NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 082
Akauhisi Mchezo, mchezo wa Hatari ambao unachezwa hapo. Ni wakati akilifikiria hilo likatokea Jingine. Likatokea hili ambalo hakulitegemea. Gari aliyokuja kwa mwendo wa kasi akidhani ni ya watu baki, haikuwa Hivyo, haikuwa hivyo kwa kuwa muda ule ule vioo vya magari yale vilishushwa kisha risasi zikaanza kuvulumishwa kuelekea pale pale alipokuwa amesimama Masimba. Hakuwa mzito katika kuling'amua hilo. Muda mfupi baadae masimba alikuwa angani akizikwepa Risasi. Alikuwa katika namna ambayo ilikuwa ikitia burudani Hata kwa watu wenyewe waliokuwa wakimshambulia Masimba. Alikuwa akiruka Hapa na kuruka pale. Alikuwa akiingia hapa na kutokea pale katika Ustadi wa kipekee. Katika ustadi ambao uliyonyesha kwamba hakuwa mtu wa utani. Alipokuja kutua alijikuta akiwa nyuma ya kichaka kilichopo pembezoni mwa Barabarani. Bastola ilikuwa mkononi tayari kwa kufanya kile kilichombele yake. Lakini Eneo lote lilikuwa kimya kanakwamba hapakuwa pametokea kitu chochote katika eneo hilo. Bado alikuwa ametulia akitizama. Taratibu akaanza kuburuzika kwa tumbo akiondoka hapo akielekea Sehemu Nyingine. Alitembea kwa tumbo mpaka alipofikia sehemu ambayo kulikuwa na Ukuta kwa Upande mmoja. Kufikia hapo akatulia Tena safari hii akiamua kutizama kule alipotoka. Ukimya. Ukimya ndio kitu ambacho kilitawala katika Eneo lote. Eneo ambalo muda mfupi Uliopita lilikuwa katika sekeseke la milindimo ya Risasi. Hilo halikumpa Masimba tumaini la kuinuka. Alichokifanya ni kuendelea kutizama alipotoka. Macho yake yalikuwa yakihitaji kulifanya giza, ligeuke kuwa mchana wa mwanga. Ni wakati huo alipouona umeme Ukizimwa maeneo yote na Kulifanya giza kutamalaki. Masimba akajua kinachotaka kufanywa. Sekunde hii alikuwa yupo chini akitizama Alipotoka, lakini sekunde aliyofuata Alikuwa ameparamia ukuta na kuangukia Upande wa Pili. Bado hapa kuonesha kuwepo kwa watu, bado giza lilitawala kila upande kuonyesha kuwa hapakuwepo na uwezekano wa kukosekana kwa wakora. Hazikupita Dakika mbili tokea kuzimwa kwa umeme, milio ya Risasi Ikatawala. Milio ambayo ilimuacha Masimba katika sintofahamu ya nini na nani wanapambana. Suala kuwa Veronica Alikuwa Yeye Halikuwa katika kichwa Chake, hakuliwaza kwa kuwa alijua Vero Asingeweza kukubali kumuacha Teddy. Sasa Huyu ni nani? Hilo ndilo ambalo aliliwaza. Bado milio ilikuwa Ikisikika kwa Ukaribu. Masimba akauona kuwa ulikuwa muda wa kusaidia mapambano. Swali lililokisumbua kichwa chake Je ni nani ambao walikuwa wakipambana. Je hata kama atapambana, je atajua wanaomsaidia wako upande Gani? Kuwaza huko kukamfanya Atulie. "Masimba sogea huku, ilikuwa ni sauti iliyomuita katikati ya milindimo ya Risasi. Tena hii ilikuwa sauti ya kike. Sauti ya mtu aliyemfahamu. Hii ilikuwa sauti Ya Veronica. Sauti ambayo ilimzindua na kujua kule anapotakiwa kukifanya. Hakuelekea upande ulipotokea sauti ya Vero, bali alielekea upande Tofauti. Upande ambao ulikuwa Tofauti. Akainuka na kuanza kutembea Taratibu kabisa. Akafanikiwa kukifikiwa kiwambaza cha nyumba ambayo ilikuwa mwishoni kabisa mwa Ukuta ule. Kufikia hapo Masikio yake yakanasa mchakato, mchakato wa miguu ya watu zaidi ya mmoja. Akatega Masikio yake zaidi ya Zaidi. Bado michakato ya miguu akaisikia ikizidi kusogea. Akauinua mkono wake wenye Bastola tayari kwa kuachia Risasi. Alikuwa makini kwa kuwa alijua anapambana na Oda kutoka mamlaka za Juu. Alitakiwa kuwa makini zaidi na Zaidi. Wakati akiwa hapo akawaona watu wawili wenye sub machine Gun Mikononi wakitokea kwa mbele yake. Inavyoonekana watu wale hawakuwa wamemuona Masimba. Masimba akawasubiri wasogee kwa kuwa hakutaka kuitumia Bunduki Kuua Watu wale, alitaka kuitumia mikono yake pekee. Akawasubiri waendelee kusogea. Hatua mbili kabla ya kumfikia Masimba akajitokeza mbele yao. Kwa kuwa hawakuwa wamejiandaa na kitu hicho, watu wale wakashikwa na Mfadhaiko ambao uliwapotezea sekunde kadhaa za kushangaa. Ni muda huo ambao aliutumia masimba kuwapa mapigo yaliyowaacha watu hawa wakianguka chini. Hakusubiri wainuke, hajusubiri wafanye chochote. Mlio mdogo mfano wa chafya ya binadamu kutoka kwenye bastola yake ilitosha kuruhusu Risasi zilizowapata watu wale na kuwaulia mbali.
Baada ya kuhakikisha watu wale wamekufa, hakutaka kuchelewa. Aliondoka hapo kwa kuuparamia ukuta kisha kuangukia Nje Tena. Baada ya kutua chini akatembea taratibu huku akikutana na miili ya Askari ikiwa chini ikivuja Damu. Akatambua hii ilikuwa kazi ya Veronica. Ilikuwa kazi ambayo ilionyesha ujuzi na Utaalam wa Veronica. Ilimuonyesha ni kiasi gani Veronica alikuwa Hatari. Akatembea na kutokea barabarani. Alipotokea tu barabarani, gari moja ikaja kusimama mbele yake. Kabla hajakaa sawa mlango ukafunguliwa na Kutakiwa kuingia ndani ya gari. Masimba akasita kwanza, lakini Baada ya kumuona Veronica Yupo ndani ya Gari, naye akaingia. "Teddy Yuko wapi? Lilikuwa swali la kwanza baada ya Masimba kutulia. "Amepewa hifadhi Kwenye Ubalozi wa Marekani. Nadhani kuna mpango unataka kufanyika kumuwezesha kumfikisha Ikulu." Akajibu Veronica Huku Akimuangalia Masimba. "Mbona uko hapa, nani atamuona atakapotolewa. Ukizingatia kuna Handaki limechimbwa Chini kwa Chini Mpaka Baharini?" Akauliza Masimba akionyesha Umakini wa Hali ya Juu. Kila kitu kipo kwenye utaratibu. Hataweza kuondoka hapo pasipo sisi kujua." Akajibu Veronica Akionyesha kutokuwa na wasiwasi kabisa. Lilikuwa jibu ambalo lilimfanya Masimba ageuke na kumtizama Veronica. Macho yake yenye maswali yalikuwa yakimuangalia mwanamke huyu katika aina fulani ambayo hata Veronica mwenyewe Aliitambua. "Unamjua Teddy Vizuri? Unakijua kile kichwa? Nipe majibu ya kuniridhisha. Usiongee Juu juu Veronica." Alisema huku akiendelea kumuangalia. Vero hakujibu bali alichomoa kidude fulani ambacho kilikuwa na ukubwa kama wa Simu. Akakiwasha na kumpa Masimba akiangalie Kwa Umakini. Macho ya masimba yalikuwa yakiliangalia jengo la Ubalozi Wa Marekani kupitia Kile kitu mfano wa Simu. Alikuwa akiangalia pande zote mpaka ndani ya Ubalozi. Kilikuwa kitu kilichomfanya Masimba amtizame Tena Veronica. Moyoni kwake alikubali kwamba ni kweli mtu huyu alikuwa ni Hatari. "Aiseee!! Nimeamini hiki unachokitenda. Hakika Ulijiandaa vya kutosha kutokana na Hali hii." Aliongea Masimba akikirudisha kile kidude mikononi kwa Veronica. "Una mpanga gani kwa Muda huu ambao tunamtega mtu wetu? Akauliza Veronica akimuuliza Masimba. "Usiku huu nataka niutumie kujua pale alipo Mkurugenzi Wa Idara ya Ujasusi. Nikitoka hapo nataka nikamalizane na Jimmy Lambert kabla ya kummaliza huyu Teddy." Akajibu huku akitizama kwa nje. "Unaijua Sehemu iitwayo Buzuruga ndani ya Jiji la Mwanza? Akauliza Veronica. "Napafahamu sana, nilishafika mara nyingi kila nilipokuwa na kwenda kuwahifadhi watu hapo." Akajibu Masimba. "Basi Chief inasemekana Yupo huko, na Ameshushwa Jioni Hii Kwa Usafiri wa Helkopta." Akajibu Veronica. Wakati akiongea na Masimba, kile kitu mfano wa Simu kikatoa Mlio. Veronica akakitoa haraka kisha kukiwasha. Macho yao yakawaona watu zaidi ya Sita wakiingia Mle ndani. Muonekano wa watu wale haukufichika machoni kwao. Walikuwa wana Usalama tena Wale Walinzi Binafsi Wa Rais. "Kazi imeanza, naona Rais ametuma Walinzi binafsi kwenda kumchukua Teddy." Akasema veronica Huku akimuonyesha masimba. "Tunatakiwa kufanya Jambo. Walinzi hawa ni wale wenye nafunzo ya Hali ya Juu. Na hawawezi kwenda sehemu bila uwepo wa Rais mwenyewe. Ninachoamini Rais yupo hapo na atakuwa katika Mazungumzo na Teddy. Hembu tusogee kuelekea maeneo hayo." Aliongea Masimba huku akiwaaangalia Vizuri Walinzi wale.
*******
Ulikuwa Ujio wa Siri kufanywa na Rais wa Nchi katika Ubalozi wa marekani. Ziara hiyo siri ilifanyika pasipo kujulikana popote. Na pia imefanywa baada ya mazungumzo ya Rais Wa marekani na Rais Wa nchi hii. Mkakati uliokuwepo ilikuwa ni lazima Biashara iendelee ili waendelee kupata pesa bila kujali Athari ambazo zilikuwa zinawapata Wananchi. Msaada wa mamilioni ya shilingi anayopewa sambamba na mikopo ilisababisha kiongozi wa nchi akubali kila mpango unapangwa na serikali ya marekani. Ni usiku huo baada ya mazungumzo na Rais Wa Marekani. Ndipo Rais alipoamua kuifanya Ziara ya Kuja hapo ubalozini kwa kutumia Njia maalum ambayo ilipita chini ya Ardhi nia ni kuja kuonana na Teddy. Sio rais wala wasaidizi wake waliotambua kuwa teddy alikuwa ni wakala maalum wa CIA. Hakuna aliyejua kuwa Teddy alikuwa ni special Agent wa CIA. Walimchukulia Teddy kama mwenzao. Walichukulia kile anachokifanya kinatokana na kile ambacho ameahidi Rais. Hawakujua katika pesa ambayo rais ameahidi itarudi katika mikono ya Serikali ya Marekani. Ulinzi ulitisha kila upande. Chumba alichokuwa amewekwa Teddy kilikuwa kikilindwa na mitambo maalum ambayo ilikuwa na uwezo wa kutokuruhusu Makombora ya Aina yoyote kuingia na hata kulipua. Rais alitembea akiongozwa na Makomandoo maalum ambao ndio waliokuwa Walinzi Binafsi wa Ubalozi. Sambamba na walinzi Binafsi wa Rais. Kila mmoja alikuwa ni mwenye Tabasamu. Kila mmoja sura yake ilikuwa ikionyesha furaha. Mavazi ambayo alivaa Rais Kwa siku Hiyo yaliupoteza muonekano wake. Hakuweza kugundulika kuwa ni yeye. Hata ule mtambo maalum Haukuweza Kumtambua Rais, ingawa Masimba alijua kuwa kuwepo kwa kikosi kile hata Rais hakuwa Mbali. Ilikuwa ni lazima wa hakikishe kwa njia yoyote ile Wanazuia Kitu hicho kutua mikononi mwa kiongozi. Ilikuwa ni lazima wauvamie Ubalozi wa Marekani na Kuufanya mashambulizi. Lakini swali lilikuwa Je Watafanikiwa? Hilo likabaki kuwa swali lililomtoa Masimba ndani ya gari. Alihitaji kufika Ndani Ya Ofisi Za Ubalozi na alihitaji kumzuia Teddy na pia alihitaji kuipata betri maalum yenye kuzalisha kemikali ambazo hutengenezwa kwa kuongezwa kwenye Madawa na kuyafanya madawa kuwa na Thamani kubwa. Ilikuwa ni lazima azuie hilo katika Aina yoyote na kwa Njia Yoyote. Hata kama alikuwa ni kufa yeye Hakujali hilo.