RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

RIWAYA: Sauti ya Mtutu (mtazika kila ikisikika)

Umeme unasumbua sana ndugu zangu sifanyi kusudi asee
 
Maruwe ruwe live ya huku kule ya Kule hukoo almrad tafaran!
 
Maruwe ruwe live ya huku kule ya Kule hukoo almrad tafaran!
Kuna mtu huwa namwomba apost kutoka kwenye komputa yangu nipo nayo mbali ndie anachanganya naifuta
 
matuyrubai na taa zikiwaka huku kukiwa na makelele mengi upande huo na hapo nikatazama chini nikamwona mwanajeshi mmoja amelala chini na bunduki yake akigalagala nikamfuata na kumtandika teke la mbavu na nikamsikia akikohoa nakutema kitu nikajua ni damu hiyo.
Nikamtazma mwingine tena alikuwa katulia kimya chini kama mfu huyu ni yule niliekuwa nimempiga teke msawazo na nilipomkazia macho nikaona anakimo na mwili kama mimi sikuchelea kumvua mavazi yake na kuyatia mwilini kwangu pamoja na viatu vyake vya kutoka kampuni ya didasi,navyo nikaviyia mguuni na kuutikisa kidogo mguu wangu nikatambua havinitoshi viatu vile.
Pale nilipokuwa kulikuwa na kimlima kidogo na hivyo ikanilazimu kushuka bondeni kulikokuwa na makele ya watu huku nikikutana na mashimo mengi yaliochimbwa na kuachwa na hapo akili yangu ikatambua kabisa nilkitaka kutolewa kafara na watu wale wapuuzi.
Sikutaka maumivu yautawale mwili wangu hivyo nikajikaza na kuanza safari ya kuelekea kule kunakosikika kelele nyingi za watu na umeme ukiwaka vyema.
Nilianza kuyakaribia makazi yale na hapo nikapokelewa na sauti za muziki wa kilevilevi kutoka kwa wasanii wa pale Burundi,mitaa ile ya machimboni ilikuwa imechangamka kweli huku walevi wakiwa ni wengi kuliko waliosafi kiakili.
Kadri nilivyozidi kusogea ndivyo nilivyozidi kujionea mambo ya ajabu eneo lile kuna watu walikuwa wakijamiaana hadharani huku kitu pekee kilichowasitiri ni vijumba vya maturubai,miguno ilisikika huku na huko na baadhi ya watu wanavuta bangi hadharani kabisa yaani ilimradi kila mtu alifanya kile alichojisikia.
Macho yangu yakavutiwa na watu wawili waliokuwa wamegandiana kwenye kichochoro kimoja hivi,kilichonivutia ni yule mwanume aliekuwa amemwinamisha mwanamke mmoja wakingonoka,kilichonivutia kwake ni mavazi yake,alikuwa amevaa koti refu lililomfunika kichwani na nilihitaji lile koti.
Niliwafuata wale watu huku mwanamke akiwa wa kwanza kuniona na kujichomoa kwa mwanaume wake huku mwanaume akitoa tusi kubwa kulaani kitendo kile lakini mwanamke wake akamnyooshea kidole kuja nilipo yule bwana huku akiongozwa na pombe akanifuata kwa gadhabu za kukatishiwa uroda wake na mimi sikutaka kumkawiza nilikuwa nimejiandaa kumpa ngumi nzito.
Aliponifikia kweli sikutaka kumkawiza nikampiga ngumi katikati ya kifua katika uzito wa kumfanya asife ila asinyanyuke kwa muda huo na kweli kaenda chini na alivyotaka kunyanyuka akashndwa na nilipotazama pale alipokuwa yule mwanamke hakuwepo tena.
******
Nikiwa tayari nina lile koti refu nakisu kirefu nilichokikuta kwa yule bwana mfanya sodoma,nikaingia kwenye bar ya makuti iliokuwa ikitoa mziki mnene na makele ya watu na nilivyoingia hakuna ailienitilia shaka yoyote maana niliingia huku nikiwa nimeigiza kulewa hivi na nikawa nikiwapita watu walikuwa wamebambiana,huku wengine wakipepesuka huku na huko lakini cha ajabu hakuna alieangusha chupa ya pombe.Nikawapita kwa tabu huku nikiwapiga vikumbo watu kadhaa na kuelekea ilipo kaunta.
Nilipofika nikamkuta mhudumu wa kule kaunta kiwa bize kuhudumia watu na huku wengine wakiingia kule aliko wanachukua pombe na kulipa kisha wanendelea kuburudika na mimi niakingia kule kaunta lakini nilipofika nikaufunga ule mlango wa kaunta na nikamgusa yule dada wa pale kaunta makalio yake akaruka juu huku akigeuka na kucheka lakini alichokutana nacho ikabidi aanze kutetemeka na nikamwekea kidole kimoja mdomoni kama ishara ya kumwashiria haruhusiwi kupiga kelele nae akatii.
Watu waliendelea kupiga kelele lakini mimi nilikuwa nimedhibiti muuzaji yule na tayari alikuwa ameanza kunihesabia pesa aliokuwa ameuza.
Alinipa pesa sawa na tsh.laki mbili hivi ambayo ni sawa na faranga miamoja na sabini elfu.Alipokwisha kunipa nikaanza kutoka mule ndani huku sasa nikipiga hesabu za kuchomoka mule baani haraka kabla mabo hayajaharibilka.
Wakati nimeshajichanganya na walevi yule dada akaanza kupiga makele lakini kelele zake zilimezwa na muziki mkubwa na kelele za waponda raha wale.
Nilifanikiwa kutoka hadi nje kabisa ya ukumbi ule na huko nikalitupa koti lile na nikabaki na kisu kile kirefu nilichokitia kwene pindo la nguo nilizozivaa na kisha nikachukua kofia niliokuwa nimepora kichwani mwa mlevi mmoja wakati natoka mle ndani ya ukumbi ule wa anasa.
Safari yangu ilikuwa ni kujaribu kutafuta uelekeo wa kule kituo cha polisi ambako niliamini nikifika huko basi uelekeo wangu wa kumtafuta mzee Niyonzima ungerudi kidogo kichwni pangu.
Nikazidi kupishana na watu kadhaa wakiwa katika harakati walizozijua wao usiku ule,nikazidi kwenda mbele kwa kufuata barabara iliokuwa ikiingia mgodini mle,sasa mimi nilikuwa naifuata kwa kutoka yaani kwa kuelekea kule inakotokea barabara ile.
Kwa mbele niliona kibao kikiwa pembeni mwa barabara ile na hapo tabsamu jepesi likajijenga usoni pangu nikajikuta nakimbia ili kukifikia maana niliamini kitakuwa na jina la mgodi ule mdogo.
“WELCOME CAMP DE BUKAMBO” kibao kile kiliandikwa vile na hapo nikajaribu kuvuta kumbukumbu za ramani yangu ililokuwa kwenye begi ambalo sijui hadi wakati huo litakuwa wapi.
Kumbukumbu zangu zilinionesha kutoka hapo Bukambo hadi kule Salimbe kulikuwa na mwendo wa kama kilomita 9,lakini eneo ninalolitafuta nilo hilo Bukambo hivyo sikuwa nahaja ya kurudi kule ilihitajika nitafute makazi ya Mzee Niyonzima ndani ya Bukambo.
Ijapokuwa hapo nilipokuwa hapakuonesha kuwa na makazi ya watu lakini niliamini kabisa ndani ya eneo lile kulikuwa na makazi karibu maana nilitoka mbali kuja kulitafuta eneo hilo la Bukambo,hivyo nikafanya shauri la kurudi kule vilabuni ili nipate kuutega usiku na pakikucha basi nijue pa kuanzia.
*********
Katika pitapita zangu usiku ule nikafanikiwa kuona sehemu palipokuwa pameandikwa GEUST.Na nilipoingia kweli kulikuwa vyumba na chumba kilikuwa ni faranga 850,nikapewa chumba na kwenda kujipimzisha.
Huko chumbani nilijuta kulipia yaani mara mia ningelala nje kuliko pale ndani,kitanda kilikuwa kina chaga za miti huku godoro likiwa ni la pamba na limechakaa sana,lakini kulikuwa na kero ya kutoka vyumba vya jirani ambapo watu walikuwa wakifanya ngono na kupiga makele kwa sauti ya juu,ama hakika migodini ni sehemu zilizolaaniwa si kwa sodoma ile.
Nikajaribu kuweka hisia zangu katika mawazo ya harakati zangu huku nikitupilia mbali kelele zile za wapuuzi waliokuwa wakistarehesha miili yao,lakini ilikuwa ni kama kuruka mkojo ukanyage kinyesi.
Kunguni waliutafuna mwili wangu kadiri walivyotaka lakini sikutaka nishindwe kupata usingizi wakati nilikuwa sijapata usingizi ndani ya siku tatu,nikaupumzisha ubongo na hapo ndipo niliposikia mwili unavyouma kwa mateso na hekaheka za siku tatu.
********
Nilisikia kwa mbali kama watu wakibishana kwa gadhabu na huku mwingine akitoa matusi makali ya Kiswahili kibovu kabisa,ugomvi ule ulipokolea ikabidi niamke sasa na hapo nikasikia ule mzozo dhahiri kabisa,nikatega sikio kilikuwa ni chumba cha pili,nikasimama nikajiyoosha kidogo kisha nikapata kujitazama katika mwili wangu hasa mikononi nikapata kuona mwili wangu ulivomwekundu kwa adha ya kushambuliwa na kunguni na wakati bado nikizidi kujichunguza nikapata kuona kunguni mmoja akihama kutoka kwenye pindo la shati nililovaa nikamkamata kwa hasira na kumbinyia kwenye vidole vyangu na kisha nikatoa tusi kubwa la nguoni kumlaani kunguni yule.
Ugomvi ule wa watu wale huko chumbani kwao ukazidi kunikera kwenye masikio yangu name niakaona ni bora nitoke mule ndani kabala hakujapapmbazuka kabisa ili niwahi kulizungukia eneo lile.
Wakati natoka nikasikia watu wale ambao walikuwa ni mwanaume na mwanamke,tayari sasa mwanaume alikuwa ameanza kumpiga mwanamke,hapo nikashikwa na hasira kali sana yaani mtu usiku kucha kamsatrehesha afu muda wa kuachana anampiga mwenzie au kisa mwanamke hawezi kujitetea? Niakaona isiwe tabu badala ya kutoka nikavuta hatua kukiendea chumba kile na sikupata tabu kilikuwa wazi huku mlango ukipata tabu maana mwanamke alikuwa kaushika anataka kukimbia na mwanaume anazuia.
Niliusukuma kwa nguvu malango ule na kuufanya ufunguke na mimi nikaingia kwa kasi na hapo nikapata kushudia mwanaume akiwa uchi huku uume wake umesimama dede lakini pia mwanamke nae alikuwa uchi wa mnyama.
Waliponiona wote wakasogea pembeni huku mwanamke akiweweseka kwa kilio,na mimi ikabidi niulize kwa lugha ya Kiswahili chanzo cha wao kupigana ashusubuhi ile,jibu la mwanamke yule likanifanya nimtazame mwanaume yule katika namna ya ajabu kabisa,eti alikuwa anataka kumwingilia mwanamke kinyume na maumbile na alipokataa ndo ukazuka ugomvi.
 
Nikamfata bwana yule,nilipomfikia nikampiga kichwa kimoja tu na kumwacha akidondoka kwenye kitanda kile chenye chaga za fito na hakunyanyuka tena fahamu zilikuwa mbali na yeye, kisha nikachukua nguo na kumrushia yule dada nae bila kuuliza akaanza kuzivaa kwa haraka na alipomaliza akataka kutoka kwa kasi lakini nikawahi kumzuia na jambo lile lilimchanganya akaanza kubembeleza nimwachie ili aaende na safari zake,lakini nikaamua kumtoa hofu kisha nikaanza kumuuliza kwa lugha ya Kiswahili maana nilisikia akitukana kwa lugha ile japo ilionesha hakuwa akiijua vizuri.
“kutoka hapa hadi kwenye kijiji cha bukomba ni…” sikumalia kkauli yangu tayari akawa kadakia
“ ndo nyumbani huko ni hapo nyuma tu” alimaliza kuongea huku akiwa kisha fika mlangoni na mimi sikutaka kumwacha ikabidi nimfuate.
Alikuwa akikimbia nusu anatembea na kwa kuwa kulianza kupambazuka nikapata kuuona uzuri wa mwanadada yule alikuwa ni mwanamke mzuri sana huku mungu akiwa amempa msambwanda wa haja huku nyuma na kila hatua aliopiga iliacha lawama kwenye akili yangu lakini sikuapswa kumfikiria zaidi.
Mbali na yote hayo uzuri na umbo lakini alikuwa I mtu anaeuza utu wake kwa wavuta bangi kama yule mwanume alietaka kumlawiti binti yule.
Tulizidi kwenda mbele zaidi huku yule binti akigeuka na kunitazama kwa gadhabu na hakusita kunionesha gadhabu zake waziwazi na hapo ndipo nilipata kumchunguza na kumdadisi mwanadada yule.
Macho yake yalioniesha kitu zaidi ya nilivyofikiri,yule dada alisumbuliwa na jambo gumu kulikubali na hata mtazamo wake kwangu hakuwa sawa na wale madada poa ninaowajua ambao huwa macho juujuu kama wanataka kukata roho,huyu alikuwa tofautio kabisa na ilionekana anafanya yote haya kwa sababu ya jambo flani.
“mbona unanifuata kila ninakoenda?,..” aliniuliza baada ya muda wa dakika kadhaa za kutazamana huku tayari watu wakiwa wameanza kutupita wakienda na shuguli zao.
‘nakufuata kwa sababu nahitaji kufika kijijini Bukomba” nilimjibu huku bado tukiwa tunatazamana na binti yule.
Nikiwa bado nashangaa nikstukia ananinasa kofi na alipotaka kuongeza nikamwahi na kumshika mkono kisha nikamsogelea na tukawa tunatazamana kwa karibu zaidi,alikuwa anathema kwa jaziba kubwa na hapo nikamshudia akiangusha chozi na kufuatiwa na kilio cha kwikwi lakini kikubwa akaangukia kifuani pangu na kuanza kunipigapiga nikashangaa sasa alah! Hii ni kwa sababu ya ukahaba wake au kuna linguine?
“watamuua mme wangu watu wale….”alizungumza kwa tabu huku kilio kikichukua nafasi yake kwa wakti ule.
“mtu akilia,mwache alie hadi sumu ya hasira imwishe katika nasfi yake,ukimbembeleza utamwachia msongo wa mkubwa wa uchungu katika nasfi yake na jeraha halitamwisha” niliyakumbuka maneno ya mlezi wangu Kmanda Malebo.
Alizidi kulia huku akiwa amekiagamia kifua change kipana,na hapo nikajisikia toafauti katika mwili wangu kuna hisia ambayo sijawahi kuipata tangu nizaliwe lakini pia mwili wangu na nafsi yangu vilipata faraja kwa sababu tangu nizaliwe sikuwahi kukumbatiwa na mwanamke na hata kusogelewa tu sikuwahi na hapo nikamwona yule dada ni mtu tofauti katika dunia hii na nilijikuta wivu ukijengsa kwa huyo anaemwita mume wake,ama hakika amepata mwanamke asie na ubaguzi na ni mwenye upendo haswaa.
Alinyamaza kulia na mimi nikapata nafasi ya kumwambia jambo
“tuondoke sasa na utanambia kina nani wanaotaka kumuua mumeo’’ alinitazama baada ya kumwambia maneno yale na punde akageuka na kuanza safari kimya bila kunijibu na mimi nikamfuata kwa nyuma.
*******
Ilikuwa ni nyumba kubwa na kulikuwa na geti,na hapo ndipo safari yetu ilikomea na binti yule ambae sikumjua jina hadi muda.
Aligonga geti mara mbili hivi kisha akatulia.punde mlango ukafunguliwa na kijana mdogo yapata miaka kama kumi hivi na alitukaribisha ndani.
Wakati tunaingia nadni ya uzio wa nyumba ile ndipo nilipopata maswali mengi yasio na majibu kuhusu msichana huyu alienifikisha hapa.
Ilikuwa ni nyumba nzuri ya thamani japo ilionesha imejengwa miaka mingi huko nyuma lakini bado ubora wake ulionekana,si hivyo tu palikuwa na gari mbili mpya zilizoonesha zimenunuliwa miaka ya karibuni na ni za garama kubwa zile gari,mbali na hayo yote kubwa ni kuhusu huyu dada mbona uwezo wa hapa kwao haufananii na kumshawishi yeye akajiuze nahapo nikapata shauku ya kutaka kujua kuna nini nyuma ya yote haya.
Yule dada alinikaribisha ndani,tulipoingia ndani bado mshangao wangu ulibaki pale pale kwa sababu pale ndani kulipmbwa na samani nyingi za kisasa,huku kukiwa na meza moja ya vioo ikiwa imezungukwa na sofa kama tatu hivi.
Yule dada alinikaribisha kwenye sofa moja wapo huku yeye akiniaga ya kuwa anaenda kuoga kwenye moja ya bafu zilizokuwamo ndani ya nyumba ile,huku mimi akiniacha pale sebuleni na yule motto alietufungulia mlango.
Nikiwa hapohapo nimekaa nikajaribu kutazama rangi iliotumika kung’arisha nyumba ile ilikuwa ni rangi ya bluu bahari,nilizidi kutazama ufundi wa fundi yule aliepaka rangi mle sio siri ni mtu aliejua anafanya nini kwenye kazi yake.
Nilizidi kuutazama ukuta ule lakini kuna la ziada lilinivutia kwenye moja ya kuta zile,mchoro,kulikuwa na mchoro wa kama ua hivi leneye majani matatu,lakini ua hili niliwahi nimewahi kuliona kwenye moja ya vitabu vya kamanda Malebo,lakini pia nimewahi kuliona kwenye moja ya maeneo niliopita na hapo kumbukumbu ijkanijia ni kule kwenye kambi ya E.Musaza wakai nikiteswa na nilipotazama pembeni nikaona ule mchoro lakini sikuutilia maanani maana nilikuwa kwenye maumivu makali sana wakati ule lakini sasa naanza kupata mashaka juu ya ua hili kwanini lionekane sehemu kama hizi na kwanini lichorwe kwenye kuta,lakini kama ni hivyo inaaman kwamba huku kote aliwahi kupita kamanda Malebo.
Wasiwasi ukanijaa hasa nilipokumbuka kuhusu usalama wa kamanda Malebo ambae sikujua yuko wapi hadi wakati huo na kimsingi ndie amenifanya nije kumtafuta kwenye hii nchi ambapo kiasili ndo nilikotoka.
Na kama alitekwa nay eye ina maana aliteswa pale nilipokuwa mimi lakini pia hata hapa aliwahi kupita pia,lakini yuko wapi huyu mtu,nikashindwa kupata jibu kwa wakti huo na hakuna mtu aliekuwa tayari kunipa hilo jibu.
Nikanyua kichwa change baada ya kuwa kwenye tafakuri ya muda mchache na hapo macho yangu yakanasa kwenye picha kama tatu zilizokuwa zimebandikwa ukutani,ikabidi nisimame nakuziendea ili niweze kuziona kwa karibu zaidi na nijiridhishe na kile nikiaonacho.
Kweli macho yangu hayakunidanganya zilikuwa ni picha tatu nakila picha kulikuwa na watu wawili ninao wafahamu.
Picha ya kwanza inaonekana ilipigwa maeneo ya hoteli ama sehemu yenye kufanana na hivyo na picha hii ilimuonesha kamanda Malebo na kiongozi wa nchi ya kongo miaka ya 1987 ndugu Mobutu wakiwa wameketi kwa pamoja na wakifurahia jambo,lakini hawakuwa peke yao walikuwa n mtu mwingine aliekuwa kavalia suti safi kabisa na tofauti na wenzie huyu yeye hakucheka na mguu wake mmoja alikuwa ameuweka juu ya mwingine.
Picha ya pili pia ilipigwa eneo lile lile ila tofauti yake ni kuwa watu hawa wote walicheka lakini pia kiongozi yule wa Zaire ama kongo hivi sasa,yeye alikuwa amevaa kofia ama kibandiko chake cha chuichui na miwani mikubwa ilioficha macho yake.
Picha ya tatu ndio ilionichanganya zaidi ilikuwa imepigwa na watu wawili tu na hapa walionekana wakiwa nje ya eneo zuri na la kuvutia,alikuwa ni kamanda Malbo na yule mtu wa aliekuwa amevaa suti katika picha mbili za mwanzo,lakini nilipojaribu kuichunguza vizuri picha ile nikaliona ua nyuma yao na lile ua lilikuwa sawa na lile ua nilionalo kwenye michoro ile ilioko kwenye kuta na vitabu baadhi lakini ua hili lenyewe lilikuwa limeongeza tawi moja na hivyo kuwa na matawi manne
Nilizitazama picha zile lakini sikupata jawabu la kujua ni kipi hasa kitajijenga katika akili yangu na mwenendo mzima wa hili liloko mbele yangu.lakini kuna swali ni lazima nijiulize ilikuwaje kamanda malebo awepo pale ikiwa ndie alikuwa mlinzi mkuu wa rais wa wamu ya pili bwana Hussein mwinyi ama mzee waruksa,sikupata jibu na kwa nini hii picha ipo katika nyumba hii.
 
‘we mkaka’’ niliitwa na nikanyanyua macho yangu kwenda kwenye ile sauti ilioniita,alikuwa ni yule dada lakini muda huu alivalia vazi la kanga tu iliokuwa imefungwa kuanzia kifuani na kushuka chini,pia laikuwa maesimama huku mkononi akiwa kashika kikombe cha maji.
Alipoona namtazama bila kusema kitu,akapita moja kwa moja hadi lilipokuwa sofa moja wapo mle sebuleni na kukaa huku mguu mmoja ukiwa juu ya mwngine na kumfanya upande mmoja wa paja lake uonekane vyema na hpo nikajikuta nameza mate kwa uchu lakini sikutaka hisia hizo zinaitawale.
Nikaachana na zile picha nikarejea na kukaa kwenye sofa pia na kubaki tukitazamana na yule dada ambae muda huo alikuwa anatoa kikombe mdomoni na kukiweka juu ya meza ya kioo iliokuwa pale.
‘unaitwa nani na kwanini umnafanya biashara ile hatari ikiwa unamaisha mazuri kabisa hapa nyumbani kwenu’ nikaamua kumuuliza na kabla hajanijibu nikaona anaelekeza jicho lake upande wa nyuma ya sofa lile nililokuwa nimekalia hivyo kunifanya na mimi nigeuke nyuma na hapo nikapata kuiona picha nyingine ambayo mimi sikuwa nimeiona hapo kabla.
Picha hii ilikuwa inawatu wawili wazima na watatu alikuwa ni Mtoto.
Picha ile nilipoitazama vizuri niliona mmoja ya wale waliopo mmoja ni huyu mwanamke na mwingine alikuwa ni kijana yapata umri wangu hivi na walikuwa na furaha huku wakiwa wamempakata motto kwenye miguu yao.
Nikarudisha macho kwa huyu binti na nikamshudia akiwa bado macho yake akiwa ameyaelekeza kwenye ile picha lakini cha zaidi alikuwa atiririkwa na machozi na aliporudisha macho kwangu akashusha pumzi nyingi kwa wakti mmoja na akaushusha mguu mmoja chini hivyo akawa kaka sawa na kuihifadhi vyema hazina yake na akaanza kjibu maswali yangu,lakini kabla hajaendelea zaidi akamtazama yule kijana aliekuwa kakaa pale sebuleni pamoja na sisi na akamwonyesha ishara na yule kijana akatoka hivyo kumpa huru zaidi wa kuzungumza.
“Huyo umwonae ni mume wangu anaitwa Disuza na mimi naitwa Zamda’’ alisema kisha akameza mate na kunitazama mimi napo akaniuliza
“unaitwa nani na kwa nini upo hapa bukomba.’’
Nikaamua kumjibu “naitwa James,hapa bukomba nipo kwa kazi moja ya kumtafuta mzee wangu tuliepotezana miaka mingi sana lakini kabla sijaendelea naomba unambie zaidi kuhusu familia yako” nikaamua kumjibu kisha kumrudishia yeye mpira aendelee kusema pia.
“Mume wangu alikuwa ni kijana mtafutaji sana,na moja ya malengo yake yalikuwa ni kuwa mwanasiasa siku moja,hapa nyumbani tulikuwa tunaishi na babu yake ambae ndie yule unaemwona kwenye picha ile akiwa amevaa suti.’’ Alivuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa mkupuo kisha akaendelea
‘muda wa kama miaka miwili hivi tulikuwa tukitembelewa na wageni wa ajabu ajabu ambapo walikuwa wanamlenga babu na kila walipofika babu hakutaka Disuza ashiriki maongezi yao na hapo ndipo udadisi ukaanza kujengeka kichwani petu kuhusu mienendo ya babu na watu wale.Disuza alipojaribu kuuliza babu aliishia tu kuwa mkali,lakini utata ulianza kuibuka hapa nyumbani baada ya kutembelewa na mwanajeshi mmoja wa jeshi la wananchi wa Burundi,mwanajeshi huyu alikuja kwa mara ya kwanza kiungwana tu walizungumza na babu kisha akaondoka lakini mara ya pili alipokujaalikuja kishari sana na hapo alikuwa ameongozana na watu ambao hawakuwa wanajeshi ila walikuwa ni vijana wenye asili ya kisomali na mara zote walikuwa wakijifunga skafu shingoni mwao..’’
Nilistuka baada ya kusikia kuhusua hao watu wanaovaa skafu na wenye asili ya kisomali,na hapo nikaaa sawakwenye sofa ili nisipitwe japo na neon hata moja juu ya watu hao na huyo mwanajeshi na dada yule alikuwa anaendela kusema
“……..walifanya upekuzi mwingi sana hapoa ndani na nilipojaribu kutetea niliambualia kupigwa na vitakao vya bunduki huku wakimwacha babu akiwa hoi kwa kipigo na waliondoka na nyaraka kadhaa muhimu za mzee yule na hata Disuza alipokuja kutoka kazini kwake alijaribu kutaka kulipeleka swala lile kituo cha polisi lakini haikusaidia,babu alikataa kabisa,na zaidi ya hapo aliomba awasiliane na mtu alieko Tanzania na kweli waliwasiliana na hazikupita siku mbili akaja mzee mmoja hivi ambae alijitambulisha hapa kwa jina la kamanda malebo mwanajeshi mstaafu na siku hiyo hiyo waliondoka hapa wakiwa na mabegi ya kuhifadhia nyaraka na hwakurudi tena laikini yule mzee wa Tanzania kabla hajaondoka alichora pale..”
Alinisontea kidole kuelekea kule kulipokuwa na mchoro ule wa majani matatu na hapo nikatambua kabisa alikuwa nafanya vile makusudi,laikini kusudi gani hili ikiwa hajui kama mlengwa wa kusudi lile atafika katika maeneo yale,lakini pia hii ilinipa picha kuwa kamanda malebo,alipeleke
Wa kwenye kile chumba cha mateso kule kambi ya jeshi na hivyo bila shaka yule mwanajeshi anaezungumziwa hapa ni yule luteni usu E.Musaza wa kambi ya Rwaruzambo,alienipa mateso makali kisha wakaamua kuniuza kwa wachimba madini ili wanitoe kafara.
Lakini swali lilibaki kwanini kamanda Malebo anatumia huyu mchoro kila sehemu anayopita na je huko aliko yuko salama au kuna jipya limemkuta,nikajikuta napatwa na hasira iliochanganyika na woga juu ya maisha ya mzazi wangu mlezi.
‘Na mumeo!!’ nilijikuta nauliza kizembe kabisa huku akili yangu ikiwa tayari imeanza kupoteza uwezo wa kufikiri kwa kina juu ya matukio yale.
‘baada ya kupotea kwa babu na mgeni wake mume wangu aliamua kufuatilia kwenye vyombo vya dola lakini huko akaishia tu kuambiwa upelelezi unaendelea na kabla hata polisi hawajaja kutupa mwongozo wa uchunguzi wao wakaja tena wale wavaa skafu na wakamchukua mume wangu na kuondoka nae na hadi leo hajawahi kurudi,mume wangu ndie alikuwa kila kitu hapa lakini tangu apotee hata pesa ya kula ikakosekana na hivyo sikuwa na njia yoyote zaidi ya kufanya kile ulichokiona nafanya’
Alimaliza kuzungumza huku sasa akianza kuangua tena kilio na mimi nilibaki namtazama tu mwanamke huyu,wakati akijifuta machozi akatumia upande mmoja wa kanga huku upande mwingine ukiwa umeshikwa kwa mkono wa kushoto ili kuyasitiri matiti yake,na hapo nikakaza macho ili kuona kile nilichokuwa nimekiona kama kipo sahihi,nikatazama tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom