua katika uzito wa kumfanya asife ila asinyanyuke kwa muda huo na kweli kaenda chini na alivyotaka kunyanyuka akashndwa na nilipotazama pale alipokuwa yule mwanamke hakuwepo tena.

******

Nikiwa tayari nina lile koti refu nakisu kirefu nilichokikuta kwa yule bwana mfanya sodoma,nikaingia kwenye bar ya makuti iliokuwa ikitoa mziki mnene na makele ya watu na nilivyoingia hakuna ailienitilia shaka yoyote maana niliingia huku nikiwa nimeigiza kulewa hivi na nikawa nikiwapita watu walikuwa wamebambiana,huku wengine wakipepesuka huku na huko lakini cha ajabu hakuna alieangusha chupa ya pombe.Nikawapita kwa tabu huku nikiwapiga vikumbo watu kadhaa na kuelekea ilipo kaunta.

Nilipofika nikamkuta mhudumu wa kule kaunta kiwa bize kuhudumia watu na huku wengine wakiingia kule aliko wanachukua pombe na kulipa kisha wanendelea kuburudika na mimi niakingia kule kaunta lakini nilipofika nikaufunga ule mlango wa kaunta na nikamgusa yule dada wa pale kaunta makalio yake akaruka juu huku akigeuka na kucheka lakini alichokutana nacho ikabidi aanze kutetemeka na nikamwekea kidole kimoja mdomoni kama ishara ya kumwashiria haruhusiwi kupiga kelele nae akatii.

Watu waliendelea kupiga kelele lakini mimi nilikuwa nimedhibiti muuzaji yule na tayari alikuwa ameanza kunihesabia pesa aliokuwa ameuza.

Alinipa pesa sawa na tsh.laki mbili hivi ambayo ni sawa na faranga miamoja na sabini elfu.Alipokwisha kunipa nikaanza kutoka mule ndani huku sasa nikipiga hesabu za kuchomoka mule baani haraka kabla mabo hayajaharibilka.

Wakati nimeshajichanganya na walevi yule dada akaanza kupiga makele lakini kelele zake zilimezwa na muziki mkubwa na kelele za waponda raha wale.

Nilifanikiwa kutoka hadi nje kabisa ya ukumbi ule na huko nikalitupa koti lile na nikabaki na kisu kile kirefu nilichokitia kwene pindo la nguo nilizozivaa na kisha nikachukua kofia niliokuwa nimepora kichwani mwa mlevi mmoja wakati natoka mle ndani ya ukumbi ule wa anasa.

Safari yangu ilikuwa ni kujaribu kutafuta uelekeo wa kule kituo cha polisi ambako niliamini nikifika huko basi uelekeo wangu wa kumtafuta mzee Niyonzima ungerudi kidogo kichwni pangu.

Nikazidi kupishana na watu kadhaa wakiwa katika harakati walizozijua wao usiku ule,nikazidi kwenda mbele kwa kufuata barabara iliokuwa ikiingia mgodini mle,sasa mimi nilikuwa naifuata kwa kutoka yaani kwa kuelekea kule inakotokea barabara ile.

Kwa mbele niliona kibao kikiwa pembeni mwa barabara ile na hapo tabsamu jepesi likajijenga usoni pangu nikajikuta nakimbia ili kukifikia maana niliamini kitakuwa na jina la mgodi ule mdogo.

“WELCOME CAMP DE BUKAMBO” kibao kile kiliandikwa vile na hapo nikajaribu kuvuta kumbukumbu za ramani yangu ililokuwa kwenye begi ambalo sijui hadi wakati huo litakuwa wapi.

Kumbukumbu zangu zilinionesha kutoka hapo Bukambo hadi kule Salimbe kulikuwa na mwendo wa kama kilomita 9,lakini eneo ninalolitafuta nilo hilo Bukambo hivyo sikuwa nahaja ya kurudi kule ilihitajika nitafute makazi ya Mzee Niyonzima ndani ya Bukambo.

Ijapokuwa hapo nilipokuwa hapakuonesha kuwa na makazi ya watu lakini niliamini kabisa ndani ya eneo lile kulikuwa na makazi karibu maana nilitoka mbali kuja kulitafuta eneo hilo la Bukambo,hivyo nikafanya shauri la kurudi kule vilabuni ili nipate kuutega usiku na pakikucha basi nijue pa kuanzia.

*********

Katika pitapita zangu usiku ule nikafanikiwa kuona sehemu palipokuwa pameandikwa GEUST.Na nilipoingia kweli kulikuwa vyumba na chumba kilikuwa ni faranga 850,nikapewa chumba na kwenda kujipimzisha.

Huko chumbani nilijuta kulipia yaani mara mia ningelala nje kuliko pale ndani,kitanda kilikuwa kina chaga za miti huku godoro likiwa ni la pamba na limechakaa sana,lakini kulikuwa na kero ya kutoka vyumba vya jirani ambapo watu walikuwa wakifanya ngono na kupiga makele kwa sauti ya juu,ama hakika migodini ni sehemu zilizolaaniwa si kwa sodoma ile.

ASALAAM KUDO

0758573660
0658564341for whatsap
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom