Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

Hahahaaa kuna lugha niliisikia kwa waswahili wakisema kama ushuzi basi ushapata mjambaji yaani rais ataomba Poo sasa Teddy Ndiyo kabisa kifo chake kimefika maana kama usingizi masimba kashampata Veronica
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 066

Haikuwa sura ile ya mwanzo, hii ilikuwa sura nyingine kabisa. Macho yalikuwa yakimtizama mzee yule pasipo kupepesa kuangalia kando. "Bila shaka unamfahamu huyo mtu, na pia unafahamu kazi zake. Nahitaji kumjua na kujua ni lini alianza kufanyakazi hapa." Akaongeza Masimba. "Mr John nadhani hayo maswali sipaswi kuulizwa na wewe. Muajiri wangu ndiye mwenye mamlaka hiyo pale aonapo kitu hakiendi sawa. Pia hata wanausalama ndiyo wanaweza kufanya hivyo lakini sio mtu wa hazina." Alijibu mzee huku hofu ikiwa imetawala ndani yake. "Mimi ndiye nimekuja badala ya bodi ya mamlaka ya bandari, pia nimekuja kama special Agent.. so nahitaji kupata majibu kuhusu mtu huyo mm0ja mwenye majina matatu tofauti." Alinguruma Masimba huku uso wake ukizidi kuuondoa Uhalisia. "Kijana ya nini tusumbuane, kwanza unaniuliza wewe kama nani? Akabwata yule mzee huku akionyesha kughafilika. "Kama John Raphael kutoka hazina, lakini pia unaongea na Mto roho ambaye ukiendelea kuupoteza muda wangu kesho hutaiona." Aliongea Masimba sasa akilazimisha macho yake yatizamane na macho ya mkurugenzi. "Huyo mtu mimi simfahamu na hata hapa hatuna Jina kama hilo." Akajibu mzee Majibu ambayo kwa kumuangalia tu, alihisi kuwa amedanganywa. "Humjui huyu mtu? Unashindwa kumjua mtu uliyemuajiri mwenyewe? Nikisema unamjua na kumtambua utasema nadanganya? Nikisema nawe ni kibaraka wa Jimmy Na Suresh kama alivyo huyu mtu wako utakataa? Je upo tayari risasi yangu ipenye kichwani kwako kwa sababu ya kuuficha ukweli wa mtu asiyekuhusu? Sasa naomba unijibu kwa umakini, usijaribu kunificha. Nikibadilika nitakupoteza kwa dakika tu." Aliongea Masimba huku akimtizama kwa macho makali. Mshtuko na mfadhaiko vilikuwa dhahri machoni na hata usoni. Mikono ikamtetemeka huku jasho likichuruzika Taratibu licha ya kuwepo kwa mashine za kuleta baridi. Kitendo cha kutajiwa watu hawa wawili kilimvunja nguvu na kumfanya asiwe na la kuongea. Akabaki akimtizama Masimba huku akionekana kutetemeka zaidi. Ni wakati Masimba akilitizama hilo akamuona mzee yule akibadilisha macho na muda ule ule kitu mfano wa damu kikaonekana kifuani kwake. Masimba hakuwa mjinga kiasi hicho asijue kilichotokea. Risasi iliyopitia Dirishani ilikuwa imepenya kwenye kifua cha mkurugenzi. Alikuwa amezibwa mdomo, alikuwa ameondolewa uhai asije kuutapika ukweli wote. Ilikuwa ni njia moja wapo inayotumiwa sana na majasusi kuficha siri husika. Akainua macho kutizama pale ilipotokea Risasi.. akakutana na nafasi ndogo kwenye pazia. Nafasi ambayo alihisi ndio imetumika kumuua Mkurugenzi huyu. Licha ya nafasi hiyo, pia usawa na ukaribu wa alipokaa yeye ilikuwa ni rahisi sana kupigwa yeye Risasi kabla ya mkurugenzi. Kwa nini ameachwa yeye akauliwa mkurugenzi? Lilikuwa swali lililoamsha mashaka. Mtu aliyemuua mkurugenzi alikuwa ni mtu anayemfahamu ama mtu ambaye alipewa oda ya kumuua mkurugenzi na kumuacha yeye. Kilikuwa kitu kigumu kukiamini katika uuaji ule. "Teddy" ndio jina pekee lililopenya kichwani na kuuvuruga ubongo wake. Lakini hilo alilioinga baada ya kutambua Teddy hawezi kuwa pale kutokana na msiba wa Vicky. Ilikuwa ni ngumu Teddy kuiacha maiti ya Vicky kisha aje afanye hivi. Lakini ni nani? Swali hilo alijiuliza wakati ameshaufikia mlango na kutokea ofisi ya sekretari. Kuufungua mlango tu, macho yake yakatua juu ya mwili wa Mwanadada yule ukiwa umelalia juu meza damu ikivuja taratibu na kuilowanisha Sakafu. Naye alikuwa ameuawa katija aina na namna ile ile. Namna ya kufumbwa mdomo asiweze kubweka. Masimba akaiona Hatari, hatari yakuendelea kuwepo ndani ya ofisi zile. Mkurugenzi, kisha sekretari, ilikuwa picha mbaya kwake. Ilikuwa ni lazima aondoke hapo. Aondoke kwa kupitia uelekeo mwingine, alijua alikuwa akitizamwa mahala fulani. Licha ya kutizamwa huko, lakini bado alimhitaji kumuona mwanadada yule wa mapokezi. Mambo kutokea kwa kasi namna hii ni wazi kuwa taarifa ilikuwa imesambaa. Imesambaaa kupitia kwa mtu, mtu ambaye amemuona kwa mara ya kwanza. Nani ameniona kuisambaza Taarifa hii katika muda mfupi huu? Jibu lilikuwa moja tu, veronica Senka Alikuwa msambaza taarifa , ilikuwa ni lazima apatikane kwa njia yoyote ile. Akaondoka akipitia sehemu tofauti na alikoingilia. Wakati akitoka Nje ya jengo, akauona msululu wa magari ya polisi wakikosi maalum ukiingia pale. Kilikuwa kikosi cha kupambana na uharifu wa aina yoyote. Kuuona msafara huo na alipounganisha na matukio ya kuuawa watu wawili katika muda mfupi.. alipata Jibu kuwa ni yeye aliyekuwa akitafutwa, ni yeye aliyetumiwa kikosi kile, ni yeye anayetafutiwa sababu ili wanaomuamini Wasimuamini. Hilo likamfanya azidi kuwa makini katika uondokaji. Uondokaji machoni mwa watu ambao walikuwa hapo.

********
Kwanza alishikwa na kitu kama ganzi, pili akashindwa hata kuongea na kipi akifanye. Butwaa hili lilimfanya mtu huyu aingie pasipo yeye kufanya maamuzi. Uso wake ukatagayari pale macho yake yalipogongana na macho ya mtu huyu aliyeingia kwenye ofisi zao katika mchana huu. Tabasamu mdomoni na uchangamfu wa kuzuga ukauchukua uso wake. Hata kijana huyu alipomsogeleo, bado tabasamu tamu halikuondoka usoni kwake. Hata alipojitambulisha kuwa anaitwa John Raphael, hakuonyesha kushangaa kwa kuwa alishamjua mtu huyu. Hakukuwa na mtu ambaye hakumjua Masimba. Lakini alipohitaji kuonana na mkurugenzi Muajiri, kengele za tahadhali zikalia kichwani kwa binti huyu.. hata pale masimba wakati akielekea kwa mkurugenzi hakuwa na maamuzi yoyote. Hakujua angeamua nini kwa wakati ule. Mpaka anaanza kuzipanda ngazi, bado hakujua nini afanye. Alimuona Masimba kama mtu ambaye anasingiziwa, mtu ambaye hafanani na kile kisemwacho juu yake. Wakati akiyawaza Hayo simu yake ikapata uhai. Simu yake ilikuwa ikiita. Namba ya mpigaji ndio iliomfanya akurupeke. "Jimmy" ndio neno ambalo lilisomeka Juu ya kiio cha simu yake. "Boss wangu.!! Alipokea Veronica.

"Yeah mtoto mzuri uko wapi leo?"aliuliza Jimmy.. "nipo kazini ila tumetembelewa leo." Akajibu Veronica. "Mmetembelewa na nani? Rais au nani?. Akauliza Jimmy safari hii kwa sauti tulivu. "Masimba yupo hapa, ametutembelea na sasa anaelekea kuonana na mkurugenzi muajiri. Nadhani kunatatizo boss maana alivyoingia sio kawaida." Aliongea Veronica. Hata aliposubiri jibu kwa Jimmy hakulipata kwa muda ule. Alipoita tena akagundua simu ilikuwa imekatwa. Baada ya Jimmy kupewa taarifa ya masimba kufika bandarini na kuhitaji kuonana na mkurugenzi ili mshtua sana. Kwa jinsi alivyomjua Masimba, alijua hapakuwa na usalama. Akapiga simu hotelini kwa vijana wake, jibu alilopewa lilimfanya atetemeke. Mmoja wa vijana wake shupavu maarufu kwa Jina la Jike dume alikuwa ameuawa. Akahisi mambo kutokuwa sawa, haraka akapiga simu kwa Ben kisha kumpa maelekezo ya nini cha kufanya. Ndicho ambacho kilitumika kuwaondoa watu walea katika ofisi ile.

******

Alifika msibani kwa mara ya pili tena, aliwakuta watu wapo katika makaburi tayari kwa muhifadhi vicky. Alisogea taratibu akikwepesha macho yake kumuangalia Teddy aliyekuwa ameshikiliwa huku na huko akilia kwa uchungu. Sala ya kumuombea marehemu ikachukua nafasi yake. Baada ya sala mwili wa Vicky ukaanza kushushwa kaburini kuhitimisha safari yake ya mwisho hapa duniani. Ulikuwa wakati mgumu sana. Mama Vicky hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea. Wakati wote huo masimba alikuwa makini akiangalia macho na sura za waliohudhuria mazishi. Hakutaka kuamini kwamba usalama ulikuwepo. Muda wote hakutulua akigeuka huku na kule. Akigeuka katika ya kupendeza. Uvaaji na hata muonekano wake haukuwa kama ule aliotoka nao ofisi za bandari. Hapa alikuwa ni Masimba mwingine. Kila hatua na kila ishara ya waombolezaji ilichunguzwa na kutiliwa mashaka. Vijana walioongezwa kuudumisha ulinzi na kunusa chini kwa chini nao walikuwa makini sana. Hata kama mtu alikuwa akijikuna basi aliangaliwa mara tatu tatu. Aliangaliwa na hata kufuatiliwa. Alichunguzwa kwa ukaribu zaidi na hata kupewa kashkash ambazo hazikuonekana machoni kwa waombolezaji. Macho yao yalikuwa katika sura ya mwanamke fulani ambaye alikuwa ametokea hapo na katika muda huo. Macho ya wanausalama yakamkaribisha katika aina ya tunakushuku. Tunakutuhumu na tutakujua. Akaangalia kila hatua na kila macho yake yalipokuwa yakigeuka kwa kutembea huku na kule. Huyu alikuwa yule mwanamke aliyekuwa pale ofisi za bandari. Huyu alikuwa yule aliyeisambaza taarifa za kufika hapo kwa masimba, taarifa iliyosababisha kuuawa kwa mkurugenzi. Lakini sasa alikuwa hapa makaburini, amekuja kama na nini na amefuata kipi? Hilo ndilo lililojengeka kichwani kwa masimba, hilo ndilo lililojengeka kuwa kuna namna. Mpaka mtu huyu kufika hapa makaburini ni wazi kuwa alikuwa akintafuta yeye. Alikuwa akijua kabisa binti huyu alikuwa hapo kwa kazi maalum. Kazi ya kumpeleleza yeye. Hilo likamvutia kwa kuwa alikuwa anamtaka na kumhitaji. Mazishi yakafika tamati na watu wakaanza kurudi majumbani kwao. Vijana wa usalama walikuwa wakitembea pembeni mwa familia ile kwa karibu sana kuonyesha kuwa walinusa chochote kitu. Masimba bado macho yake yalikuwa kwa Veronica. Bado macho yake yalitaka kujua kile ambacho msichana huyu amekifuata. Kile ambacho angekihisi machoni na hata kupitia mienendo yake. Kumkuta ofisi za bandari, mauaji ya mkurugenzi na sekretari wake, kisha kuja kwenye mazishi ya Vicky ni mambo ambayo yalimuacha katika maswali ambayo hayakupata majibu. Alihisi hata taarifa ya kufika kwake pale Bandari yeye ndiye aliyeisambaza na kisha kutumwa watu wa kuua.

Watu waliendelea kurudi nyumbani kwa wafiwa bila kujua chochote. Bila kutambua kuwa palikuwa na mchezo wa aina yake. Macho kwa mwanamke yule hayakuganduka. Aliitizama miguu yake na kuutizama mwendo wake. Mwende ambao ulimuonyesha kuwa mwanamke yule hakuwa peke yake. Mwili wake ulikuwa ukitoa ishara fulani katika kujulisha watu kitu fulani. Wakati mwili wake ukitembea katika namna ya kutoa taarifa. Macho yake yalikuwa yakitembea kwa aina fulani ya kinyonga ili kuwapoteza waliokuwepo na wale ambao alijua wako mahali na wanamuangalia yeye. Hakujua hilo na pia hakulitambua hilo. Hakutambua kuwa kuna macho mawili ambayo hayajawahi kushindwa kugundua kitu. Macho ambayo hung'aza mpaka ndani. Kila uelekeo wa macho yake hata masimba aliangalia huko. Kila alipokuwa akiuchezesha mguu hata macho ya Masimba yalikuwa yakitizama. Hatua zisizopungua kumi mbele mkono Wa Veronica ukawa unashushwa taratibu kuelekea mahala fulani katika vazi lake.. Hata mkono wa Masimba nao ukafanya hivyo, na Hakuwa masimba pekee, bali Hata wanausalama Wengine mikono ilikuwa Mfukoni tayari kwa tukio la aina yoyote.
Aah Ibra ee kuanzia ya kwanza naweza kuipata?
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 089

Hakuwa na Haraka ya kuinuka kwa kuwa alijua kuna mtu yupo sehemu akimtizama. Hata wale watu wawili ambao walikuwa wamesimama umbali mfupi kutoka kilipokijiwe cha kahawa bado hawakuondoka. Walionyesha bado walikuwa na maongezi marefu. Hata Mtu yule naye akakakaa na kuwatizama. Haukupita muda mmoja kati ya watu waliokuwa wakifanya mazungumzo akaaga na kuondoka akiivuka barabara kuelekea maeneo ya Posta mpya. Yule mmoja naye Alikuwa amerudi nyuma akiongoza kama alikuwa akielekea chuo cha Elimu ya Biashara. Mtu huyu alikuwa akiwatizama huku akicheka kimoyomoyo. Aliitambua kasumba ya Wana usalama wengi. Aliitambua staili yao na pia aliitambua aina yao ya maigizo. Kilichokuwa kikifanywa na watu wawili waliokuwa wakizungumza ndicho kitu kilichotoa mwanya kwa Wana usalama wengine kuondoka na mtoto wa Rais. Baada ya kuhakikisha hakuna mtu mwingine wa kumtilia mashaka. Alilipa pesa ya kahawa kisha akainuka na kuiendea Gari yake aliyekuwa ameipaki pembezoni kidogo mwa barabara. Akaingia ndani ya gari, safari ya kuelekea alikopaswa ikaanza. Wakati gari ikiendelea kutembea taratibu, bastard akafungua sehemu fulani ndani ya gari na kutoa kitu mfano wa Saa. Baada ya kukitoa kitu Hicho akaingiza maneno kadhaa. Katika sekunde ile ile kitu kile kikawaka. Akasubiri Kidogo Kisha Akaingiza namba za Gari Iliyoondoka na Mtoto wa Rais. Akaendelea kusubiri huku Gari ikiendelea kutembea. Dakika Tano mbele Kitu kile mfano wa Saa Kikaonyesha Neno Oysterbay block no 451. Bastard akatabasamu na wakati huo huo akakizima kitu kile mfano wa saa. Kwa mara nyingine alikuwa ameingia kwenye mission ya Hatari. Mission ambayo Ina mkutanisha mara nyingine na Wana usalama. Wana usalama wa Tanzania. Kichwa chake hakikusahau mission ya kwanza ambayo ilimlazimu Kusafiri mpaka Nchini Canada. Alikuwa sambamba na MOA, JENIPHER Sambamba Na Neema. Ilikuwa mission ngumu sana kupambana na mashirika makubwa ya Kijasusi Duniani. Ni mkasa ambao ukiwapa Sifa kubwa, Sifa ambayo ilishawishi mpaka mataifa makubwa ya kijasusi kuamba kufanya kazi na watu hao. Mkasa ambao Uligundua Siri kubwa Iliyojificha Nyuma ya Mauaji ya Mke Wa Rais. Leo hii alikuwa amekutana tena na Masimba. Lakini safari hii sio masimba pekee yake, bali alikutana na Veronica. Vero Mwanamke Kutoka Nchini Italy. Veronica Ambaye alikuwa ni mwanachama Mwandamizi wa Kundi la Mafia. Gari akazidi kushika kasi, alihitaji kwenda kumchukua Mtoto wa Rais kwa sababu ya kymshinikiza Baba yake Aitoe ile betri. Alijua ilikuwa kazi ngumu, lakini ilikuwa Lazima Aifanye. Ilikuwa lazima atengeneze hilo. Akalivuka daraja la Salenda. Mbele kidogo akaingia kulia kam anaelekea Masaki. Kufika Mbele kidogo akaingia kushoto na kuingia katika Eneo hilo. Akaongoza mpaka sehemu maalum ya kuegeshea magari. Baada ya kuegesha gari, akashuka akaifunga milango vizuri kisha kusogea mpaka alipomlizi wa Sehemu hiyo. Baada ya kumfikia mlinzi alichomoa noti ya Elfu kumi akamkabidhi mkononi akimuacha mlinzi yule akifurahi. Baada ya kumalizana na Mlinzi, Bastard akatembea kwa kawaida kuliacha eneo hilo. Akatokea kwenye Chochoro moja Ambayo ilimuongoza kuelekea lilipo jengo ambalo aliishi mtoto wa Rais. Hakuogopa chochote kile.

Alikuwa tayari kwa kila ambacho kiko mbele yake. Akaupita uchochoro ule pasipo kutokea rabsha yoyote. Mbele kidogo akauvuka Uzio wa Kiwanda fulani. Baada ya kuuvuka Uzio Huo akajikuta akitizamana na jengo ambalo alikuwa akiishi mtoto wa Rais. Akatulia kwanza akilitizama Jengo lile Kwa Umakini Mkubwa. Macho yake yalikuwa yakitizama na kuhesabu askari ambao walikuwa hapo. Askari wa nne wenye Bunduki walikuwa Geti la mbele sambamba na wana usalama wengine watatu. Upande wa nyuma wa Jengo hili pia walisimama Askari watatu na wengine ambao walivaa kiraia. Akaamua kuhama Eneo hilo na kuizunguka lile Jengo. Muda wote alikuwa akiwatizama walinzi ambao walikuwa mbele yake. Hawa walikuwa wawili tu, huku mmoja akionyesha kuwa Amelala. Akaona hapa ndipo sehemu sahihi ya kuingia ndani Alitaka kuingilia hapo katika namna yoyote ile. Alitambua sehemu ile ndiyo ingeweza kumfanya aingie ndani bila wasiwasi. Akahama Upande ule na kukivuka kibarabara fulani. Baada ya kuvuka hapo. Sasa alikuwa amewakaribia Walinzi hawa wawili. Akatembea Akinyata taratibu, alikuwa akitembea mfano wa chui. Kwa mwendo wa silika akachupa na kutua katikati ya walinzi hawa. Kilikuwa kitendo cha sekunde tu kutendeka. Mlinzi mmoja alikuwa chini akiwa ameshika koromeo. Wakati mlinzi huyu wa pili akikurupuka kutoka usingizini. Akakutana na Ngumi moja ya Shingo iliyompeleka Chini. Wakati mlinzi huyu akihangaika kuinuka, bastard akamuwahi pale chini na kumnyonga Shingo. Baada ya Kummaliza Huyu akageuka kumuendea huyu mwingine. Lakini akakuta Tayari Alikuwa Amekufa. Hapo akaongoza kuelekea kwenye Nyumba hii. Haukupita Muda alikuwa ameshauparamia ukuta na kuingia Ndani. Kitendo cha kutua tu, akaichomoa Bastola Yake. Akaanza kutambaa taratibu kuelekea ndani kabisa ya nyumba. Alitembea akifuata vivuli vya miti. Kufika mbele kidogo akasimama kwenye shina la mti baada ya kusikia sauti za watu kwa mbali. Akatega sikio zaidi na zaidi. Akagundua sauti zilikuwa zikitokea ndani kidogo ya Jengo lile. Akatulia hapo zaidi na zaidi. Punde mlango ukafunguliwa kisha uso wa binti mrembo ukaonekana kuchomoza katika tabasamu tamu. Hakuwa binti pekee bali alikuwa na Mtoto wa Rais. Kila moja alikuaa amevaa pajama wakionyesha kuutafuta ubaridi. Ubaridi ambao hakuujua ni wa nini mpaka pale binti yule aliyekuwa na mtoto wa Rais alipolitoa vazi lile pekee Mwilini. Pale alipobakia kama alivyozaliwa. Alipokewa na Chuchu safi na za kuvutia kama za Mtoto Swahiba. Chuchu ambazo zilifaa kwa kunyonya kulamba na hata kumalizia kwa Shida nyingine. Alikuwa mweupe chuchu zikisimama mithili ya michongoma. Huyu alikuwa ni zaidi ya Shunie na Hata Heaven Sent. Huyu alikuwa Akivutia na kutia hamasa mfano wa Black woman Wa Jf. Alivutia na kutia hamu. Uwanja wake wakuchezea ulikuwa na Majani Madogomadogo ambayo yaliupendezesha na kuufanya upendeze. Ni umbo lililoutatanisha Ubongo wa Mwanaharamu. Umbo ambalo lilisababisha mtafaruku kichwani kwa binadamu huyu aliyelaaniwa. Akatamani aitumie bastola kumuondoa mtoto wa Rais ili akichukue kiumbe hiki. Kiumbe ambacho hakikufanana na Nuru na Hata Mwadi. Huyu alifanana kabisa na Tete. Tete ambaye alikuwa akimilikiwa na Jasusi liitwalo muteba. ( R.I.P Elvis Musiba) akatamani kuitupa bastola yake ilikuwavamia watu hawa aondoke na Binti Huyu. Hata pale binti alipojilaza kwenye kitanda maalum pale nje kisha kuiachanisha miguu yake huku na Huko bado Mwanaharamu alilitizama tukio hili. Hata pale mtoto wa Rais aliposogea na kukaaa karibu ya malaika yule. Bado Mwanaharamu akatulia kanakwamba hakuwa anakiangalia kitendo hiki. Macho yake yakajakubadilika baada ya mkono wa Binti Yule usio na Adabu ulipoingia ndani ya Vazi la Mtoto wa Rais. Mkono ambao ulitulia kwa muda ukitafuta kitu ambacho ulipoteza. Mkono huo ndio uliomkumbusha kuwa alikuwa hapo kwa mission maalum. Yupo hapo kwa Ajili ya kumchukua Huyu mtu. Dakika hii alikuwa ameinuka akielekea pale walipokuwa watu hawa wakifanya ufirauni. Binti mdomo wake ulikuwa ukipanda na kushuka maeneo fulani, wakati mtoto wa Rais alikuwa amesinzia akisikilizia kitu ambacho hakikujulikana. Kutokana na kilichokuwa kikitendeka pale, watu hawa hawakumuona Mwanaharamu alipokuwa Akisogea hapo. Mwanaharamu akatembea na muda mfupi alikuwa Amesimama hatua mbili kutoka Walipo watu hawa. Mdomo wa bastola kumgusa mwanamke huyu ndicho kilichowashtua wote. Mwanamke kuinua Macho yake na kukutana na Mdomo Wa Bastola, akajikuta akipiga yowee. Ni yowee lililoifanya Bastola Ya mwanaharamu Ikohoe. Risasi zikiingia kifuani Kwa Binti Huyu na kumtupa umbali wa hatua kumi na tano. Risasi Nyingine Zikikifumua kichwa Cha Mtoto wa Rais. Hapakuwa na Jinsi zaidi ya alichokifanya. Mipango yake Ilikuwa imevurugwa na Mwanadada huyu. Hakutaka kuupoteza muda. Akataka kuondoka na kutoweka eneo hili. Lakini hakuwahi kufanya hivyo. Akashuhudia wana usalama katika namna iliyovutia. Kuvutia kwa mapambano. Muda huo huo akasikia Risasi zikivurumishwa kuelekea kwake. Hakuchelewa wala kusubiri chochote kitokee. Alikuwa amechupa tayari na wakati huo huo akiachia risasi mfululizo kuelekea walipo walinzi. Risasi Zilivurumishwa bila kukoma. Walinzi hawa hawakutaka kumpa nafasi Mwanaharamu. Mwanaharamu akatambua hapo ilikuwa ni Lazima Aondoke hapo kabla ya wana usalama wengine kufika. Akainyanyua Bastola yake na kuilenga taa. Muda mfupi baadae Sehemu yote ilikuwa Giza. Hapo ndipo alipoinuka taratibu na kutambaa mpaka usawa wa ukuta. Akajivuta Taratibu na kufanikiwa kuanguka upande wa pili. Baada ya kutua salama, akatembea taratibu na giza mpaka fukwe za coco. Kutoka hapo akajichanganya na watu ambao walikuwepo hapo. Kabla ya kurudi kwenye maegesho ya Magari na kuichukua gari yake, nakuondoka taratibu katika eneo hilo. Wakati akijua ameshamaliza kile alichokitenda. Akawaona watu watano Wenye Silaha wakiwa mbele yake. Baada ya kuwafikia mmoja akampa Ishara ya kumtaka asimamishe gari. Mwanaharamu Akatiii!! Akaisimamisha Gari na kuizima kabisa. Akatulia tuli kuwasubiri watu hawa ambao sasa walikuwa wakimsogelea.
 
Mmh mdogo wangu ibra ndio umeshampenda shunie nini? Maana sio kwa kumpaisha huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom