Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

Mkuu IBRA nandle LA wiki nzima hilo nimekutumia
 
Kama badle nishamuwekea tatizo ni nini?
 
Sidhani kama huwa anashindwa kuweka sababu ya bandle, siku zote anaweka kwa upendo wake tu, yeye pia ana mambo mengine ya kibinadamu! Tuvumilie tu atakuja!
Aliweka namba ya kuwekewa bandle ndo maana nikaweka mkuu
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 022

"Tokea niliposhikiwa bastola na walinzi wa Jimmy, nilishaamua kuachana nao. Nilishaamua kuondoka katika kile tulichokuwa tunakifanya. Nipo upande wako tokea pale ulipokoswakoswa kulipuliwa. Nilifadhaika sana kwa kushindwa kugundua kile kilichotendwa. Ulikuwa mpango wao na hawakupenda kunishirikisha. Kule kuuona ule mlipuko nikauona moyo wangu ukiingia simanzi. Nipo na wewe na nitakuwa na wewe mpaka mwisho wa hili. Lakini nina hofu, wanaweza kuniua Masimba." Aliongea Teddy akimuangalia Masimba. "Lakini nina hofu" lilikuwa neno lililojirudia kichwani mwake. Teddy alikuwa ana hofu, teddy alikuwa akiogopa, akiogopa kitu gani? Lilikuwa swali pekee kichwani kwa masimba. Hakuwahi kumsikia popote teddy akiwa na hofu ya kitu chochote. Aliipenda damu na kuyapenda mapigano. Hakuogopa kifo bali alikuwa akipenda sana kuua. Lakini kwa nini leo ana hofu? Hofi ya nini? Hofu ya kuuawa ama? Hilo likamfanya masimba amgeukie Teddy na kumuangalia. Macho yake peker yalijenga maswali lukuki kwenda kwa teddy. "Umeanza lini kuogopa teddy, umeanza lini kuwa muoga? Hukuogopa Tulipokuwa Syria, uje uogope hapa, tena kwa watu wasio na chochote kile. Unaweza kunieleza kile unachoogopa?. Teddy alimuangalia masimba kwa muda, alimuangalia kana kwamba ndio alikuwa akimuona leo. Kweli aliyapenda mapambano, hakuiogopa damu na hakukiogopa kifo. Lakini leo alikuwa akikiogopa kifo na kuiogopa damu. Alijishangaa na kutokujiamini. Teddy leo alikuwa akikiogopa kifo? Lilikuwa jambo pekee lililokisumbua kichwa chake. "Masimba ingawa unawaona watu hawa si lolote lakini ni hatari hasa kwa watu ambao wapo nyuma ya mzigo uliouchukua. Mtu huyo alie nyuma, ndiye mtu pekee ninaye muogopa. Anaweza kuamua chochote kwetu na tukapotea. Unadhani ni mtu gani mwenye uwezo wa kuruhusu mzigo kama ule uchukuliwe kirahisi? Unadhani na afisa gani mwenye uwezo huo? Aliye nyuma ya tukio hili mi mtu mkubwa. Tunaweza kupotea endapo hatutakuwa makini. aliongea teddy akiendelea kumuangalia masimba. Hata masimba alinyamaza kwanza akimuangalia Teddy. Alizidi kushangazwa na uoga wa mwanamke huyu. Uoga ambao hakuwahi kuuonyesha huko mwanzo. "Teddy tulipokuwa Syria tulikuwa tukipambana na watu gani? Tulipitia mangapi Teddy? Ni mara ngapi tumenusurika kifo? Mbona huwa muoga kama leo hii? Hiki unachonionyesha leo ni tofauti? Tuachane na uoga nataka kumjua huyu mtu. Nataka kumfahamu usiku wa leo ama kesho. Nataka nimfahamu kwa njia yoyote. Suresh ndio atakaye niambia. Lakini hata wewe naamini unamjua mtu huyo. Inaonyesha kuna kiapo umekula cha kutokutoa siri nio maana unaogopa. Lakini kama wewe unashindwa kuniambia mimi kwa kuhofia kuuawa, basi mimi nitauawa kwa kumtafuta na kumjua huyu mtu." Aliongea masimba huku akionyesha kutokuwa na masihara. Teddy akachwa katika tafakuli zito, ni kweli aliogopa na kuhofia. Ni kweli alimuogopa mtu huyu, lakini atakuwa tayari kumuona masimba akiuawa kwa sababu ya woga wake? Yupo tayari kukisaliti kiapo kwa ajili ya uoga wake? Hapana! Hapana! Alijikuta akitamka maneno hayo kwa sauti kubwa, sauti iliomtoa kwenye uoga na kumpa ujasiri. Muda mfupi alikuwa akibembea kwenye kifua cha Masimba. Alikuwa tayari kupambana bila kuhofia. Na moyo wake ulimtuma kufanya hivyo pasipokuogopa.

*******
Moshi mzito ulikuwa angani ukipita na kupenya kwenye matundu ya watu mbalimbali kabla ya kutoka ndani ya chumba kile. Chupa tatu za Jack Daniels zilikuwa mezani zikitekezwa kama sio kuteketea. Watu wanne walikuwa wameizunguka meza hiyo wakiendelea kuburudika tani yao. Mwanaume alikuwa mmoja lakini wanawake walikuwa watatu. Kila mmoja alikuwa ana uhuru wa kuushika mwili wa mwanaume yule pasipo na masharti yoyote. Mwanaume naye alikuwa akifurahishwa na vitendo vyote. Akicheka na kuongea hili, punde akamuona mtu mmoja akingia chumbani hapo pasipo na taarifa. Mtu huyu alikuwa akionekana akivuja jasho sambamba na mavazi yake kuchafuka kwa damu. Hilo likamfanya kinywaji kilichopo mdomoni kumpalia. Akaruhusu mshangao machoni mwake, mshangao ambao haukudumu hasa pale mtu yulr alipoanza kuvuta hatua kusogea pale alipo. Bado macho hayakuweza kuupoteza kabisa mshangao ule. Hata pale mtu yule alipoifikia meza yake ndipo alipogundua kama kuna watu ambao hawakupaswa kuwepo pale. Akawapa ishara wanawake wale watoke. Hata wao hawakuchelewa. Baada ya kutoka kwa wanawake wale, sasa alikuwa akimtizama mtu huyu. Hakuwa mwingine bali alikuwa Jimmy
Alikuwa Jimmy akionyesha kulowa damu.

Jimmy alikuwa na hofu kubwa Moyoni, machoni na hata uso wake uliongea hofu. Alikuwa akitetemeka kanakwamba ametoka kunyeshewa mvua, alitetemeka kanakwamba ndani ya chumba kulikuwa na baridi kama ya Arusha na Hata mbeya. Hilo lilikuwa geni kwa Suresh, hilo lilikuwa geni machoni mwa kijana huyu mwenye asili ya India. Jimmy amelowa damu na tena alikuwa akitetemeka!! Jimmy leo alikuwa na hofu? Jimmy leo alikuwa akiogopa? Hilo likawa gumu kwa mhindi yule kulikubali. Bado mhindi yule alimuangalia Jimmy Kwa wasiwasi. Akainua glass na kupiga mafunda matatu kisha kuirudisha pale pale. Alimjua Jimmy kindani, alimjua jimmy kimipango na hata kimapigano, jimmy hakuwahi kumuogopa mtu, hakuwa kutetemeshwa na mtu, leo hii Jimmy alikuja akitetemeka tena huku amelowa Damu. Nani amelifanya hili? Teddy? Hapana! Teddy hawezi kufanya kitu kama hiki. Bado hakutaka kuamini kile alichokuwa akikiwaza. Maswali yake mengi sana yalikosa majibu kwa kuwa mtu mwenyewe wa kumjibu alikuwa kimya. Alikuwa kimya kama bubu ama zuzu. Hilo likamfanya Mhindi yule kusimama. Akapiga hatua huku akiyumba huku na huko kumfuata Jimmy. Sasa alimkaribia kwa karibu sana. Akamuangalia kwa umakini wa hali ya juu. Akashangaa kumuona Jimmy akiwa hana hata kovu, akiwa hana hata jeraha la kucha. Hilo likaendelea kumshangaza. Hilo likaendelea kumuweka njia panda. Akataka kuinua mdomo kuongea kitu, lakini hakufanikiwa kufanya hivyo kwani muda ule ule Teddy alikuwa akiingia pale katika mwendo wa twiga nyikani. Alikuwa akitembea na kunesa huku na kule, macho yake yakiangalia hapa na kucheki kule. Ulikuwa mshangao wa mhindi yule uliomshtua Jimmy na kumfanya naye ageuke kuangalia kule mlangoni.

Ndio aligeuka, na akakiona kilichopo nyuma yake midomo ikamkauka jimmy. Hofu ikaongezeka maradufu. Akataka kurudi nyuma lakini akajikuta miguu ikiwa mizito. Miguu haikuweza kusogea popote. Yule mhindi mkono ulishashuka tayari kwa kuichomoa bastola yake. Lakini jicho alilotazamwa na Teddy,. Likaufanya mkono wake uondoke hapo haraka. Teddy akaendelea kutembea zaidi na zaidi, alikuwa makini kwa kila hatua aipigayo. Masikio yalikuwa yakinasa kila mchakato hata kama ulikuwa wa sisiminzi. Akasimama hatua mbili kutoka waliposimama Jimmy na Suresh. Macho yake yalikuwa yakimtizama mmoja mmoja pasipo kuongea chochote kitu. Bado Mhindi yule akashangazwa na hali ile, bado Mhindi yule hakuamini kama Teddy anaweza kufanya kile anachokifanya pale.

"Nimekuja kuuliza mgao wangu kutoka kwenye ule mzigo." Aliongea teddy akizidi kuwatizama. Licha ya hilo swali lakini hapakuwa na aliemjibu. Wote walikuwa kimya.

"Naondoka siku nitakayokuja tena naomba niukute mgao wangu, kinyume na hapo nitaondoka na Roho zenu." Baada ya kuongea maneno hayo teddy akageuka akiondoka kwa mwendo ule ule. Mpaka unapotelea mlangoni, si Jimmy wala Suresh aliyeongea kitu. Wote walikuwa kimya. Jeuri ya Teddy ilipitiliza. Uso wa Jimmy sasa Ulibadilika kabisa. Mishipa ya Hasira ilionekana waziwazi.

"TEDDY LAZIMA UFE, LAZIMA TUKUONDOE HAPA DUNIANI." akanong'ona Jimmy Kwa Sauti ya Chini.

"Yeah, lazima afe lazima tumuue. Kinyago tulichokitengeneza wenyewe hakiwezi kututisha. Sasa ameitangaza vita na hatafika popote tutamzima.
 
TANGAZO MUHIMU

HARAMBEE KABAMBE iitwayo
MWEZESHE MWANDISHI KUYAFIKIA MALENGO.

Kwa wale wote wadau na wapenzi wa simulizi, Mwandishi wenu nakuja na ombi la kunichangia kiasi cha pesa ulichonacho ili kuniwezesha kutimiza ndoto yangu. Nimechukua maamuzi haya baada ya kuwahudumia kwa kuwapa simulizi zangu kwa njia ya mitandao zaidi ya miaka3 bure.

Mtoto wenu, kinama mwenzenu, kaka yenu , nimeona ni wakati wangu mwafaka wa kupiga hatua katika fun hii ya uandishi. Haja yangu kubwa ni kutoa vitabu na kuvisambaza,lengo likiwa ni kuwafikishia ujumbe wa kuelimisha na kuburudisha watu wengi ndani nan je ya Tanzania pia nami nipate ridhiki.

Sikumoja nilipata email toka OMAN kuna mtu aliniambia anafatilia sana simulizi zangu kwa njia ya midandao, lakini kwakuwa ninatabia za kuziondoa baada ya muda alitamani sana nimtumie vitabu kupitia ndugu yake ambaye yupo TZ. Niliumia kuona napoteza fulsa ile ya kujiingizia kipato lakini pia kuitangaza Lugha yetu ya Kiswahili. Ninapata simu mara kwa mara za watu kuhitaji vitabu vyangu ila sina. Hata hivyo niliamini muda wangu ulikuwa bado.

Wadau wa kundi hili la PUMZISHO LA UBONGO ninaimani mengi nimeeleza kwenye MAKALA yangu niliyopost ndani ya kundi, kama hujaisoma basi nakuomba itafute na uisome. Hakika utajifunza mengi.

Wadau, hakuna kidogo kwangu,mchango wako wowote angalau kuanzia Tsh. 500/= na kuendelea unaumuhimu mkubwa sana kwangu. Naomba tuhamasike ili nasi waandishi wachanga tupige hatua na kufika walipo waandishi wakubwa. Tazama leo Shigongo amekuwa balozi wa timu ya vijana TZANZANIA ili kukusanya pesa za kuendesha shughuli zao. Ni wazi anaumuhimu katika taifa. Lakini ukifatilia utagundua hakuanza yeye mwenyewe bali aliwezeshwa akainuka na sasa anategemewa hadi na taifa kwa namna moja au nyingine.

Tazama wasanii mfano Diamond, leo amekuwa na nafasi kubwa katika taifa kwakuwa aliwezeshwa. Ingawa wewe haukumpa pesa moja kwa moja ila eidha uliingia kwenye show yake, uli vote alipokuwa anawania TUNZO, au kununua kazi zake kama WCB kupitia wasafi.com wanavyouza sasa. Hii yote inamaanisha mchango wako wewe mdau ndio mafanikio ya yule umpendaye.

Ibrahim Masimba naomba nichangie kwa njia kuu mbili:
Ukiwa umeguswa na kazi zangu naomba toa mchango wako wowote ili kufanikisha hili
Unaweza nichangia pia kwa kulipia kila ninapotangaza kuuza simulizi yangu kupitia mitandao ambazo zitakuwa zinapatikana kwa bei rahisi sana.

TUTAMBUE HESHIMA YA MTUNZI NI KUWA NA NAKALA ZA VITABU, KAMA ILIVYO KWA MSANII WA KUIMBA AMBAPO HESHIMA HUJA KAMA ANA ALBUM.

Tuma mchango wako kwenda namba moja tu. TIGO PESA 0675191162
M PESA 0745373585
HALO PESA 0628969272

*************************

KUMCHANGIA MWANDISHI NI STAHIKI KWAKUWA HUFANYA KAZI KWAAJILI YAKO.
*************************

Ahsanteni .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom