Nikafanya jitihada za kujitoa pale mbele kwenye kiti cha dereva na kufungua mlango,lakini kabla sijafungua mlango tayari wale watu wenye skafu nao wakawa wamefika na niliposhuka tu chini nikawa nimeamuriwa kunyoosha mikono juu na muda wote huo damu zilikuwa zinanichuruzika kama maji na kulowesha uso wangu kiasi cjha kunifanya nisione vizuri maana macho yalkuwa yameingiwa na damu tayari.
Nikiwa vile vile nimenyoosha mikono juu nikapata kumshuhudia mtu mwembmba na mrefu huku akiwa anapua ndefu kama ya mr bean,lakini pia alivaa viatu vya moka na suti ya bluu lakini pia koti laile suti lilikuwa fupi kuliko shati alilovaa ndani,na nilipomtazama miguuni tena nikaona suruali yake ikiwa fupi vile vilen na kufanya soksi zake zionekane nahapo nikashindwa kuelewa alivaa vile kwa ajili gani au ana maana gani kuvaa suti fupi kumliko yeye.
Ikabidi nimwite Kisuti mtu yule.
Alisimama mbele yangu huku akiwa ameweka mikono mfukoni,nahapo nikaona tena mikono ikiwa haijaenea kwenye mifuko hiyo ina maana mifuko ni mifupi pia,aliniacha hoi mtu yule.
Nikiwa mikono juu alinisogelea hadi karibu kabisa na uso wangu kisha kwa kutumia kidole chake gumba akanifuta damu iliokuwa jichoni kwangu kisha bila kufanya jitihada za kuindoa kwenye mikono yake akarudisha mfukoni nakisha akacheka kicheko chembamba huku akipandisha mabega juu na hapo nikashuhudia mtu mmoja akija kwa kasi pale nilipo na sikujua amenipiga ngumi au teke ila nilishuhudia tu giza likianz kuufunika uso wangu na nilipofnaya jitihada za kujizuia nisifumbe macho nikajikuta nashindwa nahapo nikasikia kichwa kizito na kilichoendelea pale barabarani sikjua tena.
************
Nilisikia mlio wa filimbi kwa mbali sana,nikafanya jitihada za kuyafumbua macho yangu nahapo nikashududia paa la nyumba ile,huku kukiwa na taa iliofungwa kwa juu,macho yangu yakahamia pembeni yangu napo nikashudia miguu ya mtu akiwa amekaa ila kutoka na nilivyokuwa nimelala pale sakafuni sikupata kumuona vizuri hivyo ilinipasa nisimame.
Nikajiinua kutoka chini pale na kisha nikazungusha macho yangu pande zote za chumba kile na sikupata kuona kitu kingine zaid ya yule mtu aliekuwa ameinama na kichwa chake akiwa amekiweka juu yamikono yake ailiokuwa imepata igemeo kwenye magoti ya miguu yake.
Nikakaa chini na kujipa muda wa kukumbuka yaliotokea nyuma.
Nilipokwisha kukumbuka mambo yalivyokuwa ikabidi nisimame ili kujinyoosha viungo vyangu,lakini nilipokuwa nimenyoosha mikono juu nikasikia maumivu makali juu kidogo ya kwapa langu ikabidi nijitazame na hapo nikaona kimshono kidogo usawa huo wa mkono wangu.
Haikuwa kimshini hicho tu pia kulikuwa na bandeji niliokuwa nimefungwa kichwani ila yenyewe nilihisi ilitumika kuziba jereha langu nililolipata kwenye gari,lakini nililjiuliza hiki kimshono kidogo kina maanisha nini kwangu ama kwa nini kimewekwa hapa sikupata jibu.
Nijiweka sawa kwa kurukaruka kidogo kisha nikapiga push up kadhaaa na kujiwka sawa kimtindo,wakati nikifnaya yote hayo yule mtu alikuwa bado yuko vilevile na hapo nikashindwa kujua,amelala au ni pozi tu huku akingojea kitu flani lakini sikupata jibu na kwanini nihangaike kutafuta jibu wakati mtu wa kunipa jibu yupo.
Nikamsgelea na kumtikisa mara kadhaa hivi kisha nikasubuiri na punde nikaona ananynanyua kichwa chake na kunitazama.
Baada ya kunitazama nikagundua uso wake umepitia maswahibu makali sana na pia alikuwa amekata tamaa kabisa kuwepo duniani na macho yalionesha hana tumaini lolote katika nafsi yake.
Sikutaka kumsemesha kabisa nikaamua kumwacha tu na kugeuka ili niendelee kufanya mazoezi kwenye kile chumba tulichokuwamo
Roho yangu huwa ipo mbali na wasiwasi hasa pale ninapogundua adui ananitegemea mimi ili apate kile anachokihitaji hivyo sikuwa na shaka juu ya uhai wangu kabisa.
Nikaendelea kupasha misuli yangu huku sasa jasholikiwa limeanza kunitoka na hivyo kufanya kidonda change kilichokuwa kichwani pangu kianze kuuma,nikaona bora niachane na mazoezi yale na nikaenda hadi karibu kabisa na alipokuwa mtu yule na kukaa pembeni yake huku wote macho yetu tukiyaelekeza kwenye mlango mdogo uliokuwa pale chumbani na hakuna aliemsemesha mwenzie.
Baada ya muda wa kama dakika kumi za ukimya,nikamsikia yule bwana akishusha pumzi nyingi kwa mkupuo na hapo nikageuza shingo yangu na kumtazama,macho yetu yalikutana,lakini yake yalikuwa yanatoa machozi na hapo nikamkazia macho zaidi na nikaona yeye anaacha kunitazma na kurudisha macho yake kule tulikokuwa tunatazama mwanzo na kisha akasema.
“usishangae nalia,nalia kwa sababu siui kwa nini haki yangu ya uhuru imewekwa mikononi mwao nakuniacha nikiteseka bila kujua familia yangu inaishije huko nje,lakini pia babu yangu alienipenda nikampenda sijui kwa nini wamemchukua pia,mali ya yote wamenitesa ili niwambie kile nisichokijua kabisa.’”
Hapo akaacha kusema na kuanza kulia tena hivyo ikapaswa nimseme ili anyamaze.
‘hupaswi kulia ikiwa hujui utafanikiwa vipi kuurudisha uhuru wako na wa babu yako,lakini pia yakupasa uwe makini kwa kila ufanyacho ili kuurudisha uhuru wako,kulia hakutokusaidia,hebu nione mimi ni mlemavu wa ngozi lakini bado wananiweka matatizoni kila kukicha lakini sijawahi kutokwa na chozi kabisa’ nilimaliza kuzungumza na hapo nikaona ananigeukia tena nakuliita jina langu,nilishangaa lakini sikutaka kujipa muda wa maswali peke yangu ikabidi nimgeukie na nimuulize amenijuaje
“James nakufahamu kabisa,picha yako nilioneshwa na kamanda Malebo alipouja kumtembelea babu yangu mzee Niyonzima,lakini kubwa zaidi alinambia mimi na wewe ni mapacha na baba yetu ndie aneleta matatizo katika familia yetu hadi leo hii’
Hapo nikasimama nay eye akasimama na kunikumbatia na kwa mara ya kwanza chozi la furaha lilinidondoka,ahatimae nilikuwa nimekutana na ndugu yangu wa damu kabisa wa baba mmoja.
Nikajifuta machozi nakuendelea kulia kwa uchungu kwa nini sijakutana nae kwenye wakati wa furaha nakutana nae kwenye wakati kama huu,lakini pia nikakumbuka mke wake bi Zamda anaejiuza ili wapate chakula na watoto,hapo chozi likazidi kunimwagika na nikayaamini maneno ya kamanda Malebo aliwahi kunambia ipo siku niytaipata furaha ya raha na uchungu kama nikikutana na babu yangu ama pacha wangu na kweli ndicho kinanitokea wakati huu.
“Disuza” hatimae nilijikuta naongea peke yangu na kumfuta tena na kumkumbatia na hapo picha ya sura yake ikanirudia akilini ni hii sura niliona kule kwa mzee niyonzima.
Ili kuijihakikisha zaidi nikamfunua upande wa bega lake la kulia nikamkuta kweli ana ile tatuu inayoonesha kama makazi na tauu hii ni karibia sawa kabisa nah ii iliopo mwilini kwangu.
Disuza akanishika mkono na kuniongoz kwenda kukaaa na kuegemea ukutani kisha akaaanza kusema kwa uchungu sana huku akilia
“babu alinambia ya kuwa ulikuwa ni wakati mgumu sana kuamini ya kuwa baba yetu alimsaliti na kumwibia nyaraka kadhaaa za siri na kwenda kuziuza kwa wajerumani,nyaraka hizo alizipata wakati akiwa ndie afisa mipango wa kiongozi wa Kinshasa miaka ile,lakini pia alikuwa ndie afisa madini na mipango wa wizara ya Mobutu sessiseko.babu anasema baba alikuwa na rafiki yake mjerumani aliemshawishi kufanya hivyo na alimlipa pesa nyingi baada ya wizi ule na kila alipojaribu kumtafuta hakumpata baba yetu na wakati akitoroka alituacha tukiwa wadogo sana na mama yetu nae akliamua kutoroka na mpaka leo haijulikani wako wapi na wako pamoja au tofauti hilo halijulikani na baba hajawahi tena kukanya Burundi tangu alipofanya hivyo mwaka 1992”
Alinyamaza kuongea baada kuhisi pale mlangonikulikuwa na mtu anatusikiliza na alinionesha ishara name nikaona kivuli kikihama kwa kasi kutoka pale mlangoni na sikutaka aendelee kusema nmaana sikujua kwanini yule mtu alikuwa natusikiliza.
Kiukweli sikuwahi kutaka kumfahamu huyo baba yetu japo jina niliambiwa anaitwa Masulu lakini pia sikuwa nimeelewa hizo nyaraka zinahusiana nini na haya yanayotukuta hivi sasa,tulizungumza mengi nahpo nikajikuta nasahau machungu yote na tabasamu likjaa usoni pangukila muda.
Nilikuwa sijui ni muda gani hadi wakati huo,japo tulikadiria inaweza kuwa ni zaidi ya saa saba za mchana kulingana na mwanga uliokuwa umeingia mle ndani.
----------------------------
Tumbo langu liliunguruma na hapo nikahisi njaa ya wazi kabisa na nilipotizama alipojiegesha Disuza tayari alikuwa amepitiwa na usingizi,nikasimama kwa na kulekea tena mlangoni nikaanza kuupiga kwa nguvu kisha nikarudi kukaa.
Haukupita muda mrefu nikasikia sauti ya miguu ya watu ikija usawa wa kile chumba tulimo.