Riwaya: Nitakupata tu

Riwaya: Nitakupata tu

Duuuuh mambo bado magumu jaman masimba masimba
 
Ahsante Sana Mkuu, kweli ninayo bahati mbaya lakini cjamkuta ndugu yangu Masimba huyu ndugu anapata bahati mbaya hasa
 
NITAKUPATA TU

SEHEMU YA 085

Ilikuwa sehemu ngeni machoni mwake, licha ya ugeni huo lakini vile vile Giza lilikuwa limechukua sehemu yake, macho yake hayakuweza kukiona chochote kilichopo hata hatua tatu kutoka pale alipolazwa. Mikononi alikuwa na pingu kuonyesha kuwa alikuwa mikononi mwa watu wa usalama. Maumivu kichogoni yakairudisha kumbukumbu yake, kumbukumbu ambayo ilimrudisha mpaka viunga vya ubalozi wa Marekani. Kumbukumbu iliyomkumbusha mapigo mawili aliyoyapata wakati alipokuwa akiiruka miili ya marehemu. Hisia kuwa ulikuwa mtego juu yake zikampitia kichwani. Miili ya watu kutambarajika chini, kisha muda ule ule kushambuliwa. Haikuwezekana katika hilo. Haikuwezekana katika kuliamini kichwani mwake. Licha ya kuamini huko, lakini alipomkumbuka Veronica tabasamu likatamalaki, tabasamu ambalo liliishia usoni kwake. Tabasamu ambalo halikufika kwa mwingine Zaidi Yake. Hakujua kuwa Veronica Ni Special Agent wa Mafia na KGB, hakujua kuwa Veronica Alikuwa Naye akiihitaji Ile betri. Hakujua kuwa Veronica na Teddy walikuwa wakufahamiana. Walikuwa katika mission moja lakini kwa malengo tofauti. Aliamini Vero alikuwa ameshuhudia kutekwa kwake. Alitambua muda wowote angefika Hapo. Akauvuta muda huku akijaribu kuifanya mikono yake kutoka Nyuma na kurudi kwa mbele. Lakini kabla hajafika popote akausikia mlango ukifunguliwa kisha kuisikia miguu ya mtu ikitembea Taratibu kuelekea pale alipokuwa Amelala. Hisia kuwa mtu huyu alikuwa sio mwema kwake ikamjia kichwani. Muda mfupi kidogo akajibingilisha na kuihama ile Sehemu. Ni sekunde mbili ya kufanya hivyo akapishana na mvua ya Risasi zikichimba Mahala ambapo alikuwepo. Baada ya Risasi kuvurumishwa kwa muda kisha kuachwa, taa za chumba kile zikawashwa. Sehemu yote ikawa nyeupe kutokana na Mwanga. Mbele ya macho yake Alikuwa amesimama Teddy akionyesha kushangazwa. Licha ya Risasi alizopiga lakini sehemu haikuwa na Mtu. Risasi za Semi Automatic zilikwenda patupu zikiichimba Sakafu. Teddy akashikwa na mshangao, mshangao ambao ulimpa masimba mwanya wa kusimama na kwenda kumkumbuka. Wote wakaanguka chini huku bastola ikiruhusu risasi ambazo hazikuleta madhara. Sasa ilikuwa ni purukushani. Teddy alikuwa Chini huku masimba akuwa juu akimkandamiza kwa mikono yake miwili. Teddy alikuwa akifurukuta. Teddy hakuwa na uwezo wa kugeuka. Lakini wakati hilo likiendelea Masimba alijikuta kitu chenye ncha kali mfano wa sindano kikiingia shingoni. Haukupita muda mrefu masimba akayaona macho yake yakiingia giza. Muda ule ule akawa kimya. Teddy aliinuka kutoka pale chini alipokuwa amebanwa akiwa ameishika shingo yake huku akikohoa. Bila kujali Masimba alikuwa katika hali gani, Teddy akaanza kumtandika masimba kwa Mateke huku akitukana na matusi ya nguoni. Baada ya kumtandika vya kutosha Teddy alimuacha Masimba akivuja damu kisha yeye kuondoka. Watu wawili walioonekana kuwa walinzi walimuangalia Masimba kwa Muda Mrefu bila kuongea kitu. Masimba alikuwa amelala kama mzoga akionyesha kama hakuwa na Uhai. Mateso yote hayo kwa sababu ya kuitetea nchi yake. Ilikuwa akiitetea Tanzania na watu wake.

Alikuwa amelala chini mfano wa mfu. Hawakujali hilo wala Teddy hakuiona huruma kutoka moyoni mwake. Alisahau mapenzi yao, akasahau wema wa masimba. Akasahau ahadi zote.. na hata mwisho kuutoa upendo ndani ya moyo wake. Hakuwa Teddy yule wa kipindi kile. Huyu alikuwa mnyama. Huyu alikuwa tayari kumpoteza masimba kwa mkono wake. Huyu alikuwa tayari kumuua. Tayari betri ilikuwa mikononi mwake. Tayari alishafanya mawasiliano na Makao makuu ya CIA kuwaeleza kila kitu. Kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea kwenye mission hii. Hakuwa na mapenzi tena na Masimba. Hakuwa na mapenzi tena katika moyo wake. Alitii miko ya ujasusi, alitii kanuni za kikachero. Teddy hakuwa na ile huruma Tena. Teddy alikuwa akiusadifu utaalam wake. Masimba akaburuzwa na kuwekwa ndani kabisa. Damu bado ilikuwa ikishuka taratibu kutoka mdomoni, puani na hata sehemu nyingine za mwili. Wakamuacha hapo kamzoga ulioachwa ufe. Mlango ukafungwa na taa zikazimwa Tena na watu wote kuondoka mle ndani. Masimba bado alikuwa chini akiwa hanafahamu. Wadudu wakali wakaanza kumshambulia kutoka pale chini. Hakujua chochote kwa kuwa alikuwa amepoteza fahamu. Akaendelea kushambuliwa kwa usiku ule. Hata kulipokucha mwili wake ulikuwa umefimba, mwili wake ulikuwa hautamaniki kwa kuutizama. Hakuwa akiangalika na hata kutamanika. Alikuwa sio masimba yule aliyekuwa akipambana, hakuwa masimba yule aliyekuwa akiwadhibiti watu takribani Ishirini. Huyu alikuwa mfu ambaye alibakiza muda mfupi tu kuivuta Pumzi ya Dunia hii. Aliachwa afe taratibu, aliachwa apotee katika chunba kile. Hapakuwa na Msaada tena.

******

"Hapana Haiwezekani, nasema haiwezekani. Siwezi kumuacha Masimba afe, siwezi kuliacha hili litendeke. Masimba hastahili kufa, masimba hastahili." Aliongea Veronica akiwa amekaa chumbani kwake. Alikuwa amejikunyata akifikiria hali ambayo alikuwa nayo Masimba. Ilikuwa ni lazima afanyekazi kumuondoa pale ndani ya chumba alichofungiwa. Kwa mara ya kwanza alikuwa akikiuka miiiko ya mafia. Alikuwa akikiuka miiko ya kijasusi. Aliamua kuutoa Moyo wake kwa sababu ya Masimba. Muda mfupi uliopita alimuona Masimba akiwa katika hali ambayo ilimhuzunisha. Kwa muda mfupi ambao alikuwa amekaa na Masimba alitokea kumpenda sana. Alitokea kumheshimu na kuipenda kazi yake. Alikuwa mzalendo na Alikuwa mpiganaji wa Kweli. Veronica akajiinua pale kitandani. Akaelekea mpaka kwenye droo. Alipofika aliifungua kisha kuchomoa bastola yake na kuipachika kiunoni. Baada ya hapo akatoka moja kwa moja mpaka Nje ya hoteli anayoishi. Kufika hapo akasimama kwa muda kabla ya kuchukua usafiri wa tax kuelekea bagamoyo kwenye moja kati ya kambi za Siri za Idara ya Usalama Wa Taifa. Sehemu ambayo ndipo alipohifadhiwa masimba. Hakujutia kile ambacho kingetokea baada ya hapo. Alichowaza ni kumtoa Masimba katika Eneo lile. Hakujali adhabu atakayo pewa atakapo Gundulika. Alikuwa tayari katika mapambano yoyote ambayo yangemlazimu. Ulikuwa usiku hivyo barabara iliruhusu. Tax ilikuwa ikitembea katika mwendo wa kasi sana. Muda mfupi walikuwa wakiingia bagamoyo. Kufika bagamoyo Veronica akashuka kisha kulipa, harafu akachepuka kuingia kwenye uchochoro ambao ulimuongoza moja kwa mmoja mpaka kwenye jengo fulani ambalo kwa Nje yake ilionekana ni kama kampuni Fulani. Kwa kuwa alijulikana hakupata tabu ya kuingia ama kuulizwa maswali. Alichokifanya ni kuingia moja kwa moja mpaka ndani kabisa. Jengo lilikuwa kimya kuonyesha kuwa hapakuwepo na walinzi wengi. Alitembea akikutana na baadhi ya wana usalama, lakini kwa kuwa alikuwa akifika hapo, Veronica aliachiwa apite. Muda mfupi alikuwa kwenye chumba ambacho alihifadhiwa Masimba. Bado alimkuta Masimba akiwa bado yupo kwenye hali mbaya. Bado alikuwa amelala pale pale damu zionekana kuganda. Veronica alimuangalia masimba kwa Muda, alimuangalia kwa kipindi kirefu sana. Kwa mara ya kwanza Chozi lake likashuka na kudondoka chini. Alikuwa akilia kwa mara ya kwanza. Akamuinamia na kumgusa kifuani. Akagundua alikuwa akihema kwa nguvu, aligundua Masimba bado Alikuwa Hai. Alichokifanya ni kusogea pembeni na kuiziba na kitambaa camera ya Usalama. Baada ya kuhakikisha kuwa kila kitu kipo tayari, Veronica akachuchumaa kujitutuma kwa nguvu zake zote. Akafanikiwa kuumbeba Masimba na kuanza kutoka naye kwenye chumba kile. Kwa kuwa aliifahamu ile kambi vizuri, hakupata tabu katika kutoka huku akiwa na masimba begani. Baada ya kufanikiwa kutoka hapo salama. Aliingia ndani ya Msitu ulioizunguka kambi ile. Alitembea akiwa na Masimba begani bila wasiwasi. Alihitaji kufika kwenye kijiji chochote kile ili kuutafuta Usafiri ndani ya Usiku ule tayari kwa kuondoka na Masimba kuelekea Sehemu yoyote ile ambayo itakuwa mbali na Bagamoyo na Hata Dar es salaam. Alitembea usiku ule wa giza bila kukutana na kitu chochote. Ingawa alikuwa amechoka lakini hakutaka kupumzika. Baada ya kutembea kwa muda wa masaa mawili, hatimaye akatokea kwenye kijiji kimoja ambacho hakikuwa na nyumba nyingi. Baada ya kutokea kijijini hapo, akapata matumaini ya kuupata usafiri wa kuwaondoa Sehemu hiyo. Alisimama kwa Muda wa saa kama moja hivi akiusubiria usafiri. Lakini bado hapakutokea usafiri aina yoyote. Akaendelea kuvuta muda, mara wakausikia mngurumo wa Gari Ukitokea umbali fulani kuonyesha kuna Gari ambayo ilikuwa akija maeneo yale. Veronica Akamuinua Masimba na kusimama katikati ya Barabara huku Masimba Akiwa Begani. Punde akauona mwanga wa taa za gari ukitokea kwa mbele yake. Ilikuogopa kuwatisha watu kwenye gari, akaichomeka Bastola yake kiunoni. Akaanza kuupunga mkono hewani. Gari ikaendelea kuja kwa mwendo wa kawaida. Gari ilipofika karibu na aliposimama Veronica, Ikasimama.

"Naomba Msaada mpenzi Wangu anaumwa." Aliongea Veronica Huku akisogea Dirishani.

"Mnaenda Wapi kwani? Kwa nini usimpeleke Bagamoyo Mjini? Aliuliza Dereva huku akiufungua mlango na Kushuka. Kitendo cha Dereva Huyu kushuka kilikuwa kikisubiriwa kwa hamu na Veronica. Muda ule ule mdomo wa bastola ulikuwa Shingoni kwa Dereva yule. "Naomba tusaidiane kumpandisha Huyu mgonjwa wangu Garini. Nitakupa kiasi fulani cha pesa. Ila ukileta ujanja maiti yako itaokotwa Hapa kesho." Alinguruma Veronica huku akiendelea kuugandamiza mdomo wa Bastola shingoni kwa dereva. "Taratibu dada na bastola hiyo. Nipo tayari kukupeleka popote." Alijibu dereva huku akimshika Masimba Vizuri. Veronica Hakujibu, alichokifanya nikusaidiana na Dereva yule, punde walikuwa Njiani wakielekea Chalinze, kupitia msata. Ndani ya gari hapakuwa na mtu wa kuongea na mwenzake. Veronica Alikuwa kimya akiifikiria hali ya Masimba, wakati Dereva alikuwa akifikiria Bastola Aliyoshikiwa na Mwanamke huyu. Baada ya ukimya wa kipindi kirefu, dereva akashindwa kuvumilia.

Akaona Amuulize Veronica. "Dada kwani Mgonjwa Anatatizo gan?.

"Haikuhusu, unachotakiwa Endesha gari nisijefumua kichwa chako kwa Risasi.," akajibu Vero akionyesha hakutaka Mashauriano wala hakuhitaji kuulizwa Maswali. Lakini kwa upande wa Dereva hakukoma kuuliza maswali. Aliendelea kuuliza maswali huku akiuondoa woga machoni mwake. "Dada Hali ya mgonjwa ni mbaya, kumbuka hapa tupo wawili na gari yenyewe haitembei kwa mwendo wa Haraka. Tunachotakiwa ni kuutafuta msaada. Msaada wa kumsaidia huyu mgonjwa. Hayo mambo ya Amri achana nayo." Alisema yule dereva huku akimuangalia Veronika. Veronica akabaki kimya akifikiri cha kufanya. Kichwa chake kilikuwa na vitu viwili. Kimoja ni kutaka kumuamini Dereva na Chapili ilikuwa ni kutokumuamini. Baada ya kufikiria sana akaona amuamini. Akaona ni kweli kile kilichosemwa na Dereva. "Nahitaji msaada, mpenzi wangu amechomwa sindano ya sumu. Mpaka kufika Chalinze naweza kumpoteza. Naomba unisaidie. Ila nakuonya Ukiufungua Mdomo tu.. Nitakuua kwa mikono yangu." Aliongea Veronica Akionyesha Hatanii. "Sawa nitazingatia Dada yangu."alijibu Dereva Huku akihama barabara ya rami na kuingia ya Vumbi. Gari ikatembea usiku ule mpaka katikati ya Pori. Giza lilikuwa limetanda kila upande. Veronica tayari Bastola ilikuwa mkononi. "Tumshushe Mgonjwa tutembee nae." Akaongea dereva huku akimshusha Masimba toka ndani ya gari, kisha kumuweka Begani. Safari ya kutembea kuelekea katikati zaidi ya msitu ikianza. Walitembea kwa muda wa dakika kumi. Mbele yao wakakiona kijumba cha bati. Kilikuwa kijumba ambacho kilijengwa katikati Ya msitu. Baada ya Dereva kukifikia kibanda akamshusha Masimba na kumuweka chini. Wakati akijiandaa Kuugonga Mlango, Akasikia sauti ikitoka nyuma yao. Tulia Hivyo hivyo na Utupe Bastola yako Chini. Veronica Akatiiiiiiii
 
NITAKUPATA TU

Mbele yao wakakiona kijumba cha bati. Kilikuwa kijumba ambacho kilijengwa katikati Ya msitu. Baada ya Dereva kukifikia kibanda akamshusha Masimba na kumuweka chini. Wakati akijiandaa Kuugonga Mlango, Akasikia sauti ikitoka nyuma yao. Tulia Hivyo hivyo na Utupe Bastola yako Chini. Veronica Akatiiiiiiii
duh hadi huku porini ni mwendo wa kutekana naomba wasiwe watu wabaya Masimba apate msaada
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom