[06-09, 15:30] Ibrahim Masimba: NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 079
Wakati Teddy akisubiri gari ili kuondoka eneo lile, ndio Muda Huo ambao Masimba alikuwa akishuka hapo akiwa katika mawazo sana. Alitembea taratibu akihakikisha hakuna macho ya mtu ama watu yanayomuangalia. Muda wote alikuwa makini kwa Kila Hatua. Wakati anaukaribia mlango wa nyumba ile akauhisi mwili wake ukisisimka. Kitendo hicho kilitokea vbaada ya kuuona mlango wa nyumba ile ukiwa wazi. Haikuwa kawaida kwa mlango wa nyumba kama hizo kuwa wazi, haikuwa kawaida kwa kuwa ni sehemu ambayo haikupaswa kuachwa wazi. Akajikuta akijipapasa mfukoni mahala ambapo aliihifadhi bastola yake. Alipoigusa akaachia tabasamu mwanana. Akaipiga hatua nyingine huku miguu na mikono ikiwa tayari kwa lolote. Akaufikia mlango kisha kuingia moja kwa moja ndani. Kengele za hatari zikalia baada ya kukutana na michirizi ya Damu. Michirizi ambayo iliachwa kutokana na muonekano wa kitu kilichojiburuza. Roho yake ikampaa huku bastola ikiwa mkononi mwake. Miguu ilikuwa ikimtetema kila pale alipohisi kuwa Mtu aliyeiacha damu hapo ni Teddy. Hakuwa Tayari Teddy afe, hakuwa Tayari Teddy auawe. Hakuwa tayati kumpoteza Teddy kutokana na kuwa alimpenda. Alimpenda zaidi ya anavyowaza na Hata kufikiria. Akaufuata mburuziko ule. Hatua tatu mbele akakiokota kitu, kitu kilichomfanya akubali kuwa mtu aliyepigwa Risasi alikuwa Teddy. Chini aliiona bahasha. Bahasha ambayo ilikuwa na Siri kubwa. Akaikota huku mikono ikitetemeka. Moyo ukazidi kumpasuka baada ya kuiona bahasha imefunguliwa huku kile kilichodhaniwa kuwa siri hakikuwepo. Akahisi Dunia ikizunguka. Ni vipi kama Teddy ameuawa na kilichopo ndani ya Bahasha kupitea? Ataishi kweli katika amani wakati kilichopo ndani ya bahasha ndio kilikuwa kitu cha kumuweka kwenye usalama? Akaitupa bahasha na kuzidi kuufuatilia ule mburuziko. Mbele kidogo akamuona mtu ambaye hakuamini kama alikuwa Yeye, Meja Jenerali chomboko alikuwa amelala katikati ya Dimbwi la Damu. Damu ambayo ilikuwa ikitembea sakafuni kuonyesha mauaji haya hayakutendeka muda mrefu. Hilo likamfanya Masimba azidi kuchanganyikiwa. Muda mfupi baadae alikuwa pembeni mwa mwili wa Meje Jenerali Chomboko. Masikio yake yakausikia mkoromo na sauti dhaifu kutoka kwa Mzee huyu. Hii ilimaanisha kuwa hakuwa amekufa, alikuwa katika hatua za mwisho kufa. Akamuinamia na kujaribu kuongea naye.. lakini haikuwezekana, haikuwezekana kwa kuwa mzee hakuwa akiongea chochote. Hakuweza kuongea kwa kuwa hakuwa na muda mrefu wa kuishi. Hakuonyesha kama ni mwenye kupona. Punde akauona mkono wa Mzee Chomboko ukinyooka huku kidole chake kukichofya katikati ya Damu kisha kuandika pale sakafuni. "Teddy ameasi. " yalikuwa maneno makali yalioukata Moyo wa Masimba. Akajikuta akitetemeka huku Hasira juu ya Teddy ikizidi kuchukua nafasi. Akiwa katika Hilo akamuona Mzee chomboko akinyoosha miguu, kisha kutulia. Alikuwa amekufa, alikuwa amekufa katika kifo cha kumpigania yeye. Teddy alikuwa amesababisha kupotea tena kwa mtu muhimu katika Maisha Yake. General chomboko alikuwa ni mtu muhimu kwake akimlinda katika hatari, hatari ambayo ingeshampoteza. Leo hii alikuwa amelala katikati ya dimbwi la damu tena akiwa maiti. Tena akiuawa na Mkono wa Teddy. Teddy aliyekuwa akilia muda mfupi uliopita. Teddy aliyenusurika kuuawa mara kadhaa. Teddy aliyesema alikuwa akimpenda, aliyekuwa akimhitaji na kulia kwa Ajili yake. Lakini leo hii amemuuua Mzee chomboko na kutoroka na bahasha ambayo ndiyo ilikuwa zamana ya Maisha yake. "TEDDY NITAKUPATA TU NA NITAKUUA KWA MIKONO YANGU." Baada ya kutamka hilo akainuka na kutoka katika jengo hilo la Siri. Maandishi ya jenerali chomboko yalikuwa yakijirudia Kichwani "TEDDY AMEASI". Alihisi akili yake haifanyi kazi kwa muda ule. Hakuiona furaha tena. Wakati hilo likiendea kumsumbua kichwani, simu yake ya mkononi ikatoa mlio. Ilikuwa ikiita. Akaichomoa na kukutana na Jina la Chief. Mkurugenzi Wa Idara ya Ujasusi alikuwa akimpigia.
Akaipokea haraka na kuipeleka sikioni. "Naomba wahamishe watoto wangu kutoka hapo walipo. General Chomboko No more. Teddy Ameasi na Bahasha ametoroka nayo." Aliongea masimba kwa Haraka bila kusubiri maelezo. "Nililifahamu hilo mapema, nilimfahamu yule mtoto ni mwenye tamaa. Vijana wangu wamemuona katikati ya Mji. Nadhani anataka kwenda kuonana na Rais. Cha kufanya wewe sasa hivi unatakiwa kushughulikiwa. Kwahiyo unachotakiwa ni kuwa makini na usijionyeshe. Vijana wangu wapo sambamba naye na nataka wamzuie kabla hajaingia lango la Ikulu. Nimehuzunika sana kumpoteza Chomboko. Teddy Hastahili kuachwa Hai. Ukishindwa wewe nitaifanya mimi hiyo kazi." Aliongea Chief kisha kukata simu. Masimba akaganda kwa muda, Teddy ameonekana katikati Ya Mji. Anaonyesha kuwa anaelekea Ikulu. Ni maelezo hayo yaliompa masimba muelekeo sahihi kwa kipindi hicho. Damu ya Asteria P Paulo Damu ya Dee Plus damu ya Mama yake na Sasa Damu ya Mzee chomboko ilikuwa mikononi mwake. Ulikuwa ni muda wa kuilipa Damu Hiyo. Ulikuwa muda wa kuwawahi kabla ya kumuwahi. Ulikuwa muda wa kuelekea Posta, ulikuwa muda wa kutembea kila anapokanya Teddy. Ilikuwa ni lazima ampate. Ilikuwa nilazima Amuue.
******
Alikuwa akitembea bila kujua alikuwa akitembea na watu. Hakujua kuwa vijana wasiopungua wanne walikuwa wakitembea naye kwa kila hatua. Walitakiwa kuhakikisha haiingii katika viunga vya ikulu. Hiyo ndio ilikuwa amri kutoka kwa Chief. Teddy hakujua kuwa wauza urembo wawili, muuza pweza kwenye sinia na hata muuza vitambaa walikuwa vijana ambao walikuwa wakimfuatilia yeye. Aliwachukulia kama wamachinga bila kujua kuwa yupo kwenye tageti. Alitembea Kwa mwendo wa kawaida mpaka eneo la Feri. Akatafuta sehemu nzuri na kutulia kandokando ya bahari. Alikuwa akitizama maji huku mawazo yakimzonga. Kile alichokifanya alijua sio kizuri lakini moyo wake ulikuwa tayari kwa lolote. Kwa kuwa alitambua Kitu alichokichukua Kwenye Bahasha ndio dhamana ya Uhai wa masimba. Alijua Masimba Angeuawa muda wowote kitu ambacho kitasababisha yeye kupata pesa zote. Hilo likamfanya asahau mapenzi na ubinadamu wote. Alikuwa tayari Masimba afe ili mradi yeye achukue mamilioni ya shilingi. Muda wote vijana waliokuwa wakimfuatilia bado hawakumpa nafasi. Lakini wakati wakiendelea na hilo wakamuona Teddy akisimama akitembea taratibu kuelekea soko la samaki feri. Hata wao bado walikuwa nyuma katika namna hiyo hiyo. Wakimuangalia kwa umakini. Teddy akaingia ndani ya Soko la samaki, lakini wakatia akiingia hapo akageuka kwa chati kutizama nyuma. Tabasamu la kugundua kitu fulani likatamalaki. Aligundua kuwa alikuwa akifuatiliwa kwa nyuma na vijana wa usalama wa Taifa. Hapo akaongeza umakini akiitafuta njia ya kuwatoroka watu hawa. Kitendo cha kuwaona watu hawa wakimfuatilia, kulitoa majibu kuwa tayari ameshagundulika kile alichokitenda. Kilichokuwa kikimpa nguvu ni kule kujua kuwa Masimba alikuwa Ikulu na isingeweza kutoka huko. Na mpaka kuja kutoka kwake, yeye tayari alikuwa yupo mbali na hatakuwa hapa nchini. Kwa mara ya kwanza akamkumbuka Jimmy, ilikuwa ni lazima ukutane na Jimmy. Ilikuwa ni lazima aongee na Jimmy ili kufanikisha adhma yake. Alijua kabisa akichelewa na akaingia mikononi kwa masimba basi angeuawa hata kwa kukatwakatwa. Hakuwa tayari kwa hilo. Ilikuwa ni Lazima amtafute Jimmy. Au ilikuwa lazima Atafute njia ya kuonana na Rais Wa Nchi. Alikuwa tayari kuitoa karatasi ile aliyoichukua kwenye bahasha. Ilikuwa tayari kuitoa ili apate pesa za kumuondoa hapa nchini.
**********
[06-09, 16:04] Ibrahim Masimba: Alishuka posta mpya akiwa kwenye utofauti wa sura, mavazi na hata utembeaji. Alikuwa ni kama babu kizee mwenye kutembelea mkongoja. Mvi zilipangana kichwani kuonyesha kuwa mzee huyu alikuwa amekula chumvi nyingi. Baada ya kushuka hapo akasogea pembeni sehemu ambayo hukaa watu. Naye akakaaa hapo. Baada ya kukaa, akatoa kitabu chake na kuanza kusoma taratibu huku macho yake yakizunguka kwa hila yakiitizama sura ya kila apitaye na hata wale ambao walikuwa wakipanda magari. Alikuwa masimba akiwa hapo kwa sababu maalum. Alikuwa hapo akimtafuta Teddy katika Utofauti kama huo. Aliamua kuingia kazini kwa staili hiyo akiamini anaweza kuuepuka mkono wa wana usalama. Pia alitambua angeweza kumpata Teddy kwa urahisi. Muda wote macho yake hayakutulia sehemu moja. Alikichunguza hiki na kukiangalia kile. Hata waliokuwa kwenye bajaj alikuwa akiwatizama katika namn ambayo hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kuligundua Hilo. Muda ukasonga bila kumuona mtu. Kagiza kakaanza kuiingia akiwa bado yupo hapo. Alikuwa ametulia safari hii akionyesha akipuliza kiko. Moshi ulikuwa ukipaa hewani taratibu na kuileta burudani kwenye nafsi yake. Wakati akilifurahia hilo simu yake ikaingia Sms.. "Kuku wako imeshindwa kuingia kwenye banda. Wanao wamemtafuta lakini hawamuoni." Ulikuwa ujumbe ulioandikwa kwa lugha ya mafumbo. Ujumbe ambao ulipokelewa kwa mwili wake kusisimka. Teddy alikuwa amewapotea vijana waliokuwa wakimfuatilia. Ilikuwa taarifa iliyousisimua sana mwili wake. Taarifa ambayo ilimfanya ahisi Teddy alikuwa ameshagundua hilo la kufuatiliwa. Akasimama hapo akitaka kuelekea upande wa pili wa barabara. Wakati ikitaka kulifanya hilo, akamuona mwanamke aliyevaa nguo chakavu huku juu akiwa amebeba kapu lililoonyesha kuwa lilikuwa na samaki. Licha ya uchakavu wa mavazi, licha ya ubebaji wa Kapu lile, licha ya kuonekana kama muuza Samaki, bado hakuweza kumpotea Masimba, bado hakuweza kumpoteza masimba. Alimtambua na alimjua. Lakini kwa nini yuko hivi? Lilikuwa swali ambalo halikujibiwa, lilikuwa swali ambalo halikupata muda wa kuulizwa. Misuguano ya tairi za gari zikaleta mayowe kwa watu waliokuwa karibu na kituo cha daladala posta mpya. Gari aina ya Coaster iliyokuwa ikifanya safari yake kati ya Mbezi na Posta ilikuwa nyang'anyang'a baada ya kugongwa na gari kubwa iliyokuwa akipita kwa mwendo wa kasi. Hilo likaifanya shingo ya Masimba kugeuka, kugeuka kutizama kwenye ajali hiyo. Hata pale alipokuja kugeuza shingo na kukumbuka kuwa alikuwa amemuona Mwanamke Anayemfahamu.. Hakuweza Kumuona Tena, licha ya kutokumuona lakini pia hata lile kapu alilokuwa amelibeba kichwani, lilikuwa limeachwa pale pale chini Watu Wakilishangaa. Hakuamini