Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 083

Ilikuwa ni lazima waingie ndani ya Jengo la ubalozi wa Marekani. Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo ili kumzuia Teddy. Ilikuwa ni kazi ngumu sana kuingia katika Jengo hilo. Jengo lenye mitambo mbalimbali ya kuzuia watu na hata mabomu kupenya. Hilo likawa zito kulitenda, licha ya kuonekana kuwa zito, lakini ilikuwa ni lazima kuwakabili watu wote na kuzuia kilichokuwa kikitaka kutendeka. Ilikuwa ni lazima watende kwa sababu ya wananchi wa Tanzania. Ilikuwa ni Lazima walitende kwa sababu ya kuwaokoa Vijana wengi. Wakaivuka barabara wakiwa sambamba na Veronica. Walikuwa wakielekea kule kule kwenye Jengo. Akili na mawazo ya kila mmoja yalikuwa kule. Bastola zilikuwa zimekaa mahali salama tayari kwa kazi. Wakaipita salama Barabara na kuufikia upande wa pili. Walitembea kana kwamba hawakuwa wakienda sehemu hiyo kwa pamoja. Masimba alikuwa mbele huku veronica akisogea kwa nyuma. Alikuwa akimlinda Masimba. Alikuwa akimwangalia Masimba, kila hatua aliyokuwa Akipiga Masimba alihakikisha hata yeye jicho lake lilitua hapo. Ilikuwa kazi ngumu na ya hatari. Walikuwa Tayari kuua hata wao kufa. Nia ilikuwa ni kuizuia Betri maalum isiingie mikononi mwa Kiongozi wa Nchi. Ilikuwa nilazima Wamzuie Teddy. Baada ya kitembea Chini kwa chini wakatokea sehemu yenye Kichaka. Hapo Masimba akasimama akimsubiri Vero. Hata vero alipofika Masimba Alimvuta Pembeni kisha kuanza kumwambia kile walichopaswa kufanywa. "Veronica hii ni nafasi ya mwisho ambayo inaweza kuamua Uhai wa Maisha Yetu. Hii ni nafasi ya kuutangaza Ushujaa wa Nchi yetu. Lakini vile vile inaweza kuwa ni nafasi ya mwisho kuivuta hewa Hii kama hatutakuwa Makini. Tambua unakwenda kupambana Sababu ya Tanzania. Unaenda kupigana sababu ya wananchi wote waliokata tamaa kutokana na viongozi kusaini mikataba ya kinyonyaji. Tunakwenda kupigana kuzuia kuendelea kuharibika kwa vijana kutoka na Biashara Inayoendelea. Na Mwisho nakwenda kupambana kwa sababu ya Roho ya Asteria, familia Yake, Dee plus, vicky, Mzee Chomboko na Mwisho ni Roho Ya Mama Yangu Mzazi. Twende tukaikomboe nchi kutoka mikononi mwa wachache." Aliongea Masimba Huku wakikumbatiana na Veronica. Muda mfupi walikuwa njiani wakielekea katika uwanja wa Vita. Damu zilikuwa zimechemka. Aliujua Ugumu ambao wangekutana nao. Alitambua ugumu walionao katika kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.

Masimba na Veronica walitembea kwa uangalizi mkubwa. Muda wote bastola zilikuwa mkononi kumlenga mtu yoyote. Wakafanikiwa kuukaribia ubalozi huo ambao muda huo bado Palikuwa peupe kutokana na Taa zilizokuwa zikiwaka. Taa hizo zilisababisha ugumu wa Masimba na Veronica kupita hapo. Wakiwa wametulia wakiangalia Jinsi ya kuingia. Wakashtushwa baada ya umeme kuzimwa karibia eneo lote la Jiji la Dar es salaam. Jiji lote lilikuwa Giza katika namna ambayo hawakuitegemea. Hawakutegemea kwa kuwa waliuhisi kama ni mtego. Mtego wa kuwatega wao. Kwa nini umeme uzimwe wakati wao wakiwa kwenye eneo la tukio? Kwa nini usizimwe kabla ya hapo. Wote wakatulia kwa sekunde kadhaa wakiliangalia hilo. Ni muda huo Veronica alipomuangalia Masimba kisha kumwambia kitu. Kitu ambacho kilitamkwa kwa sauti ndogo ambayo haikuweza kupenya na kufika hata umbali wa hatua mbili. Lilikuwa neno ambalo likiwafanya kila mmoja ainuke na kuitafuta Njia. Jengo la ubalozi wa marekani lilijengwa katika uthabiti wa hali ya Juu.. Huku Mitanbo ya Ulinzi ikilizunguka eneo lote. Hali hii ilikuja baada ya milipuko ya Mabomu katika Majengo ya Balozi Zao mwaka 1998 hapa Dar es salaam na Nairobi nchini Kenya. Tokea milipuko hiyo serikali ya marekani aliamua kujenga Majengo ya Kisasa ambayo hayakuwa rahisi kuingilika na hata kushambuliwa. Wakati masimba akielekea kaskazini Veronica alikuwa akielekea Magharibi. Kila mmoja akatembea huku akizidi kuwa makini kutokana na hali ya sintofahamu iliyotokea Hapo. Upande Wa Veronica Akafanikiwa kuufikia ukuta uliozungushiwa katika Jengo hilo. Akauangalia Ukuta ule kwa muda mrefu akiangalia namna ya kuingia Humo ndani. Akiwa bado ametulia Huku Giza likimsaidia kutoonekana, akasikia Vishindo vikitokea Nyuma yake. Haukupita Muda Akawaona askari wawili wenye silaha nzito wakisogea sehemu alipokuwa amejificha. Akatulia tuli katika ya giza. Kwa kuwa alikuwa katika mavazi meusi ilikuwa ni vigumu sana watu kumuona kutokana na kuendana kwake na giza. Askari wale wakazidi kusogea wakionyesha kuwa hawakushtuka na wala hawakumuona. Akawasubiri wasogee Zaidi.. safari ikiirudisha Bastola mahala pake. Alihitaji kupambana kwa mikono. Alitaka kupambana katika aina hii ya Ugumu katika Hilo. Akaivuta subira na kuanza kuhesabu hatua ya kwanza, hatua ya pili na hata ya tatu. Hatua ya nne na tano ikamkuta Veronica akiwa hewani kwa mapigo kadhaa. Mapigo ambayo hayakusaidia kwa Askari wale kujitetea. Baada ya kuwaua, Veronica alimvua Askari mmoja mavazi yake, kisha kuyatia Mwilini. Alifanana kabisa na walinzi wa Ubalozi. Akachukua Bunduki ya mlinzi mmoja sasa akiiweka begani. Akaanza kutenbea huku akikumbuka maelezo aliowahi kupewa na Mkuu wake wa Genge la Mafia. Maneno ambayo yaliendelea kuishi moyoni na hata kichwani. Maneno hayo yalimsaidia na kumtoa katika Hatari nyingi sana wakati wa mission katika Nchi ya marekani. "Kila palipo na Ubalozi wowote wa Marekani. Katika nchi yoyote Duniani, kazima kuwe na Ulinzi unaoonekana na Ulinzi Usio onekana. Ulinzi Unaoonekana ni Ule Wa walinzi na mitambo mingine yakiusalama. Na Ule ambao hauonekani ni wa milipuko ambayo hupandikizwa chini ya Ardhi. Kwa hiyo unapotembea katika Sehemu Hiyo ni Lazima Uwe muangalifu na uwe Makini katika kile unachokifanya. Yalikuwa Baadhi ya Maneno kutoka kwa mkuu wake. Akatembea akiyafuatilia maelezo hayo. Bunduki ilikuwa mkononi akitembea mfano wa walinzi wenyewe. Hatua zisizo pungua Kumi mbele akawaona walinzi wengine watatu wenye bunduki na Sare mfano wake.. alichokifanya ni kuchomoa Bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia mli0. (Silence ). Ilikuwa ni lazima aitumie bastola hiyo katika namna ya kuirahisisha kazi yake. Ilikuwa ni ngumu kwa Sehemu Alipokuitumia mikono yake na Hata bunduki yake. Ndicho alichokifanya. Muda Mfupi Baadae Risasi zikatoka na kuelekea zilipotumwa. Hazikuweza kukosea njia katika namna yoyote ile. Kila risasi ilipita na kuingia Sehemu husika. Sehemu ambayo ilitumwa ama kuagizwa kufika hapo. Walinzi watatu walikuwa wakipaa angani katika namna Iliyotia Burudani kutoka kwa mtumaji mwenyewe. Hata Veronica alipofika eneo ambalo waliangukia Askari wale Hakuhangaika katika Kuwaangalia. Aliwapita Safari hii akiiingia ndani Ya Geti. Akiingia kama mlinzi wa Eneo husika. Akapita kana kwamba alikuwa akipita katika mlango wa chooni na hata nyumbani kwake. Hakuwa na mashaka, hakuwa na wasiwasi na hata hofu haikusomeka usoni na Hata machoni Mwake. Aliingia kama sehemu aliyoizoea na hata kuijua.

Wakati Veronica akilifanya hilo kwa upande wake. Upande Wa masimba hakuwa amekutana na ugumu huo. Upande wake hapakuwa na Labsha na hata kasheshe. Alipita hapa na pale kama kawaida. Ukuta Mrefu uliozunguka Jengo lile Haukuwa Tatizo kwake. Alijua angeweza kuingia. Mawazo yake yalikuwa ni Kumteka Teddy na kuondoka naye. Hakuhofia kile ambacho kingetokea. Muda mfupi alikuwa akitizamana na geti dogo na La Siri. Ni muda huo akilitizama hilo geti, akaliona geti likifunguliwa, kisha muda ule akawaona watu wakichungulia. Akabana kwenye giza. Punde akawaona makachero wa CIA ambao walikuwa wakihudumu hapo Wakitoka. Kisha wakafuata Walinzi Maalum Wa kiongozi wa Nchi. Mtu aliyefuatia alikuwa Teddy akiwa katikati ya Makomandoo kadhaa wa Marekani na Watanzania. Teddy alikuwa katika Ulinzi mzito kama kiongozi Wa Taifa la Marekani. Walinzi wenye Silaha Nzito walikuwa wakimuongoza na kumkinga. Licha ya kuonekana kwa Walinzi Maalum Wa Rais, lakini kiongozi huyo hakuwepo. Hakuwepo na hakuonekana kabisa hapo. Akili ya masimba ikafanyakazi kwa Haraka. Alijua Teddy alikuwa akiwapeleka Watu hawa Mahala ambapo alikuhifadhi kitu hiki. Wakati akiendelea kukiangalia hiki akamuona mtu mwingine akiwa kwenye mavazi yanayofanana na Walinzi. Naye alikuwa nyuma akifuatia. Mtu huyu wa mwisho kutoka akaufanya uso wake Uchanue kwa Tabasamu. Tabasamu malidhawa.. kwa Mara ya kwanza akaukubali uwezo wa Veronica. Kwa Mara ya kwanza akamuona Veronica kuwa ni Jasusi wa kutupwa. Kile kitendo cha kumuona katika Msafara ule wa majasusi wale wa CIA ni moja ya sifa kubwa Ambayo makachero wengi hawana. Lakini walikuwa wakielekea wapi na Teddy? Lilikuwa swali ambalo alijua angelipata Wapi na saa Ngapi. Akatulia akiendelea kuusoma Mchezo.
 
Naona Masimba anamvizia Teddy wake,amteke akambembeleze,kumuua hawezi.Mambo ya mahaba hayo.
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 084

Teddy alikuwa kwenye ulinzi wa hali ya juu. Ulinzi ambao uliongozwa na makomandoo sambamba na majasusi wa CIA. Lakini licha ya hilo, kilichomburudisha Zaidi ni Kule kumuona Veronica. Veronica aliyekuwa naye muda mfupi uliopita. Alikuwa katika msafara ule tena akiwa katika sare na mavazi maalum wanayovaa walinzi Wa Jengo hili la ubalozi wa Marekani. Amefikaje ndani na kuwa mmoja kati yao? Ni swali lililomsisimua Masinba, sio kumsisimua kwa woga ama burudani. Bali mwili ulimsisimka kwa utembeaji ule wa Majasusi wale. Walikuwa wakitembea kanakwamba wapo katika Ardhi ya Marekani. Licha ya kuinyonya nchi yenye rasilimali nyingi sana, pia waliimfanya Nchi hii kama shamba la kuchuma mali na kutokomea nazo. Akauvuta Muda naye akitaka kujua kule wanapoelekea. Hata walipompita pale ambapo alikuwa amejificha, bado Masimba alitulia akiwatizama. Alikuwa na Uwezo wa Kumtwanga Teddy Risasi, lakini Hakutaka iwe hivyo. Alitaka kumuonyesha Teddy kuwa anauwezo kuliko hata yeye. Alitaka kumuonyesha kuwa alikuwa akiifuatilia na kuipigania Tanzania. Akaruhusu Teddy na walinzi wake wampite. Akatembea nao kwa nyuma kila pale walipotembea. Alitaka kuwatizama ni wapi walipokuwa wakielekea. Alitaka kujua ni wapi Teddy ameuhifadhi betri ile. Majasusi wakimarekani wakazidi kutembea wakiingia Ndani Zaidi. Bado Veronica alikuwa nyuma na Hata Masimba hakuwa mbali na watu hawa. Tanzania yake ilikuwa katika moyo wake. Hakutaka kujua wapi alipokuwa rais. Alichotaka kufanya ni kukipata kile ambacho kilisababisha Teddy kuwa msaliti. Muda mfupi watu wale wakatokea katika barabara fulani ya vumbi. Hapo walikutana na msululu wa magari yapatayo matano. Yalikiwa magari yasio na namba. Yalionekana kuwa magari mapya. Baada ya Teddy na majasusi wale kuyafikia magari yale, milango ikafunguliwa katika aina fulani ya Uharaka. Teddy akatakiwa kuingia ndani ya Gari. Wakati Huku wakilifanya hilo kwa Teddy, tayari bastola ya Masimba ilikuwa mkononi. Tayari alikuwa tayari kulizuia hilo. Muda mfupi baadae alikuwa ameiruhusu Bastola kutoa Risasi. Risasi ambayo ilikwenda kutua katikati ya kifua kwa jasusi mmoja wa kimarekani. Akapiga yowe kubwa huku akitupwa angani mithiri ya furushi. Ilikuwa risasi iliyopenya katika kifua cha Jasusi yule. Risasi ikamtupa angani huku yowee kubwa likifuatia. Majasusi wengi wa kimarekano wakacharuka. Kila mmoja alikuwa akichupa na kuangukia mahala pengine. Kilikuwa kitendo kilichofanywa katika muda mfupi ambao ulimacha Teddy akiwa amesimama tena akiwa katika mzubao. Kulikuwa na uwezekano wa kumshuti. Lakini muda mfupi Komandoo mmoja wa kimarekani akampitia kwa kumbo mpaka chini. Kila kitu kilichokuwa kikitokea Masimba alikuwa pembeni akitizama. Kutokumuona Vero katika viunga vile, hakukumpa shaka. Hakukumpa shaka kwa kuwa alijua na kutambua kinachotokea. Hata yeye alikuwa akihama hapa akienda kusimama sehemu nyingine. Sehemu ambayo ilikuwa na giza totoro tofauti na kule alipotoka. Ukimya ulikuwa umechukua sehemu kubwa sana. Hapakuonekana uwepo wa watu. Hapakuonekana ni sehemu ambayo ilikuwa na Rabsha. Masimba akatulia akiendelea kutizama mbele. Kutizama kama angemuona Veronica. Komandoo yule aliyemkumba Teddy hakuinuka katika wakati ule. Alijua nini ambacho kinaendelea Hapo. Alijua watu wale walikuwa wakipotea katika namna fulani. Ni wakati huo akikiangalia hicho, ndipo hapo akakiona kile ambacho alitaka kukiona hapo mwanzo. Veronica Tayari alianza kugawa tiketi katika aina ile ile ambayo ilitakiwa. Miili ya watu kadhaa ilikuwa imetambarajika chini kuonyesha kuwa Vero alikuwa akiua watu taratibu. Ulikuwa uuaji ambao ulimfanya Masimba aamini kuwa huyu alikuwa Mafia kweli. Hilo likampa nguvu ya kuinuka na kuanza kusonga kuelekea kule kule. Kuelekea pale walipolala watu wale walioonyesha hawakuwa na Uhai. Hatua ya kwanza ikamuacha ikiivuka barabara, hatua ya pili alishaivuka barabara. Hatua ya tatu alijikuta akiisalimia Ardhi baada ya kujikuta akiisalimia Ardhi. Wakati akitaka kujitayarisha kuinuka akakutana na kitu kizito ambacho kilitua kisogoni na kumfanya Arudi chini. Giza likaanza kuyagubika macho yake. Akataka kujaribu kupambana na Giza. Hakuweza, hakuweza kwa kuwa alihisi kitu kingine kikitua kichwani. Hakupata nguvu na Uwezo Tena wa kufumbua macho yake. Alijikuta akizidiwa na giza. Akatulia kana kwamba Alikuwa Maiti.

********

Moscow Russia.

Mkurugenzi wa Shirika la Kijasusi la Urusi (KGB) Bwana Vandelov Pashovic. Alikuwa Ofisini kwake akiwa ametulia akiangalia hiki na kile upenuni mwa Ofisi ile ambayo ilikuwa katikati mwa jiji la Moscow. Alikuwa akiangalia hiki akiwaza kuhusu taarifa aliyoipata muda mfupi uliyopita kutoka africa, kuwa Kuwa shirika la Kijasusi la Marekani lilikuwa limeiuzia Nchini Ya Tanzania Mtambo maalum wa kutengeneza Kemikali hatari zinazotumika kuchanganywa na madawa ya kulevya. Mara ya kwanza baada ya kupewa taarifa hiyo alitaka kuipuuza. Lakini badala ya kuifuatilia hiyo taarifa na kuupata ukweli kuhusu hilo. Akajikuta akihitaji kulichunguza Hilo suala. Alihitaji kuujua huo Mtambo, alihitaji kuuondoa huo mtambo mikononi mwa Serikali ya Tanzania. Baada ya kutafakari kwa Kina akaona awasiliane na Vijana wake ambao walikuwa Nchini Rwanda kwa . maalum ya Umoja wa Mataifa. Aliwataka Vijana Hao waingie katika nchi ya Tanzania ili kuchunguza taarifa hizo na wampe Majibu katika Masaa sabini na mbili. Ni kweli vijana hao watatu wakaingia Nchini Tanzania kama Watafiti wa Masuala Ya Ufaidikaji wa Rasilimali kwa Watanzia Wenyewe. Walipoingia katika nchi ya Tanzania Cha kwanza Walichokifanya ni kuonana na Mtu Mmoja Aitwaye Mr Raymond ambaye alikuwa ni Mshirika wa karibu wa Genge la Mafia Katika nchi ya Italy. Ni mtu huyu ambaye aliletwa na Kanisa katoriki kama msimamizi mkuu wa madhehebu hayo katika Afrika. Msukumo wa kuonana na Mtu huyu, ulitokana na Taarifa ambayo waliipata baada tu ya kuingia Chini Tanzania kuwa kuna mzee mmoja anaweza kuwasaidia katika Hilo. Ni usiku huo ambao Vijana wale walifika pale, ndio usiku ambao Walikutana na Veronica. Kukutana kwao hapo ni baada ya Veronica kuitwa na Mr Raymond kukifuatilia kile kile ambacho vijana hawa watatu walitaka kuijua Taarifa yake. Baada ya vijana hawa tatu kufika katika makazi ya Mzee Huyu ambaye alipachikwa cheo cha Usimamizi wa makanisa ukanda wote wa Africa ya Mashariki. Ndipo walipokutana na Veronica Senka Ambaye naye alitumwa na Genge la mafia kuufuatilia mtambo huo ambao kwa upande wa Kundi la Mafia waliihitaji betri pekee ambayo ndio husukuma Mtambo huo. Baada ya vijana wale kufika na kufanya mazungumzo ya kina na Mzee Raymond kisha kugundua kuwa wapo katika kufuatilia kitu kimoja. Wakatuma Taarifa hiyo kwenye Ofisi za KGB Jijini Moscow. Baada ya Taarifa Hiyo kutua mezani kwa mkurugenzi wa KGB. Mazungumzo ya kina yajafanyika kwa pande mbili. Upande wa Mafia pamoja na Shirika la Kijasusi la Urusi. Baada ya mazungumzo ambayo yalichukua Takribani siku sita makubaliano yalifikiwa kwa Shirika la kijasusi la Urusi kukubaliana na Kundi la Mafia kuangalia Namna ya Kuipata hiyo betri kisha watajua nini cha kufanya. Baada ya makubaliano Hayo Kufikiwa. Veronica ndipo alipopewa Jukumu la kuipata Hiyo Betri Kutoka mikononi mwa Serikali ya Tanzania. Jukumu ambalo alitakiwa kulifanya akiwa na Special Agent's wa KGB. Kazi ya kufuatilia ikaanza kwa Watu hawa kuanza kujiingiza ndani ya Serikali. Ni katika ukaribu huo wakaweza kuunda ukaribu na Serikali hasa kwa Waziri. Ni katika ukaribu huo ndipo walipoambiwa Betri Hiyo ipo mikononi kwa watu wawili ambao waliheshimika katika jamii yote ya Kitanzania. Wakati hilo likiendelea likatokea Suala la kupotea Kwa mzigo wa Mamilioni ya Shilingi. Mzigo ambao ulichukuliwa katika mazingira ambayo special Agent's wa KGB pamoja na Veronica walikuwa nyuma ya Hilo. Nikatika hilo kuliko ibua mzozo kati ya Washirika wa mzigo huo. Ni mzozo huo uliomuibua Masimba, ni mzozo huo ambao ulichukua maisha ya Asteria P Paulo ambaye alikuwa akiujua ukweli. Wakati Special Agent's walipomuua Asteria Walikuwa wakipata maagizo kutoka kwa Teddy na Hata Veronica. Kwahiyo Veronica na Teddy ni watu ambao wanafahamiana lakini pia ni watu ambao walikuwa wakiwakilisha mashirika tofauti. Wakati Teddy akiwa ni Afisa Usalama wa Shirika la kijasusi la Tanzania (Tiss) pia alikuwa ni Special Agent wa Shirika la kijasusi la Marekani CIA (Central Intelligence Agency ). Pia Veronica Alikuwa ni Special Agent wa Mafia, na Vile vile alikuwa akiwakilisha shirika la Kijasusi la Urusi (KGB) (KOMITET GOSUDARSTVENNOE BEZOPASNOSTI) AMBALO kwa kiingereza lilijulikana kama (committee for state Security, foreign intelligence and Domestic security Agency of the Soviet Union ). Licha ya kufahamiana Huko na kuifanya kazi kwa pamoja. Teddy na Veronica Kila mmoja alikuwa akitumiwa na Mtu ambaye yupo nyuma. Wakati Teddy akitumiwa na Viongozi Wakuu wa Nchi. Veronica yeye alikuwa akitumiwa na Mzee Raymond wa Kundi la Mafia. Waliifanya kazi ya kufuatilia Mtambo Hasa Wakiitaka Betri ya ule mtambo. Wakati wao wakiendelea ndipo hapo Masimba alipoibuka na kuanza kulifuatilia hilo suala. Kitendo cha masimba kuanza kulifuatilia lile suala kukaleta Ugumu katika kufanikisha uzalishaji wa Kemikali hizo kitendo ambacho kilisababisha rais Amruhusu Teddy kumuua Masimba. Wakati mpango wa kumuua Masimba ukiendelea kusukwa kwa umakini ndipo ulipotokea Mzigo wa Madawa kupotea nyumbani kwa Jimmy. Kabla suala la Mzigo halijapoa ndipo yalipotokea Mauaji Ya Waziri. Mauaji Ambayo yalifanyika baada ya Waziri mkuu kumteka teddy, kisha kutaka kwenda kumuingilia kimwili. Mauaji ya waziri mkuu ndiyo yalimfanya Rais Aamue kuitoa Betri ile Kisha Kuikabidhi kwa Watu Wawili ambao walikuwa Maarufu Sana Katika Jamii kutokana na Ucha Mungu Wao. Betri ilikuwa mikono mwa Askofu Ibrahim Lexandre Rengima sambamba na Sheikh mkuu Wa Mkoa Dk Ramadhani Chilemba. Hili suala alilifanya Rais Kwa Siri akimshirikisha meja Jenerali Chomboko. Licha ya kulifanya hili kwa Siri, lakini Veronica na Teddy waliinusa fununu ya hilo. Na siku ambayo alipewa maagizo na Masimba kwenda kumuua Askofu na kukuta ameshauawa. Alitambua veronica ndiye aliyeyafanya mauaji yale. Licha ya kumuwahi Baba askofu lakini hawakuipata bahasha kwa kuwa Baba Askofu Hakuwa tayari kuitoa kwa kuwa alitaka imfikie Masimba. Kwahiyo Veronica na Teddy walikuwa ni watu wawili wanaofanya kazi pamoja lakini kila mmoja akiwakilisha upande Mwingine. Baada Ya Veronica kugundua masimba anauwezekano wa kuipata Ile betri ndipo hapo likipoundwa Tukio fake ili kumuaminisha masimba kuwa Veronica Alikuwa mtu sahihi Kwake. Ndio maana aliipata hamu ya kwenda pale Kanisani kuonana na mzee Raymond Bila kujua kuwa watu hawa hawakuwa upande wake.

*********

Alifumbua macho taaratibu kama mtu aliyekuwa akitoka kwenye usingizi. Maumivu nyuma ya kichwa chake yalimkumbusha kitu kilichotokea Mpaka yeye kufika Hapo Ndani. Akataka kuupeleka mkono wake kisogoni, lakini alipojaribu kufanya hivyo akajikuta hawezi kwa kuwa mikono yake ilikuwa imefungwa pingu. Akaendelea kuangaza huku na huko kama angeweza kuona kitu. Lakini Giza totoro ndani ya Chumba kile, halikumpa uwezo macho yake kuona Chochote. Akatulia akimuwaza Veronica. Alitambua kama Veronica ameliona tukio la kutekwa kwake, basi atafanya lolote kumuokoa. Hakujua kwamba hata Veronica Hakuwa Rafiki kwake.
 
Dah Veronika umemrubuni masimba jaman!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom