NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 087
Alichanganyikiwa kwa taarifa aliyopewa. Taarifa iliyomlazimu kurudi Tanzania. Masimba alikuwa ametoroshwa, masimba alikuwa ameondoshwa kwenye kambi ya usalama wa taifa. Kilikuwa kitu kigumu kukiamini. Kichwa chake kilikaribia kupasuka kwa mawazo. Aliujua ugumu wa kazi endapo itakuwa ni kweli masimba ametoroka. Kwa mbali Teddy alikuwa akiipata hofu, hofu ya kifo na hofu ya kuuawa na Masimba. Alitambua safari hii hata weza kuachwa akiwa hai. Tax ikatembea kwa mwendo wa kawaida pasipo kufanya haraka. Hata walipofika Uwanja wa Ndege wa Jommo Kenyatta Tayari alikuwa amechelewa. Moja kwa moja ikabidi afanye mawasiliano na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani. Baada ya mawasiliano hayo muda mfupi baadae akawaona watu wawili wakisogea kuelekea pale iliposimamia Tax. Watu wale wakajitambulisha kisha kumwambia kuwa walikuwa pale kwa maagizo ya Waziri wa Marekani. Teddy akaeleza kile alichokuwa akikihitaji kwa muda ule. Akaambiwa awafuate Watu wale kwa nyuma. Safari yao iliishia mpaka kwenye kampuni Moja binafsi. Akaambiwa asubiri kidogo. Muda wote Teddy alihitaji kuondoka hapo. Alitaka kwenda kuhakikisha mwenyewe. Taarifa hii ilikuwa imemchanganya kabisa. Kwenye account yake ya benki tayari pesa yake ilikuwa imeingizwa kama Ahsante yake. Ilikuwa pesa nyingi sana pesa ambayo kama angeamua kuondoka Hapa nchini na kwenda kuishi popote Duniani Angeliweza hilo. Lakini alitambua hata kama angeenda wapi basi nilazima Angetafutwa na Masimba popote pale. Alitambua kwa kile alichokifanya angesakwa popote pale. Alichotaka kukifuata ni kwenda kulihakiki hilo. Alijua kuwa lazima kuna mtu ambaye ameshiriki katika kumtorosha Masimba. Taarifa kuwa camera za Usalama hazikupata tukio lolote hilo lilimfanya aamini kuna Mtu ndani Ya Idara lazima atakuwa Amekengeuka. Muda mfupi baadae mlango ukafunguliwa kisha akaongozwa na watu wale kutoka Nje sasa wakielekea ndani kabisa ya Uwanja Wa Ndege. Baada ya kuingia kabisa akaongozwa mpaka kwenye ndege moja ambayo aliambiwa ndio hiyo ambayo itamsaidia kutoka hapa kuelekea Nchini Tanzania.
*******
Alishuka uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere majira ya saa mbili na nusu. Kukanyaga Ardhi ya Uwanja tu macho yake yakapokewa na macho ya watu ambao aliwatambua. Hawa walikuwa (I.0) intelligence officers. Hawa walikuwa watu ambao ni nadra sana kuwatanbua kutokana na unyeti wa kazi zao. Hawa watu huwa ni marufuku kujitambulisha popote na kamwe huwezi kuwakuta wamebeba silaha yoyote. Intelligence Officers silaha yao namba moja ni Akili yake tu. Taarifa zao huwa zinakusanywa kupitia Informers Volunteers (watoa taarifa wa kujitolea) ama bribed informers (watoa taarifa wa kununuliwa kwa pesa) Hata Coerced informers (watoa taarifa wa kulazimishwa kwa nguvu ama vitisho). Teddy aliwaangalia mara moja tu kisha kuongoza moja kwa moja kutoka ndani ya kiwanja hicho. Hakushangazwa na Usalama waliojazana kiwanjani, alitambua wote walikuwa wakimtafuta masimba. Baada ya kutoka Nje ya uwanja alichukua Tax ambayo ilimpeleka moja kwa moja Bagamoyo Usiku ule ule. Kichwa chake hakikuamini Kama Masimba alikuwa Nje ya Tanzania, Hakuamini kuwa masimba anaweza kutoroshwa kupitia uwanja wa Ndege. Alitambua masimba alikuwa ndani Tanzania. Na alitambua atakuwa Dar es Salaam ama atakuwa kule kule bagamoyo. Alitaka kuutumia Usiku ule kunusa taarifa zote ili kujua pale alipo Masimba. Tax ilitembea kwa mwendo wa kasi huku ukimya ukichukua Nafasi yake. Hakuna ambaye aliongea wala kuzungumza. Tax ikatambaa na kutambaa mpaka saa mbili na Nusu walikuwa tegeta. Kila tax ilipokuwa ikizidi kutembea, ndivyo Moyo wa Teddy ulipokuwa ukizidi kukosa Amani. Hakuwa akijiamini Tena. Hakuwa akijiamini kutokana na woga. Licha ya woga huo lakini ilikuwa ni lazima Afike na ilikuwa Lazima Atambue kule ambapo amepelekwa Masimba na Nani ambaye amefanyakazi hiyo.
******
Wakati Teddy akielekea bagamoyo kutafuta chanzo cha kutoroshwa kwa Masimba. Veronica Alikuwa ndani ya Nyumba ya Siri akiwa ametulia akifikiria kile ambacho ameamua kukifanya. Kilikuwa kitu cha hatari sana kuwasaliti watu kama Mafia. Siku zote unapokuwa katika kundi hili hutakiwi kutoka ama kusaliti kwa Njia yoyote. Alijua hukumu ambayo angeipata kama angegundulika na genge la mafia kuwa amesaliti. Moyo wake ulikuwa umemsukuma kumsaidia Masimba. Alikuwa tayari kwa chochote ambacho kingetokea huko mbeleni. Alikuwa tayari kupambana hata na viongozi wake lakini hakuwa Tayari kumuona Masimba akiuawa. Aliamini anauwezo wa kumsaidia na aliamini anauwezo wa kuipata betri Ambayo tayari iliingia mikononi kwa mwa Serikali. Muda wote alikuwa akitamani kumuona Masimba akitembea. Mawazo hayo yakamfanya Veronica Asimame na kutoka ndani ya hoteli ile. Hakujua alielekee wapi katika usiku ule, lakini mawazo yake yalimtaka kufanya hovyo. Akaufunga mlango na kuanza kutembea Taratibu kuelekea upande wa ukumbi wa kulia Chakula. Alitembea taratibu macho yake yakiangalia Huku na kule. Akai ngia ukumbini akitembea taratibu. Sura yake nzuri ikiwa katika tabasamu matata sana. Macho yake mazuri yalikuwa yakimtizama kila mmoja kanakwamba alikuwa akiwatega ili wamtizame. Hatua zake zilikuwa kawaida huku macho yake yakivuta kila sura ya mtu aliyekaa Hapo. Macho yake hayakushindwa kuwagundua wana usalama watatu ambao walikaa katika utatu tofauti. Kila mmoja alikuwa sehemu yake akipata kile ambacho aliagiza. Hakuwajali wala kuwatizama. Akawapita akiendelea kuitafuta sehemu Nzuri ya Kukaa. Muda wote machale hayakuondoka kichwani. Licha ya wapelelezi wengi wa Tanzania kutawaliwa na Usiri, lakini wengi hugundulika kwa sababu ya staili zao. Akawapita akiongoza kama mtu anayeelekea Msalani. Haikuwa msalani kama wengi walivyotegemea. Kwani baada ya kufika msalani akachepuka kidogo na kuuparamia ukuta na kuangukia upande wa pili. Alimkumbuka Masimba na Alitaka kurudi Bagamoyo Usiku ule ule. Aliiona hamu kubwa ya kutaka kukaa na Masimba. Alichapua mpaka upande wa pili wa Barabara. Wakati anaumaliza ukingo wa barabara hiyo, simu yake ikaingia Ujumbe. Kwa haraka Huku akitembea akaufungua kisha kuusoma. "Teddy yupo Bagamoyo Ameshuka Muda huu. Nenda kaichukue Betri. Ukishaipata itumbukize Risasi kichwani Kwa Masimba. Tiketi yako utaikuta Inakusubiri Hapa." Ulisomeka Ujumbe ule uliotumwa kwa Veronica ukitoka kwa Mr Raymond. Veronica akauangalia tena Ule ujumbe alijikuta akitabasamu. Tabasamu la kejeli. Tabasamu ambalo liliishia Usoni tu. Aliuona ugumu kwake kuitumbukiza Risasi kichwani Kwa Masimba. Alikuwa tayari kumuua Teddy, lakini Hakuwa Tayari kumuua Masimba. Akauangalia ujumbe ule pasipokuongea kitu. Kitu kilichomtisha ni watoto wa Masimba kuwa Mikononi kwa Mzee Raymond. Na alitambua hilo litaleta ugumu pale masimba atakapo upata nafua na kuamua kurudi kazini. Kichwa chake kikaanza kuwaza kitu cha kufanya. Kama alikuwa anautaka usalama wake nilazima awaondoe watoto wale mikononi kwa Mzee Raymond. Ni lazima Yasser na France waondoke. Mawazo yake hayo yalinfanya aache safari ya kwenda Bagamoyo. Akaamua kuelekea Nyuma ya Kanisa la St Joseph kuwapata watoto wa Masimba. Hakuchelewa katika hilo. Muda mfupi alikuwa akishuka Maeneo ya Posta ya Zamani. Akachepuka kidogo na kuuzunguka upande wa nyuma. Wakati anaanza kupiga hatua kuelekea hapo, akaiona gari moja akitoka pale. Ilikuwa gari aina ya Nissan patrol. Veronica akijabanza pembeni kwanza ili Gari ile ipite. Baada ya Gari ile kupita, veronica akajitokeza akaanza kutembea akielekea ndani. Kengele za tahadhali zikaanza kugonga baada ya kuufikia mlango wa kijumba na kuukuta upo wazi. Sijui ni kitu gani alichohisi, lakini Muda ule ule bastola ilikuwa mkononi. Akaingia taratibu huku macho yake yakitizama kila upande. Ukumbi ulikuwa kimya kuonyesha kuwa hapakuwa na mtu hapo ndani. Hapo umakini Ukaongezeka Maradufu. Sasa alikuwa akiupita ukumbi ule katika namna ya kufutia na kutia Raha. Ni muda mfupi tu ameonyesha kutumiwa ujumbe na Mr Raymond. Lakini cha Ajabu hata dakika mbili bado anakutana na hili la kutokuwepo kwa Mr Raymond. Kufika hapo akakumbuka kuwa France Na Yasser waliishi hapo ndani baada ya kutoroshwa Kutoka kwenye Jengo la Siri walilokuwa Wakiishi. Kuwakumbuka watoto hao kukamfanya auvuke ukumbi ule akielekea kule walipokuwa wakiwekwa watoto wale. Kabla hajakifikia Chumba walichokuwa wakiishi watoto wale, akayaona matone ya damu chini. Hayakuwa matone kama matone, bali yalikuwa madimbwi madogo madogo ya Damu. Damu ambayo bado ilikuwa mbichi kabisa. Akajiongeza na kusogea zaidi na Zaidi. Kidole tayari kilikuwa kwenye Trigger. Kidole kilikuwa tayari kuiruhusu Risasi. Veronica Akatembea zaidi sasa na Kuufikia mlango wa chumba Husika. Akaufungua mlango wa chumba ambacho waliishi watoto wa Masimba. Alipougusa tu mlango ukafunguka kuonyesha kuwa haukuwa umefungwa. Mlango ulikuwa wazi hata France na Yasser hawakuwepo. Lakini kilichomshangaza humu ndani ya chumba hapakuwa na Vurugu ama damu. Akatoka na kuurudisha mlango. Akaondoka Eneo lile..
Akili yake haikuwa imetulia kabisa, kutokuwepo kwa Mzee Raymond sambamba na Watoto wa Masimba ni kitu ambacho kilimchanganya sana. Aliijua hii ingekuwa vita ya Mafia na FSB dhidi ya CIA na Serikali Ya Tanzania. Kama ni kweli Mr Raymond Ameuawa, basi Kitakachotokea hapa nchini ni kitu ambacho kingeondoka na watu wengi. Sasa alikuwa Njiani Akielekea Bagamoyo. Alikuwa Njiani kumfuata Teddy katika Usiku huu. Usiku ambao alipata taarifa kuwa Teddy Alikuwa huko. Naye akaamua kwenda huko ili wakakutane tena.
*******
Kwanza alihisi labda alikuwa katika usingizi, kitu cha pili akahisi labda alikuwa nje katika sehemu ambayo alikuwa ametupwa. Alijaribu kufumbua macho taratibu, lakini hakuweza hilo kutokana na uzito wa macho kutokutaka kufumbuka. Akatulia akisikiliza kwa makini kana angetambua mahala ambapo alikuwepo. Bado hakusikia sauti wala vishindo vya binadamu. Bado kulikuwa na ukimya ulisadifu kuwa hakuwepo katika sehemu yenye mkusanyiko wa watu. Bali alikuwa katika Sehemu ya peke yake. Sehemu ambayo hapakuwepo na kiumbe chochote. Akatulia akiendelea kuipa Akili yake utulivu. Utulivu wa kukumbuka kile ambacho kilimfikisha hapo. Wakati akiivuta hiyo kumbukumbu hiyo. Akasikia Vishindo vya mtu vikisogea mpaka mahala alipokuwa amelazwa. Mtu huyu akaanza kumshika kuanzia kichwani mpaka Maeneo ya Kifuani. Hii haikuwa mikono ya Mwanamke bali mwanaume. Mikono iliyomikakamavu. Mikono Ambayo ilikuwa migumu kupindukia. Bado akatulia na Kitulia. Bado akatulia Huku akitamani Kufumbua macho lakini Bila mafanikio. Punde akakisikia kitu kama sindano kikiingia kweny mshipa wake. Punde akauhisi Usingizi mzito. Usingizi ambao haukuchukua Muda kumfanya Asikumbuke tena alichokuwa akikikumbuka. Akatulia akiuruhusu usingizi kuichukua NAFASI.