NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 091
punde alikuwa akitembea sambamba na kijana hiyu. Kijana ambaye hakujua mtu aliye hapo nyuma yake alikuwa nani. Ni muda huo huo wakati hawa wakitembea sambamba wakiingia ndani, ni wakati huo ambao Veronica Alikuwa akiinuka naye akaongoza kuelekea ndani alikoambiwa aelekee. Bastola zake mbili zilikuwa sehemu fulani katika mwili ule. Alikuwa akitembea akionyesha kutokuwa na wasiwasi. Kuonyesha kutokuwa na kitu chochote cha kuhofia. Veronica alitembea kanakwamba alikuwa ndani ya sebule ya nyumba yake. Hakuogopa wala hakuwa na mashaka, achilia mbali hofu. Hakuiona hofu, hakuuona Woga. Alikuwa tayari kwa chochote kile. Aliivuta miguu yake akizihesabu hatua zake, macho yake yalikuwa mbele yasimpotee yule kijana aliyeambiwa amfuatilie. Alihakikisha hafanyi makosa kwenye hili. Ni wakati akiangalia akamuona mtu akijiunga kwenye msafara wa kijana yule. Akitembea nyuma kidogo ya kijana yule. Hilo likampa fikra katika kichwa chake, mstari wa uhatari ukapita kichwani na tabasamu likashuka usoni. Naam! Alikuwa akiangaliana na Mwanaharamu, Mwanaharamu ambaye waliachana mahali akimuaga kuwa anakwenda kumfuatilia mtoto wa Rais. Lakini dakika hii alikuwa akimuona hapa tena akiwa sambamba na Mshenga wake. Mshenga ambaye alitumwa kama kiunganishi na mtu huyu ambaye walimhitaji na kuihitaji Roho yake. Hilo likamshangaza Akiamini kuwa Binadamu huyu aliyelaaniwa Anaweza kuharibu mipango yake. Lakini haikuwa Hivyo, punde akamuona Kijana yule akiingia kwenye chumba kimoja kati ya vitatu vilivyosehemu moja. Lakini mwanaharamu akapita akikifuata chumba kingine. Alama ya dole gumba katika kificho likauzindua Utimamu Wa Veronica. Sasa Alitambua kuwa Walikuwa katika kazi Moja. Ni hatua tano kutoka chumba alichoingia kijana yule pua zake zikainasa Harufu ya Manukato. Kabla hajajua nini kinafuata akauona Mkono wa mtu ukikishika kiuno chake. Mtu huyu hakuishia kukishika kiuno tu, bali mkono ukashuka kidogo na kuligusa paja kabla ya mkono kuanza kupanda juu kuliko kosa Adabu. Veronica Hakuonyesha Kujali. Ndiyo kwanza aĺikuwa amejilegeza huku akijitahidi mkono ule usifike kule ambapo alihifadhi Bastola yake. Mtu huyu akamlazimisha watembee wakielekea katika chumba kile. Mlango ulikuwa wazi na alitakiwa aingie Ndani. Veronica Hakusita. Alimhitaji Jimmy na Aliihitaji Roho ya Jimmy. Akamtii kama Ngamia anavyotii pale anapotakiwa kuchinjwa. Hata pale mkono wa Jimmy ulipokuwa Unagusa urembo ule wa Kiafrika uliopangiliwa kiunoni. Bado Veronica Hakuleta fujo na Hata kutulia. Wakaingia ndani kisha mlango ukasindikwa na kufungwa kwa Ndani. Veronica Akajikuta Akitupwa Kitandani na kwenda kuangua Chali. Miguu yake haikutaka tena kuzuia kile ambacho Jimmy alikitaka. Alihitaji kumlegeza Jimmy Hatimaye kumuua. Punde akamuona Jimmy Akiuvua mkanda wa Suruali yake. Punde akaiona Suruali ya Jimmy ikifika Magotini. Veronica Bado Alijigeuza Huku na Kule. Bado alikuwa akiichanua Miguu yake kumtega Jimmy. Jimmy akavutika kwa paja lile la Veronica. Macho yakamtoka na tamaa kumuingia. Veronica alikuwa akimsoma kwa Umakini Mkubwa. Hakutaka kufanya kosa lolote. Alitambua kosa lolote ambalo angelifanya lingemghalimu Maisha Yake. Alihitaji kumuua Jimmy katika Namna Impendezayo. Aina ambayo aliipenda yeye. Bado alikuwa amejilegeza akimsubiri Jimmy apande kitandani. Jimmy Naye akasogea na kujilaza kwa pembeni.
Lakini katika namna ambayo hakuitariji. Akauona Mkono wa Jimmy Ukiwa na kitu cha moto. Jimmy alikuwa na Bastola mkononi. Bastola ambayo tayari mdomo wake uligusa mbavu za Veronica. Hilo likaonyesha kumgutusha Veronica. Akili alitaka kuanzisha labsha. Lakini hilo akalipinga, alihitaji utulivu. Alihitaji kuutumia mwili wake kumpumbaza Jimmy. Akatulia Tuli akimuangalia Jimmy kwa macho yake malegevu. Macho ambayo yalikuwa na uwezo wakumlevya wa Aina Fulani. Macho haya yalifuatiwa na mkono wa Vero kuushika mkono wa Jimmy na kuupeleka katikati mwa Mlima usambara.. mkono wa Jimmy ukatulia hapo katika namna ya kucheza na mlima huo. Mlima ambao ulipendezeshwa na kizibo kile cha Asali kilichofiti. Veronica Alitaka kuhakikisha Jimmy anakamatika kiurahisi. Akaulazimisha mkono ule uendelee kutalii mahala hapo. Ukigusa hiki na kugusa kile. Punde mkono ule wa Jimmy ukaanza Kukishusha kizibo kile Cha Asali. Bastola bado ilikuwa imenyooshwa kwa Veronica ambaye bado alikuwa katika uigizaji mkuu. Uigizaji wa Kupendezwa na kilichotendeka. Ndani ya Dakika moja Tayari nguo ile ilishafika Miguuni. Sasa Jimmy alikuwa akipanda kifuani Huku Bastola Ikiwa kwenye paji la Uso la Veronica. Jimmy hakuonyesha tabasamu licha ya kuonyesha tamaa. Wakati akiishusha bukta yake Tayari kwa kitendo kinachofuata, mlango ukagongwa. Jimmy Akageuza Shingo.... Hilo lilikuwa kosa kubwa, kosa ambalo hakutakiwa kulifanya katika maeneo yale. Kitendo cha kugeuka kilimpa nafasi Veronica Kuachia mateke matatu ya haraka Ambayo yalimtupa Jimmy Huku na Bastola yake kule. VERONICA akachupa na kutua Chini. Mkononi Alikuwa amekamatia Bastola Akitembea Taratibu pale alipoangukia Jimmy ambaye kwa wakati huo alikuwa Akijizoazoa. "Jimmy Lambert NSA special Agent.. Kutana na Veronica Senka Mafia Special Agent. Aliongea Veronica Akitembea taratibu ndani ya Chumba kile. "Uroho wenu na tamaa zenu ndio zimewafanya mkubali kuwaharibu vijana wengi wa Tanzania. Tamaa Yenu ya kumiliki utajiri mkubwa ndio umewafanya hata watu waliopewa Madaraka makubwa ya kuongoza nchi. Kufanya mambo ya ajabu yasio na Ubinadamu. Mtambo ambao uliletwa hapa nchini na serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wenu sambamba na Nyie Vibaraka. Umeharibu Mamia na maelfu ya Vijana hapa nchini. Sasa nimekuja hapa kuichukua Roho Yako. MASIMBA ndiye amenituma kujakuichukua Roho yako. Aliongea Veronica Huku Bastola ikiwa imetangulia mbele. Hakuwa na masihara na wala hakuonyesha chochote usoni. Uso wake ulibeba matamshi yake. Uso wake ulibeba kile ambacho alikuwa akikinena. Jimmy Aliyekuwa Amesimama akitweta hakuwa na namna. Alikuwa akikiona kifo machoni mwake. Alikuwa akikiona usoni na hata machoni kwake. Mdomo wa bastola ulikuwa ukimtizama yeye. Bastola ambayo ilikamatwa vizuri mikononi kwa Mtu huyu. Wakati Veronica Akiendelea kumuangalia Jimmy, Taratibu Akamuona Mwanaharamu Akiingia taratibu. Aliingia katika aina ambayo ilimshangaza na kumuogopesha Jimmy. Bila kutegemea Jimmy akajikuta akiropoka pale macho yake yalipotizamana na Macho ya Mwanaharamu. "Bastard!!!!???. Licha ya kuita lakini hakujibiwa. Hakujibiwa kwa Mdomo bali kwa Risasi Ya jicho. Risasi ambayo ilikifumua kisogo cha Jimmy. Hilo halikutarajiwa Na Veronica. Hakulitaraji Kabisa. Alishawahi kuwaona Mafia wakiua lakini Hiki alichokuwa Akikiona kwa Bastard kilikuwa kitu ambacho kilimsisimua. Hakutaka kumuacha Mwanaharamu Amuadhibu Jimmy. Naye alihitaji kuipenyeza Risasi Kichwani Kwa Jimmy kwa Ajili ya Masimba. Muda huu Risasi Mfululizo zilikuwa zikiingia Kwenye Mwili Wa Jimmy Lambert. Na huo Ndio Ukawa mwisho Wa Jimmy. "Okota Nguo yako tuondoke Haraka." Mwanaharamu Akamwambia Veronica Huku akicheka. Kwa aibu za Kike Veronica akaiokota nguo yake kisha bila mwanaharamu kutarajia, Veronica Akavaa pale pale mbele ya macho ya Mwanaharamu.
*******
Mipaka yote ilikuwa imefungwa, viwanja vya ndege havikuruhusu ndege kuruka. Anga ilikuwa imezibitiwa Huku ndege za jeshi la wana Anga zikionekana kuzunguka Anga lote. Vizuizi viliwekwa kila mahala katika barabara. Mabasi na magari makubwa ya mizigo hayakuachwa hivi hivi. Kila gari lilikuwa likipekuliwa na kukaguliwa. Watu walikuwa wakiangaliwa zaidi ya mara tano na Hata sita. Mtu mmoja alitizamwa na hata kuangaliwa na macho laki moja. Kila jicho lilimtizama na kumsoma. Kila Jicho halikumuacha katika aina yoyote ile. Walitizamwa na kuangaliwa sana. Askari walisambazwa kila mahali. Taarifa ya kifo cha mtoto wa Rais ilikuaa imesambaa kama Upepo. Amri ya kuzuia magari na ndege kutokusafiri ikatolewa katika uharaka unaotakiwa. Nyumba za kulala wageni safari hii hazikuachwa kabisa. Hata zile bubu zilikuwa zikivamiwa na kupekuliwa. Mitaa Yote ya Tungi Ilikuwa haiangaliki kutokana na uwingi wa wana usalama. Tokea kifo cha mtoto wa Rais kilipotokea usiku ule, tayari vijana kadhaa walishakamatwa kila upande wa Tanzania. Wana usalama walikuwa wakihaha kila upande nia ikiwa ni kumpata Muuaji ambao wao walijua ni Masimba. Licha ya kuwakamata vijana Hao lakini Tageti yao haikuwa hivyo. Kila saa Simu za Siri zilikuwa zikipigwa kila upande wa upekuaji ule. Msisitizo wa masimba kuuawa ulikuwa ukitolewa katika kila simu ambayo ilikuwa ikipigwa. Neno apigwe risasi kabla ya mahojiano ndiyo amri iliyotawala katika kila wale wote walioshiriki upekuzi Ule. Magazeti nayo hayakuwa Nyuma katika Kuripoti tukio lile. Kila gazeti lilikuwa na kichwa cha habari kilichosheheni habari zilizochambuliwa. "MTOTO WA RAIS AUAWA AKIWA NA HAWARA." Kilikuwa kichwa cha Habari chw Gazeti la HANDENI LEO. Chini kukawa na maandishi madogo yasemayo. "Inasemekana mpelelezi mashuhuli Tanzania ndiye aliyefanya Mauaji Hayo". "MTOTO WA RAIS AUAWA KINYAMA. ALIKUWA NA HAWARA." hili lilikuwa Gazeti La Mwananchi. "WHAT GOES AROUND COMES AROUND" hili lilikuwa Gazeti la JAMII FORUMS LEO. hili ndio gazeti pekee lililogusa na kuchambua habari yote kwa kina. Mwandishi alionyesha kulijua Hili kwa undani. Akaingia Ndani Akiuandika mgogoro kati ya mtu anayetuhumiwa. Aliuandika mgogoro tokea pale ulipopotea mzigo wa madawa. Kuuawa kwa Asteria Sambamba na watu wengine. Kuuawa kwa Dee Plus, sambamba na Salha Lema. Alidadavua hata kifo cha mama wa masimba huku akiongeza na kunusurika kuuawa kwa masimba mara kadhaa. Tena wakitumiwa Watu wanne. Akiwemo mpenzi wa Masimba Aitwaye Teddy. Gazeti hili lilimfunua kila mtu ambaye alihusika. Mwisho likamaliza kwa Kusema. "Kuruhusu masimba kufa ni sawa na kuruhusu vijana wote wa Taifa Hili kuangamia. Tusiruhusu hilo litokee." Lilimaliza gazeti hili huku mwandishi akionekana ni mwenyekujua Mengi ambayo yanaendelea katika sakata la mauaji ya mtoto wa Rais. Ni habari ambayo iliwapendeza wasomi wengi Wasomi wengi waliisoma ile Habari kwa Utulivu Mkubwa. Kila mmoja akausoma mstari kwa mstari. Wanasiasa nao wakaichukua Habari ile wakijiapiza kuipeleka Bungeni ili kwenda kujadiliwa kwa Maslahi mapana ya Nchi. Maswali mengi yalijengeka vichwani mwao kuhusu kilichoandikwa. Kwa nini Huyu Mpelelezi aliyekuwa akililetea Sifa Taifa letu leo anataka kuuawa. Ni hili lililowafanya wabunge kumhitaji Masimba kwa Udi na Uvumba. Walihitaji kumuona, walihitaji kufanya Mahojiano. Hawakujua kuwa Masimba kwa wakati huo alikuwa Amelikamata Gazeti La JAMII FORUMS LEO. Alikuwa akiipitia Habari ile kwa Umakini. Akiusoma Mstari kwa Mstari. Akisoma kwa vituo na kuweka Alama kwa sehemu ambayo alihisi hakuwa ameelewa. Alimsoma Mwandishi Yule katika Namna ya kutaka kumjua. Kichwani kwake Alitambua aliyeandika Hakuwa Mwandishi Wa Habari Wa Kawaida. Hakuwa Mwandishi Wa Habari Za Uchunguzi Kama Marehemu Josephat Isango. Huyu alikuwa ni Jasusi tena Jasusi Wa kupindukia. Jasusi ambaye alionyesha Kulijua Hili Suala kwa Undani Zaidi. Akaitizama Tena na tena Habari ile. Akiuangalia Uandishi ili kumtambua aliyefanya kazi hiyo. Ni kitu kilichomchukua dakika kumi kumgundua Mwandishi wa Habari hii. "CHIEF" ndio neno pekee alilotamka huku akitabasamu. Chief ndiye aliyekuwa ameifanya kazi ile. Chief ndiye mwandishi Wa Habari Hii Mfano wa Makala. Akatabasamu na kutabasamu. Kitendo cha kugundua kuwa Mzee Godliving Kimaro Yup0 Hai kulimpa furaha sambamba na Tabasamu. Alitambua kwa maandishi yale na mapambano yanayoendelea. Basi Muda sio Mrefu vita hii itafika Mwisho. Baada ya kuisoma ile habari, taratibu Akainuka kutoka pale kitandani na kusimama. Akajionyoosha kidogo mwili wake. Akauona Uzima wa Mwili wake. Muda huu alikuwa ameamua kuupasha mwili Wake. Aliamua kuunyoosha Mwili wake kwa Mazoezi Makali. Alikuwa amerudi kwenye utimamu wa Mwili na Akili. Katika Utimamu wa kimapambano. Baada ya kupasha mwili wake akaelekea Bafuni Kujimwagia Maji. Taratibu akawa anayaacha Maji ya mwagike Huku akimuwaza Teddy. Alikuwa Tayari kumuua kwa Mikono yake. Tukio la kummiminia Risasi Mfululizo ndani ya chumba alichokuwa Amefungiwa. Kulimpa Jibu Kuwa Teddy Hapaswi Kuishi.. Teddy Hapaswi kuachwa Hai. Na Sio Teddy tu, Hata kichwa Cha Mkuu Wa Nchi ni lazima Kiondoke. Ni lazima aelekee kule walikoelekea Masikini wote waliokufa kwa njaa Sababu ya Mikataba Mibovu sambamba na Waathirika Wote wa Kemikali iliyonyunyiziwa kwenye Madawa. Baada ya Kumaliza Kuoga, akatoka Bafuni. Akajifuta Maji. Baada ya Hapo Akavaa Mavazi Yake kisha akaanza kutoka ndani ya Chumba. Wakati Akiukaribia Mlango.. Akausikia Ukigongwa. MASIMBA AKATULIA HUKU MKONO UKISHUKA PALE ALIPO HIFADHI BASTOLA YAKE.
EID MUBARAK KWENU WASOMAJI WANGU. NAOMBA MUALIKO JAMANI.